Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110185 articles
Browse latest View live

TBL YATOA SOMO LA UKULIMA BORA WA ZAO LA SHAYIRI MKOANI ARUSHA

$
0
0

 Joel Msechu mtaalamu wa zao la shayiri kutoka Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) akiwaonesha wakulima magonjwa wa shayiri na namna ya kuzuia magonjwa hayo katika katika mashamba yaliyopo Kijiji cha Emairete Monduli juu, mkoani Arusha. Wakulima hao huwezeshwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) katika uzalishaji wa zao hilo ambalo ni malighafi ya kutengenezea bia zinzozalishwa na kampuni hiyo.



 Meneja wa Zao la Shayiri Dk. Bennie Basson akiwaonesha wakulima kijitabu cha muongozo wa kilimo cha shayiri katika Kijiji cha Emairete Monduli juu, mkoani Arusha juzi. Wakulima hao huwezeshwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) katika uzalishaji wa zao hilo ambalo ni malighafi ya kutengenezea bia zinzozalishwa na kampuni hiyo.

 Meneja wa Shayiri wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) D.. Bennie Basson akizungumza na wakulima wa shayiri ktk kijiji cha Emairete Monduli juu, mkoani Arusha. Wakulima hao huwezeshwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) katika uzalishaji wa zao hilo ambalo ni malighafi ya kutengenezea bia zinazozalishwa na kampuni hiyo.


 Meneja wa Zao la Shayiri Dk. Bennie Basson akiwaonesha wakulima wa shayiri chati ya matumizi ya mbolea na viuatilifu vinavyoweza kuongeza mavuno ya shayiri katika Kijiji cha Emairete Monduli juu, mkoani Arusha. Wakulima hao huwezeshwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) katika uzalishaji wa zao hilo ambalo ni malighafi ya kutengenezea bia zinazozalishwa na kampuni hiyo.
 Meneja wa Zao la Shayiri Dk. Bennie Basson, akiwaonesha magugu ambayo ni hatari kwa zao la shayiri  alipowatembelea wakulima wa zao hilo Kijiji cha Emairete Monduli juu, mkoani Arusha juzi. Wakulima hao huwezeshwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) katika uzalishaji wa zao hilo ambalo ni malighafi ya kutengenezea bia zinazozalishwa na kampuni hiyo.
 Mtafiti wa zao la shayiri Geremia Mremi kutoka Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) akitoa elimu juu ya mbegu bora zilizothibitishwa kutoka TBL alipowatembelea wakulima wa zao hilo katika Kijiji cha Emairete Monduli juu, mkoani Arusha juzi. Wakulima hao huwezeshwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) katika uzalishaji wa zao hilo ambalo ni malighafi ya kutengenezea bia zinazozalishwa na kampuni hiyo.

introducing Warriors From The East - "Maisha Magumu"

SMART CODES goes to the next level with award nomination

$
0
0
Smartcodes, a tech startup from Dar-es-Salaam has been nominated in the 2014 Awwwards from awwwards.com as one of the best websites. As the #1 pick from Tanzania, Smartcodes has been nominated on an international platform going against web development and tech companies from around the world.

About the nomination for best website

The Awwwards are judged by a jury and users from the site who also get a say in which nominees have the chance of winning. Smartcodes will be judged on criteria such as design, user interface, content and creativity. As the #1 pick from Tanzania to be nominated, CEO Edwin Bruno said: “We were thrilled to hear that we have been nominated for this award. As the top choice from Tanzania to be nominated, we hope to represent our country well in this award competition. To be put amongst the best in the world for nominations, we couldn’t be happier.”
  
As an IT company, Bruno says that Smartcodes is defined by its mission to bring technology to everyone. The company achieves this thanks to products and services such as website design, mobile application, domain hosting and software development. Edwin Bruno continued to say: “We think our nomination for the Awwwards for website design is a sign that people appreciate beautifully-designed websites because design is the centre of what makes a website special. We look forward to sharing our philosophy on website design with everyone in Tanzania.”
  
You can read more about the Awwwards here (http://www.awwwards.com/about-us) and you can vote for Smartcodes by clicking VOTE here http://www.awwwards.com/best-websites/smart-codes

VIKUNDI 6 VYAKABIDHIWA MASHINE ZA KUKAMUA ASALI

$
0
0
 Katibu wa  Mtandao wa Jamii wa Usimamizi wa Misitu Kanda ya Kitapilimwa (MJUMIKK), Samson Fuko akisoma taarifa mbele ya mgeni rasmi Jesca Msambatavangu wakati wa hafla ya kukabidhiana mashine za kukamua asali na mizinga ya nyuki pamoja na mavazi maalum ya uvunaji asali   iliyofanyika katika kijiji cha Kinywang'anga hivi karibuni.
 Mgeni rasmi Jesca Msambatavangu mwenye kashda ya Tanzania shingoni akiwa na baadhi wa wavunaji wa asali kabla ya kwenda kuvuna asali na baadaye katika hafla ya kukabidhiana mashine za kukamua asali na mizinga ya nyuki pamoja na mavazi maalum ya uvunaji asali iliyofanyika katika kijiji cha Kinywang'anga hivi karibuni.
 Mgeni rasmi Jesca Msambatavangu na mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa akikabidhi mmoja wa wenyeviti wa vikundi mashine ya kukamua asali hafla ya kukabidhiana mashine za kukamua asali na mizinga ya nyuki pamoja na mavazi maalum ya uvunaji asali.
 Afisa misitu mstaafu Teresphory Kahatano akitoa maelekezo kwa walinaji wa asali kabla ya kwenda katika mizinga ya nyuki.
 Baadhi ya mashine za kukamua asali na mavazi rasmi yaliyokabidhiwa kwa vikundi 6 vya ujasiliamali.
Mgeni rasmi Jesca Msambatavangu na mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa akikabidhi mmoja wa wenyeviti wa vikundi moja ya mizinga iliyotolewa na TaFF kwa kushirikiana na MJIMUKK. (Picha zote na Denis Mlowe)

Na Denis Mlowe,Ismani

MFUKO wa Hifadhi ya Misitu Tanzania (TaFF) kwa kushirikiana na Mtandao wa Jamii wa Usimamizi wa Misitu Kanda ya Kitapilimwa (MJUMIKK) umewakabidhi mashine sita  za kukamua asali na mizinga ishirini kwa  vikundi vya ujasiriamali vinavyojishughulisha na ulinaji wa asali katika kata za Kitapilimwa na Kiwele katika jimbo la Ismani mkoani Iringa

Akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano iliyofanyika katika kijiji cha Kinywang’anga hivi karibuni, katibu wa mtandano wa MJUMIKK, Samson Fuko alisema lengo la msaada huo ni kuleta ufanisi wa kulinda, kutunza na kutumia kwa njia endelevu rasilimali za misitu na kuongeza kipato cha mwananchi mjasiriamali.

Alisema mashine hizo zitakuwa shamba darasa la ufugaji wa nyuki na upandaji miti utakaotumika kutoa mafunzo kwa vitendo kwa wanachama wake na kutoa elimu kwa jamii juu ya uhifadhi wa mazingira.

Fuko alisema mtandao huo umefanikiwa kuongeza idadi ya wanachama kutoka 50 waliokuwa mwanzao hadi wanachama 200 walioko sasa ambao unajihusisha na ufugaji wa nyuki unaotekelezwa katika vijiji sita kati ya vijiji 11.
 Alivitaja vikundi vilifaidika na msaada huo kuwa ni Kinywang’anga, Faraja group, Twiga group, Mshikamano. Jitegemee na kikundi cha Umoja vyote vikipatiwa  mizinga mashine na za kukamulia asali pamoja na mavazi maalumu ya kuvaa wakati wa kulina asali vyote vikiwa na thamani ya sh. milioni 4.5

Aidha aliwataka wadau kuvisaidia vikundi vya ufugaji nyuki mizinga ya nyuki na mbegu za miti kwa lengo la kuanzisha shamba darasa la ufugaji wa nyuki na shamba darasa la upandaji miti na mavazi ya kuvunia asali kwa vikundi hivyo.

Kwa upande wake mgeni rasmi Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Iringa Jesca Msambatavangu aliyekuwa mgeni rasmi katika makabidhiano ya mashine hizo amewaasa wazazi na walezi kuwahamasisha vijana kujiunga katika shughuli za maendeleo  wasiwaache  wakilegalega kwani vijana hao ndio nguvu kazi ya taifa.

 Alisema maendeleo ya mtu hayaletwi kwa kukaa bila kujishughulisha na kukaa vijiweni na kuwataka wajasiliamali hao kutumia  fursa waliyoipata kuitumia katika kujiletea maendeleo yao na taifa kwa ujumla.
 Aidha Msambatavangu aliwahidi wafugaji nyuki kuwatafutia soko la bidhaa zao kuweza kuwafikia watu wengi zaidi katika jamii ya mkoa wa Iringa na nje ya nchi.

Msambataangu ambae pia ni mlezi wa vikundi hvyo amewaeleza  wananchi kuwa kiongozi bora ni yule anaetekeleza majukumu  aliyopewa na wananchi na sio kuwadharau wale waliompa dhamana ya kuwa kiongozi
 Msambatavangu  amewataka viongozi wote waliopewa dhamana na wananchi kuwatumikia na kuwatatulia matatizo yao mda wowote wanapowahitaji na kuwajibika  sio kukaa na kutoa lawama

Aidha amempongeza   Mkurugenzi wa Halmashauri  ya wilaya ya Iringa  Pudensiana  Kisaka kwa kazi anayofanya  ikiwa  ni moja  ya utekelezaji wa majukukumu aliyopewa na serikali  na amesema kuwa kiongozi huyo anapaswa kuigwa na viongozi wa halimashauri nyingine kwani amekuwa akisikiliza matatizo ya wananchi katika halimashauri  yake na kuyafanyia  kazi.

MAADILI YAHIMIZWA NA KUTILIWA MKAZO KATIKA VYUO VYA ELIMU YA JUU NCHINI

$
0
0
Na Rocky Setembo – Afisa Habari, Tume ya Maadili ya Viongozi.

Viongozi wakuu kutoka Chuo cha Biashara ‘CBE’ wameaswa kuwa mstari wa mbele katika kulinda na kusimamia uadilifu wa Chuo hicho ili kuhakikisha Taifa linapata wasomi waliojengeka vyema kielimu na kimaadili.

Rai hiyo imetolewa na Katibu Viongozi wa Umma, Ofisi ya Rais - Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Bw. Tixon Tuyangine Nzunda, wakati akitoa Mafunzo ya Maadili kwa Wakurugenzi Wakuu na Wakurugenzi Wasaidizi, kutoka Kanda zote, wakiongozwa na Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Emanuel Mjema, jijini Dar es Salaam, hivi karibuni.

Alisema uadilifu na uwajibikaji katika Utumishi wa Umma, hususani katika eneo muhimu kama la Elimu, husababisha kuondoa au kupunguza migongano mibovu ya kimahusiano kazini, matumizi mabaya ya rasilimali za umma, kuleta tija na kuongeza thamani ya Elimu ya juu nchini, hali ambayo itaongeza ufanisi na udhibiti wa mianya ya ukiukwaji wa maadili na rushwa nchini.

Aliongeza kuwa, uongozi ulioadilifu hujenga ujasiri wa kusimamia sheria, kanuni na utaratibu bila uoga wala upendeleo, hivyo, ili waongozwao waende katika mstari uliosawa, yawabidi Viongozi wawe mfano bora na kioo kwa jamii.

“Kiongozi muadilifu huwa ni mfano katika kuleta mabadiliko. Awali, Chuo hiki cha Biashara, ambacho ni moja kati ya vyuo vikongwe nchini, kilikuwa hakina sifa sana hususani kwa upande wa wanachuo kuwa huru kuvaa vyovyote vile watakavyo. Hivi sasa, chuo hiki kimekuwa mfano wa kuigwa, hii ni kutokana na kuwepo na Uongozi uliobora na adilifu ambao umethubutu na umeweza kwa asilimia kubwa kukiweka chuo hiki katika hali iliyobora, kiuadilifu na kitaaluma. Hii ni hatua nzuri sana, na ni mfano wa kuigwa kwa vyuo vingine nchini” Alisisitiza Bw. Nzunda.

Awali, akifungua mafunzo hayo ya siku mbili, Mkuu wa Chuo cha “CBE” Profesa Emanuel Mjema alisema, lengo la kuyapokea na kuratibu mafunzo hayo ni kwanza kupata uelewa kuhusu Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma na matakwa yake, pili kupata muongozo uliobora utakaosaidia kuboresha na kuimarisha utekelezaji wa majukumu ya Kamati ya Maadili ya Chuo hicho.

Mafunzo hayo ya siku mbili yaliyoratibiwa na Chuo hicho, yalihusisha Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Kitengo cha Uratibu, Utawala Bora - Ikulu na Kitengo cha Sheria cha Chuo cha Biashara - CBE.
Mratibu Msaidizi kutoka Kitengo cha Uratibu,Utawala Bora, Ikulu, Bw. Emanuel Mwanga akiwasilisha mada kwa Viongozi wa Chuo cha Biashara – CBE.
Katibu Viongozi wa Umma, kutoka Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma,Bw. Tixon Nzunda, akiwasilisha mada kwa Viongozi wa Chuo cha Biashara – CBE.
Mkuu wa Chuo cha Biashara (CBE) Profesa Emanuel Mjema (mwenye suti nyeusi) akiwa katika picha ya pamoja na Wakurugenzi wa Chuo hicho na Wawezeshaji mara baada ya Mafunzo ya Maadili, yaliyofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu Viongozi wa Umma, Bw. Tixon Nzunda.

WAZIRI MEMBE AALIKWA LONDON KUHUDHURIA MKUTANO KUHUSU UKOMESHAJI WA UDHALILISHAJI WA KIJINSIA KWENYE MIGORORO

$
0
0

Serikali ya Uingereza imemwalika Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) kuhudhuria Mkutano wa Kimataifa kuhusu Ukomeshwaji wa Udhalilishaji wa Kijinsia kwenye Maeneo yenye Migogoro (“End Sexual Violence in Conflict”) utakaofanyika mjini London, Uingereza kuanzia tarehe 10 hadi13 Juni, 2014.

Mwaliko huo unakuja kufuatia mchango mkubwa wa Tanzania katika kufanikisha kuwepo kwa Tamko la Umoja wa Mataifa linalohusu suala hilo (Declaration of Commitment to End Sexual Violence in Conflict).Vile vile itakumbukwa kuwa, Tanzania imekuwa mstari wa mbele katika kuchangia vikosi vya kulinda amani katika maeneo yenye migogoro Barani Afrika ambayo pia yana wahanga wengi wa udhalilishwaji wa kijinsia.

Pamoja na masuala mengine, Mkutano huo utajadili hatua za kuchukua ili kumaliza tatizo la udhalilishaji wa kijinsia katika maeneo yenye migogoro; mchango au nafasi ya vijana katika kupambana na udhalilishaji wa kijinsia katika maeneo yenye migogoro; kiwango cha udhalilishaji wa kijinsia unatokea katika maeneo yenye migogoro na kuweka makubaliano ya kimataifa ya namna ya kutekeleza  mikakati iliyomo katika maazimio ya G8 na Umoja wa Mataifa; na kusikia matatizo na athari za udhalilishaji wa kijinsia katika migogoro moja kwa moja kutoka kwa Wahanga. 

Pia washiriki watajadili changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na udhaifu unaotokana na kutoadhibiwa kwa wanaofanya vitendo hivyo.
Mkutano huo utazikutanisha nchi zilizoathiriwa na migogoro, nchi wahisani, Umoja wa Mataifa, Asasi zisizo za Kiserikali, Mashirika ya Kimataifa na Taasisi za Kijamii na wadau wengine.

Aidha, wakati wa ziara hiyo, Mhe. Membe atakutana kwa mazungumzo na Waziri wa Uingereza anayeshughulikia masuala ya Afrika, Mhe. Mark Simmonds. Miongoni mwa masuala watakayozungumza ni kuimarisha ushirikiano baina ya Tanzania na Uingereza.

IMETOLEWA NA: WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA, DAR ES SALAAM
10 JUNI, 2014

M-PESA YAENDELEA KURAHISISHA HUDUMA KWA WATANZANIA

$
0
0
Dar es Salaam,Tanzania Juni 10, 2014 , Tangu kuanzishwa kwake mwaka 2008, huduma ya M pesa imendelea kuwa huduma yenye mafanikio zaidi katika utoaji wa huduma za kifedha huku ikiwanufaisha watanzania ambao wanauwezo wa kutuma na kupokea pesa kupitia mawakala zaidi ya 70,000, walioenea nchini kote.

Akizungumzia mafanikio ya huduma hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Rene Meza amesema kuwa tangu kuanzishwa kwake, huduma hiyo imeleta mapinduzi makubwa katika sekta ya huduma za fedha kwa njia ya mtandao kwa watumiaji wa huduma za simu za mkononi zaidi ya Milioni 27 ambao wamekuwa wamkuwa wanufaika wkaubwa bila kujali mipaka ya mtanado.

"Huduma hii ya M pesa imekuwa na mafanikio makubwa katika kubadili maisha ya Watanzania, na sio tu katika kutuma na kupokea pesa bali imekuwa na mchango mkubwa katika kukuza uchumi wa nchi yetu kutokana na kuwaweka mamilioni ya Watanzania katika mzunguko wa huduma za kifedha" alisema Meza. Meza aliongeza kuwa huduma hiyo imewezeshwa na ubunifu wa kipekee ambao muda wote imewawezesha watanzania kufurahia kutuma na kupokea pesa kupitia mitandao yote huku mawakala zaidi ya 70,000 wakiwa msaada mkubwa kwa wananchi hao kuweza kutimiza miamala yao kwa urahisi, uhakika na usalama zaidi mahala popote wakati wowote.

"Mafanikio ambayo tumeyapata tangu kuanzishwa kwa huduma hii mwaka 2008 ni namna ambavyo tumewawezesha watanzania kutuma na kupokea pesa katika mitandao yote nchini kupitia mawakala zaidi ya elfu 70000, walioenea nchi nzima, alisema Meza na Kuongeza, "Tuko katika mazungumzo na watoa huduma wengine wa fedha kupitia njia ya mitandao kuangalia namna ambavyo tunaweza kuboresha huduma hii zaidi" Aidha, Meza aliongeza kuwa utofauti wa huduma ya M pesa na huduma nyingine ni kuwa M-pesa imewezesha kwa kiasi kikubwa kuunganisha mifumo ya malipo ya biashara mbalimbali.

"Tuko katika ushirikiano na mabenki zaidi ya 26 nchini ambayo yameunganishwa na huduma yetu, na kuwawezesha wateja kutoa pesa au kuweka moja kwa moja kwenye akaunti zao, hii ni mbali na baihsra nyengine zaidi ya 300 ambazo zimatumia huduma ya M-pesa pamoja na idadi kubwa ya mawakala zaidi ya elfu 70000 ambao pia wanatoa huduma kwa Watanzania." Alisema.

Mkurungezi Mtendaji huyo alisema kuwa taarifa zinaonesha kuwa utumiaji mkubwa wa huduma ya M pesa ni kuweka na kutoa Pesa katika kuendesha shughuli za maisha za kila siku hivyo Vodacom itaendelea kuwawezesha Watanzania kutuma na kupokea pesa kupitia mitandao yote nchini ili kufikia malengo ya kurahisisha huduma za kifedha kwa Watanzania wote pale wanapohitaji na popote walipo nchini.

Meza alisema kuwa zaidi ya Shilingi Trilioni 1.5, zimekuwa zikishuhudiwa kila mwezi kupitia Miamala mbalimbali inayofanywa na wateja wa huduma ya M pesa, huku ikiwa inachangia zaidi ya asilimia 35 ya pato la taifa.

"Sisi kama Vodacom tunajivunia kuwa sehemu ya mafanikio haya makubwa katika utoaji wa huduma za kifedha na kuongeza upatikanaji wa ajira kwa Watanzania." Alihitimisha Mkurugenzi huyo.

MAMA SALMA KIKWETE AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA HOSPITALI YA WATOTO HUKO ZINGA BAGAMOYO

$
0
0
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA, Mama Salma Kikwete akisalimiana na Rais wa Shirika la International Health Partiners (IHP)-JEMA Tanzania, Mama Mary Ellen Kitundu mara baada ya kuwasili katika kijiji cha Zinga huko Bagamoyo, mkoani Pwani. Mama Salma alikwenda kijijini hapo kwa ajili ya kuweka jiwe la msingi la hospitali ya watoto inayojengwa na Shirika la IHP-JEMA Tanzania tarehe 10.6.2014. Katikati ni Mkurugenzi wa Mradi huo Dkt. Jesse Kitundu.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akifuatana na Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Ndugu Ahmed Kipozi wakitembelea eneo linalojengwa hospitali ya watoto itakayo kuwa na uwezo wa vitanda 500 katika kijiji cha Zinga huko Bagamoyo tarehe 10.6.2014.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akizungumza na wageni waalikwa na wananchi wa Kijiji cha Zinga wakati wa sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi la hospitali ya watotot itakayokuwa na uwezo wa vitanda 500 tarehe 10.6.2014.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akifungua kitambaa kuashiria uwekaji rasmi wa jiwe la msingi la ujenzi wa hospitali ya watoto katika Kijiji cha Zinga huko wilayani Bagamoyo tarehe 10.6.2014. Kushoto kwa Mama Salma ni Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Ndugu Ahmed Kipozi.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipanda mti kwenye eneo linalojengwa hospitali ya watoto katika kijiji cha Zinga wilayanI Bagamoyo mara baada ya kuweka jiwe la msingi tarehe10.6.2014.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa serikali, shirika la IHP-JEMA Tanzania na viongozi wa Kijiji cha Zinga mara baada ya sherehe ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa hospitali ya watoto kijijini hapo tarehe 10.6.2014. PICHA NA JOHN LUKUWI.

Watanzania Watakiwa Kuchangamka Fursa za Biashara, DITF

$
0
0
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania, TANTRADE Bibi Jaqueline Mneney Maleko akizungumza na waandishi wa habari (hawako pichani) kuhusu Maonyesho ya 38 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi wa Biashara ya Nje wa TANTRADE, Bibi. Anna Bulondo.

Umetolewa mwito kwa Watanzania kuzichangamkia fursa mbalimbali za kibiashara, zinazoletwa na Maonyesho ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam,  DITF ambapo Maonyesho ya huu, yatajumuisha makampuni zaidi ya kimataifa toka nchi yatashiriki.

Wito huo umetolewa na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania, TANTRADE, Bibi  Jaqueline Mneney Maleko wakati akizungumzia maandalizi ya Maonyesho ya 38  Kimataifa ya Dar es Salaam,  kwa waandishi wa Habari, ofisi za TANTRADE jijini Dar es Salaam jana.

Bibi Maleko amesema,  lengo kuu la Maonyesho ya Kimataifa ya Biashara, ni kufungua fursa za kibiashara, kama fursa za kutafuta wabia, fursa za kutafuta wawekezaji, na fursa za kuona bidhaa za viwango vya kimataifa ili  wazalishaji wa bidhaa za Tanzania kujitahidi kufikia viwango hivyo vya kimataifa badala  mtindo uliopo sasa kwa watu kujitokeza kwa wingi kuja, kununua tuu bidhaa..

Maonyesho ya mwaka huu, yatashirikisha  waonyeshaji bidhaa zaidi ya 1,200 kati yake Wizara, Idara na Wakala za serikali zaidi ya 60, na  makampuni zaidi ya 400 ya kimataifa yamethibitisha kushiriki.

Bibi Maleko amesema  hii ni fursa nzuri kwa Watanzania na Makampuni ya Kitanzania  kujitokeza kwa wingi na kuchangamkia fursa zinazoambatana na maonyesho ya kimataifa.

Kauli Mbiu  ya Maonyesho ya 38 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam ni  ni Kuunganisha Uzalishaji wa Bidhaa na Masoko, ili kutoa fursa kwa wazalishaji wa bidhaa za Tanzania,  kupata fursa za masoko ili bidhaa hizo ziweze kukidhi vigezo vya  kimataifa hivyo kuziwezesha kuingia kwenye masoko ya  kimataifa.

Bibi Maleko, ametoa wito kwa wafanyabiashara wa Tanzania na haswa wazalishaji bidhaa za Tanzania, ili kuweza kuingia kwenye ushindani wa masoko ya ndani nay a kimataifa, ni muhimu kwanza ukajua mahitaji ya soko, ndipo uzalishe bidhaa zitakazo kwenda sambamba na mahitaji na vigezo vya masoko.

Ameeleza kama kawaida kutakuwa na banda maalum la Tanzania lenye bidhaa za ndani zilizikidhi viwango vya kimataifa ili kuwahamasisha  Watanzania kupenda bidhaa za ndani kwa kupenda chako, jenga chako.

Pia maonyesho ya mwaka huu tayahusisha maonyresho ya biashara za bidhaa za ubunifu na vipaji, zikiwemo bidhaa za mavazi, sanaa za maonyesho na hata zanaa za muziki, hivyo kutakuwemo wanamuzi wataoonyesha bidhaa zao za muziki.

Bibi  Maleko ametoa wito kwa Watanzania wasio na ajira, kuzitumia fursa za maonyesho hayo ili waweze kujiajiri. TANTRADE itafanya kazi ya kuwajengea uwezo, wakiwemo watu wenye makundi maalum kama wanawake, vijana na watu wenye ulemavu, hivyo TANTRADE iko kwa ajili ya kuwashika mkono, kuwanjengea uwezo, kuwatafutia mitaji, uwezo na kuwatafutia masoko.


Bi Maloke aliwataka washiriki wote wa maonyesho hayo kufanya maandalizi mapema na kufikia tarehe 27 ya mwezi huu, mabanda yote lazima yawe yamemalizika, ili kukidhi viwango vya kimataifa vinavyosimamia  Taasisi ya Maonyesho ya Kimataifa ya UFI.

KUSITISHWA KWA MUDA HUDUMA YA TRENI YA ABIRIA KWENDA BARA

$
0
0
Uongozi wa Kampuni ya Reli Tanzania – TRL unawataarifu abiria wote na wananchi kwa jumla  kuwa kutokana na kutetereka kwa  daraja la reli kati ya stesheni ya Ruvu na mchepuko wa reli ya Ruvu kwenda Mruazi usiku wa kuamkia leo, umeamua kusitisha kwa muda huduma ya usafiri wa abiria hadi ukarabati wa  daraja utakapokamilika.

Tokea asubuhi ya leo Mkurugenzi Mtendaji wa TRL Mhandisi Kipallo Aman Kisamfu na Wahandisi waandamizi na Mafundi ujenzi walifika katika daraja hilo lililopo km 82/5 na kulifanyia tathmini kuwa linahitaji kuimarishwa  ili lirejee katika kiwango cha usalama kuruhusu treni za abiria kupita.

Kwa taarifa hii  wananchi na wateja wa TRL na wananchi kwa jumla  ambao walikuwa wasafiri kwenda bara kwa treni ya leo  Juni 10, 2014 wanatakiwa kufika katika stesheni zilizokaribu nao ili warejeshewe nauli zao ili watafute usafiri mbadala.
 Aidha Uongozi wa TRL unaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.


Imetolewa na Afisi ya Uhusiano kwa Niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa TRL Mhandisi Kipallo Aman Kisamfu
Dar es Salaam
Juni 10, 2014

NETHERLANDS, US ACCREDIT ENVOYS TO EAC

$
0
0
The Ambassadors of Netherlands and United States of America to the United Republic of Tanzania, their Excellences Ambassadors Jaap Frederiks and Mark Bradley Childress today presented their accreditation letters to the Secretary General, Amb. Dr. Richard Sezibera appointing them as their country’s Representatives to the EAC bloc.

The Netherlands Ambassador Jaap Frederiks was the first to present his letter of accreditation. The NNetherlands envoy lauded the progress registered by the Community and said it was important for his country to continue to build a stronger relationship with the regional bloc.

He said Netherlands was already enjoying strong relationships with individual EAC Partner States. Amb. Sezibera warmly welcomed the Netherlands Ambassador and briefed him on the progress being registered by the Community so far that include the coming into force of Protocols on the Customs Union, Common Market and the signing of the Protocol on the establishment of the East African Monetary.

He also informed the Ambassador about the achievement of the Single Customs Territory as the one of the key regional integration priority policy interventions to consolidate the EAC Customs Union.

The United States of America Ambassador to the United Republic of Tanzania H. E Mr. Mark Bradley Childress was the second to present his accreditation letter to the EAC Secretary General. He hailed the existing cordial relations between the US and the EAC.

Ambassador Mark Bradley Childress assured the EAC of the continued support to the EAC regional initiatives and cooperation. “l believe that regional integration is important for the growth of African economies’’, affirmed the Ambassador.

The Secretary General Amb. Sezibera informed the US envoy that EAC was interested in the increasing more investment in Air transport sector as well as the Fisheries industry in the region and would like to see increased US support in those areas.

Amb Sezibera embraced President Obama’s initiative towards Power Africa and stated that he would like to see EAC join the initiative as a regional bloc.
Amb. Dr Richard Sezibera stressing a point during the discussion with Amb Jaap Frederiks.
S Amb Mr. Mark Bradley Childress receives a gifts from EAC Secretary General Amb. Dr Richard Sezibera
EAC Secretary General Amb. Dr Richard Sezibera open letter of accreditation from Netherlands Ambassador to the United Republic of Tanzania HE Ambassador Mr Jaap Frederiks

NEWS ALERT: historia yawekwa Mbeye leo kwa uzinduzi wa lifti ya kwanza jijini humo

$
0
0
Bango la Uzinduzi wa lifti ya kwanza jijini Mbeya.
Sherehe za uzinduzi rasmi wa lifti ya kwanza Jijini Mbeya ukifanyika huku shamra shamra zikiendelea.
 Wadau wakipanda na kushuka kwenye lifti hiyo ikiwa ni sehemu ya kusherehekea uzinduzi wake.
Baada ya uzinduzi  - hodiiii......

RUFANI YA MICHAEL WAMBURA KUGOMBEA URAIS SIMBA SC

$
0
0
Uamuzi kuhusu rufani ya Michael Wambura kupinga kuenguliwa kugombea urais wa Rais utatangazwa kesho (Juni 11 mwaka huu) saa 6 kamili mchana na Mwenyekiti wa Kamati ya Rufani ya Uchaguzi ya TFF, Wakili Julius Lugaziya.

ziara mafunzo ya wanachuo na wanafunzi wa shule za msingi bungeni dodoma leo

$
0
0
 Mbunge wa viti maalum,  Mhe.Susan Kiwanga akiwapa maelezo wanachuo kutoka chuo cha Uuguzi  cha Edgar Maranta Ifakara ambao wapo katika ziara ya kimafunzo Bunge.
 Mbunge wa Chalinze Mhe.Ridhiwani Kikwete akizungumza na Wanafunzi kutoka Mvomero ambao wapo katika ziara ya kimafunzo katika kujionea shjughuli za Bunge.
 Mhe.Ridhiwani Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na na Wanafunzi kutoka Mvomero katika viwanja vya Bunge.
 Mbunge wa Mvomero Mhe Amos Makala ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maji (katikati mbele) akiwatembeza wanafunzi kutoka jimboni mwake ambao wametembelea  Bunge katika ziara ya ziara ya kimafunzo.
 Wanafunzi kutoka Shule ya Saba Saba Iringa Wakiwa katika picha ya pamoja na Waziri Ofisi ya Rais Asiye na Wizara Maalum amahe Prof.Marck Mwandosya ( Mstari wa NyumaKatikati) mbele ya Ukumbi wa Bunge.

.

 -Wanafunzi kutoka Shule ya M/Singi St.Theresia ya Mbezi Dar es  Salaam ambao wapoi katika ziara ya kimafunzo wakiwa katika picha ya pamoja mbele ya jingo nla bunge Dodoma
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Chem-Chemu Iliyopo Ndachi, Nkuhungu Dodoma wakiwa wamekaa wakijisomea vipeperushi  yenye kuonesha taratibu na shughuli za bunge kila siku,wakati wakisubiri usafiri mara baada ya bunge kuahirishwa. Na Deusdedit Moshi Mtendaji Mkuu wa Photo Solutions wawakilishi wa Mchuzi Blog Kanda ya Kati.  

OPERATIONALIZATION OF EAC CLUBS IN SECONDARY SCHOOLS IN THE OFFING ..As pilot Phase set to embark in Burundi

$
0
0

cid:image001.png@01CF8327.2B937140
East African Community

East African Community Secretariat, Arusha 10 June 2014: A Regional Workshop on establishment and operationalization of EAC Clubs in Secondary Schools in the region kicked off today at Hotel le Chandelier in Bujumbura, Burundi. 
The regional workshop facilitated by EAC Secretariat in collaboration with GIZ, brought together students and teachers from various Secondary Schools in Burundi as well as representatives from the Education Ministries within the EAC Partner States and stakeholders in the education sector.
 In her opening remarks, Minister to the Office of the President Responsible for EAC Affairs from the Republic of Burundi, Hon. Leontine Nzeyimana emphasized "the need to ensure that the Youth within the EAC are well equipped with the necessary tools and skills to actively participate in the regional integration process and therefore contribute to the overall development of the region." 
She highlighted that Article 120 (c) of the Treaty for establishment of the East African Community provides for adoption of a common approach for involvement of the youth in the integration process through education, training and mainstreaming youth issues into the EAC policies, projects and programs for strategic interventions. 
The three-day workshop's overall objective is to sensitize and raise awareness among East African Youth especially at the Secondary School level, to understand and own the stakes and opportunities of the EAC integration.
Speaking  on behalf of the EAC Secretariat, the Principal Education Officer, Mr. Aloysius Chebet underscored the importance of youth involvement and active participation of the youth towards building a stronger and solid foundation for the current people-centred EAC integration process, since they are the majority and most crucial part of the EAC citizenry.  
Various presentations were incorporated in the workshop such as the Status of EAC Regional Integration specifically within the Education sector, the Role of the Youth in the EAC integration and the opportunities, how the EAC Clubs are structured and functioning and challenges experienced so far within the Secondary Schools where EAC Clubs have already been established. 
Some of the expected outcomes of this project include; familiarizing the youth with the benefits and opportunities of the EAC integration process; sensitizing them about different projects and programmes in different sectors that generate economic growth; and establishment of EAC Clubs in Secondary Schools in the other four Partner States.

Introducing "LINAH" by E.M.A THE BOY

Shirika la Nyumba NHC leo limesaini mkataba wa ujenzi wa nyumba 5,000 na Halmashauri ya Wilaya Mpya ya Busokelo

$
0
0
Shirika la Nyumba la Taifa (NHC)  leo limesaini mkataba na Halmashauri ya Wilaya Mpya ya Busokela iliyopo Mkoani Mbeya ya Ujenzi wa Nyumba 5,000 za gharama nafuu.
Utiaji saini makubaliano hayo umefanyika leo mchana katika Hoteli ya New Dodoma mjini Dodoma na kuhudhuriwa na Wabunge wanaotoka Mkoa wa Mbeya wakiongozwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Kazi Maalum)  Mhe.Prof Mark Mwandosya, ambaye Wilaya hiyo Mpya iko katika Jimbo lake la Rungwe Mashariki,  na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa,(TAMISEMI) Mhe.Aggrey Mwanri.
 Pichani wanaosaini kuanzia kulia ni kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHC,Bwa.Felix Maagi,Bw.Meckson Mwakipunga (M/Kiti wa Halmashauri  ya Wilaya Mpya ya Busokela iliyopo Mkoani Mbeya na Bw. Said Mderu.
 Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHC,Bwa.Felix Maagi akibadilishana Mkataba  na M/Kiti wa Halmashauri  ya Wilaya Mpya ya Busokela Bw.Meckson Mwakipunga  baada ya kutiliana  saini Ujenzi wa nyumba 5,000 katika Wilaya Mpya ya Busokela iliyopo Mkoani Mbeya .
 Mwenyekiti wa Halmashauri  ya Wilaya Mpya ya Busokela Bw.Meckson Mwakipunga akielezea kuhusu Mradi mzima,  baada ya kutiliana  saini Ujenzi wa nyumba 5,000 katika Wilaya Mpya ya Busokela iliyopo Mkoani Mbeya .
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Kazi Maalum) Mhe.Prof Mark Mwandosya. Waziri ambaye Wilaya hiyo Mpya iko katika Jimbo lake la Rungwe Mashariki akitoa shukurani baada ya mkataba  wa Ujenzi wa Nyumba 5,000 za gharama nafuu kusainiwa.
Baadhi ya Wabunge wanaotoka Mkoa wa Mbeya wakifuatilia  utiaji saini wa Mkataba wa Ujenzi wa nyumba 5,000 za gharama nafuu katika Halmashauri ya Wilaya Mpya ya Busokela iliyopo Mkoani Mbeya .Na Deusdedit Moshi Mtendaji Mkuu wa Photo Solutions wawakilishi wa Michuzi Blog Kanda ya Kati

Watanzania Watakiwa Kuchangamka Fursa za Biashar kwenye Maonyesho ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam DITF

$
0
0
Umetolewa mwito kwa Watanzania kuzichangamkia fursa mbalimbali za kibiashara, zinazoletwa na Maonyesho ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam,  DITF ambapo Maonyesho ya huu, yatajumuisha makampuni zaidi ya kimataifa toka nchi yatashiriki. 
Wito huo umetolewa na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania, TANTRADE, Bibi  Jaqueline Mneney Maleko wakati akizungumzia maandalizi ya Maonyesho ya 38  Kimataifa ya Dar es Salaam,  kwa waandishi wa Habari, ofisi za TANTRADE jijini Dar es Salaam leo. 
Bibi Maleko amesema,  lengo kuu la Maonyesho ya Kimataifa ya Biashara, ni kufungua fursa za kibiashara, kama fursa za kutafuta wabia, fursa za kutafuta wawekezaji, na fursa za kuona bidhaa za viwango vya kimataifa ili  wazalishaji wa bidhaa za Tanzania kujitahidi kufikia viwango hivyo vya kimataifa badala  mtindo uliopo sasa kwa watu kujitokeza kwa wingi kuja, kununua tuu bidhaa. 
Maonyesho ya mwaka huu, yatashirikisha  waonyeshaji bidhaa zaidi ya 1,200 kati yake Wizara, Idara na Wakala za serikali zaidi ya 60, na  makampuni zaidi ya 400 ya kimataifa yamethibitisha kushiriki.
 Bibi Maleko amesema  hii ni fursa nzuri kwa Watanzania na Makampuni ya Kitanzania  kujitokeza kwa wingi na kuchangamkia fursa zinazoambatana na maonyesho ya kimataifa. 
Kauli Mbiu  ya Maonyesho ya 38 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam ni  ni Kuunganisha Uzalishaji wa Bidhaa na Masoko, ili kutoa fursa kwa wazalishaji wa bidhaa za Tanzania,  kupata fursa za masoko ili bidhaa hizo ziweze kukidhi vigezo vya  kimataifa hivyo kuziwezesha kuingia kwenye masoko ya  kimataifa. 
Bibi Maleko, ametoa wito kwa wafanyabiashara wa Tanzania na haswa wazalishaji bidhaa za Tanzania, ili kuweza kuingia kwenye ushindani wa masoko ya ndani nay a kimataifa, ni muhimu kwanza ukajua mahitaji ya soko, ndipo uzalishe bidhaa zitakazo kwenda sambamba na mahitaji na vigezo vya masoko. 
Ameeleza kama kawaida kutakuwa na banda maalum la Tanzania lenye bidhaa za ndani zilizikidhi viwango vya kimataifa ili kuwahamasisha  Watanzania kupenda bidhaa za ndani kwa kupenda chako, jenga chako.
 Pia maonyesho ya mwaka huu tayahusisha maonyresho ya biashara za bidhaa za ubunifu na vipaji, zikiwemo bidhaa za mavazi, sanaa za maonyesho na hata zanaa za muziki, hivyo kutakuwemo wanamuzi wataoonyesha bidhaa zao za muziki. 
Bibi  Maleko ametoa wito kwa Watanzania wasio na ajira, kuzitumia fursa za maonyesho hayo ili waweze kujiajiri. TANTRADE itafanya kazi ya kuwajengea uwezo, wakiwemo watu wenye makundi maalum kama wanawake, vijana na watu wenye ulemavu, hivyo TANTRADE iko kwa ajili ya kuwashika mkono, kuwanjengea uwezo, kuwatafutia mitaji, uwezo na kuwatafutia masoko. 
Bi Maloke aliwataka washiriki wote wa maonyesho hayo kufanya maandalizi mapema na kufikia tarehe 27 ya mwezi huu, mabanda yote lazima yawe yamemalizika, ili kukidhi viwango vya kimataifa vinavyosimamia  Taasisi ya Maonyesho ya Kimataifa ya UFI. End.
 Kulia ni Mkurugenzi wa Biashara ya Nje wa TANTRADE, Bibi. Anna Bulondo. akiongea
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara  Tanzania, TANTRADE  Bibi Jaqueline Mneney Maleko akizungumza na waandishi wa habari (hawako pichani) kuhusu Maonyesho ya 38 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi wa Biashara ya Nje wa TANTRADE, Bibi. Anna Bulondo. 

MWENYEKITI WA JUMUIYA YA WAZAZI ABDALLAH BULEMBO AWAAPISHA WANACHAMA 367 WAPYA WA CCM WILAYA YA NYASA MKOANI RUVUMA

$
0
0
 Mwenyekiti  wa Jumuiya ya wazazi ya Chama Cha mapinduzi CCM (Taifa) Bw. Abdallah  Bulembo aliyevaa taji shingoni akicheza ngoma ya asili katika kijiji cha Kingirikiti Wilaya ya Nyasa wakati wa Ziara yake 

 Kikundi cha akina mama  kikitoa burudani

 Mwenyekiti  wa Jumuiya ya wazazi ya Chama Cha mapinduzi CCM (Taifa) Bw. Abdallah  Bulembo akitoa kadi kwa mwanachama mpya wa CCM kata ya LUMEME kijiji cha KINGIRIKITI wilaya ya Nyasa, kwa wanachama 367 waliojiunga na chama hicho cha CCM
 Mwenyekiti  wa Jumuiya ya wazazi ya Chama Cha mapinduzi CCM (Taifa) Bw. Abdallah  Bulembo akiwaapisha wanachama wapya wa  CCM
Wananchama wapya wa CCM wakiwa wamenyoosha kadi za Chama Cha Mapinduzi juu wakati wakiapa
Mwenyekiti  wa Jumuiya ya wazazi ya Chama Cha mapinduzi CCM (Taifa) Bw. Abdallah  Bulembo akizungumza katika mkutano wa hadhara baada ya kuwaapisha wanachama wapya kijiji cha KINGIRIKITI kata ya LUMEME wilayani NYASA , Picha na kikosi cha Demashonews

KUMBUKUMBU

$
0
0
Ni Miaka mitatu sasa imekatika toka ulipoitwa na Mwenyezi Mungu kwenye Makazi ya Milele,Mama yetu Mpendwa Clara Abraham Mandara.

Unakumbukwa sana na Watoto wako na Wajukuu wako wote.Tunakuombea kwa Baba Muumba akusamehe Makosa yako yote na aiweke roho yako mahala pema Peponi.

-Amin.
Viewing all 110185 articles
Browse latest View live




Latest Images