Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 48 | 49 | (Page 50) | 51 | 52 | .... | 3272 | newer

  0 0

  Ukingoni mwa Ziwa Nyasa- Revo Meza-Imeandikwa na Freddy Macha .

  Ndesanjo Macha Ukingoni mwa Ziwa Tanganyika- picha ya Revocatus Meza, Desemba 2012. Wimbi la “blogging” liliikumba dunia kati ya 1995 hadi 1998 na kuanza kumea kwetu Tanzania kupitia mwanahabari Ndesanjo Macha miaka kumi iliyopita. Wakati Ndesanjo anaanza kublogu si wengi tuliomwelewa. Nakumbuka alivyokua akiniongelea juu ya fani hii kwa hamasa kwenye 2002. Baadaye kidogo aliendesha Jikomboe, blogu lililokua na taswira ya majani mabichi ya ukoka. Enzi hizo hakukua na hata senti moja aliyoichuma. Ndesanjo Macha- mwasisi wa blogu Tanzania Ndesanjo alikua akisema blogu ni dunia ya kesho ya mawasiliano. Wakati huo vyombo vikubwa vya habari nchi zilizoendelea vilianza kuona umuhimu wa blogu vikaanza kuunda idara pembezoni mwa tovuti zake mama. 
  Goats feeding on rubbish
  Kwetu wenye magazeti wengi hawakupenda wanablogu;waliwaona washindani. Mwaka ambapo wanablogu wetu walianza kuchomoza ilikua 2006 baada ya kifo cha wapenzi wawili wa Kitanzania waliouliwa kinyama Marekani. Blogu la Michuzi (ambalo halikua maarufu kama leo) na Radio Butiama (inayojulikana kwa jina Podcast) zilisimama dede kutangaza habari hizo. Hapo ndipo miye binafsi nilipoanza kuona namna wanablogu walivyokuwa na mwendo mkali - zaidi ya vyombo vya habari vya kijadi. Niliingia rasmi uwanjani mwaka 2007- nikisaidiwa na Ndesanjo na wanabloga wengine walionitangulia; akina Simon Kitururu, Jeff Msangi (Bongo Celebrity) mathalan. Nilichogundua siku za mwanzo ni kwamba Blogaz husaidiana sana. “Ukiwa mbinafsi huendelei kama Bloga” alisisitiza Ndesanjo. Mbuzi wetu Bongo wakila kila aina ya takataka mitaani. Nyama yake tamu. Lakini je, ina nini kinachotudhuru tusichokijua? Nilipiga picha hii, Zanzibar, mwaka 2011.  
  Leo Jikomboe na ule ukoka havipo tena. Ndesanjo, mwasisi wa blog za Kiswahili duniani, anafanya kazi shirika la habari- Global Voices. Kati ya mamia ya waandishi wa shirika hilo la kimataifa, Mtanzania huyu anaongoza kwa habari asilia za uchambuzi zaidi ya 4,200 . Tofauti ya mtu kama Ndesanjo na baadhi ya blogaz ni kwamba yeye kiasilia ni mwanahabari hivyo anachanganya ujuzi na mitindo hii miwili ya kusanifu matukio. Si ajabu mwaka jana Ndesanjo alishinda tuzo la Mwanablog bora wa Afrika.
  Lugha ya blogaz na vyombo asilia vya habari zi tofauti. Wanahabari lakini ni watu waliosemea sawasawa kazi zao na kufuata utaratibu wa lugha, kusahihisha na kuhariri kazi. Bloga ni mtu yeyote tu mitaani au kijijini anayetaka kuelezea jambo. Kuhe -samaki- by Revo MezaSamaki aitwaye Kuhe katika Ziwa Tanganyika. Picha nimeletewa na mwandishi Revocatus Meza. Mvua ya blogaz Tanzania imejaza bahari safi tena ya faraja. Blogaz ni wengi tena wa kila rangi na jinsia; wanatupasha matukio kila sekunde! Wakati tukianza, wanawake hawakua wengi. Mwaka jana mshindi wa Blogaz bora Bongo alikuwa Mwanamke na Nyumba. Nyingine zimekuwa makutano au baraza la maoni na malumbano muhimu- mfano Jamii Forums, iliyoundwa 2006. Zipo zenye mafunzo mazito- angalia Al Hidaaya inayofunza masuala ya Kiislamu na Korani tutaelewana n’na maana gani. Zile zenye kurasa moja (kama zangu) zimegeuzwa viwanda vidogo; mathalan ya Maggid Mjengwa ambayo ni kijigazeti cha ajira. Ajira zinazowahudumia na kuwafariji wanahabari wake. Mara nyingine zina maudhi maana hata kuzifungua zinakua shida maana matangazo yamejazana pale juu kiasi ambacho si tena habari bali duka. Ama kweli mtandao umekuwa biashara. Uzuri upo ndiyo; ubaya tuuseme pia! Msukuma Mkokoteni-Magomeni 2009-pic by F MachaMsukuma mikokoteni akitotwa jasho saa za alasiri, mitaa ya Magomeni Mapipa. Niliipiga picha hii mwaka 2009, Dar es Salaam. Watanzania tunakwenda na wakati si uongo. Maana ukitazama wenzetu nchi zilizoendelea wanaelekeza kila jicho katika mtandao na inteneti. Maduka makubwa makubwa asilia nchi magharibi yanapata hasara na kufunga virago vyake. Mwishoni mwa mwaka jana asilimia 25 ya biashara zote nchi zilizoendelea zilitokana na makampuni yenye mauzo ya mitandaoni – yakaingiza dola bilioni 1.7! Linaloongoza sasa hivi ni Amazon inayouza kila kitu bei rahisi na kwa ufanisi zaidi kuliko maduka asilia. Makisio ya faida ya Amazon mwaka jana yalikuwa dola bilioni 63. Uingereza duka maarufu la muziki, sinema na vitabu- HMV- lilipunguza wafanyakazi mwezi jana na tetesi ni kuwa wameshafifia kibiashara. Ama kweli mtandao ndiyo soko mzazi wa biashara leo na kesho (kama alivyosema Ndesanjo) na wanabloga wetu wanakwenda na wakati. Mwandishi gwiji wa Kiswahili Ebrahim Hussen aliwahi kuandika “wakati ukuta ukipigana nao utaumia.” Ndiyo maana wafanya biashara wanatangaza bidhaa kupitia blogu. Ndiyo hali halisi ilivyo. [caption id="attachment_1655" align="aligncenter" width="500"]Kitabu kipya cha Prof Said Ahmed Kitabu kipya cha Prof Said Ahmed[/caption] Kitabu kipya cha Mwandishi nguli, Profesa Said Ahmed- Mhanga Nafsi Yangu- ambacho kinamwangalia mwanamke wa Kibongo anayekwenda kusoma ughaibuni. Kimetolewa na Sasa Sema (Longhorn) wa Kenya,2012. Ila tutathmini zaidi hilo... Blogu zilibuniwa kutangaza mambo na kadhia ambazo hazipo ndani ya vyombo habari mama na runinga. Zilibuniwa kumfaidisha mwananchi yeyote wa kawaida akibeba kamera na simu yake mkononi akaeleza habari za pale anapoishi. Hicho ndicho chanzo... Kama hukua na nafasi kuna Twitter ambayo ni fupi zaidi (maneno 30 tu!). Zana hizi ni muhimu sana kwa jamii ya leo. Hizi ni “habari za raia wa kawaida” . Umuhimu wa Blog, Twitter na You Tube umeonekana pale yalipotokea machafuko na harakati mbalimbali duniani kama Tunisia, Misri, Libya na Mashariki ya Kati nzima miaka miwili iliyopita. Dhoruba za mauaji ya mwanahabari Daudi Mwangosi zilisambaa dunia nzima haraka kutokana na uwezo huu muadhama. Nguzo zake ndizo hizo. Google ambaye hulipa matangazo ya biashara kutokana na “maudhui ya habari” husisitiza wanablogu na waandishi kuwa wa kweli na kutochezea kazi za wenzao. Kwetu Bongo hapana. Miaka ya karibuni makampuni makubwa makubwa na mabenki kama National Microfinance (NMB) yanasaidia kuwekezea wajisiria mali wadogo wadogo (yaani Blogaz). Mara nyingi makampuni haya hayaangalii kama wanablog hawa wananukuu kazi za wenzao, wanaandika mambo yao wenyewe au wanakopi tu na kubandika. Logo- Sema Ndiyo-2Nembo ya kutetea haki za wanyama pori wanaouliwa ovyo. Kampeni hii inaongozwa na Kidon Mkuu Ngoille Mkuu, wa Arusha. Dili zinapatikana kwa kujuana juana, mathalan. Bahati mbaya kumezuka mtindo wa wanablogu wengi kutwaa kazi na picha za wenzao bila kuandika zimetoka wapi. Ukilinganisha sasa hivi Blogu zetu Tanzania ni tofauti sana na za nchi nyingine maana wengi hatuandiki vitu tulivyovibuni au tunavyoviona. Mmoja akishaandika tu basi wengine wote tunakopi na kubandika tu bila kuangalia sana kazi ikoje. Siku Google na mashirika miliki ya hizi blogu wakifahamu yatakua mengine. Kwa sasa tunajificha ficha tu. Saria akikochi vijana DodomaMwanamichezo na mwanahabari Israel Saria akiwa kazini na vijana Dodoma miaka ile ya Themanini. Niliongea na Israel Saria, anayeendesha blogu-tovuti la Michezo Tanzania (Tanzania Sports) tokea London karibuni. Saria ameendesha shughuli hii toka 2005 na anafadhiliwa na NMB. Mbali ya kuwa mtangazaji wa michezo BBC, Saria ni mwalimu rasmi wa mchezo wa mpira wa nyavu aliyekuwa kocha miaka mingi Tanzania. Alipendekeza wawekezaji kuangalia thamani ya blog mbalimbali kabla ya kuzipachikia matangazo: “Hebu linganisha blogu zetu na za majirani wa Kenya. Wakenya wengi huandika mambo wanayobuni. Sisi tunakosa ubunifu na uhalisia. Mwenzetu akiandika habari- baada ya dakika tano –mabloga wengine wote tunainukuu na kuitangaza ikiwa imejazana makosa. Tunalipua tu. Hatuna hata muda wa kuichunguza au kuihariri. Tunadhani kublogu ni suala la umaarufu na kuonekana kwamba na mimi nipo; eti sitaki nionekane kwamba nimekosa ile habari iliyotangazwa na mwenzangu!” Saria anaongeza kusema kwamba wengi wetu tunashindwa kutambua kwamba Google huwa wanajua na kuangalia kazi asilia. “Ukishatundika tu kazi yako, baada ya dakika chache tayari inasajiliwa kama ni mali yako. Yeyote anayeinukuu au kuitumia hatambuliwi kama mwenye hiyo kazi.” Mabloga wengi Bongo basi wanarudia rudia tu kazi za wenzao kwa kuzitapika na kuzitafuna kama ambavyo ng’ombe wanavyofanya baada ya kula majani. Matokeo baadhi ya blogu leo zimegeuka mabango ya matangazo badala ya kazi muhimu za kifasihi. Zipo blogu nyingi zinazobuni mambo- lakini pia zipo ambazo zinacheza tu. MaandaziPicha ya Maandazi toka tovuti la Taste of Tanzania. Picha ya Miriam Rose Kinunda... Miriam Rose Kinunda anayeendesha tovuti-blogu ya mapishi (Taste of Tanzania) amekuwa akisanifu blogu na kusaidia wenzake kuzijenga toka 2004. Anasema ni mara nyingi sana ambapo kazi na picha zake zimetumiwa bila idhini. “Awali nilikua nikiblogu Kiswahili na Kiingereza, lakini kutokana na huu wizi wa kazi, nimeondoa kabisa kitengo cha Kiswahili nikabakisha Kiingereza kwa wasomaji wa kimataifa.” Miriam ambaye karibuni atatoka na kitabu chake cha mapishi anataja mfano ambapo tovuti moja maarufu ya Kenya iliiba kazi na picha zake. Akaamua kuwapigia simu. “Baada tu ya dakika tano, jamaa walinitumia barua pepe kunitaka radhi. Walionyesha namna walivyo waungwana.” Miriam Rose KitundaMiriam Rose Kinunda Je nini kifanyike? Saria na Bi Kinunda wanashauri wawekezaji (mathalan benki inayowafariji wanablogu kama NMB) kufadhili na kusaidia tu wale wanaokua wabunifu na wanaofuata kanuni za fani hii muhimu katika jamii. KigodaKigoda nyumbani kwa mpigania utamaduni wetu na mfanyabiashara mashuhuri wa Dar es Salaam, Mwafrika Merinyo anayeendesha shughuli za Afrika Sana. Nilipiga picha Novemba 2011. Makala hii iliandikwa pia kwa Kiingereza katika safu ya Mwandishi gazeti la Citizen mwezi jana

  0 0

  Na Maelezo Zanzibar 
   Mamia ya Wananchi wa Zanzibar leo wameshiriki Mazishi ya Padri Evaristus Mushi aliyeuwa kwa kupigwa Risasi na Watu wasiojulikana ambayo yamefanyika katika kijiji cha Kitope Wilaya ya Kaskazini B,Unguja. Katika mazishi hayo Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein, Makamo wa Kwanza wa Rais Maalim Seif Shariff Hamad,Viongozi wa Serikali na Vyama vya siasa walihudhuria. 

   Akitoa salamu za Serikali katika Mazishi hayo Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais Mohammed Aboud Mohammed alisema Serikali imeguswa sana na kifo cha Padri huyo na kuongeza kuwa itahakikisha waliohusika na tukio la mauji hayo wanakamatwa na kufikishwa katika vyombo vya sheria. 

  Kwa upande wake Askofu wa Kanisa la Anglikacana Michael hafidh amewataka Waamini wa dini ya kikristo kuwa watulivu bila kulipiza kisasi bali waiachie Serikali kufanya kazi yake ili kuwabaini waliopoteza Uhai wa Marehemu huyo. 

   Awali Mazishi hayo yalitanguliwa na Misa takatifu ya kumuombea Marehemu iliyoendeshwa na Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo kuu la Dar es Salaam Muadhama Policarp Kadinali Pengo katika Kanisa la Minara Miwili Mjini Zanzibar. 

  Padri Mushi alifariki dunia Februari 17 baada ya kupigwa risasi na watu wasiojulikana wakati akielekea Kanisani kuendesha Misa ya Asubuhi katika Kigangwe cha Mtakatifu Teresia eneo la Beit El Raas mjini Unguja Enzi za uhai wake Padri Mushi alikuwa Msomi wa Shahada ya Uzamivu ya Elimu ya Ushauri nasaha aliyoipata nchini Marekani ambapo umauti ulimkuta akiwa anaelekea kuendesha Ibada ya Jumapili ya kwanza ya Kwarezma. Padri Evarist Mushi wa Kanisa la Minara Miwili mjini Zanzibar alizaliwa June 15, 1957 Mkoa wa Kilimanjaro akiwa ni mtoto wa nne katika familia ya watoto sita ya Mzee Mushi. 
  Rais wa Zanbzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt,Ali Mohamed Shein,(katikati) akifuatana na Askofu wa Kanisa  Katoliki Jimbo la Zanzibar Augustino Shao, wakielekea katika Mazishi ya Padri Evaristus Gabriel  Mushi,aliyezikwa katika viwanja vya kanisa la Kitope,Wilaya ya Kaskazini B Unguja
  Vijana waumini wa Dini ya Kikiristo wakiteremsha jeneza lenye mwili wa marehemu  Padri Evaristus Gabriel  Mushi,katika kaburi alilozikwa  leo katika viwanja vya kanisa la Katoliki la Kitope,Wilaya ya Kaskazini B Unguja,marehemu alifariki kwa kupigwa risasi Jumapili iliyopita na watu wasiojulikanwa
  Rais wa Zanbzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt,Ali Mohamed Shein,(katikati) akitia udongo  katika kaburi la Marehemu  Padri Evaristus Gabriel  Mushi,wakati wa mazishi yake yaliyofanyika leo  katika viwanja vya kanisa la Kitope,Wilaya ya Kaskazini B Unguja
  Waziri  wa  Mambo ya Ndani ya Nchi Emanuel Nchimbi ,akitia udongo  katika kaburi la Marehemu  Padri Evaristus Gabriel Mushi,wakati wa mazishi yake yaliyofanyika leo  katika viwanja vya kanisa la Kitope,Wilaya ya Kaskazini B Unguja
  ASkofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam Muadhama Policup Kadinari Pengo,kwa pamoja na maaskofu wengine wakichomeka Msalaba katika kaburi la marehemu  Padri Evaristus Gabriel Mushi,aliyezikwa leo  katika viwanja vya kanisa Katoliki la Kitope,Wilaya ya Kaskazini B Unguja,ambae alifariki Jumapili Iliyopita
  kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana 
  Rais wa Zanbzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt,Ali Mohamed Shein,(katikati) akiweka shada la mauwa katika kaburi la Marehemu  Padri Evaristus Gabriel  Mushi,wakati wa mazishi yake yaliyofanyika leo  katika viwanja vya kanisa la Kitope,Wilaya ya Kaskazini B Unguja.


   Baadhi ya waumini wa kanisa katoliki  wakiwa katika mazishi ya marehemu  Padri Evaristus Gabriel  Mushi,aliyezikwa leo  katika viwanja vya kanisa Katoliki la Kitope,Wilaya ya Kaskazini B Unguja,
  Picha na Ramadhan Othman,IKULU.  0 0

  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha Rais Mwai Kibaki wa Kenya muda mfupi baaada ya kuwasili katika uwanja wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere kwa ziara ya kiserikali (State Visit) ya siku mbili.
  Rais Mwai kibaki wa Kenya akikaribishwa  kwa maua na Mwanafunzi Tazmina Rasul(6) muda mfupi baada ya kuwasili nchini kwa ziara ya kiserikali (State Visit) ya siku mbili huku mwenyeji wake Rais Dkt.Jakaya Kikwete akiangalia. (Picha na Freddy Maro).

  0 0

  Meneja wa Mfuko wa Pensheni wa PPF Kanda ya Ilala,Evans Musiba (watatu kushoto} akimkabidhi Mganga Mkuu wa Hospital ya Amana kitanda cha kupasulia wagonjwa wanaoshuhudia ni Mbunge wa Ilala Mhe.Mussa Zungu Azzan na kushoto ni Afisa Mwandamizi Mr. Mordgard Lumbanga.
  Wafanyakazi wa PPF wakiwa kwenye picha ya pamoja na Mhe.Mussa Zungu Azzan Mbunge wa Ilala mara baada ya kukabidhi kitanda cha kupasulia wagonjwa kutoka kushoto ni Meneja Uhusiano Bi.Lulu Mengele, Meneja wa Kanda ya Ilala Bw.Evans Musiba na wa pili kulia ni Afisa Mwandamizi Bw. Mordgard Lumbanga.

  0 0

  Peter Amandus mfanyakazi wa TRA (kati) akifurahia Tshs 5,000,000 alipozawadiwa na DStv kwa kulipia akaunti yake ya DStv kabla ya kukatika. Kulia ni Barbara Kambogi (Meneja Uhusiano), Ronald Shelukindo (Meneja Uendeshaji) na Furaha Samalu (Meneja Masoko) wa kampuni ya MultiChoice Tanzana

   Mwaka huu DStv kwa kuridhishwa na ushirikiano mkubwa inayopata kutoka kwa wateja wake imeaanda kampeni mpya iitwayo DStv Rewards. Kampeni hii itakuwa inazawadia wateja wake Shilingi za Tanzania 5,000,000 kila wiki endapo mteja atalipia malipo ya mwezi kabla akaunti yake haijakatika.
  Mpango huu umekuja miezi michache tu baada ya DStv kuzindua kampeni ya punguzo ya malipo ya mwezi kwa asilimia kumi (10%) kwa vifurushi vyake vyote. Hii ni kama moja ya zawadi zake kwa wateja endepo mteja atalipia  malipo ya mwezi kabla akaunti yake haijakatika.


  0 0
 • 02/20/13--19:00: CHEKA UNENEPE
 • KAMA HUJAPATA KUMUONA NA KUMSIKIA MVUNJA MBAVU WA NIGERIA AITWAYE BASKETMOUTH UJUE UMEKOSA MENGI

  0 0
 • 02/20/13--19:00: ngoma azipendazo ankal
 • Marvin Gaye a ngoma yke ya 'Let's Get It On' walikuwa hawashikiki

  0 0

  Product: www.vinjari.co.tz (A Tanzanian Online Booking and Payment Site) Vinjari.co.tz was established in September 2012 as a one-stop destination for travelers interested with Tanzania and those traveling within Tanzania. 

  Vinjari offers a wide range of services from discounted hotel bookings, tour packages and a travel guide that includes attractions, events listing and eat out places. Unlike other travel sites, Vinjari is 100% Tanzania owned offering prices that include all fees and charges that can be paid for up front with Tanzanian payment channels (Vodacom MPesa, TiGo Pesa) and VISA card that are authorized to transact online. 

   Come join us, as the brains behind VINJARI.CO.TZ shares with us their More details at: http://www.kinu.co.tz/1st-startup-saturday-with-vinjari-co-tz-02-2013

  0 0
 • 02/20/13--21:05: Article 20


 • 0 0


  Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi,Profesa Anna Tibaijuka akikata utepe wakati wa uzinduzi wa hoteli mpya yenye hadhi ya nyota 4 ya palace jijini Arusha jana.Wanaoshuhudia ni Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Mh. Lazaro Nyalandu,Mkurugenzi Mkuu wa NHC,Bw. Nehemia Mchechu na kulia mmiliki wa hoteli hiyo Dr.Hans Macha.
  waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi Profesa Anna Tibaijuka akiangalia jiwe la msingi baada ya uzinduzi wa hotel yenye hadhi ya nyota 4 Palace hoteli iliyopo katikati ya jiji la Arusha.
  WAZIRI wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi Profesa Anna Tibaijuka akikata keki yenye taswira ya jengo la hotel ya palace pamoja na mke wa mkurugenzi mkuu wa Palace hotel Bibi Vaileth ,Macha wakati wa uzindizi rasmi wa hoteli hiyo.
  WAZIRI wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi Profesa Anna Tibaijuka,naibu waziri wa maliasili na utalii Lazaro Nyalandu,Waheshimiwa Wabunge wa Majimbo ya Arusha na Arumeru Mashariki,Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Nyumba na Mkutugenzi Mkuu wa Hoteli hiyo waliongozana kuingia ndani ya jengo la hoteli hiyo.
  Watu mbalimbali wakati wa kufungua hoteli wakishuhudia. 

  WAJASIRIAMALI nchini, wametakiwa kujitokeza katika ujenzi wa hoteli za kitalii nchini, ili kukabiliana na tatizo kubwa la uhaba wa vitanda katika hoteli za kitalii ambao unalikabili Taifa. Naibu waziri wa Maliasilia na Utalii, Lazaro Nyarandu, alitoa wito huo jana wakati wa uzinduzi wa hoteli ya kitalii ya Palace Hoteli, ambayo imejengwa kwa ubia na Shirika la nyumba nchini(NHC). 

   Lazaro alisema uwekezaji huo utasadia kuongeza idadi kubwa ya watalii na mapato,”mwaka jana tulipata watalii 800,000 ukilinganisha na nchi ya Rwanda na udogo wake ilipata wageni 600,000 tatizo kubwa la nchi yetu ni upungufu wa vyumba vya kulala wageni”alisema. 

  Alisema mkakati huo utaufanya mkoa wa Arusha ambao ni kitovu cha utalii kuzidi kuongeza idadi ya vitanda vya kisasa kulala wageni ambapo kwa sasa ina vitanda 2,800 tu nyuma ya mkoa wa Dar es salaam wenye vitanda 3,800 na kuzidi mkoa wa Mwanza wenye vitanda 900 licha ya ukubwa wake. 

   “Tunaomba shirika la nyumba lijitanue hadi maeneo hasa ujenzi wa hoteli za kisasa za kitalii…na sisi wizara tunahitaji wawekezaji wa ndani na nje kujitokeza kujenga katika maeneo ya wazi na ndani ya hifadhi zetu panapofaa…na tumejipanga kukabiliana na watumishi wenye urasimu wanaokwamisha watu wenye nia njema”alisisitiza.

   Awali Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Nehemia Mchechu alisema ujenzi wa hoteli hiyo yenye hadhi ya nyota nne, umegharimu kiasi cha sh 16 bilioni ambapo NHC imetoa ardhi n ash 9 bilioni huku kiasi kingine kikitolewa na Palace Hoteli. 

   Alisema mradi wa hoteli hiyo ni moja ya miradi ambayo imekuwa na manufaa makubwa, kutokana na uwazi katika uendeshwaji wake na hivyo kuingiza mapato kwa pande zote NHC na Mbia. “binafsi nampongeza sana Mkurugenzi wa Palace hoteli, Dk Hans Macha kwa uwazi katika uendeshwaji wa mradi huu na tunamkaribisha katika miradi mingine aje tushirikiane”alisema Mchechu. 

  Naye Dk Ha Macha alisema mradi huo hadi sasa imetoa ajira ya wafanyakazi 120 na unatoa huduma nyingine kadhaa, ikiwepo huduma za kibenki na utachangia kwa kiasi kikubwa kikuza uchumi wa mkoa wa Arusha na Taifa. 

   “hoteli hii tunatumia malighafi za hapa Arusha toka kwa wajasiriamali ikiwa ni njia ya kuongeza ajira na kipato na pia tumekuwa na miradi mbali mbali ikiwepo na utunzwaji wa mazingira”alisema Macha.

   Akifungua mradi huo rasmi, Waziri wa Nyumba na Maendeleo ya Makazi, alipongeza mradi huo na kutoa wito kwa wajasiriamali wengine kujitokeza na kuingia ubia na NHC katika kutekeleza miradi mbali mbali. Alisema mradi huo unakwenda vizuri na umeongeza mapato ya NHC kwani katika eneo hilo, kabla ya ujenzi wa hoteli walikuwa wakipata kwa mwaka kiasi cha sh 31 milioni pekee lakini sasa wanapata 151 milioni. 

   “natoa agizo rasmi kwa wabia wengine walioingia mikataba na NHC kama huu, kama hawajatekeleza hadi sasa basi mikataba yao ifutwe kwani ni hasara kwa shirika la Taifa”alisema Profesa Tibaijuka.

  0 0

  MWENYEKITI mpya wa CCM Kata ya Jangwani Mohamed Bawazir, akipeana mkono na aliyekuwa mpinzani wake Abubakar Mzuka katika uchaguzi wa kuwania uenyekiti wa kata hiyo uliofanyika wiki iliyopita katika Ukumbi wa CCM, Ilala, Dar es Salaam.
  MWENYEKITI Mpya wa CCM Kata ya Jangwani, Mohamed Bawazir, akizungumza na wanachama wa kata ya Jangwani mara baada ya kushinda nafasi hiyo.
  Bawazir akipongezwa na Diwani wa Kata ya Jangwani Abuu Jumaa mara baada ya kutangazwa mshindi.

  0 0

   Meneja huduma kwa wateja wa Airtel Hawa Bayumi akimkabithi Afisa elimu wa mkoa wa Mwanza Hamisi Maulidi msaada wa vitabu kwa shule tatu za sekondari za Kalebezo, Buhongwa, and Kabuhoro zilizopo mkoani Mwanza. wakishuhudia kulia ni Meneja Mauzo wa Kanda Ally Maswanya na Meneja huduma ya Airtel money wa Kanda Galus Mgawe.
  Afisa elimu wa mkoa wa Mwanza Hamisi Maulidi  akipokea msaada wa vitabu kutoka kwa Meneja huduma kwa wateja wa Airtel Hawa Bayumi zilivyokabithiwa  na Airtel chini ya mradi wake wa Shule yetu, shule 3 za sekondari za  Kalebezo, Buhongwa na  Kabuhoro za mkoani Mwanza zilifaidika na Msaada huo.
   =======  ======= ====== 
  Mradi wa “Airtel shule yetu” kuleta ufanisi katika masomo ya Sayansi
  ·         Airtel yachangi vitabu vya sayansi kwa shule 3 za sekondari mkoani Mwanza
  Wakati Tanzania ikikabiliwa na uhaba wa wataalamu wa fani ya sayansi,wanafunzi wametakiwa kutohofia masomo ya sayansi na kukimbilia kusoma masomo mengine kwa lengo la kulifanya taifa liwe na wataalamu wengi wa fani mbalimbali.Kauli hiyo imetolewa jijini Mwanza na Afisa Elimu wa Mkoa wa Mwanza Hamis Maulid wakati akikabidhi vitabu kwa shule nne za sekondari za mkoa huo vilivyotelewa na kampuni ya simu za mkononi ya Airtel.
  Afisa Elimu wa mkoa wa mwanza ameendelea kwa kusema elimu ni urithi endelevu na kusoma masomo ya sayansi kunamwezesha mwanafunzi kuwa katika nafasi nzuri ya kulisaidia taifa katika Nyanja ya kitaalamu. mataifa mengi duniani yamepiga hatua kutokana na wanafunzi kupewa msukumo wa kusoma masomo ya mchepuo wa sayansi.
  Akiongea katika halfa ya makabithiano ya vitabu mkoani Mwanza, Meneja wa huduma kwa jamii wa kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Hawa Bayumi amesema Airtel imeguswa na tatizo la ukosefu wa vitabu mashuleni na kusababisha kiwango cha ufaulu kushuka hasa katika masomo ya sayansi. Na leo tunayofuraha kutoa msaada wa vitabu kwa shule za sekondari  za mkoa wa mwanza zikiwemo: Kalebezo  sekondari iliyopo wilayani Sengerema, shule ya sekondari ya Buhongwa na Kabuhoro sekondari.
  Tunaamini mchango huu wa vitabu mashule utakuwa chachu ya maendeleo ya elimu nchini na kuongeza kiwango cha ufaulu nchini. Tunaahidi kuendelea kushirikiana na serikali chini ya wizara ya elimu katika kuhakikisha tunafikia malengo waliojiwekea. Aliongeza Bayumi.
   Naye Mwalimu mkuu wa shule ya sekondari ya Kalebezo iliyopo wilayani Sengerema Thomas Muswaga na mwanafuzi Julieth John wa kidato cha nne katika shule ya sekondari ya Buhongwa wanazungumzia changamoto mbalimbali zikiwemo uhaba wa vitabu na kushukuru Airtel kwa msaada wa vitabu walioutoa katika shule hizo za mkoa wa Mwanza
  Airtel chini ya mpango wake wa shule yetu imeendelea kutoa msaada wa vitabu kwa shule za sekondari mbalimbali nchini. kwa mwaka huu shule 93 za sekondari  tangu kuanzishwa kwa mradi huo shule zaidi  ya shule za sekondari 900 zimekabithiwa

  0 0

   Naibu Spika na ujumbe wake wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kumaliza ziara ya kibunge katika Bunge la Singapore.Picha zote kwa hisani ya Ofisi ya Bunge.
   Mkuu wa sehemu ya lugha, ukalimani na Mawasiliano  wa Bunge la Singapore, Bw Palaniappan Pan akitoa maelezo kuhusu ukumbi wa Bunge la nchi hiyo kwa Ujumbe wa Tanzania.Wa kwanza kushoto ni Katibu wa Bunge, Dr Thomas Kashililah.Wengine pichani ni Mhe.Godfrey Zambi (kwanza kulia) na Mhe.Saleh Pamba.
   Naibu Spika Mhe.Job Ndugai na ujumbe wake wakiangalia mfumo wa utunzaji kumbukumbu katika Bunge la Singapore.
  Naibu Katibu wa Bunge la Singapore Bw.Siaw Huan Han akitoa maelezo kwa ujumbe wa Bunge la Tanzania unaoongozwa na Naibu Spika Job Ndugai ambao upo Singapore kwa ziara ya mafunzo na ushirikiano.

  0 0
 • 02/21/13--00:12: Sheli ya Kiwese Kimanzichana
 • Jamaa hawa ambao majina yao hayakuweza Patikana mara moja,walinaswa na Kamera ya Globu ya Jamii maeneo ya Kimanzichana Wilayani Mkuranga,Mkoani Pwani wakijaza mafuta aina ya Petrol kwenye vikopo vya maji na soda tayari kwa kuwauzia watu wanaotumia zaidi usafiri wa PikiPiki maarufu kama Boda Boda,kutoka kwenye Madumu.Sheli za Mafuta za aina hii zimekuwa zikitumika sana hasa katika maeneo yaliyo mbali na vituo maalum vya kuuzua Mafuta.

  0 0


  0 0

   
   Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mgeni wake Rais Mwai Kibaki wa Kenya wakiongozwa na Meya wa Kinondoni Mstahiki Yusuph  Mwenda kutembea hatua chache kabla ya kuzindua rasmi jina la Barabara ya Mwai Kibaki linalochukua nafasi ya jiba la barabara ya Old Bagamoyo leo kwenye makutano ya barabara ya Bagamoyo na Rashid Kawawa na iliyokuwa Old Bagamoyo leo Februari 21, 2013. Barabara hiyo, yenye urefu wa kilomita 10.1 inaanzia makutano ya barabara za Rashid Kawawa na Bagamoyo hadi njia panda ya kwenda Africana karibu na uwanja wa kulenga shabaha wa JWTZ Mbezi Beach
   Rais Mwai Kibaki wa Kenya akifunua pazia, akishuhudiwa na mwenyeji wake Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Waziri wa Ujenzi Dkt John Pombe Magufuli na Meya wa Kinondoni Mstahiki Yusuph Mwenda akizindua rasmi  jina la Barabara ya Mwai Kibaki linalochukua nafasi ya jiba la barabara ya Old Bagamoyo leo kwenye makutano ya barabara ya Bagamoyo na Rashid Kawawa na iliyokuwa Old Bagamoyo leo Februari 21, 2013.
  Vifijo na nderemo baada ya uzinduzi huo. 
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na mgeni wake Rais Mwai Kibaki wa Kenya muda mfupi kabla ya kufanya mazungumzo rasmi(official talks)Ikulu jijini Dar es Salaam jana jioni. 
   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwatambulisha kwa rais Mwai Kibaki baadhi ya Mawaziri waliohudhuria dhifa ya kitaifa ikulu jinni Dar es Salaam
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akigonga glasi na mgeni wake Rais Mwai Kibaki wa Kenya wakati wa dhifa ya kitaifa aliyoiandaa Ikulu kwa heshima ya Rais Kibaki aliyeko nchini kwa ziara yaka ya mwisho ya kiserikali.

  0 0
 • 02/21/13--02:45: Article 12
 • HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI

  TAARIFA KWA UMMA
  Gazeti la Mwananchi ISSN-0856-7573 Na.4621 la tarehe 20 Februari 2013 lilichapisha habari katika ukurasa wake wa pili iliyokuwa na kichwa cha habari “Muhimbili Wavamia Ofisi ya Mkurugenzi”. Awali ya yote tunapenda ieleweke kuwa  wafanyakazi hawakuvamia ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji kwa kuwa kulikuwa na mawasiliano na wafanyakazi waliotaka kumuona kupitia kwa Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi TUGHE Tawi la Muhimbili na alikuwa amekubaliana na ombi la kukutana nao.

  Pili, tunapenda kutoa ufafanuzi kwamba wafanyakazi hawa hawakuvamia kama gazeti linavyodai. Aidha, tunakanusha sababu zilizotolewa na Gazeti la Mwananchi kwamba wafanyakazi walivamia ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wakishinikiza kulipwa mishahara ambayo kwa mujibu wa taarifa za gazeti hili ni kuwa haijalipwa kwa muda wa miezi mitatu tangu mwaka jana mwezi wa 11.

  Tunapenda kuueleza umma kwamba taarifa hizi ni upotoshaji wa hali halisi ya ulipaji wa mishahara kwa wafanyakazi na taarifa hizi hazijatafitiwa kutoka mamlaka za Hospitali kuthibisha ukweli wake. Habari hizi siyo za kweli kwa kuwa Hospitali haijawahi kukosa mishahara ya wafanyakazi, hususan katika kipindi kinachodaiwa wafanyakazi hawakupata mishahara. Tumebaini pia gazeti hili limetumia majina ya watu likidai ni wafanyakazi wa Hospitali hii wakati siyo kweli kwa nia ya kuufanya umma uamini kwamba habari hizi ni halali na za kweli wakati ni kinyume chake. Watu wenye majina Anna Msigwa alitajwa kama Muuguzi na Anthony Semukasi siyo miongoni mwa wafanyakazi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili hivyo ni majina bandia. Kwa hiyo habari hii ni ya uzushi usio na ukweli wowote. Ni mtu mmoja tu aliyetajwa kwa jina la Ndg. Faustine Fidelis, ndiye tunamtambua kuwa mfanyakazi katika Hospitali hii na Katibu wa tawi la TUGHE Muhimbili.

  Tunapenda umma uelewe kwamba kama kuna mfanyakazi hapati mshahara basi atakuwa ni mfanyakazi mpya ambaye taratibu za kupata mshahara wake kutoka serikalini zinafanyika. Wafanyakazi wa aina hii ni wachache na tunaamini kwamba hawakulengwa na taarifa hizi ambazo zilitaka umma uamini kwamba wafanyakazi wote wa Hospitali ya Taifa Muhimbili hawajapata mishahara tangu Novemba 2012 hadi sasa.

  Tunapenda kutoa ufafanuzi kwamba wafanyakazi walienda kwenye ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji kudai motisha iliyotokana na mapato kupitia huduma iliyotolewa kwa wagonjwa wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Taifa (NHIF) ambayo iliahidiwa kulipwa na Uongozi wa Hospitali. Malipo haya siyo sehemu ya mishahara bali ni motisha kwa wafanyakazi yenye lengo la kuongeza tija. Malipo haya yalichelewa kulipwa kwa baadhi ya wafanyakazi lakini yalikuwa katika hatua za mwisho za maandalizi ya kulipwa. Wafanyakazi walielezwa hili na walielewa na kuendelea na kazi.

  Hospitali ya Taifa Muhimbili iko tayari kutoa ushirikiano kwa vyombo vya habari kuviwezesha kutoa taarifa sahihi kwa umma. Tunawasihi waandishi wa habari kupata ufafanuzi wa taarifa zozote wanazopata kuhusu Hospitali kabla ya kuandika na kupotosha umma.

  Imetolewa na Ofisi ya Uhusiano

  Februari 22, 2013

  0 0

  Mgeni Rasmi katika Kongamano la Nane la Wanahabari na Wadau wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF),Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii,Dkt. Seif Rashid akitoa hotuba yake ya ufunguzi wa Kongamano hilo linalofanyika hivi sasa kwenye Ukumbi wa Benjamin Mkapa uliopo ndani ya Chuo cha Ualimu Mkoani Mtwara.Kauli mbiu ya Kongamano hilo kwa mwaka huu ni “Matumizi Sahihi ya Fedha za Uchangiaji Katika Halmashauri ili kuboresha huduma katika vituo vya matibabu”.
  Mkuu wa Mkoa wa Mtwara,Mh. Joseph Simbakalia akizungumza machache kabla ya kumkaribisha mgeni Rasmi kuhutubia na kufungua Kongamano hilo.
  Mkuu wa Mkoa wa Mbeya ambaye ni Mwenyekiti wa Wakuu wa Mikoa yote Nchini,Mh. Abbas Kandoro akitoa salamu kwa Wanahabari na Wadau wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) wanaoshiriki Kongamano hilo.
  Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF),Emmanuel Humba akitoa taarifa fupi ya Mfuko wa Bima ya Afya kutokana tafiti mbali mbali zilizofanywa na baadhi ya Wanahabari katika Halmashauri 26 hapa nchini.
  Katibu Mkuu wa Jukwaa la Wahariri wa vyombo vya Habari hapa nchini,Nevile Meena akizungumza machache wakati wa Kongamano hilo la nane la Wanahabari na Wadau wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya,linaloendelea hivi sasa kwenye Ukumbi wa Benjamin Mkapa uliopo ndani ya Chuo cha Ualimu Mkoani Mtwara.
  Baadhi ya Wanahabari kutoka Vyombo mbali mbali vya Habari wakifatilia kwa makini Kongamano hilo la nane la Wanahabari na Wadau wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF),linalofanyika hivi sasa kwenye Ukumbi wa Benjamin Mkapa uliopo ndani ya Chuo cha Ualimu Mkoani Mtwara.


  0 0

  Maria had just got married and being a traditional Italian,  she was still a virgin. So, on her wedding night, staying at her mother's house, she was nervous. But her mother   reassured her. "Don't worry, Maria. Tony's a good man. Go  upstairs and he'll take care of you."

    So up she went. When she got upstairs, Tony took off his  shirt and exposed his hairy chest. Maria ran downstairs to  her mother and says, "Mama, Mama, Tony's got a big hairy  chest." "Don't worry, Maria," says the mother," all good men  have hairy chests. Go upstairs. He'll take good care of  you."

    So, up she went again. When she got up in the bedroom, Tony  took off his pants exposing his hairy legs. Again, Maria ran  downstairs to her mother. "Mama, Mama, Tony took off his  pants and he's got hairy legs!"

    "Don't worry. All good men have hairy legs. Tony's a good  man. Go upstairs and he'll take good care of you." So up she  went again. When she got up there, Tony took off his socks  and on his left foot he was missing three toes. When Maria  saw this, she ran downstairs. "Mama, Mama, Tony's got a foot  and a half!"

    "Stay here and stir the pasta," says the mother. "This is a  job for Mama."

  0 0
  Gari la Kampuni ya GAME FRONTIERS OF TANZANIA likirejea katika Ofisi ya Kanda ya Kusini Magharibi ya Pori la Akiba la SELOU likitokea ndani ya Pori 

  Hawa ni wafanyakazi wa Game frontiers of Tanzania wakiwa wamebeba pembe za ndovu
  Pembe za ndovu, Risasi na Silaha zilizokamatwa

  Kampuni ya GAME FRONTIERS OF TANZANIA kwa kushirikiana askari wanyamapori wa Selou na Askari wa vijiji vinavyozunguka pori la Akiba la Selou wamefanikiwa kukamata meno ya tembo 15 yenye thamani ya milion miambili, Risasi 9, Bunduki moja aina ya RIFFLE 458 na Gobole moja ambavyo hutumika kuulia wanyama .

  Doria hiyo imechukua takribani siku tatu katika pori la Akiba la Selou ikiwa ni sehemu ya kuwatafuta majangili wanaofanya mauaji ya wanyamapori katika pori hilo.

  Akizungumza na mwandishi wetu Bw. Mohamed Mpapa ambaye ni mwakilishi wa kampuni hiyo ya GAME FRONTIERS OF TANZANIA, Amesema kuwa hiyo ni kujituma kutokana na motisha ya fedha anayoitoa mwezeshaji wa kampuni ya GAME FRONTIERS OF TANZANIA ndio chachu ya mafanikio ya kukamata meno,bunduki na risasi.

   Akiendelea kuzungumzia tukio hilo Bw. Mohamed Mpapa amesmea baada ya majangili kuwaona Game Frontiers Tanzania wakiwa katika doria ndani ya pori hilo huku wakiwa wamekamilika kimapigano majangili hao waliweza kukimbia na kuacha nyara hizo baada ya kuona nguvu yao ni ndogo katika kupambana na kundi la doria.

  Ameongezea kwa kusema Kampuni yake imefurahishwa na mafanikio na ushirikiano uliopo kati yao, Serikali na wanavijiji kukabiliana na ujangili unaoendelea kuwamaliza tembo katika Pori la Akiba la Selou pia ametoa wito kwa jamii kuendelea kutoa ushirikiano katika kuwafichua majangili.

  Nae Kaimu Mkuu wa Kanda ya Kusini Magharibi ya Pori la Akiba la Selou Bw. Bernald Lijaji amesema Pembe zilizokamatwa ni 15 pamoja na Bunduki aina ya RIFLE 458,Gobole moja na Risasi 9 aina ya 458 vimekamatwa katika Doria iliyofadhiriwa na Mwekezaji wa Kampuni ya GAME FRONTIERS OF TANZANIA.PICHA NA HABARI KWA HISANI YA Hamza mashole Songea- ( www.demashonews.blogspot.com)

older | 1 | .... | 48 | 49 | (Page 50) | 51 | 52 | .... | 3272 | newer