Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 47 | 48 | (Page 49) | 50 | 51 | .... | 3270 | newer

  0 0
 • 02/19/13--19:53: Article 23

 • The Aga Khan Hospital, Dar es Salaam is now offering Cardiology Clinics.
  FREE February Clinic on Wednesdays and Thursdays.
  For Booking / more information call: +255 22 2115151-53 ext 4702.

  0 0

   Wajumbe wa Tume walioambatana na Naibu Spika Mhe Job Ndugai wakifuatilia mazungumzo baina ya Mhe Ndugai na mwenyeji wake Mhe.Charles Chong ambae ni Naibu Spika wa Singapore. .Pichani toka shoto ni Mhe Godfrey Zambi , Mhe.Hamad Rashid, Mhe.Saleh Pamba na Mhe Beatrice Shellukindo. Picha zote na Saidi Yakubu wa Ofisi ya Bunge 
   Katibu wa Bunge, Dr Thomas Kashililah akimkabidhi zawadi Katibu wa Bunge la Singapore Bi Sheau Jiuan wakati wa ziara hiyo.kulia ni Mkurugenzi wa Sekretarieti ya Tume, Ndg Raphael Nombo.
  Mhe.Naibu Spika Ndugai akimkabidhi mwenyeji wake picha ya jengo la Bunge la Tanzania kama zawadi.Mhe Ndugai pia alimpa mwenyeji wake mwaliko maalum wa kutembelea Tanzania.Viongozi hao wawili wamekubaliana kuanzisha Chama cha Urafiki wa Kibunge baina ya Singapore na Tanzania kwa lengo la kubadilishana uzoefu katika nyanja mbalimbali za kibunge.

  0 0

  Suluhisho kwa waTanzania wenye makazi ya kudumu ughaibuni wenye nia ya kuja kutembea Tanzania kwa ndugu zao na wanapenda kukaa kwenye makazi yao wenyewe na familia zao

  4T TARVEN inaruhusu wapangaji wa muda mfupi katika nyumba ambayo ina vyumba vitatu vyote fitted with AC, mengine ni hot water heater, Flat screen,nyumba ina unlimited supply of water, kuna generator incase of power failure na vyombo vya ndani (fridge, gas cookers etc )kwa ajili ya kujihudumia; usafiri toka airport ni bure kama unabook kwa siku 7 na kuendelea; ulinzi masaa 24


  Nyumba ipo Mbezi Louis off Morogoro Road , kwa mawasiliano book thetarvenfourt@yahoo.com pia piga simu +255784312199

  0 0

   Baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari ya wasichana ya MT.Theresa wa Avila,wakipokea moja ya kati ya kompyuta kumi toka kwa Mkuu wa Vodacom Foundation Bw.Yessaya Mwakifulefule zenye thamani ya shilingi Milioni  zilizotolewa msaada na Vodacom Foundation hivi karibuni.

    Mkuu wa Vodacom Foundation Bw.Yessaya Mwakifulefule (kushoto)akimkabidhi Bi. Jacquline Augustine moja ya kompyuta kati ya 10 zenye thamani ya Milioni 7 zilizotolewa kwa msaada na Vodacom Foundation kwenye shule ya sekondari ya wasichana ya MT.Theresa wa Avila,anaeshuhudia kulia ni Meneja biashara wa kitengo cha Mahusiano Vodacom Bi.Lilian Kisamba.

   Mkuu wa Vodacom Foundation Bw.Yessaya Mwakifulefule na Meneja biashara wa kitengo cha Mahusiano Vodacom Bi.Lilian Kisamba,wakimkabidhi kompyuta kati ya 10 zenye thamani yua shilingi Milioni 7,Mwl.Joyce Martin wa shule ya sekondari ya wasichana ya MT.Theresa wa Avila.Iliyopo Mkoa wa Shinyanga Wilaya ya Kahama.
   Baadhi ya wananchi na wazazi wa wanafunzi wa shule ya sekondari ya wasichana ya MT.Theresa wa Avila.Iliyopo Mkoa wa Shinyanga Wilaya ya Kahama,walifika kushuhudia makabidhiano ya ya kompyuta kati ya 10 zenye thamani ya Milioni 7 zilizotolewa na Vodacom Foundation mwishoni mwa wiki.


  Wanafunzi wa shule ya sekondari ya wasichana ya MT.Theresa wa Avila.Iliyopo Mkoa wa Shinyanga Wilaya ya Kahama,wakifatilia kwa ukaribu makabidhiano ya kompyuta kati ya 10 zenye thamani ya Milioni 7 zilizotolewa msaada na Vodacom Foundation.


  0 0

  Bondia kijana na anayeinukia kwa kasi Albinu Felesianu wa nchi ya Namibia amepewa ofa ya kugombea ubingwa wa dunia wa Featherweight kwa vijana walio chini ya miaka 25 unaotambuliwa na IBF. Albinus amezoea kupewa zawadi za Christmas na siku kuu yake ya kuzaliwa lakini hamna kilichomwandaa na mshtuko mkubwa ambao aliupata wakati IBF ilipotangaza hivi karibuni kuwa imempatia nafasi ya kugombea mkanda wa dunia kwa vijana walio chini ya miaka 25.

  Mtua ambaye anaweza kuiua furaha yake ni mmoja wa watoto wa Nkrumah, Mghana Ishmael Ayeetey ambaye amekulia katika moja ya viunga vinavyosifika kwa kutoa mabingwa wa ngumi wa dunia kama kina Azumah Nelson, Joseph Agbeko na Ike Quartey.

  Albinus Felesianu kulia akimrushia ngumi mpinzani wake kushoto


  Mpambano huo utafanyika katika jiji la Windhoek nchini Namibia tarehe 29 March chini ya kampuni ya Kinda Boxing promotions ya bwana Kinda Nangolo!

  Hili litakuwa pambano la pili la ubingwa wa dunia kwa vijana baada ya bondia Ilunga Makabu wa Jamhuri ya Watu wa Kongo (DRC) kumtwanga bondia Gogito Gorgiladze wa Georgia jijini Johannesburg nchini Afrika ya Kusini jumamosi iliyopita.

  ISSUED BY:
  INTERNATIONAL BOXING FEDERATION AFRICA (IBF/AFRICA) 
  DAR-ES-SALAAM, TANZANIA

  0 0

  MKOA wa Dar es Salaam umeshinda katika mchakato wa kuchagua mkoa wa kwanza ambao Tamasha la Pasaka mwaka huu litaendeshwa.

  Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari  leoa na Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama alisema kamati yake ilikuwa ikiendesha kura za maoni kwa mashabiki wao wa eneo lipi tamasha hilo lifanyike.

  “Tulifanya kura za maoni kwa njia ya simu za mkononi, pia tulikuwa na vipindi maalum kwenye baadhi  ya redio kwa mashabiki kutoa maoni yao.“Mikoa ya Dar es Salaam, Mbeya, Dodoma na Mwanza ilikuwa ikichuana vikali katika kupata mahali ambapo tamasha litafanyika, maana tulikuwa bado hatujatangaza.

  “Lakini leo (jana) tumechagua Dar es Salaam, ambapo zaidi ya mashabiki 15,000 walichagua tamasha lifanyike Dar es Salaam, mashabiki 13,000 walitaka lifanyike Mbeya, mashabiki 7,000 walitaka Mwanza na mashabiki 3,000 walitaka Dodoma,” alisema Msama. Alieleza kuwa hivi sasa wanatazama mkoa upi lifanyike Jumatatu ya Pasaka na siku zingine zitakazofuata.

  “Siku yenyewe ya pasaka tushapata kwamba ni Dar es Salaam, sasa tunajipanga kwa siku zingine maana mwaka huu tunataka mikoa saba tufanye tamasha letu,” alisema Msama na kuongeza kuwa kwa Dar es Salaam litakuwa Machi 31 mwaka huu.

  Pia alisema bado wanaendelea na mazungumzo na wasanii mbalimbali  kwa ajili ya kushiriki tamasha la mwaka huu. Baadhi ya wasanii walioshiriki tamasha la mwaka jana ni Rose Muhando,Rebecca Malope, Christina Shusho, Upendo Nkone, Upendo Kilahiro, Solomon Mukubwa, Atosha Kissava, Ephraim Sekeleti na kundi la Glorious Celebration.

  Pia kwaya mahiri ya Kinondoni Revival, Mwinjilisti Faraja Ntaboba kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) zilikuwa miongoni mwa burudani zilizokuwepo siku hiyo.


  0 0

   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein,(kushoto) akitoa salamu ya Mwisho kwa mwili wa Marehemu Padri Evarest Mushi,katika Kanisa la MinaramiwiliMjini Zanzibar, Padri Gabriel Mushi,aliyefariki kwa kupigwa risasi na watu wasijuilikanwa Jumapili iliyopita,na atazikwa leo Kijini Kitope Wilaya ya Kaskazini B Unguja,(katikati) Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Zanzibar Augustino Shao.
   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein,akitia saini kitabu cha maombolezi ya Padri Evarist Gabriel Mushi,katika Kanisa la Minaramiwili MjiniZanzibar,ambapo alifika kutoa salamu ya mwisho kwa Padri huyo,aliyefariki kwa kupigwa risasi na watu wasijuilikanwa Jumapili iliyopita,na atazikwa leo Kijini Kitope Wilaya ya Kaskazini BUnguja,(kushoto)  Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Zanzibar Augustino Shao.
  Baadhi ya Waombolezaji wakiwa ndani ya Kanisa la Minaramiwili Mjini Zanzibar wakati wa kutoa salamu ya Mwisho kwa Padri Evarist Gabriel Mushi,aliyefariki kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana Jumapili iliyopita,na atazikwa leo Kijijini Kitope Wilaya ya Kaskazini B Unguja.[Picha na Ramadhan Othman Ikulu.]
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Zanzibar Augustino Shao wakati alipofika katika Kanisa la Minaramiwili Mjini Zanzibar kutoa salamu ya Mwisho kwa Padri Evarist Gabriel  Mushi,aliyefariki kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana Jumapili iliyopita,na atazikwa leo Kijijini Kitope Wilaya ya Kaskazini B Unguja.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein,akiwasalimia wananchi wakati alipofika katika Kanisa la Minaramiwili Mjini Zanzibar kutoa salamu ya Mwishokwa Padri Evarist Gabriel Mushi,aliyefariki kwa kupigwa risasi na watu wasijuilikanwa Jumapili iliyopita,na atazikwa leo Kijini Kitope Wilaya ya Kaskazini B Unguja.[Picha na Ramadhan Othman Ikulu.]

  0 0

   Libeneke jipya la Burger kinondoni karibu na  kituo cha Vijana kinondoni barabara ya Mwananyamala. Burger za nyama ya ng'ombe na kuku na ya mbogamboga zinapatikana.karibuni sana mpate burger bora in Town.Tunafungua kuanzia saa sita mchana mpaka saa nne usiku kila siku,kama kuna oda zaidi ya 5 tunafungua muda wowote kutimiza ahadi ya mteja.karibuni sana  Kenzie Dream Burger mpate kitu roho inataka.

  0 0

   President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete welcomes to the State House the USAID Administrator Dr.Rajiv Shah this morning.
  President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete in conversation with the USAID administrator Dr.Rajiv Shah at State House Dar es Salaam this morning.(photos by Freddy Maro)

  0 0

  Jaji Kiongozi wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Fakih Jundu akiongelea juu madhumuni ya ziara  yake leo asubuhi katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Pangani. Mhe. Jaji Kiongozi alitembelea ofisini hapo kabla ya kuelekea Mahakama ya Wilaya ya Pangani.
   Mkuu wa Mkoa wa Tanga Ltn, Chiku Gallawa akiongea na Ugeni wa Viongozi mbalimbali wa Mahakama ukiongozwa na Mhe. Jaji Kiongozi katika ziara yake mkoani Tanga. Mhe. Mkuu Mkoa pamoja na Mhe.Jaji Kiongozi wamesisitiza juu ya uimarishaji wa ushirikiano katika utendaji kazi.(picha na Mary Gwera,Mahakama ya Tanzania). 
   Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Pangani, Mhe. Frank Moshi akitoa mkono wa salamu kwa baadhi ya Watumishi wa Mahakama ya Wilaya ya Pangani Mara baada ya kuwasili Leo asubuhi Mahakamani hapo pamoja na msafara wa Mhe. Jaji Kiongozi, Mhe. Moshi ameteuliwa hivi karibuni kuwa Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Pangani baada ya kustaafu kwa Mfawidhi wa Mahakama hiyo, nyuma ya Mhe. Moshi ni Mkurugenzi wa Mahakama za Mwanzo nchini, Mhe. Euphemia Mingi, Kushoto kwa Mhe. Mingi ni Naibu Mkurugenzi wa Mahakama za Wilaya hadi Rufani, Mhe. Eddie Fussi. (Picha na Mary Gwera, Mahakama) 

  0 0

   Balozi wa Nigeria hapa nchini Dr Ishaya Majanbu mweyekofia nyekundu akiwa anapata maelezo kutoka kwa meneja wa mradi wa ujenzi wa Dangote Sementi Mkoani Mtwara Eng D Musale  ya kuhusu maendeleo ya ujenzi wa kiwanda cha semeti cha Dangote kinacho jengwa Mkoani Mtwara Balozi huyo ameridhishwa na kasi ya ujenzi wa mradi huo alipotembelea mkoani mtwara. picha na Chris Mfinanga.
   Balozi akiwa ana angalia badhi ya vifaa vilinavyo tumika katika mradi wa ujenzi wa kiwanda hicho cha sementi kunacho jengwa na kampuni ya Dangote.
  Balozi wa Nigeria hapa nchini Dr Ishaya Majanbu akiwa katika soko la Mtwara akiangalia mchele bidha mbalimbali zinazo patikana katika soko hilo wafanya biashara wasoko hilo walipata muda wa kumsomea tarifa yao ya kumuomba amfikishie mkrugenzi mkuu wa Dangote ili aweze kuwasidia kulifanya soko hilo liwe la kisasa.
   Balozi akiwa katika picha ya pamoja na wafanya biashara wa soko la mtwara.

  0 0

   Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue (kulia) akimsikiliza Mkurugenzi wa Idara ya Huduma ya TEHAMA Bw.Priscus Kiwango akiwasilisha mada ya Mfumo Shirikishi wa Taarifa za Kiutumishi na Mishahara (HCMIS) alipofanya ziara ya kikazi ya Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma jana.
   Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue (kulia) akipokea nyaraka mbalimbali za kiutumishi kutoka kwa Kaimu Katibu Mkuu ,Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw.HAB Mkwizu alipofanya ziara ya kikazi Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma
   Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue (kulia) akimsikiliza Mkurugenzi wa Idara ya Ushauri na Uchambuzi Kazi Bw.Micky Kiliba alipokuwa akiongelea masuala mbalimbali ya kiutumishi wakati wa ziara yake Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma jana
   Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue (kulia) akiongea na watumishi wa Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma alipofanya ziara ya kikazi Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma jana
  Watumishi wa Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma wakimsikiliza Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue alipofanya ziara ya kikazi Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma jana

  0 0


  Uongozi wa mtandao huu umesikitishwa na vitendo vinavyofanywa na baadhi ya wamiliki wa blogs, kuwa wakiiba kazi za watu katika blogs mbalimbali yaani ‘Kukopi na Kupaste’ kutoka katika blog Fulani na kuweka katika Blogs zao bila kujali haki miliki ya kazi ya mtu, wala kumpa haki yule aliyechukuliwa kazi yake kwa kuandika mahala ulipochukua kazi hiyo.


  Kama inavyojulikana utafutaji wa habari si lelemama na ikumbukwe ili kupata habari iliyo bora na itakayowafurahisha wasomaji wako, kwenda na wakati ni lazima uihangaikie na katika kuihangaikia kuna gharama kibao zinazotumika, ikiwa ni pamoja na usafiri, pesa, na hata mafuta ya gari kutoka mahala Fulani kwenda sehemu nyingine, gharama za simu na hata kuwalipa wale unaowatuma ili kukufanyia kazi hiyo.


  Kama umeweza kufanya mambo yote hayo kwa gharama unazozijua wewe uliyeweka stori, ama picha katika Blog yako, halafu watu wenye Blog Fulani wasio na uwezo wa kufanya kazi na kuchukua kazi yako kana kwamba ameokota tu jalalani na anaweka kwake ili wasomaji wake wasome, bila kuwajulisha kuwa kazi hiyo iliyomvutia imefanywa na mtandao Fulani kwa kweli inaumiza, inaudhi na inarudisha nyuma malengo hasa ya kuwa na mitandao hii, wote tutajaonekana wapuuzi.


  Mtandao huu umewavumilia watu hawa kiasi cha kutosha lakini sasa imezidi kukithiri, kwani jamaa hawa wapo katika ukurasa wako kukusubiri kuona tu ulichoweka kwa wakati huo, ili wao wakopi na kupaste kwao, halafu tayari wamemaliza wala hawataki kujihangaisha kufanya kazi ili kuboresha mitandao yao na kuwavutia wasomaji wao.


  ‘Unapoamua kutangaza vita ujue tayari umeshajipanga kukabiliana na kila litakalotokea mbele yako, na pia umejipanga katika kutoka upinzani wa kweli ili watu waone na wakutambue, lakini sio kwa staili hii ya kuomba mtangaziwe blog zenu kupitia kwa wale walioanza mapema halafu kumbe kazi yenyewe ni kuchukua kazi za watu tu na si kufanya kazi’ yaani kukopi na kupaste,


  Kuna msanii mmoja alichoshwa na wenzake wanaotamani kuingia kwenye gemu, lakini wanashindwa kuumiza vichwa kubuni ili kuweza kupata radha tofauti, na kuamua kuwafikishia ujumbe kwa kuwaimba kuwa ‘Si lazima wote tuimbe kuna michezo mingi hata kucheza bao kama huwezi kuimba, ikiwa kila wimbo unaotoka mpya umekopiwa, kama si mashahiri, basi ni Beat,


  Na hata katika mablogger si lazima wote tuwe na Mablogger, kama huwezi kuumiza kichwa utoke vipi, basi kaa pembeni waachie wenye uwezo wa kufanya kazi hiyo, kukopi na kupaste hadi mitandao yote inakuwa sawa nini maana ya habari za haraka mtandaoni?,


  Huoni kuwa mnawachosha wasomaji wenu, kwa kosoma habari na picha zinazofafa kwa wakati mmoja na katika mitandao yote?,


  Tena msomaji wako wakiwa ni waelewa hawawezi kusoma tena mtandao wako kwani habari kama hiyo hiyo walikwishaiona katika mtandao Fulani muda mchache uliopita na dakika chache baadaye wanaikuta vile vile walivyoisoma kwingine ikiwa katika ukurasa wako, mara moja mara mbili msomaji huyo si umempoteza?’’.


  Mablogger acheni uvivu na mjitume msisubiri kukopi na kupaste tu, na kama ukifanya hivyo basi jitahidi kumpa credit yule uliyemchukulia kazi yake.


  VITU muhimu vy kuwa navyo ili kufanikisha kazi yako ya Blog, ni Laptop ‘Kompyuta mpakato’, ama Desk Top, Modem ‘Internet Wireless’, Kamera hata ndogo tu ya mkononi, na pia ujue maana ya kuanzisha hiyoBlog yako na malengo yako kwa jamii, kwani sidhani kama unaweza kuanzisha blog ili uwe ukisoma mwenyewe na naniliu wako tu.


  Na kuwa na kamera si bora tu kuwa kamera pia ujue kuitumia ipasavyo ili kunasa picha nzuri uitakayo na itakayofikisha ujumbe kwa wasomaji wako hata kwa kuiangalia tu, kwa kile ulichokusudia kuwaarifu wasomaji wako.


  Baadhi ya Blogs zenye tabia ya kukopi na kupaste orodha yake tayari tunayo na baada ya tangazo hili, zikiendelea tutaziweka hewani ili wasomaji wajue ni Blog ipi ya kweli na ipi ni mamluki.


  0 0


  0 0


  Hon. Bernard K. Membe (MP), Minister for Foreign Affairs and International Co-operation (left), hand-delivers a special message to H.E. Andry Rajoelina, President of the Transition Government of Madagascar yesterday in the State House  in Antananarivo City. Minister Membe was in Madagascar as a Government Special Envoy to hand-deliver a special message on behalf of President Jakaya Mrisho Kikwete of the United Republic of Tanzania. 
  Hon. Membe (2nd left), in discussion with President Rajoelina.  Also in the photo are Ambassador Liberata Mulamula (left), Senior Advisor (Diplomatic Affairs) to President Kikwete and interpreter (2nd right). 

  Hon. Membe holds a press conference after his meeting with President Rajoelina of the Transitional Government of Madagascar.

  Hon. Membe in discussion with Mr. Andriatina Jacques Ulrich, Acting Minister of Foreign Affairs in Madagascar. 
   
  Hon. Membe in discussion with Acting Foreign Minister of Madagascar, Mr. Andriatina Jacques Ulrich (right) and Ambassador Mulamula.

  By TAGIE DAISY MWAKAWAGO

  Antananarivo, Madagascar

  President of Transitional Government of Madagascar, Andry Rajoelina has appealed to the international community, essentially the AU and SADC to remove the sanctions imposed on his transitional government.

  He made the request yesterday when he met with Hon. Bernard K. Membe (MP), the Minister for Foreign Affairs and International Co-operation, in his State House located in Antananarivo City.  Minister Membe was in Madagascar as a Government Special Envoy to hand-deliver a Special Message on behalf of President Jakaya Mrisho Kikwete of the United Republic of Tanzania.

  Speaking to the reporters after the meeting, Hon. Membe said that the message he carried from President Kikwete was a follow up on the development of transitional government in Madagascar, as it prepares for the upcoming Presidential elections. He further noted that President Kikwete wanted to know the outcome of discussion between President Rajoelina and the United Nations’ Secretary General Ban Ki moon in their recent meeting this year.

  President Kikwete currently serves a Chairperson of the Southern Africa Development Community (SADC –Troika), after inheriting the Chairmanship from South Africa last August 2012.

  On his part, President Rajoelina appealed to President Kikwete to assist in lifting any and all sanctions imposed upon his transitional government and for perpetrating the status quo. Other sanctions targeted the 109 accomplices and confidants of President Rajoelina for their involvement in the 2009 coup d’etat. He explained that the conditions set in the roadmap by the international community have been fully implemented.

  Further, President Rajoelina availed the commitment of his transitional government to see a democratic election takes place in July 2013.

  In his response, Minister Membe said that the removal of sanctions is not conditional to the return of Marc Ravalomanana, former President of the Republic of Madagascar.  “The roadmap is for SADC-Troika to see that the upcoming elections will be fair and profound for the people of Madagascar,” said Hon. Membe.

  The sanctions in question were imposed by the African Union and supported by the Southern Africa Development Cooperation (SADC) and the International Community.

  Minister Membe further explained that President Rajoelina   informed him that his transitional government has fulfilled its obligation as mandated by AU, which included his withdrawal of presidential candidacy in the upcoming elections in July of this year.  Others are storing peace and normalcy back in the country in the preparation for the democratic election later this year.

  Hon. Membe led the Tanzania delegation that included Ambassador Liberata Mulamula, Senior Advisor (Diplomatic Affairs) to President Kikwete, Mr. Mkwizu of the President’s Office, Mr. Assah Mwambene, Director of Information in the Ministry of Communication, Youth, Culture and Sports and other Governmental officials.  For the Madagascar’s part, the delegation was led by President Rajoelina, Mr. Andriatina Jacques Ulrich, Acting Minister for Foreign Affairs and other transitional government officials.

  Hon. Membe is expected to return back in Dar es Salaam later today.  

  0 0
 • 02/20/13--04:31: Tangazo la msiba

 •  Kwa masikitiko makubwa tunapenda kuwataarifu ya kuwa familia ya Dennis na Gloria Shengena wamefiwa na mama mzazi wa Gloria ambaye pia ni Dada wa Jackson na William Mollel wa Minnesota.Marehemu Esther Elius Nielsen amefariki leo asubuhi (Feb 18) huko Tanzania.

  Mipango ya mazishi inaendelea huko Arusha. Ndugu wa marehemu wanatarajiwa kusafiri kwenda kwenye mazishi ijumaa wiki hii huko Arusha,Tanzania.

  Unaweza kutuma mchango wa rambi-rambi kwa Bank Account zifuatazo:-
  Dennis & Gloria Shengena,
  TCF Bank,
  A/C #6441512262

  Msiba upo Golden Valley kwenye anuani ifuatayo:

  2101 Tamarin Trail
  Golden Valley MN 55427

  Kwa maelezo zaidi unaweza kuwasiliana na wafiwa;-

  Gloria Shengena    952-649-9818
  Jackson Mollel        651-334-0163
  William Mollel        651-338-9466
  Dennis Shengena  952-992-9489

  Kwa niaba ya familia ya wafiwa,tunatanguliza shukrani kwa maombi na faraja wakati huu mgumu.
  Ahsanteni Sana.
  Joel Mburu

  0 0
 • 02/20/13--04:36: Bongo tambarare
 • Vikwangua anga vinazidi kuibuka kila kona jijini Dar es salaam. Hapo ni Barabara ya Bibi Titi na Ally Hassan Mwinyi

  0 0

   Sanamu za Tembo juu na chini ya Nyati katika sheli ya Delina Petrol Station kilichopo takriban kilomita moja toka Kibaha ukitokea Morogoro upande wa kushoto. Ubunifu huu umesifiwa sana na wapita njia na kumtaka mwenye sanaa hii aingie hadi miji mingine na kuongeza urembo na pia kutangaza vivutio vyetu vya utalii


  0 0
 • 02/20/13--04:44: watani wa jadi
 • Watani wa jadi hawa walio maeneo ya Kibamba, barabara ya Morogoro road, walikamatwa na kamera ya Globu ya Jamii mwaka jana mwezi kama huu. Leo bado wapo bega kwa bega katika kuonesha ukomavu wa kisiasa. Hata hivyo bendereza zao zinaonekana kuchoka na bila shaka wahusika wataliangalia hilo kwa herufi kubwa....

  0 0

  Na Heka Paul na Shakila Galus_MAELEZO –Dar
   
  Wakaguzi wa Ndani wa Serikali wametakiwa kubadilika na kuacha kufanya kazi zao za kila siku kwa kufuata mazoea ili kuongeza ufanisi katika kuwatumikia wananchi.
   
  Kauli hiyo imetolewa leo na Msaidizi wa Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali Amin Mcharo wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya viwango vya kimataifa vya ukaguzi wa ndani kanda ya mashariki.
   
  Alisema kuwa wengi hawapendi mabadiliko na kusema kuwa ni vema kwa watu wa aina hiyo wakaangalia uwezekano wa kutafuta kazi au taalum nyingine ili kutochafua kazi ya ukaguzi.
   
  Mcharo alisema kuwa Ukaguzi wa Ndani ni taalum inayohitaji kwenda na mabadiliko kwa kuzingatia mabadiliko katika miongozo ya kimataifa na inayozingatia uadilifu.
   
  Aliongeza kuwa Tanzania haiwezi kubaki kama kisiwa na hivyo ni vema wakaguzi wake wa ndani wakawa chachu ya utekelezaji wa utendaji wa kazi unaozingatia viwango vya kimataifa vya ukaguzi wa ndani.
   
  Aidha Mcharo alisema kuwa Ofisi ya Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali imejipanga kufuatilia kwa karibu utendaji wa Wakaguzi wa Ndani ili kubaini kama utendaji wao unaozingatia maadili ya kazi na ikibainika wanakwenda kinyume na maadili haitasita kuishauri Mamlaka husika kuwaondoa katika nafasi zao.

older | 1 | .... | 47 | 48 | (Page 49) | 50 | 51 | .... | 3270 | newer