Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live

HIVI NDIVYO HALI ILIVYO KATIKA SOKO LA ILALA MCHIKICHINI JIJINI DAR BAADA YA KUTEKETEA KWA MOTO

$
0
0
 Sehemu ya wafanyakazi wa Kikosi zimamoto wakiendelea na zoezi la kuzima moto ulioteketeza kabisa Soko la Ilala Mchikichini Jijini Dar es salaam leo.Moto huo ulianza majira ya saa sita usiku wa kuamkia leo na kuteketeza kila kilichokuwepo katika eneo la soko hilo. Chanzo cha kutokea kwa moto huo bado hakijajulikana mpaka sasa.Picha zote na Othman Michuzi.
 Kazi ya kuzima moto ikiendelea.
 Jitihada za kuuzima moto huo bado zinaendelea.
 Moto bado unaendelea kuwaka mpaka wakati huu,huku jitihada mbali mbali za kuuzima moto huo zikiendelea.


INVITATION TO A MOTIVATIONAL SEMINAR FOR MINDSET AND "KUONGEZA KIPATO"

$
0
0

Dear Sir,
We invite you to extremely exceptional Motivational Seminar for Self-Recognition involving changing the Mindset and MBINU ZA KUONGEZA KIPATO. The Seminar will mainly feature: JINSI YA KUBADILI FIKRA; KUONGEZA KIPATO na KUTIMIZA NDOTO. Your Organization can invite some key prospect clients and existing clients to attend. Your Organization may wish to provide any kind of Sponsorship and will be able to take advantage to promote its products and services at the events.

The Seminar will be presented by two Key Trainers & Motivational Speakers; Entrepreneurs; Business Owners & Consultants including Sanctus Mtsimbe, the presenter of “Wake-Up & Change” (AMKA NA BADILIKA) Motivational TV Program and Felix Maganjila Trainer of Trainers and Facilitators for SME’s. There will be two seminars and your invited to choose one. The first will take place on Thursday; 19th June 2014 and the second one on Sunday 22nd June 2014. Time for both are Seminars will be from 2.00 PM to 8.00 PM. The venue is  Chuo cha Utalii cha Taifa (National Institute of Tourism) at the junction of Shaaban Robert Street and Samora Avenue near Institute of Financial Management (IFM).

The participation or seminar fee per person per seminar is TZS 30,000/=. We have invited professionals; business people and representatives from companies to attend and we request and encourage you to invite your friends and other colleagues. This kind of training has proved to be very effective for company’s performance because of increased sales.

Registration for this Seminar is on going. For payments and further details, please contact:  +255 767 767 676 (timizandoto@gmail.com). In this event Ladies are strongly encouraged to attend to leverage their business opportunities.

NHC yavutia wawekezaji katika maonyesho ya Nyumba ya Dubai

$
0
0
    Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Mchechu akizungumza wakati wa kongamano
    Makamu wa Rais, Dr Bilal akizungumza
 Wageni waalikwa katika kongamano.

Dubai, United Arab Emirates-Katika kile kinachoonekana ni hatua kubwa katika kuelekea kutengeneza fursa kwenye sekta ya uendelezaji wa makazi, Shirika la Nyumba la Taifa limeweka historia kwenye soko la kimataifa na kufanikiwa kwa mara ya kwanza kufanya kongamano la uwekezaji hapa Dubai ambalo limefanikiwa kufikia lengo lake la kuonyesha fursa zilizopo kwenye sekta ya ujenzi kwa makampuni makubwa ya ujenzi yaliyopo Mashariki ya Kati na kwingineko.
                            Tukio hili la kipekee na kihistoria kwa Tanzania lilizinduliwa na Makamu wa Rais Mheshimiwa Gharib Bilal na lilihudhuriwa na makampuni makubwa ya ujenzi Dubai kama Damac, Nahkeel, Jumeirah na Emaar, ambayo yamehusika na ujenzi wa majengo makubwa na maarufu Dubai kama Burj Khalifa, Hoteli za Jumeira na Dubai Mall.
Makampuni mengine yaliyohudhuria kutoka ukanda wa Guba kama Qatar na Bahrain pamoja na nchi nyingine kama Korea, Sweden na Romania yameonyesha kuwepo kwa nia ya makampuni makubwa kuwekeza kwenye sekta ya makazi Tanzania.
Malengo ya Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa;
Kongamano la Wawekezaji Wa Sekta ya Makazi Tanzania ni sehemu ya lengo kuu la Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Mchechu, ambaye kwa sasa analiongoza shirika hilo kubwa Afrika Mashariki. Kipindi cha Msechu kwenye uongozi kimeonyesha mabadiliko na ubunifu mkubwa kwenye uendelezaji wa sekta ya makazi nchini.
Mchechu anasema lengo kuu la kongamano hili ni hatua kubwa kuelekea mkakati wa kuionyesha dunia kuwa Tanzania ni sehemu pekee likija swala la uwekezaji na urudishaji wa faida kwenye sekta ya makazi.
‘Tanzania inatoa fursa ya pekee linapokuja swala la uwekezaji kwenye sekta ya makazi barani Afrika na hii ni kutokana na uwazi pamoja na utulivu wa kisiasa na amani inayopatikana nchini, uchumi unaokua pamoja na ushirikiano mkubwa unaotolewa na serikali’ anasema Mchechu.
‘Tukio hili la kihistoria ni sehemu tu ya mpango kamili wa kuifahamisha dunia kuhusu fursa za uwekezaji kwenye sekta ya makazi zinazopatikana nchini’ alisema Mchechu.
Mchechu anaamini kuwa huu ni muda mwafaka kwa wawekezaji kuitazama Tanzania na Afrika kwa ujumla. ‘Zamani ilikuwa ni hatari kwa wawekezaji kuwekeza Afrika na Tanzania, lakini kwa uchumi wa leo, ni hatari kutokuwekeza Tanzania’ alisema Mchechu.
Kati ya miradi iliyoonyeshwa kwa wawekezaji ni pamoja na miradi mitatu ambayo itaendelezwa kwa kwa kipindi cha miaka 5. Hii inajumuisha miradi miwili ya kuendeleza Arusha inayoitwa Safari City na USA River ambayo kwa pamoja itakuwa na jumla ya nyumba 8000, pamoja na mradi mwingine wa kuendeleza makazi Dar es Salaam utakaofahamika kama Salama Creek Satellite City ambao utakuwa na jumla ya nyumba 9,500.

Miradi hii yote iko tayari kwa maana ya kuwa vibali vyote vya mradi vimepatikana na kinachotakiwa ni kuwekeza tu, na ndio maana kongamano hili lilikuwa muhimu kwa ajili ya kupata uwekezaji unaotakiwa.

BAHATI IDD NI MLEMAVU WA MIKONO ALIEJIKITA KWENYE KILIMO

UPASUAJI WA MATOBO LAPAROSCOPIA WAFANYIKA LIVE KAIRUKI HOSPITALI

$
0
0
 Daktari Bingwa wa upasuaji Dk. Muganyizi Kairuki akizungumza wakati wa semina ya upasuaji kwa njia  matobo Laparoscopia uliofanyika LIVE katika Hospitali ya Kairuki Mikocheni jijini Dar es Salaam. Semina hiyo iliwashirikisha madakatari wa ndani na nje ya nchi.
 Daktari Bingwa wa upasuaji kutoka Afrka Kusini, Prof. Zacharia Koto (wa pili kulia), akisaidiana na daktari bingwa wa upasuaji kutoka Namibia Dk. S. Kaikai (kulia) na Dk. Muganyizi Kairuki wakimfanyia operesheni ya kuondoa mawe tumboni mmoja wa wagonjwa waliolazwa katika hospitali ya Kairuki, wakati wa semina ya upasuaji kwa njia ya matobo iliyofanyika katika hospitali ya Kairuki Mikocheni jijini Dar es Salaam.
 Madaktari wakiwa kazini.

BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI

kombe la dunia laanza kwa brazil kuichapa croatia 3-1 katika mchezo unaolalamikiwa kuwa wenyeji wamebebwa na refa

$
0
0
Wenyeji Brazil  wameanza michuano ya Kombe la Dunia kwa ushindi finyu wa mabao 3-1 dhidi ya Croatia usiku wa kuamkia leo  wa jijini Sao Paulo, na kuponea chupuchupu kutoka sare katoka mchezo ulioanza kwa mabingwa hao mara tano kujikuta nyuma kwa goli moja la kujifunga wenyewe mwanzoni mwa kipindi cha kwanza. 
Nyota wa Brazil Neymar analalamikiwa kubebwa na refa Yuichi Nishimura kutoka Japana baada ya kuambulia kadi ya njano (badala ya nyekundu)  kwa kumpiga kwa makusudi kipepsi mlinzi Luka Modric wa Croatia mbele ya mashabiki 61,000. 
Dakika chache baada ya rafu hiyo, Neymar alisawazisha kwa mkwaju wa mita 25, kabla ya wenyeji kupata bao la pili, la penati (ya kubebwa) pale Fred alipojirusha ndani ya boxi baada ya kuguswa kidogo tu.


Oscar, aliyetajwa kuwa nyota wa mchezo, naye alifunga bao tamu la mchezo, kuihakikishia ushindi wa Brazil ambayo, hata hivyo, inatajwa  kubwebwa na FIFA ambayo inaonekana kutaka wenyeji washinde kombe hilo kwa hali yoyote ile.

 Hii inatokana na mbeleko tatu za wazi ambazo refa aliwabebea Brazil (kutomtoa Nyemar, kutoa penati kwa Fred kujirusha na kukataa bao la Croatia), kiasi hata makelele yanasikika kila kona kwamba Kombe la Dunia safari hii lina mizengwe mingi kama iliyoiandama FIFA (ya tuhuma za rushwa kuipa Qatar wenyeji wa mashindano), na wadadisi wanasema ngoja tuone iytavyokuwa.





  

HOTUBA YA WAZIRI WA FEDHA MHESHIMIWA OMAR YUSSUF MZEE KUHUSU MAPENDEKEZO YA MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA SERIKALI KWA MWAKA WA FEDHA 2014/15 KATIKA BARAZA LA WAWAKILISHI

$
0
0
WAZIRI WA FEDHA  WA ZANZIBAR MHESHIMIWA OMAR YUSSUF MZEE AKIINGIIA KATIKA UKUNBU WA BARAZA LA  WAWAKILISHI LEO

HOTUBA YA WAZIRI WA FEDHA MHESHIMIWA SAADA MKUYA SALUM (MB), AKIWASILISHA BUNGENI MAPENDEKEZO YA SERIKALI KUHUSU MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI KWA MWAKA 2014/15

$
0
0
MHESHIMIWA SAADA MKUYA SALUM (MB), AKIWASILI BUNGENI MJINI DODOMA KUWASILISHA MAPENDEKEZO YA SERIKALI KUHUSU MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI  KWA MWAKA 2014/15 LEO. 

JARIDA LA WIZARA YA NISHATI NA MADINI NAMBA 20

taswira mwanana ufukweni wakati wa mawingu ya mtawanyiko bila jua

$
0
0
 Siku moja moja Ankal huweka kamera begani na kwenda kusaka taswira. Hapa ni ufukwe wa Kunduchi jijini Dar es salaam ambako baharini kuna wadau wakicheza mchezo wa baharini


Watumishi wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma wahimizwa kuzingatia Maadili.

$
0
0
Na. Ally Mataula
Watumishi wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma wametakiwa kuzingatia maadili wanapokuwa wanatimiza majukumu yao ya kila siku. Wito huo umetolewa na Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais – Ikulu Bw. Peter Ilomo wakati akifungua Mkutano wa kumi na mbili wa Baraza la Wafanyakazi wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma uliofanyika Jijini Mbeya tarehe 28 Mei, 2014. 
Bw. Ilomo alisema kuwa jukumu kubwa la Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma ni kusimamia Maadili ya Viongozi wa Umma, hivyo basi ni muhimu kwa watumishi wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kuzingatia maadili mema. 
Bw. Ilomo aliendelea kufafanua kuwa huwezi kuwa mwangalizi wa maadili ya wengine wakati wewe mwenyewe huna maadili mema. 
 “Watumishi wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma wanatakiwa kuwa mfano wa kuigwa na watumishi wengine wa umma katika nyanja ya Uadilifu. Pamoja na changamoto nyingi mnazokabiliana nazo katika kazi zenu za kusimamia Maadili, ninawaomba sana Msikubali kuyumba au kuyumbishwa. 
Muendelee kufuata misingi ya Utawala Bora na Maadili mema katika utendaji kazi kwa kuepukana na Rushwa na kushinda vishawishi vya Rushwa na tamaa nyinginezo” alisisitiza Bw. Ilomo. 
Awali akimkaribisha Mgeni Rasmi kufungua Mkutano huo Kamishna wa Maadili Mhe. Jaji (Mst.) Salome Kaganda alisema kuwa ili kusogeza huduma karibu na wananchi, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma ilianzisha Ofisi za Kanda ambapo mpaka sasa kuna Ofisi za Kanda saba katika Mikoa ya Arusha, Mbeya, Tabora, Mtwara, Mwanza, Kibaha- Pwani na Dodoma. 
Mhe. Kagana alutumia fursa hiyo kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kwa Kuweza kuridhia kuongeza wigo wa Viongozi wanaowajibika na Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma, ambapo Maafisa Ugavi Wakuu wa Wizara, Wakuu wa Idara na Vitengo wa Serikali za Mitaa, pamoja na Viongozi mbalimbali waliopo Serikalini. 
 Pia , Mhe Kaganda aliomba Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma iwezeshwe kwa kuongezewa bajeti yao pamoja na idadi ya watumishi. 
Mikutano ya Mabaraza ya Wafanyakazi ni utekelezaji wa Waraka wa Rais Na. 1 wa mwaka 1970 wenye lengo la kuwashirikisha Wafanyakazi katika kubuni, kushauri na kupendekeza namna bora ya uendeshaji na utendaji kazi.
 Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais – Ikulu Bw. Peter Ilomo katikati akiwa katika picha ya pamoja na Kamishna wa Maadili Mhe. Jaji (Mst.) Salome Kaganda wa pili kutoka kulia pamoja na Watumishi wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma mara baada ya kufungua Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi  wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma.

Kamishna wa Maadili Mhe. Jaji (Mst.) Salome Kaganda akizungumza na Waandishi wa Habari mara baada ya ufunguzi wa Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma uliofanyika jijini Mbeya.

WABRAZILI WALIOPO TANZANIA WASHEREKEA UZINDUZI WA KOMBE LA DUNIA

$
0
0
 Balozi wa Brazili Tanzania Mhe. Francisco Carlos na Mkewe wakisheherekea uzinduzi wa Kombe la Dunia ambalo limeanza usiku wa kuamkia leo. Balozi huyo aliandaa tafrija katika hoteli ya Serena ambapo Wabrazili waishio Tanzania walishiriki pamoja na marafiki mbalimbali 
 Balozi wa Brazili hapa Tanzania Bw Frcisco Carlos akibadilishana mawazo na Rosalie Lehel kutoka IFAD ambaye alikuwa miongoni mwawageni walio alikwa katika kusheherekea uzinduzi wa kombe la dunia ambao linafanyika nchini Brazil
Wananchi wa Brazili waliopo Tanzania wakisheherekea kuanza kwa michuoano ya kombe la Dunia ilioanza jana nchini Brazili. Picha na Chris Mfinanga

BALOZI KAMALA AWAAGA MABALOZI WALIOMALIZA KIPINDI CHA KUWAKILISHA NCHI ZAO JUMUIYA YA ULAYA

$
0
0
Balozi wa Tanzania Jumuiya ya Ulaya na Mwenyekiti wa Kamati ya Mabalozi wa Afrika, Karibiani na Pasifiki (ACP) akimkabidhi zawadi Balozi wa Togo Jumuiya ya Ulaya Balozi Kodjo Sagbo kwa niaba ya Kamati ya Mabalozi wa ACP. Balozi wa Togo amemaliza kipindi chake cha kuwakilisha nchi yake Jumuiya ya Ulaya.
Balozi wa Tanzania Jumuiya ya Ulaya na Mwenyekiti wa Kamati ya Mabalozi wa Afrika, Karibiani na Pasifiki (ACP) Dr. Diodorus Buberwa Kamala (wa kwanza kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Malawi Jumuiya ya Ulaya Brave Ndisale (wa tatu kutoka kulia) aliyemaliza muda  wa kukilisha nchi yake Jumuiya ya Ulaya na Balozi na wanne kutoka kulia ni Balozi wa Togo Jumuiya ya Ulaya Balozi Kodjo Sagbo aliyemaliza muda wa kuwakilisha nchi yake Jumuiya ya Ulaya. Wa kwanza kutoka kushoto ni Katibu Mkuu wa ACP Alhaji Muhammad Mumuni na wa pili kutoka kulia ni Balozi wa Guyana Jumuiya ya Ulaya Balozi Patric Gomes.

NEWS ALERT: PATASHIKA MLIMANI CITY LEO BAADA YA DUKA LA SHOPRITE KUUZWA KWA NAKUMAT...

$
0
0
Makundi makubwa ya watu  yanaonekana yametapakaa katika eneo la shopping mall ya Shoprite ndani ya Mlimani City jijini Dar muda huu,baada ya Super Market mpya ya NAKUMAT iliyoinunua Shoprite kuamua kufanya SALE ya bidhaa mbalimbali zilizokuwepo kwenye Super Market hiyo,ili waweze uingia mzigo mpya. Pichani ni baadhi ya watu wakichangamkia SALE ya bidhaa hizo.
 Hili ni Nyomi linaloonekana kwa nje na ndani kuna idadi kuwa ya watu waliobahatika kuingia toka asubuhi,kwa ajili ya saula saula hiyo ya bidhaa.Milango ilifungwa kutokana na kutokea kwa vurugu kubwa la watu waliojitokeza kwa wingi kwenye Super Market hiyo.Mpaka sasa hakuna anaeruhuhusiwa kuingia.
 Wengine wameamua kukaa chini kusubiri kuona bahati iliwadondokea ya kuingia ndani ya Super Market hiyo kujipatia chochote kwa bei chee.
 Wengine wamejichokea kama hivi.


TASWIRA YA LEO KUTOKA BAGAMOYO.


AJALI ILIYOTOKEA ENEO LA MOROCO-POSTA LEO JIJINI DAR

$
0
0
Majeruhi akipewa huduma ya kwanza na mmoja wa akina mama aliyekuwa akifanya usafi kando kando ya barabara mapema leo asubuhi,katika ajali hiyo hakuna aliyepoteza maisha. 
Baadhi ya Watu wakitazama ajali ya magari mawili kama yaonekanavyo pichani,iliyotokea mapema leo asubuhi eneo la Moroco-Posta jijini Dar,katika ajali hiyo ambayo chanzo chake hakikufahamika mara moja,mtu mmoja alijeruhiwa na kukimbizwa hospitali kwa huduma ya kwanza,hakuna aliyepoteza maisha.
Mama ambaye jina lake halikufahamika mara moja moja aliyekuwa kwenye gari lenye usajili wa namba T679 CKC,akipewa huduma ya kwanza mara baada ya kupoteza fahamu
Moja ya gari ambalo pia lilipata ajali mara baada ya kuacha barabara na kuvamia mtaro kama lionekanavyo pichani.
Moja ya gari ambalo pia lilipata ajali mara baada ya kuacha barabara na kuvamia mtaro kama lionekanavyo pichani,huku abiria wake mmoja akiwa amepoteza fahamu,kama aonekavyo kwa mbali.

TFF YAINGILIA KATI KUOKOA MASHINDANO YA VIJANA UKANDA WA MAZIWA MAKUU.

$
0
0
Na Bertha Mollel – Arusha.
Shirikisho la kandada nchini Tanzania (TFF) limeingilia kati kuokoa mashindano ya vijana ukanda wa maziwa makuu ambayo yalikuwa hatihati kufanyika na sasa yataendeshwa kwa kushirikiana na waratibu wa mashindano hayo Rollingstone Sports academy ya mjini Arusha chini ya mwamvuli wa mtandao wa taasisi za za soka la vijana afrika mashariki na kati ECAYFA.

Mashindano hayo ya wazi hufanyika kila mwaka mkoani Arusha mwaka huu yatafanyika jijini dar es salaam na kushirikisha timu za vijana za under 20 na under 14 kutoka nchi za Burundi, Rwanda, Kenya, ,Zanzibar, na jamhuri ya kidemokrasia ya kongo (DRC) na yatafanyika wiki ya kwanza ya mwezi julay.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi mkurugenzi wa rollingstone football academy ally mtumwa masoud alisema mashindano hayo yalikuwa katika hatihati ya kufanyika au kutofanyika baada ya TFF kuchelewa kutoa kibali cha kuendesha mashindano hayo kwani taasisi hiyo iliandika barua ya kuomba kibali tangu mwezi wa pili lakini hawakupatiwa kibali kwa wakati.

Mtumwa alisema kuwa kufuatia kuchelewa kwa kibali hicho walishindwa kufanya maandalizi ya mashindano hayo ikiwa ni pamoja na kutafuta wafadhili na kualika timu hususani zile zinazotoka nje ya nchi  hali iliyosababisha kufikiria kuyasogeza mbele au kutofanyika kabisa kwa mashindano hayo.

Hata hivyo baada ya kufuatilia TFF walikiri kupokea barua hiyo na kusema sababu zilizochangia kutofanyiwa kazi kwa barua hiyo ni piikapilika za TFF kuhama ofisi kupisha ukarabati wa ofisi za karume lakini kwa kujua umuhimu na ukubwa wa mashindano hayo waliamua yafanyike kwa ushiriano wa pamoja na Rolly store kwa sharti la mashindano kufanyika jijini dare s salaam ili waweze kushuhudia.

Hii itakuwa mara ya pili kwa mashindano hayo ya 14 kufanyika nje ya Arusha kwani mwaka 2012 yalifanyika nchini Burundi na utakuwa mwanzo wa mashindano hayo kuzunguka katika mikoa na nchi mbalimbali ambazo zitakuwa tayari kuandaa na kukidhi vigezo ikiwa ni pamoja na kuhudumia malazi na chakula kwa timu zinazotoka nje ya nchi.

TFF, rollingstone na ECAYFA wameunda kamati ya maadalizi itakayokuwa chini ya uratibu wa afisa uhusiano na mawasiliano wa rollingstone Wilbrode Alfonce na tayari nchi wanachama wa CAYFA na taasisi za sika nchini Tanzania zimeshatumiwa barua za mialiko huku baadhi ya nchi kama burundi ,Kenya na DRC zikionyesha nia ya kushiriki.

PUKU YAJA NYUMBANI RASMI

$
0
0


Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya PUKU,Bwa.Meck Mbwana akizungumza kuhusiana na bidhaa hiyo,mbele ya Waandishi wa habari (hawapo pichani),mapema leo jijini Dar.
Pichani wa pili kulia ni Mwanamitindo Millen Magese ambaye ni balozi wa bidhaa ya PUKU akiwa na waanzilishi wa bidhaa hiyo ya PUKU mara baada kuzungumza na Wanahabari jijini Dar leo

===============

WATUMIAJI wa simu za kisasa za Smart Phone wametakiwa kutumia chaji za Puku kuchajia simu zao ili kujihakikishia usalama wake.

Akizungumza na waandishi wa habari katika uzinduzi wa chaji hizo, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya PUKU alisema kuwa chaji hizo kwa sasa zinapatikana hapa nchini.


Alisema kuwa ni chaji ambazo zinahifadhi umeme kwa muda mrefu ambao unakuja kutumiwa kuchajia simu hasa pale ambapo panakuwa hakuna umeme. Aliongeza kuwa bei yake kwa sasa ni kuanzia 160,000 kutokana na ubora wake na pamoja na namna ambavyo inasaidia.

"Mimi ni mtanzania kutoka Tanga na nilisoma hapa hapa ila nilielekea Marekani kusoma na ninaishi huko na nimebuni hii chaji kwa lengo la kusaidia watu mbalimbali ambao wanakuwa wakisumbuliwa na tatizo la kuchajia simu zao pale ambapo panakuwa hakuna umeme wa uhakika"alisema Meck Mbwana ambaye ni mvumbuzi na mkurugenzi mtendaji wa PUKU.


Aliongeza kuwa " kumekuwa na ongezeko kubwa la matumizi ya simu za smart phone huku watumiaji wakilalama kuwa wanakosa uhakika wa umeme wa kuzihudumia sasa hii bidhaa itasaidia".


Aliongeza kuwa kwa sasa zinapatikana hapa nchini na aliwataja wahusika wakubwa kuwa ni pamoja na Ed Kavishe-mshirika mwenza, Joseph sikare – Rais Tanzania huku Mwanamitindo Millen Magese akiwa ni mshirika mwenza na balozi wao.  Kwa upande wake Millen aliwataka wananchi kutumia bidhaa hiyo kwa kuwa mbali na kuwa ni ubora bali pia ni bidhaa ya watanzania wenyewe.

Tayari PUKU wameshajikita na uchangiaji wa huduma kwa jamii ambapo asilimia kadhaa ya mauzo itaelekezwa kwenye kampeni ya uelewa wa hali ya endometriosis na ujenzi wa hospital kwa ajili ya magonjwa yanayowasumbua akina mama. 

Mbali na udhamini wa kampeni ya endometriosis PUKU watachangia ujenzi wa madarasa mawili yaliyoko chini ya mradi wa Millen Magese Foundation yanayojengwa huko Mtwara ambapo mpaka sasa madarasa matatu yameshakamilika.

MKUTANO WA WADAU WA MFUKO WA TAIFA WA BIMA YA AFYA MKOANI TABORA

$
0
0
Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya NHIF nchini Balozi Ali Mchumo akizungumza na Wadau wa mfuko huo ambapo alisema NHIF imekusudia kuboresha mfuko huo ili kuondoa kero kwa wanachama  hususani upatikanaji wa dawa.
Mgeni rasmi katika Mkutano wa Wadau wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya mkoa wa Tabora Bw.Elibariki Kingu ambaye alimwakilisha mkuu wa mkoa wa Tabora,Mkutano uliofanyika katikaukumbi wa Isike Mwanakiyungi ambapo wadau walikuwa wakijadili Changamoto mbalimbali ikiwa na lengo la kuboresha mfuko huo kwa wanachama wake.
Kaimu mkurugenzi mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya NHIF Bw.Hamisi Mdee akielezea malengo ya mkutano huo wa wadau ambapo pamoja na mambo mengine alihimiza wadau kujitokeza kufungua maduka ya dawa muhimu vijijini ambayo yatasajiliwa  NHIF na yatakuwa yakitoa huduma kwa wanachama wa Mfuko wa Afya ya Jamii.
Katibu tawala mkoa wa Tabora Bi.Kudra Mwinyimvua akizungumza katika mkutano huo

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

Times Fm yachangia chama cha Albino wilaya ya Temeke shilingi milioni tatu

$
0
0
100.5 Times Fm Radio imetoa kiasi cha shilingi milioni tatu kwa albino wa wilaya ya Temeke, Dar es Salaam kama sehemu ya mchango wao kwa jamii hiyo yenye ulemavu wa ngozi inayokumbwa na changamoto nyingi.

Katibu wa Kampuni ya Times Fm Radio, Amani Joachim ameukabidhi uongozi wa chama hicho hundi halisi akiwa ameambatana na Aluta Warioba (Meneja Vipindi Msaidizi) na Mzee Chapuo kutoka katika idara ya ubunifu.

Amani Joachim aliwaomba wapokee kiasi hicho kwa kuwa bado Times Fm itaendelea kushirikiana nao katika kupambana na changamoto zinazowakabili na kuhamasisha jamii kuendelea kuonesha upendo kwa walemavu.

Baada ya kupokea hundi halisi ya kiasi hicho cha fedha, mwenyekiti wa chama cha Albino Temeke, Khasim Kibwe alitoa shukurani zake kwa chombo hicho cha radio na kueleza kuwa fedha hizo zitasaidia sana katika kununua mafuta maalum ya ngozi kwa wanachama wake.

“Kwanza nafurahi sana kwa kutujali sisi Albino. Lakini vilevile wito kwa jamii nao waige mfano huu wa 100.5 Times Fm nao waweze kuwachangia watu wenye albinism. Baada ya kuwa kiongozi, nakumbuka hata mlipotushirikisha katika mpira mwaka 2008 tuliona urafiki wenu wa karibu, vilevile sasa tunauona urafiki wenu umekamilika zaidi. Ni watu ambao mnajali watu wenye mahitaji maalum.

“Jamii iendelee kusikiliza Times Fm na wale wenye mahitaji wengine basi waipende Times kwa kuwa inapenda watu wa aina zote.” Amesema bwana Kibwe. Viongozi wengine wa chama hicho waliokuwepo ni pamoja na muweka hazina, Said Ndonge na katibu wa chama, Gaston Mcheka.
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live




Latest Images