Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 464 | 465 | (Page 466) | 467 | 468 | .... | 3348 | newer

  0 0

  The EAC Partner States’ Ministries responsible for Animal Resources and National Statistics have been called upon to strengthen their collaboration in order to enhance animal resources data management within the region.

  The call was made during the meeting of Experts on Animal Data and Animal Resources Information System (ARIS 2) that concluded over the week end in Kampala, Uganda. Experts from the EAC Partner States line Ministries responsible for Animal Health and Production, Fisheries Development, Trade and EAC Affairs attended the meeting.

  The five-day meeting recommended to the EAC Sectoral Council on Agriculture and Food Security to urge all the five Partner States to immediately initiate the use of ARIS 2. A Technical Working Group on animal resources data should also be established at National and Regional levels and the draft Terms of Reference adopted.

  The meeting urged the Fisheries sector to review and update its ARIS 2 modules; and  urged the Livestock Data Innovation Project in Africa to expand its coverage to all the remaining EAC Partner States of Burundi, Kenya and Rwanda to support improvement of livestock data collection in its 2nd phase of the Project.


  0 0

  Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Iddi Hassan Kimanta kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya akikata utepe kuashiria kuzindua rasmi huduma ya Option B Plus Mkoani Rukwa jana tarehe 07 Juni, 2014 katika Kijiji cha Tamasenga Wilayani Sumbawanga. Huduma hiyo ina lengo la kutoa tiba ya kuzuia maambukizi ya virusi vya ukimwi kutoka kwa mama mjamzito kwenda kwa mtoto mchanga. Kaulimbiu ya huduma hiyo ikiwa "Amka Sasa Tokomeza VVU kwa Watoto, Kama mjamzito Pima VVU kwa maisha Bora, Tiba inapatikana"
  Mkuu wa Wilaya Nkasi Iddi Hassan Kimanta (kulia) akipokea taarifa ya utaratibu maalum na tiba ya kuzuia maambukizi ya VVU kutoka kwa mama mjamzito kwenda kwa mtoto mchanga kutoka kwa wataalamu wa tiba alipotembelea banda la Hospitali Kuu ya Rufaa ya Mkoa wa Rukwa muda mfupi kabla ya uzunduzi wa huduma hiyo katika viwanja vya Tamasenga Wilayani Sumbawanga. Katika salam zake Mkuu huyo wa Wilaya amewataka wahudumu wa afya kuzingatia viapo vyao kwa kutunza siri za wagonjwa hususani walipomwa na kukutwa na maambukizi ya virusi vya Ukimwi.
  Mganga Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Dkt. John Gurisha akisoma risala kwa Mgeni Rasmi katika hafla hiyo ya uzinduzi wa huduma ya Option B Plus. Katika risala yake amesema maambukizi ya virusi vya Ukimwi Mkoani Rukwa yameongezeka ambapo sasa yapo kwa kiwango cha asilimia 6.2. Alisema mpaka sasa jumla ya watumishi 225 sawa na asilimia 75% wameshapatiwa mafunzo ya utoaji wa huduma hiyo ambapo matarajio ni kufikia watumishi 302. Alieleza kuwa mpaka sasa jumla ya vituo 116 vinatoa huduma hiyo sawa na asilimia 83% lengo likiwa kufikia vituo 139 hadi kufikia mwezi Septemba 2014.
  Hafla hiyo ya uzinduzi ilipambwa na maandamano ya awali yaliyokuwa yakitoa ujumbe wa mapambano dhidi ya virusi vya Ukimwi kutoka kwa mama mjamzito kwenda kwa mtoto mchanga. 
  Meza kuu ikipokea maandamano hayo kwa kupiga makofi. Wakwanza kushoto ni Naibu Meya Manispaa ya Sumbawanga,  Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Ndugu Erasmus Rugarabamu, Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Iddi Kimanta na Mganga Mkuu Mkoa wa Rukwa Dkt. John Gurisha.
  Mganga Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Dkt. John Gurisha kushoto akiteta jambo na Mratibu wa Ukimwi Mkoa wa Rukwa Dkt. Hansi Ulaya muda mfupi kabla ya uzinduzi wa huduma hiyo.
  Baadhi ya wadau wa huduma ya afya waliohidhuria katika hafla hiyo. 
  - Na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa @rukwareview.blogspot.com

  0 0


  0 0

   Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Kanisa Katoliki, Muadhama Policarp Kadinali Pengo,akiongea wakati wa sherehe za siku ya Wazazi ya sekondari za Marian, huko Bagamoto, mkoani wa Pwani 
   Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Kanisa Katoliki, Muadhama Policarp Kadinali Pengo, akimshukuru Meneja Uhusiano na Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Lulu Mengele, kutokana na Mfuko huo kudhamini sherehe za siku ya Wazazi ya sekondari za Marian, huko Bagamoto, mkoani Pwani Jumamosi Juni 7, 2014
   Mmoja wa wanafunzi wanaofaidika na fao la Elimu, litolewalo na Mfuko wa Pensheni wa PPF, Rosalia Faustin Madulu, (Kulia), akieleza jinsi yeye binafsi ambaye kwa sasa yuko kidato cha Kwanza shule ya sekondari Marian iliyoko Bagamoyo, jinsi anavyofaidika na fao hilo tangu apoteze mzazi wake miaka 9 iliyopita. Aliyasema hayo wakati wa siku ya wazazi ya sekondari hiyo, Jumamosi Juni 7, 2014.Wakwanza kushoto ni Meneja Uhusian na Masoko wa PPF, Lulu Mengele, na wengine ni wanafunzi wengine wa shule hiyo wanaofaidika la fao hilo, Deborah Kibona, (Wapili kushoto) na Eileen Amon Urio

   Joyce Nachenga, (Kusho), mwakilishi wa Mfuko wa PPF, Kanda ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, akiwaeleza wazazi wa wanafunzi wa shule ya sekondari Marian, faida za kujiunga na Mfuko huo, wakati wa sherehe za siku ya wazazi iliyofanyika shuleni hapo.

  0 0


  0 0


  0 0

  ipo katika hali nzuri.  Ni ya mwaka 2001, 4WD, Petrol, Automatic, engine capacity 1998, Milleage 82000, ina Air Conditioning, Airbags, Alloy Wheels, AM/FM Radio, Anti-Lock Brakes, Electric Windows ,Front Fog Lamps ,Power Steering,  n.k. Gari ipo Dar es Salaam. Bei milioni 14. Kwa mawasiliano zaidi   piga namba 0655657911 au 0754573435.
  0 0

   Dada za Marehemu wakitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu wakati wa kuuaga Mikocheni B jijini Dar.


  Maafisa wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Kikosi cha 37 Tanga, wakitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu wakati wa kuuaga nyumbani kwa
   Mjane wa Marehemu, Bi. Maria Singano akilia kwa uchungu wakati akiuaga mwili wa mpendwa  mume wake, nyumbani kwao katika eneo la Sahare mkoani Tanga.
  Mtoto wa Marehemu, ambaye ni Mkuu wa Mahusiano wa kampuni ya simu za mkononi ya Airtel, Bi. Beatrice Singano akilia kwa uchungu wakati akiuaga mwili wa mpendwa baba yake, nyumbani kwao katika eneo la Sahare mkoani Tanga.

   Waziri Mkuu mstaafu, Dk. Salim Ahmed Salim akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu wakati wa kuuaga Mikocheni B jijini Dar.

  0 0


  0 0

  MUIGIZAJI MKONGWE HAPA NCHINI, SAID WA NGAMBA MAARUFU KWA JINA LA MZEE SMALL AMEFARIKI DUNIA USIKU WA KUAMKIA LEO KATIKA HOSPITALI YA TAIFA YA MUHIMBILI ALIKOKUWA AMELAZWA AKIPATIWA MATIBABU YA KIHARUSI. ALIKUWA NA MIAKA 59.

  AKITHIBITISHA TAARIFA YA KIFO CHA MZEE SMALL, MWANAE AITWAE MAHMOUD AMESEMA MZEE WAKE AMEFIKWA NA MAUTI HAYO MAJIRA YA SAA NNE USIKU WAKATI AKIWA HOSPITALINI HAPO AKIENDELEA KUPATIWA MATIBABU.

  MIPANGO YA MAZISHI INAFANYIKA NYUMBANI KWAO TABATA AMBAPO MAZISHI YANATARAJIWA KUWA KESHO SAA KUMI ALASIRI KATIKA MAKABURI YA  TABARA SEGEREA JIJINI DAR ES SALAAM.

  MZEE SMALL ATAKUMBUKWA KAMA MMOJA WA WACHEKESHAJI MAHILI KUTOKEA HAPA NCHINI, MARA KWA MARA AKIWA NA "MKEWE" WA JUKWAANI BI. CHAU.

  MAISHA YA SANAA YA MZEE SMALL YALIANZIA KATIKA NGOMA ZA UTAMADUNI, AKIWA MMOJA WA WASANII WALIOKIWEZESHA KIKUNDI CHA MAGEREZA KUTAMBA SANA TANGIA MIAKA YA 1970 NA 1980. 
  ALIENDELEA KUWA NYOTA WA UTAMADUNI HATA BAADAYE ALIPOSTAAFU MAGEREZA NA KUJIUNGA NA KIKUNDI CHA RELI "KIBOKO YAO" NA BAADAYE NASACO,  KABLA YA KUANZISHA KUNDI LAKE MWENYEWE NA HATIMAYE KUJITOSA KWENYE FILAMU, AKIWA MUIGIZAJI WA KWANZA KUCHEZA KOMEDI KWENYE TV.

  GLOBU YA JAMII IMEPOKEA TAARIFA HII KWA MASIKITIKO MAKUBWA SANA NA INAMUOMBEA KWA MWENYEZIMUNGU AIWEKE ROHO YAKE MAHALA PEMA PEPONI.
  -AMIN.

  0 0

  sheriaDiamond
  Diamond Platinumz with  Wema Sepetu.
  Being nominated in an internationally recognized Music Awards worldwide, is a sign of hardworking and thirst to achieve more. You are really flying our Tanzanian flag globally and in the same vein paved the way for international attention indeed. Congratulations Diamond Platinumz, you have set a Benchmark. Keep up the good work.
  Deogracious Kessy- Head of Marketing
  #Sheria Ngowi Brand#

  0 0

  Mke wa Waziri Mkuu Msaafu (Mh. Edward Lowassa),Mama Regina Lowassa (kushoto) akimsikiliza kwa makini Dada yake mkubwa wakati akizungumza machache kwenye hafla fupi ya kusherehekea kuadhimisha miaka 60 ya kuzaliwa kwake iliyofanyika leo nyumbani kwake,Masaki jijini Dar es salaam.
  Mama Regina Lowassa akiwa na Marafiki zake wakati hafla hiyo ikiendelea.
  Mama Regina Lowassa akipokea zawadi ya Kitabu kutoka kwa mmoja wa Marafiki zake waliohudhulia hafla hiyo.
  Watoto wa Mh. Edward na Mama Regina Lowassa, Dkt. Adda (kushoto) na Bi. Pamela Lowassa wakiimba wimbo maalum wa kumpongeza Mama yao kwa kutimiza miaka 60 ya kuzaliwa kwake.
  Waziri Mkuu Msaafu na Mbunge wa Monduli,Mh. Edward Lowassa akisoma shairi alilolitunga mwenyewe,ikiwa ni sehemu ya pongezi kwa Mkewe Mama Regina Lowassa kutimiza Miaka 60 ya kuzaliwa kwake.
  Mama Regina Lowassa akikata keki.

  BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI
  0 0

  Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwahutubia wananchi wakati akizindua huduma za uchunguzi wa saratani ya mlango wa kizazi na saratani ya matiti Mkoani Tabora, katika uwanja wa Chipukizi mkoani humo Jumamosi Mei 7, 2014.
  "....It takes two to Tango", anasema Rais Kikwete akimaanisha kwamba ili kufanikisha jambo ni lazima watu wawili walio pamoja washirikiane,  wakati  akiwahamasisha wakina baba na walezi kusaidia katika juhudi za kuzuia na kutibu magonjwa haya ya saratani ya wanawake.  
  Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na baadhi ya akina mama wa Tabora.
  Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza Dkt. Joseph Komwihangiro, Mkurugenzi wa Marie Stopes kwa kuwa mstari wa mbele katika huduma na elimu ya NYOTA YA KIJANI (uzazi wa mpango)  Jumamosi Mei 7, 2014 wakati akizindua huduma za uchunguzi wa saratani ya mlango wa kizazi na saratani ya matiti Mkoani Tabora, katika uwanja wa Chipukizi mkoani humo. Wengine toka kushoto ni Mama Salma Kikwete, Mlezi wa MEWATA, Dkt. Serafina Mkuwa, Mwenyekiti wa MEWATA, Mhe. Kebwe Steven Kebwe (Mb.), Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, kulia kabisa ni Mbunge wa Tabora Mjini Mhe. Ismail Aden Ragge.
  Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na wanakwaya wa kambi ya Msange JKT ya Tabora Jumamosi Mei 7, 2014 baada ya kuzindua huduma za uchunguzi wa saratani ya mlango wa kizazi na saratani ya matiti Mkoani Tabora, katika uwanja wa Chipukizi mkoani humo.
  Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza jambo na Mbunge wa Tabora Mjini Mhe. Ismail Aden Ragge baada ya kuzindua huduma za uchunguzi wa saratani ya mlango wa kizazi na saratani ya matiti Mkoani Tabora, katika uwanja wa Chipukizi mkoani humo.
  -------------------------------------------------
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Mrisho Kikwete ameamuru Jeshi la Polisi kupeleleza na kisha kuwachukulia hatua mara moja watu wote wanaotuhumiwa kwa wizi na ubadhilifu katika vyama vya ushirika mkoani Tabora.

  Rais Kikwete amesikitishwa sana na tuhuma hizo zilizosababisha kuwepo kwa  tatizo la muda mrefu kwa wakulima wa tumbaku kwa kutokulipwa stahili zao na vyama vya ushirika kwa muda mrefu.

  Alisema:  "Kwa upande wa tatizo la wakulima wa tumbaku kutokulipwa stahili zao na vyama vya ushirika nimeelezwa na kulielewa.  Kuna tuhuma za wizi na ubadhilifu.  

  “Nimemuagiza Inspekta Jenerali wa Polisi atume watu wake wa upelelezi wa makosa ya Jinai waje wafanye uchunguzi ili wahusika wakamatwe na kufikishwa Mahakamani na kupewa adhabu zinazostahili. 

  “Ameniahidi kuwa keshokutwa (Jumatatu)  watu hao watakuja.  Wapeni ushirikiano unaostahili ili tukomeshe uhalifu na dhuluma zinazofanywa na Maofisa wa Vyama vya Ushirika na taasisi za fedha kwa muda mrefu sasa".

  Rais aliyasema hayo Jumamosi Mei 7, 2014 wakati akizindua  huduma za uchunguzi wa saratani ya mlango wa kizazi na saratani ya matiti Mkoani Tabora, katika uwanja wa Chipukizi mkoani humo.

  Rais Kikwete alisisitiza kwamba zoezi la kuchukuliwa hatua watuhumiwa wa wizi na ubadhilifu katika vyama vya ushirika lisifanywe la kisiasa, na kwamba asiogopwe wala kuonewa haya mtu yeyote anayehusika hata awe nani.

  BOFYA HAPA KUSOMA HOTUBA YA MH. RAIS

  0 0

   Huo msalaba uuonao hapo ni taa za magazri zilizo katika foleni mishale ya saa moja jioni kwenye makutano ya barabara za Morogoro road na Nelson Mandela jijini Dar es salaam. Hakika kuna haja ya kutafuta njia mbadala za kupunguza foleni ya magari katika jiji hili. Ushauri wa bure kwa Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi na Madiwani wa Manispaa za Ilala, Temeke na Kinondoni. Boresheni njia za pembeni ili magari yaweze kupungua katika barabara hizi kuu. 
  Picha na Sultani Kipingo wa Globu ya Jamii


  0 0


  Photo Credits: EyesOnNews.com 
  Siku chache kabla ya kuanza kwa michuano ya Kombe la Dunia la Soka huko Brazil, mambo mengi yamekuwa yakizungumzwa kuhusu maandalizi ya michuano hiyo.
  Kuna malalamiko na maandamano nchini humo ambavyo kwa hakika vinaleta taswira isiyo njema kuhusu maandalizi ya michuano hiyo
  Kutaka kujua mengi, Kwanza Production imefanya mahojiano na Halifa Ramadhan.
  Mtanzania mwenye maskani yake nchini Brazil ambaye amezungumzia mengi kuhusu maandalizi ya fainali za kombe la dunia na pia maisha ya nchini humo kwa ujumla.
  KARIBU UUNGANE NASI
  Kwa maoni ama ushauri tuandikie kupitia kwanzaproduction at gmail.com

  0 0

  Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi,(MUWSA) Mhandisi Cyprian Luhemeja (mwenye suti)akiwaongoza madiwani wa halmashauri ya manispaa ya Moshi kutembelea vyanzo vya maji vinavyosimamiwa na mamlaka hiyo.

  Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi,(MUWSA) Mhandisi Cyprian Luhemeja(aliyenyoosha mkono)akitoa maelezo kwa Madiwani walipotembelea chanzo cha Maji cha Cofee Curing.
   Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi,(MUWSA) Mhandisi Cyprian Luhemeja akiongoza Madiwani kutembelea Mabwawa ya kuhifadhia Maji taka eneo la Mabogini .


  0 0
 • 06/08/14--23:57: KUMBUKUMBU
 • KUMBUKUMBU YA KIFO CHA MAMA YETU MPENDWA MRS K. MNUBI

  sasa ni miaka miwili tangu mama yetu kipenzi ulioitikia sauti ya Mungu hapo tarehe 07.06.2012. Sisi kama familia tunatoa shukrani za pekee kwa Mungu kwa jinsi alivyoweza kutulinda na kutupa Faraja ya pekee katika kipindi chote cha majonzi na hadi sasa tunatimiza miaka miwili bila kuwa nawe. Tunakukumbuka sana mama japo kimwili haupo nasi, pengo lako daima haliwezi kuzibika.

  Tunakukumbuka kwa upendo wako, ushauri wako kama mama na mke. Kipekee unakumbukwa sana na mume wako mpendwa Kedmond, watoto wako Catherine, Restituta, mama ako mpendwa na ndugu jamaa na marafiki.

  Dua ya kumuombea marehemu itafanyika nyumbani kwake Msamala, Songea tarehe 07.06.2014

  INNALILAHI WAINA ILLAIHI RAJIUUN.

  0 0

  Kamisha wa Elimu nchini Prof, Eustella Bhalalusesa akikata utepe kuashiria uzinduliwa rasmi Maktaba inayo tembea Wilayani Bagamoyo.
  Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Sayansi Teknolojia na Mawasiliano Bw John Mngodo akiwa washa Piki piki ya Miguu mitatu aina ya TOYO iliyo beba makta kama kiashirio cha Maktaba hiyo inayo tembea ipo tayari kuanza kazi.
  Mkurugenzi Mkazi wa ITIDO Bi Mwawi Mlekano akimkabidi Kamisha wa Elimu nchini Prof, Eustella Bhalalusesa alioko kushoto Kadi ya TOYO iliyo undwa mahususi kuwa Maktaba inayo Tembea.
  Baadhi ya wanafunzi na Walimu wa Shule za Wilayani Bagamoyo walio udhuria uzinduzi wa mpango wa ICT 4 GIRLS.

  Na Madau Sixmund J. Begashe.
  Kamisha wa Elimu nchini Prof, Eustella Bhalalusesa ameihasa jamii kuacha kuwakandamiza watoto wakike na kuwaona kuwa hawawezi katika kujiendeleza bali wapewe nafasi sawa kama wanavyo pewa watoto wakiume, Prof Bhalalusesa aliyasema hayo alipo kuwa akizindua mpango maalum wa kuwawezesha wanafunzi wa Wilayani Bagamoyo hasa wasichana kwa njia ya TEHAMA.

  Prof Bhalalusesa ameto wito kwa wasichana hasa waliopo mashuleni kutumua vyema miradi inayo anzishwa kwa ajili yao ili kuaondoa dhanapotofu iliyojengeka dhidi yao, hata ivyo aliwahasa kuitumia vyema teknolojia hii ya mawasiliano ili kuwaletea tija na si vinginevyo.

  Nae kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Sayansi Teknolojia na Mawasiliano Bw John Mngodo akizungumza na wakazi hao wa Bagamoyo alisema kuwa mchango huu wa ITIDO umekuja wakati muafaka kwani maendeleo ya TEHAMA ni ya kasi sana, hivyo amewashauri wanatanzania kuendana na kasi hii kwa maendeleo ya nchi yetu.

  Akizungumza na mwandishi wa Habari hizi Mkurugenzi Mkazi wa ITIDO Bi Mwawi Mlekano alisema kuwa Taasisi yake imeona itoe mchango wake kwenye Maktaba ya Wilaya ya Bagamoyo kwa kuikarabati na Kuipatia vifaa vya ICT ili kutoa fursa kwa wanafunzi hasa wakike kutumia vifaa hivyo katika kujisomea kwani wamekuwa wakikosa fursa hiyo kwa muda mrefu.

  Bi Mlekano aliongeza kuwa kwakuwa shule nyingi za Bagamoyo azina Maktaba hivyo Taasisi yake imeona ni vyema ikabuni Mabkata inayotembea na kulikabidhi Shirika la Maktaba ya Taifa ili Maktaba hiyo iweze kutoa huduma kwenye shule zilizo mbali na Maktaba ya Wilayani hapo.

  Licha ya kuishukuru ITIDO kwa Mchango wa kielimu, Bagamoyo, Mwl Adbeel Kitungwa wa Shule ya Sekondari ya Bagamoyo aliishauri Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi nchini, kuanzasha mtaala wa mafunzo ya TEHAMA kwa matendo na kufanyiwa mtihani wa kitaifa kuliko hilivyo hivi sasa ambapo hakuna kipaombele katika kuwawezesha wanafuzi kimatendo.

  Mpango huu wa kuwawezesha wanafunzi wa shule za Bagamoyo hususani wasichana kutumia TEHAMA katika kujiendeleza kielimu umegharimu Dola 80,000 za kimarekani zilizo fadhiliwa na Shirika la Kiswidish linalo ratibiwa na Chuo kikuu cha Stockholm cha Sweden (SPIDER) na mradi huo kutekelezwa na ITIDO, EIFL, TLSB na SLADS, Milioni 5 zilizo tolewa na ITIDO Kununulia Maktaba inayo tembea.

  0 0
 • 06/09/14--00:30: Article 20

 • 0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mh. Joel Bendera akifafanua jambo wakati alipofungua Mkutano wa Saba wa Baraza la Wafanyakazi wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima uliofanyika katika Ukumbi wa WAMO Mjini Morogoro, (wa pili Kulia) ni Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima Bw. Fedelis Mafumiko na (wa kwanza kulia) ni Naibu Mkurugenzi Taaluma, Bw. Welberforce Meena (Kushoto) ni Naibu Mkurugenzi Fedha na Utawala Bw.Edward Lugakingira.
  Baadhi ya Watumishi wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mh. Joel Bendera (hayupo pichani) akifafanua jambo wakati alipofungua Mkutano wa Saba wa Baraza la Wafanyakazi uliofanyika katika Ukumbi wa WAMO Mjini Morogoro.
  Mwenyekiti wa Baraza la Baraza la Wafanyakazi wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima , Bw.Edward Lugakingira akifafanua umuhimu wa Baraza hilo, (kulia) ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mh. Joel Bendera (wa pili kulia ni ) Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima Bw.Fedelis Mafumiko na (wa kwanza kulia) ni Naibu Mkurugenzi Taaluma Bw. Welberforce Meena, wakati wa Mkutano wa Saba wa Baraza la Wafanyakazi uliofanyika katika Ukumbi wa WAMO Mjini Morogoro.
  Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mh. Joel Bendera (waliokaa watatu kutoka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima mara baada ya kufungua mkutano huo uliofanyika katika Ukumbi wa WAMO Mjini Morogoro.

older | 1 | .... | 464 | 465 | (Page 466) | 467 | 468 | .... | 3348 | newer