Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110025 articles
Browse latest View live

TIPER YAIKABIDHI SERIKALI GAWIO LA SHILINGI 1,275,000.00

$
0
0
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt. Servarcius Likwelile (wa pili kushoto) akipokea hundi yyenye thamani y ash. Bilioni moja ktoka TIPER gawio la hisa katika hafla iliyofanyika leo mjini Dodoma. Wa kwanza kshoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa TIPER Daniel Belair, Wa pili kulia ni Mwenyekiti Mtendaji wa Bodi ya Wakurugenzi ya TIPER Prof. Abdulkarim Mruma na Wizara ya fedha Kaimu Msajili wa Hazina Elius Mwakabinga (wa kwanza kulia).
Mkurugenzi Mtendaji wa TIPER Daniel Belair (kushoto) akitoa taarifa ya kampuni ya TIPER invyoshikiana na Serikali katika kukuza uchumi na kuongeza soko la ajira nchini wakati wa kukabidhi gawio linalotolewa na kampuni yake kwa serikali leo mjini Dodoma. Kulia ni Mwenyekiti Mtendaji wa Bodi ya Wakurugenzi ya TIPER Prof. Abdulkarim Mruma.

Serikali imepokea shilingi bilioni moja kutoka TIPER ikiwa ni gawio ambalo kampuni hiyo imekuwa ikilipa kwa Wanahisa wake kila mwaka. Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt. Servarcius Likwelile alipokuwa akipokea gawio hilo katika hafla iliyofanyika leo mjini Dodoma.

Dkt. Likwelile alisema kuwa gawio hilo litaelekezwa kwenye bajeti ya mwaka huu wa fedha 2013/2014 unaomalizika kwa kuangalia maeneo ambayo yanawagusa wananchi ikiwemo sekta ya elimu, afya na maji. Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Daniel Belair alisema kuwa si mara ya kwanza kwa kampuni yake kutoa gawio kama hilo kwa Serikali ambapo mwaka jana muda kama huu kampuni ilitoa kiasi kama hicho kama gawio.

Mkurugenzi huyo alisema kuwa kampuni yake imeendelea kufanya vizuri katika kukuza maisha ya kijamii na kiuchumi ambapo kwa sasa inafanyakazi kwa saa 24 na siku saba za wiki. Kwa kuzingatia utendaji huo, kampuni ya TIPER imekuwa kichocheo kukuu cha kuzalisha ajira nchini ambapo hadi sasa asilimia 99 ya wafanyakazi wake ni nguvu kazi ya Watanzania.

Naye Mwenyekiti Mtendaji wa Bodi ya Wakurugenzi ya TIPER Prof. Abdulkarim Mruma alisema kuwa imekuwa ni muhimu kwa kampuni yao kuwa na akiba ya kutosha ya mafuta kwa nchi na kuleta mafanikio makubwa ya upatikanaji wa mafuta nchini.

Aidha, TIPER Prof. Mruma alisema kuwa kwa sasa kampuni yao imejikita katika kuleta mafuta yaliyosafishwa nchini ili kupunguza gharama zisizokuwa za lazima.

“Kwa sasa tunaleta mafuta yaliyosafishwa badala ya mafuta ghafi ambayo yanazalisha tope jingi ambalo limekuwa ni hatari katika kutunza mazingira yetu” alisema Prof. Mruma Pamoja na ufanisi huo, kumekuwepo na changamoto za kuboresha mkataba wa utendaji na usimamizi wa hesabu masuala ambayo wanahisa wote wawili wanaendelea kuyafanyia kazi kwa madhumuni ya kuwa na matokeo mazuri zaidi kwa pande zote.

Kiutendaji kampuni ya TIPER inaendeshwa kwa ubia kati ya Serikali ya Tanzania ambayo inahisa zenye asilimia 50 na Kampuni ya Oryx Energies SA asilimia 50.

Pamoja na Tanzania Kampuni ya Oryx Energies SA inafanyakazi katika mnchi mbalimbali duniani ambazo ni Benin, Burkina Faso, Côte d'Ivoire, Guinea Conakry, Kenya, Mali, Niger, Nigeria, Senegal, Sierra Leone, Afrika Kusini, Uhispania (Visiwa vya Canary), Togo, Uganda na Zambia.

mchemsho mwingine wa refa washuhudiwa wakati Mexico ikiibanjua Cameroon bao 1-0 leo

$
0
0
Mshambuliaji Oribe Peralta wa Mexico amehakikisha kwamba haki inatendeka katika michezo ya awali ya Kombe la dunia alipoiwezesha nchi yake kuifunga Cameroon bao 1-0 jioni huu mjini Natal wakati michuaono hiyo ikiwa katika hatihati ya kashfa ingine ya uamuzi mbovu. 
Endapo kama Mexico wasingeshinda ni hakika Refa huyo kutoka Colombia Wilmar Roldan angekuwa katika wakati mgumu baada ya kukataa magoli mawili ya wazi ya timu hiyo kwa madai kuwa ni ya kuotea baada ya mchezaji wa zamani wa Tottenham Giovani dos Santos kutingisha nyavu za Cameroon mara mbili katika kipimdi cha kwanza. 
Ndio kusema refa huyo na FIFA walipata ahueni ya aina yake baada ya Mexico iliyotaewala mchezo ilipozawadiwa goli safi la siku, baada ya kipa wa Acmeroon kupangua mkwaju wa Dos Santos na kumwekea Peralta aliyetumbukiza ngoma kimiani 
 Matokeo hayo yanaifanya Mexico kuwa katika nafasi nzuri ya kusonga mbele pamoja na Brazil katjka kundi lao la A . Wababe hawa wawili (Mexico na Brazil) wanakutana siku ya Jumanne katika mji wa Fortaleza.
Kocha wa Mexico  Miguel Herrera akimpa maneno yake Refa kutoka Colombia Wilmar Roldan wakati wa mapumziko kwa kuwabania mabao mawili kipindi cha kwanza

Oribe Peralta akimchenga Samuel E'too kuifungia Mexico bao katika dakika ya  61 ya mchezo



Oribe Peralta akishangilia bao la Mexico dhidi ya Cameroon

MASHINDANO YA KOMBE LA DUNIA: CAMEROON YAANZA KWA KICHAPO CHA BAO 1 - 0 KUTOKA KWA MEXICO

welcome to Simu TV: Tanzania's first Video on Demand mobile portal

$
0
0
Kindly follow Push Mobile media simu.tv twitter page :  https://twitter.com/SIMUTVTanzania and mention Push Mobile media using the handle @SimuTVTanzania to get the latest news delivered directly to your mobile phone with Tanzania's first Video on Demand mobile portal via VODACOM Tanzania. Call *149*01//

WENGI WAJITOKEZA KWENYE SEMINA MAALUM YA UONGOZI BORA ILIYOANDALIWA NA MIKONO SPEAKERS

$
0
0
Nguli wa Maswala ya Uongozi na Mwenyekiti Mtendaji wa kampuni ya Kimataifa ya Brian Tracy kutoka nchini Marekani,Brian Tracy akikiongoza semina maalum ya uongozi bora iliyoandaliwa na Mikono Speakers,iliyofanyika leo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere,Jijini Dar es Salaam.Nguli mwingine alietoa mada kwenye Semina hiyo ni Azim Jamal ambaye ni Mwanzilishi na Mkurugenzi wa Corporate Sufi Worldwide Inc. kampuni inayojihusisha na kusaidia wadau na makampuni kupata muhimili stahiki katika kazi zao.
Sehemu ya Wadau kutoka nyanja mbali mbali wakiwa wamejitokeza kwa wingi kwenye Semina hiyo iliyoongozwa na Manguli wa Maswala ya Uongozi Duniani, Brian Tracy na Azim Jamal,iliyofanyika leo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere,Jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya Wadau wakifatilia kwa makini Mada mbali mbali kwenye semina hiyo.

WAOMBAJI WA NAFASI YA MKAGUZI MSAIDIZI UHAMIAJI WAFANYA USAILI WA AWALI UWANJA WA TAIFA JIJINI DAR LEO

$
0
0
Sehemu ya waombaji zaidi ya 10,000 wa nafasi ya Mkaguzi Msaidizi, Idara ya Uhamiaji wakifanya usaili wa awali wa kuandika ulioandaliwa na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa ajili ya kujaza nafasi 70 za kazi ambazo zinahitajika katika Idara hiyo. Usaili huo uliongozwa na Maafisa Utumishi wa wizara hiyo, umefanyika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam leo ambapo baada ya wiki moja waliofaulu vizuri wataitwa kwa ajili ya usaili wa mwisho.
Afisa Utumishi Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Penina Isamuyo akigawa makaratasi ya mitihani kwa waombaji wa nafasi ya Mkaguzi Msaidizi, Idara ya Uhamiaji kwa ajili ya kufanya usaili wa awali wa kuandika. Zaidi ya waombaji 10,000 walifanya usaili huo Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam leo ambapo baada ya wiki moja watakaofaulu vizuri wataitwa kwa ajili ya usaili wa mwisho.
Afisa Utumishi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwanamridu Jumaa (aliyevaa kiraia) na askari Magereza wakiwa wamebeba maboksi yenye makaratasi ya mitihani ya usaili iliyofanywa na zaidi ya waombaji 10,000 Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam leo. Baada ya wiki moja waombaji waliofaulu vizuri wataitwa kwa ajili ya usaili wa mwisho.
Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Lilian Mapfa akisimamia usahihishaji wa mitihani ya usaili ya waombaji wa nafasi ya Mkaguzi Msaidizi wa Idara ya Uhamiaji inayosahihishwa na Maafisa Utumishi wa wizara na askari Magereza. Zaidi ya waombaji 10,000 wamefanya usaili wa awali Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo kwa ajili ya kugombea nafasi 70 zilizotangazwa na Katibu Mkuu wa wizara hiyo.
Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Lilian Mapfa akisimamia usahihishaji wa mitihani ya usaili ya waombaji wa nafasi ya Mkaguzi Msaidizi wa Idara ya Uhamiaji inayosahihishwa na Maafisa Utumishi wa wizara na askari Magereza. Zaidi ya waombaji 10,000 wamefanya usaili wa awali Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo kwa ajili ya kugombea nafasi 70 zilizotangazwa na Katibu Mkuu wa wizara hiyo.
Maafisa wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Lubert Fransis (kulia) na Mwanamridu Jumaa wakipanga maboksi kwa ajili ya kuhifadhia makaratasi ya mitihani ya usaili. Zaidi ya waombaji 10,000 walifanya usaili wa awali Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam leo ambapo baada ya wiki moja waliofaulu vizuri wataitwa kwa ajili ya usaili wa mwisho. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Mining Companies Are Not Tax Cheats

$
0
0
TANZANIAONE3
Chairman, Tanzania Chamber of Minerals and Energy, Ami Mpungwe (Photo by Library).

WASANII WA TANZANIA WAPATA PA KUUZIA KAZI ZAO MTANDAONI

$
0
0
Baada ya kuhaha kwa muda mrefu kutafuta jinsi ya kuuza kazi zao, mkombozi wa swala la kuibiwa jasho lao amekuja kwa njia ya MKITO, mtandao ambao unauza kazi za wasanii mtandaoni kirahisi kabisa. 
KWA WASANII Tafadhali wasiliana na Mkito kwa simu namba +255 767 769 921 au kwa barua pepe support@mkito.com kwa mawasiliano zaidi.
Angalia banner hapo juu ya BLOG kama hiyo pichani na BOFYA uende kwenye mtandao huo moja kwa moja. La, kama vipi acha tukusaidie - BOFYA HAPA 

Tanzia: Bondia wa zamani iraq hudu afariki dunia leo, kuzikwa kesho kisutu Dar es salaam

$
0
0
BONDIA wa zamani wa ngumi za kulipwa nchini, Iraq Hudu 'Kimbuga' (49) amefariki dunia, baada ya kuugua kwa muda mfupi. 
 Akizungumza jijini Dar es Salaam leo,  Dada wa Marehemu Tiba Takadiri, alisema kuwa Hudu amefariki jana majira ya saa 11 ya alfajiri kwenye hospitali ya Hindu Mandal, alikokuwa amelazwa. Takadiri, alimesema kuwa mazishi ya Hudu yatafanyika leo kwenye makaburi ya Kisutu, Dar es Salaam.
 Alisema kuwa marehemu alikuwa akisumbuliwa na tatizo la ini na figo kutofanya kazi, ambapo vilimsumbua kwa muda mchache kabla ya kufariki kwake. 
 "Marehemu alilazwa hospitali Hindu Mandal siku tatu zilizopita, ambapo majuzi jioni alizidiwa na jana asubuhi kukutwa na umauti", alisema Dada Tiba.
Hudu amezaliwa mwaka 1965 Ujiji Kigoma, na kupata elimu ya msingi mkoani humo na baadae kuja Dar es Salaam ambapo alimaliza shule ya Sekondari na baadae kuanza shughuli za ngumi katika miaka ya 1990 mpaka miaka ya 2000 alipoacha. 
 Marehemu ameacha watoto watatu, ambao ni Daniel alikuwa akitarajia kufunga ndoa Juni 20, wakati mtoto mwingine Msawila ambaye ni mwanafunzi wa darasa la sita. 
 Maandalizi ya msiba yanaendelea nyumbani kwa marehemu Buguruni Lozana Dar es Salaam ambapo kesho saa 7, atazikwa Kisutu. 
 Marehemu Hudu aliwahi kutamba akiwa na mabondia kina Joseph Marwa, Stanley Mabesi, na baadae wakaja mambondi wengine Rashid Matumla na Maneno Osward 'Mtambo wa Gongo'. Mwenyezi mungu aiweke roho ya marehumu amina
Marehemu Iraq Hudu (kulia) enzi za uhai wake akiwa na mwanae Daniel Hudu siku kijana wake huyu alipokula nondozzz yake katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) Novemba mwaka jana.
Daniel na familia yake walikuwa katika maandalizi ya harusi aliyopanga kuifanya Juni 20, mwaka huu. Globu ya Jamii inatoa pole kwa wafiwa kwa msiba huu mzito. 
Iraq Hudu alikuwa mmoja wa wadau wetu wa karibu sana na Michuzi Blog ambapo yeye marehemu na nduguye Sensei Rumadha Fundi aliyeko Marekani alikuwa mshauri mkubwa wa kazi zetu. 
Mola Ipunzishe kwa amani
 roho ya marehemu peponi - Amin

Mabingwa watetezi wa kombe la Dunia Spain Mbendembende mbele ya Holland, yachapwa 5-1

$
0
0

Na Sultani Kipingo 
wa Globu ya Jamii
Siku ya tatu tu tokea michuano ya kombe la Dunia ianze nchini Brazil, tayari mabingwa watetezi Spain wanakuta kombe hilo linateleza mikononi mwao. 
Japokuwa miaka minne iliyopita walipoteza mchezo wao kwa kwanza dhidi ya Switzerland huko Afrika ya Kusini, lakini hiyo haiwezi kulinganishwa na kilichotokea uwanja wa Fonte Nova katika mji wa Salvador ulio Kaskazini-Mashariki ya Brazil usiku wa kuamkia leo baada ya kuchwapwa bao 5-1 na Holland.

Hilo ni pigo kubwa kwa Spain kupata tokea mwaka 1963 walipochabangwa na Scotland, ila safari hii aibu yake ni maradufu kwa vijana hao wa kocha Vicente del Bosque. Ni sawa na matokeo ya ndondi pale Tyson alipopigwa na kuvuliwa ubingwa Las Vegas. Wadadisi wanasema ni timu chache zinaweza kuzinduka baada ya kipigo kama hicho. Sasa wanasubiri kuona Spain itakuwaje.

Kimchezo Holland ngoma iliwakubali. Walikuwa wakihaha kila pembe ya uwanja kusaka magoli, huku nyota wao tishio  Robin van Persie na  Arjen Robben wakiwatoa raha Spain  kila sekunde. Matokeo yakaja kama ilivyokuwa mwaka 1990 wakati Cameroon walipoichapa Argentina, ama Ufaransa kufungwa na Senegal mjini Seoul miaka 12 baadaye.


Ukifikiria sana unajikuta unakubali kwamba kipigo cha 5-1 ni janga kwa Spain, hasa ukizingatia ilianza kuongoza kwa bao 1-0 na kuwa mbele kabla ya mapumziko. Saa moja baadaye Spain wakajikuta wanasujudu kwa mabao hayo ambayo kama si kipa wao Iker Casillas kuokoa mikwaju mingine kibao ingekuwa 7-1 ama hata 8-1. Kitu pekee kilichowaokoa isiwe hivyo ni kipyenga cha mwisho…

Ngoma ilianza kuwa tamu pale Spain ilipojipatia bao la kwanza kwa njia ya penati iliyopigwa na Xabi Alonso. Dakika moja kabla ya ya mapumziko, ndipo Robben Van Persie  akaanzisha kalamu ya magoli pale aliposawazisha kwa goli tamu la kichwa cha kuchupa (pichani) akiwa mita 30, kabla ya kuongeza lingine kwa kumpita Gerard Pique.  Stefan de Vrij akaweka kimiani bao la 3, kabla Van Parsie hajautumia kwa manufaa yake uzembe wa kipa Iker Casillas na kufunga la nne na la tano. 

Katika mchezo mwingine Chile imeifunga Australia bao 3-1 katika uwanja wa Pantanal Cuiba. 
Leo timu ingine ya Afrika, Ivory Coast, inatupa karata yake ya kwanza kwa kucheza na Japan katika uwanja wa Pernambuco mjini Recife, wakati Enland inakipiga na Italy katika mchezo mwingine wa kukata na shoka katika uwanja wa Amazonia mjini Manaus.
Leo pia Columbia watacheza na Greece, wakati Uruguay itapambana na Costa Rica. Kuona muda wa kuanza michezo hiyo angalia ratiba hapo juu.


TONIGHT 14 June>>>SANSKRITIK SANGAM

Chuo cha Bahari-DMI cha saini makubaliano ya mafunzo ya ubaharia na UNRA(U)

$
0
0
Chuo cha Bahari (DMI) kimetia saini makubaliano ya mafunzo ya ubaharia na Mamlaka ya Barabara ya nchini Uganda (Uganda National Road Authority) Makubaliano hayo yalitiwa saini alhamisi 12.06.2014 jijini Kampala katika ofisi za UNRA zilizopo Lourdel rd plot 5 Nakasero.

Kaimu Mkuu wa Chuo cha Bahari,Ing. Yassin M. Songoro , Mkuu wa Idara ya fedha,Bw. Mussa Kondo na Mkuu wa kozi fupi,Bw. Hilal Salum waliiwakilisha DMI na kwa upande wa UNRA Mkurugenzi Mtendaji,Bw. Ssebbugga Kimeze,Ing. Helbert Mutyaba waliwakilisha.

DMI ni chuo pekee cha Ubaharia katika ukanda huu wa Afrika Mashariki na kati kimepata fursa hiyo baada ya kushinda tenda iliyotangazwa na UNRA kupitia kitengo cha manunuzi (procurement),pia dmi imepewa fursa ya kufungua kituo cha mafunzo ya ubaharia Uganda ili kusaidia kutoa mafunzo hayo.

ombi hilo limeletwa hasa baada ya Uganda kuanza utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi.

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LEO TAREHE 14.06.2014.

$
0
0
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WAWILI KWA TUHUMA TOFAUTI.


KATIKA MSAKO WA KWANZA:


MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA EDGAR PATRICK (24) MKAZI WA MAPOROMOKO ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA AKIWA NA BHANGI KILO 12 AMBAYO ALIIFICHA KATIKA NDOO YA PLASTIC.


MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 13.06.2014 MAJIRA YA SAA 13:36 MCHANA KATIKA MTAA WA MAPOROMOKO, KATA NA TARAFA YA TUNDUMA, WILAYA YA MOMBA, MKOA WA MBEYA.


MSAKO WA PILI:


MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA JACKSON EMANUEL (22) MKAZI WA ILEMI JIJINI MBEYA ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA AKIWA NA NOTI BANDIA 17 ZA TSHS 10,000/= SAWA NA TSHS 170,000/= NOTI 12 ZA TSHS 5,000/= SAWA NA TSHS 60,000/=.


MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 13.06.2014 MAJIRA YA SAA 22:00 USIKU KATIKA MTAA WA MAGEGE-ILEMI, KATA YA ILEMI, TARAFA YA SISIMBA JIJI NA MKOA WA MBEYA. NOTI HIZO ZILIKUWA NA NAMBA DW 5621984 – NOTI 17 NA NOTI 12 ZA TSHS 5,000/= ZIKIWA NA NAMBA BB 119382.


TARATIBU ZA KUWAFIKISHA MAHAKAMANI WATUHUMIWA ZINAENDELEA KUFANYIKA. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA MATUMIZI YA BHANGI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA ZAO. AIDHA ANATOA WITO KWA WANANCHI KUWA MAKINI MATAPELI HASA KATIKA MAENEO YA BIASHARA PIA KUTOA TAARIFA MAPEMA ZA WATU WANAOJIHUSISHA NA BIASHARA YA UTENGENEZAJI NA USAMBAZAJI WA NOTI BANDIA.

Imetolewa na:

[AHMED Z. MSANGI – SACP]

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.





Zoezi la Uandikishaji wa Kaya Maskini Mpanda Mjini

$
0
0
 Shughuli za uandikishaji wa kaya maskini linaloendeshwa na TASAF chini ya Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini katika awamu ya tatu ya TASAF. TASAF ni mfuko ulio chini ya Ofisi ya Rais ambao umepewa jukumu la kupambana na umaskini. Hapa ni katika mtaa wa Tambukareli, kata ya Mpanda Hoteli. Zoezi hili linafanyika piakatika Halmashauri ya wilaya ya Mpanda na Halmashauri ya wilayaya Mlele.
 Shughuli za uandikishaji wa kaya maskini linaloendeshwa na TASAF zikiendelea  wakati wa Zoezi la Uandikishaji wa Kaya Maskini Mpanda Mji
Wananchi wakisubiri Zoezi la Uandikishaji wa Kaya Maskini Mpanda Mjini

President Obama Makes a Statement on Iraq


Mbunge Filikunjombe avunja rekodi ya kutembelewa na wageni wengi bungeni kutoka jimboni kwake Ludewa

$
0
0
Mbunge wa Namtumbo Mhe Vita Kawawa akisalimiana na  wajumbe 92  kutoka  jimbo la Ludewa  ambao ni  wenyeviti kata na makatibu kata kutoka kata  zote 25  za  jimbo la  Ludewa 
Sehemu ya  wajumbe 92  kutoka  jimbo la Ludewa  ambao ni  wenyeviti kata na makatibu kata kutoka kata  zote 25  za  jimbo la  Ludewa 
Waziri mkuu Mizengo Pinda akisalimiana na  wajumbe 92  kutoka  jimbo la Ludewa  ambao ni  wenyeviti kata na makatibu kata kutoka kata  zote 25  za  jimbo la  Ludewa 
Waziri mkuu Pinda akisalimiana  na wageni  kutoka jimbo la  Ludewa kwa mbunge Mhe. Deo Filikunjombe  waliotembelea  bungeni. kulia ni mbunge Filikunjombe
Kwa picha zaidi BOFYA HAPA 

WADAU KUTOA MAONI YA MISWADA YA SHERIA YA: VALUE ADDED TAX ACT, 2014, TAX ADMINISTRATION ACT, 2014 NA FINANCE ACT, 2014

2014 East Africa Budget Highlights by Deloitte

$
0
0

We are pleased to share with you our East Africa Budget Highlights covering Kenya, Rwanda, Tanzania and Uganda.


Please click here to download the 2014 Budget Highlights. More information and analysis of 2014 Country Budgets will be published on our website

We would also like to take this opportunity to remind you of our event ("East Africa Budget 2014: The Balancing Act")  to be held on Tuesday, 17June 2014 at the Hyatt Regency – The KilimanjaroKibo Conference Room from 4:00pm to 6:30pm, followed by a cocktail thereafter. 




We look forward to fruitful deliberations as we explore the shifting business landscape, new regulations and compliance requirements as well as the implications of the new tax measures.

NHIF WAENDELEA KUSAIDIA HUDUMA KWENYE WODI YA AKINA MAMA NA WATOTO KITUO CHA AFYA MLANDIZI

$
0
0
 Mwenyekiti wa kamati ya kituo cha afya Mlandizi, bw Makamba Mwaluka (watatu kushoto), akiwakaribisha wageni kutoka Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya baada ya kufanya ziara katika wodi ya akina mama na watoto Kituo cha Afya Wilayani Mlandizi. Juni 12,2014 na kukabidhi mashuka kwenye kituo hicho (kulia kwake), Muendeshaji shughuli mama Gaudensia Ndegea (katikati kulia), Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Kibaha, Michael John, na Mjumbe wa bodi NHIF, bwana Charlse Kajege.  
 Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti wa NHIF, Raphael Mwamoto (kulia), akiwakaribisha wageni aliyoambatana nao kutoka katika mfuko huo(wakwanza kulia), Mjumbe wa bodi NHIF, Charlse Kajege, Mjumbe wa bodi wa NHIF Dr. Hashim Mohamed, Diwani wa Mlandizi  mama Ndessi, Mkurugenzi wa Matibabu na Huduma za kiufundi  Dr. Frank Lekey
 Mjumbe wa bodi wa NHIF Dr. Hashim Mohamed(kushoto), akikabidhi mashuka kwa mgeni rasmi, diwani wa Mlandizi  mama Ndessi baada ya kufanya ziara katika katika wodi ya akina mama na watoto Kituo cha Afya Wilayani Mlandizi na kukabidhi mashuka kwenye kituo hicho.
 Mjumbe wa bodi aliyemuwakilisha Mwenyekiti wa bodi ya NHIF Dr. Hashim Mohamed (katikati), akisisitiza jambo mara baada ya kumaliza ziara hiyo wilayani Mlandizi.
 Wajumbe wa bodi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya ndugu Charlse Kajege na Dr. Mohamed Hashim wakiwa na diwani wa Mlandizi Mama Dessi       wakitandika moja ya mashuka yaliyotolewa na NHIF.katika wodi ya akina mama na watoto Kituo cha Afya Wilayani Mlandizi.
Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti,Raphael Mwamoto(kushoto), akimtambulisha Mkurugenzi wa huduma za utabibu na ufundi  Dr. Frank Lekey ambaye waliambatana katika ziara hiyo wilayani mlandizi.

Wafanyakazi wa Citi Bank tawi la Tanzania watoa msaada kwenye Kitengo cha Watoto wenye Ulemavu wa akili,Tandika jijini Dar

$
0
0
Wafanyakazi wa Citi Bank tawi la Tanzania wameweza kujichangisha wenyewe kwa wenyewe na kupata fedha zilizofanikisha ukarabati wa jengo litakalotumika kama jiko la kupitia na ukumbi wa kulia chakula kwenye Kitengo cha Watoto wenye Ulemavu wa akili cha Shule ya Msingi Tandika,Wilayani Temeke jijini Dar es Salaam,Wafanyakazi hao wameamua kufanya hivyo leo ikiwa ni muendelezo wa mpango wao wa kusadia watu wenye Mahitaji,wanaofaunya mara moja kwa mwaka Duniani kote,mbali na ukarabati huo waliweza pia kujitolea kufanya usafi wa Mazingira ya eneo la Shule hiyo.
 Baadhi ya Wafanyakazi wa Citi Bank tawi la Tanzania wakiwa wamejumuika pamoja na Wanafunzi wa Shule ya Msingi Tandika ambao wanaulemavu wa Akili.
Wanafunzi hao wakifurahia ugeni huo uliowatembelea leo.
Meneja Mkuu wa Citi Bank tawi la Tanzania,Noel Sangiwa (kulia) na Mkuu wa Kitengo cha Watoto wenye Ulemavu wa Akili Tandika,Mary Batamula (katikati) wakishirikiana kukata Utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa jengo litakalotumika kama jiko la kupitia na ukumbi wa kulia chakula kwenye Kitengo cha Watoto wenye Ulemavu wa akili cha Shule ya Msingi Tandika,Wilayani Temeke jijini Dar es Salaam leo.
Sehemu ya Wafanyakazi wa Citi Bank tawi la Tanzania wakifanya usafi wa Mazingira katika eneo la Shule ya Msingi Tandika ambako kuna Kitengo cha Watoto wenye Ulemavu wa Akili.

Viewing all 110025 articles
Browse latest View live




Latest Images