Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 478 | 479 | (Page 480) | 481 | 482 | .... | 3272 | newer

  0 0

  DSC_0397
  Mkali wa muziki wa reggae nchini, Ras Innocent Nyanyagwa na bendi yake wakitumbuiza kwenye tamasha la 17 la ZIFF 2014 linaloendelea kwenye viunga vya Ngome Kongwe visiwani Zanzibar.

  DSC_0438
  DSC_0461
  Ras Inno akiwapa mzuka mashabiki wake kwa kuruka na wamasai ndani ya Ngome Kongwe alipotoa show ya aina yake baada ya kuhudhuria tamasha la ZIFF miaka minane iliyopita.

  MKALI wa muziki wa rege nchini Innocent Nganyagwa anajiandaa kutoa filamu inayohusu maisha yake kama sehemu ya kufunza kizazi kijacho kuhusu muziki huo.
  Filamu hiyo ambayo itabeba maisha yake ya kuishi katika muziki wa reggae inatolewa kama ile ya Jimmy Cliff  "The hader they Come".
  Ras Nganyagwa mwenye albamu nne na tuzo tano za hapa nyumbani alisema pamoja na kukaa kimya kwa muda mrefu alikuwa hajaondoka katika muziki wa reggae lakini alikuwa anafundisha vijana ili reggae iwe na uendelevu nchini.
  Ras Nganyagwa ambaye alitumbuiza kwenye viunga vya Mambo Club iliyopo Ngome Kongwe amesema kwamba amekuja katika tamasha la ZIFF akiwa na mpya nyingi kuonesha wazi kwamba hakuwa mkaa bure.
  Akijibu swali kuhusu mahadhi ya muziki wake na imani yake ya kirastafarian amesema kwamba muziki wa rege japo upo ndani ya imani ya kirasta, unasimama wenyewe ndio maana mtu kama yeye hapigi rege ya Jamaica kama ilivyokuwa kwa Jimmy Clief, Burning Spear au Bob Marley.
  Amesema muziki wake ni wa kitanzania kwa sababu taifa hili lina vionjo vingi vya kufanya katika kuuza utamaduni wake nje kupitia muziki.
  Amesema japo miondoko ya mfumo wa Babylon bado ipo kuna mstari mwembamba sana kati ya dini ya rasta na muziki wa rege na mwitikio wa muziki wa ukombozi.Hata hivyo amesema kwamba sasa hivi anapiga muziki ‘mtamu’ (sweetie reggae) muziki wa mapenzi.

  0 0
 • 06/20/14--20:00: ngoma azipendazo ankal
 • Boyz II Men - "End Of The Road"

  0 0

         
       


                Leo hii Ijumaa Juni 20, 2014, kuanzia saa 5 mchana kwa saa za Marekani na saa 12 jioni kwa saa za Tanzania nimegundua kwamba akaunti yangu binafsi ya barua pepe kidundo2001@yahoo.comimevamiwa na wahalifu. 
  Nimechukuwa hatua stahili na za haraka katika kushughulikia tatizo hili. Naomba kuwashukuru wote walionitanabahisha kwa kufahamu kwamba niko Washington DC, Marekani,  na wakashangazwa kupokea barua pepe nyingi ambazo zimedai kwamba niko Nassau, Bahamas, Manila Philippines, Rio de Janeiro, Brazil na Singapore na kwamba nimepata matatizo ya kuvamiwa na majambazi na kuibiwa kila kitu na hivyo kuomba msaada wa dharura.

     Naomba kuchukuwa fursa kutoa taarifa hii  kwamba mimi niko salama Washington DC, Marekani, na ninaendelea na shughuli zangu za kazi katika Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania bila ya matatizo yeyote. Pia naomba mtu yeyote atayepata email kwa anuani hiyo aipuuze, si ya kweli. Nitatoa tena taarifa mara nitapokuwa na anuani yangu halisi muda si mrefu ujao.

     Namshukuru Ankal Muhidin Issa Michuzi kwa kunitumia taarifa ya kwanza kuhusiana na uhalifu huu, na kunishauri kuchukua hatua haraka.


  Suleiman Saleh

  Washington DC


  Juni 20, 2014


  0 0

   Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete leo amekumbuka enzi za kuwa mwalimu katika Chuo cha Jeshi la Wananchi wa Tanzania cha Monduli, Arusha, alipotoa  mhadhara  katika Chuo cha Taifa cha ulinzi (National Defence College -NDC- ) kilichopo Kunduchi  jijini Dar es salaam ambako aliahidi kwamba baada ya kustaafu Urais mwakani atakuwa mwalimu chuoni hapo. Pichani anaonekana  Rais Kikwete akisikiliza swali kutoka kwa mmoja wanafunzi hao baada ya mhadhara wake.
    Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete leo amekumbuka enzi za kuwa mwalimu katika Chuo cha Jeshi la Wananchi wa Tanzania cha Monduli, Arusha, alipotoa  mhadhara  katika Chuo cha Taifa cha ulinzi (National Defence College -NDC- ) kilichopo Kunduchi  jijini Dar es salaam ambako aliahidi kwamba baada ya kustaafu Urais mwakani atakuwa mwalimu chuoni hapo.  Pichani Rais Kikwete akijibu maswali kutoka kwa wanafunzi baada ya mhadhara wake
  Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Wahadhiri na wanafunzi wa  Chuo cha Taifa cha ulinzi (National Defence College -NDC- ) kilichopo Kunduchi  jijini Dar es salaam ambako aliahidi kwamba baada ya kustaafu Urais mwakani atakuwa mwalimu chuoni hapo.
  (PICHA NA IKULU)


  0 0

  Meneja wa Bia ya Ndovu Special Malt, Pamela Kikuli akizungumza na wadau wa bia hiyo wakati wa hafla ya kupongezana baada ya bia hiyo kutwaa tuzo ya ubora wa kimataifa(Ndovu High Quality Trophy) kutoka kwenye Taasisi ya Kimataifa ya Monde Selection nchini Ufaransa hivi karibuni.Hafla ilifanyika jijini Mwanza katika Hoteli ya JB Delmonte.
  Meneja wa Bia ya Ndovu Special Malt, Pamela Kikuli(katikati),Meneja Masoko TBL, Fimbo Butallah(kulia) na Meneja Masoko na Usambazaji TBL Kanda ya Ziwa, Malaki Sitaki wakigonganisha chupa wakati wa hafla ya kupongezana baada ya bia hiyo kutwaa tuzo ya ubora wa kimataifa(Ndovu High Quality Trophy) kutoka kwenye Taasisi ya Kimataifa ya Monde Selection nchini Ufaransa hivi karibuni.Hafla ilifanyika jijini Mwanza katika Hoteli ya JB Delmonte .
  Wadau wakipata Bia ya Ndovu Special Malt wakati wa hafla ya kupongezana baada ya bia hiyo kutwaa tuzo ya ubora wa kimataifa(Ndovu High Quality Trophy) kutoka kwenye Taasisi ya Kimataifa ya Monde Selection nchini Ufaransa hivi karibuni.Hafla ilifanyika jijini Mwanza katika Hoteli ya JB Delmonte .
  Meneja Masoko TBL, Fimbo Butallah(kulia) akizungumza na wadau wa bia ya Ndovu Special Malt wakati wa hafla ya kupongezana baada ya bia hiyo kutwaa tuzo ya ubora wa kimataifa(Ndovu High Quality Trophy) kutoka kwenye Taasisi ya Kimataifa ya Monde Selection nchini Ufaransa hivi karibuni.Hafla ilifanyika jijini Mwanza katika Hoteli ya JB Delmonte.Kushoto ni Meneja Masoko na Usambazaji TBL Kanda ya Ziwa, Malaki Sitaki na Meneja wa Bia ya Ndovu Special Malt, Pamela Kikuli.


  0 0

  Msanii Nguza Viking (kulia) na Mwanae Jonson Nguza Maarufu kwa jina la Papii Kocha ambao wanatumikia Kifungo chao kwenye Gereza la Ukonga jijini Dar,wakiwa na Bendi ya Wafungwa wakiimba Wimbo Maalum kuhusu Urekebishaji wa Wafungwa unavyofanyika Magerezani,Wanamuziki hao walitumbuiza katika Maadhimisho ya Magereza Day yaliyofanyika Juni 20, 2014 katika Viwanja vya Chuo cha Maafisa Magereza Ukonga.

  0 0

  Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote (EOTF) utaendesha mafunzo ya siku tatu -Jumatatu 23 -Jumatano 25 Juni 2014, katika ukumbi wa Mabati Jeshi la Kujenga Taifa Mgulani, Temeke, jijini Dar es salaam.

  Lengo la mafunzo haya kwa mwaka huu ni kuwaelimisha na kuwawezesha wanawake wajasiliamali jinsi ya kupata mitaji, masoko na kufanya biashara endelevu.

  Mada kuu zitahusu: Uwekezaji na Ukuazaji mtaji, Mtaji sio Lazima Uwe Fedha; Utunzaji wa Kumbukumbu za Biashara yako, Kuwaunganisha Wazalishaji na Masoko; Mnyororo wa Bidhaa; Mbinu za kushiriki Maonyesho ya Biashara, Usindikaji na Mazao, Usajili na Matumizi ya “Bar Code” na Elimu na uhamasishajiwa wa maradhi sugu na hatari kwa wanawake yanayorudisha Maendeleo yao – Saratani ya Matiti na Shingo ya Kizazi, Fistula, UKIMWI, Dengue/Malaria na Homa ya Ini.

  Watoa Mada ni pamoja na Wajasiriamali maarufu - IPP, Soko la Hisa la Dar-es-salaam- DSE, Wakufunzi kutoka TRA, TanTrade Chuo Kikuu cha Dar-es-salaam, Madaktari Kutoka CCBRT, Ocean Road, Ilala na Temeke .

  Wanawake wote mnakaribishwa kuhudhuria Mafunzo haya yenye lengo la kuwakomboa kiuchumi, Kiafya na kuwakutanisha kubadilishana ujuzi, Uzoefu na biashara.

  Hakuna malipo kwa kushiriki.
  KARIBUNI

  Mkurugenzi Mtendaji,
  Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote (EOTF).
  0715 263284
  DAR ES SALAAM

  0 0

  Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kiikwete akifungua Semina ya Africa Rural Commodity Exchange iliyofanyika katika ukumbi wa St.Gasper mjini Dodoma leo.Wapili kushoto ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue na watatu kushoto ni Mtaalamu wa Masoko ya mitaji kutoka Ethiopia Dkt.Eleni Gabre Madhin.
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akitoa hotuba ya ufunguzi wa semina ya Africa Rural Commodity exchange iliyofanyika katika ukumbi wa St.Gasper mjini Dodoma leo, Semina hiyo yenye maudhui Toward a vibrant Tanzania Commodity Exchange ilihudhuriwa na Mawaziri na makatibu wakuu.Semina hiyo iliendeshwa na mtaalamu wa masoko ya mitaji kutoka Ethiopia Dr.Eleni Gabre Madhin.Kushoto ni Waziri mkuu Mizengo Pinda.Picha na Freddy Maro

  0 0

  Mkurugenzi wa Huduma wa Kituo cha Uwekezaji Nchini (TIC), Bi. Nakuala Senzia (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari mwishoni mwa wiki kuhusiana na kongamano la siku mbili la uwekezaji na biashara linalotarajiwa kuanza kesho jijini Dar es Salaam. Wengine katika picha ni Meneja Mawasiliano wa TIC Bi. Pendo Gondwe, (katikati) na kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Stanbic Tanzania, Bw. Paul Omara. Benki hiyo ndiyo inayodhamini mkutano huo.
  Meneja Mawasiliano wa TIC Bi. Pendo Gondwe akizungumza na waandishi wa habari mwishoni mwa wiki kuhusiana na kongamano la siku mbili la uwekezaji na biashara linalotarajiwa kuanza kesho jijini Dar es Salaam. 

  0 0

  Mgeni rasmi katika ufunguzi wa Maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utawala Bora), George Mkuchika (kushoto), akisaini kitabu cha wageni, wakati alipotembelea banda la Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), katika ufunguzi huo. Kulia ni Ofisa Uhusiano wa SSRA, Agnes Lubuva.
  Mgeni rasmi katika ufunguzi wa Maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utawala Bora), George Mkuchika (kushoto), akisikiliza maelezo kutoka kwa Ofisa Uhusiano wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Agnes Lubuva (kulia), alipotembelea banda la mamlaka hiyo, wakati wa ufunguzi maonesho hayo hivi karibuni. 
  Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Uhamasishaji wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Sarah Kibonde, akiwapatia maelezo kuhusu kazi na majukumu ya mamlaka hiyo, baadhi ya wananchi walifika kwenye banda la mamlaka hiyo, katika maonesho ya wiki ya Utumishi wa Umma, Viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Saalaam jana.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

   Watu zaidi ya kumi wamepoteza maisha kwenye ajali ya Daladala inayofanya safari zake kati ya Ubungo - Tegeta jijini Dar mchana huu,baada ya kushindwa maarifa ya kiudereva kwa Dereva wa daladala hilo hali iliyompelekea dereva huyo kuhama mpaka upande wa pili wa barabara na kulivaa lori kwa nyuma.Chanzo cha ajali hiyo inaelezwa kuwa ni mwendo kasi.
   Hili ndilo lori lililokuwa likipita katika upande huo wa Barabara na kufatwa na daladala hiyo.  0 0

  MKUU wa Wilaya wa Magharibi, Hassan Mussa Takrima amewataka watendaji wa wizara ya afya kushirikiana na masheha katika kuelimisha wananchi juu ya utekelezaji wa mpango wa afya kwa jamii ili uweze kutatua changamoto za kifya nchini.

  Amesema kuwa endapo mpango huo ukihamasishwa kwa jamii utaweza kuwasaidia wananchi katika kujikwamua na matatizo ya kujikinga na maradhi mbalimbali yanayojitokeza katika maeneo yao .

  Akizungungumza katika ufunguzi wa mafunzo juu ya mkakati wa afya ya jamii kwa kamati kiongozi za shehia za Magogoni,Meli nne na Chukwani zilizopo katika wilaya Magharibi ili ziweze kufanya kazi kwa ufanisi katika kupunmguza matatizo ya kifya yanayozikabili shehia hizo.

  Alieleza kuwa serikali ya mapinduzi Zanzibar imeamua kutoa fursa kwa watendaji wa sekta ya afya waweze kufanya kazi kwa mashirikiano na viongozi kuanzia ngazi ya shehia kwa lengo la kuhakikisha kila mwananchi anakuwa na afya bora.

  “Tumieni mafunzo yenu vizuri kwa hekima na upole kwani nyinyi mnaenda kuielimisha jamii, na uko kuna makundi mbalimbali yanayotakiwa kupewa taaluma juu ya umuhimu wa kutunza afya na utekelezaji wa mpango huu kwa vitendo.”alisema Takrima.

  Nae Afisa wa afya wa wilaya hiyo, Abubakar Mohamed Ali ameeleza kuwa katika katika mafunzo hayo washiriki watafundishwa njia mbadala ya kuwawezesha masheha na viongozi wengine kutumia rasilimali zilizomo katika maeneo yao ili kutatua changamoto za kiafya bila kusubili utekelezaji kutoka serikali kuu.

  Kwa upande wake afisa mipango wa Wilaya hiyo Ameir Ali Haji alifamisha kuwa lengo la mkakati huo ni kuimarisha mahusiano baina ya sekta ya afya na jamii ili kuinua huduma za afya zinazotolewa ziweze kuendana na viwango vilivyowekwa na serikali.
  Mkuu wa Wilaya ya Magharibi Hassan Mussa Takrima akitoa nasaha kwa washiri wa mafunzo ya siku tano juu ya mkakati wa Afya ya jamii kwa viongozi wa kamati za Afya za Shehiya, katika ukumbi wa Ofisi ya walemavu Kikwajuni weles Mjini Zanzibar.
  Afisa Mipango na Utumishi wa Wilaya ya Magharibi Unguja Bw. Ameir Ali Haji akitoa maelezo juu mafunzo ya siku tano kwa viongozi wa kamati za Afya za Shehiya tatu za Magharibi, (kulia) Mkuu wa Wilaya ya Magharibi Hassan Mussa Takrima ambae ni mgeni rasmin katika mafunzo hayo. Yaliofanyi ukumbi wa Ofisi ya walemavu Kikwajuni weles Mjini Zanzibar.
  Muezeshaji kutoka kitengo cha elimu ya Afya ya jamii Wizara ya Afya Zanzibar Bi. Amina Sleyum akitoa mafunzo juu ya elimu ya Afya kwa jamii.

  Sehemu ya washiriki wa mafunzo hayo.Picha na Makame Mshenga wa Maelezo Zanzibar

  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amesema kuwa mfumo wa vyama vingi vya siasa ni mzuri, umeleta matumaini kwa kupanua wigo na kufungua zaidi uwanja wa kisiasa pamoja na kuiwajibisha Serikali.

  Hata hivyo, Rais Kikwete amesema kuwa ili mfumo huo uboreshwe zaidi na uweze kuimarisha misingi mikuu ya maendeleo ni lazima uendeshwa kwa watu kufuata sheria na wala siyo kuingiza matumizi ya nguvu ambayo yanaweza kuvuruga nchi.

  Rais Kikwete ambaye pia ni Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama aliyasema hayo jana, Ijumaa, Juni 20, 2014, wakati alipotoa Mhadhara (Lecture) kuhusu Usalama wa taifa – The Security of a Nation- kwenye Chuo cha Taifa cha Ulinzi  - National Defence College (NDC) Kunduchi, mjini Dar Es Salaam.

  Rais Kikwete alikuwa anajibu swali la mwanafunzi wa kozi ya pili kwenye chuo hicho kutoka Kenya ambaye alitaka kujua jinsi gani vyama vingi vya siasa vinavyoathiri umoja wa kitaifa na kuibadilishaTanzania kufuatia miaka zaidi ya 30 ya Tanzania kuwa nchi yenye kuleta matumaini kwa nchi nyingine za Afrika na Waafrika.

  Rais kikwete alisema: “Vyama vingi ni vizuri. Mfumo wa vyama vingi unaleta matumaini kwa kupanua wigo wa kisiasa ambao haukuwa mpana kiasi hicho huko nyuma. Sasa mtu anaweza kuamua kujiunga na chama chochote cha siasa anachokipenda yeye.”

  Aliongeza rais Kikwete: “Ni mfumo ambao unaiwajibisha Serikali. Ni mfumo mzuri kwa upanuzi wa demokrasia. Sasa watu wanaweza hata kuamua kupunguza bajeti ya safari za Rais nje ya nchi. Wanadhani kuwa Rais anaweza kufanikiwa zaidi na Tanzania kupita hatua za maendeleo haraka zaidi kama Rais atabakia amejifungia ndani ya nchi.”

  Rais Kikwete alizidi kujibu swali hilo: “Jambo la maana ni kwamba tunahitaji aina mbali mbali ya mawazo. Mawazo ya namna hiyo hayaathiri demokrasia. Mawazo ya namna hiyo yanasaidia hata chama changu kuimarika zaidi.”

  Hata hivyo, Rais Kikwete amesema kuwa mfumo huo utavurugika endapo baadhi ya watu wataendekeza matumizi ya nguvu na hoja za nguvu badala ya kupambana kwa hoja na nguvu ya hoja.
  “Wasiwasi wangu ni kuingiza matumizi ya nguvu katika ujenzi wa demokrasia. Ni makosa kwa watu kukimbilia kutumia nguvu baada ya kushindwa kwenye hoja. Na hili halivumiliki na likitokea basi Serikali itaingilia kati kudumisha amani.”

  Imetolewa na:
  Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
  IKULU
  DAR ES SALAAM 

  21 Juni, 2014


  0 0

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Tanzania Dkt Mohammed Gharib Bilal akikatautepe kuzindua mtambo wa Maji taka ya kiwanda cha Serengeti cha Mjini Mwanza kulia Mwenyekiti wa Bodi Nehemiah Mchechu kushoto Mkurugenzi Mtendaji Bw Steve Gannon.
   Makamu wa Rais wa jamhuri ya Tanzania Dkt Mohammed Gharib Bilal akisalimia wananchi wakati wa uzinduzi wa Mtambo wa Maji taka wa Kiwanda cha Serengeticha mjini Mwanza
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Tanzania Dkt Mohammed Gharib Bilal akiwa katika picha ya Pamoja na wafanyakazi wa kike wa Kiwanda cha Serengeti cha Jijini Mwanza.
   Makamu wa Rais wa jamhuri ya Tanzania Dkt Mohammed Gharib  Bilal akifungua kipazia kuzindua Mtambo wa Maji taka wa Kiwanda cha Serengeti cha Mjijini mwanza kushoto Mwenyekiti wa Bodi ya kiwanda cha Serengeti.
  Makamu wa Rais wa jamhuri ya Tanzania Dkt Mohammed Gharib Bilal akipata maelezo kwa Inspekta wa Mazingira Bi Anna Mangara  juu ya maji yaliyosafishwa kwenye Mtambo wakusafishia Maji taka kwenye kiwanda cha serengeti cha mjini mwanza.

  0 0

   Mke wa Rais na Mjumbe wa NEC Taifa kutoka Lindi Mjini Mama Salma Kikwete akiongea na baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Chikonji Kusini waliofika kuchota maji baada ya Mama Salma kutembelea chanzo hicho
   Mke wa Rais na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha MapinduziWilaya ya Lindi Mjini Mama Salma Kikwete akipata maelezo ya mradi wa maji wa Kwamtokama ulioko Kata ya Chikonji Wilayani  Lindi kutoka kwa Mhandisi Mshauri wa Kampuni ya Don Consult Limited Ndugu Ahmed Salum (kulia) huku baadhi ya wananchi wakichota maji kuhusu utekelezaji wa mradi. Mradi huo utakapokamilika utanufaisha wananchi waishio katika vijiji vinne vilivyopo katika kata hiyo ambavyo ni Chikonji Kaskazini na Kusini, Jangwani na Nanyanje vyenye wakazi wapatao 7000.  

  0 0

  Na Othman Khamis Ame, OMPR
   Mjumbe wa Kamati Kuu ya Hakmashauri Kuu ya Taifa ya  CCM Balozi Seif Ali Iddi alisema Chama cha Mapinduzi kina wajibu wa kuhakikisha kinashinda kwenye uchaguzi Mkuu ujao wa mwaka 2015 ili kiendelee kusimamia uhimili wa amani ya Taifa iliyopo hivi sasa.
  Balozi Seif alisema hayo wakati akizungumza na Viongozi pamojana Wana CCM wa Kisiwa Panza Wilaya ya Makoani Pemba mara baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa Tawi la Chama cha Mapinduzi la Mtondooni Kisiwani humo.
  Alisema ushindi huo utapatikana endapo wana CCM wenyewe na hasa Vijana watajitahidi kushikamana katika kuhakikisha kwamba kila mwanachama wa chama hicho atakuwa na kitambulisho kitakachompa fursa kamili ya kupiga kura kwenye uchaguzi huo.
  Balozi Seif aliwataka wana CCM hao kuwa makini wakati huu wa uhakiki wa Daftari la kudumu la wapiga kura na kumbanini mtu yeyote asiyestahiki kupiga kura kwenye eneo lao ili wamuekee pingamizi.
  Aaliwapongeza wana CCM hao wa Kisiwa Panza kwa uamuzi wao wa kuendelea kukiunga mkono chama hicho hasa katika kipindi hichi ambacho taifa liko katika mchakato wa kupata katiba mpya ya Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.
  Alisema umakini wao wa kuamini mfumo wa serikali mbili unaopendekezwa na Chama cha Mapinduzi unaongwa mkono na wazanzibari walio wengi katika maeneo mbali mbali ya Unguja na Pemba.
  Katika kuunga mkono juhudi za wana CCM hao Balozi Seif alichangia shilingi Milioni 2,000,000/- taslim kwa ajili ya kuongeza nguvu za ujenzi wa Tawi hilo la CCM la Mtondooni Kisiwa Panza.
  Akigusia suala la amani Balozi Seif ambae pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwapongeza Wananchi wote wa Kisiwa cha Pemba kwa kuendelea kuilinda amani iliyopo Nchini.
  Alisema Serikali inaendelea na operesheni kufuatilia tukio la hivi karibu la kuripuka kwa bomu katika eneo la Darajani na kusababisha kuuawa kwa mtu mmoja asiye na hatia na wengine kadhaa kujeruhiwa.
  Vitendo hivyo viovu vinavyotishia wasi wasi kwa wananchi vinaweza pia kuleta athari kubwa katika kuboresha sekta ya utalii inayotegemewa sana hivi sasa katika kukuza uchumi wa Taifa.
  “ Kwa kweli Serikali haitavumilia kuona vikundi vya baadhi ya watu vinasababisha au kuchangia katika kuchochea amani ya nchi. Vitendo hivi vinatishia kuporomoka kwa sekta ya Utalii “. Mahoteli mengi tumejenga sasa kwa muendelezo wa tabia hii atakuja kukaa nani ? Alisema Balozi Seif “.
  Kuhusu suala la jengo la Skuli ya Sekondari ya Kisiwa hicho lililokamilika Balozi Seif aliwaeleza wana CCM na wananchi wa Kisiwa hicho kwamba atawasiliana na Waziri wa Elimu ili kuapatiwa vikalio skuli hiyo ili ianze kazi mara moja.
  Alisema hatua ya kuanza kwa darasa hilo la sekondari itawaondoshea usumbufu na mashaka wanafunzi hao ya kuvuka mkondo wa bahari kila siku jambo ambalo ni hatari hasa wakati wa hali mbaya ya bahari.
  Mapema katika taarifa yao iliyosomwa na Mjumbe wa Halmashauri ya Tawi la Mtondooni Kisiwa Panza Nd. Khamis Juma Othman alisema wananchi wa kisiwa hichobado wanakabilisha na ukosefu wa mikopo kwa ajili ya kuendeshea miradi yao ya maendeleo.
  Nd. Juma alieleza kwamba wananchi wa kisiwa hicho wanakipongeza chama cha Mapinduzi kupitia serikali zake mbili kwa juhudi zake za kutekeleza ilani na chama hicho kwa vitendo.
  Alisema juhudi zilizochukuliwa na Waziri wa sayansi teknolojia wa Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Makame Mnyaa Mbarawa za kuwapatia huduma za maji safi na salama zimeleta faraja kubwa kwa wananchi hao.
   Msafara wa Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Balozi Seif Ali Iddi ukielekea Kisiwa panza kukagua shughuli za Chama ndani ya kisiwa hicho kiliopo kusini mwa Mkoa wa Kusini Pemba.

   Balozi Seif akishuka kwenye boti kuelekea katika maeneo ya Kisiwa Panza kwa ajili ya kuzungumza na wana CCM na wananchi wa kisiwa hicho.
    Kikundi cha ngoma cha Mkuta ngoma cha jimbo la mkanyageni kikitopa burdani kwenye mkutano wa hadhara wa Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Balozi Seif Kisiwani Panza.
   Mjumbe wa Halmashauri ya CCM Tawi la Mtondooni Kisiwani Panza Nd.Khamis Juma Othman akimfahamisha Balozi Seif hatua waliyofikia ya ujenzi wa Tawi lao .
  Mwenyekiti wa Tawi la CCM Mtondooni Kisiwa Panza Nd.Nassor Juma Amir akipokea mchango wa shilingi Milioni 2,000,000/- kutoka kwa Balozi Seif kusaidia uendelezaji wa Tawi lao la CCM. Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.  

  0 0

  Mkurugenzi wa Huduma wa Kituo cha Uwekezaji Nchini (TIC), Bi. Nakuala Senzia (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari mwishoni mwa wiki kuhusiana na kongamano la siku mbili la uwekezaji na biashara la China na Tanzania (China-Tanzania Business Forum) linalotarajiwa kuanza kesho jijini Dar es Salaam.  Wengine katika picha ni Meneja Mawasiliano wa TIC Bi. Pendo Gondwe, (wa pili kushoto), Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Stanbic Tanzania, Bw. Paul Omara (wa tatu kushoto), Afisa Habari Mkuu wa benki hiyo, Bi. Naomi Vincent na Mkuu wa kitengo cha huduma kwa wateja Wakubwa, Bi. Sylivia Shelukindo (kulia). Benki hiyo ndiyo inayodhamini mkutano huo. 

  0 0


  0 0

   "Ohoooooo.... Gari langu maskini...." Dereva wa teksi anatoka nje kuangalia jinsi gari lake lilivyoingia kwenye chemba ya maji machafu ambayo mfuniko wame umeeshaenda kusikojulikana na kuacha shimo kubwa katikati ya barabara ya Mtaa wa Zanaki jijini Dar es salaam leo
   Wasamaria wema wanasogea kuja kumuokoa
   "Hayaaaa....twendeeeeee" Gari linatoka
   Anapiga rivasi taratibu huku mshimo ukiwa umeachama  
  Anaondoka taratibu huku akisikitika na kujiuliza nini kifanyike kuondoa adha hii jijini....

  0 0

  Dotto Mwaibale, Morogoro
  WAANDISHI wa Habari nchini wametakiwa kutumia taaluma yao kwa ajili ya kuhamasisha Umma kuhusu umuhimu wa Takwimu.
  Wito huo umetolewa na Mkurugenzi wa Takwimu za Kiuchumi Morice Oyuke kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa.mjini Morogoro leo asubuhi wakati akifungua Warsha ya siku moja ya kuwajengea uwezo wanahabari kuhusu namna bora ya kuandika habari za kitakwimu.
  "Ninyi wanahabari ni muhimu katika masuala ya takwimu hivyo ni vizuri mjifunze jinsi takwimu zinavyoisaidia serikali, wadau wa maendeleo na wadau wa takwimu katika kupanga Sera na kufanya tathmini ya utekelezaji wa mipango mbalimbali ya kitaifa na kimataifa kama vile Dira ya Taifa ya Maendeleo ya mwaka 2025 Tanzania Bara na mwaka 2020 Tanzania Zanzibar" alisema Oyuke.
  Oyuke alitaja mambo mengine wanayopaswa kujifunza ni Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini Tanzania Bara (Mkukuta) Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini Zanzibar (Mkuza) na Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano 2010/11 mpaka 2015/16 na Malengo ya Melenia (MDGs).
  Alisema eneo jingine watakalofundishwa ni kuhusu Pato la Taifa na jinsi linavyokokotolewa na bei za ajira, takwimu za jamii na umuhimu wake.
  Dk.Chuwa alisema vyombo vya habari vinajukumu la kutoa taarifa sahihi zilizo rasmi ambazo zinazalishwa na tafiti mbalimbali nchini ili ziwafikie wadau wote nchini bila ya kupoteza maana.
  Mkurugenzi wa Takwimu za Kijamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Morice Oyuke (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari mjini Morogoro leo wakati akifungua Warsha ya siku moja ya kuwajengea uwezo wanahabari kuhusu namna bora ya kuandika habari za kitakwimu. Kulia ni Meneja wa Takwimu za Pato la Taifa, Daniel Masolwa.
  Meneja wa Takwimu za Pato la Taifa, Daniel Masolwa (kulia), akitoa mada katika warsha hiyo. Kushoto ni Watakwimu, Stephano Cosmas na Hashim Njowele.
  Mtakwimu, Stephano Cosmas, akitoa mada katika warsha hiyo.
  Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali wakiwa kwenye warsha hiyo.

older | 1 | .... | 478 | 479 | (Page 480) | 481 | 482 | .... | 3272 | newer