Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110167 articles
Browse latest View live

BIA YA SAFARI LAGER NA NDOVU SPECIAL MALT ZAREJEA NCHINI NA TUZO YA UBORA WA KIMATAIFA 2014 “INTERNATIONAL HIGH QUALITY TROPHY”

$
0
0
Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo akiwasili katika Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere akitoka Ufaransa kuchukua tuzo ya Ubora wa Kimataifa(Safari Lager High International Quality Trophy iliyoshinda hivi karibuni kutoka katika taasisi ya Kimataifa ya Monde Selection nchini Ufaransa.
Picha ya Pamoja mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere akitoka Ufaransa kuchukua tuzo ya Ubora wa Kimataifa(Safari Lager High International Quality Trophy) iliyoshinda hivi karibuni kutoka katika taasisi ya Kimataifa ya Monde Selection nchini Ufaransa.
Picha ya Pamoja mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere akitoka Ufaransa kuchukua tuzo ya Ubora wa Kimataifa(Ndovu High International Quality Trophy) iliyoshinda hivi karibuni kutoka katika taasisi ya Kimataifa ya Monde Selection nchini Ufaransa.
Meneja wa Bia ya Ndovu Special Malt, Pamela Kikuli (kulia) akimkabidhi Meneja wa Kiwanda cha Bia cha Dar es Salaam, Calvin Martin tuzo iliyopata bia ya Ndovu Special Malt mara baada ya kuwasili kutoka nchini Ufaransa(Ndovu High International Quality Trophy) Dar es Salaam jana.


TFF YATOA SALAMU ZA RAMBIRAMBI MSIBA WA KANALI MWANAKATWE

$
0
0
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko kifo cha aliyekuwa Katibu Mkuu wake (wakati huo ikiitwa FAT), Kanali mstaafu Ali Hassan Mwanakatwe kilichotokea leo asubuhi (Juni 7 mwaka huu) katika Hospitali Kuu ya Jeshi (GMH) Lugalo jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa binti wa marehemu, Sophia, baba yake alianguka bafuni nyumbani kwake Mbezi Beach ambapo alikimbizwa katika Hospitali ya Lugalo ambapo ndipo umauti ulipomfika wakati madaktari wakimpatia matibabu.

Kanali Mwanakatwe alichaguliwa kuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Mpira wa Miguu Tanzania (FAT) katika uchaguzi uliofanyika mwaka 1993 mjini Kibaha mkoani Pwani.

Baada ya kuondoka FAT, aligombea nafasi ya Katibu Mkuu wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) na kufanikiwa kushinda katika uchaguzi uliofanyika mwaka 1997.

Msiba huo ni mkubwa katika fani ya mpira wa miguu nchini na Afrika kwa ujumla kwani, Kanali Mwanakatwen enzi za uhai wake alitoa mchango mkubwa akiwa kiongozi, na mkufunzi wa utawala wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF). Pia aliwahi kuwa Kamishna wa CAF.

TFF tunatoa pole kwa familia ya marehemu Kanali Mwanakatwe, DRFA, na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na kuwataka kuwa na subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha msiba huo mzito.

Taratibu za mazishi zinaendelea kufanywa na familia yake nyumbani kwake Mbezi Beach karibu na hoteli ya Giraffe wakati ndugu wakisubiriwa kutoka mikoani. TFF tunasubiri taratibu hizo ili tujipange jinsi ya kushiriki katika msiba huo.

Sisi sote ni waja wake Mola. Hakika kwake tutarejea.

BONIFACE WAMBURA
OFISA HABARI NA MAWASILIANO
SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

WAZIRI MKUU ACHARUKA, AKATAA KUKAGUA JENGO LA ZAHANATI

$
0
0
ILE HALI ya kufanya kazi kwa mazoea (business as usual)  iliyojengeka kwa baadhi ya watendaji wa Serikali leo imewatokea puani watendaji wa Manispaa ya Dodoma wakati Waziri Mkuu alipoamua kufanya ziara kukagua miradi ya maendeleo.

Akiwa katika eneo la kwanza ambalo alipangiwa kukagua ujenzi wa kituo cha afya cha Mkonze leo asubuhi (Jumamosi, Juni 7, 2014) Waziri Mkuu alipokea taarifa ya ujenzi wa kituo na kubaini kuwa hawajafanya chochote ili kutekeleza maagizo yake aliyoyatoa Machi 22, 2014.

Katika taarifa yake, Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma, Mhandisi Lusako Kilembe alimweleza Waziri Mkuu kwamba walifanya tathmini ya ujenzi wa kituo hicho na kubaini kuwa zinahitajika sh. Milioni 24.15 na kwamba maombi ya matumizi hayo yamepangwa kujadiliwa kwenye kikao cha kamati ya fedha na uongozi kitakachofanyika Juni 10, mwaka huu.

Akiwa katika maadhimisho ya kilele cha wiki ya maji ambayo Kitaifa yalifanyika mkoani Dodoma, Waziri Mkuu alizindua mradi wa maji jirani na kituo cha afya cha Mkonze na kubaini kuwa kuna hitilafu za ujenzi. Ndipo akaagiza kwamba ufanyike ukarabati na yeye akaahidi kuja kukagua ukarabati huo mwezi Juni, 2014.

Mara baada ya kusomewa taarifa ya mradi, Waziri Mkuu akahoji ni kwa nini hawajafanya chochote tangu alipotoa maelekezo Machi, mwaka huu. Hakupata jibu la kueleweka kutoka kwa viongozi wa wilaya na mkoa.

Waziri Mkuu aliwasalimia wananchi waliokuwepo kwenye eneo hilo na kuwaeleza kwamba hawezi kukagua kituo hicho ilhali hakuna kilichotekelezwa tangu afike hapo Machi mwaka huu.

Alisema haiwezekani yeye atoe maagizo katika kipindi chote hicho halafu kisifanyike kitu chochote. Akaondoka na kuendelea na ziara hadi kijiji cha Manzase ambako alikagua mradi wa kisima cha maji.
Mapema, katika taarifa yake, Mhandisi Kilembe alisema kituo hicho cha afya kilijengwa chini ya ufadhili wa ubalozi katika makubaliano yaliyofikiwa Novemba 11, 2009 kwamba ingetoa dola za marekani 84,307 sawa na sh. Milioni 152.86.

Hata hivyo, mara baada ya ujenzi kukamilika Agosti 29, 2012, kituo hicho kilipata nyufa nyingi hali iliyosababisha kifungwe na wananchi walitoa malalamiko yao kwa Waziri Mkuu Machi mwaka huu wakati alipokwenda kuzindua mradi wa maji kwenye kijiji cha Mkonze jirani na kituo hicho.

Akiwa katika kijiji cha Manzase Waziri Mkuu aliridhishwa na ujenzi wa mradi wa maji kwa ajili ya wakazi 9,000 wa eneo ambapo alielezwa kwamba utakamilika Julai 16, 2014.

TASWIRA MBALI MBALI ZA TAMASHA LA NYAMA CHOMA JIJINI DAR

$
0
0
 Wadau ndani ya Tamasha la Nyama Choma,toka kulia ni Dimo Dibwe,Carol Ndossi (Muandaaji wa Tamasha hilo la Nyama Choma) pamoja na Mdau Edwin MacTemba.
 Nyama ikiendelea kuiva jikoni huku walaji wakiendelea kuimezea Mate. 
 Mtaalam wa kuchoma nyama toka jamii ya Kimasai akitest mzigo kama uko poa.
 Wadau wakiendele kutafuna nyama huku zingine zikiendelea kuiva taratibu.
 Maandalizi ya Nyama yakiendelea.
 Mshkaki maridadi kabisa.

NAPE azungumza na wanachama wa CCM Tawi la SAUT jijini MWANZA

$
0
0
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na wanachama wa CCM Tawi la SAUT Kambarage ambapo aliwaambia kuwa wasomi wa vyuo wanatakiwa kuchangia mawazo yao kwenye chama ambayo yatasaidia kuleta mabadiliko hasa ya kiuchumi ,alisema ni vyema kuja na mikakati ya kuonyesha uchumi umepanda kwa mwananchi kuliko huu wa sasa ambao unaonyesha uchumi umepanda lakini ni uchumi wa kwenye makaratasi.Uongozi Tawi la SAUT Kambarage ulimualika Katibu wa Itikadi na Uenezi kuja kushuhudia makabidhiano ya Uongozi na tathmini ya Tawi kwa miaka minane sasa.
 Aliyekuwa Rais wa Serikali ya Wanafunzi katika Chuo cha SAUT Mwanza Ndugu Dova Mcheshi akizungumza wakati wa shughuli ya kukabidhiana Uongozi wa Tawi la SAUT Kambarage ambapo aliwaambia wanachama wa CCM katika Chuo cha SAUT kuwa kuanzia sasa chama kinajiimarisha zaidi kwenye Chuo cha SAUT.Dova laiyekuwa CHADEMA lakini sasa amejiunga na CCM .
 Wadada wakiwa wamependeza na Sare yao ya Chama.
 Viongozi wa CCM mkoani Mwanza na Viongozi wa Serikali ya wanafunzi wakiwa kwenye picha ya pamoja na Katibu Mwenezi wa CCM Taifa Ndugu Nape Nnauye.
 Wanachama wa Tawi la CCM SAUT Kambarage,Mwanza.

PPF yadhamini sherehe za siku ya Wazazi ya sekondari za Marian,Bagamoto

$
0
0
Eliamini Amon Urio, (Katikati), mzazi wa Eileen, ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha tatu shule ya sekondari ya wasichana, Marian, iliyoko Bagamoyo mkoani Pwani, akielezea jinsi fao la elimu litolewalo na Mfuko wa Pensheni wa PPF, linavyosadia kumsomesha motto wake, baada ya kumpoteza mumewe mwaka 2005. Aliyasma hayo wakati wa sherehe za siku ya wazazi ya shule hiyo, Jumamosi Juni 7, 2014. Kushoto ni Meneja Uhusiano na Masoko wa PPF, Lulu Mengele na kulia ni Afisa Michango wa PPF, Kanda ya Kinondoni, Kwame Temu.
Joyce Nachenga, (Kusho), mwakilishi wa Mfuko wa PPF, Kanda ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, akiwaeleza wazazi wa wanafunzi wa shule ya sekondari Marian, faida za kujiunga na Mfuko huo, wakati wa sherehe za siku ya wazazi iliyofanyika shuleni hapo Jumamosi Juni 7, 2014.
Mmoja wa wanafunzi wanaofaidika na fao la Elimu, litolewalo na Mfuko wa Pensheni wa PPF, Rosalia Faustin Madulu, (Kulia), akieleza jinsi yeye binafsi ambaye kwa sasa yuko kidato cha Kwanza shule ya sekondari Marian iliyoko Bagamoyo, jinsi anavyofaidika na fao hilo tangu apoteze mzazi wake miaka 9 iliyopita. Aliyasema hayo wakati wa siku ya wazazi ya sekondari hiyo, Jumamosi Juni 7, 2014.Wakwanza kushoto ni Meneja Uhusian na Masoko wa PPF, Lulu Mengele, na wengine ni wanafunzi wengine wa shule hiyo wanaofaidika la fao hilo, Deborah Kibona, (Wapili kushoto) na Eileen Amon Urio.
Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Kanisa Katoliki, Muadhama Policarp Kadinali Pengo,akinzungumza wakati wa sherehe za siku ya wazazi ya shule ya sekondari ya wasichana, Marian, iliyoko Bagamoyo mkoani Pwani, Jumamosi Juni 7, 2014.
Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Kanisa Katoliki, Muadhama Policarp Kadinali Pengo, akimshukuru Meneja Uhusiano na Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Lulu Mengele, kutokana na Mfuko huo kudhamini sherehe za siku ya Wazazi ya sekondari za Marian, huko Bagamoto, mkoani Pwani Jumamosi Juni 7, 2014.

UZINDUZI SIKU YA MSANII WAFANA SANA JIJINI DAR

$
0
0
KAMPUNI ya Haak Neel Production kwa kushirikiana na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), imezindua rasmi Siku ya Msanii Tanzania itakayoenda sambamba na utoaji tuzo kwa kwa wasanii na wadau wanaotoa mchango katika sanaa ili kuenzi, kuhamasisha, kukuza na kuendeleza vipaji vyao.

Akizungumza katika uzinduzi huo uliofanyika Jumamosi usiku katika Hoteli ya Sea Cliff, jijini Dar es Salaam, Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukanagara, alisema Siku ya Msanii ni programu iliyobuniwa na Basata mwaka 2008 lakini ilishindikana kutekelezeka kutokana na ufinyu wa bajeti na kukosekana mtu wa kuendesha mradi huo ambaye angeweza kuingia ubia na Basata kama ilivyo kwa Tuzo za Muziki Tanzania.

“Nichukue fursa hii kuwapongeza Kampuni ya Haak Neel Production pamoja na Basata kwa kubuni na kufanikisha uzinduzi wa Siku ya Msanii, lakini program hii itatuwezesha kuungana na wenzetu duniani kuadhimisha ‘Siku ya Kimataifa ya Msanii’ ambayo huadhimishwa kila Oktoba 25,” alisema.

Alisema Wizara inataka wasanii kujituma na kuzalisha kazi bora zitakazotambulika ndani na nje, kutokana na kuwepo Siku ya Msanii.

Alisema amefurahishwa na fursa ambazo zimeelezwa kuwepo katika Siku ya Msanii kama semina, uwepo wa tuzo, ambazo zitaonyesha utambuzi wa kazi za wasanii.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Haak Neel Production, Emmanuel Mahendeka, alisema Siku ya Msanii ni fursa nzuri kwa wasanii kuona na kujifunza kutoka kwa wenzao na hivyo kuboresha kazi zao na Taifa kwa ujumla.

“Uhai wa sanaa yoyote inategemea kwa kiasi kikubwa uwezo wa kurithishana kutoka kizazi hadi kizazi, ni matumaini yangu Siku ya Msanii itasaidia sana kujenga misingi imara na endelevu ya kurithisha sanaa katika jamii zetu,” alisema.

Naye Kaimu Katibu Mtendaji wa Basata, Godfrey Mungereza, alisema baraza hilo limekuwa likibuni miradi mbalimbali kwa lengo la kuleta maendeleo ya sanii nchini na kushirikiana sekta binafsi katika kuendeleza sanaa na utamaduni na ndio maana wameshirikiana na Haak Neel Production ili kuendeleza sanaa.

Tuzo zitakazotolewa ni Sinema bora yenye ubunifu halisia na vionjo vya Kitanzania, kikundi bora cha sanaa za maonyesho kinachochipukia, Mpigaji mahiri wa ala za asili za muziki , Mbunifu wa mitindo ya mavazi yenye vionjo vya Kitanzania, Msanii chipukizi anayeibukia, Msanii aliyetoa mchango mkubwa katika jamii na Msanii aliyetumia maisha yake vkatika sanaa.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo, Dk. Fenella Mukangara, akipiga Gitaa kuashiria uzinduzi wa siku ya Msanii katika hafla iliyofanyika kwenye hoteli ya Sea Cliff Dar es Salaam.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo, Dk Fenella Mukangara akipokea zawadi ya picha aliyochorwa na msanii chipukizi, Meddy Jumanne wakati uzinduzi wa sherehe ya Siku ya Msanii uliofanyika mjini Dar es Salaam.
Meneja wa Masoko wa Siku ya Msanii, Catherine Metili (kulia) akiwa na ofisa Masoko wa Mradi, Veronica Martin (kushoto) wakiangalia kitabu cha wageni wakati wa uzinduzi wa Siku ya Msanii.
Mkurugenzi wa Utamaduni, Profesa Hermas Mwansoko akiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo, Sihaba Juma wakifuatilia tukio la Siku ya Msanii.
Wageni walialikwa wakimesimama kutoa heshima kwa wasanii mbalimbali waliofariki katika kipindi cha mwezi mmoja uliopita.
Mkurugenzi wa Haak Neel Production, Sebastian Mahendeka akizungumza wakati wa uzinduzi wa Siku ya Msanii.

Burudani ya Ngoma ya Asili.

MBUNGE JOSHUA NASSARI NA ANANDE NNKO WAMEREMETA KWENYE KANISA LA PENTEKOSTE KILINGA,MERU

$
0
0
Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki,Mh. Joshua Nassari na Mai Waifu wake Anande Nnko wakishangiliwa kwa shangwe mara baada ya kumeremeta kwao kwenye kanisa la Kipentekoste la Kilinga,Meru jijini Arusha.
"Mmetuona "ni kama ndio maneno yaliyokuwa vichwani mwao maharusi,Joshua Nassari na Anande Nnko wakionesa vyeti vyao vya ndoa.
Maharusi wakiwasalimia waumini waliohudhuria ibada ya ndoa yao (hawapo pichani).




ZIARA YA WAZIRI MKUU WILAYANI CHAMWINO DODOMA

$
0
0
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na Bibi Gilita Mlong'ose wakati alipotembelea Hospitali ya Mvumi wilayani Chamwino akiwa katika ziara ya wilaya hiyo mkoani Dodoma Juni 7, 2014. Bibi huyo alikuwa ni miongoni mwa wagonjwa waliofika hospitalini hapo kutibiwa macho. Kushoto ni Mbunge wa Mtera, Livingstone Lusinde.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akipokea zawadi ya mkuki kutoka kutoka kwa mwenyekiti waCCM wa Tawi la Ilolo wilayani Chamwino akiwa katika ziara ya wilaya hiyo mkoani Dodoma Juni 7, 2014. Katikati ni Mbunge wa Mtera, Livingstone Lusinde. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

TAARIFA YA MSIBA

$
0
0
Tunasikitika kutangaza kifo cha Pamela Sima Ruhago kilichotokea jijini Dar es salaam jana tarehe sita June, 2014.

 Maombelezo yanaendelea Mbweni nyumbani kwa Mama yake, Eva Ruhago.Mtaa wa MICA.

  Ibada ya mazishi itafanyika kesho tarehe 08 June, 2014 TISA KAMILI  mchana katika kanisa la KKKT BOCCO - Mbweni na  Mazishi yatafanyika MARA BAADA YA IBADA NA KUAGA katika makaburi ya Bahari beach kwa  Kondo kuanzia saa kumi jioni.

Bwana  ametoa bwana ametwaa jina lake lihimidiwe. Roho ya marehemu Pamela Sima Ruhago ipumzike amani Amin

THE WINNERS OF THE 2014 MTV AFRICA MUSIC AWARDS

$
0
0
Best Male: Davido (Nigeria)
Best Female: Tiwa Savage (Nigeria)
Best Group: Mafikizolo (South Africa)
Best New Act: Stanley Enow (Cameroon)
Best Live Act: Flavour (Nigeria)
Best Collaboration: “Y-tjukutja” – Uhuru Ft. Oskido, DJ Bucks, Professor and Yuri Da Cunha (South Africa/Angola)
Best Hip Hop: Sarkodie (Ghana)
Best Alternative: Gangs of Ballet (South Africa)
Best Francophone: Toofan (Togo)
Best Lusophone: Anselmo Ralph (Angola)
Artist of the Year: Davido (Nigeria)
Song of the Year: “Khona” – Mafikizolo ft Uhuru (South Africa)
Best Video: Clarence Peters (Nigeria)
Best Pop: Goldfish (South Africa)
Best International: Pharrell
Personality of the Year: Lupita Nyong’o (Kenya)
MTV Base Leadership Award: Ashish J. Thakkar (Tanzania)
Transform Today Award by Absolut: Clarence Peters (Nigeria)

Maalim Seif afungua rasmi wa jengo la maalum la mchezo wa Judo, Gombani Chake Chake,Pemba

$
0
0
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad na Balozi wa Japan nchini Tanzania Masaki Okada, wakikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa jengo la Judo, Gombani Chake Chake Pemba.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akisalimiana na Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Mhe. Said Ali Mbarouk wakati wa uzinduzi huo.
Rais wa heshima wa mchezo wa judo Zanzibar Bw. Shima Oka, akizungumza wakati wa uzinduzi wa jengo hilo Gombani Pemba.
Baadhi ya vijana wakionesha umahiri wao wa mchezo wa karati wakati wa uzinduzi wa jengo la judo Gombani Chake Chake Pemba.
Picha na Salmin Said, OMKR

kiwanda cha nguo cha Mazava cha Morogoro chaadhimisha miaka mitano ya kiutendaji

$
0
0
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Bi. Janet Mbene (kulia) akiingia katika ukumbi kwa ajili ya halfa fupi ya miaka mitano ya kiwanda cha nguo cha Mazava cha Morogoro mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam. Wengine ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Ukanda Maalumu wa Uwekezaji nchini (EPZA), Dkt. Adelhelm Meru na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Bw. Joel Bendera (kushoto). Kiwanda hicho kinafanya kazi kwa leseni ya EPZA.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Ukanda Maalumu wa Uwekezaji nchini (EPZA), Dkt. Adelhelm Mer akiongea wakati wa halfa fupi ya miaka mitano ya kiwanda cha nguo cha Mazava cha Morogoro mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam. Kiwanda hicho kinafanya kazi kwa leseni ya EPZA.
 Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Bi. Janet Mbene akiongea wakati wa halfa fupi ya miaka mitano ya kiwanda cha nguo cha Mazava cha Morogoro mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam. Kiwanda hicho kinafanya kazi kwa leseni ya EPZA.

WASANII 20 WALIOMO KATIKA TUZO ZA KORA WIKI HII - DIAMOND NDANI!

KONGAMANO LA MAJI LAFANYIKA JIJINI DAR,WADAU WAJIONEA TEKNOLOJIA MPYA YA MABOMBA

$
0
0
Wiki hii jijini Dar es salaam kumefanyika Kongamano kubwa la wadau wa maji kutoka kila kona ya nchi hii. kubwa lililofanyiwa kazi na wataalam hao wa maji ni kujulishwa teknolojia mpya ya mabomba iliyokuwa inatambulishwa na kampuni kubwa ya teknolojia ya mambomba ya Borouge kutoka Falme za Kiarabu. 

Borouge ilileta wataalam wanne ambao ni Mario Andrade, Farraj Tashman, Andrew Wedgner na Reda Ashkar. walionufaika na mafunzo hayo ni waliotoka Mamlaka za Maji mijini na vijiji, Wahandisi, Washauri katika fani zote za maji, ujenzi na gesi. 

pia washiriki walifahamishwa kuwa sasa lile tatizo la mabomba ya matumizi yote yamefika mwisho kwani kiwanda cha pipe industries cha vingunguti mjini dar es salaam kitakidhi mahitaji ya nchi nzima na kuwa na ziada ya kuuza nje kwa amabomba ya aina zote kama vile hdpe, pvc, grp na mabomba chuma kwa upenyo wa 60mm mpaka zaidi ya 3,200mm. 

Mgeni Rasmi katika kongamano hilo alikuwa Waziri wa Maji,Professor Jumanne Maghembe ambaye alionyeshwa kufurahishwa kwake na uwepo wa kiwanda kama hicho ambacho kinamilikiwa na wazawa kinahesabika kama kikubwa kuliko vyote afrika mashariki na kati pia cha aina yake kwa kuweza kuwa na uzalishaji wa mabomba aina yote katika kiwanda kimoja na chenye uwezo wa kuajiri watu 500.
Waziri wa Maji Professor Jumanne Maghembe (kulia) akikagua bidhaa za mabomba yanayozalishwa na kiwanda cha Pipe Industries cha mjini Dar es salaam wakati wa kongamano la wataaalam wa maji lilifanyika hivi karibuni. wa pili kushoto ni Mwekezaji Mzawa wa Kiwanda hicho Bwana Nassor Ally Seif.
Mwekezaji Mzawa wa Kiwanda cha Pipe Industries Bwana Nassor Seif (kushoto) akimsikiliza Waziri wa Maji Professor Jumanne Maghembe akimweleza jambo kuhusiana na mabomba yanayozalishwa na pipe industries wakati akikagua maonyesho ya kiwanda hicho katika kongamano la maji lilofanyika mjini dar es salaam.
Waziri Mageembe akizungumza na waandishi wa habari baaada ya kufungua kongamano la maji.


KIJITONYAMA VETERANS YATII KIPIGO CHAMABAO 3-1 BILA SHURUTI DHIDI YA WAUKAE VETERANS

$
0
0
Kikosi cha timu ya Kijitonyama Veterans, ambacho hii  kimekubali kipigo cha mabao 3-1 bila shuruti kutoka kwa wapinzani wao, Waukae Veterans, katika mchezo wa kirafiki uliochezwa leo asubuhi katika Uwanja wa Kijitonyama, Dar es salaam. Mabao ya Waukae yamefungwa na Felix Kopou na mawili yakifungwa na Athuma Bamia. Bao la kufutia machozi la Kijitonyama Veterans, likifungwa na Norbert.
Kikosi cha Waukae Veterans.
Wachezaji wa timu zote mbili wakishoo love kabla ya mchezo huo.
Mafoto akisubiri kuchukua nafasi..

Castle Lager Perfect Six yapata wawakilishi wa kwanza fainali za taifa

$
0
0
Kanda ya Kati imekuwa ya kwanza kupata wawakilishi kwenye fainali za mashindano mapya ya soka ya Castle Lager Perfect Six baada ya timu ya Schalke 04 ya Dodoma kutwaa ubingwa wa kanda hiyo katika fainali za kanda hiyo zilizopigwa kwenye uwanja wa Fire manispaa ya Morogoro wikendi hii.

Ubingwa huo kwa timu ya Schalke 04 inatoa nafasi ya kuwa mwakilishi kutoka kanda ya Kati kugombea nafasi ya kwenda nchini Hispania kutembelea uwanja wa Camp Nou na kushuhudia michezo ya klabu ya Barcelona katika La Liga endapo itashika nafasi ya kwanza katika michezo ya fainali ya ngazi ya taifa ya mashindano hayo yatayofanyika jijini Dar es Salaam siku za baadaye baada ya kupata mabingwa kutoka kanda saba.

Akizungumza na mwandishi wa gazeti hili mjini Morogoro, Meneja wa Bia ya Castle, Kabula Nshimo alisema kuwa katika michezo ya ligi ndogo ya kanda ya kati ilikuwa na ushindani mkali kutokana na kila timu kujiandaa kushinda na kuibuka mabingwa katika kanda hiyo ambapo Schalke 04 ndiyo mabingwa wa kihistoria katika kanda ya kati.

Nshimo alisema kuwa Schalke 04 ilifanikiwa kushika nafasi ya kwanza kwa kushinda michezo yake mitatu na kujikusanyia pointi tisa huku nafasi ya pili ikichukuliwa na Mzinga FC ya Morogoro iliyopata pointi sita wakati Ndezi FC ya Morogoro imekusanya pointi tatu na kushika nafasi ya tatu na Market FC ya Dodoma ikiishia kupoteza michezo yote.

Nshimo alisema kuwa mechi zilizochezwa wikendi hii zimeonyesha jinsi gani Watanzania wana mwamko na shauku kubwa ya kushiriki mashindano kutokana na watu kujitokeza kwa wingi maeneo mbalimbali ambapo yalifanyika mashindano hayo ya kwanza.

Nshimo alisema mashindano ya Castle Lager Perfect Six yamelenga kuzungumza na wanywaji wa Castle Lager ambao wana shauku ya kucheza mpira wa miguu, kuleta pamoja wanywaji wa Castle Lager kutoka sehemu mbalimbali nchini ili wafurahie pamoja na kuwapa zawadi wateja hao wa bia hiyo.Vilevile wikendi hii yalifanyika mashindano hayo kwenye mkoa wa Arusha na

Kahama katika hatua za awali kupata wawakilishi watakaocheza fainali za Kanda husika na pia zilifanyika fainali mkoa wa Temeke katika hatua za kupata wawakilishi wa Kanda kwenye fainali za taifa. Mashindano ngazi ya fainali za Kanda yataendelea wikendi ijayo kwenye mikoa ya Mwanza na Ilala na hatua ya kufuzu kucheza fainali za kanda itafanyika Moshi, Mbeya na Kinondoni.
Meneja Mauzo wa Kampuni ya Bia Tanzania Kanda ya Mashariki, Julius Nyaga kushoto akimkabidhi kombe nahodha wa timu ya Schalke 04 ya Dodoma, Mussa Gaidi baada ya timu yake kushika nafasi ya kwanza ya Castle Lager Perfect Six kutoka kanda ya Kati katika michezo iliyofanyika uwanja wa Fire Morogoro kwa kukusanya pointi tisa ambapo itawakilisha kanda kwenye ngazi ya taifa kuwania safari ya kwenda Hispania kutembelea uwanja wa Camp Nou na kushuhudia michezo ya klabu ya Barcelona.
Nahodha wa timu ya Schalka 04 ya Dodoma Mussa Gaidi akiwa na wachezaji wenzake wakifurahi kutwaa ubingwa wa kanda ya Kati wa mashindano ya Castle Lager Perfect Six baada ya kushika nafasi ya kwanza kutoka kanda ya Kati katika michezo iliyofanyika uwanja wa Fire manispaa ya Morogoro kwa kukusanya pointi tisa ambapo itawakilisha michezo ya ngazi ya taifa kuwania safari ya kwenda Hispania kutembelea uwanja wa Camp Nou na kushuhudia michezo ya klabu ya Barcelona.
Mshabuliaji Ibrahim Nyagawa (Chuji) wa Schalke 04 ya Dodoma akikokota mpira wakati wa fainali za Kanda ya Kati hizo Morogoro.
Issa Kandula wa Mzinga FC na Delta Thomas wa Ndezi FC wakipambana kwenye fainali za Castle Lager Perfect Six kanda ya ya kati huko Morogoro wikendi hii.

MAZIWA YA ASAS DAIRIES LTD NDIO MAZIWA BORA TANZANIA YASHINDA TUZO YA UBORA KWA MIAKA MIWILI MFULULIZO ,MAKAMPUNI 30 YAACHWA MBALI

$
0
0
Afisa masoko wa kampuni ya maziwa ya Asas  Dairies Ltd ya mkoani Iringa Bw Jimy Kiwelu akishangilia baada ya  kampuni yake  kuwa ndio kampuni  bora ya uzalishaji maziwa nchini Tanzania katika mashindano yaliyofanyika mkoani mara
Watoto  wa mkoa wa Mara  wakishangaa ubora wa maziwa ya Asas kutoka Iringa
Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Dr. Titus Kamani kulia na  viongozi  wengine wakifuatilia maonyesho hayo huku  wakifurahia ubora wa maziwa ya Asas Dairies Ltd.
Picha zaidi BOFYA HAPA

MAKAMU WA RAIS DKT BILAL MGENI RASMI KWENYE HAFLA YA KUCHANGISHA FEDHA KWA AJILI YA MISITU YA MILIMA

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Tanzania Dkt Mohammed Gharib Bilal akizungumza kwenye Hafla ya kuchangisha Fedha za kuwezesha Uhifadhi wa misitu ya milima ya Toa la mashariki kwenye ahotel ya Hyatt Regency Jijini Dar es salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Tanzania Dkt Mohammed Gharib Bilali akizindua Tovuti ya (EAMCEF)kwajili ya kuwezesha kuchangia kwa njia ya mtandao kwenye,Hafla ya kuchangisha Fedha za Uhifadhi wa Misitu ya Milima ya Toa ashariki iliyofanyika kwenye hotel ya Hyatt Regency, Jijini Dar es Salaam.
Makamu waRais wa Jamhuri ya Tanzania Dkt Mohammed Gharib Bilal akimkabidhi picha iliyopigwa mnada Bw Robert Vyampiga wa( DECO) Baada ya Kuinunua kwenye Harambe ya kuchangisha Fedha za Kuwezesha Uhifadhi wa Misitu ya Milima ya Toa la Mashariki iliyafanyika kwenye Hotel ya Hyalt Regency Jijini Dar es Salaam.(Picha OMR}

CUF kutowavumilia watendaji watakaobainika kuendeleza fitna na majungu

$
0
0
 Katibu Mkuu wa CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akizindua kamati tendaji za Wilaya za Pemba katika ofisi za CUF Wilaya ya Chake Chake.
Wajumbe wa  kamati tendaji za Wilaya za Pemba wakianza kikao kwa dua katika ofisi za CUF Wilaya ya Chake Chake.
 Mwenyekiti wa CUF Wilaya ya Magharibi Unguja Bi. Raisa Abdallah Mussa, akizungumza wakati wa uzinduzi wa kamati tendaji kwa Wilaya za Unguja katika ofisi za CUF Wilaya hiyo zilizoko Kilimahewa.
 Baadhi ya wajumbe wa kamati tendaji Wilaya sita za Unguja (CUF) wakisikiliza maelekezo wanayopewa na Katibu Mkuu wa Chama hicho Maalim Seif Sharif Hamad, Kilimahewa Unguja. (Picha na Salmin Said, 
OMKR)
-----------------------------------
Chama Cha Wananchi CUF kimesema hakitowavumilia watendaji watakaobainika kuendeleza fitna na majungu ndani ya chama hicho.
Katibu Mkuu wa Chama hicho Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad ameeleza hayo kwa nyakati tofauti, wakati akizindua kamati tendaji za (CUF) kwa Wilaya zote za Unguja na Pemba.
Kwa upande wa Unguja mkutano huo ulifanyika ofisi za (CUF) Wilaya ya Magharibi zilizopo Kilimahewa, ambapo mkutano kwa Wilaya nne za Pemba umefanyika ofisi za CUF Wilaya ya Chake Chake.
Akizungumza katika Mikutano hiyo Mhe. Maalim Seif amesema chaguzi kwa ngazi za Wilaya sasa zimekamilika na kuwataka watendaji hao kuendelea kukijenga chama, badala ya kuendekeza fitna na chuki ambazo zinaweza kuwagawa wanachama.
Katika hatua nyengine Maalim Seif ametangaza rasmi kuwa Makamu Mwenyekiti wa chama hicho taifa Mzee Machano Khamis Ali hatogombea tena nafasi hiyo kutokana na kuzorota kwa hali ya afya yake.
Hata hivyo amesema Chama kitaendelea kumtunza Mzee Machano kutokana na mchango mkubwa alioutoa katika kukijenga na kukiimarisha chama hicho.
“Mzee Machano ni kisima chetu, na tutaendelea kukitumia hata akiwa nje ya safu ya uongozi wa chama”, alifahamisha Maalim Seif.
Amesema wakati mchakato wa kuchukua fomu kwa ajili ya uchaguzi wa viongozi wa kitaifa ukiendelea hadi tarehe 10/06/2014, nafasi hiyo iko wazi na yeyote anayetaka kugombea nfasi hiyo yuko huru kufanya hivyo.
Ameelezea kuridhishwa na jinsi chaguzi hizo zilivyofanywa kwa uwazi na kupatikana viongozi waliochaguliwa kwa kura nyingi, licha ya kuwepo upinzani mkali katika baadhi ya Wilaya zikiwemo Wilaya ya Mjini na Micheweni, ambapo chaguzi za Wenyeviti zililazimika kurejewa baada ya kukosekana washindi katika duru ya kwanza ya uchaguzi.
Kwa mujibu wa Naibu Katibu Mkuu wa Chama hicho Mhe. Hamad Massoud Hamad, kwa mara ya kwanza chama hicho kimepata mwenyekiti wa Wilaya mwanamke ambapo wajumbe wa mkutano mkuu Wilaya ya Magharibi walimchagua Bi. Raisa Abdalla Issa kuwa Mwenyekiti wao.
Mhe. Hamad Massoud alisema uchaguzi kwa upande wa Unguja ulikuwa wa aina yake kwani bila ya kutarajiwa wajumbe wa mikutano mikuu Wilaya za Unguja waliwachagua wajumbe 47 wanawake kati ya wajumbe 94 waliochaguliwa, na kufanya idadi sawa katika ya wanawake na wanaume wanaounda kamati tendaji za Wilaya za Unguja.

Viewing all 110167 articles
Browse latest View live




Latest Images