Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 489 | 490 | (Page 491) | 492 | 493 | .... | 3272 | newer

  0 0

   Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimjulia hali Mbunge wa Geita Donald Max aliyelazwa katika hospitali ya Taifa Muhimbili leo jioni.Rais Kikwete akiwa hospitalini hapo alimjulia hali pia Brigedia Jenerali Mstaafu Hashim Mbita aliyelazwa hospitalini hapo(picha na Freddy Maro).

  0 0

  Mwanamfalme Akishino
  Mwanamfalme Akishino wa Japan na Mkewe wanatarajiwa kuwasili nchini tarehe 02 Julai, 2014 kwa ziara rasmi ya siku tano.

  Akiwa hapa nchini Mwanamfalme Akishino atakutana kwa mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete kabla ya kutembelea Kituo cha Mafunzo cha Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO); Makumbusho ya Taifa na Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

  Akiendelea na ziara yake, Mwanamfalme Akishino atatembelea Visiwa vya Zanzibar na kufanya mazungumzo na Mhe. Dkt. Ali Mohammed Shein, Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kabla ya kutembelea eneo la Mji Mkongwe na hatimaye kuelekea kwenye Hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro na Mbuga ya Wanyama ya Serengeti.

  Aidha, katika siku ya mwisho ya ziara yake Mwanamfalme Akishino atatembelea Banda la Japan kwenye Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya Sabasaba.

  Mwanamfalme Akishino ambae ni mtoto wa pili kati ya watoto watatu wa Mfalme Akihito anatarajiwa kumaliza ziara yake hapa nchini tarehe 06 Julai, 2014 na kuondoka siku hiyo hiyo kurejea nchini kwake.

  IMETOLEWA NA: WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA, DAR ES SALAAM.
  01 JULAI, 2014

  0 0

   Banda la Umoja wa Mataifa katika Maonesho ya SabaSaba jijini Dar es salaam
   Kijana majasiriamali akionesha kazi zake kwa waliotembelea banda la Umoja wa Mataifa kwenye Maonesho ya SabaSaba. Yeye ni mmoja kati ya vijana wengi wanaofadhiliwa na Umoja wa Mataifa katika mafunzo ya ujasiriamali kufuatia mpango wa Umoja huo wa kuendeleza watoto, vijana na kinamama 
   Mkurugenzi wa mipango na mahusiano wa TIB Development Bank Bw. Jaffer S. Machano (mwenye miwani) akiwa na wafanyakazi wenzie wa benki hiyo inayokuja juu kwa kasi kwenye banda lao katika Maonesho ya SabaSaba
    Afisa mauzo mwandamizi wa kampuni ya Property International Ltd Bw. George Colyvas (kushoto) akitoa maelezo kwa mteja aliyewatembelea bandani kwao leo kwenye Maonesho ya SabaSaba. Kampuni hii inajishughulisha na mipango miji, uuzaji wa viwanja vilivyopimwa, ujenzi wa nyumba za makaazi na biashara pamoja na ushauri na mambo mengine kibao (BOFYA HAPA)   Ankal akiwa na wadau wa TTCL bandani pao kwenye Maonesho ya SabaSaba. Shirika hili la umma hivi sasa linatamba na huduma za intaneti ya kasi iitwayo "BANJUKA PLUS" (BOFYA HAPA) yenye modem inayokuwezesha kuperuzi bila kikomo (unlimited time) ambapo hutoa punguzo maalumu katika saa tofauti za matumizi.

   Banda la IFM 
   Banda la Tanzania Standard Newspapers, wachapaji wa Daily News na HabariLeo. Kwa taswira zaidi BOFYA HAPA


  0 0

  Timu ya soka ya Biashara United ya mjini Musoma Mkoani Mara (pichani) inayojiandaa kwa  mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya soka ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mwishoni mwa wiki imewabamizia Timu ya Polisi Veteran ya Mjini Musoma mabao 2-0 katika mchezo wa kirafiki uliofanyika katika uwanja wa Kumbukumbu ya Karume mjini Shinyanga.
  Mchezo huo ambao ulikuwa na kila aina ya ufundi kutoka kwa wachezaji wa timu zote kipindi cha kwanza kilimalizika baada ya timu hizo kutosha nguvu ya 0-0. Katika kipindi cha Pili timu hiyo inayoongozwa na Kocha Mchezaji Aman Richard ilifanya mabadiliko kwa baadhi ya wachezaji ambapo katika safu ya ushambuliaji aliingia Augustine Mgendi mabadiliko ambayo yaliinufaisha timu hiyo ya Biashara United baada ya mchezaji huyo kuifungia timu hiyo mabao hayo mawili.
  Akiongea baada ya mchezo huo,Kocha huyo alisema kuwa bado timu hiyo inahitaji kufanya maboresho kabla ya mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya Bunge Mjini Dodoma. Tumeshinda mchezo wetu lakini bado tuna kazi kubwa maana tunapata nafasi nyingi lakini hatuzitumii ipasavyo,sasa kwa mchezo uliopo mbele yetu lazima tubadilike” alisema Kocha Amani.
  Katika mchezo huo ambao ulishuhudiwa na baadhi ya wakazi wa Manispaa ya Musoma mkoani hapa ni maandalizi ya mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya Bunge utakaofanyika mwanzoni mwa mwezi August mjini Dodoma.

  0 0

   Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na Wananchi wa Kijiji cha Mvuleni Shehia ya Kidoti Jimbo la Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja kuhusiana na masuala ya huduma za maji na umeme.Kulia ya Balozi Seif ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kaskazini Unguja Nd. Haji Juma Haji, kushoto yake ni Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Mh. Pemba Juma Khamis na Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Zanzibar { ZAWA } Dr. Mustafa Garu.
   Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na Wananchi wa Kijiji cha Mvuleni Shehia ya Kidoti Jimbo la Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja kuhusiana na masuala ya huduma za maji na umeme.Kulia ya Balozi Seif ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kaskazini Unguja Nd. Haji Juma Haji, kushoto yake ni Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Mh. Pemba Juma Khamis na Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Zanzibar { ZAWA } Dr. Mustafa Garu.
   Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Zanzibar { ZAWA } Dr. Mustafa Garu akitoa ufafanuzi  kwa Wananchi wa Kijiji cha Mvuleni wa mtandao wa huduma za Maji safi na Salama ndani ya jimbo la Nungwi.
  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akitembelea Kijiji cha Mvuleni Shehia ya Kidoti ndani ya Jimbo la Nungwi  akiwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kaskazini Unguja Nd. Haji Juma Haji. Kushoto yake na Katibu wa CCM Wilaya ya Kaskazini “ A “  Nd. Ame Omar Kulia yake.
  Picha na Hassan Issa wa OMPR, ZNZ. Habari kamili BOFYA HAPA

  0 0


  0 0

  Ile filamu mliyokuwa mnaisubiri kwa hamu iitwayo “Cultural Wars” iliyoandikwa na kutengenezwa na Deogratius Mhella (Mtanzania anayeishi New York) akishirikiriana na Watanzania na Wamarekani waishio New York, New Jersey Boston na Connecticut sasa imetoka kwa mara ya kwanza na inapatikana kwenye DVD na unaweza kupata “electronic Copy” na vile vile unaweza kuiona online kupitia: www.createspace.com/405841 
   Filamu hii inazungumzia baadhi ya changamoto za kimapenzi wazipatazo vijana wa Kitanzania hapa Marekani. Na ni ya kwanza iliyochezwa na Watanzania na Wamarekani hapa New York kwa kutumia lugha ya Kiingereza. 
  Baadhi ya “Actors” wa Kitanzania ni Khalifa Siwa aka “Bob”, Ibra aka “Vijimambo New York”, Akida aka “Mshenga”, Chemi Whitlow aka “Chemponda” na Isaac Kibodia aka “Father”. Wote mliosaidia katika kufanikisha filamu hii ambao hamjatajwa hapo juu, mnapewa shukrani za dhati kabisa.
   Usikose kujipatia nakala yako ya DVD kwa kuinunua au kuiona kupitia: www.createspace.com/405841

  0 0


  Marehemu Daniel Anael Lema enzi za uhai wake


  Mwili wa Daniel Anael Lema, aliyekuwa mwanafunzi wa mwaka wa nne wa shahada ya sheria katika Chuo Kikuu Kishiriki cha Mt. Augustino, Tawi la Iringa (Ruaha University College - RUCO) umeagwa leo na kusafirishwa kuelekea mkoani kwao kilimanjaro kwa mazishi.
  Wanafunzi wa chuo hicho na wananchi wa manispaa ya Iringa walioguswa na tukio hilo walijitokeza katika hospitali ya mkoa wa Iringa ambako shughuli ya kuuga mwili huo ilifanyika.
  Jeshi  la Polisi mkoani iringa   linawashikilia watu wanne ambao ni walinzi wa duka usalama waliokuwa wakilinda nyumba moja ya kulala wageni iliyopo Kihesa katika manispaa ya Iringa kwa tuhuma  ya kumchoma moto mwanafunzi  huyo.
  Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoani Iringa Ramadhani Mungi alisema tukio hilo lilitokea Juni 24 majira ya saa tisa usiku baada ya wasamaria wema kutoa taarifa polisi kuwa kuna mtu anatembea akiwa anawaka moto. 
  Mungi alisema mara baada ya kupata taarifa hiyo   Jeshi la Polisi lilifika katika  eneo hilo  na kumkuta Daniel  Lema (25)  akiwa ameanguka chini huku akiwa amefungwa mikono nyuma. 
  Kamanda huyo aliwataja  watuhumiwa hao kuwa ni  Mussa Nganga (28), Costa Mgayuka (38), Steven Kalole (24) na Samson Peter (24) wote wakazi wa Kihesa.
    “Tulipopata taarifa tulifika eneo hilo kwa haraka na tukamkuta ameanguka chini tulimfungua ile mikono na kumchukuza vizuri tulimkuta akipumua kwa shida ndipo tukamkimbiza hospitali ya rufaa ya mkoa wa Iringa kwa ajili ya kupata matibabu.”alisema Kamanda Mungi. 
  Alisema kuwa  mwanafunzi huyo alikuwa baa moja inayoitwa Inbox bar inayomilikiwa na Katibu Mkuu wa zamani wa TFF, Frederick Mwakalebela akipata kinywaji huku akiangalia michuano ya mpira wa miguu (kombe la dunia) ambayo inaendelea nchini Brazili. 
  “Mwanafunzi alikuwa anaangalia michuano hiyo ya mpira wa miguu kwenye baa hiyo na baada ya mpira huo kuisha aliondoka na kuelekea nyumbani kwako Kihesa kabla ya kufika nyumbani eneo hilo kuna nyumba ya kulala wageni iitwayo Glory lodge ambapo pembeni yake kuna grocery moja iitwayo Glory grocery  akaingia hapo akifikiri ipo wazi ili aendeleze kinywaji,” alisema.
  Alisema wakati akigonga mlinzi wa nyumba ya kulala wageni Glory lodge  ambae ni mmasai aitwaye Mussa Nganga alimuona na kumuita ndipo kijana akakimbia na baada ya kukimbia alimfukuza na kuwaita wenzake watatu na kumfanyia kitendo kama hicho.”alisema Mungi.
  Baada ya kufikishwa Hospitali ya Rufaa ya Iringa, Lema aliendelea na matibabu yake mpaka alipokutwa na mauti jana majira ya saa nane mchana. 

  0 0

  Courtesy of White House

  0 0

  Waziri wa Ujenzi Mh.John Pombe Magufuli ameendeleza wimbi la kuzoa wanachama wa CHADEMA hasa katika kata zinazoongozwa na Madiwani wa CHADEMA. Awamu hii amekomba wanachama wapatao 98 eneo la Mganza (Kasenda) na wanachama 160 eneo la Mganza (Katemwa) yote kata ya Mganza wilaya ya Chato.
    Mh.Maduka Diwani wa CHADEMA Kata ya Mganza Wilaya ya Chato akimpongeza Mh.Magufuli baada ya Magaufuli kuzoa wanachama wa CHADEMA wapato 258.
   Wanachama Wapya wakiorodheshwa ili kuapishwa na kugawiwa kadi
   Umati mkubwa wa watu uliohudhulia mkutano Katemwa Kata ya Mganza Wilaya ya Chato
  Mh.Magufuli akipata BIG UP kutoka kwa wanachama wapya Kasenda Kata ya Mganza Wilaya ya Chato

  0 0

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano mwa Tanzania Mhe. Dkt Moahammed Gharib Bilal, Rais wa Burundi Mhe. P. Nkurunziza wakipokea maandamano ya maadhimisho ya Miaka 52 wa Uhuru wa Nchi hiyo yaliyofanyika leo Julai 1-2014 katika uwanja wa Prince Louis Rwegasore jijini Bujumbura Burundi. 
   Rais wa Burundi Mhe. P. Nkurunziza akikagua gwaride rasmi kwa ajili ya maadhimisho ya Miaka 52 wa Uhuru wa Nchi hiyo yaliyofanyika leo Julai 1-2014 katika uwanja wa Prince Louis Rwegasore jijini Bujumbura Burundi.
   Vijana wa halaiki wakitumbuiza kwenye maadhimisho ya Miaka 52 wa Uhuru wa Nchi hiyo yaliyofanyika leo Julai 1-2014 katika uwanja wa Prince Louis Rwegasore jijini Bujumbura 
   Ujumbe wa Tanzania uliofuatana na Makamu wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Bilal kwenye maadhimisho ya Miaka 52 wa Uhuru wa Nchi hiyo yaliyofanyika leo Julai 1-2014 katika uwanja wa Prince Louis Rwegasore jijini Bujumbura Burundi.  (Picha na OMR)
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani Mhe.Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimpongeza  Rais wa Burundi Mhe. P. Nkurunziza  kwenye Uwanja wa Prince Louis Rwegasore jijini Bujumbura Burundi wakati wa maadhimisho ya Miaka 52 wa Uhuru wa Nchi hiyo yaliyofanyika leo

  0 0

   Jukwaa likitengenezwa kwaajili ya Washiriki Wa fainali ya Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) kupanda jukwaani na kuanza kuonyesha vipaji vyao, Onyesho hili ni onyesho la kwanza la kuelekea Kwenye Mchujo wa kumpata mshiriki Mmoja atakayejinyakulia kitita cha Shilingi Milioni 50 katika fainali kubwa itakayofanyika mwishoni mwa Mwezi wa Nane.
  Mahost wa Show ya Tanzania Movie Talents (TMT) Joti na Lulu wakiwa kwa Steji tayari kwa Show kuanza
  Timu ya Tanzania Movie Talents (TMT) ikiwa katika maandalizi ya mwisho mwisho kabla ya Show ya Tanzania Movie Talents katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa usiku huu
   Baadhi ya wakazi wa jiji la Dar waliohudhuria kwaajili ya kutazama onyesho la washiriki wa fainali ya Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) linaloendelea kufanyika katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa.
   Wadau waliojitokeza kwaajili ya Kushuhudia onyesho la Tanzania Movie Talents.Picha zote na Josephat Lukaza
  Na Josephat Lukaza - Proin Promotions - Dar Es Salaam.
  Washiriki 20 wa Shindano la Tanzania Movie Talents ambao ni washindi kutoka kanda 6 za Tanzania wamepanda kwa steji katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa kwaajili ya kuanza kuonyesha vipaji vyao vya kuigiza.  Sasa ni safari kwa washiriki kuelekea kwenye kinyanganyiro cha kuwania Milioni 50 za Kitanzania katika fainali kubwa itakayofanyika Mwisho wa Mwezi wa Nane.
  Katika Onyesho hili litakalorushwa katika Runinga ya ITV siku ya Jumamosi saa 4 usiku kitakuwa kipindi cha kwanza kwa watanzania kuanza kuangalia na kuwapigia kura washiriki ambao watakuwa wamewavutia na kukonga nyoyo zao na hatimaye kuwawezesha kushiriki katika fainali kubwa Mwishoni mwa Mwezi wa Nane.
  Watanzania wanatakiwa kuendelea kutazama muendelezo wa vipindi vya TMT kupitia Kituo cha Runinga cha ITV saa nne Usiku siku ya Jumamosi na hatimaye kuanza kuwapigia kura washiriki. Ili kuweza kupata Taarifa za TMT unaweza kutuma neno "TMT" kwenda namba 15678
  Mchujo kwa washiriki sasa waanza rasmi ili kuweza kumpigia kura mshiriki umpendae unatakiwa kutuma neno "TMT ikifuatiwa na namba ya Mshiriki" kwenda namba 15678

  0 0
 • 07/01/14--13:29: Miss Tanzania USA Pageant


 • 0 0

   Afisa Biashara Mkongo wa Taifa wa mawasiliano,Bwa.Thomas Lemunge akielezea kuhusiana na Mkongo wa Taifa wa mawasiliano unavyofanya kazi, mapema leo ndani ya maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea hivi sasa jijini Dar Es Salaam.

  Bwa.Thomas amebainisha kuwa Mkongo wa Taifa wa mawasiliano umekwisha sambaa maeneo mengi ikiwemo mikoa 21 ya Tanzania mpaka sasa,Amesema kuwa Makampuni yote ya ndani yanatumia mkongo huu wa mawasiliano kupeleka huduma kwa wananchi na kuongeza kuwa Mkongo huo unaunganisha mataifa mbalimbali kupitia mkongo huu wa Taifa wa Mawasiliano ambao umerahisisha mambo mengi katika jamii ikiwemo suala zima la mawasialiano ya simu za kiganjani na mambo mengineyo.

  Bwa.Thomasa amewataka wananchi kuhakikisha wanautunza na kuulinda Mkongo huo wa mawasiliano ili kuendelea kurahusisha upatikanaji wa huduma mbalimbali.
  Afisa Mahusiano wa kampuni ya Simu ya TTCL-Tanzania,Bwa.Edwin Mashashi akielezea  kuhusiana na huduma zao mbalimbali zitolewazo na kampuni hiyo,ikiwemo masuala ya Internet na huduma nyinginezo mbalimbali kwa wateja wao.

  Bwa.Edwin ameeleza kuwa kwa sasa kampuni yao iko katika mchakato mkubwa wa kuziboresha huduma zao ziwe na ubora zaidi,ameongeza kusema kuwa pia Wanatarajia kufunga Wi-Fi katika maeneo mbalimbalu ya jiji la Dar, ambapo gharama itakuwa ni ya bei nafuu.

  Edwin amesema kuwa Kampuni ya TTCl-Tanzania,wanatarajia kuzindua kituo kikubwa Afrika Mashariki cha kuuzia internet,kituo hicho kinatarajia kuzinduliwa mwishoni mwa mwezi Julai ama Agosti,''mtambo huo tayari umekwishafungwa hapa hapa nchini tayari kwa kuanza kutoa huduma hiyo Afrika Mashariki,hivyo kutakuwa hakuna haja tena ya kununua tena Internet nje'',amedema Bwa.Edwin.
   Pichani ni baadhi ya wateja wakipata maelezo maelezo mbalimbali kuhusiana na huduma zitolewazao na Kampuni ya simu TTCL,ndani ya banda la kampuni hiyo ndani ya maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea hivi sasa jijini Dar Es Salaam.
   Wahudumu wa TTCL wakihudumia wateja wao kwa njia ya simu ndani ya banda lao,katika  maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea hivi sasa jijini Dar Es Salaam.
   Namna mkongo wa Taifa unavyofanya kazi na maeneo mbalimbali ulivyosambaa nchini.
   Baadhi ya Wahudumu wa kampuni ya simu ya TTCL wakiendelea kuwajibika.
  Ankal wa tatu kushoto akiwa na Wadau wa TTCL ndani ya banda lao lililopo ndani ya viwanja vya maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea hivi sasa jijini Dar Es Salaam.

  0 0

  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (wapili kulia) akitoka kwenye Banda la Wizara yake wakati wa  Maonyesho ya 38 ya Kimataifa ya Biashara ya Sabasaba yanayoendelea Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya Soko la Ndani, Edwin Rutageruka na kulia ni Afisa Habari wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Christina Mwangosi. Waziri Chikawe na Maafisa wa Jeshi la Polisi wametembelea viwanja hivyo kuangalia hali ya usalama. 
   Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade), Jacquline Maleko akimfafanulia Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe  (wapili kushoto), Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) Ernest Mangu (kushoto) na Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova (kulia) jinsi Mamlaka hiyo kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi walivyojipanga kuimarisha usalama katika Maonyesho ya 38 ya Kimataifa


   Msafara wa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe wakizunguka katika viwanja vya Sabasaba katika Maonyesho ya 38 ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam. Waziri Chikawe na Maafisa wa Jeshi la Polisi wametembelea viwanja hivyo vilivyopo Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam, kuangalia hali ya usalama katika viwanja hivyo.

  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (wapili kulia) akikiangalia cheti cha usajili wa vyama katika Banda la Wizara yake wakati wa Maonyesho ya 38 ya Kimataifa ya Biashara ya Sabasaba yanayoendelea Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu. Waziri Chikawe na Maafisa wa Jeshi la Polisi wametembelea viwanja hivyo vilivyopo Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam, kuangalia hali ya usalama katika viwanja hivyo. Kushoto ni Afisa Sheria, Flora Mlope ambaye alikuwa akitoa maelezo ya usajili wa vyama. Picha zote na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.


  0 0

  ADDRESS YETU MPYA NI:
  UNIT 16D TILBURY INDUSTRIAL COMPLEX
  TILBURY FREEPORT
  ESSEX
  RM18 7HB

  KUANZIA SASA MZIGO WA NDEGE NI SIX DAYS GUARANTEE
  SALOON CARS TO DAR NOW £680
  4 X 4 CARS TO DAR  NOW £770
  UKISHIP MAGARI ZAIDI YA MOJA UNAPATA BIG DISCOUNT!
  AIR CARGO TO DAR £3.80 INCLUSIVE CLEARANCE
  KAMA UNA MZIGO WA MSAADA TUNASAFIRISHA BURE
  FREE STORAGE IN OUR OFFICE
  FREE COLLECTION FROM EAST LONDON 
  £50 COLLECTION FROM ANYWHERE IN UK
  COLLECTION POINT IS
  ILALA MTAA WA BUKOBA
  CONTACT; TORNADO +255713607116
  SIMPLY THE BEST IN BUSINESS
  JUST DROP YOUR CAR AT OUR OFFICES AND WE WILL TAKE CARE OF IT
  WE WILL GET IT INSPECTED AND LOAD IT TO THE SHIP FOR YOU!
  BEI ZETU HAZINA WASHINDANI NDIO MAANA TUMEZIANIKA WATU WAJUE
  THE DIFFERENCE IS CLEAR!
  WE ARE NOW OPEN ON SATURDAYS
  WE PROMISED, WE DID IT AND WE ARE MAKING IT EVEN BETTER!
  Tupigie kwa namba hizo hapo Chini au  tutumie email tafadhali
  SIMON  LOUIS +44 (0) 79 506 89 243
  JONSTONE MALUNDA +44 (0) 7404298077 

  0 0

   Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimpokea Malkia Nomsa Matsebula wa Swaziland kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere 

   Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akisalimiana na baadhi ya wageni waliofuatana na Malkia Nomsa Matsebula mara baada ya mgeni huyo kutua kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere 
   Malkia Nomsa Matsebula wa Swaziland akipokea ua mara baada ya kuwasili  kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere.
  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiongea na mgeni wake Malkia Nomsa Matsebula wa Swaziland wakati wakielekea kupanda magari kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere tarehe 1.7.2014.
   PICHA NA JOHN LUKUWI

  0 0


  0 0

  Wow, what a last half hour, right? Three goals in 30 minutes with plenty of U.S. chances at the end to attempt to equalize. This means Belgium will go on to meet Argentina in the quarterfinals and the United States will go home. They will go home, though, with their heads held high. The Americans put up one heck of a fight in Brazil.And goalie Howard? That might be the most memorable performance of this World Cup. Sixteen saves! 
  I’ll end this post how I began it — WOW.

  0 0

   Bidhaa mchanganyiko za Afri Tea and Coffee Blenders (1963) LTD katika banda la kampuni hiyo kwenye maonesho ya SabaSaba jijini Dar es salaam
   Mdau Sinda Leonard Sinda, Afisa Mauzo Mwandamizi wa  Afri Tea and Coffee Blenders (1963) LTD akiwa tayari kukuhudumia bandani pao
   Sehemu ya bidhaa mchanganyiko za Afri Tea and Coffee Blenders (1963) LTD
   Mgeni akipewa maelezo ya bidhaa ya Mchaichai (Green Tea) inayotengenezwa na  Afri Tea and Coffee Blenders (1963) LTD
  Kikosi kazi cha  Afri Tea and Coffee Blenders (1963) LTD kwenye maonesho ya SabaSaba

older | 1 | .... | 489 | 490 | (Page 491) | 492 | 493 | .... | 3272 | newer