Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 480 | 481 | (Page 482) | 483 | 484 | .... | 3286 | newer

  0 0


   Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na wanachama wa CCM wa Tawi la STEMMUCO mkoani Mtwara wakati wa sherehe za kuwaaga wanachama wa CCM waliohitimu masomo yao katika Chuo cha SAUT ambapo aliwaambia wasomi washiriki katika kukisaidia chama hasa katika kuboresha sera mbali mbali.
   Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mtwara Ndugu Mohamed Sinani akizungumza wakati wa sherehe za kuwaaga wanachama wa CCM Tawi la STEMMUCO mkoani Mtwara ambao wamehitimu masomo katika Chuo cha SAUT ,Mwenyekiti aliwaeleza wanafunzi hao kuwa CCM ni chama pekee kinachoweza kuwavusha kutoka hapa walipo na kusonga mbele.
   Katibu wa CCM Mkoa wa Mtwara Ndugu Shaibu Akwilombe akizungumza wakati wa sherehe za kuwaaga wanachama wa CCM Tawi la STEMMUCO mkoani Mtwara ambao wamehitimu masomo katika Chuo cha SAUT ambapo alisisitiza wasomi kufanya tafiti zao kabla ya kuchagua chama gani cha siasa kinaweza kuwasaidia.
   Baadhi ya wanachama waliohitimu kutoka chuo cha SAUT wakifuatilia kwa makini hotuba kutoka kwa viongozi wao wakati wa sherehe za kuwaaga rasmi zilizofanyika kwenye ukumbi wa Pentecoste COCO Beach Mtwara
   Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akionyesha juu moja ya kadi za Chadema zilizorudishwa  kisha wanachama hao kujiunga na CCM

  0 0

  Waziri Mkuu,Mizengo Pinda akiongozana na Makamu wa rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Li Yuanchao baada ya mgeni huyo kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Arusha Juni 21, 2014 kwa ziara ya kikazi nchini.
  Waziri Mkuu,Mizengo Pinda akiongozana na Makamu wa rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Li Yuanchao baada ya mgeni huyo kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Arusha Juni 21, 2014 kwa ziara ya kikazi nchini. Kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Utawala Bora, Capt.George Mkuchika.
  Waziri Mkuu, Mizego Pinda akizungumza na Makamu wa Rais wa China , Li Yuanchao baada ya mgeni huyo kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Arusha Juni 21, 2014 kwa ziara ya kikazi nchini.
  Waziri Mkuu,Mizengo Pinda akizungumza na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Li Yuanchao baada ya mgeni huyo kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Arusha Juni 21, 2014 kwa ziara ya kikazi nchini. Kulia ni Waziri wa Nchi,Ofisi ya Waziri Rais, Utawala Bora, Capt. George Mkuchika. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0

  Uongozi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ukiongozwa na Jamal Malinzi Juni 21 mwaka huu mjini Dodoma umekutana na Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Maendeleo ya Jamii chini ya Mwenyekiti wake Mheshimiwa Said Mtanda (Mbunge wa Mchunga).

  Katika kikao hicho TFF ilielezea mikakati yake ya maendeleo ya mpira wa miguu pamoja na maandalizi ya timu ya Taifa kwa ajili ya mchezo wake dhidi ya Msumbiji.

  TFF iliiahidi Kamati ya Bunge kuwa itaendelea kuwa inafanya shughuli zake kwa karibu na Serikali na kamati hiyo ya Bunge.

  Katika kikao hicho, ujumbe wa benki ya CRDB ukiongozwa na Meneja wa Electronic Banking, Bw. Mangire Kibanda ulihudhuria ili kutoa ufafanuzi juu ya mradi wa kuuza tiketi za elektroniki, mradi ambao maandalizi yanaendelea vizuri.

  0 0

  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mathias Chikawe(katikati) akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Kiwanda cha kutengeneza Bakuli na Vikombe vitakavyokuwa vinatumika na Wafungwa Magerezani kulia chakula(wa kwanza kulia) ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja.
  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mathias Chikawe(kushoto) akiwaonesha Maafisa na Askari wa Jeshi la Magereza Mkoa wa Dar es Salaam jiwe la msingi la Jengo la Magereza Duty Free Shop iliyopo Gereza Keko, Jijini Dar es Salaam(kulia) ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja. Uzinduzi huo wa Magereza Duty Free Shop umefanyika juzi katika eneo la Gereza Keko.
  Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Nchini, John Casmir Minja akitoa maelezo mafupi kwa Mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mathias Chikawe(wa tatu kulia) kabla ya kumkaribisha rasmi kwa uzinduzi wa Magereza Duty Free Shop ya Gereza Keko (wa kwanza kushoto) ni Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini Namibia, Raphael Tuhaferi.
  Baadhi ya Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza waliohudhuria hafla fupi ya uzinduzi wa Magereza Duty Free Shop ya Gereza Keko, Jijini Dar es Salaam wakisikiliza hotuba ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mathias Chikawe(hayupo pichani).

  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mathias Chikawe(kulia) akikagua baadhi ya bidhaa zinazopatikana katika Magereza Duty Free Shop ya Gereza Keko, Jijini Dar es Salaam(wa kwanza kulia) ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Nchini, John Casmir Minja.
  Mabakuli na vikombe ambavyo vitakuwa vikitengenezwa katika Kiwanda cha Gereza Kuu Ukonga. Vifaa hivyo mabakuli na vikombe vitatumiwa na Wafungwa waliopo Magerezani kulia chakula. Katika picha anayeonekana ni Mpiga picha wa Jeshi la Magereza, Mkaguzi wa Magereza, Deodatus Kazinja akiwajibika ipasavyo wakati wa uzinduzi rasmi wa Kiwanda hicho, Gereza Kuu Ukonga, Jijini Dar es Salaam.

  0 0

  Tanzanian Atlanta-based Designer Linda Bezuidenhout ( LB ) will design a formal gown for Ms. Tanesha, that will be worn at the Nationals Finals of the Miss Plus America 2014 which will be held in Georgia at the Westin Hotel & Resort ( last year they were in Louisiana and the best dress winner was a Linda Bezuidenhout dress, worn by Mrs Alabama Octavia Mcclandon). This year the nationals of MISS AMERICA PLUS PAGEANTS will be held in Atlanta  Georgia starting  July 1st to 5th.

  Linda Bezuidenhout is also one of the sponsors of Miss Georgia Plus America Pageants  for the second year now and has been enjoying working with the CEO of Miss Georgia Plus America, Mr. Philip Micheal Bailey aka the "Professor of Pageantry" and the Co. Director Lady Marcella Meyer. 
   Ms. Georgia Plus America 2014 TANESHA SMART in LB STUDIOS when she went for dress fittings and consultations 
  This was sometime in november 2013 when Linda Bezuidenhout was the featured designer at the QUEENS OF THE NIGHT event, which was Organized by MISS GEORGIA PLUS AMERICA  PAGEANTS at  IWI SPAA Downtown ATL. Tanesha was one of the models, she was crowned Ms. Georgia Plus America in april 12th 2014. 

  0 0

  Washiriki wakifuatilia Majadiliamo katika Kongamano la  Kukaribisha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani la Mwaka 2014 ambapo "Vijana Wetu, Hazina Yetu" ndio  Kauli Mbiu ya Mwaka huu.
   Dr. Salha Mohamed akichangia mada kuhusu hali za Vijana Mayatima na Jinsi Jamii ya Kitanzania inavyoshindwa kuwaangalia na kuwaokoa na Changamoto za Dunia ya Leo katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam.
   Prof Mohamed Badamana akifafanua jinsi gani Malezi na Maadili Bora ya Vijana yanaweza kuwa Chachu ya Nchi zetu za Kiafrika kupiga hatua za Maendeleo ya haraka.
   Bro Ali Masoud AKA Masoud Kipanya Akitoa mada ya Umuhimu wa kufahamu Kuwasaidia vijana kuwa na Fikra Kubwa kuwawezesha Kumfahamu Mungu na Mazingira Yao Kuleta Maendeleo ya Jamii na Nchi.
   Washiriki wa Kongamano la Kukaribisha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani Wakimsikiliza kwa Makini Sheikh Mussa Kundecha alipokuwa akielezea Usomaji Qur'an, Ushiriki wa Katiba ya Nchi na Hatima ya Vijana.
   Wanataaluma wa Kiislam wakifuatilia kwa makini Mjadala wa Nafasi ya Vijana na Maendeleo ya Jamii ya Kitanzania Miaka Ijayo Katika Ukumbi wa JNICC - Dar es Salaam.
   Prof Mohamed Badamana wa Chuo Kikuu Cha Nairobi, Dr. Mohamed Mohamed Said, Mwanahistoria wa Tanzania na Sheikh Khaled Mtwangi wakibadilishana Mawazo wakati wa Kongamano la Kuukaribisha Mwezi Mtukufu.
   Washiriki wakiwa na Furaha Kwa Kujaaliwa Kushiriki Kongamano la Ramadhani Ambalo zaidi ya Wanataaluma  na Wanazuoni 700 walikutana na Kujadili nafasi ya Vijana na Mustakabali wa Nchi.
  Baadhi ya Wanataaluma Washiriki wa Kongamano la Kukaribisha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani wakati wa Mapumziko na Kubadilishana Mawazo.

  0 0
 • 06/22/14--16:42: lugha gongana hapa....


 • 0 0
 • 06/22/14--20:00: ngoma azipendazo ankal

 • Roxette - "It Must Have Been Love"

  0 0

  Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Tanzania Salum Mwalim akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kutangaza gulio la bidhaa za mawasiliano ikiwemo simu na ipad za kisasa lililoandaliwa na kampuni yake Juni 28 na 29 katika viwanja vya Leaders Kinondoni jijini Dar es salaam. Kulia ni Meneja Uhusiano wa Umma wa kampuni hiyo Matina Nkurlu. Hii ni mara ya pili kwa Vodacom kuandaa gulio la aina hiyo ikiwahusisha watengeneza bidhaa za simu za mkononi.

  Kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania imeandaa gulio kubwa la wazi kwa ajili ya mauzo ya bidhaa mbalimbali za simu, ipad na bidhaa nyengine zinazofanana na hioz kwa lengo la kuwakwezesha wateja wake na watanzania kwa ujumla kupata simu hizo kwa gharama nafuu zaidi ya gharama za kawaida za sokoni.

  Gulio hilo maarufu kwa jina la Vodacom Expo ni la pili kuandaliw ana Vodacom na linatarajiwa kufanyika kwa siku mbili mfululizo kuanzia tarehe 28 na 29 mwezi huu katika viwanja vya Leaders Club Kinondoni, jijini Dar es Salaam.

  Meneja Uhusiano wa Nje wa kampuni hiyo, Salum Mwalim amebainisha kuwa Vodacom Expo ni tukio kubwa ambalo wateja wa Vodacom na watanzania kwa ujumla hupata fursa ya kununua simu za kisasa na bidhaa za mawasiliano zenye ubora kwa bei ya chini tofauti na wanazouziwa madukani.

  "Mwaka jana kwa mara ya kwanza tulipoitisha gulio hili tulishuhudia idadi kubwa ya watu wakifurika kwa ajili ya kupata bidhaa mbalimbali za simu za mkononi, hali hiyo ilitupatia ujumbe kuwa wazo tulilolibuni limepokelewa vema na watanzania na kwmaba ipo haja ya kurudio tena tukio hilo ili tuwapatie tena fursa ya kupata simu za aina mbalimbali kwa gharama nafuu zaidi."

  Mwalim amesema uamuzi wa kufanya gulio hilo katika viwanja vya Leaders ni kuweza kukabiliana na changamoto ya msongamano wa watu kufuatia idadi kubwa ya watu wlaiohudhuria gulio la mwaka jana.

  Akizungumzia baadhi zitakazopatikana siku hiyo, Mwalim amesema "Safari hii simu za kisasa zikiwemo za smartphone ni nyingi zaidi kutoka makampuni tofauti na kizuri zaidi zitakuwa zimeunganishwa na ofa za vifurushi mbali mbali kutoka Vodacom kama vile muda wa maongezi, sms na intaneti."Aliongeza

  Mwalim amesema kuw lengo la Vodacom ni kutaka kuhakikisha kila mtanzania anakuwa na uwezo wa kumiliki simu bora na ya kisasa kwa ajili ya mawasiliano ya sauti na huduma za intanenti ili kuendana na aksi ya maendeleo kwenye huduma za simu za mkononi ambayo Tanzania kama ilivyo kwa mataifa mengine yanayoendelea.

  "Kupitia mtandao wetu tunajitahidi kadri ya uwezo wetu kumuwezesha kila mtanzania kumudu kumilki smartphone. Ningependa kuwaondoa shaka wateja wetu kuwa safari hii bidhaa ni nyingi, bei nafuu, muda wa manunuzi umeongezwa zaidi na hii yote ni kutokana na maoni tuliyoyapokea kutoka kwenu na kuyafanyia kazi, naomba mjitokeze kwa wingi siku hiyo."Aliongeza Mwalim.

  0 0

  Katika kile kinachoonekana kama nia thabiti ya kuzuia tatizo sugu la msongamano wa magari katika jiji la Dar es Salaam, utaratibu mpya wa kudhibiti changamoto hiyo uko mbioni kutangazwa.
  Mara utakapotangazwa, kila anayehusika hasa madereva katika jiji hilo kubwa la biashara watatakiwa kuuheshimu na kuufuata.
  Akitangaza utaratibu huo mpya unaotarajiwa kuanza hivi karibuni, Afisa Mkuu Mtendaji wa Wakala wa Mabasi yaendayo Haraka (DART), Bi. Asteria Mlambo hatua hiyo inalenga kuondoa msongamano, kuimarisha usalama na usafi katika njia zote zilizokamilika za mradi wa mabasi hayo.
  Mradi unaoendelea wa mabasi yaendayo haraka katika jiji la Dar es Salaam, unalenga kuimarisha huduma za usafiri na kuwa za kisasa zaidi pamoja na kupunguza msongamano ambao umekuwepo kwa kipindi kirefu sasa.
  Katika awamu hii ya kwanza mradi huo unahusisha ujenzi wa barabara maalum ya umbali wa kilometa 20.9 kutoka Kimara hadi Kivukoni; barabara ya Msimbazi kuanzia Faya hadi eneo la Kariakoo-Gerezani na sehemu ya barabara ya Kawawa kuanzia Magomeni hadi njia panda ya Morocco.
  “Tunatarajia utaratibu huu kuanza hivi karibuni,” Bi. Mlambo aliwaambia waandishi wa habari.
  Akizungumzia mahitaji ya utaratibu huo mpya alisema gari zote zitakazotumia njia katika mfumo wa njia hizo mpya hazitatakiwa kuzidi mwendo wa kilometa 50 kwa saa hasa katika barabara ya Morogoro ambapo mradi huo unakaribia kukamilika.
  Akielezea zaidi alisema magari hasa daladala hazitaruhusiwa kusimama njiani na pia itakuwa marufuku kufanya biashara ndogondogo au biashara ya aina yoyote katika maeneo ya njia hizo.
  “Kwa sasa tunaangalia maeneo ya muda ambayo daladala zitaruhusiwa kusimama,” alisema na kuongeza kuwa taratibu zote zimekamilika na kuwa polisi wataanza kuhakikisha kuwa utaratibu huo unafuatwa hivi karibuni.
  Kwa mujibu wa Afisa huyo wa DART, kupaki magari au kufanya biashara katika maeneo ya waenda kwa miguu haitaruhusiwa na watakaokiuka watakumbana na adhabu kali kwa mujibu wa taratibu.
  Pamekuwa na mazoea ya madereva wa bajaji na pikipiki kupaki vyombo vyao katika njia za watembea kwa miguu.“Napenda pia kuwataarifu wafanyabiashara kuacha kupaki magari ya mizigo katika njia kuu na kupakua au kupakia mizigo,” alisisitiza.
  Aliongeza kuwa itakuwa marufuku pia kupaki magari katika njia za pembeni na wala pikipiki hazitaruhusiwa kupita katika njia za waenda kwa miguu.

  “Makosa yatahusisha adhabu kali na faini ya pesa taslimu,” alisema.

  Utaratibu huo utasimamiwa na kufuatiliwa na vyombo mbalimbali kama DART, askari wa usalama barabarani, Mamlaka ya Usafiri wa majini na nchi kavu (SUMATRA) pamoja na TANROADS.


  0 0

   Mama Maria Nyerere akitoa nasaa wakati wa Ufunguzi wa Semina kwa Wanawake Wajasiliamali kutoka Mikoa yote ya Tanzania, akiwa ni Mwanamke Mjasiliamali pia, amewahakikishia wanawake mafanikio iwapo watajiamini na kumsirikisha Mungu katika kazi zao. 
   Mwenyekiti wa EOTF Mama Anna Mkapa, akitoa utangulizi wa Mafunzo na ntambulisho wa Waalikwa, wakati wa ufunguzi wa Mafunzo ya siku tatu kwa Wanawake Wajasiliamali, kuanzia Juni 23-25/2014, kuanzia saa2  asubuhi  katika ukumbi wa Bwalo la Maafisa wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Mgulani jijini Dares Salaam.Picha na Maelezo. 
   Mkurugenzi  Mtendaji wa Mfuko wa Fursa Sawa Kwa Wote(EOTF), Ndugu, Stephen Emmanuel akimkaribisha Mwenyekiti wa EOTF, Mama Anna Mkapa (hayuko pichani) leo, tarehe 23/06/2014 wakati wa Ufunguzi wa Semina kwa Wanawake Wajasiliamali kutoka Mikoa yote ya Tanzania Bara na Zanzibar. Mafunzo hayo yanalenga kumsaidia Mwanamke kukabiliana na changamoto za Ujasiliamali.
   
  Wanawake kutoka Mikoa Mbalimbali ya Tanzania Bara na Zanzibar wakiwa katika Ufunguzi wa Semina ya Mafunzo ya Wajasilaimali, Mafunzo ni ya muda wa siku tatu kuanzia Juni 23-25/2014, kuanzia saa2  asubuhi  katika ukumbi wa Bwalo la Maafisa wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Mgulani jijini Dares Salaam.
  Mgeni rasmi, Mwenyekiti wa IPP, Dkt. Reginald Mengi (aliayevaa Suti) akiwasili katika Ufunguzi wa Semina ya Mafunzo kwa Wanawake Wajasiliamali, Mbele ya Msafara ni Mama Maria Nyerere na Mwenyekiti wa EOTF Mama Anna Mkapa. Semina kwa Wajasiliamali imeandaliwa na Mfuko wa Fursa Sawa Kwa wote(EOTF), Mafunzo ni ya muda wa siku tatu kuanzia Juni 23-25/2014, kuanzia saa2  asubuhi  katika ukumbi wa Bwalo la Maafisa wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Mgulani jijini Dares Salaam

  0 0

   Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dkt. Fenella Mukangara (kulia) akisainiana mkataba na Naibu Waziri wa Wizara ya Biashara ya Wau wa China, Li Jinzao, wa Makabidhiano ya gari la matangazo la Shirika la Utangazaji la TBC, yaliyofanyika mapema mwaka huu. Shughuli hiyo ya kutiliana saini imefanyika leo Juni 23, 2014, Ikulu jijini Dar es Salaam, ikishuhudiwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Li Yuanchao
  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dorothy Mwanyika, (kulia) akisainiana mikataba miwili na Naibu Waziri wa Wizara ya Biashara ya Wau wa China, Li Jinzao, ya makubaliano ya ushirikiano wa Kitaalamu utakaoiwezesha China kuwapa mafunzo Wanariadha wa Tanzania nchini China na wa makubaliano ya awamu ya tatu ya Ushirikiano wa kiufundi baada ya China kusaidia na kukamilisha Ujenzi wa Uwanja wa Taifa. Shughuli hiyo ya kutiliana saini imefanyika leo Juni 23, 2014, Ikulu jijini Dar es Salaam, ikishuhudiwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Li Yuanchao. Picha na OMR
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika mazungumzo na  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Li Yuanchao, wakati alipowasili Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo June 23, 2014. Li Yuanchao, yupo nchini kwa ziara ya siku sita
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal (wa pili kulia) na baadhi ya Mawaziri wake, akiwa katika mazungumzo na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Li Yuanchao, aliyeongozana na ujumbe wake  wakati alipowasili Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Juni 23, 2014 kwa ajili ya mazungumzo.  Li Yuanchao, yupo nchini kwa ziara ya siku sita.
   Baadhi ya Mawaziri waliofika katika mazungumzo hayo Ikulu jijini Dar es Salaam, na baadhi kusaini mikataba na watu wa China.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkaribisha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Li Yuanchao, wakati alipowasili Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo juni 23, 2014 akiongozana na Ujumbe wake kwa ajili ya mazungumzo.  Li Yuanchao, yupo nchini kwa ziara ya siku sita.

  0 0

   Mhe. Fakih Jundu, Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania (kushoto) Akitia sahihi katika kitabu cha wageni alipotembelea Mahakama ya Wilaya GEITA mapema Leo, kulia Mhe. Jaji Mwangesi, Kaimu Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza.
   Baadhi ya Watumishi wakimsikiliza Mhe. Jaji Kiongozi mapema Leo
  Hakimu Mkazi Mfawidhi Mahakama ya Wilaya GEITA, Mhe. Kamugisha akisoma risala katika Mkutano wa Mhe. Jaji Kiongozi na Watumishi mapema Leo. (Picha na Mary Gwera, Mahakama ya Tanzania)

  0 0

   Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akitoa hotuba yake ya ufunguzi wa Mkutano wa Mwaka wa wakaguzi wa Hesabu za Serikali uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo(pich na Freddy Maro) .
  Baadhi ya wajumbe walioshiriki katika hafla ya ufunguzi wa Mkutano wa Mwaja wa wakaguzi wa Hesabu za Serikali uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Julius Nyerere(JNICC) jijini Dar es Salaam leo.(picha na Freddy Maro).
   Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali Bwana Ludovick  Utouh  akimkaribisha Rais Dkt.Jakaya Kikwete na kuwatambulisha baadhi ya wageni na viongozi waandamizi walioshiriki katika hafla ya ufunguzi wa Mkutano wa Mwaka wa wakaguzi wa Hesabu za Serikali uliofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Julius Nyerere(JNICC) jijini Dar es Salaam leo.

  Kutoka kushoto ni balozi wa Sweden Mh.Lennarth Hjelmaker, mdhibiti na mkaguzi Mkuu wa Serikali ya Sweden Bwana Jan Landahl, na watatu kutoka kushoto ni Bibi Lara Tayloir Pearce ambaye ni mdhibiti na mkaguzi mkuu wa Serikali ya Sierra leone.
   

  0 0

   Wakimbiaji wakitimua vumbi katika mashindano ya Bagamoyo Historical Marathon, mjini Bagamoyo, Pwani  jana. Mashindano hayo yaliandaliwa na Kampuni ya 4Beli.
   Mkurugenzi Msaidizi wa Maendeleo ya Michezo wa Wizara ya Habari,Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Juliana Yassoda (katikati) akihutubia wakati akifungunga mashindano ya Bagamoyo Marathon mjini Bagamoyo jana.
  Washiriki wa Bagamoyo  Marathon 2014  mara baada ya kumaliza mbio hizo ambazo kwa wanariadha wengine walikuwa bado wanawasili.
  KWA PICHA ZAIDI INGIA HAPA

  0 0

  Meya wa Manispaa ya Kinondoni Yusuph Mwenda (katikati) akisaini mkataba wa Ujenzi wa daraja la Mabwepande kwenda Kitongoji cha Kikwete Vision Mji Mpya na Meja Jenerali Dk,Charles Muzanila (kulia) wa Shirika la Ujenzi la Mzinga na Diwani wa Kata ya Mabwepande,Clement Boko (kushoto) huku wadau wakishuhudia.Sherehe ya kusaini ilifanyika eneo la ujenzi.
   Meya wa Manispaa ya Kinondoni Yusuph Mwenda (pili kulia) wakibadilishana nyaraka baada ya kutia saini ya ujenzi wa Daraja na Meja Jenerali Dk,Charles Muzanila (kulia) wa Shirika la Ujenzi la Mzinga na Diwani wa Kata ya Mabwepande,Clement Boko (kushoto) akishuhudia.
  Meya wa Manispaa ya Kinondoni Yusuph Mwenda (wa pili kushoto),Diwani wa Kata ya Mabwepande Clement Boko (kushoto) Naibu Meya Songoro Mnyonge (wa pili kulia) na Meja Jenerali Dk,Charles Muzanila (kulia) wa Shirika la Ujenzi la Mzinga,wadau wakiwa katika sherehe ya kusaini mkataba wa Ujenzi wa Daraja linalounganisha Mabwepande na Kitongoji cha Kikwete Visheni.
   Hili ndiyo eneo linalotarajiwa kujengwa Daraja Upande zinakoonekana nguzo za umeme Mabwepande na kwenye watoto ni Kitongoji cha Kikwete Visheni.
  Eneo la bonde lenye mto litakapo pita Daraja.

  0 0


    Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu akizindua maabara ya kompyuta katika  chuo cha Taasisi ya Taaluma ya wanyamapori Pasiansi Mwanza wakati wa mahafali ya 49 ya chuo hicho. Kulia ni Balozi wa Marekani Mark Childless.

  Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu na Balozi wa Marekani Mark Childless wakikagua gwaride la heshima la wahitimu wa chuo hicho.

  Wahitimu wakionesha utaalamu wa Karate.
   Wahitimu wa Uhifadhi wa wanyamapori katika chuo cha Taasisi ya Taaluma ya wanyamapori Psiansi Mwanza wakionyesha ujuzi wa kutumia silaha wakati wa mahafali ya 49 ya chuo hicho juzi.
   Wahitimu wa Uhifadhi wa wanyamapori katika chuo Taasisi ya Taaluma ya wanyamapori Psiansi Mwanza wakicheza gwaride juzi, wakati wa  wa mahafali ya 49 ya chuo hicho juzi.


  0 0

   Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Makamu wa Rais wa China, Li Yuanchao wakitazama picha za ziara ya hayati Baba wa taifa Mwalimu Julius Nyerere kabla ya mgeni huyo kufungua mkutano wa Uwekezaji kati ya Tanzania na China kwenye ukumbi wa Benki Kuu jijini Dar es salaam  Juni 23, 3014. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
   Waziri Mkuu, Mizengo Pinda  akimkabidhi zawadi ya kinyago, Makamu wa Rais wa China, Li Yuanchao  kabla ya mgeni huyo kufungua mkutano wa Uwekezaji kati ya Tanzania na China kwenye ukumbi wa Benki Kuu jijini Dar es salaam  Juni 23, 3014.
   Waziri Mkuu, Mizengo Pinda   na  Makamu wa Rais wa China, Li  Yuanchao wakifungua  vitambaa kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi la Kitegauchumi la Mfuko wa Mwalimu Nyerere mjini Dar es salaam Juni 23, 2014. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0

    The Director General of World Wide Fund for Nature (WWF) International Dr.  Marco Lambertini (Middle) cutting a ribbon to officially launch the Africa vision 2020 document. Left is Mr. Bell’Aube Houinato WWF Tanzania’s Country Director and right is Dr.Julius Ningu, Director of Environment – VPO witnessing in Dar es salaam on June 22nd  2014.
    The Director General of World Wide Fund for Nature (WWF) International Dr.  Marco Lambertini (Middle) showing the  Africa vision 2020 document , left is Mr. Bell’Aube Houinato WWF Tanzania’s Country Director and right is Dr. Julius Ningu, Director of Environment during the launch ceremony in Dar es salaam on June 22, 2014.
    The Director General of World Wide Fund for Nature (WWF) International Dr. Marco Lambertini giving a speech during the Africa vision 2020 document launch in Dar es salaam on June 22nd, 2014. 
   WWF International Dr. Marco Lambertini in group photo with WWF Tanzania  employees at their Dar es salaam Country Office.

  0 0

   Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisisitiza jambo wakati akizungumza na makamu wa Rais wa Jamhuri  ya Watu wa China Mh. Li Yuanchao ikulu jijini Dar es Salaam leo.
  -Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na mmiliki wa kampuni kubwa ya kuzalisha saruji DANGOTE Industries Ltd Alhaji Aliko Dangote ikulu jijini Dar es Salaam leo  (picha na Freddy Maro)

older | 1 | .... | 480 | 481 | (Page 482) | 483 | 484 | .... | 3286 | newer