Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live

MWENYEKITI CHAMA CHA ALBINO TANZANIA (TAS) AIOMBA SERIKALI KUPITISHA ADHABU YA KIFO KWA WANAOWATENDEA ALBINO UNYAMA IWE FUNDISHO KWA WENGINE

$
0
0

Mwenyekiti wa chama cha watu wenye ulemavu Tanzania (TAS) "Tanzania Albino Society" ndugu Ernest Kimaya akizungumza kwa uchungu mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya (Pichani chini) kuelezea juu ya tukio la kinyama alilofanyiwa Maria Chambanenge (39) la kukatwa mkono wake wa kushoto kwa kile kinachodaiwa kwa imani za kishirikina kuwa ni kupata utajiri. Watuhumiwa waliohusika na tukio hilo ambao pia yupo mume wake na muathirika wameshakamatwa na polisi na kuonyesha mkono huo, taratibu za mashitaka zinaendelea ili haki iweze kupatikana. Mwenyekiti huyo ameiomba Serikali kufkiria adhabu kali kwa watuhumiwa kama ho ikiwepo kunyongwa ili fundisho kwa wengine na Albino waweze kuishi katika nchi yao kwa amani.
Mwenyekiti wa TAS akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa ofisini kwake. Kulia ni Katibu Mkuu wa chama hicho ndugu Mohammed Chanzi.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akizungumza kwa uchungu na kutoa onyo kali kuwa vitendo hivyo vya kinyama havitavumiliwa. Alitoa wito kwa wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kutokomeza vitendo hivyo.
Kabla ya kwenda kumtembelea mgongwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa aliandaa chakula kwa wageni wake.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya na msafara wake pamoja na viongozi wa chama cha Albino Tanzania (TAS) wakimfariji Mama Maria Chambanenge walipomtembelea katika hospitali kuu ya Mkoa Rukwa ambapo hali yake kwa sasa inaendelea vizuri japo ameongezewa ulemavu mwingine wa viungo kwa kukatwa mkono wake wa kushoto.
Mwenyekiti wa chama cha watu wenye ulemavu Tanzania (Albino) ndugu Ernest Kimaya akimfariji Mama Maria Chambanenge ambaye anaendelea kupatiwa matibabu katika hospitali kuu ya Mkoa Rukwa kufuatia kukatwa mkono wake wa kushoto na watu walioshirikiana na mume wake na ambao tayari wapo mikononi mwa polisi.

NA HAMZA TEMBA - OFISI YA MKUU WA MKOA RUKWA

Mwenyekiti wa chama watu wenye ulemavu wa ngozi Tanzania "Tanzania Albino Society" (TAS) ndugu Ernest Kimaya ameiomba serikali kupitia upya sheria ya haki ya kuishi kwa kuwapatia adhabu kali ya kifo wale wote wanaohusika kwa vitendo vya kinyama dhidi ya albino ikiwepo mauaji na ukataji wa viungo vyao wakiwa hai kwa kile kinachoaminika katika imani za kishirikina kuwa ni kujipatia utajiri.

Aliyasema hayo jana akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya ofisini kwake alipomtembelea akiongozana na viongozi wengine wa chama hicho kumpa pongezi zake za dhati kwa kile alichosema ni mfano wa kuigwa kwani tangu vitendo hivyo vianze hapa nchini kwa muda wa miaka mitano iliyopita ni Mkoa wa Rukwa pekee umefanikiwa kuwakamata wahalifu wa namna hiyo pamoja na kiungo husika kwa muda mfupi usiozidi siku tatu.

Amesema kuwa maalbino wamenyanyasika sana katika nchi yao kwa kukosa uhuru na amani kama watu wengine jambo ambalo ni kinyume na haki za binadam. "Watu waliokamatwa sio wa kuachiwa huru, wabanwe hata kuchomwa moto wataje wahusika wengine kwani mtandao wao ni mmoja na inatia uchungu sana kwa sisi maalbino" alisema mwenyekiti huyo.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Rukwa alimshukuru mwenyekiti wa chama hicho na viongozi wenzake kwa kufika Mkoani kwake kujionea hali halisi baada ya kuskika kwa matukio hayo ya kinyama kwa Albino wenzao na pia kuwashukuru wananchi na jeshi la Polisi kwa ushirikiano mzuri walioutoa kufanikisha watuhumiwa kutiwa mbaroni ili haki iweze kutendeka. Mkuu huyo wa Mkoa alisema vitendo kama hivo kaamwe havitaweza kuvumilika Mkoani kwake.

Kumekuwepo na matukio ya kusikitisha hivi karibuni ya ukatili kwa Albino ambapo mama mlemavu wa ngozi Maria Chambanenge (39) mkazi wa kijiji cha kavifuli katika Wilaya ya Sumbawanga alivamiwa nyumbani kwake usiku wa manane na kukatwa mkono wake wa kushoto na watuhumiwa ambao wameshakamatwa na jeshi la polisi na taratibu za mashitaka yao zinaendelea.

Vilevile katika bonde la ziwa Rukwa kata ya Milepa mtoto wa kiume mwenye ulemavu wa ngozi ‘albino” Mwigulu Matomange Magessa mwenye umri wa miaka saba ameshambuliwa na vijana watatu waliovaa kininja na kumkata mkono wake mmoja na kutokomea na kusikojulikana. Polisi wanaendelea na uchunguzi kuwabaini wahusika.
Matukio yote hayo yanahusishwa na wahalifu kutoka Mkoa jirani wa Mbeya ambapo vitendo hivi vya imani za kishirikina vimeshamiri.

KANISA LINGINE LACHOMWA MOTO ZANZIBAR

$
0
0
Na Mohammed Mhina, wa Jeshi la Polisi - ZANZIBAR 

WAKATI Watanzania wakiendelea kutafakari tukio la kuuawa kwa kupigwa risasi kwa Padre Evaristus Mushi, wa Kanisa Katoriki Zanzibar, watu wasiojulikana wamelishambulia kwa mawe na baadaye kulichoma moto Kanisa la Walokole la Shaloom lililoko eneo la Kiyanga kwa Sheha mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Kusini Unguja Zanzibar, ACP Augostine Olomi, amesema leo kuwa tukio hilo limetokea majira ya saa 9.30 usiku. Amesema moto huo ulizuka mara baada ya kikundi cha watu watatu kuonekana wakipita njia karibu na kanisa hilo na baada ya muda mlinzi wa kanisa hilo alisikia kanisa likishambuliwa kwa mawe juu ya makapaa.

Amesema baada ya mlinzi huyo kubaini kuwepo kwa hatari, alilazimika kukimbia kwenda kujificha lakini huku akiangalia kwa mbali kinachoendelea. Kamanda Olomi amesema kuwa wakati mlinzi huyo akiwa amejibanza mafichoni huku akiangalia kinachotokea, mara aliona moto ukiwaka ndani ya kanisa na ndipo alipopiga simu kwa kiongozi wa kanisa hilo naye kuwajulisha Polisi.

 Amesema Polisi walipofika hapo walisaidiana na wananchi kuuzima moto huo lakini wakati huo tayari ulishateketeza thamani za kanisa hilo na vitu vingine vilivyokuwa kanisani hapo. Kamanda Olomi amesema moto huo ungeweza kusababisha athali kubwa kama usingedhibitiwa mapema.

Hata hivyo amesema uimara wa dali lililotengenezwa kwa Gibsam kumesaidia kuunusuru moto huo kuunguza mapaa na kuliteketeza kabisa kanisa hilo. Amesema wakati uongozi wa kanisa hilo ukifanya tathimini ya harasa iliyopatikana kutokana na moto huo, Jeshi la Polisi limeanza kuwasaka washukiwa kwa kutafuta taarifa kwa raia wema na bado hakuna mtu ama watu waliokamatwa kuhusika na tukio hilo.

Hata hivyo Kamanda Olomi amesema Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na vikundi vya Ulinzi Shirikishi na Polisi Jamii, wataanza utaratibu wa kuyalinda makanisa yote ili kuzuia matishio mengine kama hayo.

anahamia mtaa wa saba.......

WOMEN CELEBRATIONS 2013 IMEWADIA

$
0
0
HAYA WANAWAKE TIKETI YA SHUGHULI YETU SASA ZIKO MTAANI NA KWA WALE MLIOKUWA MMEBOOK MEZA, NI NYIE KUSEMA MKO TAYARI ILI TUWEZE KUWALETEA TIKETI ZETU (RESERVED)
NA KAMA UNAHITAJI MEZA YA WATU KUMI 
SHOSTISTO TABLE  300,000/=
PIGA NAMBA
0784 418941 AU 0755  551077 (ULETEWE TIKETI)
KWA TIKETI ZA MOJA MOJA ZITAPATIKANA
SHEAR ILLUSIONS (MLIMANI CITY)
8020 FASHIONS (SINZA MAPAMBANO)
SILVER BOUTIQUE (POSTA AZAM)
VIATUZI (SEA VIEW UPANGA)
ROZELLA FASHIONS (KINONDONI)
MAZNAT BRIDAL SALOON ( MIKOCHENI )
JACKZ COSMETICS( KINONDONI TX MARKET)UTAPATA NA ZAWADI
FABAK FASHIONS (MIKOCHENI KWA WARIOBA) AMAYA BEAUTY SALOON & SPA (POSTA) ANGALIZOTIKETI HAZITOUZWA MLANGONI
                                                                       TIKETI HIZI HAPA

MAMA SALMA KIKWETE AENDELEA NA ZIARA YAKE MKOANI LINDI

$
0
0
 Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akisalimiana na  Muasisi wa Chama, Mohammed Matipa alipowasili Ofisi ya CCM, Tawi la Tulieni Kata ya Jamhuri Lindi mjini, leo Feb. 19, 2013.
 Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Mama Salma Kikwete akiimba wimbo wa 'Wanawake na Maendeleo', kabla ya kuhutubia mkutano wa hadhara katika kijiji cha  Tulieni, Kata ya Jamhuri Lindi mjini,  leo Feb 19, 2013.
 Wakereketwa wa CCM Mwajabu Abdulrahman (kulia) na Saida Mtopa, wakishangilia wakati Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Mke wa Rais Mama Salma Kikwete alipokuwa akihutyubia mkutano wa hadhara katika kijiji cha Tulieni, Kata ya Jamhiri, Lindi mjini leo, Feb 19, 2013.
 Wanachama wapya wa CCM wakila kiapo baada ya kukabishiwa kadi zao na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Mama Salma Kikwete, katika mkutano wa hadhara uliofanyika leo Feb 19, 2013, kwenye Kijiji cha Tulieni Kata ya Jamhuri Lindi mjini.
 Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, Kata ya Jamhuri Lindi mjini, wakimsikiliza Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Mke wa Rais, Mama Salma Kikwete (hayupo pichani), alipozungumza nao katika kikao cha ndani, kwenye Ofisi ya CCM, tawi la Tulieni katika Kata hiyo leo, Feb 19, 2013.
 Bi, Fatuma Jaluo (78) akifuatilia kwa makini msafara wa Mke wa Rais Mama Salma Kikwete ulipopita karibu na nyumbani kwake, katika kijiji cha Tulieni, Kata ya Jamhuri wilaya ya Lindi mjini leo, Feb 19, 2013.
 Kina Mama wa CCM, wakishiriki kula kiapo cha mwanachama wa CCM wakati wanachama wapya waliokabishiwa kadi na Mama Salma Kikwete walipokuwa wakipa, kwenye mkutano uliofanyika kijiji cha Tulieni,  kata ya Jamhuri wilaya ya Lindi mjini, leo Feb 19, 2013. Kutoka Kushoto ni Fatuma Mohamed, Aswila Ditopile na Zitta Maliyaga ambaye ni Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Lindi.
 Vijana 36 waliokuwa wanachama wa CUF na kuamua kuhamia CCM, wakimsiliza mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipohutubia mkutano wa hadhara jana, Feb 19, 2013, kwenye Kijiji cha Mitandi, Kata ya Mbanja, Lindi mjini.
Baadhi ya waandishi wa habari, waliopo kwenye ziara ya Mama Salma Kikwete mkoani Lindi, wakiwa wameketi kwenye mkeka wakati wa mkutano uliofanyika kijiji cha Tulieni, Kata ya Jamhuri Lindi mjini leo Feb 19, 2013. Kushoto ni Mwenyeji wa kijiji hicho, Khalfan Dimoso. (Picha zote na Bashir Nkoromo, wa Daily Nkoromo Blog).

Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania ziarani kutembelea Mahakama mkoani Tanga

$
0
0
Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Fakih Jundu (mwenye tai nyekundu) akiwa Katika msingi wa jengo la Mahakama ya Mwanzo Duga mkoani Tanga,Mahakama hii inajengwa kwa fedha za Mahakama. Mhe. Jaji Kiongozi yupo mkoani Tanga kujionea kasi ya utoaji haki na changamoto za kiutendaji na maendeleo ya miradi mbalimbali ya Mahakama. Waliosimama ni baadhi ya Watendaji wa Mahakama alioongozana nao Katika ziara yake. (Picha na Mary Gwera, Mahakama)

bei ya madafu leo

Rais Mwai Kibaki wa Kenya kuwasili nchini kesho kwa ya Ziara ya kitaifa ya siku mbili

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Kenya, Mhe. Mwai Kibaki anatarajia kuwasili nchini tarehe 20 Februari, 2013 kwa ziara ya kitaifa ya siku mbili. Ziara hiyo ya Mhe. Rais Kibaki inafuatia mwaliko wa Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Aidha, ziara ya Mhe. Rais Kibaki inafanyika kufuatia ziara ya Mhe. Rais Kikwete nchini Kenya mwezi Septemba, 2012.

Mhe. Rais Kibaki ambaye anatarajiwa kuwasili katika  Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere tarehe 20 Februari, 2013 saa 9.00 alasiri, atapokelewa na mwenyeji wake, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete.

Akiwa hapa nchini, Mhe. Rais Kibaki atafanya mazungumzo rasmi na Mhe. Rais Kikwete tarehe 20 Februari 2013 kabla ya kushiriki katika Dhifa ya Kitaifa itakayoandaliwa kwa heshima yake na Mhe. Rais Kikwete, Ikulu, Dar es Salaam.

Mhe. Rais Kibaki anatarajiwa pia kukutana na  Wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam tarehe 21 Februari, 2013, kuzindua Barabara ya Mwai Kibaki na kutembelea Gereza Kuu la Ukonga Jijini Dar es Salaam ili kujionea shughuli mbalimbali zinazolenga kuwarekebisha Wafungwa kuwa Raia wema na kuwapa mafunzo ya kiufundi kuwawezesha kujitegemea wanapomaliza vifungo vyao. Shughuli hizo ni pamoja na ushonaji, useremala na kilimo cha kisasa.

Mhe. Rais Kibaki ataondoka nchini tarehe 21 Februari, 2013 kurejea nchini kwake.

IMETOLEWA NA: WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA, DAR ES SALAAM.
19 FEBRUARI, 2013

FIFA YAPIGA NYUNDO MCHAKATO WA UCHAGUZI TFF

$
0
0


SHIRIKISHO la Kimaifa la Mpira wa Miguu (FIFA) limeahirisha uchaguzi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kutokana na mkanganyiko uliojitokeza katika mchakato wa uchaguzi huo.

Akizungumza na Waandishi wa Habari katika ofisi za TFF jijini Dar es Salaam leo mchana (Februari 19 mwaka huu), Rais wa TFF, Leodegar Tenga amesema FIFA imetuma barua ikiagiza mchakato wa uchaguzi usimame baada ya kupata malalamiko.

Amesema kutokana na mkanganyiko huo, FIFA katika barua yake ya leo (Februari 19 mwaka huu- imeambatanishwa) imeagiza mkutano wa uchaguzi wa TFF ambao awali ulipangwa kufanyika Februari 24 mwaka huu uahirishwe hadi hapo itakapotuma ujumbe wake nchini.

Ujumbe huo wa FIFA unatarajiwa kufika nchini katikati ya mwezi ujao (Machi) ambapo utafanya tathimini ya hali hivyo, kutuma ripoti yake katika shirikisho hilo na baadaye kutoa mwongozo wa nini kifanyike.

Rais Tenga amewaomba radhi wajumbe wa Mkutano Mkuu wa TFF kwa usumbufu uliojitokeza kutokana na uamuzi huo wa FIFA, hivyo kwa sasa hakutakuwa tena na mkutano huo mpaka hapo watakapopewa taarifa nyingi.

Amesema TFF inakaribisha kwa mikono miwili uamuzi huo wa FIFA kwa sababu ni chombo ambacho cha juu kimpira duniani, na hatua hiyo ina lengo la kuhakikisha kuwa kila mhusika katika mchakato huo wa uchaguzi anapata haki yake.

“Nia yetu ni kuona watu wanatendewa haki, na nia ya FIFA ni kutafuta ukweli. Hivyo wahusika (waathirika) wajiandae, watumie wakati huu kuandaa hoja zao ili FIFA wakifika wawasikilize, wapate maelezo ya kina kuhusu utaratibu na malalamiko yaliyotolewa,” alisema Tenga.

Rais Tenga amesema timu hiyo ya FIFA itakapofika yenyewe ndiyo itakayopanga izungumze na nani kwa wakati gani, hivyo ni vizuri waathirika na vyombo vyote vilivyohusika na mchakato wa uchaguzi wakajiandaa.

Amesema ilikuwa ni muhimu suala hili likatatuliwa katika ngazi ya FIFA kwa lengo la kuhakikisha uchaguzi utakapofanyika TFF inaendelea kuwa chombo kimoja badala ya kurudi katika migogoro iliyokuwepo huko nyuma.

“Nataka tubakie kama tulivyokuwa. Malumbano yaishe. Pangeni hoja, wakija hao waheshimiwa (FIFA) muwaambie. FIFA ni chombo cha juu, nafurahi wamekubali kuingia katika hili, kwani wana shughuli nyingi wangeweza kukataa,” amesema.

Kuhusu fursa ya kufanya marejeo (review) kwenye Kamati ya Rufani ya Uchaguzi inayoongozwa na Idd Mtiginjola ambayo aliielezea Jumamosi, Rais Tenga amesema kwa vile hicho ndicho chombo cha mwisho nchini katika masuala ya uchaguzi alishauriwa kuwa kingeweza kufanya review.

“Kwa vile hakuna chombo kingine, nikashauriwa kuwa kinaweza kufanya review. Katika utaratibu wa kutoa haki, uamuzi ni lazima uwe wa wazi kwa kutoa sababu. Nilidhani hilo linawezekana, kwani Mahakama Kuu hufanya hivyo. Kwa hili uamuzi wa Mtiginjola ni sahihi,” amesema Rais Tenga.

Kamati ya Mtiginjola iliyokutana jana (Februari 18 mwaka huu) ilitupa maombi ya review yaliyowasilishwa mbele yake na waombaji uongozi watano kwa vile hakuna kipengele chochote kwenye Katiba ya TFF na Kanuni za Uchaguzi kinachotoa fursa hiyo.

Waombaji hao walikuwa Jamal Emil Malinzi aliyeenguliwa kugombea urais wa TFF na Hamad Yahya aliyeondolewa kwenye kinyang’anyiro cha kuwania uenyekiti wa Bodi ya Ligi Kuu (TPL Board).

Wengine ni walioomba kuwania ujumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF na Kanda zao kwenye mabano; Eliud Peter Mvella (Iringa na Mbeya), Farid Salim Nahdi (Morogoro na Pwani) na Mbasha Matutu (Shinyanga na Simiyu).

SERENGETI FREIGHT FORWARDERS LTD WAZEE WA KAZI

$
0
0

  CONTAINER PRICE CUT!
40'HC TO DAR/MOMBASA NOW £1,950
20' CONTAINER TO DAR/MOMBASA £1,350
THIS IS MORE THAN £300 DISCOUNT!
THIS IS FOR MAERSK LINE, CMA-CGM, WEC LINE NA SAFMARINE

RATIBA YA MELI MPYA FEBRUARY 2013
 
FROM TILBURY 25/02/2013
VESSEL CUT OF IS 22/02/2013
FROM SHEERNESS 25/02/2013
VESSEL CUT OF IS 22/02/2013

TUNATOA HUDUMA ZA UKAGUZI WA MAGARI MOT/VOSA OFISINI KWETU
VEHICLE INSPECTION FOR KENYA A NOW CAN BE DONE IN OUR OFFICES

WENGI WAMUAGA MAREHEMU GRACE CHAO JIJINI DAR ES SALAAM LEO

$
0
0
Hatimaye Ndugu Jamaa na Marafiki waishio Jijini Dar es Salaam pamoja na Wafanyakazi wenzake na Marehemu Grace Mathew Chao leo wametoa heshima za Mwisho kwa Mwili wa Marehemu Mpendwa wao Grace katika zoezi lililofanyika Katika Hospitali ya Aga Khan Jijini Dar es Salaam ambako mauti yalimkuta Februari 17, 2013. Grace Chao alizaliwa Desemba 13, 1985.

Mwili wa Grace ulisafirishwa kuelekea Mazimbu Mkoani Morogoro ili kuwapa fursa wana jamii ya Mazimbu na Mzumbe ambako marehemu alizaliwa na kuishi zoezi ambalo litafanyika kesho Jumatano kabla ya Msafara kuelekea Marangu kwa mazishi. 

 Vijana mbalimbali wa Kundi la Home Sweet Home – Kimzumbe Mzumbe waishio jijini Dar es Salaam kwa shughuli za kazi na masomo walijitokeza kuuaga mwili wa Mwana Mzumbe mwenzao.
 Mama wa Marehemu Grace (kushoto) akiwa na mwana familia mwingine wakati wa zoezi hilo leo.


Ilikuwa ni majonzi sana katika tukio hili, kwa Vijana mbalimbali wa Kundi la Home Sweet Home – Kimzumbe Mzumbe waishio jijini Dar es Salaam walijitokeza kuuaga mwili wa Mwana Mzumbe mwenzao.

 Wafanyakazi wa CRDB Bank waliita kutoa heshima kwa Mwili wa Mfanyakazi mwenzao.
 Vijana wa Mzumbe Wengi sana walijitokeza kumuaga Grace katika safari yake hiyo ya Mwisho.
Marafiki na vijana wa Mzumbe wakimfariji kaka wa Marehemu Edwin Ndesamburo Chao (kulia) kufuatia msiba wa dada yake.
Picha na Father Kidevu blog.

SEMINA YA MAFUNZO YA UANZISHWAJI WA KITENGO MAALUM CHA KUFILISI MALI NA VITENDEA KAZI VINAVYOTOKANA NA VITENDO VYA KIHALIFU

$
0
0
Mtaalam wa masauala ya kufilisi mali na vitendea kazi vilivyotokana na uhalifu kutoka Afrika ya Kusini Bi. Hermione Cronje akitoa mada kwa maafisa wa idara mbalimbali za Serikali walioshiriki semina hiyo jijini Dar es saloaam  leo
Mkurugenzi Msaidizi idara ya Uratibu wa Kesi, Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka Ayubu Mwenda (wa kwanza kulia) akimsikiliza Bw. Jack Titsworh kutoka STAR Initiative wakati wa mafunzo ya kufilisi mali zilizotokana na uhalifu yaliyofanyika jijini Dar es salaam leo
Mkurugenzi wa Mashtaka Dkt. Eliezer M. Feleshi (katikati waliokaa) kwenye picha ya pamoja na Maafisa wa wizara na idara za serikali(waliosimama) waliohudhria semina ya mafunzo ya kufilisi mali zilizotokana na uhalifu

Ziara ya Waziri wa Habari, Vijana , Utamaduni na Michezo mkoani Arusha

$
0
0
 Waziri wa  Habari, Vijana , Utamaduni na Michezo Mh. Dkt. Fenella Mukangara (mwenye miwani ) leo amepokea taarifa ya kikundi cha Petu Saccos na kuongea na  vijana wa kikundi cha Youth Welding Group cha Sanawari  - Arusha (pichani) alipotembelea na kuangalia jinsi fedha za mfuko wa vijana zilizotolewa  wizara yake zilivyowanufaisha  vijana katika kujikomboa kimaisha na kujiajiri wenyewe.

 .Waziri  wa Habari , Vijana, Utamaduni na Michezo  Mh. Dkt. Fenella Mukangara (alivaa miwani ) akiongea na wana Saccos wa Petu kupitia kikundi cha Youth Welding group cha Sanawari  mkoani Arusha leo


 Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na .  Michezo Dkt. Fenella Mukangara (kushoto)leo akizungumza na Mjasiriamali Martha  Yusuph alipotembelea  Soko kuu Saccos Arusha na kuangalia wanufaika wa mikopo ya mfuko wa vijana uliotolewa na Wizara yake

 Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dkt. Fenella Mukangara (kulia) akipata maelezo kutoka kwa mjasiriamali wa  Krokon Saccos Asha Muhamed jinsi alivyonufaika  mkopo wa mfuko wa Vijana kutoka Wizara yake .

Waziri wa Habari, Vijana , Utamaduni na Michezo, Mh. Dkt. Fenella Mukangara (alievaa miwani) akiongea na wafanyakazi wa  TBC na Mafundi wa Star Times leo alipotembelea  Njiro mkoani Arusha  kuangalia shughuli mbalimbali. 

Picha zote na Mwanakombo Jumaa- MAELEZO 

MBUNGE WA UINGEREZA AKUTANA NA WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI DK. EMMANUEL NCHIMBI

$
0
0

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Dk Emmanuel Nchimbi akizungumza na Mbunge wa Uingereza, Lord Dholakia (katikati), ambaye amekuja nchini kwa ziara ya kikazi. Kulia ni Mkuu wa Jeshi la Magereza, Kamishna Jenerali John Minja. Waziri alibadilishana mawazo na mbunge huyo katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, kuhusu shughuli mbalimbali zinazofanywa na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Dk Emmanuel Nchimbi (wa tatu kutoka kulia) akizungumza na Mbunge wa Uingereza, Lord Dholakia (wa pili kutoka kulia), na maofisa mbalimbali wa ubalozi wa Uingereza nchini. Kulia ni Mkuu wa Jeshi la Magereza, Kamishna Jenerali John Minja, wengine ni maofisa wa wizara hiyo.
Mbunge wa Uingereza, Lord Dholakia (wapili kutoka kulia) akizungumza katika kikao hicho.
--
PICHA ZOTE NA-FELIX MWAGARA 
KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI  
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

MHE CHIKAWE AFANYA MAZUNGUMZO NA VIONGOZI MBALIMBALI OFISINI KWAKE LEO

$
0
0
Mheshimiwa Mathias Chikawe (Mb), Waziri wa Katiba na Sheria leo amekutana na viongozi mbalimbali kwa nyakati tofauti na kufanya nao mazungumzo kuhusu masuala mbalimbali ya kitaifa na kimataifa ambayo Wizara ya Katiba na Sheria inashughulika nao.
 Mheshimiwa Chikawe pia amefanya mazungumzo na Balozi wa Denmark hapa Nchini Bw Johnny Flentoe ambaye alimtembelea Waziri Ofisini kwake. Katika mazungumzo yao wameongelea ziara wa Waziri Mkuu wa Denmark itakayofanyika hivi karibuni na kuongelea mahusiano ya Denmark na Serikali katika nyanja mbalimbali. Mhe Chikawe aliishukuru Serikali ya Kifalme ya Denmark kwa kuwa mdau Mkubwa wa Sekta ya Sheria Nchini na kwa misaada yao kupitia Shirika lake la Maendeleo ya Kimataifa la DANIDA katika Programu ya Maboresho ya Sekta ya Sheria Nchini. Misaada yao imefanikisha kuboresha miundombinu ya taasisi za kisheria na kujenga mifumo imara ya sheria na kupanua wigo wa fursa za wananchi kupata haki.
 Mhe. Chikawe akiwa kwenye picha ya pamoja na Lord Dholakia (kushoto) na Bw Julian Chandler (Naibu Balozi wa Uingereza Nchini) mara baada ya kufanya mazungumzo ofisini kwa Waziri

 Mheshimiwa Chikawe amefanya mazungumzo na Lord Navnit Dholakia ambaye ni Naibu Kiongozi wa chama cha Liberal Democrats cha Uingereza na mjumbe wa All Party Parliamentary Group ambalo linajihusisha na kufutwa kwa adhabu ya kifo. Lord Dholakia yuko nchini kwa ziara ya kikazi na moja ya mambo aliyozungumza na Mhe. Chikawe ni mustakabali wa adhabu ya kifo Nchini na kushauri kuwa wakati umefika kwa Serikali ya Tanzania kuangalia umuhimu wa kuwepo au kutowepo kwa adhabu ya kifo na ameshauri uwezekano wa adhabu hiyo kufutwa. Kwa upande wake pamoja na mambo mengine Mhe Chikawe amemuhakikishaia Lord Dholakia kuwa kupitia


Mhe Chikawe akiwa kwenye mazungumzo na Bw. Bongani Majola ambaye ni Msajili wa Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari (ICTR

Waziri Chikawe pia amefanya mazungumzo na Msajili wa Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR) Bw. Bongani Majola ambaye alimtembelea Ofisini kwake leo, lengo likiwa ni kujitambulisha na na kuongelea shughuli mbalimbali za Mahakama, mafanikio na changamoto za Mahakama hiyo. Mhe Chikawe amemuhakikishia Msajili huyo kuwa Tanzania itaendeleza ushirikiano wake na Mahakama hiyo na kumuomba wawe tayari kusaidia pale ambapo sekta ya sheria itaona inahitaji msaada. Picha na 

Charles Joseph Mmbando

Barabara ya Old Bagamoyo Road kuitwa Mwai Kibaki Road kuanzia kesho

$
0
0
Hapa ni Msasani Kwa Warioba katika barabara ya Old Bagamoyo Road ambayo kuanzia kesho itaitwa Barabara ya Mwai Kibaki Road kwa heshima aliyotunukiwa kiongozi huyo wa Kenya na Hlmashauri ya Wilaya ya Kinondoni kufuatia ziara yake ya kitaifa ya siku mbili itayoanza kesho jijini Dar es salaam.

Kwa mujibu wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Saidi Meck Sadik, barabara hiyo yenye urefu wa kilomita 10.1 ni kuaniza kwenye mataa ya Moroccco karibu na makao makuu ya Airtel hadi mzunguko wa kuelekea Africana kule Mbezi Beach, mkabara na uwanja wa kulenga shabaha wa JWTZ.

Akiongea usiku huu, Mkuu huyo wa Mkoa amesema Rais Kibaki anatarajiwa kuwasili kesho saa 9 alasiri na kupkewa na mwenyeji wake Rais Jakaya Mrisho Kikwete, ambapo usiku atamwandalia dhifa ya kitaifa Ikulu.  Keshokutwa. Alhamisi, Rais Kibaki ataongea na wazee wa Dar es salaam katika ukumbi wa PTA ulioko viwanja vya SabaSaba barabara ya Kilwa Road. Pia atatembelea sehemu mbalimbali atazopangiwa katika ziara yake hiyo ambayo pia ataitumia kuwaaga Watanzania kwani muhula wake wa uongozi utafikia kikomo baadaye mwaka huu.

Kilaji cha kiasili cha Nzagamba chazinduliwa Mwanza

$
0
0
Na Mwandishi Wetu 

KIWANDA kipya cha kuzalisha bia ya asili ijulikanayo Nzagamba kimefunguliwa rasmi jana na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhandisi Evaristi Ndikilo. Kiwanda hicho ambacho kipo chini ya Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), kitajihusisha na kutengeneza bia hiyo ya asili, ambayo tayari imeanza kupokelewa kwa shangwe na wenyeji wa Kanda ya Ziwa. Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kiwanda hicho, Mhandisi Ndikilo alisema, amefarijika mno kuona kimejengwa Mwanza, kwani kitachangia kwa kiasi kikubwa mapato ya mkoa huo.

 “Niwapongeze sana wenzetu wa Nzagamba kwa kuja na wazo zuri kama hili la kuanzisha bia ya asili, tena wakaipa jina lenye asili ya Kanda ya Ziwa hususani kabila la Wasukuma. 

 “Hii imenifurahisha. Lakini kikubwa zaidi ni uamuzi wa kukiweka kiwanda hiki hapa Mwanza, kwa sababu mlikuwa na uwezo wakuamua kujenga mkoa mwingine wowote ule lakini mkatoa upendeleo wa dhati kwa mkoa wetu. Kwa uamuzi huo tunashukuru sana,” alisema. 

 Aliwataka wananchi kuhakikisha wanaonyesha uzalendo wa dhati kwa kupenda kutumia vitu vya asili, huku akitolea mifano ya nchi za Zambia na Malawi, ambapo bia za asili zinapewa nafasi kubwa. 

 Mkurugenzi wa Kiwanda cha Nzagamba, Kirowi Suma naye alisema watahakikisha wanazalisha bidhaa bora zaidi na kuwataka Watanzania wapende vitu vya asili ili kuonyesha uzalendo wao. 

 “Kwetu Nzagamba tunaamini tutaendelea kupigania ubora wa bidhaa yetu na naomba Watanzania watuunge mkono kwa kuipa nafasi bia hii ya asili,” alisema Suma. Nzagamba tayari imeanza kusambazwa, huku ikipokelewa vizuri zaidi na watumiaji, kutokana na kuwekwa katika ubora unaotakiwa.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Eng.Evalist Ndikiro akiwasili katika  kiwanda cha kinywaji aina ya Nzagamba jijini Mwanza
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Eng.Evalist Ndikiro akitembelea kiwanda cha kinywaji aina ya Nzagamba wa pili Kushoto ni Kilowi Suma Mkurugenzi wa tatu ni Nyamoronga John Meneja uzalishaji wa nne ni Ashraf Gugu meneja mauzo .
Kushoto ni Mkurugenzi wa kinywaji cha Nzagabwa Kiroi Suma akitoa maelekezo kwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Eng.Evarist Ndfikilo Kulia alipo tembelea kiwanda hicho katikati ni Mkuu wa kiwanda cha Nzagamba Bw.Patrick Phiri
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Eng.Evarist Ndfikilo Kulia alipo tembelea kiwanda hicho katikati 
Meneja masoko wa kampuni ya Bia nchini TBL Fimbo Butallah akishiriki kushika nyoka kwenye burudani ya uzinduzi wa kiwanda kipya cha bia ya Asili cha NZAGAMBA kilichopo mkoani Mwanza ambapo uzinduzi huo ulifanywa na mkuu wa mkoa wa Mwanza Mhandisi Evarist Ndikilo
Kikundi cha Burudani cha Bia ya Asili cha NZAGAMBA kilichopo mkoani Mwanza kikitoa burudani ya kipekeekwenye uzinduzi wa kiwanda kipya cha kutengeneza Bia ya Asli ambapo uzinduzi huo ulifanywa na mkuu wa mkoa wa Mwanza Mhandisi Evarist Ndikilo

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NJE AKUTANA NA MSAJILI WA MAHAKAMA YA ICTR

$
0
0
Mhe. Mahadhi (kulia) akiendelea na mazungumzo na Mhe. Bongani Majola, Msajili Mpya wa Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR) alipofika Ofisini kwa Mhe. Mahadhi kwa mazungumzo.


Mhe. Mahadhi akifafanua jambo kwa Mhe. Majola wakati wa mazungumzo yao. Wengine katika picha ni wajumbe waliofuatana na Mhe. Majola. Kulia ni Bw. Roland Konassi Amoussouga ambaye ni Mshauri Mwandamizi wa Sheria na Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mipango wa ICTR na kushoto ni Bw. Jerry Mburi, Afisa Sheria na Utawala wa ICTR.

Mhe. Majola akiendelea na mazungumzo na Mhe. Mahadhi.
Mhe. Mahadhi na Wajumbe wengine wa ICTR wakimsikiliza Mhe. Majola.

RAIS KIWEKTE AKUTANA NA WANACHAMA WA SIMIYU COMMUNITY BANK LEO IKULU

$
0
0
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na ujumbe wa Benki ya Jamii ya Simiyu (Simiyu Community Bank) uliomtembelea Ikulu jijini Dar es salaam leo Februari 19, 2013 kumwelezea mipango ya kufungua benki hiyo itayoshirikisha jamii katika mkoa huo mpya na ya jirani katika azma ya kumkomboa mjasiriamali na mkulima mdogo.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na ujumbe wa Benki ya Jamii ya Simiyu (Simiyu Community Bank) uliomtembelea Ikulu jijini Dar es salaam leo Februari 19, 2013
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na na ujumbe wa Benki ya Jamii ya Simiyu (Simiyu Community Bank) uliomtembelea Ikulu jijini Dar es salaam leo Februari 19, 2013.PICHA NA IKULU

ngoma azipendazo ankal

$
0
0
Mwaka 1994 mwanamama Millie Jackson aliwika na ngoma ya 'If Loving You Is Wrong'
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live




Latest Images

<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>
<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596344.js" async> </script>