Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 484 | 485 | (Page 486) | 487 | 488 | .... | 3272 | newer

  0 0

   Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi,Mh.Prof Anna Tibaijuka akizungumza mbele ya wageni waalikwa mbalimbali wakiwemo baadhi ya Wakuu wa Mikoa na Wadau mbalimbali kwenye jukwaa la Uwekezaji katika Sekta ya Nyumba.Prof.Tibaijuka alisema kuwa Serikali inaridhishwa na utendaji unaofanywa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC).

  Alisema katika kipindi kifupi Shirika limefanya mageuzi makubwa kwenye sekta ya makazi na kwamba miradi hiyo itakapokamilika,itaifanya miji hiyo kuwa ya kisasa.Prof.Tibaijuka alisema kuwa kampuni za uwekezaji kwenye sekta ya nyumba ni muhimu na hunyanyua uchumi wa nchi,alisema kuwa ili Taifa liweze kuendelea ni lazima liwe na mipango miji na kwamba kupanga miji sio kukata viwanja bali ni kunahitaji mambo mengi.Prof Tibaijuka amewataka wananchi kuwa tayari katika suala la kupanga miji,na maeneo yote yatakayopangwa ni lazima yafidiwe.
  Mkurugenzi Mkuu wa NHC,Nehemia Mchechu akizungumza mbele ya wageni waalikwa mbalimbali wakiwemo baadhi ya Wakuu wa Mikoa na Wadau mbalimbali kwenye jukwaa la Uwekezaji wa sekta ya nyumba lililofanyika jijini Dar.Bwa.Mchechu alisema kuwa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC),limedhamiria kuyabadilisha maeneo ya jiji la Dar na mikoa mingine nchini baada ya kuzindua ujenzi wa miji midogo.

  Alisema kuwa Miradi hiyo itakapokamilika itabadilisha mandhari ya maeneo mbalimbali nchini na kuyafanya kuwa ya kisasa,Mchechu alisema kuwa wataanza na miradi mitatu ikiwemo miji midogo katika majiji ya Dar es salaam na Arusha na kuendeleza nyumba zao zilizobomolewa.

  Alisema kuwa katika jiji la Dar,watakuwa na mradi wa salama Kigamboni na Kawe mbayo italifanya jiji hilo kubadilika kuwa la kisasa,aliongea kuwa katika miradi hiyo,kutajengwa nyumba nyingi za kuishi, biashara na sehemu za huduma muhimu .

  Mchechu amesema kuwa mradi mwingine utakaotekelezwa ni wa Usa River Safari City utakaojengwa jijini Arusha,ambao utalenga kulibadilisha jiji hilo na kuwa la kisasa,aliongeza kusema kuwa mradi huo utagharimu dola za Kimarekani bilioni mbili (zaidi ya shilingi bilioni 3.4) na itakamilika kati ya kipindi cha miaka saba mpaka 12.Bwa.alisema kuwa miradi mingine ambayo itatekelezwa ni pamoja na  Bagamoyo,Dodoma,Mbeya,Mtwara,Lindi,Mwanza na maeneo Mengine.
  Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC),Bi.Zakhia Meghi akizungumza kwa ufupi mbele ya wageni waalikwa mbalimbali wakiwemo baadhi ya Wakuu wa Mikoa na Wadau mbalimbali kwenye jukwaa la Uwekezaji wa sekta ya nyumba.
  Sehemu ya meza kuu ikifuatilia yaliyokuwa yakijadiliwa kwenye jukwaa hilo la uwekezaji wa sekta ya Nyumba,lililofanyika jijini Dar
  Wageni waalikwa mbalimbali waliofika kwenye kwenye jukwaa la Uwekezaji wa sekta ya nyumba.

  0 0


  CLEAN 9 ni nini na ina nini??

  Ina mchanganyiko wa bidhaa nne (Alovera Gel chupa 3, Ultra Lite, Bee pollen na Garcinia. Pia ina tape measure pamoja na chupa ya kupimia)

  Ina kitabu cha muongozo wa jinsi ya kutumia.
  CLEAN 9 ni muhimu katika kupunguza mwili kwasababu inafanya kazi ya kusaidia mfumo wako wa mmeng'enyo wa chakula,kuondoa sumu mwilini,kuondoa mafuta yaliyozidi mwilini na kukupa mfumo bora wa ulaji chakula.

  Matumizi yake ni rahisi sana. Tumia bidhaa kwa usahihi kisha utahitaji kufanya mazoezi walau dakika 20 (kutembea,kuruka kamba,kukimbia au gym ukipenda), Kunywa maji ya kutosha angalau lita tatu kwa siku pungza au acha kabisa ulaji wa vyakula vyenye sukari,wanga na mafuta.

  Unatumia kwa siku tisa na itakusaidia kupungua kilo 3 mpaka 8 na kupungua zaidi utatumia Nutri lean ambayo ina bidhaa za mwezi mzima na una uwezo wa kupungua kilo 10 mpaka 15. Rahisi eeh??
  Wasiliana nasi kwa kupiga au watsup kwa maelezo zaidi +255 713 418 475

  0 0

  Mratibu wa shindano la Redd's miss Sinza 2014 Tinna Matutuna katikati akizungumza na waandishi wa Habari katika ukumbi wa mikutano wa Meeda Night Club sinza juu ya Shindano la Redd's Miss Sinza litakalofanyika kesho ijumaa katika ukumbi wa Meeda Night Club kwa kiingilio cha 5,000 kwa viti vya kawaida na 10,000 kwa Viti Maalum .kushoto na kulia ni baadhi ya warembo wa shindano hilo.

  0 0

   Washiriki wa fainali ya Shindano la Tanzania Movie Talents wakipewa maelekezo ya jinsi magazeti ya kampuni hiyo yanavyoandaliwa hadi yanaponunuliwa na wadau wa habari
   Maelekezo yakiendelea kwa washiriki wa fainali ya Shindano la Tanzania Movie Talents
  Washiriki wa Fainali ya Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) wakiwa katika picha ya Pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya Global Publisher mara baada yakutembelea ofisi zao leo zilizopo 

  Bamaga Mwenge Jijini Dar Es Salaam.
  Na Josephat Lukaza - Proin Promotions Limited - Dar Es Salaam
  Washindi wa Kanda zote Sita za Tanzania wa Shindano la Tanzania Movie Talents ambao ni washiriki wa Fainali ya Shindano hilo kubwa kabisa nchini na Afrika Mashariki na Kati watembelea ofisi za Kampuni ya Uchapishaji wa Magazeti ya Risasi, Ijumaa, Uwazi nk ya Global Publishers limited kwaajili ya kujionea jinsi magazeti kutoka kampuni hiyo yanavyoandaliwa mpaka yanapowafikia wasomaji.

  Washiriki hao pia waliweza kupata fursa ya kuuliza maswali kwa wafanyakazi hao wa Kampuni ya Global Publishers kwaajili yakufahamu mambo mbalimbali yanayohusu kampuni hiyo Kubwa kabisa Tanzania.
  Washiriki wa Fainali ya shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) wanatarajia kuingia kambini leo tayari kwa mchakato wa kushindania shilingi Milioni 50 za Kitanzania kwa mshindi mmoja.

  Huu ndio muda wa Watanzania kuweza kumchagua mshindi wa Milioni 50 kwa kumpigia kura mshiriki ambae ataonekana kukuna nyonga zao kwa kuonyesha kipaji cha kweli. Watanzania wataweza kuwapigia kura washiriki watakaoonekana kuwa na vipaji kwa kutuma namba za washiriki kwenda namba maalumu itakayotolewa.

  0 0

   Wadau kutoka nchi mbali mbali barani Afrika wakiwa kwenye tafrija maalum ya Universal Channel inayoonyeshwa kwenye DStV ikiwa ni sehemu ya uonyeshaji wa kazi mbali mbali za MultiChoice Africa.Picha zote na Othman Michuzi.
   MC wa Kimataifa ambaye pia ni Muongozaji wa Mashindano ya Big Brother Africa, IK Osakioduwa akiongoza shughuli hiyo iliyofanyika jana usiku kwenye Hoteli yenye hadhi ya Kimataifa ya Trou Aux Biches,nchini Mauritius. 

   IK akifanya mahojiano na waigizaji wa moja ya filamu zinazoonyeshwa na  kituo cha Telemundo.

  Meneja Mahusiani na Mawasiliano na MultiChoice Tanzania,Barbara Hassan (kulia) akiwa na Waandishi wa Habari wa Tanzania wakati wa tafrija ya Universal Channel inayoonyeshwa kwenye DStV ikiwa ni sehemu ya uonyeshaji wa kazi mbali mbali za MultiChoice Africa.Toka kushoto ni Sidi Mgumia (Mtanzania),Barbara Hassan (Clouds FM),Esther Mngodo (Mwananchi) na Malio Njedengwa (TBC).
   Wadau wakiwa kwenye tafrija hiyo

   AU 

  0 0

   Bi Farida Abdul Akikabidhi bandeji kwa ajili ya kufungia wagonjwa kwa Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Palestina Dk Hugoline Mselle
   Bi Farida Abdul akimuonyesha kaimu Mganga mkuu wa Hospitali ya Palestina Dk Hugoline Mselle Vifaa ambavyo vimeletwa kama msaada kwenye Hospitali hiyo.Vifaa vilivyotolewa ni pamoja na Viti vya magurudumu vitatu ambavyo vitasaidia kubebea wagonjwa,Bandeji za kufungia vidonda,Ndoo za kuwekea taka,na vinginevyo.
   Hivi ni viti Vitatu vya kubebea wagonjwa ambavyo vilitolewa kama msaada kwenye Hospitali ya Palestina(sinza) na Farida Foundation.


  0 0

  Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Kilimanjaro, Robert Boaz akizungumza na waandishi wa habari wakati akitoa taarifa ya kukamatwa kwa bunduki mbili pamoja na mali kadhaa kufuatia operesheni tokomeza uhalifu inayoendeshwa na Jeshi la Polisi mkoani Hapo.
  Kamanda Boaz akiwaonesha waandishi wa habari, bunduki mbili, ya kulia ni Shotgun Greener, ambayo imekatwa kitako pamoja na nyingine aina ya shotgun (ya kushoto), namba za usajili 68022, ambazo zinaaminika zimekuwa zikitumika katika matukio kadhaa ya ujambazi mkoani humo.
  Baadhi ya vito vya thamani vilivyokamatwa katika operesheni hiyo zikiwemo bunduki hizo mbili .
  PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

   Rais wa Bongo Movie, Steve Nyerere (katikati) akitoa taarifa ya kukanusha uzinduzi wa filamu ya "I Love Mwanza" kujihusisha na masuala ya kisiasa. Kushoto kwa Nyerere ni Sabrina Lupia (Cathy) na kulia kwake n Wastara Juma na Salama "Sandra" Salimin.
    Rais wa Bongo Movie, Steve Nyerere (katikati) akitoa tarifa ya kukanusha taarifa za uzinduzi wa filamu ya "I Love Mwanza" kujihusisha na masuala ya kisiasa. Kuanzia kushoto kwa Nyerere ni Sabrina Lupia (Cathy) , Katibu wa TAFF mkoa wa Mwanza, Hussein Kimu na kulia kwa Nyerere ni Rais wa Wasanii wa Filamu Mkoa wa Mwanza, Anitha Rwezaura, Wastara Juma na Salama "Sandra" Salimin.
    Rais wa Bongo Movie Mkoa wa Mwanza, Anitha Rwezaura (katikati) akizugumza katika mkutanona waandishi wa habari kukanusha taarifa ya uzinduzi wa filamu ya "I Love Mwanza" kujihusisha na masuala ya kisiasa.

  0 0

   Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akifurahia jambo katika mazungumzo na msanii tenzi, nyimbo na mashairi  kutoka Mkuranga, Sauda Shaaban ambaye  alikwenda Bungeni mjini Dodoma Juni 25, 2014 kwa mwaliko wa Mbunge wake, Adam Malima  (kulia) ambaye pia ni Naibu Waziri wa Fedha. (Picha na Ofis ya Waziri Mkuu).

  0 0

   
  Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Dk. Reginald Mengi (kushoto) akielezea jambo kwa Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC), Prof. Lucian Msambichaka (katikati) na Mkurugenzi Mstaafu wa TIC na pia Balozi wa heshima wa Botswana hapa nchini, Eng. Emmanuel Ole Naiko wakati wa kongamano la pili la biashara kati ya Tanzania na China lililomalizika hivi karibuni jijini Dar es Salaam.

  0 0
  0 0

   Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue ambaye pia ni mgeni rasmi akifungua mkutano mkuu wa mwaka wa Wakurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu Serikalini katika ukumbi wa St. Gasper  mjini Dodoma leo.

   Kaimu Mkuu Mkoa wa Dodoma Bi Fatma Salum Ally (katikati) akiwakaribisha wageni waalikwa wa mkutanomkuwa mwaka wa Wakurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu Serikalini mkoani Dodoma, kabla ya mgeni rasmKatibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue (kulia) kufungumkutano huo katika ukumbi wa St. Gasper  mjini Dodoma leo.Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-Utumishi Bw. HAB Mkwizu .
   Katibu Mkuu Ofisi Rais, Utumishi wa Umma Bw.George D. Yambesi (katikati) akimkaribisha mgeni rasmi Balozi Ombeni Sefue (kushoto) kufungua mkutano mkuu wa mwaka wa Wakurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu Serikalini katika ukumbi wa St. Gasper  mjini Dodoma leo.Kulia ni Katibu wa Tume ya Utumishi wa Umma Bi.Claudia Mpangala.

   Baadhi ya washiriki wa mkutano wa mkuwa mwaka wa Wakurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu Wizarani, Idara za Serikali zinazojitegemea, Taasisi za Umma na Makatibu Tawala Wasaidizi Sehemu ya Utawala na Rasilimaliwatu katika Sekretariati za Mikoa na Mameneja Rasilimaliwatu katika Wakala la Serikali wakimsikiliza mgeni rasmi Balozi Ombeni Sefue  (haypo pichani) wakati wa ufunguzi wa mkutano huo katika ukumbi wa St. Gasper  mjini Dodoma leo.

  0 0

  IMG-20140625-WA0044
  Mkurugenzi  Mkuu wa wakala wa barabara (TANROADS) ,Injinia Patrick Mfugale akizungumza katika uzinduzi wa mradi wa Arusha-Holili /TAVETA –VOI kilometa 122 pamoja na Arusha –bypass (km 42)  unaofadhiliwa na benki ya maendeleo ya Afrika (ADB)uliyofanyika  jijini Arusha
  IMG-20140625-WA0045-1
  Mkuu wa Mkoa Arusha Magessa Mulongo akiongea katika uzinduzi huo
  IMG-20140625-WA0040Mwakilishi wa benki ya maendeleo ya Afrika (ADB), Injinia Patrick Musa akiongea kwenye uzinduzi huo

  HALMASHAURI mbalimbali nchini kwa kushirikiana na wananchi wametakiwa kutoa ushirikiano wa kutosha katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo ili kuweza kukamilika kwa wakati uliopangwa.
   
  Aidha kumekuwepo na changamoto mbalimbali ambazo zimekuwa zikikwamisha miradi hiyo ikiwemo ya wananchi kukataa kulipwa fidia kwa taratibu za sheria za nchi ili kutoa maeneo ya kuchimbwa changarawe, kokoto na kuchota maji.
   
  Hayo yalisemwa juzi na Mkurugenzi  Mkuu wa wakala wa barabara (TANROADS) ,Injinia Patrick Mfugale wakati akizungumza katika uzinduzi wa mradi wa Arusha-Holili /TAVETA –VOI kilometa 122 pamoja na Arusha –bypass (km 42)  unaofadhiliwa na benki ya maendeleo ya Afrika (ADB) uliofanyika katika ukumbi wa naura springs mjini hapa.
   
  Alisema kuwa,kumekuwepo na changamoto kubwa sana zinazosababishwa na wananchi na baadhi za halmashauri katika utekelezaji wa miradi hiyo hali ambayo imekuwa ni kikwazo kikubwa katika kufikia malengo yaliyowekwa.

  0 0

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia kwenye maadhimisho ya siku ya kupiga vita madawa ya kulevya yaliyoadhimishwa kitaifa leo Juni 26-2014 katika viwanja vya Ruanda Nzovwe Mkoani mbeya. 
    Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal. akipata maelezo juu ya athari za utumiaji wa madawa ya kulevya kutoka kwa Msanii Rehema Charamila (RC) wakati alipotembelea mabanda ya maonesho, kwenye maadhimisho ya siku ya kupiga vita madawa ya kulevya yaliyoadhimishwa kitaifa leo Juni 26-2014 katika viwanja vya Ruanda Nzovwe Mkoani mbeya. 
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal. Akionyeshwa baadhi madawa ya kulevya na Mkemia Daraja la kwanza Alois Ngonyani, alipotembelea mabanda ya maonesho kwenye maadhimisho ya siku ya kupiga vita madawa ya kulevya yaliyoadhimishwa kitaifa leo Juni 26-2014 katika viwanja vya Ruanda Nzovwe Mkoani mbeya.


  0 0

  Video imepigwa  na Dixon Busagaga wa globu ya jamii kanda ya kaskazini..

  0 0
 • 06/26/14--12:45: APRM yapata CEO mpya

 • Na Mwandishi Wetu, Malabo

  MPANGO wa Afrika Kujitathmini Kiutawala Bora (APRM) umempata Mtendaji wake Mkuu mpya atakayeongoza ofisi ya taasisi hiyo katika ngazi ya Bara la Afrika iliyoko mjini Midrand, Afrika Kusini.

  Uamuzi huo umefikiwa katika Mkutano wa 21 wa Wakuu wa Nchi za APRM uliofanyika mjini hapa, ambapo aliyekuwa Mtendaji Mkuu wa Mpango wa NEPAD, Dkt. Ibrahim Assane Mayaki kutoka Niger ndiye amehamishiwa APRM.

  Mabadiliko hayo yamekuja wakati ambapo wakuu wa Nchi za APRM waliokutana mjini hapa wakiwa wamesisitiza umuhimu wa mageuzi na APRM kutekeleza majukumu yake kwa wakati katika kufanya tathmini za utawala bora Barani Afrika.

  Dkt. Mayaki ambaye kabla ya uteuzi huo alipata kuisimamia APRM ilipokuwa taasisi moja na Nepad anaingia katika APRM akichukua nafasi ya Bw. Assefa Shifa raia wa Ethiopia.

  Akizungumza mjini hapa, Katibu Mtendaji wa APRM Tanzania, Bi. Rehema Twalib anayehudhuria mikutano hiyo, alithibitisha kufanyika kwa uteuzi huo. Tanzania ni miongoni mwa nchi 35 za Umoja wa Afrika zilizokwishajiunga na APRM.

  Kitaaluma Dkt. Mayaki anashahada ya umahiri Kutoka Chuo Kikuu kiitwacho National School of Public Administration (Enap), Quebec, Canada na pia ana shahada ya uzamivu (PhD) katika sayansi za utawala kutoka Chuo Kikuu cha Paris I.

  Kati ya mwaka 1996 na 2000 alitumikia nafasi mbalimbali katika Baraza la Mawaziri nchini mwake kabla ya kuhamia katika masuala ya utafiti na uhadhili.

  Akizungumza katika ufunguzi wa mkutano huo uliofanyika juzi, Rais wa Liberia Mama Ellen Johnson-Sirleaf ambaye ndiye Mwenyekiti wa APRM katika ngazi ya Afrika, aliziasa nchi wananchama kutekeleza Mpango huo kwa umakini na kutaka mageuzi makubwa.

  Katika mkutano huo pia wakuu wa nchi walipitisha wazo la kuwa na semina mbalimbali za uhamasishaji ambapo Tanzania iliteiuliwa kuwa mwenyeji wa semina itakayohusisha nchi za Afrika Mashariki.

  0 0

  Meneja wa Bia ya Ndovu Special Malt, Pamela Kikuli akizungumza na wadau wa bia hiyo wakati wa hafla ya kupongezana baada ya bia hiyo kutwaa tuzo ya ubora wa kimataifa(Ndovu High Quality Trophy) kutoka kwenye Taasisi ya Kimataifa ya Monde Selection nchini Ufaransa hivi karibuni.Hafla ilifanyika jijini Arusha mwishoni mwa wiki.
  Warembo wa bia ya Ndovu Special Malt wakiwa katika picha ya pamoja na kikombe wakati wa hafla ya kupongezana baada ya bia hiyo kutwaa tuzo ya ubora wa kimataifa(Ndovu High Quality Trophy) kutoka kwenye Taasisi ya Kimataifa ya Monde Selection nchini Ufaransa hivi karibuni.Hafla ilifanyika jijini Arusha mwishoni mwa wiki.
  Wadau Mbalimbali wakisherehekea Party ya Bia ya Ndovu Special Malt wakati wa hafla ya kupongezana baada ya bia hiyo kutwaa tuzo ya ubora wa kimataifa(Ndovu High Quality Trophy) kutoka kwenye Taasisi ya Kimataifa ya Monde Selection nchini Ufaransa hivi karibuni.Hafla ilifanyika jijini Arusha mwishoni mwa wiki.
  Meneja wa Bia ya Ndovu Special Malt, Pamela Kikuli(katikati),Meneja Masoko TBL, Fimbo Butallah(kulia) na mdau wa bia ya Ndovu Special Malt wakigonganisha chupa wakati wa hafla ya kupongezana baada ya bia hiyo kutwaa tuzo ya ubora wa kimataifa(Ndovu High Quality Trophy) kutoka kwenye Taasisi ya Kimataifa ya Monde Selection nchini Ufaransa hivi karibuni.Hafla ilifanyika jijini Arusha mwishoni mwa wiki.
  Wanamuziki wakitoa burudani wakati wakati wa hafla ya kupongezana baada ya bia hiyo kutwaa tuzo ya ubora wa kimataifa(Ndovu High Quality Trophy) kutoka kwenye Taasisi ya Kimataifa ya Monde Selection nchini Ufaransa hivi karibuni.Hafla ilifanyika jijini Arusha mwishoni mwa wiki.

  0 0

  Naibu Mkurugenzi wa kanda wa Mamlaka ya Mawasiliano nchini ,Victor Nkya akizungumza wakati semina ya siku moja kwa maofisa wa polisi wa ngazi mbalimbali mkoa wa Kilimanjaro.
  Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro ,SACP ,Robert Boaz akizungumza wakati akifungua semina ya siku moja kwa maofisa wa polisi wa ngazi mbalimbali mkoa wa Kilimanjaro iliyoandaliwa na Mamlaka ya Mawasiliano nchini TCRA kushoto kwake ni Naibu Mkurugenzi wa kanda wa Mamlaka ya Mawasiliano nchini ,Victor Nkya
  Washiriki wa semiana wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi .Na Dixon Busagaga wa globu ya jamii kanda ya kaskazini.
  PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

  Na Allan Ntana, Tabora

  TUME ya Haki za Binadamu na Utawala Bora hapa nchini imeanza kuboresha huduma zake kwa jamii baada ya kuanzisha huduma mpya ya kupokea malalamiko ya wananchi kwa njia ya ujumbe mfupi kupitia simu za kiganjani.

  Hayo yalibainishwa jana na Maofisa wa Tume hiyo katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa stendi ya zamani mjini Tabora ambao ulilenga kutambulisha na kuhamasisha matumizi ya huduma hiyo kwa wananchi na wadau mbalimbali wenye malalamiko yoyote au kutotendewa haki mkoani hapa.

  Afisa uchunguzi  na mwanasheria  wa tume hiyo Caroline Shayo alisema tume hiyo iliyoanzishwa Julai 2001hapa nchini imelenga kulinda na kutetea maslahi ya wananchi ambapo imejiwekea utaratibu wa kupokea na kushughulikia malalamiko mbalimbali ya wananchi kuanzia ngazi ya serikali kuu mpaka ngazi ya vijiji.

  ‘Mpaka sasa tume hii ina ofisi katika kanda  4 tu ambazo ni Lindi, Mwanza, DSM na Zanziba, lengo letu ni kuelimisha umma ili wafahamu wajibu wao ni nini, haki zao ni zipi, wanawezaje kuzipata na kwa utaratibu gani’, aliongeza Shayo.

  Mchambuzi Mkuu wa mifumo ya habari na mawasiliano wa tume hiyo Wilfred Warioba, alisema ili kurahisisha mawasiliano ya tume hiyo na wananchi, wameamua kuanzisha teknolojia hiyo ya kutuma malalamiko moja kwa moja kupitia mitandao ya simu zao kwa njia ya ujumbe mfupi yaani ‘sms’.

  Aliongeza kuwa tume ya haki za binadamu na utawala bora ni chombo huru ambacho kiko kwa ajili ya kutetea wananchi wote na hakitozi gharama yoyote ya kuwasilisha malalamiko.

  Mtaalamu huyo aliongeza kuwa tume inapokea malalamiko ya aina yoyote ile bila kujali yameletwa na nani ili mradi yawe na ukweli ndani yake, kinachotakiwa ni mhusika kuandika malalamiko yake kwenye sehemu ya kuandika ujumbe mfupi kwenye simu yake ya mkononi na kisha kuutuma kwenye namba 0754 460 256.

  Ujumbe huo ukishapokelewa mhusika (mlalamikaji) atapigiwa simu na kuulizwa baadhi ya mambo ili kujua kiini cha malalamiko yake kwa lengo la kujiridhisha ikiwa ni pamoja na kufahamu anaitwa nani, yuko wapi na mambo mengine yatakayoturahisishia kushughulikia malalamiko yake kwa wepesi zaidi, aliongeza.

  Aidha Warioba alisema mwananchi yeyote atakayeleta malalamiko yake kwa ‘sms’ anatakiwa kutumia majina yake halisi na kutaja mahali alipo na si kusema uongo lengo likiwa kurahisisha kazi ya kushughulikia malalamiko yake.

  Alifafanua kuwa tume hii haina upendeleo wowote wa kijinsia katika kushughulikia malalamiko ya wananchi yanayopokelewa huku akibainisha kuwa wananchi walio wengi  bado hawajajua wajibu wao kwani wanayo matatizo mengi ila wanayanyamazia tu ndio maana tumewatembelea ili waseme waziwazi.

  Naye Catherin Malimbo, Afisa Uchunguzi Mwandamizi idara ya haki za binadamu, aliwataka wananchi wote wenye malalamiko ya masuala ya ardhi, viwanja, biashara na ndoa kuleta malalamiko yao pia kwani wapo tayari kuyafanyia kazi sambamba na kutoa ushauri kwa mamlaka husika namna ya kumaliza kero hizo kisheria.

  0 0

  Kamera man wa Globu ya Jamii alipo kwenye Mji wa Mto wa Mbu,Wilayani Monduli Jijini Arusha ametuletea taswira hii ya Mbuzi wakiwa machungoni.

older | 1 | .... | 484 | 485 | (Page 486) | 487 | 488 | .... | 3272 | newer