Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109936 articles
Browse latest View live

TPCC 2013 DISTRIBUTORS GALA NIGHT

$
0
0

  Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Saruji ya Twiga, Pascal Lesoinne (kushoto), akikabidhi mfano wa hati kwa mmoja wa wasambazaji wa saruji ya TPCC, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Mwanza Huduma Co Ltd, Zully Manji baada ya kampuni hiyo kuibuka mshindi wa jumla wa wasambazaji bora wa saruji ya Twiga,  katika hafla ya Usiku wa Wasambazaji wa Twiga Cement jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Kulia ni Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo wa Twiga, Ekwabi Majigo. Alipewa zawadi ya tani 40 za saruji.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Saruji ya Twiga, Pascal Lesoinne (kushoto), akikabidhi cheti cha shukrani kwa mmoja wa wasambazaji wa saruji ya TPCC, Bi. Chaba Mavura ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa
kampuni ya Samks Traders Ltd, katika hafla ya Usiku wa Wasambazaji wa Twiga Cement jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Kulia ni Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo wa Twiga, Ekwabi Majigo.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Saruji ya Twiga, Pascal esoinne (kushoto), akikabidhi mfano wa hati kwa Mkurugenzi  wa kampuni ya V.G.K Ltd, Valence Msack kama uthibitisho wa zawadi ya tani 25 za saruji iliyopewa  kampuni hiyo baada ya kuibuka mshindi wa tatu wa wasambazaji bora wa saruji za Twiga, katika hafla ya Usiku wa Wasambazaji wa kampuni hiyo jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Kulia ni Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo wa Twiga, Ekwabi Majigo
 Baadhi ya wasambazaji wa saruji ya Twiga na wafanyakazi wa TPCC wakiselebuka katika hafla hiyo kwenye Hoteli ya Hyatt Kilimanjaro jijini Dar es Salaam.

Montage Charity Ball kufanyika Februari 22,Serena Hotel,jijini Dar

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Montage,Teddy Mapunda (katikati) akizungumza na Waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akitandaza kufanyika kwa tafrija maalum la harambee ya kuchangisha fedha kwa ajili ya kusaidia wanawake wenye matatizo ya afya hapa nchini kupitia mfuko wa Montage Charity Ball,itakayofanyika Februari 22 kwenye Hoteli ya Serena,jijini Dar es Salaam.ambapo malengo ni kukusanya kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 100 kwa ajili ya kusaidia matibabu ya Wanawake wenye matatizo mbali mbali.Mgeni rasmi katika Tafrija hiyo anatarajiwa kuwa Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA),Mke wa Rais Mama Salma Kikwete.Kulia ni Meneja Masoko na Mauzo wa Serena Hoteli,Seraphin Lusala na kushoto ni Mwenyekiti Kamati ya Maandlizi ya Tafrija hiyo,Barbara Hassan.
Meneja Masoko na Mauzo wa Serena Hoteli,Seraphin Lusala akifafanua jambo kwa wanahabari juu ya tafrija hiyo.
Mwenyekiti Kamati ya Maandalizi ya Tafrija hiyo,Barbara Hassan akizungumzia maandalizi yalivyofikia.Kushoto ni Mkurugenzi wa Fedha wa Kampuni ya Montage,Zainab Mkindi.

MATOKEO YA KIDATO CHA NNE YATANGAZWA LEO

$
0
0
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa (MB) leo ametangaza rasmi matokeo ya Mitihani ya Kidato cha Nne, maarifa na QT.

Jumla ya watahiniwa waliofaulu kwa Mujibu wa Matokeo hayo ni 23520 kuanzia daraja la I hadi la IV huku katika mchakato huo wasichana waliofaulu katika mchakato huo ni 7178 na wavulana ni 16342.Aidha Waziri Kawambwa amesema kuwa waliofaulu kwa daraja la kwanza ni 1641, daraja la pili ni 6495 na daraja la tatu ni 15426 na waliofeli ni 24903.

Shule bora ni pamoja na St. Francis Girl ya Mbeya, Marian Boys ya Bagamoyo, Feza Boys Dar es Salaam, Marian Girls Bagamoyo na Simini,hizo ndizo zilizopo kwenye tano bora huku shule nyingine ni Kanosa, Jude, St. Mary.

TAARIFA YA WIZARA KULAANI VITENDO VYA UKATILI DHIDI YA WATU WENYEULEMAVU WA NGOZI, WANAWAKE NA WATOTO

UHOLANZI YATILIANA SAINI MRADI WA KUIMARISHA AFYA YA MAMA WAJAWAZITO NA WATOTO ZANZIBAR

$
0
0
Katibu Mkuu Wizara ya Nchi ofisi ya Rais fedha, uchumi na mipango ya Maendeleo Zanzibar, Khamis Mussa (kulia) akitiliana saini na Balozi wa Uholanzi Nchini Tanzania, Dk. Ad Koekkoek mkataba wa mradi wa kuimarisha Afya ya Mama wajawazito na watoto katika Hospitali za Zanzibar.Makubaliano hayo yalitiwa saini Wizara ya Fedha Vuga mjini Zanzibar jana.
Katibu Mkuu Wizara ya Nchi ofisi ya Rais fedha, uchumi na mipango ya Maendeleo Zanzibar, Khamis Mussa (kulia) akibadilishana hati ya mkataba na Balozi wa Uholanzi Nchini Tanzania, Dk. Ad Koekkoek, mkataba huo ni wa mradi wa kuimarisha Afya ya Mama wajawazito na watoto katika Hospitali za Zanzibar.Makubaliano hayo yalitiwa saini Wizara ya Fedha Vuga mjini Zanzibar jana.
Balozi wa Uholanzi Nchini Tanzania, Dk. Ad Koekkoek akifafanua jambo katika utiaji wa saini mradi wa kuimarisha Afya ya Mama wajawazito na watoto katika Hospitali za Zanzibar. Makubaliano hayo yalitiwa saini Wizara ya Fedha Vuga mjini Zanzibar.(Picha na Haroub Hussein).

VIONGOZI WA MAHAKAMA YA KIMATAIFA YA MAUAJI YA KIMBARI YA RWANDA (ICTR) WAMTEMBELEA WAZIRI NCHIMBI OFISINI KWAKE

$
0
0
Msajili wa Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR), Bongani Majola (katikati) akizungumza na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi (kushoto) kuhusiana na mafanikio na changamoto mbalimbali ya Mahakama hiyo ambayo Makao Makuu yake yapo jijini Arusha. Kulia ni Msemaji wa Mahakama hiyo, Roland Amoussouga.
Msemaji wa Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR), Roland Amoussouga akimfafanulia masuala mbalimbali Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi (kushoto) wakati viongozi hao walipomtembelea waziri huyo ofisini kwake, jijini Dar es Salaam leo. Wa pili kutoka kushoto ni Msajili wa Mahakama hiyo, Bongani Majola. Kulia ni Mwanasheria wa mahakama hiyo, Jerry Mburi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi akizungumza ofisini kwake na Msajili wa Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR), Bongani Majola (katikati). Ziara hiyo, ambayo pia ilikuwa na lengo la msajili huyo kujitambulisha na kumsalimia Waziri Nchimbi, na kumuelezea shughuli mbalimbali zifanywazo na mahakama hiyo pamoja na kumuelezea changamoto mbalimbali zinazoikabili mahakama hiyo. Hata hivyo, Waziri Nchimbi aliahidi kushirikiana na mahakama wakati wowote itakapohitaji msaada kutoka ofisini kwake.

TAARIFA YA MSIBA DAR ES SALAAM NA MOROGORO

$
0
0

FAMILIA  ya Marehemu Mathew Ndesamburo Chao wa Mazimbu Morogoro, inasikitika kuwatangazia Msiba wa Binti yao Mpendwa Grace Chao kilichotokea leo asubuhi katika Hospitali ya Agha Khan jijini Dar es Salaam alikokuwa amelazwa kwa Matibabu.

Mipango ya Mazishi kwa sasa inafanyika nyumbani kwa dada wa Marehemu Yombo kwa Abiola jijini Dar es Salaam na Maiti itasafirishwa kesho Jumaane kwenda Mazimbu Morogo na kutolewa heshima kwa ndugu jamaa na marafiki waishio Morogoro Mjini na Mzumbe.

Jumatano Mwili wa Mpendwa wetu Grace Chao, utasafirishwa kutoka Mazimbu Morogoro kwenda Marangu Mamba kwa Makundi, Moshi,  kwa mazishi.

Mwana Mzumbe na Morogoro kwa Ujumla unaombwa sana kushirikiana na Familia ya Marehemu katika kipindi hiki kigumu cha Maombolezo.

Taarifa hii ni kwa Mujibu wa Kaka wa Marehemu, Edwin Chao.
            
Bwana Alitoa na Bwana Ametwaa Jina lake Lihimidiwe.

Mwanafunzi Makongo ashinda Vitz ya Valentine CampaIgn

$
0
0
Meneja Masoko na Mauzo wa kampuni ya Push Media Mobile, Rodney Rugambo akisisitiza jambo baada ya kupatikana kwa washindi wa ‘Valentine Campaign’ ambapo Mwanafunzi wa shule ya sekondari ya Makongo, Mudhir Ndonya alishinda gari aina ya Vitz lenye thamani y ash milioni 8. 
=======  ======  =======
MWANAFUZI wa  shule ya Sekondari ya Makongo, Mudhir Ndonya (20) ameshinda zawadi ya gari aina ya Vitz kufuatia shindano la siku ya wapendanao (Valentine campaign) lililomalizika Februari 14.

Mbali ya droo ya Vitz lenye thamani ya sh Milioni 8, pia washindi mbali mbali walipatikana katika siku ya mwisho wa shindano hilo lililofanyika kwenye ofisi za African Media Group (AMG). Meneja Mauzo na Masoko wa Kampuni ya Push Media Mobile Rodney Rugambo alisema kuwa Ndonya ameibuka mshindi  baada ya namba yake kuibuka ya kwanza katika shindano hilo lililodumu kwa takribani miazi mitatu na kutumia zaidi ya sh milioni 30.

Rugambo alisema kuwa wahsindi wengine katika droo hiyo ni Daudi Samson (22) ambaye pia ni mwanafunzi aliyejishindia Ipad, Tabia Lihonde (44) ambaye ni nesi anayefanya kazi Mtwara na kuibuka mshindi wa simu ya mkononi aina ya blackberry na Emmanuel Sanga aliyeshinda home theare.

Akizungumza kwa baada ya ushindi huo, Ndonya alisema kuwa amefurahi sana kwani ndoto yake ya kushinda gari imetimia. “Nilishiriki katika shindano kama washindani wengine, ndoto yangu ilikuwa ni kushinda, nashukuru nimeshinda na ushindi huu ni chachu ya kuendelea kushiriki katika mashindano mengine yajayo, ” alisema  Ndonya. Mbali ya Push Media Mobile, droo hiyo pia iliendeshwa na kituo cha televisheni cha Channel Ten na Radio ya Magic FM na kudhaminiwa na Alliance Insurance.


Tamko la Muadhama Askofu Mkuu Polycarp Kardinali Pengo juu ya mauaji ya PAdri Evarist Mushi

$
0
0
Muadhama, Askofu Mkuu Polycarp Kardinali Pengo wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, ambaye pia ni Rais wa Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu Katoliki Afrika na Madagascar, aongelea mauaji ya Padri Evarist Mushi huko Zanzibar Jumapili iliyopita, wakati alipoongea na waandishi wa habari jijini Dar es salaam leo Februari 18, 2013

KAMATI YA MTIGINJOLA YATUPA MAOMBI YA MAREJEO YA WAGOMBEA UONGOZI TFF

$
0
0


KAMATI ya Rufani ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) inayoongozwa na Idd Mtiginjola imetupa maombi ya kufanyia marejeo (review) uamuzi wake kama yalivyowasilishwa mbele yake na waombaji watano.

Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za TFF, Dar es Salaam leo mchana (Februari 18 mwaka huu), Mtiginjola ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo amesema wamepitia Katiba ya TFF na Kanuni za Uchaguzi za TFF na kubaini kuwa hakuna Ibara yoyote inayotoa fursa ya review kwa uamuzi ambao wameshaufanya.

Amesema Kanuni za Mwenendo wa Madai (CPC) katika mahakama za kawaida zinaruhusu Hakimu aliyefanya uamuzi katika kesi kufanya marejeo, lakini katika masuala ya mpira wa miguu hakuna fursa hiyo, hivyo hawawezi kujitungia kitu kipya kwani kazi yao ni kufanya uamuzi kwa kutafsiri Katiba na kanuni walizopewa na mamlaka ya uteuzi (TFF).

Waombaji watano waliokuwa wakitaka Kamati hiyo ifanyie marejeo uamuzi wake kutupa rufani zao ni Jamal Emil Malinzi aliyeenguliwa kugombea urais wa TFF na Hamad Yahya aliyeondolewa kwenye kinyang’anyiro cha kuwania uenyekiti wa Bodi ya Ligi Kuu (TPL Board).

Wengine ambao waliomba kuwania ujumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF na Kanda zao kwenye mabano ni Eliud Peter Mvella (Iringa na Mbeya), Farid Salim Nahdi (Morogoro na Pwani) na Mbasha Matutu (Shinyanga na Simiyu).

Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

Rais kikwete akutana na Pope theodors II,Kiongozi wa Kanisa la Orthodox ikulu jijini Dar leo

$
0
0
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha Kiongozi wa Kanisa la Orthodox Pope Theodoros II ikulu jijini Dar es Salaam leo.Kiongozi huyo wa Kanisa la Orthodox yupo hapa nchini kwa ziara ya kikazi ambapo pamoja na mambo mengine atatembelea miradi mbalimbali inayoendeshwa na kanisa hilo hapa nchini ikiwemo Zahanati na shule ya msingi Iringa pamoja na Hospitali ambayo inaendelea kujengwa huko Bukoba Mkoani Kagera.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na Kiongozi wa Kanisa la Orthodox Pope Theodoros II ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Kiongozi wa Kanisa la Orthodox Pope Theodoros II (wapili kushoto) mara baada ya kufanya mazungumzo na kiongozi huyo ikulu jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Askofu wa Mwanza na Bukoba Askofu Jeronymos. Nyuma ya Rais mwenye tai nyekundu ni mwenyekiti wa Hellenic society of Tanganyika Dimitris Mantheakis, na kulia ni askofu mkuu wa Dar es Salaam na mashariki askofu Dimistrious.picha na Freddy Maro

DW yaadhimisha miaka 50 ya uandishi wa habari uliotukuka

$
0
0

Deutsche Welle (DW) Idhaa ya Kiswahili  inaadhimisha miaka 50 ya idhaa yake ya Kiswahili chini ya maudhui ya “Maarifa na Mwamko“ katika hafla maalumu itakayofanyika jijini Dar es Salaam.

Kwa nusu karne, Deutsche Welle (DW) imekuwa ikitangaza taarifa na habari za uhakika kwa lugha ya Kiswahili kwa ajili ya wasikilizaji kwenye maeneo ya Mashariki mwa Afrika na eneo la Maziwa Makuu. 

Tarehe 22 Februari, saa 9.oo mchana katika jengo la Makumbusho ya Taifa, DW itasherehekea maadhimisho haya kwa hafla maalumu jijini Dar es Salaam, Tanzania, ikiwaleta pamoja wachambuzi wanaoheshimika katika mjadala wenye maudhui ya “ Maarifa na Mwamko kupitia Vyombo vya Habari“.

Hotuba maalumu zitatolewa kwa lugha ya Kiingereza na Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania, Klaus-Peter Brandes, na mkuu wa Idhaa ya Kiswahili ya DW, Andrea Schmidt.

“Idadi kubwa ya wasikilizaji wetu wanaishi hapa Tanzania, kwa hivyo lilikuwa chaguo la uhakika kwa ajili ya sherehe zetu,“ alisema Andrea Schmidt. “Kwa miaka 50 iliyopita, DW imejitolea katika utoaji wa habari zenye uwiano na taarifa za uhakika, ikiwapa watu wa Afrika ya Mashariki habari na uchambuzi wa kina juu ya masuala yenye uzito mkubwa.“

Uchambuzi utafanywa na jopo la majadiliano lililotayarishwa kwa msaada wa Shirika la Maendeleo la Ujerumani (GIZ) ofisi ya Dar es Salaam na utafanywa kwa lugha ya Kiswahili. Mohammed Khelef wa DW ataongoza majadiliano hayo akiwa na wataalamu wa vyombo vya habari wanaoheshimika nchini Tanzania, akiwemo Assah Andrew Mwambene (Mkurugenzi wa  Idara ya Habari, Maelezo), Mohamed Abdulrahman (DW), Jenerali Ulimwengu (Mwandishi wa habari), Valerie Msoka (Mkurugenzi wa TAMWA) na Maggid Mjengwa (Mtaalamu wa mitandao ya kijamii). 

Wahudhuriaji watakuwa pia na fursa ya kukutana na kubadilishana mawazo na waandishi wa DW kutoka Rwanda, Burundi, Uganda, Kenya, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Tanzania, ambao wanahudhuria hafla hiyo katika jengo la Makumbusho ya Taifa.

Katika kufanya taarifa ziwe na maana Idhaa ya Kiswahili ya DW hutangaza mara tatu kwa siku kwa ajili ya maeneo ya Afrika ya Mashariki na Maziwa Makuu. Ikishirikiana na redio washirika
zinazotangaza kwa masafa ya FM kwenye eneo hilo, DW inaweza kuwapa wasikilizaji habari zenye uwiano juu ya kile kinachoendelea ulimwenguni kwa ujumla na hasa yale yanayoendelea barani Afrika. Ili kupata mtazamo huu wa kimataifa, timu ya waandishi wa habari kutoka mataifa matano ya Kiafrika inafanya kazi na mtandao wa wawakilishi wetu walioko kote Afrika Mashariki na Kati.

Idhaa ya Kiswahili ni moja ya idhaa mashuhuri sana za DW. DW ina kipindi cha kuelimisha kilichoshinda tuzo kadhaa cha “Noa Bongo! Jenga Maisha Yako!“ na makala za aina mbalimbali zinazogusa masuala ya afya, haki za binaadamu, mazingira, wanawake na maendeleo, vijana na mitindo ya maisha na utamaduni.

PRESS: WWW.DW.DE/PRESS
INSIDER BLOG: BLOGS.DW.DE/INSIDER

Article 1

$
0
0

Waziri wa Nishati na Madini wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Prof. Dk Sospeter Muhongo, anatarajia kufanya ziara ya kikazi nchini Uingereza kuanzia tarehe 25 hadi 28 Februari 2013.

Akiwa London Mhe. Waziri angependa kukutana na Watanzania waishio Uingereza kuzungumzia maendeleo ya sekta ya nishati na madini Tanzania na pia kubadilishana nao mawazo kuhusu maendeleo ya sekta hiyo.

Ubalozi wa Tanzania, London unapenda kuwakaribisha watanzania siku ya Jumanne tarehe 26, Februari 2013,Ubalozini saa 11 Jioni. Anuani ya Ubalozi ni 3 Stratford Place, W1C 1AS, London

 Wote mnakaribishwa.

Masahihisho ya punguzo la gharama za kuunganisha umeme mikoa ya lindi na mtwara

$
0
0

My dear Michuzi,

Greetings, napenda kumrekebisha mwandishi wa habari aliyeandika habari kwamba gharama za  kuunganisha umeme zilikuwa Sh milini mbili na sasa zimepunguzwa na kuwa sh laki nne na elfu arobaini. Hiyo si sahihi gharama halisi kwa sasa ni kama ifuatavyo;

Katika umbali usiozidi mita 30., 

Bei ya punguzo  itakuwa ni shilingi 99,000/- kwa umeme wa njia moja na tatu. Hii ni tofauti na bei ya zamani ambayo ilikuwa ni shilingi 455,104.76 kwa njia moja na 912,104.74 kwa njia tatu. 


Punguzo hili limetolewa na serikali ili kuhakikisha kuwa wananchi wengi katika mikoa hiyo  wanapata huduma ya umeme ili kuharakisha maendeleo katika mikoa ya Lindi na Mtwara.

Badra Masoud

Msemaji TANESCO

adha ya kuingia barabara ya njia moja

$
0
0
Huyu mdau, ambaye bila shaka ni mgeni jijini Dar es salaam, anajikuta katika hali ngumu baada ya kuingia mtaa wa Samora akitokea kaskazini kuelekea kusini. Bahati nzuri madereva wenzake walimstahi na kusimama kumpisha ili ageuze na kuingia mtaa wa Zanaki. Bahati nzuri pia kina Ras Makunja hawakuwepo wakati huo la sivyo wangemkunja...

ijue clouds fm ilivyoanza mpaka ilipo hivi sasa.

Vodacom Foundation yatoa msaada wa kompyuta 10 zenye thamani ya Milioni saba kwenye shule ya sekondari ya wasichana ya MT.Theresa wa Avila

$
0
0
Mkuu wa Vodacom Foundation Bw.Yessaya Mwakifulefule na Meneja biashara wa kitengo cha Mahusiano Vodacom Bi.Lilian Kisamba,wakimkabidhi kompyuta kati ya 10 zenye thamani yua shilingi Milioni 7,Mwl.Joyce Martin wa shule ya sekondari ya wasichana ya MT.Theresa wa Avila.Iliyopo Mkoa wa Shinyanga Wilaya ya Kahama.
Mkuu wa Vodacom Foundation Bw.Yessaya Mwakifulefule (kushoto)akimkabidhi Bi. Jacquline Augustine moja ya kompyuta kati ya 10 zenye thamani ya Milioni 7 zilizotolewa kwa msaada na Vodacom Foundation kwenye shule ya sekondari ya wasichana ya MT.Theresa wa Avila,anaeshuhudia kulia ni Meneja biashara wa kitengo cha Mahusiano Vodacom Bi.Lilian Kisamba.
Wanafunzi wa shule ya sekondari ya wasichana ya MT.Theresa wa Avila.Iliyopo Mkoa wa Shinyanga Wilaya ya Kahama,wakifatilia kwa ukaribu makabidhiano ya kompyuta kati ya 10 zenye thamani ya Milioni 7 zilizotolewa msaada na Vodacom Foundation.
Baadhi ya wananchi na wazazi wa wanafunzi wa shule ya sekondari ya wasichana ya MT.Theresa wa Avila.Iliyopo Mkoa wa Shinyanga Wilaya ya Kahama,walifika kushuhudia makabidhiano ya ya kompyuta kati ya 10 zenye thamani ya Milioni 7 zilizotolewa na Vodacom Foundation mwishoni mwa wiki.

TTCL GETS NEW CHIEF EXECUTIVE OFFICER (CEO)

$
0
0
Tanzania Telecommunications company Limited Board of Directors confirmed Dr. Kamugisha Kazaura as a Chief Executive Officer (CEO) of the Company effectively from yesterday. 

Dr. Kazaura replaces Mr. Said Amir Said who had been an Acting CEO and reached his retirement age recently. 

Before his appointment, Dr. Kazaura was TTCL’s Chief Technical officer (CTO). The Board of Directors calls upon all TTCL Staff and Management to give support to the new CEO and to build team spirit and to commit to reinvigorate the TTCL, bring efficiency and increased cost effectiveness and take the Company to much higher heights.

 The Board emphasizes by saying “let us move forward together as a united team and committed to promoting good Governance, transparency and inclusiveness.” 

Dr. Kamugisha Kazaura (42) holds Master and a PhD of Science degree in Information and Telecommunications Studies from the University of Waseda, Tokyo-Japan.

Dk. Kamala awa mwenyekiti mabalozi wa Afrika Ubeligiji

$
0
0
Balozi Joel M Nheleko wa Swaziland nchini Ubeligiji, ambaye alikuwa Rais wa Mabalozi wa Afrika nchini Ubeligiji aliyemaliza muda wake, akimkabidhi Balozi wa Tanzania Dk. Diodorus Kamala mfuko wenye vitendea kazi kama ishara ya kumkabidhi Urais wa Mabalozi wa Afrika Ubeligiji jijini Brussels juzi.

Balozi wa Tanzania nchini Ubeligiji, Dk. Diodorus Kamala ameteuliwa na mabalozi wa nchi za Africa wanaoziwakilisha nchi zao nchini humo kuwa Mwenyekiti wao.

Balozi Kamala amepokea uenyekiti huo kutoka kwa Balozi wa Swaziland nchini Ubeligiji, Joel Nheleko aliyemaliza muda wake. Tanzania itashikilia kiti hicho kwa muda wa miezi sita hadi Julai 1, 2013.

“Nimefurahi kupewa heshima hii, na naamini nitaitumia fursa hii kufahamiana vizuri na mabalozi wenzangu na kuvutia fursa za kiuchumi kwa nchi yetu,” alisema Balozi Kamala.

Wakati huo huo, juzi mabalozi wa nchi tano zinazozunguka Bonde la Ziwa Tanganyika, walimchagua Balozi Kamala kuwa mwenyekiti wao.

Nchi wanachama wa Bonde la Ziwa Tanganyika ni Burundi, Rwanda, Tanzania, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo na Zambia.

Nchi hizi zimeunganisha nguvu kutafuta wafadhili kwa ajili ya maendeleo ya Bonde la Ziwa Tanganyika, ambapo eneo la bonde hili lenye wakazi wastani wa milioni 40 wanalenga kuliendeleza kwa ajili ya kujenga miundombinu, kurahisisha usafiri na usafirishaji, kujenga reli mpya na kuendeleza utalii.

Chini ya mpango huu wanalenga pia kuboresha viwanja vya ndege vya nchi wanachama vya Mbala, Kalemie, Bujumbura, Kigoma na Kasanga kwa nia ya kurahisisha usafiri wa anga katika ukanda huu.

Dk. Kamala amekabidhiwa jukumu la kuratibu mpango huu na kwa pamoja watatafuta fedha kutoka kwa wafadhili kwa ajili ya mradi huu.

ALLY REHMTULLAH ALONGA NA VIJIMAMBO

Viewing all 109936 articles
Browse latest View live




Latest Images