Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 467 | 468 | (Page 469) | 470 | 471 | .... | 3348 | newer

  0 0

  Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kuzindua rasmi chapisho la tatu la taarifa za msingi za kidemografia,kijamii na kiuchumi pamoja na tovuti katika kupata taarifa za Sensa na Makazi katika hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwl.Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo.Viongozi wengine walioshiriki katika hafla ya uzinduzi huo kutoka kushoto ni Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, Bibi Mariam Khan Mwakilishi wa UNFPA,Waziri Mkuu Mizengo Pinda,Waziri wa Fedha Bi.Saada Mkuya na kulia ni Kamishna wa Sensa na Makazi Hajjat Amina Mrisho Said
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia wageni waliohudhuria hafla ya uzinduzi  wa Chapisho la tatu la taarifa za msingi za kidemografia,kijamii na kiuchumi pamoja na tovuti itakayowezesha kupatikana kwa taarifa mbalimbali za sensa ya watu na Makazi katika hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Mwalimu Julius Nyerere Dar es salaam 

  0 0


  0 0

  Uongozi wa Kampuni ya Reli Tanzania – TRL unawataarifu abiria wote na wananchi kwa jumla  kuwa kutokana na kutetereka kwa  mojawapo ya madaraja katika bonde la mto Ruvu katika  reli ya kati , umeamua kusitisha kwa muda huduma ya usafiri wa abiria hadi ukarabati wa  daraja utakapokamilika.

  Hapo jana  Mkurugenzi Mtendaji wa TRL Mhandisi Kipallo Aman Kisamfu na Wahandisi waandamizi na Mafundi Mchundo Ujenzi walifika katika daraja hilo lililopo km 82/5 na kulifanyia tathmini ili kuona uharibifu uliotokea na mahitaji kuliimarisha ili lirejee katika kiwango cha usalama kuruhusu treni za abiria kupita.

  Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji, ukarabati wa kulirejesha katika hali ya kutumika utachukua takriban wiki moja na hivyo kuanzia jana saa 12 jioni eneo la reli kati ya Dar es Salaam na kilomita 82/5 Ruvu limesitishwa kwa huduma za usafiri wa reli.

  Kwa taarifa hii  wananchi na wateja wa TRL na wananchi kwa jumla  ambao walikuwa wasafiri kwenda bara kwa treni ya jana ya  Juni 10, 2014 wanatakiwa kufika katika stesheni zilizokaribu nao ili warejeshewe nauli zao ili watafute usafiri mbadala. Wakati taarifa hii inatolewa katika vyombo vya habari zoezi la kuwarejeshea nauli abiria wapatao 1000 lilikuwa zinaendelea   katika stesheni mbali mbali za TRL na hasa katika Stesheni  kubwa ya Dar es Salaam ambapo safari kwenda bara huanzia.

   Aidha Uongozi wa TRL umeomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.

  Imetolewa na Afisi ya Uhusiano kwa Niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa TRL Mhandisi Kipallo Aman Kisamfu
  Dar es Salaam
  Juni 11, 2014


  0 0

  Na Abdulaziz Lindi

  Watu watatu wamefariki Dunia baada ya Magari mawili yenye tela kila moja kuacha njia na kupinduka na kufasabisha vifo vya watu hao na kujeruhi wengine wawili katika ajali iliyotokea Jana Huko Tarafa ya Rondo wilaya ya Lindi Mkoani Lindi.

  Ajali hiyo Iliyohusisha gari aina ya HOWO lenye Usajili T270BZU na Tela na T260AZU Pamoja na Lori aina HOWO T871 BTH Tela T 626 BTT yote yaliacha njia

  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi kamishna msaidizi Renatha Mzinga amethibitsha kutokea kwa ajali hiyo na kuwataja marehemu hao ambao ni Marehemu Jackson Francis Kayombo (DEREVA) mwenye umri wa miaka 42,marehemu Lazaro Michael Chaula,(Mkinga) miaka 27 Dereva na Marehemu Mohamed Jumanne Said (Mmakonde) miaka 23.

  Kamanda Mzinga amewataja waliojeruhiwa katika ajali hiyo ni ambao ni Given Mussa Mohamed na Seleman Ibrahim Hamis ambapo pia alibainisha kuwa Maiti na majeruhi wote wamefikishwa katika Hospital ya Sokoine Manispaa ya Lindi.

  Aidha kamanda Mzinga pia alieleza matukio ya mwishoni mwa wiki ambapo Wakazi wanne wa wilaya za Nachingwea,Ruangwa na Manispaa ya Lindi, wamefariki dunia katika matukio tafauti,likiwemo mtu anayesadikiwa kuwa na matatizo ya akili kuwapiga vikongwe wawili mwishoni mwa wiki iliyopita mkoani hapa.


  0 0

  Twaweza, kama sehemu ya kazi zake kwenye Mpango wa kuendesha shughuli za serikali kwa uwazi (OGP), imetoa tuzo za kompyuta (aina ya laptops) na taa zinazotumia nishati ya jua kwa waandishi 37 kutokana na mawazo yao juu ya namna Serikali na wananchi wanavyoweza kuboresha utoaji huduma kwenye sekta za elimu, afya na maji.

  Shindano hili la kutafuta maoni ya wananchi lilizinduliwa kwa ushirikiano wa Twaweza pamoja na Serikali ya Tanzania mwezi Desemba 2012. Twaweza iliisaidia Serikali kukusanya maoni haya kwa kusambaza taarifu kuhusu shindano hili na maelezo yake kwenye vijitabu takriban milioni tano vyenye kueleweka kiurahisi na pia ilipitia na kuchambua maoni yaliyowasilishwa.

  Kati ya maoni 250 yaliyopokelewa, 12 bora walizawadiwa kompyuta na maoni 25 yaliyofuatia walipewa pongezi kubwa na taa zinazotumia nishati ya jua. Majina ya washindi hao ni:

  Washindi 12 bora zaidi: Rahma Chanzi, Yavan N. Eslon, Amani Frank, Kingstone W. Kahumuza, Sarah Lucas Kisusange, Castory Luoga, Noely Sosimaria Mapunda, Allen Richard Materu, Abdul Walter Moshi, Einoth Justine Ngotoroi, Editha M. Tairo na Godwin Waziri.

  Washindi 25 waliofuatia: waliopata pongezi na taa inayoitumia nishati ya jua ni- Godfrey Baraka, Sande John, KenethKammu , Gabriel Erick Mvingira, Fatuma M. Athumani, Joseph Mathew Buyende, Rachel Philip Bwathondi, Johanita Chimwanga, Christina K. Christopher, William Gabriel Lugis Benjamin John, Specioza Joseph Kalekwa, Kelvin CosmasMacha, Kaliro M. Magoro, Emmanuel Deus Malimi, Filipo Faraja Maliwa, Mariamu Omary Mcholo, Simon Sabaya Mollel, Dorcus Ayoub Mollel, Mary Richard Msukwa, Dativa Mugashe, Abubakar Khasim Mweli, Erick Rwelamila, Vincent Deo Simba na Hedwiga Medard Tairo.

   Baadhi ya mawazo yaliyoshinda yalikuwa pamoja na:
  ·         Uwepo wa gazeti maalum linalochapishwa na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kuwajulisha wanafunzi, walimu, wazazi na watu wengine kuhusu maendeleo ya sekta ya elimu na takwimu muhimu kama vile viwango vya kufaulu mitihani, mitaala na matukio mengine muhimu.
  ·         Upungufu wa wafanyakazi wa afya nchini Tanzania kwa sehemu unaweza kuhusishwa na ukosefu wa wanafunzi waliosomea masomo ya sayansi. Ili kukabiliana na tatizo hili Serikali inapaswa kuanzisha mfumo wa motisha, kama vile kutoa zawadi, ili kuvutia wanafunzi kusoma masomo ya sayansi.

  Zawadi zilitolewa kwenye mkutano ulioitishwa na Serikali ya Tanzania ili kushauriana na wadau juu ya rasimu ya pili ya Mpango wa Kuendesha Serikali kwa Uwazi (OGP).. Mgeni rasmi, Mheshimiwa George Mkuchika, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais -Utawala Bora, aliwazawadia wanafunzi vyeti na tuzo zao.

  OGP ni jitihada ya kimataifa inayolenga kuziongoza Serikali kuwajibika zaidi kwa wananchi kwa kukuza uwazi, kuwawezesha wananchi, kupambana na rushwa, na kutumia teknolojia mpya kuimarisha utawala. Hadi sasa, ni mataifa 64 yaliojiunga na OGP, Tanzania ikiwa mmoja wapo.

  Mpango Kazi wa  kwanza  wa OGP kwa Tanzania inapatikana hapa: http://bit.ly/1mZCPj4. Mpango huu umeweka kipaumbele kwenye utoaji huduma na upatikanaji wa taarifa kama nguzo muhimu kwenye harakati za Tanzania kuelekea Serikali wazi. Mpango Kazi wa pili wa Tanzania kwa sasa uko hatua za mwisho kukamilishwa kufuatia mashauriano na wadau mbalimbali.

  Rakesh Rajani, Mkuu wa Twaweza, alisema "Mawazo mapya yanatoka sehemu mbali mbali na shindano hili lilikuwa ni njia moja ya kuibua michango mipya kutoka kwa vijana. Huu ndiyo moyo wa OGP; kutambua kuwa serikali haina ukiritimba juu ya ufumbuzi wa changamoto zetu kuu na huitaji kutoa nafasi na fursa kwa wengine kuchangia mawazo."

  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Balozi wa Marekani nchini Tanzania Mhe,Mark Bradley Childress alipofika Ikulu Mjini Unguja Kujitambulisha leo.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein akizungumza na Balozi wa Marekani nchini Tanzania Mhe,Mark Bradley Childress alipofika Ikulu Mjini Unguja Kujitambulisha leo.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein akifuatana na Balozi wa Marekani nchini Tanzania Mhe,Mark Bradley Childress (kushoto) baada ya mazungumzo yao alipofika Ikulu Mjini Unguja kujitambulisha leo.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]

  0 0

  Mnamo tarehe 11/06/14 majira ya 0100hrs huko kituo kidogo cha Kimanzichana Pwani,watu wasiojulikana waliojifanya kuwa ni raia wema waliingia kituo kidogo cha Polisi Kimanzi Chana huku wakikimbia wakiwa na silaha za jadi kiasi cha askari wa zamu kuamini kuwa ni watu wanaohitaji msaada. 

  Cha kushangaza watu hao walimvamia askari mwenye silaha ambaye amefahamika kwa jina la JOSEPH
  NGONYANI na kuanza kumkatakata mapanga na hatimaye kupora silaha aina ya SMG ikiwa na risasi
  30.

  Ndipo walipoanza kushambulia kwa risasi askari wengine na kufanikiwa kupora SMG ya pili na risasi 30. Hatimaye watu hao wakapora risasi za akiba 41 na kutoweka kusikojulikana.

  Askari Ngonyani alifariki dunia alipokuwa anapatiwa matibabu kwenye hospitali ya wilaya ya Mkuranga. Askari mwingine aitwaye VENANCE amejeruhiwa mgongoni kwa risasi ambayo bado imo ndani, na kwenye paja la mguu wa kulia.

  Mgambo Mariam alijeruhiwa kichwani, shingoni na kuvimba bega kutokana na kupigwa sana mateke na kujeruhiwa mbavuni. 

  Kwa mujibu wa mganga Mkuu wa zamu wa Hospitali hiyo aitwaye VERONICA MUSIME, anathibitisha askari huyo kufariki akiwa anapatiwa matibabu hapo Mkuranga wakati wengine wamekimbizwa Muhimbili kwa matibabu ya kina. 

  Kazi ya Mungu haina makosa; vituoni tuwe makini sana na stahili hii ya ujambazi; HESHIMA PEKEE kwa marehemu na majeruhi hawa ni kuwapata watuhumiwa wote na silaha walizoiba bila kuchelewa. Bila kujali mkoa ulipo, taarifa za haraka tunatarajia kupata toka kwako
  kuhusiana na wahusika wa tukio hili. AMEN

  0 0
 • 06/11/14--10:09: UTEUZI WA NAIBU MABALOZI
 • Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, amefanya uteuzi wa Naibu Mabalozi wawili.Walioteuliwa ni Bw. Robert Kahendaguza (pichani kushoto) anayekuwa Naibu Balozi, Ubalozi wa Kudumu kwenye Ofisi za Umoja wa Mataifa, Geneva, Uswisi, na Bw. Msafiri Marwa (pichani chini) anayekuwa Naibu Balozi wa Tanzania London, Uingereza.

  Kabla ya uteuzi huu, Bw. Kahendaguza alikuwa Kaimu Mkurugenzi, Idara ya Ushirikiano wa Kikanda, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Bw. Marwa alikuwa Ofisa Mambo ya Nje Mkuu.
  Uteuzi huu unaanza tarehe 25 Mei, 2014.

  IMETOLEWA NA:

  KATIBU MKUU

  WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA,

  DAR ES SALAAM

  JUNI 11, 2014

  0 0

  Mhe. Bernard K. Membe, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa akiwa kwenye mazungumzo na Mhe. Mark Simmonds, Waziri wa Uingereza anayeshughulikia masuala ya Afrika kwenye Wizara ya Mambo ya Nje ya Uingereza leo tarehe 11 Juni 2014. 
  Pamoja na mambo mengine, Mawaziri hao wamezungumzia maazimio ya Mkutano wa Kimataifa kuhusu Ukomeshwaji wa Udhalilishaji wa Kijinsia kwenye Maeneo yenye Migogoro (“End Sexual Violence in Conflict”) unaoendelea mjini London, Uingereza.  
  Tanzania inashiriki mkutano huo kufuatia mualiko wa Serikali ya Uingereza kutokana na mchango mkubwa wa Tanzania katika kufanikisha kuwepo kwa Tamko la Umoja wa Mataifa linalohusu suala hilo (Declaration of Commitment to End Sexual Violence in Conflict).  

  0 0
 • 06/11/14--10:27: mambo ya gado


 • 0 0  Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

  MAHAKAMA kuu kanda ya Moshi imetoa adhabu ya kunyongwa hadi kufa kwa washtakiwa wawili raia wa Kenya katika  kesi ya mauaji ya askari Polisi, Pc Michael Milanzi, wakati wa tukio la uporaji  wa fedha katika benki ya NMB tawi la Mwanga mkoani Kilimanjaro.
  Mbali na hukumu hiyo iliyosomwa na Jaji mfawidhi wa Mahakama kuu, Kakusulo Sambo kwa zaidi ya saa, nne ,Mshatakiwa wa tatu katika kesi hiyo ,Karisti Kanje(Mtanzania) yeye amehukumiwa kutumikia kifungo cha miaka mitano(5) jela kwa kosa la kuhifadhi na kutorosha watuhumiwa wa mauaji ya askari polisi.

  0 0

   Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (wapili kushoto), Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP) Ernest Mangu (kushoto), Kamishna Mkuu wa Idara ya Uhamiaji, Sylvester Ambokile (wanne kushoto) wakipokea taarifa kuhusu Mfumo wa Ufuatiliaji wa Mienendo ya Watu (Public Surveilance Sytem (Global eye)  kutoka kwa Mtaalam wa Kampuni ya Telecom ya nchini China. Waziri Chikawe na ujumbe wake wapo jijini Beijing, China kwa ziara ya kikazi. 

   Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (kushoto) akimsikiliza kwa makini Mwenyekiti wa Kampuni ya Kutoa Huduma ya Mawasiliano nchini China, Li Ping alipokuwa akimfafanulia masuala mbalimbali ya mawasiliano yanayofanywa na Kampuni yake. Waziri Chikawe yupo jijini Beijing nchini humo na Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP) Ernest Mangu, Kamishna Mkuu wa Idara ya Uhamiaji, Sylvester Ambokile kwa ajili ya ziara ya kikazi. 

  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (wapili kushoto), Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP) Ernest Mangu, Kamishna Mkuu wa Idara ya Uhamiaji, Sylvester Ambokile wakiwa katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Kampuni ya Kutoa Huduma ya Mawasiliano nchini China, Li Ping. Waziri Chikawe na ujumbe wake wapo jijini Beijing, China kwa ziara ya kikazi. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

  0 0
 • 06/11/14--10:45: JK ATUA DODOMA LEO
 • Rais Jakaya Kikwete Akisalimiana na Mwenyekiti Mstaafu wa CCM wa mkoa wa Dodoma MzeePancras Ndejembi  baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma leo Juni 11, 2014. 
  Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

  0 0

   Naibu Waziri wa Fedha Mhe.Mungulu Nchema akigombewa kusalimiwa na Wanafunzi kutoka Shule ya Msingi Assumpta iliyopo Hai Mkoani Kilimanjaro.Wanafunzi hawa wanatembelea Bunge kwa ziara ya kimafunzo.
   Naibu Waziri wa Fedha Mhe.Mungulu Nchema katikati Mstari wa Nyuma akiwa katika Picha ya pamoja na Wanafunzi kutoka Shule ya Msingi Assumpta iliyopo Hai Mkoani Kilimanjaro
   Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuju,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe.Aggrey Mwanri akiwa katika Picha ya pamoja na Wanafunzi kutoka Shule ya Msingi Assumpta iliyopo Hai Mkoani Kilimanjaro.
    Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuju,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe.Aggrey Mwanri akiongea  na Wanafunzi kutoka Shule ya Msingi Assumpta iliyopo Hai Mkoani Kilimanjaro.
   Waziri wa Ujenzi Mhe.John Magufuli (kulia)  akijadiliana na kubadilishana mawazo na Waziri wa nchi Ofisi ya Rais (Kazi Maalum)  Mhe. Profesa Mark Mwandosya mara baada ya bunge kuahirishwa leo mchan
  Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi Mhe.Prof Anna Tibaijuka kushoto akibadilishana mawazo na Waziri wa Zamani wa Ardhi Mhe. John Chiligati  mara baada ya bunge kuahirishwa leo mchana. Na Deusdedit Moshi Mtendaji Mkuu wa Photo Solutions wawakilishi wa Michuzi Blog Kanda ya Kati.

  0 0


  Here is the latest Tanzanian cultural events and news - please help us to spread the word, especially to share events that don't yet have a digital platform. The Zanzibar International Film Festival is approaching, so please find out more about the festival in this edition of the newsletter and do support and enjoy this long-running event.

  Sanaa Central is a one-stop site for Tanzanian arts and culture information - from the latest cultural events through to searchable organisations across the sectors, from theatre to literature, photography to dance. It's a resource for all of us to share who're involved with or interested in the Tanzanian cultural scene. Please add your organisations and send your events through to news@mambomagazine.com

  Sanaa Central is a collective of cultural organisers from across the arts, including ZIFF, Sauti za Busara, Culture and Development East Africa, Mambo magazine, Nafasi Artspace, Muda Africa, Tanzania Heritage Project, Arterial Network Tanzania and Kwame Mchauru, supported by Africultures, with funding from the European Union.

  For full details CLICK HERE

  0 0

   Mmoja wa wadau wa shughuli za utafutaji na uzalishaji gesi akitoa maoni yake kuhusu namna ya kuboresha rasimu ya Sera ya Petroli. Wanaofuatia ni baadhi ya wadau kutoka  Kampuni mbalimbali zinazofanya shughuli hizo nchini.

   Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Ngosi Mwihava (katikati) akifuatilia kwa karibu wadau wakitoa  maoni wakati wa warsha ya  wadau wanaoshughulika na   shughuli za utafutaji na uzalishaji gesi na mafuta ili kupata maoni yao  yatakayosaidia kuboresha Rasimu ya Sera ya Petroli. Wa Kwanza kushoto ni Kamishna Msaidizi anayeshughulikia masuala ya Umeme Mhandisi Innocent Luoga, wa pili kulia ni Kamishna Msaidizi  Nishati, anayeshughulikia  Petroli  Mhandisi Stanley Marisa na wa kwanza kulia ni Mjiolojia Mwandamizi  Wizara ya Nishati na Madini,  Adam Zuberi.

   Washiriki katika warsha ya  wadau wanaoshughulika na   shughuli za utafutaji na uzalishaji gesi na mafuta ili kupata maoni yao  yatakayosaidia kuboresha Rasimu ya Sera ya Petroli
  Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Ngosi Mwihava ( Wa nne kutoka kulia) akiwa katika picha  ya pamoja na  Wadau wa  shughuli za   utafutaji na uzalishaji gesi na mafuta  mara baada ya kufungua warsha hiyo. Picha na Asteria Muhozya

  0 0

  Ndugu wanachama, Wadau na wandishi wote wa Habari, 
   Kuna ujumbe unaozunguka miongoni mwetu, kwa wandishi wa habari wasiokuwa wanachama na kwa wadau wetu ukieleza kwamba Mbeya Press Club (MBPC) imeandaa safari ya wanachama wake kutembelea nchi Jirani ya Malawi. 
  Ujumbe huu unawataja baadhi ya wanachama wa MBPC kuwa ndio waratibu wa Safari hiyo, huku ukiwataka wanachama na wadau kuchangia safari hiyo fedha kiasi cha shilingi 200,000 (Laki mbili) kwa kila mwanachama na mwandishi wa habari yeyote asiyekuwa mwanachama wa MBPC. 
  Kwa niaba ya uongozi wa MBPC napenda kuwataarifu Wanachama wa MBPC, Wandishi wa Habari wasiokuwa wanachama na wadau wetu kuwa mpango huo hauna utashi wala Baraka za MBPC, hivyo kwa yeyote Atakayejihusisha na mpango huo atambue kuwa atafanya hivyo kwa dhamana yake mwenyewe na sio ya MBPC. 
  MBPC inawataka na kuwaonya wanachama na watu wasiokuwa wanachama walio nyuma ya mpango huo kuacha mara moja kutumia jina la MBPC katika kuratibu mambo yao la sivyo hatua kali dhidi yao zitachukuliwa. 
  Uongozi wa MBPC unawataka watu hao kama wanaona mpango huo una kila sababu ya kutumia jina la MBPC wafike ofisini na kufuata taratibu zote ili kupata Baraka za MBPC. 
  Mwisho naomba kuwaasa wanachama wa MBPC kutojihusisha wala kuupapatikia mpango huo kwani kuna dalili kuwa mwisho wake sio mzuri.
   Nawatakieni kila la Heri 
  Emmanuel Lengwa – KATIBU MBPC. 
  Asante.

  0 0

  Hey there, 
  Does music have the same effect on you that it has one me? Often times when words fail, music expresses what the heart feels. 
  I believe in its power to change people. I also believe in its power to soothe one’s soul because music bypasses the mind and speaks to your heart. Music has the power to produce a kind of happiness that human nature can’t live without. Music is magical to me. 
  I love how one can sing a very beautiful melody about a terrible life situation but in the process get some wisdom and encouragement to keep the faith. It’s the equivalent of turning lead into gold. Did I choose music or did music choose me? That I really don’t know but it has me in its warm embrace. 
   Since you last heard from me, I’ve been promoting my album “Lovebird” via interviews with local and international media. I have performed with the Tinton Band in New York City as well as other venues like the United Nations. I taught a Soukouss Dance master class and I even had time to speak at high schools and colleges about what it's like to be a global citizen and the kind of leadership required in a changing world. 
  On my birthday 2 months ago, I got to swim and interact with a pod of wild dolphins in South Florida. The biggest highlight so far has been a recent invitation to attend the first ever, AFRIMMA Awards (African Music Magazine). 
  I have been nominated for 'Best Female, Diaspora' among some of my favorite Artists. What an honor! I'm so happy, grateful and humbled. I would love your vote. Please click on the link below to vote for me under “Best Female Diaspora” 
  http://afrimma.com/afrimma-nominees-2014/http://afrimma.com/afrimma-nominees-2014/

  0 0

   Mbunge wa Mwibara Mhe.Kange Lugola  akiomba kura za kuwania nafasi ya Mjumbe  wa Tume ya Utumishi Bungeni kwenye ukumbi wa Bunge mjini Dodoma leo Juni 11, 2014.
   Mbunge wa Mwibara Mhe.Kange Lugola akivua bango alilokuwa ameva wakati akiomba kura kwa wabunge za kuwania kuteuliwa kuwa  Mjumbe wa Tume ya  Utumishi  Bungeni kwenye ukumbi wa Bunge mjini Dodoma Juni11, 2014. Aliamriwa kuvua bango hilo na Spika wa Bunge Anne Makinda. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)  0 0
 • 06/11/14--11:53: menyu


older | 1 | .... | 467 | 468 | (Page 469) | 470 | 471 | .... | 3348 | newer