Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 485 | 486 | (Page 487) | 488 | 489 | .... | 3286 | newer

  0 0

  Serikali ya Jamuhuri ya Watu wa China imekusudia kuongeza nguvu za ziada katika kusaidia kuimarisha miundo mbinu ndani ya Bara la Afrika kwa lengo la kuyajengea uwezo wa uzalishaji wa kiuchumi Mataifa mbali mbali yaliyomo ndani ya Bara hilo.

  Kauli hiyo imetolewa na Makamu wa Rais wa China Bwana Li Yuanchao wakati yeye na ujumbe wake alipofanya mazungumzo Rasmi na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiuongoza Ujumbe wa Zanzibar kwa Niaba ya Rais wa Zanzibarna Mwenyekiti wa Bararaza la Mapinduzi Dr. Ali Moh’d Shein hapo hoteli ya La gema Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja.

  Bwana Li Yanchao akiwa Zanzibar kwa siku moja akiendelea na ziara yake ya siku sita Nchini Tanzania alisema katika utekelezaji wa azma hiyo China imejipangia kutumia Yuan Bilioni 2.2 katika mipango yake ya kuimarisha miundo mbinu hiyo ya uwekezaji kwenye sekta ya biashara.

  Aliishauri Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuitumia fursa hiyo adhimu kwa kuchagua miradi yake itakayoipa kipaumbele cha kwanza kwa kuwasiliana na Ofisi ya Ubalozi mdogo wa Nchi hiyo uliopo Zanzibar ili kuratibu miradi hiyo na hatimae hatua za utekelezaji zianze mara moja.

  Naye Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akitoa shukrani zake alisema Zanzibar itaendelea kuiheshimu na kuithamini China kutokana na msimamo wake wa kuendelea kuiunga mkono Zanzibar katika harakati za kuimarisha uchumi.

  Balozi Seif alieleza kwamba Jamuhuri ya Watu wa China inastahiki kupongezwa kwa misaada yake mikubwa inayotoa kwa Zanzibar ambayo haijawahi kutokea katika Historia ya Zanzibar tokea Mapinduzi ya Mwaka 1964.

  Alisema Wananchi wa Zanzibar wamekuwa wakishuhudia misaada tofauti inayotolewa na China ndani ya kipindi cha miaka 50 tokea Mapinduzi iliyolenga katika sekta za afya, elimu, maji, miundo mbinu, kilimo pamoja na mawasiliano.
  Bwana Christopher Mush Smith wa Hoteli ya La Gema akikata Keki Maalum yenye Bendera za Tanzania na China iliyoandaliwa na Hoteli hiyo kwa ajili ya Mgeni rasmi Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Watu wa China Bwana Li Yuanchao aliyepo pembeni yake akiwa sambamba na Mwenyeji wake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi.
  Makamu wa Rais wa China Bwana Li Yuanchao akipongeza na Mwenyeji wake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi mara baada ya mazungumzo yaop yaliyofanyika katika Hoteli ya La Gema Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja.


  0 0

   Balozi Modest Mero na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Bi. Agness Kijazi katika picha ya pamoja, kwenye makazi ya balozi Tanzania nchini Geneva

  Hivi karibuni Mh. Modest Mero, Balozi wa Tanzania, Geneva alifanya mazungumzo ya pamoja na Mh. Dkt. Seif Rashid na Bi. Agness Kijazi, katika makazi ya Balozi, Geneva.

  Ujumbe wa Mh. Waziri ulikuwa Geneva kwenye kikao cha Bodi ya " Global Alliance for Vaccines and Immunization", Geneva, ambapo Mh. Waziri ni mjumbe wa Bodi. Na pia ujumbe wa Mkurugenzi wa Hali ya Hewa upo Geneva kuhudhulia kikao cha 60 cha kamati kuu ya Shirika la Hali ya Hewa Duniani (World Meteorological Organization).
   Mh. Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii katika mazungumzo na Balozi Mero, kwenye makazi ya balozi, Geneva, Uswisi.
   Wakijiandaa kupata mlo wa pamoja baaada ya mazungumzo
  Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Mh.Dkt. Seif Rashid, Balozi Mh. Modest Mero na Mrs. Rose Mero na msaidizi wa Waziri katika picha ya pamoja

  0 0


  0 0

  Mtendaji Mkuu wa MultiChoice Africa,Nico Meyer akizungumza na baadhi ya Waandishi kutoka vyombo vya mbali mbali vya habari barani Afrika (wahapo pichani) wakati wa mkutano uliofanyika wao wa kuzungumzia shunguli zinazofanya na MultiChoice Afrika kwenye ukumbi wa hoteli ya Trou Aux Biches,Morisi nchini Mauritius.Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano wa MultiChoice Africa,Caroline Creasy.
   Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano wa MultiChoice Africa,Caroline Creasy akifafanua jambo mbele ya Waandishi kutoka vyombo vya mbali mbali vya habari barani Afrika (wahapo pichani) juu shughuli zinavyofanywa na MultiChoice.Kulia anaesikiliza ni Mtendaji Mkuu wa MultiChoice Africa,Nico Meyer. 
  Sehemu ya Waandishi kutoka vyombo vya mbali mbali vya habari barani Afrika wakimsikiliza kwa makini Mtendaji Mkuu wa MultiChoice Africa,Nico Meyer (hayupo pichani).


  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mh. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiambatana na ujumbe wa Tanzania kwenye ufunguzi wa Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Umoja wa Afrika Mjini Malabo, Equatorial Guinea. Miongoni mwa masuala muhimu yanayotarajiwa kujadiliwa kwenye mkutano huu ni bajeti ya umoja huo na mkakati wa kukusanya maoni kutoka nchi wanachama kuhusu Afrika ifikapo mwaka 2063, ambapo umajo huu utafikisha miaka mia moja.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mh. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na wajumbe wenzake wa kwenye Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Umoja wa Afrika unaofanyika Mjini Malabo, Equatorial Guinea.
  Viongozi wa Wakuu wa Nchi za Umoja wa Afrika wakiwa kwenye picha ya Pamoja.Picha na IKULU.

  0 0
 • 06/26/14--20:00: ngoma azipendazo ankal

 • "My Heart Will Go On" -  Celine Dion

  0 0

  Watumishi waliostaafu katika Ofisi ya Makamu wa Rais wametakiwa kuendelea na moyo wa kuudumisha Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na uhifadhi wa mazingira.

  Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano),  Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ametoa rai hiyo jana wakati alipokuwa akizungumza katika hafla ya kuwaaga wastaafu wapatao 12 wa kada ya maafisa katika ofisi hiyo iliyofanyika katika viwanja vya Makumbusho ya Taifa jijini Dar es salaam.

  Mheshimiwa Samia alisema wastaafu hao wanapaswa kuendelea na moyo huo kwani jukumu la kuudumisha Muungano na uhifadhi wa mazingira ni la kila mmoja katika jamii.

  “Natambua kwamba ninyi nyote mliostaafu na mtakao staafu ni mabalozi wazuri katika kuelimisha jamii kuhusu majukumu ya Ofisi ya Makamu wa Rais yanayohusu kuudumisha Muungano wetu pamoja na kuhifadhi mazingira,” alisema Waziri Samia na kuongeza

  “Natarajia mtakuwa mfano katika kuendeleza jitihada za kudhibiti uharibifu wa mazingira katika jamii inayowazunguka.”

  Aidha, aliwaasa  wastaafu hao kushirikiana na Asasi na Taasisi mbalimbali zilizoko kwenye maeneo yao ili kupitisha mawazo ambayo yatasaidia kuwaletea wananchi maendeleo 

   “Kupitia mawazo yenu Taasisi kama hizi zitaweza kujenga uwezo zaidi katika masuala ya maendeleo ya jamii hususan fursa za ajira kwa vijana wetu,” alisema

  Kwa wale wanaoendelea na utumishi wa umma Waziri Samia aliwataka waige mfano kwa watumishi waliostaafu na kuendelea kujenga tabia ya uadilifu, uaminifu na uchapakazi.

  Wastaafu hao walipatiwa zawadi ya jiko la gesi kila mmoja jambo ambalo Naibu Katibu Mkuu katika Ofisi ya Makamu wa Rais Eng. Angelina Madete alipokuwa akizungumza wakati wa kumkaribisha mgeni rasmi alisema ofisi iliandaa zawadi hiyo ili  wastaafu hao wakawe mabalozi wazuri wa kuhimiza matumizi ya jiko la gesi na hivyo kusaidia katika suala zima la uhifadhi wa mazingira.


  0 0

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Mhe. Li Yuanchao (kushoto) pamoja na Makamu wa Rais wa Tanzania, Mhe, Dkt. Gharib Bilal (kulia) wakipeana maneno ya mwisho katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam ikiwa ishara ya kuagana baada ya kumaliza ziara yake ya siku sita. 
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Mhe. Li Yuanchao (kulia) akiwa katika picha ya pamoja na na Makamu wa Rais wa Tanzania, Mhe, Dkt. Gharib Bilal (kushoto) katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Mhe. Li Yuanchao akiwapungua mkono baadhi ya viongozi pamoja na wananchi waliokuja kumugaga katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam mara baada ya kukamilisha ziara yake nchini.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Mhe. Li Yuanchao akimpa mkono wa shukurani Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mhe. Dkt. Fenella Mukangara kabla ya kuanza safari yake ya kurudi nchini kwake.

  0 0
  0 0

   Wafanyakzi wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) na familia zao wakiwa kwenye foleni ya kupata msosi wakati wa hafla ya Siku ya Familia ya TBL,  kwenye ufukwe wa Bahari ya Hindi, Hoteli ya Bahari Beach, Kunduchi, Dar es Salaam.
   Wakishindana  katika mchezo wa kuvutana kamba.
   Badhi ya viongozi wa TBL wakistarehe  huku wakibadishana mawazo.
   Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), David Magese (kulia), akimkabidhi mtoto Said Shaban zawadi baada ya kuwa mmoja wa washindi wa mbio za watoto wakati wa hafla ya Siku ya Familia ya wafanyakazi wa Kampuni hiyo, katika ufukwe wa Bahari ya Hindi karibu, Kunduchi, Dar es Salaam.Kushoto ni Meneja Mauzo wa TBO Kanda ya Kusini, James Bokela.
   Bendi ya Mashujaa iktoa burudani murwa.

  0 0

   Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara( wa pili kutoka kushoto) akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa matumizi ya Gari la kurushia matangazo la TBC, kutoka kulia ni Makamu Waziri wa Biashara wa Jamhuri ya watu wa China Li Jingzao, Makamu wa Rais wa China Li Yunchao  na wa mwisho kushoto ni Mkurugenzi wa TBC Bw. Clement Mshana. 
   Gari la kisasa la kurushia matangazo ya moja kwa moja lililokabidhiwa kwa TBC likiwa katika viwanja vya Shirika hilo Mikocheni jijini Dar es Salaam. 
   Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara akikagua ndani ya Gari la kisasa la kurushia matangazo la TBC mara baada ya uzinduzi wake leo jijini Dar es Salaam.
   Pichani baadhi ya Screen zikionyesha picha mbalimbali za matukio yaliyokuwa yakirushwa moja kwa moja wakati wa hafla ya makabidhiano na uzinduzi wa Gari la kisasa la kurushia matangazo la TBC lililopatikana kwa msaada wa Serikali ya China.
   : Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara akikabidhiwa mfano wa Ufunguo wa gari la kurushia matangazo la TBC mara baada ya kuzinduliwa leo jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Waziri wa Biashara wa Jamhuri ya Watu wa China Li Jingzao.
   Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara akimkabidhi mfano wa Ufunguo wa gari la kurushia matangazo Mkurugenzi Mtendaji wa TBC Bw. Clement Mshana mara baada ya gari hilo kukabidhiwa na kuzinduliwa rasmi leo jijini Dar es Salaam.

  0 0  0 0

   Mkurugenzi wa Takwimu za Uchumi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bw. Morrice Oyuke  akizungumza na wadau mbalimbali  wakati wa kujadili Mpango Mkakati wa Takwimu za Kilimo leo jijini Dar es salaam. Mpango huo utaiwezesha Ofisi ya Taifa ya Takwimu kukusanya takwimu sahihi zinazokidhi viwango vya ndani na vile vya kimataifa.
   Mwakilishi wa Shirika la Chakula Duniani (FAO) nchini Tanzania Bi. Diana Tampelman  akizungumza na waandishi wa habari kupongeza  hatua iliyofikiwa katika kukamilisha Mpango mkakati wa Takwimu za Kilimo nchini Tanzania  na kueleza  kuwa hatua hiyo inaendana na  Mpango wa Dunia  ulioanzishwa mwaka 2010 kwa lengo la kuboresha takwimu za kilimo maeneo ya vijijini.
   Baadhi ya washiriki wa mkutano wa Kijadili Mpango Mkakati wa Takwimu za Kilimo wakifuatilia masuala mbalimbali wakati wa mkutano huo leo jijini Dar es salaam.Picha na Aron Msigwa - MAELEZO.

  0 0

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akutana na kufanya mazungumzo na Rais mpya wa Misri Mhe Abdel Fattah Al-Sisi mjini Malabo, Equatorial Guinea, pembeni ya Mkutano wa kawaida wa Umoja wa Afrika Juni 26, 2014.
   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Rais mpya wa Misri Mhe Abdel Fattah Al-Sisi mjini Malabo, Equatorial Guinea, pembeni ya Mkutano wa kawaida wa Umoja wa Afrika Juni 26, 2014.PICHA NA IKULU

  0 0

  Rais wa Shirikia la Hali ya Hewa Duniani (WMO) Prof. David Grimes  ( wanne kushoto kutoka mstari wa mbele) na Katibu Mkuu wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani Michel Jarraud (watatu kutoka kushoto mstari wa mbele) katika picha ya pamoja na wajumbe wa kamati Kuu ya Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO EC). Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa, Dkt Agnes Kijazi (wa kwanza kutoka kushoto waliosimama) akiwa miongoni mwa wajumbe 37 wa kamati hiyo kuu ya WMO.  

  Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania Dkt. Agnes Kijazi akiwa mmoja wa wajumbe wa kamati  kuu ya Shirika la Hali ya Hewa Duniani anashiriki mkutano wa 66 wa Kamati Kuu ulioanza tarehe 18 Juni 2014 huko Geneva. Mkutano wa mwaka huu utajadili masuala ya hali ya hewa katika maeneo yafuatayo : Upunguzaji wa madhara yatokanayo na hali mbaya ya hewa, Utoaji huduma za hali ya hewa, mpango maalum wa kuhakikisha huduma za hali ya hewa zinawafikia walengwa zikiwa na ubora (Global Framework for Climate Services-GFCS), Mkakati endelevu  wa kujenga uwezo, mfumo wa uangazi wa hali ya hewa wa Shirika la Hali ya Hewa Dunia na shughuli za utafiti. Kwa maelezo zaidi tembelea www.wmo.int   
  IMETOLEWA NA: MONICA MUTONI , AFISA UHUSIANO,TMA

  0 0

   Waziri wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu, akijisajili kushirikia kwenye tovuti ya Kongamano la Kwanza la Ufugaji Nyuki Afrika mwaka 2014, kama ishara ya kuzindua tovuti hiyo, shughuli iliyofanyika  kwenye ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Julias Nyerere jijini Dar es Salaam leo.Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Maimuna Tarishi na Msemaji wa Wizara Nurdin Chamuya.

   Baadhi ya washiriki wa uzinduzi huo
  Waziri wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu akizungumza na hadhiri wakati wa uzinduzi wa Kongamano la Kwanza la Ufugaji Nyuki Afrika mwaka 2014 uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Julias Nyerere jijini Dar es Salaam leo.
   Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Maimuna Tarishi akizungumza machache kabla ya kumkaribisha Wazara hiyo kuzungumza na kuzindua tovuti ya Kongamano la Kwanza la Ufugaji Nyuki Afrika mwaka 2014 uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Julias Nyerere jijini Dar es Salaam leo.

  0 0

   Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika Mkutano wa Kamati ya Viongozi wa Afrika Kuhusu Tabia Nchi  ulioitishwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Mhe Ban Ki-moon pembeni mwa mkutano wa kawaida wa Umoja wa Afrika mjini Malabo, Equatorial Guinea leo Juni 27, 2014
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete  akiteta jambo na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Mhe Ban Ki-moon pembeni mwa mkutano wa kawaida wa Umoja wa Afrika mjini Malabo, Equatorial Guinea leo Juni 27, 2014.

  PICHA NA IKULU

  0 0
 • 06/27/14--20:00: ngoma azipendazo ankal
 • Whitney Houston - "I Will Always Love"

  0 0

   Safari ya wanahabari toka Mkoani Kigoma kutembelea hifadhi ya Taifa ya arusha ikaanza
    Wanahabri toka Mmkoa wa Kigoma wakiwa ndani ya hifadhi ya Taifa ya Arusha
   Waandishi wa habri wa Mkoa wa Kigoma wakipata maelezo kuhusu hifadhi ya Taifa ya Arusha kutoka kwa Mhifadhi  Ikolojia Bi Maria Kirombo
  Mambo ya utalii wa ndani kwa wanahabri toka Kigoma ndani ya hifadhi ya Taifa ya Arusha yalikuwa kama hivi.(picha zote na Editha Karlo)

  0 0
 • 06/27/14--23:26: AFRICA SPORTS DAY -COVENTRY


older | 1 | .... | 485 | 486 | (Page 487) | 488 | 489 | .... | 3286 | newer