Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live

Msaada wa Matibabu kwa Mtoto Maimuna Yahaya (11)

$
0
0
 
 Pichani ni Mtoto Maimuna Yahaya
 Mtoto Maimuna Yahaya akiwa na Mama yake Mzazi  Tunu Juma
 **********************

Msaada wa Matibabu kwa mtoto Maimuna Yahaya Mtoto Maimuna Yahaya (11) anayesoma shule ya Msingi ya watoto wenye mahitaji maalum (wenye ulemavu) ya Irente Rainbow (Lushoto- Tanga) Darasa la pili, anasumbuliwa na tatizo la mifupa na ukubwa wa kichwa tangu kuzaliwa kwake, tatizo lililompelekea kuwa na ulemavu wa viungo na mtindio wa Ubongo.
Mama wa mtoto huyo, Bi. Tunu Juma Maziku amesema amekuwa akimpeleka mwanae huyo Maimuna katika hospitali ya KCMC kwa muda wa miaka 11. Hali ya mtoto inaendelea kuimarika, anaweza kukaa na anaweza kuongea.
Bi. Tunu amekuwa akimpeleka mwanae huyu shule na kumsubiri hadi wamalizapo masomo ya siku na kumrejesha nyumbani kwa muda wa miaka miwili. Bi. Tunu Juma Maziku  anasema kwa sasa hali yake ya kiuchumi si nzuri, anashindwa kumpeleka mwanae kuhudhuria matibabu KCMC, hivyo anaomba msaada wa kifedha kwa wasamalia wema ili mtoto wake aendelee na matibabu.   Mahali wanapopatikana: Lushoto Mabwawani 




Mawasiliano: Namba ya simu ya mama mzazi: +255712504768 Namba ya Tigo Pesa mesajiliwa kwa Jina la Maimuna Yahaya +255655779345 na Namba ya Airtel Money ni 0787204160 imesajiliwa kwa jina la Tunu Juma.
 

KIBONZO CHA NATHAN MPANGALA LEO

ZAIDI YA WAATHIRIKA 50 WA MAFURIKO WAPATIWA MSAADA WA CHAKULA KIJIJI CHA THEMI YA SIMBA ARUSHA

$
0
0

Mzee wa kanisa la Waadventista wasabato  mtaa wa kijenge   Agrey Tumaini akigawa mahindi kwa wananchi wa kitongoji cha kitongoji  cha Nyamagana  kilichopo katika kijiji cha Themi ya simba wilayani Arumeru MKoani Arusha (picha na woinde shizza,Arusha

=========  ======  ======
Na Woinde shizza,Arusha

Zaidi ya wananchi  50  wa kitongoji  cha Nyamagana  kilichopo katika kijiji cha Themi ya simba wilayani Arumeru MKoani Arusha ambao waliathiriwa na mafuriko yaliotokea mwisho mwa mwezi wa nne mwaka huu wamepatiwa msaada wa chakula na nguo kijijini hapa.

 Akikabidhi chakula hicho mzee wa kanisa la Waadventista wasabato  mtaa wa kijenge   Agrey Tumaini alisema kuwa wameamua kuwasaidia wananchi hawa kutokana na janga ambalo liliwakuta la kuingiliwa na mafuriko ya maji  ambapo yaliwasababishia nyumba pamoja na mazao yao kuezuliwa na maji hayo

Alisema kuwa wao kama kikundi cha WAMO  kutoka katika kanisa hilo waliguswa sana na tatizo hili ambalo liliwatokea hivyo wakaamua kujichanga na kununua vyakula ivyo na nguo kwa ajili ya wahanga hao wa mafuriko.
Alisema kuwa wameweza kutoa gunia kumi za mahindi ,maharage kunia tatu,unga wa ugali pamoja na nguo kwa ajili ya watoto  wa wananchi ambao walikubwa na janga hilila mafuriko.
“sisi tumeguswa sana na tukio hili wenzetu kukubwa na  mafuriko kwa kweli wameadhirika vikubwa kwani wengine awana sehemu zakukaa wengine walikuwa wamelima mazao yao kama mahindi yaliezuliwa na mafuriko hayo yaani kiukweli hadi sasa kuna watu awajui wataishije kwa mwaka huu lakini tumeona sio vibaya iwapo tukiwasaidia ichi kidogo  tulichonacho maana ata neno la mungu linasema  katika mathayo uwa mlikuja na njaa nikawapa chakula,mlikuja uchi nikawavisha sasa na sisi tumeamua kuwapa ichi kidogona tunawaomba watu wengine waendelee kujitokeza kwa wingi kuwasaidia wananchi hawa kwani wapo katika mazingira magumu sana”alisema Tumaini.

Akipokwa msaada huo mmoja wa wananchi hao alietambulika kwa jina la  Gidion Maganga alisema kuwa anashukuru sana kanisa hili la wa sabato kwa kuja kuwasaidia kwani kuna baadhi yao walikuwa hawajui hatima ya maisha yao kwani ata chakula kwao kupata ni tabu .

Alisema kuwa pamoja kuwa kuna baadhi yaviongozi na taasisi ambazo zimewapelekea chakula kama maindi ,magodoro  pamoja na nguo lakini bado wanaitaji maada kwani mvua zile ziliwachukulia vitu vyao vingi ikiwemo mazao maindi waliokuwa wameyaifadhi ndani vyombo ,magodoro na sio ivyo tu lakini pia zileweza kumuua mwananchi mmoja.

Akizungumzia tukio hilo mwananchi mungine ambaye aliyejitaja kwa jina la Zainabu Minja alisema kuwa siku hiyo ya tukio lilitokea majira ya saa saba usiku wakati wamelala  huku mvua ikinyesha ndipo gafla waliona maji mengi yamekuja na kujaa ndani  ya nyumba  kitu ambacho kiliwaogopesha zaidi ni pa le maji yale yalivyoanza kusomba vitu.

“yaani ndugu muandishi usione apa yaani maji yalikuja na kasi unaona hii chuma ina uzitowa kilomia ndio niliichukuwa nikaishika na uyu ni mama yangu na unamuona alivyo mzee nilimwambia ashikilie iyo chuma akashika mwishowe mikono ikafa ganzi ndipo nikachukua kanga na kumfunga kiunoni nikaunganisha na chuma ili asipelekwe na maji ila nashukuru mungu alituona pamoja vitu vilizolewa lakini sisi ni wazima kwakweli”alisema bi Zainabu.
Alitoa wito kwa wananchi serekali pamoja na taasisi mbalimbali kujitokeza kwa wingi kuwasiaidia kwani wapo katika halingumu sana  katika kipindi hichi.

BALOZI MPYA WA MAREKANI AJITAMBULISHA KWA MAKAMU WA RAIS,DKT. BILAL LEO

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib, akimkaribisha Balozi mpya wa Marekani nchini Tanzani, Mark Childres, wakati alipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Juni 9, 2014 kwa mazungumzo na utambulisho wa balozi huyo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika mazungumzo na Balozi mpya wa Marekani nchini Tanzania, Mark Childres, wakati alipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Juni 9, 2014 kwa mazungumzo na utambulisho wa balozi huyo. Picha na OMR.

WAZIRI WA KILIMO CHAKULA NA USHIRIKA, MHE. CHIZA NA BALOZI WA UINGEREZA NCHINI, MS. DIANNA MELROSE

$
0
0
Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika, Eng. Christopher Chiza akifanya mazungumzo na Balozi wa Uingereza nchini, Bibi Dianna Melrose. Balozi huyo alimtembleza Waziri Chiza ofisini kwake kwa lengo la kuimarisha mahusiano kati ya nchi hizo mbili yenye lengo la kukuza Sekta ya Kilimohususan kwenye eneo la uwekezaji katika mashamba makubwa(Picha na Issa Sabuni, WKCU).

WABUNGE WA TANZANIA WANAOWAKILISHA BUNGE LA AFRIKA MASHARIKI (EALA) NA SAKATA LA KUTAKA KUMVUA MADARAKA SPIKA WA BUNGE HILO

$
0
0

Mwenyekiti wa Wabunge wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EALA) wa Tanzania, Adam Kimbisa, akifafanua jambo wakati wa mkutano na  waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, kuhusu sakata la kutaka kumvua madaraka Spika wa Bunge hilo. Kulia ni mbunge wa bunge hilo, Twaha Taslima na Katibu wa Wabunge wa EALA, Shy-Rose  Bhanji.

Katibu wa Wabunge wa EALA, Shy-Rose  Bhanji akifafanua jambo wakati wa mkutano na  waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, kuhusu sakata la kutaka kumvua madaraka Spika wa Bunge hilo. Kushoto ni Mwenyekiti wa Wabunge wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EALA) wa Tanzania, Adam Kimbisa na mbunge wa bunge hilo, Twaha Taslima.Mbunge wa bunge hilo, Twaha Taslima akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini dar es Salaam leo.Wabunge wa Jumiya ya AfrikaMashariki (EALA), wakitoka katika ukumbi wa Idara ya Habari jijini Dar es Salaam, baada ya mkutano wao na waandishi wa habari. Kutoka kulia ni Mwenyekiti wa Wabunge wa Jumuiya hiyo kutoka Tanzana, Adam Kimbisa, Katibu wa Wabunge wa EALA, Shy-Rose Bhanji (katikati) na mbunge wa bunge hilo Twaha Taslima.

BOFYA HAPA KUSOMA WARAKA WAO

African Caucus elects representatives for Permanent Indigenous Peoples’ Committee (PIPC) of the Forest Stewardship Council, in Tanzania

$
0
0
By Isaac Malugu

The Forest Stewardship Council (FSC) is an international, non-profit organization founded in 1993 by environmentalists, social interest groups, responsible retailers and leading forest companies to develop standards. These standards are based on the ‘10 principles for forest stewardship’, by which forests can be responsibly managed. They also make sure that environmental, social and economic needs are balanced, and that long-term and healthy forest management plans are put into practice. 
FSC certification is internationally recognized as having the most rigorous environmental and social standards which define responsible forest management. Its great strength lies in its ability to encourage communication between people with different interests, ideas and philosophies. Bringing together businesses, governments and communities provides a unique tool for dealing with the complex issues surrounding forestry. 

The FSC Permanent Indigenous Peoples’ Committee (PIPC), is one of the important committee for discussing and championing indigenous people issues. PIPC held its last meeting in Dar es Salaam from 3-4th June 2014. The meeting was hosted by FSC East Africa sub region office, led by Regional Coordinator; Paul Opanga in collaboration with Tanzanian FSC Standard Development Group under the chair of Isaac Malugu from WWF Tanzania, WWF is keenly supporting FSC initiatives in Tanzania and currently facilitating the development of national FSC Standards.

This event was held to make recommendations to the FSC Board that will strengthen and renew the engagement of Indigenous people in FSC.  At the beginning of 2014, Indigenous People from four (4) international regions; Canada, Latin America, Northern Europe-Russia, and Asia-Oceania, met and successfully nominated members to the committee. The African Caucus was the final for completing the circle and called together to provide guidance to the PIPC and nominate its representative(s) to the committee.

Adam Ole Mwarabu from Tanzania was unanimously elected to represent the Africa region. Adam comes from Indigenous Maasai communities of Tanzania. Edna Kaptoyo from Kenya was also elected as alternate from East Africa. The Batwa communities of Central and West Africa will be represented by Venant Messe from Cameroon and Louise Kavira from Republic of Congo.  

The revised Principle Three (3) of the FSC Principles and Criteria is the strongest ‘normative’ statement on Indigenous Rights concerning a natural resource sector amongst all certification systems globally.  With the formal adoption of the United Nations Declaration on the Rights of Indigenous People and Free Prior and Informed Consent gaining strength daily, engaging and informing the FSC system is critical as indigenous people advance for their rights and partnerships in relation to the forest and their traditional territories.

In closing the caucus, the PIPC Chairperson and Executive Director of National Aboriginal Association from Canada, said, “Envision a strong committee strengthening Indigenous Peoples’ FSC engagement around the world in partnership with, by, and for Indigenous Peoples in the forest on a permanent basis”.

The PIPC membership lasts for 10 years with two terms of 5 years. The next FSC General Assembly will be held in Spain and PIPC looks forward for active participation. 

madereva wa daladala jijini Mbeya wagoma kusafirisha abiria leo

$
0
0
Wakazi wa Jiji la Mbeya leo wamejikuta wakiwa katika mazingira magumu baada ya mgomo wa mabasi madogo wa kutopakia abiria kutoka stendi kuu jijini humo,wakitaka wabadilishiwe ruti au kuongezewa nauli kwa sababu ya ruti hiyo inawapa mzungunguko mkubwa sana kulinganisha na nauli wanayoichaji kwa abiria hao.hali hiyo imepelekea abiria mbali mbali wa jiji hilo kupanga kwenye pikup na kulipa nauli ile ile wanayolipa kwenye daladala kama ionekanavyo katika picha mbali mbali zilizopigwa na Mpiga picha wa Globu ya Jamii,jijini Mbeya, Fadhil Atick.
Abiria jijini Mbeya wakiwa ndani ya lori kuendelea na safari zao.
Hivi ndivyo hali ilivyokuwa jijini Mbeya mchana wa leo.
Wengine walikuwa wakigombea kwenye Bajaj.
Hali ilikuwa tete.

KAMPUNI YA MAFUTA NA GESI YA SWALA (TANZANIA) PLC INATANGAZA UZINDUZI WA IPO

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mafuta na Gesi ya Swala (Tanzania) PLC, David Mestres Ridge (kulia), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, kuhusu ufunguzi wa ofa ya awali kwa umma ijulikanayo kwa kifupi (IPO) ambayo itakuwa na hisa za kawaida,9,600,000. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa ARCH Financial $ Investment Adivisory Limited,Iyen Nsemwa.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Mafuta na Gesi ya Swala (Tanzania) PLC, Abdullah Mwinyi (katikati), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, kuhusu ufunguzi wa ofa ya awali kwa umma ijulikanayo kwa kifupi (IPO) ambayo itakuwa na hisa za kawaida,9,600,000. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Swala, David Mestres Ridge na Mkurugenzi Mkuu wa ARCH Financial $ Investment Adivisory Limited,Iyen Nsemwa. (Na Mpiga picha Wetu)

Kampuni ya Mafuta na Gesi ya Swala (Tanzania) Plc leo imetangaza ufunguzi wa ofa yake ya awali kwa umma ijulikanavyo kwa kifupi kama ("IPO") yenye hisa za kawaida 9,600,000. Kampuni itakuwa ikiuza kila hisa kwa bei ya shilingi za Kitanzania 500 kuanzia tarehe 9 juni 2014 mpaka tarehe 4 Julai 2014.

Tangazo hili limekuja wiki moja baada ya kampuni kupokea idhini yake rasmi kutoka Mamlaka ya masoko ya Mitaji na Dhamana Tanzania ("CMSA"), na kuifanya kuwa ni ofa ya kwanza kufanyika kwenye sekta ya mafuta na gesi katika ukanda wa Afrika Mashariki.

Mkurugenzi Mtendaji wa Swala Bwana David Mestres Ridge alisema, "Tunafuraha kuwa, leo Kampuni ya mafuta na gesi ya Swala (Tanzania) Plc imezindua rasmi mpango wake wa ofa ya awali kwa umma ijulikanayo kama IPO. Hii ni hatua kubwa si tu kwa ajili ya Swala lakini pia kwa Tanzania na watu wake kwa ujumla. . Kuwekeza hisa katika mafuta na gesi ni moja ya njia za kupanua wigo wa kiuchumi kwa mtu yeyote na inaruhusu mtu yeyote kumiliki hisa katika biashara hii inayokua kwa kasi ".

Bwana Ridge alizidi kusema, "Tunaishukuru sana Serikali ya Tanzania, Shirika la mafuta na gesi Tanzania (TPDC), Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) kwa kuturuhusu kuwa kampuni ya kwanza ya Mafuta na gesi katika Afrika Mashariki inayomilikiwa na umma. Kwa niaba ya wakurugenzi wote wa Swala napenda kuukaribisha rasmi umma kuwekeza katika Kampuni ya mafuta na gesi ya Swala (Tanzania) Plc ".

Mhe. Abdullah Mwinyi, ambaye ni Mkurugenzi wa Swala Tanzania Plc aliongeza, "Kumekuwa na mjadala mkubwa kwa wazawa katika sekta hii ya uchimbaji wa mafuta na gesi; Tumefurahia kwamba leo kampuni ya mafuta na gesi ya Swala imekuwa ya kwanza kuanza utekelezaji wa haja za wazawa katika sekta hii ya mafuta na gesi. Tunaamini kwa dhati kabisa kwamba Watanzania wapewe nafasi ya kushiriki katika biashara ya mafuta na gesi; ufunguzi huu wa IPO unaruhusu wao kufanya hivyo."

Fomu za maombi na nakala ya Waraka wa matarajio zitakuwa zinapatikana katika ofisi zote za Mawakala wenye leseni kutoka soko la hisa la Dar Es Salaam (DSE) walioko karibu yako, matawi ya Benki ya CRDB Plc na ofisi za Arch Financial & Investment Advisory Ltd.

Ofa iko wazi kuanzia tarehe 9 Juni 2014 mpaka 4 Julai 2014. Kwa sasa hakuna ukomo wa kiwango cha juu cha hisa, lakini kiwango cha chini cha kununua ni hisa 100 kwa mtu. Waraka wa Matarajio wa kielektronikia unapatikana kwenye tovuti ya kampuni www.swala-energy.co.tz au

Shule ya Sekondari ya WAMA-Nakayama wapewa msaada wa basi

$
0
0
Anna Nkinda – Maelezo

Shule ya Sekondari ya WAMA-Nakayama inayomilikiwa  na Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) imepatiwa msaada wa basi na kampuni ya Ashok Leyland ya jijini Dar es Salaam.

Makabidhiano ya basi hilo yamefanyika leo katika viwanja vya Taasisi hiyo iliyopo wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam.

Akiongea mara baada ya makabidhiano hayo   Mwenyekiti wa WAMA Mama Salma Kikwete aliwashukuru viongozi wa kampuni hiyo kwa msaada walioutoa na kusema anaamini msaada huo wameutoa baada ya kuangalia vigezo maalum na kuwaomba kuzidi kuwa na  moyo wa upendo kwao na kwa  wadau wengine.

Mama Kikwete ambaye pia ni Mke wa Rais Jakaya Mrisho Kikwete alisema Taasisi ya WAMA inafanya kazi mbalimbali zinazoonekana na jamii moja wapo ikiwa ni elimu na katika hilo wanashule ya Sekondari ya WAMA-Nakayama ambayo ni ya watoto yatima na wanaoishi katika mazingira hatarishi iliyoko wilaya ya Rufiji mkoani Pwani ambayo inawanafunzi 335 wa kidato cha kwanza hadi cha nne.

“Wenzetu hawa wametoa basi ambalo litasaidia kutatua changamoto ya usafiri shuleni  kwani wanafunzi kama wanafunzi wanashughuli zao za ndani na nje ya Shule. Kwa ukubwa wa basi hili tatizo la usafiri litakuwa limepungua kwa kiasi kikubwa kwakuwa  kabla ya kupata basi hili kulikuwa na lingine dogo”, alisema Mama Kikwete.

Kwa upande wake Bhimasena Rau ambaye ni Mkurugenzi Mwendeshaji Kimataifa kutoka kampuni ya Ashok Leyland alimpongeza Mama Kikwete kwa kazi kubwa anayoifanya ya kuisaidia jamii wakiwemo wanawake na watoto hapa nchini na kusema kuwa wametoa basi hilo ambalo litasaidia katika kazi za kijamii.

Taasisi ya WAMA ilianzishwa mwaka 2006 inafanya  kazi katika eneo la elimu ya mtoto wa kike, afya, kuwawezesha wanawake kiuchumi na kuangalia watoto yatima na wanaoishi katika mazingira hatarishi.

MKURUGENZI WA KIWANDA CHA MONABAN CHA JIJINI ARUSHA ASIMIKWA RASMI KUWA KAMANDA WA VIJANA UVCCM MKOA

$
0
0
003Makamu mwenyekiti UVCCM Taifa Mboni Mhita akimuapisha Mkurugenzi wa kiwanda cha kuzalisha unga kilichopo jijini Arusha Bw.Philemon Mollel kuwa kamanda wa vijana UVCCM Mkoa sherehe zilizofanyika juzi jijini Arusha na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa chama hicho
002Mkurugenzi wa kiwanda cha kuzalisha unga kilichopo jijini Arusha Bw.Philemon Mollel akiapa kuwa kamanda wa vijana UVCCM Mkoa sherehe zilizofanyika juzi jijini Arusha na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa chama hicho
001Mkurugenzi wa kiwanda cha kuzalisha unga kilichopo jijini Arusha Bw.Philemon Mollel akiwa ameshililia ngao mkuki ishara ya kusimikwa rasmi kuwa kamanda wa vijana UVCCM Mkoa sherehe zilizofanyika juzi jijini Arusha na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa chama hicho
004Hapa akiwa anavalishwa taji
005Makamu mwenyekiti UVCCM Taifa Mboni Mhita akiwa anaongea katika sherehe hizo za kusimikwa rasmi Mkurugenzi wa kiwanda cha kuzalisha unga kilichopo jijini Arusha Bw.Philemon Mollel kuwa kamanda wa vijana Mkoa.Picha na Pamela Mollel wa Jamiiblog

GLOBAL COMMUNITY DAY- 14TH JUNE 2014 DONATIONS

Mtoto Maimuna Yahaya anahitaji msaada wako

$
0
0
 Mtoto Maimuna Yahaya akiwa 
na Mama yake Mzazi  Tunu Juma. 
Msaada unahitajika kwa ajili ya matibabu ya mtoto Mtoto Maimuna Yahaya (11) anayesoma shule ya Msingi ya watoto wenye mahitaji maalum  ya Irente Rainbow (Lushoto- Tanga) Darasa la pili. Yeye anasumbuliwa na tatizo la mifupa na ukubwa wa kichwa tangu kuzaliwa kwake, tatizo lililompelekea kuwa na ulemavu wa viungo na mtindio wa Ubongo.

Mama wa mtoto huyo, Bi. Tunu Juma Maziku amesema amekuwa akimpeleka mwanae huyo Maimuna katika hospitali ya KCMC kwa muda wa miaka 11. Hali ya mtoto inaendelea kuimarika, anaweza kukaa na anaweza kuongea.

Bi. Tunu amekuwa akimpeleka mwanae huyu shule na kumsubiri hadi wamalizapo masomo ya siku na kumrejesha nyumbani kwa muda wa miaka miwili. Bi. Tunu Juma Maziku  anasema kwa sasa hali yake ya kiuchumi si nzuri, anashindwa kumpeleka mwanae kuhudhuria matibabu KCMC, hivyo anaomba msaada wa kifedha kwa wasamalia wema ili mtoto wake aendelee na matibabu.   Mahali wanapopatikana: Lushoto Mabwawani  

 Mawasiliano: Namba ya simu ya mama mzazi:+255712504768 Namba ya Tigo Pesa imesajiliwa kwa Jina la Maimuna Yahaya +255655779345 na Namba ya Airtel Money ni 0787204160 imesajiliwa kwa jina la Tunu Juma.

kili music tour yatikisa mji wa kahama

$
0
0
 Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya, Ay akiwapa burudani ya aina yake wakazi wa mji wa Kahama wakati wa Tamasha la Kilimanjaro Music Tour 2014 lililofanyika Uwanja wa Halmashauri ya Kahama, Jumamosi. Tamasha hili limedhaminiwa na Bia ya Kilimanjaro Premium Lager.
 Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya, MwanaFA akiwachezesha bila kukunja goti wakazi wa mji wa Kahama wakati wa Tamasha la Kilimanjaro Music Tour 2014 lililofanyika Uwanja wa Halmashauri ya Kahama, Jumamosi . Tamasha hili limedhaminiwa na Bia ya Kilimanjaro Premium Lager.
 Msanii wa muziki wa dansi, Christian Bella akitoa burudani kwa wakazi wa Kahama wakati wa tamasha la Kilimanjaro Music Tour 2014 lililofanyika Uwanja wa Halmashauri ya Kahama, Jumamosi. Tamasha hili limedhaminiwa na Bia ya Kilimanjaro Premium Lager.
 Wasanii wa Kundi la Jambo Squad toka Jijini Arusha wakiwapagawisha wakazi wa Kahama wakati wa tamasha la Kilimanjaro Music Tour 2014 lililofanyika Uwanja wa Halmashauri ya Kahama, Jumamosi. Tamasha hili limedhaminiwa na Bia ya Kilimanjaro Premium Lager.
Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

RAIS KIKWETE AUNGANA NA WAOMBOLEZAJI KWENYE MSIBA WA MAREHEMU MZEE SAID NGAMBA "MZEE SMALL" JIJINI DAR LEO

$
0
0
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili kwenye Msiba wa msiba wa msanii maarufu wa filamu ya vichekesho hapa nchini,Marehemu Saidi Ngamba “Mzee Small” nyumbani kwa marehemu Tabata Kimanga jijini Dar es salaam leo Juni 9, 2014.
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akishiriki katika dua wakati alipokwenda kuhani msiba wa msanii maarufu wa filamu vichekesho Marehemu Saidi Ngamba “Mzee Small” nyumbani kwa marehemu Tabata Kimanga jijini Dar es salaam leo Juni 9, 2014.
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakiwafariji wafiwa wakati walipokwenda kuhani msiba wa msanii maarufu wa filamu vichekesho Marehemu Saidi Ngamba “Mzee Small” nyumbani kwa marehemu Tabata Kimanga jijini Dar es salaam leo Juni 9, 2014
Mama Salma Kikwete akimpa pole mjane wa Marehemu Saidi Ngamba “Mzee Smal” wakati alipokwenda kuhani msiba wa msanii huyo maarufu wa filamu za vichekesho nyumbani kwa marehemu Tabata Kimanga jijini Dar es salaam leo Juni 9, 2014.
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiwa amejumuika na waombolezaji mbali mbali kwenye Msiba wa msanii maarufu wa filamu za vichekesho nyumbani kwa marehemu Tabata Kimanga jijini Dar es salaam leo Juni 9, 2014.Kusoto ni Rais wa Chama cha Filamu nchini,Simon Mwakifwamba na kulia ni Mtoto wa Marehemu Mzee Small,Mahmoud Said Ngamba.
Rais Kikwete akisaini Kitabu cha Maombolezo.
Dua zikiendelea kusomwa kumuombea Marehemu Said Ngamba "Mzee Small".


WATUHUMIWA WA MTOTO ALIYEKUFA KUTOKA KWENYE BOX KIZIMBANI MOROGORO

$
0
0
Difenda iliyobeba watuhumiwa wa kesi ya mtoto wa boksi, Hayati Nasra Rashid,  ikiwasili Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoani Morogoro. Watuhumiwa watatu akiwemo baba yake mzazi wa Nasra, Rashid Mvungi, mama mkubwa wa Nasra, Mariam Saidi na Mume wa mama Mariam Said walifikishwa katika mahakama ya hakimu mkazi Morogoro kujibu tuhuma za mashtaka ya kula njama na kumtesa Nasra Rashidi (4) wakati wa uhai wake. 
Baba mlezi wa mtoto Nasra, Mtonga Omari akishuka kwenye
gari la polisi kwa staili ya kuruka. 
Bi. Mariam Said ambaye ni mama mkubwa wa Nasra, akishuka kwenye gari hilo. 
Baadhi ya wananachi wakiwazomea watuhumiwa waliokuwa kwenye gari hilo baada ya kesi yao kuhairishwa hadi Juni 12 mwaka huu. 
Wananachi hao wakilifukuza gari lililobeba watuhumiwa waliorejeswa polisi kwa mahojiano mapya baada ya mtoto Nasra kufariki dunia.
Pichana  Dunstan Shekidele -GPL/Morogoro

ulinzi wa kufa mtu kombe la dunia brazil

$
0
0
Ulinzi mkali kwa timu ya Taifa ya England jijini Rio de Janeiro, Brazil, kutokana na vurugu za wananchi wanaoona kuwa Kombe la Dunia kwao ni kupoteza muda na pesa wakati huduma muhimu za kijamii ni duni na mishahara haitoshi.

TEAM YA VIJANA ZANZIBAR UK (UNDER 18) YAINGIA FINALI AFRICAN NATIONS CUP UK. KUCHEZA JUMAMOSI HII 14 JUNE 2014.

$
0
0

Vijana wetu wa Timu ya Zanzibar Wanaoshiriki Africa Nations Cup -UK wenye chini ya Umri wa miaka 18 wameingia Final Baada ya kuifunga Morocco 8-0 Jumamosi jioni. 
Final itakuwa Saturday, 14th June, 2014 @3.00pm. Barking FC Arena, Mayesbrook Park, Lodge Avenue, RM8 2JR - UK. 
Ticket zinauzwa £5 Adult na £2 kwa watoto kwa maelezo Wasiliana na DJ Ommy kwa number +44 7427 447902 na Jestina George +44 7557 304940

TUNAWAOMBA TUJITOKEZEE KWA WINGI KUWASUPPORT

Ambassador Mark B. Childress to inaugurate the American Corner Unguja in Zanzibar tomorrow

$
0
0
The U.S. Ambassador to Tanzania Hon. Mark B. Childress will inaugurate the American Corner Unguja in Zanzibar tomorrow  Wednesday, June 11, 2014,  

According toa  statement issued today by the US embassy in Dar es salaam, this is a partnership program between the U.S. Embassy Dar es Salaam and Zanzibar Library Services under the Ministry of Education and Vocational Training in Zanzibar.


American Corners are partnerships between the US Department of State and host-country institutions.  
The host-country institution provides the physical space and staff, while Department of State provides staff training, technical support, equipment, and multimedia materials about the United States.  American Corners also provide access to English-language learning resources, access to the Internet, and educational and cultural programs.

TAARIFA TOKA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF) LEO

$
0
0
KARIA KUFUNGUA KOZI YA MAKOCHA LEO
Makamu wa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia (pichani) atakuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa kozi ya makocha wa mpira wa miguu ya Leseni B inayotambuliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF).

Uzinduzi wa kozi hiyo ya wiki mbili utafanywa leo (Juni 10 mwaka huu) saa 6 mchana kwenye hosteli za TFF zilizopo Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume jijini Dar es Salaam.

Makocha zaidi ya 20 wenye Leseni C kutoka Tanzania Bara na Zanzibar wanashiriki katika kozi hiyo inayoendeshwa na Mkufunzi wa CAF, Sunday Kayuni. Mkufunzi mwingine wa kozi hiyo anayetambuliwa na CAF ni Mkurugenzi wa Ufundi wa TFF, Salum Madadi.

KANALI MWANAKATWE KUZIKWA LEO BABATI
Mazishi ya aliyekuwa Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) wakati huo likiitwa FAT, Kanali mstaafu Ali Hassan Mwanakatwe yanafanyika leo (Juni 10 mwaka huu) Magugu, Babati mkoani Manyara.

Kanali Mwanakatwe alifariki dunia Juni 7 mwaka huu katika Hospitali Kuu ya Jeshi (GMH) Lugalo jijini Dar es Salaam wakati akipatiwa matibabu baada ya kuanguka bafuni nyumbani kwake Mbezi Beach.

TFF imetoa ubani wa sh. laki tano kwa familia ya marehemu Kanali Mwanakatwe, na katika maziko hayo inawakilishwa na mjumbe wa Kamati ya Utendaji wa Kanda ya Arusha na Manyara, Omari Walii.

AMBUNDO, SHIZA WATESA UHOLANZI
Wachezaji wa Tanzania walioko Uholanzi, Dickson Ambundo na Shiza Yahya wameanza kuonekana muda na waandaaji ya mashindano ya AEGON Copa Amsterdam.
Kwa mujibu wa wakala wa wachezaji wa Uholanzi, Denis Kadito, AEGON Copa Amsterdam ni mashindano ya kimataifa yanayoshirikisha timu kubwa kutoka nchi mbalimbali ulimwenguni kwa wachezaji wa miaka chini ya 19.
Kwa Uholanzi, Ajax Amsterdam huwa lazima washiriki, na pia huwa kuna timu ya ridhaa inayotengenezwa kwa kuchagua “best talent” kutoka Uholanzi. Mchujo wa wachezaji hao kutengeneza timu ya kombaini, ulianza na wachezaji wasiopungua 1,000.
Kombaini hiyo inaitwa Men United na inafundishwa na mchezaji wa zamani wa kimataifa wa Uholanzi, Ronald de Boer. Ronald e Boer ni pacha wa kocha wa Ajax (First team).
Ronald de Boer pia ni kocha wa wachezaji washambuliaji wa Ajax. Shiza na Ambundo waliingizwa kwenye mchujo na wakafanya vizuri, mwishoni wakaitwa kwenye timu ya wachezaji 18 waliotengeneza timu ya Men United. Hii ni mara ya kwanza wachezaji wasio Waholanzi kuingizwa katika timu hiyo.
Mashindano ya Copa Amsterdam yameanza juzi (Juni 8 mwaka huu) na yanaisha kesho (Juni 11 mwaka huu. Katika mashindano hayo kuna makundi mawili. Kundi A ni AFC Ajax (Amsterdam), Ajax Cape Town ( Afrika Kusini), Fluminense (Brazil), Hamburg SV (Ujerumani) wakati B ni Men United, Panathinaikos (Ugiriki), FC Aerbin (China) na Cruizero (Brazil).
Shiza na Ambundo wamecheza mechi zote tatu. Shiza amekuwa akicheza namba tatu wakati Ambundo anapiga namba tisa, saba na kumi na moja.

BONIFACE WAMBURA
OFISA HABARI NA MAWASILIANO

SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live




Latest Images