Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 479 | 480 | (Page 481) | 482 | 483 | .... | 3272 | newer

  0 0

  Jerome (26) na Kevin-Prince Boateng (27)  ni ndugu wa baba mmoja kutoka Ghana na mama mbalimbali (Wajerumani) ambao wameweka historia ingine usiku huu kwa kucheza Kombe la Dunia pamoja lakini katika timu za nchi mbili tofauti. Jerome anachezea Ujerumani wakati nduguye Kevin-Prince anachezea Ghana, japo wote wamezaliwa Berlin, Ujerumani. 
  Usiku wa leo ndugu hawa wanaweka historia ya kucheza uwanja mmoja katika  timu tofauti wakati Ujerumani inacheza na Ghana. Mara ya kwanza walikutana kwa staili hiyo mnamo Juni 23, 2010 huko Afrika ya Kusini ambapo Ujerumani iliifunga Ghana bao 1-0. 
  Leo mpira umeisha kwa Ghana 
  na Ujerumani kutoka sare ya 2-2


  0 0

  Diamond Platnumz ni msanii mwengine mkubwa wa Kitanzania aliyejiunga na Mkito.com kwaajili ya kusambaza muziki wake mtandaoni. Msanii huyu anajiunga na wengine kama Fid Q, Nay Wamitego, Rich Mavoko, Vanessa Mdee, Juma Nature, Barnaba, Linah, Belle 9 na wengine wengi katika mchakato unaoendelea kuwawezesha wasanii kujipatia kipato kutokana na muziki wao kupakuliwa kwenye mtandao. Diamond kabla ya kuondoka kuelekea Afrika ya Kusini kwaajili ya video yake mpya aliona ni vyema kuungana na Mkito.com kwani ni kampuni ya Kitanzania yenye madhumuni mazuri kwa tasnia ya muziki nchini. Watumiaji wote wa Mkito.com sasa wanaweza kupata nyimbo za Diamond kupitia www.mkito.com ikiwemo albam ya Best Of Diamond na pia wimbo wake mpya Mdogomdogo.

  0 0

  Hapana shaka umeshamsikia Mkude Simba kwenye mitandao, hasa Whatsapp, akichana watu mbavu kwa lafudhi yake ya Kiluguru na vituko kibao. Kama hujamsikia basi Mkude Simba ndio gumzo la mujini hivi sasa. Naye anapatikana katika kituo kipya cha redio inayokuja juu kwa kasi nchini E-FM 93.7 ambapo usiku ni ngoma ya mchiriku kwa kwenda mbele....Hehehheee

  0 0
 • 06/21/14--20:00: ngoma azipendazo ankal
 • Toni Braxton - Breathe Again

  0 0  SWC Fixtures Poster on SUPESPORT

  0 0

  Meya wa Ilala, Jerry Silaa akifungua rasmi tamasha la kuchangia damu katika viwanja vya Stakishari, Majumbasita, Dar es Salaam leo. Kampeni hiyo ya siku 10 iliratibiwa na Diwani wa Kipawa Bonnah Kaluwa (CCM).
  Meya Silaa akipata maelezo kutoka kwa maofisa wa Damu Salama kabla ya kuchangia damu ili kuwaokoa wagonjwa wakiwemo wakina mama wajawazito katika viwanja vya Sitakishari Majumbasita, Dar es Salaam.
  Meya Silaa na Diwani Bonnah wakiendelea kusikiliza maelezo kutoka kwa maofisa wa damu salama kabla ya kuchangia damu ili kuwaokoa wagonjwa wanaoteseka mahospitali kwa kukosa damu.
  Meya wa Ilala, Jerry Silaa akiugulia maumivu ya sindano wakati akitoa damu ili kuwaokoa wagonjwa wanaohitaji damu katika hospitali mbalimbali wakiwemo wajawazito bila kuwasahau madereva na abiria wa bodaboda wanaoandamwa na ajali.
  Diwani wa Kipawa, Bonnah Kaluwa naye akidhihirisha azma yake ya kuchangia damu kwa vitendo katika kilele cha kampeni yake ya kuchangia damu jana katika viwanja vya Sitakishari, Majumbasita ambapo mamia ya wakazi wa Dar es Salaam walijitokeza.
  Mwakilishi wa Chuo cha Diplomasia, Kennedy Ndosi (katikati) aliyewahamasisha wanafunzi wa Chuo hicho waliofika kuchangia damu akiwasikiliza Meya Silaa na Diwani Bonnah wakati wa tamasha hilo.

  0 0

  Kamishna wa Magereza Nchini Namibia, Raphael Tuhaferi(suti nyeusi) akisalimiana na Maafisa Waandamizi wa Magereza Mkoani Kilimanjaro alipotembelea Kiwanda cha Viatu, Gereza Kuu Karanga Moshi, Juni 21, 2014 Mkoani Kilimanjaro.
  Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini Namibia, Raphael Tuhaferi(suti nyeusi) akiteta jambo na Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma Malewa(vazi la drafti) alipotembelea Kiwanda cha Viatu, Gereza Kuu Karanga Moshi, Juni 21, 2014. Wengine ni Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza Mkoani Kilimanjaro.
  Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini Namibia, Rafael Tuhaferi(wa pili kushoto) akiangalia viatu vya ngozi vinavyotengenezwa na Kiwanda cha viatu, Gereza Karanga Moshi(wa kwanza kushoto) ni Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma Malewa.
  Wafungwa wa Gereza Kuu Karanga Moshi wakishona viatu vya ngozi katika Kiwanda cha Viatu, Gereza Kuu Karanga Moshi. Wafungwa hao wamepewa Mafunzo ya Ufundi wa kutengeneza viatu vya aina mbalimbali ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Programu mbalimbali za Urekebishaji wa Wafungwa ambapo kutokana na ujuzi huo pindi wamalizapo vifungo vyao watakuwa wamepata ujuzi ambao utawasaidia huko katika jamii zao.
  Viatu aina ya Buti ambavyo hutumiwa na Maafisa na Askari wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama hapa Nchini vinavyotengenezwa na Kiwanda cha Viatu, Gereza Kuu Karanga Moshi. Kiwanda hicho pia hutengeneza viatu vya ngozi vya aina mbalimbali ambavyo hutumiwa pia hata na raia.

  0 0

    Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova (katikati), na  Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya  Astarc Motors Tanzania Ltd, Sameer Musale (kushoto), akifungua kitmbaa kuashiriauzinduzi wa pikipiki mpya aina ya Hero Dawn 125cc katika hafla yailiyofanyika jijini Dar es Salaam jana.
    Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova akijaribu moja ya pikipiki mpya aina ya Hero Dawn 125cc katika hafla ya uzinduzi wa pikipiki hiyo jijini Dar es Salaam jana. Wa tatu
  kushoto ni  Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya  Astarc Motors Tanzania Ltd, Sameer Musale na  wawakilishi kutoka Astarc.
   Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova (kulia), akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya  Astarc Motors Tanzania Ltd, Sameer Musale (kushoto) katka hafla hiyo.
    Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Kanda ya Dar es Salaam Kamishna Msaidizi wa Polisi, Amiri Konja (kulia) akitoa rai kwa waendesha bodaboda kutii sheria za barabarani ili klupunguza ajali ambazo tawimu zinaonyesha kuongezeka. Kulia kwake ni  Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova (katikati), na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya  Astarc Motors Tanzania Ltd, Sameer Musale.
   Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Roma Mkatoliki akitoa burudani katika hafla ua uzinduzi wa pikipiki aina ya Hero Dawn 125cc jijini Dar es Salaam jana.

  0 0

  Na Anna Nkinda – Maelezo, Lindi.

  Wazazi na walezi wilayani Lindi mjini  wametakiwa kuwekeza katika elimu ya  watoto wao kwa kuhakikisha wanakwenda shule kwa wakati kwani  elimu ni ukombozi wa maisha na kuolewa katika umri mdogo kwa watoto hao hakutawasaidia kimaisha.

  Mwito huo umetolewa jana na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa (NEC) wilaya ya Lindi mjini Mama Salma Kikwete wakati akiongea  kwa nyakati tofauti  na viongozi wa Halmashauri kuu ya tawi ya Chama hicho katika matawi yaliyopo kweye kata za Chikonji, Tandangongoro na Ng’apa  wilaya ya Lindi mjini.

  Mama Kikwete ambaye pia ni Mke wa Rais Jakaya Mrisho Kikwete alisema  ni jukumu la mzazi na mlezi kusimamia elimu ya mtoto wake pamoja na kumpa malezi mazuri kwa  kufuata malezi ya zamani yanayoendana na mila na utamaduni wa mtanzania  kwani hivi sasa kutokana na utandawazi mienendo ya vijana wengi siyo mizuri.

  MNEC huyo pia aliwataka watoto waliofika kumsalimia mara baada ya kumaliza mkutano wake wa ndani na viongozi hao wa CCM kusoma kwa bidii na kuacha tabia ya utoro kwani elimu pekee  ndiyo itakayowakwamua na hali ngumu ya maisha.

  Aidha Mama Kikwete  aliwahamasisha viongozi wa Halmashauri kuu ya tawi ya CCM kujiunga katika vikundi mbalimbali vya maendeleo  na kuandika maandiko ya kibiashara ili wapate mkopo kutoka Serikalini  na kuweza kufanya miradi kama ufugaji wa kuku, mamalishe, ufundi seremala, kwa kujishughulisha  na biashara hizo  watakuwa wamejikwamua kiuchumi.

  “Mkijiunga katika vikundi vya ujasiriamali mtaweza kukopa fedha kutoka Serikalini jambo la muhimu mkumbuke kuwa fedha hizi  hampewi bure  mnatakiwa kuzirudisha ili na wenzenu waweze kukopa”, alisema Mama Kikwete.

  Kwa upande wa Afya aliwahimiza  kina mama kujitokeza kwa wingi kupima afya zao ikiwemo  saratani ya matiti na shingo ya kizazi ambayo inatibika ikiwa  itagundulika mapema mgonjwa atapata matibabu na kupona.

  “Hivi sasa kuna maradhi  mengi ikiwemo saratani ya matiti na shingo ya kizazi msiogope kwenda kupima na kujua  afya zenu. Nanyi kinababa wahimize wake zenu  wakapime ugonjwa huu, mkiona dalili  wawapeleke Hospitali mapema  kwani ugonjwa huu unatibika kama mgonjwa atawahi   mapema kupata matibabu”, alisisitiza.

  Alimalizia kwa kuwataka viongozi hao kuonyesha mfano kwa wananchi kwa kujenga nyumba bora za matofali ya kuchoma na kuezeka kwa bati na siyo za miti kwani moja ya sera ya CCM  ni kuwahamasisha wananchi kutunza  mazingira na kutokukata miti hovyo.

  Akiwa katika Kata ya Chikonji MNEC huyo alikagua mradi wa maji wa Kwamtokama na kujionea maendeleo ya  mradi huo ambao ukikamilika utawanufaisha wananchi wapatao  elfu saba kutoka  vijiji vya Jangwani, Nanyanje , Chikonji Kusini na Kaskazini.

  Mama Kikwete ambaye ni mjumbe wa NEC Taifa kupitia wilaya ya Lindi mjini alikutana na viongozi hao wa Halmashauri kuu ya matawi ya CCM  katika matawi ya Chikonji Kusini na Kaskazini,Nandambi, Kilolombwani na Cheleweni kwa ajili ya kuimarisha kazi za chama hicho ikiwa ni pamoja na kufanya vikao vya ndani na viongozi na kuangalia utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya mwaka 2010

  0 0

  Ndugu,Jamaa na Marafiki ,

  Tunasikitika kuwataarifu ya kuwa Ndugu yetu na mwanajumuiya mwenzetu Elibariki Mshomi amefiwa na mdogo wake,Robert Mshomi huko Moshi Tanzania.Mazishi yamepangwa kufanyika Jumatatu June 23 2014 nyumbani kwao Moshi.
   
  Kama ilivyo kawaida ya desturi yetu,tunaombwa kujitokeza kumfariji ndugu yetu katika kipindi hiki kigumu.

  Tutakuwa na Memorial Service,maombi  na nafasi ya watu kuleta rambi rambi siku ya jumapili June 22nd 2014 saa kumi na nusu jioni (4.30pm) nyumbani kwa EliBariki -Rogers Minnesota.

  Anwani: 22820 Gardner Avenue,Rogers,MN 55374.

  Bwana Alitoa,na Bwana Ametwaa,Jina la Bwana Libarikiwe !

   Kwa niaba ya Kamati,

  Gracious Msuya,
  Mwenyekiti.
  Tel:763-439-5626.

  0 0

   Diamond Platnumz akifanya mavituzz ukumbini na wacheza show wake wakiwa wanaendeleza manjonjo
   Waaaawwwoohh..ni umati haswaaa..kweli Diamond anapedwa
   Diamond Platnuz kijana mdogo mwenye mafanikio katika mziki na kimaisha akiimba wimbo wa nimpende nani
   Umati wa watu wakiendelea kupata burudani ya muziki toka kwa msanii Diamond Platnumz
  Ngololo aai ngololo mama  ngololo...... and show me how they do ngololo ngololo ni Saidi Biboze na dada yake Zuhra Biboze wakijiachia kwa raha zao.

  0 0

               
  Na: Hassan Hamad, OMKR.
  Wakati Chama Cha Wananchi CUF kikiingia katika uchaguzi Mkuu Taifa kuanzia kesho tarehe 23/06/2014, Viongozi wakuu wa Chama hicho wamewataka wajumbe watakaokosa nafasi za uongozi kutobabaika, na badala yake waendelee kukijenga chama hicho.
   
  Akizungumza katika hafla maalum ya kuagana na wajumbe wa Baraza Kuu pamoja na watendaji wengine wa ngazi mbali mbali, Katibu Mkuu wa Chama hicho Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, amesema kila mwanachama ana wajibu wa msingi wa kukijenga chama bila kujali wadhifa alionao.
   
  “Wasiorudi kwenye baraza kuu na ngazi nyengine yeyote ya uongozi bado wana mchango mkubwa wa kukijenga chama chetu ili kiweze kushika dola mwaka 2015, na jukumu hilo limo ndani ya katiba ya chama chetu”, alisisitiza Maalim Seif katika hafla hiyo iliyofanyika nyumbani kwa Mwenyekiti wa Chama hicho Prof. Ibrahim Lipumba katika eneo la Kunduchi Dar es Salaam.
   
  Amewapongeza wajumbe wa Baraza Kuu la Uongozi kwa mashirikiano waliyokuwa nayo katika kipindi chote cha miezi 64, hali ambayo amesema imeleta mafanikio makubwa ndani ya chama hicho.
   
  Maalim Seif amesema ndani ya kipindi hicho Chama pia kilikabiliwa na changamoto mbali mbali ambazo hata hivyo kwa kutumia busara na hekima za viongozi waliweza kuzitatua.
   
  Amewasisitiza wajumbe watakaochaguwa kuendeleza umoja na mshikamano uliopo, ili kuweza kufikia malengo waliyojiwekea ya kukamata hatamu za dola katika uchaguzi mkuu ujao.
   
  Mapema akizungumza katika hafla hiyo, Mwenyekiti wa CUF Taifa Prof. Ibrahim Lipumba ambaye anakabiliwa na upinzani katika uchaguzi huo, ameahidi kukubaliana na matokeo ya uchaguzi huo, na iwapo atashindwa ataendelea kukiunga mkono chama hicho kwa kutoa kila msaada unaostahiki kwa maendeleo ya chama.
   
  “Mimi nikiangushwa katika uchaguzi nitaendelea kuwa mwanachama na kutoa mchango wangu wote kwani suala hili la kugombea nafasi ni haki ya kikatiba kwa wanachama wote” alieleza Prof. Lipumba na kuongeza,
   
  “Nilikuwa mwanachama wa kawaida kwa kipindi kirefu ndipo ikafika wakati chama kikaniteua kugombea na kuchaguliwa Mwenyekiti hadi leo, kwa hivyo haki hii anaweza kuwa nayo mwanachama yeyote”, aliweka bayana Prof. Lipumba.
   
  Jumla ya wagombea watatu wamejitokeza kugombea nafasi ya Uenyekiti Taifa akiwemo Mwenyekiti wa sasa Prof. Ibrahim Haruna Lipumba.Wagombea wengine wa nafasi hiyo ya Mwenyekiti Taifa ni  M’bezi Adam Bakar kutoka Temeke Dar es Salaam na Chifu Lutalosa Yemba kutoka Shinyanga.
   
  Nafasi ya Makamu Mwenyekiti ina mgombea mmoja ambaye ni Mhe. Juma Duni Haji na Ukatibu Mkuu ni Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad.
  Aidha Prof. Lipumba ametumia fursa hiyo kuwaeleza wajumbe kuwa bado chama hicho kinaendelea na juhudi zake ili kuweza kupata katiba ya wananchi, katika mchakato wa katiba mpya unaotarajiwa kuendelea tena mwezi Ogasti, 2014.
   
  Katika hatua nyengine Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho Mhe. Machano Khamis Ali, amesema ameamua kwa hiari yake kutogombea tena nafasi hiyo kutokana na sababu mbali mbali zikiwemo sababu za kiafya.
   
  “Mimi nimeamua kuwa mfano ndani ya chama chetu, sitaki kuwa king’ang’anizi wa nafasi hii, nimeona nisigombee tena nafasi hii kutokana na sababu nilizozieleza, lakini nakuahidini kwamba sitokwenda chama chengine na nitaendelea kutoa mchango wangu wote katika kukijenga na kukiendeleza Chama chetu”, aliweka wazi Mhe. Machano.
   
  Mapema akitoa neno la shukrani kwa niaba ya wajumbe wa Baraza Kuu na watendaji wengine wa Chama  hicho, Bibi Najma Khalfan amewatanabahisha viongozi na wanachama kuungana ili waweze kupata ushindi katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.

  0 0

  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Hamis Mdee akitoa maelekezo kwa Maofisa wa Mfuko huo katika maonesho ya maadhimisho ya Wiki ya Utumishi kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja.
  Maofisa wa Mfuko katika banda la NHIF kitengo cha Usajili wa wanachama wakiendelea na uhakiki wa nyaraka kwa ajili ya vitambulisho.
  Wadau waliotembelea banda la NHIF wakipatiwa huduma.
  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Hamis Mdee akitaka ufafanuzi wa jambo katika banda la Mamlaka ya Vitambulisho (NIDA).
  Kaimu Mkurugenzi Mkuu katika picha ya pamoja na watumishi wa Mfuko walioko kwenye maonesho hayo.
  Bw. Mdee pia alipata fursa ya kutembelea banda la GEPF.
  Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti Raphael Mwamoto akifafanua jambo kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu.

  0 0

  Sensei Rumadha Fundi, akiwa katika "Japan Karate-Do Federation KATA SEMINAR " iliyofanyika Jumamosi Juni 21,2014 katika ukumbi wa University of St. Thomas, Houston, Texas chini ya Master Sensei Masataka Muramatsu Dan 8 ( Hanshi), master Tatsuo Takegawa Dan 7 ( Kyoshi), kutoka Japan na washiriki kutoka Marekani, Mexico na bara la Ulaya chini ya uandalizi wa Sensei Ramon Veras Dan 6 wa Houston, Texas, USA. 
  Sensei Rumadha Fundi akiwa katika picha ya pamoja na master Muramatsu
  Sensei Rumadha Fundi akifanya mambo yake.
  Sensei Muramatsu na Sensei Tatsuo Takegawa toka Japan. 
  Picha ya pamoja.
  Sensei Rumadha Fundi akionyesha Cheti chake.
  Sensei Rumadha na Sensei Ernie Salinas. 

  0 0
 • 06/22/14--10:44: Ubongo Kids world cup

 • 0 0

   Mwenye Koti jeusi katikati Mkurugenzi Mkuu wa Viwanja vya Ndege Nchini Suleiman S. Suleiman  akiangalia mfano wa jengo la Tatu (Termina III) ),alipotembelea banda la Taasisi yake wakati wa Maonyesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma katika viwanja vya Mnazi Mmoja jana jijini Dar es Salaam. Jengo hilo linalojengwa katika eneo la Kipawa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNIA) na linatarijiwa kutumiwa na Wasafiri wa Kigeni pindi litakapokamiilka.Mwenye kilemba kichwani ni Afisa Rasilimali Watu Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Bibi. Fatma Mtimba, anayemfuatia ni Meneja Rasilimali Watu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Bw. Mohamed Ally na anayeelezea mfano wa Jengo hilo ni Mchambuzi wa Mifumo ya Kompyuta Bw. Geofrey Youze..
    Kushoto Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Nchini Suleiman S. Suleiman akifurahia jambo na baadhi ya wafanyakazi wa Mamlaka hiyo alipotembelea Maonyesho ya Wiki wa Utumishi wa Umma yanayoendelea katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa TAA Bw. Laurent Mwigune, Afisa Habari Mwandamizi Bi. Frida Nkondokaya na Afisa Sheria na Mahusiano Bi. Nuru Nyoni.
   Afisa Habari wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga nchini (TCAA) Bw. Ally Z. Changwila akitoa ufafanuzi kwa mmoja wa mwananchi aliyetembelea banda la Taasisi yao wakati wa Maonyesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
   Katikati Afisa Vibali wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga nchini (TCAA) Bw. Christopher Peter Sabuni akielezea program yaKusaidi Wanafunzi wanaosomea masomo ya Urubani inayotolewa na Taasisi hiyo, kulia ni Afisa Habari wa Mamlaka hiyo Bw. Ally Z. Changwila. TCAA mpaka sasa imekwisha saidi jumla ya wanafunzi watano walioenda nchini Afrika Kusini kwa ajili ya masomo ya Urubani na Uinjinia wa Ndege. Picha na Frank Shija, WHVUM.

  0 0

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimsindikiza Dkt Anne Suk-Ching, Mjumbe wa Kamati ya Utendaji wa Chama Tawala cha Jamhuri ya Watu wa China baada ya kukutana naye  Ikulu jijini Dar es salaam leo Juni 22, 2014
   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Dkt Anne Suk-Ching, Mjumbe wa Kamati ya Utendaji wa Chama Tawala cha Jamhuri ya Watu wa China aliyemtembelea  Ikulu jijini Dar es salaam leo Juni 22, 2014

   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mhe Saoud Ali Mohamed Al Ruqaishi, Balozi wa Oman gapa nchini na Mjumbe Maalum wa Sultan Qaboos Bin Said wa Oman ikulu jijini Dar es salaam leo Juni 22, 2014.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea ujumbe kutoka kwa  Mhe Saoud Ali Mohamed Al Ruqaishi, Balozi wa Oman gapa nchini na Mjumbe Maalum wa Sultan Qaboos Bin Said wa Oman ikulu jijini Dar es salaam leo Juni 22, 2014.picha na IKULU

  0 0  0 0

  Mchezaji wa timu ya Ifiti, Kavin Mwandisi (kulia) akichuana na mchezaji wa timu ya Matema (FC), Hasani Njaa wakati wa fainali za Castle Lager Perfect Six Kanda ya Kinondoni zililofanika katika Ufukwe wa Coco Beach Dae es Salaam. Ifinit ilishinda mabao 5-4.
  Mchezaji wa timu ya Tegeta City, Amiry Ally (kushoto) akichuana na mchezaji wa timu ya Group six, Semi James wakati wa fainali za Castle Lager Perfect Six Kanda ya Kinondoni zililofanika katika Ufukwe wa Coco Beach Dae es Salaam. Tegeta ilishinda mabao 4-2.
  Mchezaji wa Timu ya Hot Shot, Kali Ongara (kushoto) akichuana na mchezaji wa timu ya Ifinit, Kavin Mwandisi, wakati wa fainali za Castle Lager Perfect Six Kanda ya Kinondoni zililofanyika katika Ufukwe wa Coco Beach Dar es Salaam Ifinit ilishinda mabao 8-4. 


  0 0

  Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Profesa Sifuni Mchome akimkabidhi Edward Mneda nyaraka za utendaji kazi kufuatia kuteuliwa kuwa Mkuu wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) Kanda ya Kati. Kushoto ni Mkuu wa Kanda Msaidizi wa Kanda ya Ziwa Beatrice Mpanda. Baraza hilo limefungua ofisi katika kanda tano Dodoma, Arusha, Zanzibar, Mbeya na Mwanza kurahisisha utekelezaji wa majukumu yake.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Profesa Sifuni Mchome akimkabidhi Rainey Mwinuka nyaraka za utendaji kazi kufuatia kuteuliwa kuwa Mkuu wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) Kanda ya Ziwa. Katikati ni Katibu Mtendaji wa NACTE Dk. Primus Nkwera na kushoto ni Mkuu wa Kanda Msaidizi Beatrice Mpanda. Baraza hilo limefungua ofisi katika kanda tano Dodoma, Arusha, Zanzibar, Mbeya na Mwanza kurahisisha utekelezaji wa majukumu yake.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Profesa Sifuni Mchome akimkabidhi Rainey Mwinuka nyaraka za utendaji kazi kufuatia kuteuliwa kuwa Mkuu wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) Kanda ya Ziwa. Katikati ni Katibu Mtendaji wa NACTE Dk. Primus Nkwera na kushoto ni Mkuu wa Kanda Msaidizi Beatrice Mpanda. Baraza hilo limefungua ofisi katika kanda tano Dodoma, Arusha, Zanzibar, Mbeya na Mwanza kurahisisha utekelezaji wa majukumu yake.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Profesa Sifuni Mchome (wa nne kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na watendaji mbalimbali wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) wakiwemo Wakuu Wapya wa Kanda Tano za Baraza hilo muda mfupi baada ya kuzindua rasmi kanda hizo jijini Dar es salaam. Wa tatu kushoto ni Katibu Mtendaji wa NACTE Dk. Primus Nkwera. Ofisi za kanda zilizozinduliwa ni Arusha (Kaskazini), Dodoma (Kati), Mwanza (Ziwa), Mbeya (Kusini) na Zanzibar.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Profesa Sifuni Mchome (kushoto) akibadilishana mawazo na mafias wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) wakati wa hafla ya uzinduzi wa ofisi tano za kanda za baraza hilo kwa lengo la kuharisisha utoaji huduma na usimamizi wa vyuo vya ufundi nchini. Kanda hizo ni Kaskazini (Arusha), Kati (Dodoma), Ziwa (Mwanza), Kusini (Mbeya) na Zanzibar.


older | 1 | .... | 479 | 480 | (Page 481) | 482 | 483 | .... | 3272 | newer