Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 483 | 484 | (Page 485) | 486 | 487 | .... | 3272 | newer

  0 0


  SMALL BOYS, MSHIKAMANO, PACHOTO ZAPIGWA FAINI RCL.

  Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) zimezipiga faini ya kati ya sh. 300,000 na sh. 500,000 klabu za Mshikamano FC, Pachoto Shooting Stars, Town Small Boys na Kiluvya United kutokana na makosa mbalimbali ikiwemo viongozi, wachezaji na washabiki kufanya vurugu kwenye mechi za Ligi ya Mabingwa wa Mikoa (RCL) iliyomalizika hivi karibuni.

  Uamuzi huo umefanywa na Kamati ya Mashindano ya TFF iliyokutana juzi (Juni 23 mwaka huu) jijini Dar es Salaam kupitia masuala mbalimbali ikiwemo taarifa za mechi, na malalamiko kutoka kwa baadhi ya timu zilizoshiriki RCL iliyochezwa katika vituo vya Mbeya, Morogoro na Shinyanga.

  Town Small Boys ya Ruvuma imepigwa faini ya sh. 500,000 kwa mujibu wa kanuni ya 37(13) ya Kanuni ya RCL kutokana na udanganyifu kwa kumtumia mchezaji Agaton Mapunda ambaye hakustahili ingawa usajili wake ulithibitishwa na TFF, kwa kutokuwepo pingamizi kutoka klabu yoyote katika kipindi cha pingamizi.
  Licha ya usajili wake kuthibitishwa na TFF, Kamati ilibaini mchezaji huyo hakutoka ndani ya Mkoa wa Ruvuma kama kanuni za RCL zinavyoelekeza. Hata hivyo, matokeo ya mechi hiyo dhidi ya Njombe Mji iliyomalizika kwa bao 1-1 yanabaki kama yalivyo kwa mujibu wa kanuni ya Kanuni ya 52 (3 na 4) na 31(11) ya RCL kwa kuwa mchezaji Mapunda alithibitishwa na TFF (qualified player).

  Vilevile mchezaji huyo amepigwa faini ya sh. 200,000 kwa mujibu wa kanuni za 48(4) na 31(11) za RCL. Nayo malalamiko ya Njombe Mji dhidi ya mchezaji David Noel Makakala kuwa ndiye aliyecheza mechi hiyo badala ya Carlos Mapunda yametupwa kwa kukosa vielelezo na ushahidi wa kuthibitisha hilo.

  Kiluvya United FC ya Pwani imepigwa faini ya sh. 300,000 kwa mujibu wa kanuni ya 37(1) kutokana na vurugu za washabiki wake kwenye mechi namba 46 dhidi ya Abajalo iliyochezwa mjini Morogoro.

  Pachoto Shooting Stars ya Mtwara na Mshikamano FC ya Dar es Salaam zimepigwa faini ya sh. 500,000 kila moja kwa kufanya vurugu kubwa kwenye mechi yao namba 100 iliyovunjika mjini Morogoro. Pia Mshikamano FC wamepewa pointi tatu na mabao matatu kwa mujibu wa kanuni ya 23(1na5) na 22(d).
   Wachezaji na viongozi wa Pachoto Shooting na wachezaji wa Mshikamano FC waliofanya vurugu na kupigana, suala lao linapelekwa kwenye Kamati ya Nidhamu ya TFF kwa uamuzi na hatua za kinidhamu.
   Nayo Tanzanite ya Manyara imefungiwa kucheza mashindano yote rasmi kwa msimu mmoja, na kuteremishwa daraja hadi ligi ya wilaya mara itakapomaliza kifungo chake kwa mujibu wa kanuni ya 21(3)(a), 37(14) na 22(a). Tanzanite iliadhibiwa kwa mujibu wa kanuni ya 23(1,5 na 6) baada ya kumpiga mwamuzi kwenye mechi dhidi ya AFC na baadaye kugomea mchezo. Ilishindwa kulipa faini na kujitoa mashindanoni kwa kuondoka kituoni.
  Wachezaji wanaotuhumiwa kumpiga mwamuzi mpaka kumjeruhi suala lao litapelekwa kwenye Kamati ya Nidhamu ya TFF.
   Kamati imetupa malalamiko ya African Sports ya Tanga dhidi ya Abajalo ya Dar es Salaam, Ujenzi FC ya Rukwa dhidi ya AFC, Panone FC ya Kilimanjaro dhidi ya Volcano FC ya Morogoro, na Mvuvumwa FC ya Kigoma dhidi ya Mbao FC ya Mwanza kwa kukosa vielelezo na ushahidi.

  Pia malalamiko ya Mvuvumwa FC dhidi ya Geita Veterans ya Geita juu ya kuwachezesha Ibrahim Alphonce, Zamoyoni Magoma na John Mtobesya kwa kuwa hawakusajiliwa yametupwa kwa vile wachezaji hao ni halali, isipokuwa orodha ya wachezaji wa Geita Veterans FC iliyotolewa kwa ajili ya pingamizi ilikuwa na upungufu kiuchapaji ambapo wachezaji sita hawakuorodheshwa.

  Nao makamishna Edward Hiza na Jimmy Lengwe waliokuwa kituo cha Morogoro wamepewa onyo kutokana na ripoti zao kuwa na upungufu.

  Vilevile Kamati ya Mashindano imezitangaza rasmi timu za African Sports, Geita Veterans na Panone FC kupanda kucheza Ligi Daraja la Kwanza (FDL) msimu wa 2014/2015

  BONIFACE WAMBURA MGOYO
  OFISA HABARI NA MAWASILIANO
  SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

  0 0

  Waziri Mkuu,Mizengo Pinda akizungumza na Mbunge wa Vunjo, Augustine Mrema, Bungeni mjini Dodoma Juni 25, 2014.
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Mbunge wa Mtwara Mjini Hasnan Murji,bungeni mjini Dodoma Juni 25, 2014.
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na madiwani kutoka jimbo la Mkuranga kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Juni 24, 2014. Madiwani hao walikwenda Bungeni kwa mwaliko wa Mbunge wao, Adam Malima ambaye pia ni Naibu Waziri wa Fedha.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0  JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

  WIZARA YA UCHUKUZI
   

   TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI  Kwa mujibu wa Sheria ya Wakala wa Serikali No. 30 ya mwaka 1997, Kifungu Na. 9 ikisomwa pamoja na Marekebisho yake ya Mwaka 2009, Waziri wa Uchukuzi, Mhe. Dkt. Harrison G. Mwakyembe(MB) amemteua Bw. Gilliad Wilson  Ngewe  kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) kuanzia tarehe1/6/2014.

  Kabla ya Uteuzi huo Bw. G. W. Ngewe , alikuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa SUMATRA kuanzia tarehe 12/3/2014 ambapo awali alikuwa ni Mkurugenzi wa Idara ya Udhibiti wa Usafiri wa barabara, SUMATRA.
  Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra) ilianzishwa kwa Sheria ya Bunge namba 9 ya mwaka 2009 ili kusimamia usafiri wa Nchi kavu na Majini Tanzania.
  Imetolewa na:
  Katibu Mkuu
  Wizara ya Uchukuzi.

  0 0

  Kwa mujibu wa Sheria ya Wakala wa Serikali No. 30 ya mwaka 1997, Kifungu Na. 9 ikisomwa pamoja na Marekebisho yake ya Mwaka 2009, Waziri wa Uchukuzi, Mhe. Dkt. Harrison G. Mwakyembe(MB) amemteua Bw. Gilliad Wilson  Ngewe  kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini(SUMATRA) kuanzia tarehe1/6/2014. 

  Kabla ya Uteuzi huo Bw. G. W. Ngewe , alikuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa SUMATRA kuanzia tarehe 12/3/2014 ambapo awali alikuwa ni Mkurugenzi wa Idara ya Udhibiti wa Usafiri wa barabara, SUMATRA.
  Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra) ilianzishwa kwa Sheria ya Bunge namba 9 ya mwaka 2009 ili kusimamia usafiri wa Nchi kavu na Majini Tanzania.

  Imetolewa na:
  Katibu Mkuu
  Wizara ya Uchukuzi.


  0 0

  By Damas Makangale,Tanzania

  TANZANIA has recorded an impressive improvement in performance of primary school enrolment. They have achieved remarkable enrolment of 93% after abolishing school fees in public schools with the aim of meeting the Millennium Development Goals (MDGs).

  Speaking at the National Consultations Workshop on Localization of the Post-2015 Development Agenda in Dar es Salaam recently, Permanent Secretary in the Prime Minister’s Office, Regional Administration and Local Government, Jumanne Sagini said that the country has also managed to reduce the number of deaths of children under five years old, improve gender equality and access to quality services such as safe water and health facilities.

  “Tanzania has made good progress in implementing the agreement of the strategic growth and reducing poverty… Implementation of the MDG agenda was through National Strategy for Economic Growth and Reduction of Poverty commonly known as Mkukuta and Zanzibar strategy for Economic Growth and Reduction Poverty (Mkuza),”
  DSC_0014
  Ambassador Celestine Mushy, Director of the Department for Multilateral Cooperation in the Ministry of Foreign Affairs and International Cooperation greets one of the invited guests and stakeholders before the official opening ceremony at the workshop on Localization of Post 2015 Development Agenda.


  0 0

  Kocha mkuu wa zamani wa timu ya Taifa, taifa Stars Marcio Maximo 
  amesaini mkataba  wa kuwa kocha mkuu na timu ya Yanga kwa muda wa 
  miaka miwili. makubaliano hayo yamefikiwa jana, wakala  anaye 
  mwakilisha Ally Mleh wa kampuni ya Manyara Sports Management 
  amethibitisha hilo.

  "Ni kweli kocha Marcio Maximo amekubali kuingia mkataba na timu ya  Yanga ambapo anatarajiwa kuanza kazi rasmi tarehe 27/06/2014 ambapo  atafuatana na msaidizi wake Leonardo Neiva. Mazungumzo ya makubaliano   hayo yalichukua muda mrefu kidogo hatimaye tumefikia
  makubaliano.Tunashukuru mungu kila kitu kimekamilika.

  Kwa niaba ya Marcio Maximo napenda kuushukuru uongozi wa klabu ya
  Yanga, shukrani za pekee kwa mwenyekiti wa Yanga ndg Yusuf Manji na
  makamu wake Clement Sanga,  kwa kweli wameonyesha  umakini na
  professional kwa muda wote wa  majadiliano. Nawaomba
  wachezaji,wanachama na wapenzi wote wa yanga tumpe ushirikiano.

  Baada ya kumaliza mkataba wake wa kuifundisha Taifa Stars nchini
  aliingia mkataba na timu kubwa nchini brazil  mpaka mkataba wake
  ulipoisha.Kwa wakati huu kulikuwa na mazungumzo na timu mbalimbali
  Zilizotoa  ofa nchini China, Ethiopia na Afrika kusini lakini Yanga
  wamefanikiwa kumnasa kocha huyo.

  Maximo anatarajia kuwasili kesho siku ya Alhamis saa saba mchana

   
  Maximo ilikuwa awasili nchini baada ya fainali za kombe la dunia lakini kutokana na mkataba alioingia na Yanga imebidi afupishe mkataba wa kazi ya 'commentator' aliyokuwa akiifanya nchini Brazil ili awahi kuandaa program zake Yanga.


  0 0

  Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi hapa nchini Jaji Mstaafu Damian Lubuva (katikati) akizungumza na waandishi wa habari jana, kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida, Liana Hassan na kushoto ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Singida Joseph Mchina.

  Na Hillary Shoo, SINGIDA.

  TUME ya Taifa ya Uchaguzi imeanza mchakato wa uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura,kwa kuwashirikisha kwa karibu waandishi wa habari hapa nchini.

  Lengo la kuwashirikisha waandishi wa habari ni kutokana na uwezo na hekima katika kupeleka taarifa na kuhamasisha jamii na wananchi kwa ujumla kupitia vyombo vya habari.

  Hayo yamebainisha jana mjini hapa na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Mstaafu Damian Lubuva wakati  akifungua mkutano na waandishi wa habari wa Mkoa wa Singida.

  Jaji Lubuva alisema lengo ni kuhakikisha kuwa wale wote wenye sifa za kuwa wapiga kura wanajitokeza kwa wingi katika vituo vya kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura.

  Aidha alisema kuwa Tume inatarajia kufanaya uboreshaji wa Daftari la Kudumu wa Wapiga kura kwa awamu ya kwanza hivi karibuni kwa kutumia Teknolojia mpya ya Biometric Vote Regstration ( BVR).

  Alisema mfumo huo mpya ni wa kuchukua au kupima taarifa za mtu za kibaiolojia au tabia ya mwanadamu na kuhifadhi katika kanzi data kwa ajili ya utambuzi.

  “Mfumo huu hutumika katika kumtambua mtu na kumtofautisha na mwingine, ingawa tabia hizo za binadamu ziko nyingi, lakini kwa ajili ya kuandikisha wapiga kura alama za vidole kumi vya mikono, picha na saini ndizo zitachukuliwa na kuhifadhiwa kwenye Kanzi Data (Database) ya wapiga kura.” Alisisitiza Jaji Lubuva.


  Hata hivyo alisema kwa kutumia mfumo huu wa (BVR), wananchi wote wenye sifa za kuwa wapiga kura na wale walio na kadi za mpiga kura watatakiwa kuandikishwa upya.

  Jaji Lubuva alisema mafunzo kwa Watendaji yanatarajiwa kufanyika muda kuanzia Mwezi Julai mwaka hauu kabla ya zoezi la uboreshaji wa Daftari kufanyiaka.

  Mwenyekiti huyo alibainisha kwamba uhakiki wa vituo vya kuandikisha wapiga kura umeshafanyika na kwa sasa uandikishaji utafanyika katika vituo vilivyo katika ngazi ya vitongoji, Vijiji na Mitaa. Kutokana na utaratibu huu wa sasa vituo vya kujiandikisha vimeongezeka kutoka 24,919 hadi kufikia vituo 40,015 ambavyo vimewekwa katika ngazi za Vitongoji, Vijiji na Mitaa’. Alisema na kuongeza

   “Ili kuwezesha kuwa karibu zaidi na wanancahi na hivyo kupunguza malalamiko ya auambali wa vituo vya kujiandikisha na kuaongeza mwamko wa kujiandikishwa na kupiga kura.” Alifafanua Jaji Lubuva.

  Kwa upande wake Mkurugenzi wa Manispaa ya Singida, Joseph Mchina, alisema maandalizi yote muhimu kwa ajili ya zoezi hilo katika Manispaa yake yamekamilika na hivyo kuwa na vituo 154 badala ya 84 vya awali.


  0 0

  Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti wa NHIF, Raphael Mwamoto akipokea cheti cha ushindi wa banda bora katika maonesho hayo.
    Ofisa Masoko na Elimu kwa Umma, Grace Michael akionesha kombe lililokabidhiwa kwa NHIF na Balozi Ombeni Sefue baada ya kuwa washindi.
   Maofisa wa NHIF wakifurahia ushindi
   Furaha iliendelea ndani ya banda
   Meneja wa NHIF, Mkoa wa Temeke, Ellentruda Mbogoro kushoto, Grace Michael (Katikati) na Meneja Masoko na Elimu kwa Umma, Anjela Mziray wakifurahia ushindi.

  0 0

   Mratibu wa Shindano la kumtafuta mrembo wa Redd's Miss Chang'ombe, Tom Chilala (katikati), akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, leo wakati wa kuitangaza zawadi za washindi. Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Marie Stopes, Dk. Jophn Bosco na Ofisa Uhusiano  wa TV1, Mponjoli Katule. 
   Warembo wa shindano la Redd's Miss Chang'ombe wakiwa katika picha ya pamoja na wadhamini wa shindano hilo, wasanii watakaotoa burudani siku ya fainali. 
   Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Marie Stopes, Dk. Jophn Bosco akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo.
  Rapa wa bendi ya Ruvu Stars, Msafiri Diouf 'Sokoine' akighani wakati wa mkutano na waandishi wa habari.
  Warembo wakiwa wamepozi kwa picha.

  MNYANGE atakayevishwa taji la Redds Miss Temeke  2014 linalotarajia kufanyika Juni 27 mwaka huu katika  ukumbi wa TTC Chang'ombe anatarajia kujinyakuria  kitita cha sh. laki tano. 
  Mshindi wa pili atajinyakulia laki tatu, mshindi wa tatu  laki mbili na washiriki wengine watapata kifuta jasho cha sh. 65,000.

   Mratibu wa shindano hilo Tom Chilala, alisema katika  shindano hilo anatarajia kumtoa mrembo atakafanikiwa  kutwaa taji la misi Tanzania mwaka huu hapo baadaye.

  "Mwaka huu nina warembo wazuri na wenye vigezo vyote, naamini mwaka huu nitarudisha heshima yangu ya  kufanikiwa kutoa warembo kutoka Redd's Miss Temeke hadi Redd's Miss Tanzania," alisema.

   Alisema mwaka 2010 alifanikiwa kumtoa Genevieve Emmanuel, kutoka miss Temeke hadi miss Tanzania,  hivyo na kwa mwaka huu anaamini itakuwa hivyo kutokana na warembo alionao. 

  Aidha shindano hilo litakarokuwa na washereheshaji kutoka bendi ya Ruvu Stars, Mchekeshaji Kitale pamoja na msanii anayetamba na kibao cha Basi Nenda Moshi Katena na wengine. Kiingilio katika shindano hilo kitakuwa ni sh. 20,000 kwa VIP na Elfu 10000 kawaida. 

  Naye Mkurugenzi wa Marie Stoper John Bosco ambao ni wadhamini wa shindano hilo alisema wameamua kudhamini mashindano hayo kwa lengo la kuwaelimisha vijana kuhusiana na uzazi wa mpango.

  Alisema hawataishia hapo wanaendelea kudhamini hadi miss Tanzania kutokana na kuona vijana hao wanaweza kuliwakilisha taifa."Katika sensa viijana ndio wameonekana kuwa na asilimia kubwa hivyo ni vizuri kuwa dhamini ili kuweza kujenga kizazi ambacho kimewezeshwa ambacho hakitaweza kuwa taifa tegemezi," alisema.

  0 0

   Standard Chartered Bank’s Head of Retail Clients, Mike Shio, right, spins the wheel to pick the winner of the Bank’s Salary Solution Campaign raffle. Looking on are an official from the Gaming Board of Tanzania, Mrisho Milao, centre, and the Bank’s Head of Products, Omari Mtiga.
   Standard Chartered Bank’s Head of Retail Clients, Mike Shio, right, spins the wheel to pick the winner of the Bank’s Salary Solution Campaign raffle. Looking on are an official from the Gaming Board of Tanzania, Mrisho Milao, centre, and the Bank’s Head of Products, Omari Mtiga.
  Standard Chartered Bank’s Head of Products, Omari Mtiga, centre, speaks to the first lucky winner of the Bank’s Salary Solution Campaign. Looking on are the Bank’s Head of Retail Clients, Mike Shio, left, and an official from the Gaming Board of Tanzania, Mrisho Milao, right.

  Standard Chartered Bank Tanzania Limited today held its first raffle for the Salary Solution Campaign which is running until the end of August, 14. The Salary Solution Campaign is a mix of a number of products bundled together and geared towards enhancing financial benefits to the Bank’s Clients.Clients who wish to take personal loans under the Salary Solution offering will be able to do so without any charges for loan arrangement. 

  They will also enjoy enhanced savings as they will not be charged a monthly maintenance fee on the Salary Account, called the Hifadhi Account. Additionally, clients will be able to enjoy overdraft services without having to pay any arrangement, insurance or processing fees on the Salary Overdraft aspect of the bundle. Existing and new clients who take up the Salary Solution offering will stand a chance to win an iPad at the six raffle draws that have been planned.

  0 0

  Ndg Watanzania,WanaBagamoyo na wapenda maendeleo, kwa niaba ya CCM-Bagamoyo na Ofisi ya Mbunge-Jimbo la Bagamoyo napenda kuleta kwenu Masikitiko yetu kwa niaba ya Chama na Familia ya Mheshimiwa Mbunge Shukuru Jumanne Kawambwa kutokana na Usumbufu ambao umesababishwa na habari zinazoenezwa Mitandaoni kwamba Mheshimiwa Kawambwa amekumbwa na Umauti akiwa njiani anaelekea Mwanza.


  UKWELI
  Mheshimiwa Shukuru Jumanne Kawambwa yupo Nchini Canada Akitimiza majukumu yake. Hivyo Watanzania na wana Bagamoyo mnaombwa radhi kwa usumbufu uliotokea na kwamba Mheshimiwa Mbunge yuko na Afya njema na utekelezaji wa Majukumu unaendelea kama kawaida.
  Ndg.Ridhiwani Kikwete (Mnec)
  Mbunge -Chalinze

  0 0
 • 06/25/14--13:17: Article 9

 • 0 0  0 0

  Ofisa mnadhimu namba moja wa jeshi la polisi mkao wa Kilimanjaro SSP Koka Moita akichangia jambo wakati wa semina juu ya mifuko ya hifadhi ya jamii iliyotolewa kwa maofisa wa jeshi hilo wa ngazi mbalimbali.
  Kamanda wa polisi wa wilaya ya Moshi,OCD Deusdedit Kasindo akizungumza jambo wakati wa semina hiyo.
  Viongozi wa ngazi ya juu wa jeshi la polisi mkoa wa Kilimanjaro wakifuatilia maelezo juu ya mifuko ya hifadhi ya jamii.
  Baadhi ya askari polisi wa wilaya ya Moshi wakifuatilia maelezo juu ya mifuko ya hifadhi za jamii.
  PICHA ZAIDI YA TUKIO HILI BOFYA HAPA

  0 0

  Na Hassan Hamad (OMKR) 
  Mkutano Mkuu wa CUF Taifa umemchagua tena Katibu Mkuu wa Chama hicho kuendelea na wadhifa huo kwa kupata kura 675, sawa na asilimia 99.5 ya kura zilizopigwa.
   Mkutano huo pia umemchagua Prof. Ibrahim Lipumba kuwa Mwenyekiti wa CUF Taifa kwa kupata kura 659 sawa na asilimia 95.5 na kumshinda mpinzani wake Chifu Lutalosa Yemba aliyepata kura 30 sawa na asilimia 4 nukta 3. 
  Aidha mkutano huo umemchagua Mhe. Juma Duni Haji kuwa Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho kwa kupata kura 662 sawa na asilimia 99.25. 
  Akizungumza baada ya kutangazwa mshindi Katibu Mkuu wa Chama hicho Maalim Seif Sharif Hamad, amewapongeza wajumbe wa mkutano mkuu kwa kumpa tena ridhaa ya kuongoza chama hicho kwa kipindi cha miaka mitano ijayo. 
  Wakati wa Kampeni. Mapema akizungumza katika kampeni za kuomba kuchaguliwa tena kuwa Katibu Mkuu wa Chama hicho, Maalim Seif amesema siri ya mafanikio yake kisiasa ni kutokana na kujiamini kwake kuwa kiongozi, kuwa mkweli na kuwa na dhamira njema kwa wananchi. 
  Akijibu hoja za wajumbe wa mkutano huo Maalim Seif amewataka viongozi wa chama hicho kutotangaza kuhudhuria kwa viongozi wa kitaifa kwenye mikutano ya hadhara hadi pale wenyewe watakapothibitisha kuhudhuria, ili kuepusha wananchi kutoamini utendaji wa viongozi hao. 
  Mgombea wa nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho Mhe. Juma Duni Haji amesema iwapo atachaguliwa kushika nafasi hiyo atashirikiana na viongozi wengine wa kitaifa pamoja na wananchi kuhakikisha kuwa chama kinapata maendeleo zaidi. 
  Chifu Yemba amesema ameamua kugombea nafasi hiyo kutetea demokrasia ya kweli ndani ya chama na taifa kwa ujumla. Chifu Yemba ambaye ni mwanasayansi kitaaluma, pia ni Mwenyekiti wa CUF, Wilaya ya Shinyanga Mjini. 
  Prof. Lipumba amesema akichaguliwa atahakikisha anatembelea nchi nzima kuimarisha chama kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2015. Aidha amesema atafanya juhudi za ziada kuona kuwa Tanzania inakuwa na Muungano wa kuheshimiana baina ya pande mbili za Muungano (Tanzania Bara na Zanzibar). 
  Amesema wanawake watapewa nafasi ndani ya kamati tendaji ya chama kuondosha dhana ya mfumo dume unaodaiwa kuwepo katika ngazi za juu za uongozi. 
  Mgombea mwengine wa nasafi ya Mwenyekiti wa CUF Taifa M’bezi Adam Bakar, amejitoa kwenye kinyang’anyiro hicho na kubakia wagombea wawili wa nafasi ya Mwenyekiti. Mwakilishi wa Jimbo la Mji Mkongwe (CUF) Ismail Jussa Ladhu aliteuliwa kuwa mwenyekiti wa muda wa kuongoza uchaguzi huo uliosimamiwa na mwanasheria Awadh Ali Said.
   Viongozi wakuu wa CUF wakionyesha mshikamano baada ya kuchaguliwa kukiongoza chama hicho kwa kipindi cha miaka mitano ijayo. Wa pili kulia ni msimamizi wa uchaguzi huo Awadh Ali Said (Picha na Salmin Said, OMKR)


  0 0  0 0

   Wanachama na Viongozi wa Chadema wakiwemo wa Baraza Kuu la chama hicho, wakipiga kwata kuelekea Ofisi za Msajili wa Vyama vya Siasa, jijini Dar es Salaam, leo, kupeleka barua ya kumuomba Msajili huyo wa vyama, kuwataka viongozi wa ngazi ya juu wa Chadema kuzingatia Katiba ikiwemo kuitisha kikao cha Baraza Kuu na kuzingatia matumizi bora ya fedha za Chama.
   Mjumbe wa Baraza Kuu Chadema ambaye pia ni Mwenyekiti wa chama hicho wilaya ya Temeke Joseph Yona (kushoto) akiongoza wenzake kuingia Ofisi ya Msajili wa Vyama leo kuwashitaki viongozi wa ngazi ya juu wa chama hicho kwa kudaiwa kutotekeleza Demokrasia na kufuata Katiba ndani ya Chama
   Yona akisaini kitabu cha wageni kwenye kwenye mapokezi ya Ofisi ya Msajili wa Vyama Jijini Dar es Salaam, alipowasili ya ujumbe wake. Kulia kwa Yona ni Mwenyekiti wa Chadema wilaya ya Kaliua mkoani Tabora ambaye ni Mjumbe wa  Baraza Kuu na Mjumbe wa Mkutano Mkuu Chadema, Jorum Mbogo
   Naibu Msajili wa vyama vya Siasa Nchini akimkaribisha Yona na msafara wake.
   Wanachama waliofuatana na wajumbe wa Baraza Kuu Chadema wakisubiri kuwasisha barua yao kwa Mkuu wa Masijala wa Ofisi ya Msajili wa vyama.
  HABARI PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

  Askari polisi wa kituo cha kikuu cha Polisi cha kati akiwa amemshikilia kijana mmoja baada ya kumokoa toka mikononi mwa madereva bodaboda ambao walikwishaanza kujichukulia hatua mkononi kwa kumuadhibu baada ya kutaka kuiba pikipiki.
  Askari katika ofisi za kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro walilazimika kufunga geti kuzuia kundi kubwa la madereva boda boda na watu wengine wakilazimisha kuingia ili kumfuata mwizi wao wa pikipiki.
  Madereva hao walionekana kukerekwa na kuzuiwa kumuadhibu kijana huyo na hapa walionekana wakilalamka.
  Jamaa wa nje akatamani kupita katikati ya Nondo hapa.
  Geti likafungwa na hakuna mtu aliyepita.Na Dixon Busagaga wa globu ya jamii kanda ya kaskazini.

  0 0

  BONDIA Ibrahimu Class 'King Class Mawe' amewashukuru viongozi wa ngumi nchini kwa sapoti yao wanayo mpa tangu ahanze ngumi mpaka sasa kwani yeye malengo yake ni kufika mbali zaidi baada ya kunyakuwa mkanda wa ubingwa unaotambuliwa na WPBF Africa Welterweight Title 

  Aliyasema hayo mwishoni mwa wiki iliyopita katika ukumbi wa DDC Keko kulipokuwa na mkutano mkuu wa chama cha ngumi za kulipwa nchini cha TPBC, ambapo alikutana na viongozi mbalimbali na kupongezwa kwa kunyakuwa mkanda huo wa ubingwa alioupata Zambia kwa kumpiga bondia Mwansa Kabinga kwa TKO ya raundi ya tisa katika uwanja wa Arthur Davies Stadium, Kitwe, Zambia

  bondia huyo mwenye ndoto za kuwa mmoja wa mabondia watakotamba duniani ambapo mwanzoni mwa mwaka huu aliteuliwa kuwa bondia bora wa mwaka 2013 katika uzito wake tuzo zilizoanza kufanyika mwaka huu

  fikra zake kwa sasa ni kuwa bingwa wa mikanda mbalimbali inayotambulika Duniani katika uzito wake fikra zake siku moja ni kupambana katika mapambano makubwa zaidi hususani katika ukumbi wa MGM Gland nchini Marekani.

  Bondia huyo mwenye rekodi ya kushinda mapambano 11 na kupoteza mpambano mmoja wakati ananza mchezo huo.bondia huyo anawashukurujopo la makocha wake wa kambi ya ilala linalo ongozwa na kocha mkongwe wa mchezo huo Habibi Kinyogoli 'Masta',kondo Nassoro,Sakwe Mtulya na kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' kwa kumsimamia na kumpa ushari anapokuwa ulingoni akipambana

  bila kuwasahau mashabiki wake waliojaa kila kona ya jiji la Dar es salaam na Tanzania nzima kwa ujumla

  0 0

   Ofisa Uhusiano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Dorris Malulu akimkabidhi Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa King'ongo, Benetris Mapesi mfano wa hundi yenye thamani ya sh. mil 29  za msaada wa ujenzi wa kisima cha maji katika mtaa huo uliopo Kata ya Saranga, Kinondoni Dar es Salaam. Hafla hiyo ilifanyika katika mtaa huo mwishoni mwa wiki.Wanaoshuhudia makabidhiano hayo ni Mkandarasi wa kisima hicho, Onesmo Sigala (wa pili kulia) wa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya MO Resources Limited,na Mjumbe wa Kamati ya Maji ya Mtaa wa King'ongo, Anna Kibwana ( wa pili kushoto).
  Ofisa Uhusiano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Dorris Malulu akimkabidhi Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya ukandarasi ya MO Resources Limited, Onesmo Sigala (kulia) mfano wa hundi yenye thamani ya sh. mil 29  za msaada wa ujenzi wa kisima cha maji katika mtaa huo uliopo Kata ya Saranga, Kinondoni Dar es Salaam. Hafla hiyo ilifanyika katika mtaa huo mwishoni mwa wiki.Wanaoshuhudia makabidhiano hayo ni Mjumbe wa Kamati ya Maji ya Mtaa wa King'ongo, Anna Kibwana (wa pili kushoto),Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa King'ongo, Benetris Mapesi.

older | 1 | .... | 483 | 484 | (Page 485) | 486 | 487 | .... | 3272 | newer