Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 468 | 469 | (Page 470) | 471 | 472 | .... | 3283 | newer

  0 0

  Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii -TASAF- Ladislaus Mwamanga amewataka watumishi wa Mfuko huo kuongeza kasi ya uwajibikaji katika kufanya kazi ili mpango wa kunusuru kaya maskini na zilizo katika mazingira hatarishi kuwafikia walengwa kama ilivyokusudiwa na serikali.

  Mwamanga ametoa kauli hiyo mkoani Mtwara wakati akifungua warsha elekezi ya siku mbili kwa maafisa ushauri, ufuatiliaji, wahasibu  na waratibu wa mikoa na wilaya ikiwa na lengo la kutathimini utekelezaji wa mradi wa TASAF awamu ya tatu katika halmashauri 22 ambazo zimeanza utekelezaji wa mpango huo.

  Halikadhalika Mwamanga amewataka kushirikiana, kuwa makini  na kutokiuka taratibu na matumizi ya fedha za mpango huo na kufuata miongozo sahihi ya kazi kwa sababu serikali imeona njia pekee ya kuwakomboa watu waliosahaulika ni kuwaingiza katika mpango.
   Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Bw. Ladislaus Mwamanga (katikati waliokaa) na wakurugenzi wengine wa TASAF Wakiwa kwenye picha ya pamoja na Waratibu wa mikoa wa mamlaka ya eneo la utekelezaji wa halamashauri 22 baada ya ufunguzi wa warsha ya siku mbili mjini Mtwara
   Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Bw. Ladislaus Mwamanga akifungua Warsha elekezi  ya siku mbili kwa maafisa ushauri na ufuatiliaji, waratibu wa mikoa, waratibu na wahasibu wa mamlaka ya eneo la utekelezaji wa halamashauri 22 nchini inayofanyika katika ukumbi wa chuo kikuu cha SAUT Mjini Mtwara
   Mkurugenzi wa mpango wa TASAF Bw. Amadeus Kamagenge akitoa maelezo juu ya mpango wa kuzinusuru kaya masikini na zilizo katika mazingira hatarishi katika warsha hiyo
   Washiriki wa warsha hiyo wakiwa wamenyoosha mikono juu kama ishara ya kukubaliana na jambo wakati Mkurugenzi mkuu wa TASAF Bw. Ladislaus Mwamanga (hayupo pichani) alipokuwa akifungua warsha hiyo
   Sehemu ya washiriki wa warsha hiyo wakisikiliza kwa makini uwasilishi wa moja kati ya mada ilyokuwa ikiwasilishwa. 
   Baadhi ya washiriki wa warsha hiyo wakisikiliza kwa makini uwasilishi wa moja kati ya mada iliyokuwa ikiwasilishwa
  Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Bw. Ladislaus Mwamanga, na wakurugenzi wengine toka TASAF Makao Makuu wakiwa kwenye picha ya pamoja  na waratibuwa  mamlaka ya eneo la utekelezaji wa Halamashauri 22 nchini (waliyosimama) Mjini Mtwara

  0 0

  Balozi wa Tanzania Ubelgiji Dr. Diodorus Buberwa Kamala (kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Usalama wa Chakula ya Ubelgiji Bwana. Pierre Nassens ( wa pili kutoka kushoto). Balozi Kamala ametembelea taasisi hiyo leo Brussels kushauriana nayo  jinsi inavyoweza kushirikiana na Tanzania. Wengine katika picha ni wataalamu katika taasisi hiyo.

  0 0

  The highly anticipated High Performance Leadership seminar is almost here! Tune in to Choice In The Morning on Choice FM and Jahazi on Clouds FM tomorrow to hear Brian Tracy speak LIVE on air speaking about his seminar.
  Witness the powerful transformation message by Brian Tracy and Azim Jamal live in Dar Es Salaam
  High Performance Leadership seminar | 13th June 2014| Julius Nyerere International Convention Centre

  0 0


  Kamishna wa Polisi Issaya Mngulu, Mkurugenzi wa upelelezi wa makosa ya jinai nchini (DCI), akiongea na wanahabari mkoani Tabora Leo
   Na Allan Ntana wa Globu 
  ya Jamii, Tabora 

  MKUU wa Jeshi la Polisi hapa nchini IGP Ernest Mangu ameteua timu ya askari polisi wataochunguza tuhuma za wizi wa fedha za wakulima wa zao la tumbaku katika vyama vya ushirika vya wakulima hao mkoani Tabora. 

   IGP Mangu amemteua Kamishna wa Polisi Issaya Mngulu (pichani) ambaye ni Mkurugenzi wa upelelezi wa makosa ya jinai hapa nchini kuongoza timu. 
   Timu hiyo ya upelelezi kutoka makao makuu ya Jeshi la Polisi jijini Dar es salaam tayari imewasili mkoani hapa kuanza kazi ya kuchunguza ubadhirifu huo unaofanyika katika vyama vya msingi vya wakulima wa tumbaku. 
   Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari mara baada ya kuwasili mkoani hapa Kamishna Mngulu alisema timu imeundwa kutokana na agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania la tarehe 7/6/2014 alipokuwa ziarani mkoani hapa baada ya kuguswa na kilio cha wizi mkubwa wa fedha za wakulima wa tumbaku. 
   Kamishan Mngulu alisema timu hiyo ni maalumu na imekuja mahsusi kwa ajili ya kuchunguza wizi wanaofanyiwa wakulima wa tumbaku kupitia vyama vya msingi mkoani hapa Alifafanua kuwa timu hiyo inaanza kazi mara moja kwa kuchunguza chama kimoja hadi kingine ili kubaini wizi na hujuma zote zilizofanyika na zinazoendelea kufanyika ambazo zimekuwa kero kwa wakulima wa zao hilo katika mkoa wa Tabora. 
   ‘Natoa rai kwa wananchi wa mkoa wa Tabora kutoa ushirikiano kwa timu hii mara watakapohitahika ili kuwezesha mafanikio ya kazi hii kwa wakati mwafaka, kazi hii ni ngumu lakini tutaifanikisha kwa ushirikiano wa wananchi na wadu wengine, aliongeza.

  0 0


  SWC Fixtures Poster on SUPESPORT

  0 0

  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akijibu Maswali ya Papo kwa papo bungeni mjini Dodoma leo Juni 12, 2014.
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimana na viongozi wa vijiji na kata kutoka jimbo la Ludewa kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Juni 12, 2014.
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Sarah Kasui, mwanafunzi wa Kidato cha kwanza katika shule ya sekondari ya Sejeli mkoani Dodoma kwenye viwanja vya bunge mjini Dodoma Juni 12, 2014.
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na wabunge Nyambali Nyangwine wa Tarime (katikati) na na Saidi Mtanda wa Mchinga kwenye viwanja vya bunge mjini Dodoma Juni 12, 2014.
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Profesa Mark Mwandosya kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Juni 12, 2014.
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Mbunge wa Viti Maalum,Lucy Mayenga (kushoto) na Mbunge wa Mchinga Saidi Mtanda kwenye jengo la Utawala la Bunge mjini Dodoma Juni 12, 2014.
  Waziri Mkuu, Mstaafu, Edward Lowassa akiwa katika picha ya pamoja na madiwani kutoka jimbo la Busanda, kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Juni 12, 2014. Wapili kulia ni Mbunge wa jimbo hilo, Lolesia Bukwimba.
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwa katika picha ya pamoja na madiwani kutoka jimbo la Busanda, kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Juni 12, 2014. Wapili kulia ni Mbunge wa jimbo hilo, Lolesia Bukwimba.
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na madiwani wa jimbo la Busanda kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma Juni 12, 2014. Kulia ni mbunge wao Lolesia Bukwimba. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0

  Association of Citizen Contractors (ACCT) organized a two-day seminar on the new Procurement Act of 2011, at Kunduchi Beach Hotel from 11th to 12th June 2014 has been conducted by Dr. Ramadhani Mlinga who is the former CEO of PPRA and a seasoned specialist in the Procurement area. 

  This program is very important to the construction industry as it will highlight key changes introduced in the Public Procurement Act of 2011 and its 2013 regulations and explained the impact of these changes to the stakeholders in the Construction Industry. 

  This law is used in the procurement of all public works which constitute over 80% of all construction projects in the Country. It therefore determine how most of the contractors can secure their works. The new act and its regulations became operational on 15th of December 2013.

  For more information visit www.acct.co.tz

  0 0

  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mahusiano na Uratibu, Mheshimiwa Stephen Masato Wasira (Mb) Akiwasilisha Bungeni Taarifa ya Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2013 na Mpango na Maendeleo wa Taifa 2014/15.
  Wageni wa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mahusiano na Uratibu, Mheshimiwa Stephen Masato Wasira (Mb) ambao ni baadhi ya viongozi waandamizi wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango wakifuatilia kwa umakini uwasilishaji wa Taarifa ya Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2013 na Mpango na Maendeleo wa Taifa 2014/15.
  Katibu Mtendaji wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Dkt. Philip Mpango (Kushoto) pamoja na Naibu wake, Bw. Maduka Kessy wakifuatilia kwa umakini uwasilishaji wa Taarifa ya Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2013 na Mpango na Maendeleo wa Taifa 2014/15.     

  0 0

  Na Geofrey Tengeneza - Selous

  Kundi la wandshi wa habari tisa kutoka vyombo vya habari vya Serikali na binafsi nchini Afrika Kusini wametembelea Pori la Akiba la Selous na kufurahishwa na vivutio vllivyomo katika pori hilo wakiwemo wanyama kama Simba, tembo, twiga, na ndege wa aina mbali mbali.

  Wandishi hao walivutiwa na kufurahia sana kuwaona hasa Simba na tembo kiasi cha miongoni mwao Kulikiri kuwa ni mara yao kwanza kuwaona wanyama hao kwa macho yao wakiwa katika maisha yao ya asili msituni kudaikuwa kwa muda mrefu wamekuwa wakiwaona katika televisheni na filamu tu.“Nimefurahi sana na mwki umenisisimka sana kuona Simba na tembo kwa mara ya kwanza kwa macho yangu katika historia ya maisha yangu” alisema Bwana Yolisa Mkele, mwandishi wa habari kutoka gazeti la the Times. Aidha walivutiwa sana na ziara ya boti katika mto Rufiji ambapo walifanikiwa kuona idadi kubwa ya kiboko na mamba walioko katika mto huo.

  Katika ziara hiyo ya Selous wandishi hao walitembelea na kuona kaburi la Mwingereza Kapteni F.C Selous aliyekuwa akiishi na kufanya shughuli za uwindaji katika eneo hili kabla ya kuuawa na Wajerumani katika vita ya kwanza ya dunia na kuzikwa katika eneo hili lililopewa jina lake kama kumbukumbu na heshima kwake.

  Ziara hii ya kundi la wandishi wa habari imeandaliwa na Bodi ya Utalii Tanzania-TTB kwa kushirikiana na Hoteli ya Serena na Shirika la ndege la Fast jet kwa lengo la kitangaza Tanzania nchini Afrika Kusini . Wandishi hawa wako nchini kwa ziara ya siku tatu ya kujionea vivutio vya utalii vya Tanzania hususan vilvyoko katiia pori la akiba la Selous na Zanzibar.

  Wakati huo huo wandishi wa habari watano kutoka vituo vya televisheni vya nchi za Ufalme za Kiarabu wanatembelea pia pori la akiba la Selous baada ya ziara yao katika hifadhi ya Taifa ya Serengeti kabla ya kuelekea Zanzibar. Ziara ya wandishi hao imeandaliwa na Bodi ya Utalii Tanzania TTB kwa lengo hilo kutangaza vivutio vya utalii vya Tanzania katika nchi za falme za kiarabu
  Baadhi ya wandishi wa habari kutoka Afrika Kusini wakipiga picha Simba waliotulia chini ya mti katika Pori la Akiba la Selous.
  Simba wakiwa wamepumzika chini ya mti katika Pori la A Kiba ka Selous.
  Mwongoza watalii Bw. Mohammed Kabouru akitoka maelezo kwa wandishi wa habari wa Afrika Kusini kuhusu kaburi na historia ya marehemu Selous Mwingereza ambaye jina lake ndilo asili ya pori hilo akiba maarufu hapa nchini na Afrka.

  0 0

  The Secretary General of the East African Community, Amb. Dr. Richard Sezibera has reiterated that peace and stability were critical in attracting investments in the Great Lakes Region and that the involvement of the leaders, as well as the United Nations led by the Secretary General and his Special Envoy to the Region was extremely crucial. 

  Amb. Sezibera, who was yesterday delivering the keynote speech themed Preparing the Ground For Responsible Investment, at the  Great Lakes Private Sector Investment Roundtable, held at the United Nation Economic Commission for Africa complex in Addis Ababa, said the Roundtable Dialogue on ways in which corporate activities and responsible investment can advance peace, stability, prosperity and inclusive growth in the Great Lakes region was critical, noting that “within International Conference of the Great Lakes Region (ICGLR), focus is now shifting to investment, this is a major achievement that we should all celebrate”.

  The Secretary General opined that responsible, targeted investments, during periods of conflict, or in the immediate aftermath, were crucial to ending the conflicts and promoting rapid return to normality and stability.

  He noted that promoting cross border investments and ensuring that the benefits of growth are efficiently harnessed and equitably shared was part of the inclusive growth.  “Failure to master this imperative is largely the reason behind the endless conflict we have witnessed in the region for years” commented the Secretary General, adding that “we must think differently about investment. We need to think and act regionally and put in place policies that allow for these cross border investments”.


  0 0


  0 0


  0 0

  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwa amesimama na baadhi ya viongozi wa Mkoa wa Dar es Salaam akiwemo Katibu Tawala Ndugu Theresia Mbando (wa tatu kutoka kulia), Mkuu wa Wilaya ya Ilala Ndugu Raymond Mushi (wa nne) nje ya jengo la Makumbusho ya Taifa kwa ajili ya kupokea maandamano ya wanafunzi wa shule za msingi za Dar es Salaam wakati wa sherehe ya uzinduzi wa Tamasha la vitabu vya watoto katika Mkoa huo tarehe 12.6.2014.
  Baadhi ya wanafunzi wa Shule za Msingi mkoani Dar es Salaam wakiwa wamebeba mabango yenye picha na ujumbe mbalimbali wakati wa sherehe za uzinduzi wa Tamasha la vitabu vya watoto mkoani Dar zilizofanyika kwenye ukumbi wa Makumbusho ya Taifa tarehe 12.6.2014.
  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiangalia mchezo wa sarakasi iliyokuwa ikichezwa na wanafunzi wa shule za msingi mkoani Dar wakati wa sherehe ya uzinduzi wa tamasha la vitabu vya watoto tarehe 12.6.2014.


  0 0


  0 0

  Bendi maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya Ngoma Africa Band aka FFU ughaibuni 
  wanatarajiwa kutingisha jukwaa tena katika onyesho kubwa la  
  DIETZEN FESTIVAL,litakalofanyika siku ya jumamosi 14 Juni 2014 katika anuani 
  Schwimmbad Freibad Waldschwimmbad Dietzenbach, Offenthaler Straße 85, 63128 Dietzenbach, jirani na Frankfurt,huko Ujeurimani,Muziki wa ngoma africa unafananishwa sawa na gwaride la FFU na wapenzi wa bendi hiyo. 
  Wasilikilize FFU Ughaibuni at www.ngoma-africa.com 

  0 0

  ADDRESS YETU MPYA NI;
  UNIT 16D TILBURY INDUSTRIAL COMPLEX
  TILBURY FREEPORT
  ESSEX
  RM18 7HB
  KUANZIA SASA MZIGO WA NDEGE NI SIX DAYS GUARANTEE
  SALOON CARS TO DAR NOW £680
  4 X 4 CARS TO DAR  NOW £770
  UKISHIP MAGARI ZAIDI YA MOJA UNAPATA BIG DISCOUNT!
  AIR CARGO TO DAR £3.80 INCLUSIVE CLEARANCE
  KAMA UNA MZIGO WA MSAADA TUNASAFIRISHA BURE
  FREE STORAGE IN OUR OFFICE
  FREE COLLECTION FROM EAST LONDON 
  £50 COLLECTION FROM ANYWHERE IN UK
  COLLECTION POINT IS
  ILALA MTAA WA BUKOBA
  CONTACT; TORNADO +255713607116
  SIMPLY THE BEST IN BUSINESS
  JUST DROP YOUR CAR AT OUR OFFICES AND WE WILL TAKE CARE OF IT
  WE WILL GET IT INSPECTED AND LOAD IT TO THE SHIP FOR YOU!
  BEI ZETU HAZINA WASHINDANI NDIO MAANA TUMEZIANIKA WATU WAJUE
  THE DIFFERENCE IS CLEAR!
  WE ARE NOW OPEN ON SATURDAYS
  WE PROMISED, WE DID IT AND WE ARE MAKING IT EVEN BETTER!
  Tupigie kwa namba hizo hapo Chini au  tutumie email tafadhali
  SIMON  LOUIS +44 (0) 79 506 89 243
  JONSTONE MALUNDA +44 (0) 7404298077 

  0 0


  Mchungaji Abel Orgenes (wa kwanza kulia) wa Kanisa la International Evangelism akiongea machache na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akitangaza mkesha utakaofanywa na Huduma ya AFLEWO ambao utakuwa wa kusifu na kuabudu na maombi kwa ajili ya Afrika na Tanzania. Anayefuatia ni Mchungaji Fred Okello wa Kanisa la Upper Room Ministries Tz, Mchungaji Deo Lubala wa Kanisa la Word Alive pamoja na mwenyeji wao Mchugaji Paul Safari wa Kanisa la Dar es Salaam Pentekoste.
  Mchungaji Deo Lubala (katikati) wa Kanisa la Word Alive akiongea machache na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akitangaza mkesha utakaofanywa na Huduma ya AFLEWO ambao utakuwa wa kusifu na kuabudu na maombi kwa ajili ya Afrika na Tanzania. Anayefuatia kulia ni Mchungaji Fred Okello wa Kanisa la Upper Room Ministries Tz na mwenyeji wao Mchugaji Paul Safari wa Kanisa la Dar es Salaam Pentekoste.
  Huduma ya AFLEWO imeandaa mkesha wa kusifu na kuabudu na maombi kwa ajili ya Afrika na Tanzania. Waimbaji zaidi ya hamsini kutoka makanisa mbali mbali watakuwa kwenye jukwaa moja wakisifu Mungu. Waumini na Wachungaji na maaskofu watakusanyika kumsifu na kumuomba Mngu kwa ajili ya taifa la Tanzania hasa kwa ajili ya mchakato wa katiba na uchaguzi mkuu utakaofanyika mwakani 2015.
  Mkesha huu maalum utafanyika kesho Ijumaa Juni 13, 2014 katika kanisa la City Christian Center, Upanga jijini Dar es Salaam (CCC) lililoko karibu na Chuo Kikuu cha Mzumbe. Kutakuwa hakuna kiingilio, watu wote mnakaribishwa kusifu na kuabudu.

  0 0

   Mhe. Peter Kallaghe, Balozi wa Tanzania nchini Uingereza akizungumza na  Mhe. Mark Simmonds, Waziri wa Uingereza anayeshughulikia masuala ya Afrika kabla ya ufunguzi wa Mkutano wa Kimataifa kuhusu Ukomeshwaji wa Udhalilishaji wa Kijinsia kwenye Maeneo yenye Migogoro unaoendelea Jijini London, Uingereza. 
  Kwenye sherehe za ufunguzi, waandaaji wa mkutano huo walisifia nchi zinazochangia kuleta amani kwenye maeneo yenye migogoro duniani . Aidha walisifu hatua ya Tanzania kuwa miongoni mwa nchi za kwanza kukubali na kusaini Tamko la Umoja wa Mataifa la Kukomesha udhalilishaji wa Kijinsia katika maeneo yenye migogoro. (Declaration of Commitment to End Sexual Violence in Conflict).  
  Mwandaaji wa Mkutano wa Kimataifa kuhusu Ukomeshwaji wa Udhalilishaji wa Kijinsia kwenye Maeneo yenye Migogoro, Mhe. William Hague, Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza 

   Mwandaaji mwenza ambaye ni mcheza filamu nyota  Bi. Angelina Jolie, Mwakilishi Maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu Masuala ya Wakimbizi, akitoa hotuba yake ya  ufunguzi kwenye mkutano huo unaoendelea Jijini London, Uingereza.
   Mhe. Peter Kallaghe, Balozi wa Tanzania nchini Uingereza akiweka saini hati ya tamko la jumla la mkutano huo  likiwataka washiriki kuchukua hatua sasa ya  kukomesha udhalilishaji wa kijinsia kwenye maeneo yenye migogoro.
  Mhe. Peter Kallaghe, Balozi wa Tanzania nchini Uingereza akiwa kwenye picha ya pamoja na ujumbe wa Tanzania kwenye Mkutano wa Ukomeshwaji wa Udhalilishaji wa Kijinsia kwenye Maeneo yenye Migogoro unaondelea Jijini London, Uingereza. kuanzia tarehe 11 hadi 13 Juni, 2014.

  0 0


  0 0

  Na Mwandishi Maalum, New York 
  Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika ( SADC) imetamka bayana kuwa, inajivunia mchango wake kupitia Force Intervention Brigade (FIB) inayoundwa na majeshi kutoka Tanzania, Afrika ya Kusini na Malawi katika ulinzi wa wananchi wasio kuwa na hatia , urejeshwaji wa hali ya Amani na utulivu pamoja na kuling’oa kundi la waasi la M-23. 
  Siku ya Jumatano, Baraza kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa, lilikuwa na mjadala wa wazi ulioandaliwa na Rais wa Baraza hilo kwa mwezi huu wa June ambaye ni URUSI. 
  Dhima ya mjadala huo wa wazi ililenga katika kuwapa fursa wajumbe wa Baraza hilo na wale wasio wajumbe kubadilishana mawazo kuhusu mwelekeo mpya wa Operesheni za ulinzi wa Amani chini ya Umoja wa Mataifa. 
  Akizungumza kwa niaba ya SADC, Mwenyekiti wa SADC ambaye ni Muwakilishi wa Kudumu wa Malawi katika Umoja wa Mataifa, Balozi Charles Peter Msosa amesema, SADC ilikubali ombi Baraza Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa la kupeleka FIB ambayo iko ndani ya MONUSCO pamoja na matumizi ya mamlaka nguvu kama ilivyoainishwa kupitia Azimioa namba 2098 la mwaka 2013 la Baraza Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa. 
  “ Ni kwa ushirikiano wa karibu kati yetu (SADC) na Baraza Kuu la Usalama, ushirikiano uliotufanya tukakubali ombi la kutoa majeshi yetu kuunda FIB. Sisi SADC tunajivunia mchango wetu huo na tunajivunia FIB akasema Balozi Msosa. 
  Na kusisitiza. “Mamlaka nguvu ya FIB si tu yamechangia katika kuling’oa kundi la M-23, kundi ambalo lilikuwa likiendesha mambo yake bila pingamizi lolote,hata ikafikia mahali pachukua baadhi ya maeneo ambayo yalikuwa chini ya dhamana ya MONUSCO. Lakini pia FIB imeweza kurejesha imani ya wananchi kwa MONUSCO. Tunajivunia kazi yetu hiyo nzuri na tutaendelea kushiriki kikamilifu” . Akasisitiza Balozi wa Malawi. 
  Aidha SADC kupitia msemaji wake huyo, imesema inatambua fika kuwa matumizi ya nguvu si suluhisho pekee la kumaliza vita vya muda mrefu katika eneo hilo la Mashariki ya Kongo. Na kwamba michakato ya kisiasa ukiwamo mpango mpana wa amani, usalama na ushirikiano wa kiuchumi katika Eneo la Maziwa Makuu na ambao umeasisiwa na Umoja wa Mataifa ndiyo njia sahihi ya hatimaye kurejea kwa amani ya kudumu katika eneo hilo. 
  Aidha akasema, wakati SADC ikiwakumbuka walinzi wake wa amani waliopoteza maisha wakati wakitekeleza jukumu la ulinzi wa Amani, itaendelea kushirikiana na Umoja wa Mataifa katika kuhakikisha amani na usalama katika eneo la Maziwa Makuu. 
  Wajumbe karibu 50 walizungumza wakati wa majadiliano hayo ambayo yalifunguliwa na Katibu Mkuu Ban Ki Moon. wengi wao licha ya kuzungumzia mwelekeo mpya wa mzima wa Operesheni za Ulinzi wa Amani chini ya Umoja wa Mataifa na changamoto zake, walioonyesha wazi kuunga mkono na kusifu kazi nzuri ya FIB chini ya MONUSCO. 
  Mjumbe wa Marekani Bw. Jeffrey Delaurentis katika mchango wake alisema, matumizi ya mamlaka nguvu kama ilivyofanya MONUSCO kupitia FIB imedhihirisha kuwa yanaweza kuleta mafanikio. 
  Naye mzungumzaji wa Malaysia Siti Hajjer Adrin alisema kutokana na changamoto kubwa inayowakabili walinzi wa Amani, pengine matumizi ya mamlaka nguvu yanaweza kuwa suluhisho la namna si tu ya kukabiliana na mabadiliko ya mwenendo mzima wa operesheni za ulinzi lakini pia kuwawezesha walinzi wa Amani kujilinda wao wenyewe dhidi ya mashambulizi. 
  Naye Muwakilishi wa Jordani alieleza kwamba uamuzi wa matumizi ya mamlaka nguvu si ya kwanza kufanywa katika shughuli za ulinzi wa amani chini ya Umoja wa Mataifa. 
   Kwa kile alichosema imeshawahi kufanyika katika operesheni kadhaa huko nyuma na akaelezea kushangazwa wake na wale wanaoona kama jambo hilo ni geni kwa kuwa tu FIB ndo wamepewa mamlaka hayo.
   Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,  Ban Ki Moon akizungumza siku ya jumatano wakati Baraza Kuu la Usalama lilipokuwa na majadiliano ya wazi kuhusu mweleko mpya wa Operesheni za Ulinzi wa Amani chini ya Umoja wa Mataifa. Katika Majadiliano hayo  Ban Ki Moon aliiambia  Jumuiya ya Kimataifa,  lazima ijipange upya ili kukabiliana na changamoto za ulinzi wa amani chini ikiwa  ni pamoja na ongezeko la gharama. Akasisitiza umuhimu wa matumizi ya teknolojia za kisasa katika shughuli za ulinzi.  Majadiliano  kwa sehemu kubwa yaligusia  matumizi ya  teknolojia hizo za kisasa pamoja , matumizi ya mamlaka nguvu katika ulinzi wa amani na  mazingira ya hatari  wakayokabiliana nayo walinzi wa amani.
   Muwakilishi wa  Kudumu wa  Jamhuri ya Malawi katika Umoja wa Mataifa, Balozi  Charles Peter Msosa aliyezungumza kwa niaba ya  Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika ( SADC)  katika majadiliano hayo ambapo alisisitiza kwamba SADC inajivunia  ushiriki  wake kupitia Force Intervention Brigade ambayo imo ndani ya MONUSCO katika  juhudi za  kulinda wananchi wasio na hatia,  kuyasambaratisha makundi ya waasi   yenye silaha na kurejesha imani ya MONUSCO kwa wananchi.
  Lt. Col. Wilbert A. Ibuge, Mwambata Jeshi wa Uwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa akiwasilisha mchango wa Tanzania  mbele ya  Baraza Kuu la Usalama lilipokutana siku ya Jumatano, wakati wa majadiliano ya wazi kuhusu  mwelekeo mpya wa Operesheni za Ulinzi wa Amani chini ya Umoja wa Mataifa. Mchango wa Tanzania katika  majadiliano hayo ulisisitiza  pamoja na mambo mengine, umuhimu wa Operesheni za kulinda Amani  kuwa na ushirikiano na uhusiano wa  karibu na nchi mwenyeji wakati wa utekelezaji wa mamlaka  yake.

older | 1 | .... | 468 | 469 | (Page 470) | 471 | 472 | .... | 3283 | newer