Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 458 | 459 | (Page 460) | 461 | 462 | .... | 3278 | newer

  0 0

   Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Tanzania Silas Mwakibinga akiwaonesha waandishi wa habari uthibitisho wa malipo ya shilingi milioni 400 ikiwa ni sehemu ya pili ya malipo kwa ajili ya Ligi Kuu.
   Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Azam Media Rhys Torrington (kulia) akimkabidhi  Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Tanzania Silas Mwakibinga nakala ya uthibitisho wa malipo ya fedha kwa ajili ya Ligi Kuu ya Vodacom. 
  KAMPUNI ya Azam Media imetangaza kuwa tayari imeshatuma fedha kwa Bodi ya Ligi kwa ajili ya msimu wa ligi wa Vodacom kwa mwaka 2014/ 2015.
  Fedha hizo zimetolewa mapema zaidi kwa ajili ya kusaidia maandalizi mapema kwa timu kama ilivyokubaliwa kwenye mkataba wa miaka mitatu ya udhamini wao katika ligi hiyo.

  Akizungumza na waandishi wa habari jana katika ofisi za Azam zilizopo Tazara, Dar es salaam, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Azam Media, Rhys Torrington, alisema kuwa kampuni hiyo inavutiwa na aina nzuri ya ushirikiano kati yake na bodi ya Ligi.

  Alisema kuwa kupitia bodi hiyo Azam imepiga hatua kubwa katika kufanikisha adhma yake ya kuifanya Ligi hiyo ya Vodacom kuwa ya kuvutia zaidi.
  “Ligi hii tunataka kuifanya kuwa ni moja kati ya ligi zinazovutia na kuonesha ushindani barani Afrika, ingawaje ninajua kuwa kuna mengi ambayo yanatakiwa kuendelea kufanywa ili kuipa nguvu zaidi ligi hii”alisema Torrington. Alisema kuwa kwa kutambua hilo ndio maana Azam Media imehakikisha kuwa klabu zote zinapata fedha mapema ili kusaidia suala zima la maandalizi.

  Akizungumzia mikakati ya baadae ya Azam Media alisema kuwa inatarajia kuanza kuonesha soka la mitaani (street soccer) mbalimbali moja kwa moja (live) itakayokuwa ikiendelea kwenye nchi za Kenya na Uganda.

  Alisema kuwa kwa sasa Azam Media imeanza kujikita katika nchi za Kenya, Uganda na Malawi ambapo itakuwa ikiuza ving’amuzi vyake katika nchi hizo. Aliongeza kuwa pia katika kuhakikisha kuwa inatoa mwanya zaidi wa vipindi vizuri na vya kuvutia inaendelea na vipindi vya michezo vya Morning Trumpet, sport@8 pamoja na Kwetu House.

  Kwa upande wake Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya ligi, Mr Silas Mwakibinga alisema kuwa kwa hatua hiyo ya Azam ya kuhakikisha upatikanaji wa fedha hizo kwa wakati ni nzuri na itasaidia kuzipatia timu muda mzuri wa kujiandaa. Alisema kuwa bodi yake inavutiwa sio tu na utangazaji wa vipindi unaofanywa na Azam bali pia hata nia yao ya kuendeleza soka la Tanzania.

  Azam Media ilisaini mkataba wa miaka mitatu na wenye thamani ya TSHS5,560,800,000 kuonesha mechi za live na za kurekodi mechi za Ligi Kuu na fedha hizo zinalipwa kwa awamu tatu.

  0 0

  Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe.Hussen Mwinyi (katikati), akikata utepe kuzindua rasmi kiwanda cha kutengezea vifaa vya ujenzi cha Uturuki STONE BLOCK BUILDING. Jun 2,2014.kilichopo Kawe Mbezi Beach jijini Dar es Salaam (wakwanza kushoto), Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiki, Balozi wa Uturuki nchini Tanzania Ali Davutoglu na maofisa wa Uturuki.
  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiki wakijadiliana jambo na Balozi wa Uturuki nchini Tanzania Ali Davutoglu, wakati wa uzinduzi wa kiwanda hicho.
  Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe.Hussen Mwinyi (kushoto), akijadiliana jambo na Balozi wa Uturuki nchini Tanzania Ali Davutoglu,wengine ni maofisa kutoka Uturuki.
  Wageni waalikwa wakiangalia burudani.
  Vijana wa kabila la Kimasai wakitoa burudani.
  Deus Kamwela, kutoka kikundi cha sanaa KCC akionyesha umahiri wake wa viongo.
  Wafanyakazi wa kiwanda hicho.
  Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe.Hussen Mwinyi,akiwa na Balozi wa Uturuki nchini Tanzania Ali Davutoglu.wakiwa wameambatana maofisa wengine wa Uturuki wakikagua kiwanda hicho. PICHA NA PHILEMON SOLOMON

  0 0

  Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko kifo cha Mwakilishi wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Mara (FAM) katika Mkutano Mkuu wa TFF, William Chibura kilichotokea leo asubuhi (Juni 3 mwaka huu) katika Hospitali ya Mkoa wa Mara mjini Musoma.

  Chibura aliyezaliwa mwaka 1969 alikuwa mjumbe wa Mkutano Mkuu wa TFF akiwakilisha klabu za Mkoa wa Mara kupitia FAM. Aliwahi kuichezea Musoma Shooting, na baadaye kuwa kiongozi katika klabu hiyo na ile ya Polisi Mara iliyoko Ligi Daraja la Kwanza (FDL).

  Hadi mauti yanamkuta alikuwa kiongozi wa Butiama FC, na mwakilishi wa klabu Chama cha Mpira wa Miguu Wilaya ya Butiama (MUFA) kwenye Mkutano Mkuu wa FAM.

  Msiba huo ni mkubwa katika fani ya mpira wa miguu nchini kwani, Chibura enzi za uhai wake alitoa mchango mkubwa katika mchezo huu tangu akiwa mchezaji na baadaye kiongozi.

  TFF tunatoa pole kwa familia ya marehemu Chibura, Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Mara (FAM), Jeshi la Polisi Tanzania na kuwataka kuwa na subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha msiba huo mzito.

  Taratibu za mazishi zinaendelea kufanywa na familia yake kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi Tanzania- Mkoa wa Mara, kwani marehemu Chibura alikuwa mtumishi wa jeshi hilo. TFF tunasubiri taratibu hizo ili tujipange jinsi ya kushiriki katika msiba huo.

  Bwana alitoa, na Bwana ametwaa. Jina lake lihimidiwe. Amina

  BONIFACE WAMBURA
  OFISA HABARI NA MAWASILIANO
  SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

  0 0

  NA RAMADHANI JUMA
  OFISI YA MKURUGENZI-KALAMBO

  OFISI ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Kalambo Mkoa wa Rukwa kupitia kitengo cha UKIMWI kimetumia zaidi ya shilingi milioni 8.5 kwa ajili ya kuimarisha mapambano dhidi ya ugonjwa huo katika wilaya hiyo.

  Fedha hizo zimetumika kuwanunulia wanafunzi yatima wanaoishi katika mazingira magumu sare za shule, viatu pamoja vifaa vya kujifunzia ikiwemo madaftari na kalamu, ambapo Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Godfrey Sichona alikabidhi kwa walengwa kwa niaba ya Halmashauri.

  Pia Halmashauri hiyo imenunua vifaa vya muziki kwa ajili ya vikundi viwili vya Sayuni kilichopo kata ya Legezamwendo na Sayuni cha Kata ya Mambwenkoswe ili vihamasishe wananchi kujikinga na ugonjwa huo.

  Baadhi ya vifaa vya muziki vilivyotolewa na Halmashauri hiyo ya Kalambo ni gitaa tatu kila kikundi, spika, maikrofoni, genereta pamoja na vifaa vingine vya umeme.

  Akizungumza wakati wa kukabidhi misaada hiyo, mwenyekiti huyo aliwakumbusha wakazi wa wilaya ya Kalambo na Mkoa wa Rukwa kwa ujumla kuwa, mapambano dhidi ya UKIMWI sio ya serikali pekee bali ni jukumu la kila mwanajamii zikiwezo taasisi za dini.

  Naye mwenyekiti  wa kamati ya Kudhibiti UKIMWI wilaya ya Kalambo Faustine Mwanisenga aliwataka wanavikundi waliopatiwa msaada wa vifaa vya muziki na Halmashauri hiyi kuvitunza na kuvitumia vizuri ili kufikia malengo yaliyokusudiwa.
  MWENYEKITI wa Halmashauri ya wilaya ya Kalambo Mkoa wa Rukwa Godfrey Sichona (mwenye suti) na Makamu wake Faustine Mwanisenga wakikagua gitaa wakati walipokabidhi vifaa vya muziki kwa vikundi viwili vya Kwaya katika Kata za Legezamwendo na Mambwenkoswe ili visaidie mapambano dhidi ya UKIMWI kwa njia ya nyimbo wilayani humo Kulia ni mratibu wa UKIMWI wa wilaya hiyo Mariam Kimashi.
  MWENYEKITI wa Halmashauri ya wilaya ya Kalambo Mkoa wa Rukwa Godfrey Sichona akikabidhi sare kwa mrataibu wa Elimu wa Kata ya Legezamwendo ili zigawanywe kwa wanafunzi yatima na wanaoishi katika mazingira magumu.

  0 0


  0 0

   Diwani wa kata ya Mgama Denis Lupala akizungumza na wanafunzi wa shule ya sekondari ya Mgama wakati alipowatembelea na kula pamoja chakula cha mchana.
   Diwani wa kata ya Mgama Denis Lupala akizungumza na mwalimu mkuu wa shule hiyo Simeone Lihuluku. 
   Diwani wa kata ya Mgama, Denis Lupala akimpakulia chakula mmoja wa wanafunzi wa shule ya sekondari ya Mgama wakati alipowatembelea na kula pamoja chakula cha mchana
  baadhi ya wanafunzi shule ya sekondari ya Mgama wakiwa katika foleni ya chakula kilichoandaliwa na diwani wa kata ya Mgama Denis Lupala.


  Na Denis Mlowe,Iringa

  SHULE ya sekondari Mgama iliyoko katika kata ya Mgama jimbo la Kalenga wilaya ya Iringa Vijijini inakabiliwa na changamoto ya upungufu wa matundu ya vyoo  30 yaliyopo 12 na miundo mbinu mibovu.
   
  Akizungumza na mwandishi wa habari hizi wakati wa hafla iliyoandaliwa na diwani wa kata hiyo Denis Lupala,Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Simeone Lihuluku alisema kuwa licha ya upungufu wa matundu ya choo shule hiyo inakabiliwa na ukosefu wa maktaba na maabara kwa wanafunzi wanaosoma shuleni hapo tangu kuanzishwa kwake miaka saba iliyopita.
   
  Luhuluku alisema  shule hiyo inakabiliwa na ukosefu wa mabweni ya wanafunzi na nyumba za kuishi walimu kitu kinachochangia wanafunzi kupanga mbali na maeneo ya shule changamoto inayosababisha ufaulu hafifu kutokana na utoro pamoja na upatikanaji wa mimba kwa watoto wa kike.

  Alisema mwaka huu tayari wanafunzi watatu wamekatisha masomo kutokana na kupata ujauzito huku nyumba za walimu zinazohitajika zikiwa 18 na zilizopo kwa sasa ni nyumba mbili za walimu.
   
  “Licha ya upungufu wa matundu ya vyoo vilevile tunakabiliwa na changamoto nyingi sana katika shule hii lakini kubwa zaidi ni ukosefu wa maabara na maktaba kwa ajili ya wanafunzi na tumekuwa tunatumia chumba kimoja cha darasa kama maabara kitu kinachosabisha wanafunzi kutosoma vizuri na kupunguza ufaulu naomba sana wadau waweze kuwasaidia kuondokana na changamoto hizi” alisema Lihuluku
   
  Aliongeza kuwa shule hiyo imekosa huduma ya umeme,vyanzo vya kuaminika vya maji safi na vifaa vya kufundishia pamoja na uchangiaji hafifu wa michango ya shule kwa wazazi.
   
  Kwa upande wao wanafunzi  wa shule hiyo wamemshukuru diwani huyo kwa kuwaandalia chakula huku wakimuomba kuwasaidia kutatua changamoto zinazowakabili katika shule yao kwa lengo la kuongeza ufaulu shuleni hapo.

  Shule ilianzishwa mwaka 2007 ikiwa inatoa elimu ya kidato cha kwanza hadi cha nne ikiwa na jumla ya wanafunzi 516 kati ya hao wavulana wakiwa 221 na wasichana 295 na walimu 20.

  0 0

  Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Eng. Angelina Madete (kulia) akipata taarifa kutoka kwa mkuu wa shule ya Sekondari Lumala iliyoko Wilayani Ilemela katika Mkoa wa Mwanza Bw. Christopha kuhusu mradi wa miche iliyopandwa katika shule hiyo.kwenye ziara ya wiki ya Mazingira Duniani.
  Baadhi ya walimu wa shule ya Sekondari Lumala wakisikiliza kwa makini maelezo yanayotolewa na Naibu Katibu Mkuu (hayupo pichani)kuhusu masuala ya utunzaji Mazingira na upandaji miti.
  Naibu Katibu Mkuu Eng. Angelina Madete (katikati) akijibu maswali aliyoulizwa na walimu wa shule hiyo (hawapo pichani) kuhusu suala zima la siku ya Mazingira Duniani.

  0 0

  Mkuu wa Mkoa Singida Dkt. Parseko V. Kone akizungumza na
  waandishi wa habari juu ya mbio za mwenge wa uhuru Mkoani Singida kulia
  kwake ni katibu Tawala Mkoa wa Singida Liana Hassan.
   Wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama Mkoa wa Singida (wa
  kwanza ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida ACP Geofrey Kamwela)
  wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Parseko V. Kone muda mfupi
  kabla ya kuelekea kijiji cha Rungwa tayari kwa kuupokea Mwenge wa Uhuru
  Mkoani Singida.
    Wakimbiza Mwenge Mkoa wa Singida wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa
  wa Singida Dkt. Parseko V. Kone muda mfupi kabla ya kuelekea kijiji cha
  Rungwa tayari kwa kuupokea Mwenge wa Uhuru Mkoani Singida.

  ========  =========
  Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt.Parseko V. Kone  amewataka wananchi Mkoani  humo kushirikiana katika kusimamia miradi itakayowekewa mawe ya msingi na Mwenge wa Uhuru  ili thamani halisi ya fedha zitakazotumika iweze kupatikana na miradi hiyo kukamilika kwa wakati.

  Dkt. Kone ametoa wito huo leo asubuhi katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa
  Mkoa wakati akiongea na waandishi wa habari juu ya mbio za mwenge wa uhuru   kwa mwaka 2014 Mkoani Singida zitakazoanza rasmi kesho asubuhi.

  Amesema Mwenge wa Uhuru unatarajiwa kupokelewa katika kijiji cha Rungwa  Tarafa ya Itigi Wilaya ya Manyoni ukitokea Mkoani Mbeya na utakimbizwa  katika halmashauri sita za Mkoa wa Singida kisha kukabidhiwa Mkoa wa Dodoma, Wilaya ya Chemba kijiji cha Kinyamshindo tarehe 10 Juni 2014.

  Dkt. Kone ameongeza kuwa Mwenge wa uhuru utazindua, kuweka mawe ya msingi na kutembelea miradi 60 yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 5.9 katika sekta za afya, elimu, maji, barabara, kilimo,ufugaji, ushirika,
  misitu na sekta binafsi.

  Aidha amewasihi wananchi kufika katika maeneo ambapo salamu za Mwenge zitatolewa ili kupata na kuuzingatia ujumbe huo. Dkt. Kone ameongeza kuwa moja ya ujumbe wa mwenge ni suala la kukamilisha mchakato wa katiba mpya huku akisisitiza wananchi kutumia haki yao ya kidemokrasia ya kushiriki katika mchakato huo bila ya kuathiri umoja, amani na utulivu wa nchi yetu.

  Amesema mbio za Mwenge wa uhuru kwa mwaka 2014 zimebeba ujumbe usemao  “Katiba ni sheria kuu ya  Nchi” huku kauli mbiu ikiwa ni “Jitokeze kupiga kura ya maoni tupate Katiba Mpya” Pia ujumbe huo utaambatana na kauli za uhamasishaji jamii kupitia ujumbe wa kudumu wa Mwenge kuhusu mapambano dhidi ya Ukimwi yenye kauli mbiu  isemayo “Maambukizi mapya, unyanyapaa na vifo vitokanavyo na Ukimwi sifuri”.

  Mapambano dhidi ya rushwa yatahamasishwa kwa kauli mbiu isemayo “Palipo na rushwa hakuna maendeleo” wakati huohuo kauli mbiu ya mapambano dhidi ya dawa za kulevya itakuwa ni “Furahia afya yako sio dawa za kulevya”.

  0 0

  WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo Dk. Fenella Mukangara keshokutwa anatarajiwa kuzindua Siku ya Msanii Tanzania katika sherehe zitakazofanyika katika hoteli ya Sea Cliff Dar es Salaam. Akizungumza jana mjini Dar es Salaam, Ofisa Habari wa Mradi wa Siku ya Msanii Tanzania, Petter Mwendapole, alisema Dk. Mukangara amepewa jukumu hilo kutokana wizara yake kuhusika moja kwa moja sanaa. “Waziri amekubali jukumu la kuwa mgeni rasmi kwa sababu wizara yake ndio mama wa wasanii, na anaelewa matatizo ya wasanii na amekubali kuwa kulibeba jukumu hilo na atakuwepo na timu nzima ya wizara,” alisema. Mkurugenzi wa Masoko wa Basata wa Vivian Shaluwa alisema siku ya Msanii ilibuniwa mwaka 2004 lakini Tanzania iliamua kuichukua na kuianzisha mwaka 2008 lakini baada ya mchakato wa muda mrefu, kampuni ya Haak Neel imepewa jukumu la kusimamia kazi hiyo. 
  “Siku ya Msanii itahusisha sanaa mbalimbali kuanzia urembo, muziki wa dansi, uchoraji, unenguaji, lakini pia siku ya Msanii ambayo tamati yake itakuwa Oktoba 25 itakuwa na tuzo za aina mbalimbali kutambua mchango wao,” alisema. 
  Kwa upande wake Mkurugenzi wa Haak Neel Production, Godfrey Katula alisema kampuni yake imejiandaa vyema kusimamia shughuli hiyo na kuwataka wadau mbalimbali kuhakikisha wanatumia vyema siku ya Msanii katika kutambulisha kazi. 
  “Haak Neel imejipanga kushirikiana na wasanii katika kutambua siku yao, tumeona kuna siku ya wanawake duniani, kuna Mei Mosi, kwa ajili ya wafanyakazi, kuna siku ya ukimwi kwa hiyo hii ni heshima kwa wasanii kutambuliwa kwa siku yao.” 
  Mbali na viongozi wa BASATA, Kamati ya Siku ya Msanii inahusisha wasanii kutoka sekta mbalimbali za sanaa ambao ni pamoja na Philemon Mwasanga, Asia Idarous, Kimera Billa, Abdul Salvador, Adrian Nyangamale, Sulemani Ling’ate.
   Mkurugenzi wa Masoko wa BASATA, Vivian Shalua akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari.  Ofisa Habari wa Msanii Day, Peter Mwendapole waliokaa wa kwanza kulia akizungumza  na waandishi wa habari juu ya siku hiyo.
  Mkurugenzi wa Masoko wa Baraza la Sanaa Tanzania ( Basata ),Vivian Shalua akiongea na waandishi wa habari juu ya siku ya Msanii Tanzania. Kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Haak Neel Production Godfrey Katula akifuatiwa na Ofisa habari wa Msanii Day, Peter Mwendapole na Ofisa Masoko wa Msanii Day Catherine Metili (kulia) na wajumbe wengine.

  0 0

  Mr. Japhet Mwaisupule, Minister Plenipotentiary from the Ministry of Foreign Affairs and International Cooperation reading Tanzania's statement to the NAM Ministerial Conference on behalf of Dr. Mahadhi Juma Maalim, Deputy Minister for Foreign Affairs and International Cooperation. Behind him are Mr. Noel Kaganda, First Secretary (left) from the Tanzania 's Permanent Mission to the United Nations in New York and Ms. Eva Ng'itu, Second Secretary at the Ministry's Headquarters
  ----------------------------
  Tanzania participated in the 17th Non-Aligned Ministerial Conference, which ended in the Algerian capital, Algiers, on May 29.
  The conference, which was opened by Algerian Prime Minister Abdelmalek Sellal on behalf of President Abdelaziz Bouteflika, adopted a final document asserting NAM’s position on global political, development and social issues, ranging from reform of the United Nations, peacekeeping operations, terrorism, disarmament, post-2015 development agenda to food security.
  The ministers also adopted the Algiers Declaration and five other specific statements, including reaffirmation of support for Palestinian nationhood, nuclear non-proliferation and a vote of thanks to Algerian Foreign Minister Ramtane Lamamra and the host country.
  The conference, which was held at the Palace of Nations, was attended by almost all the 120 members of the movement, many of whom made statements. Speaker after speaker reaffirmed the relevance and validity of NAM in bringing the members together to address emerging global challenges.
  The Tanzanian statement was read by Mr. Japhet Mwaisupule, Minister Plenipotentiary, on behalf of the Deputy Minister for Foreign Affairs and International Cooperation, Dr. Mahadhi Juma Maalim.
  Tanzania urged NAM to continue pressing for fair and just economic, financial and trading multilateral institutions. Reform of these institutions “will not be complete without involving the United Nations Security Council. We must stand together in calling for early reform of the Council so as to make it more effective and responsive to the aspirations of all members,” said the statement.
  It also called for new trade and investment rules that work for the benefit of developing countries to facilitate implementation of the global development agenda.
  The Ministerial Conference, which was preceded by a Senior Officials Meeting, was addressed by His Excellency Ivo Morales, President of Bolivia, in his capacity as Chairman of G-77 plus China.

  0 0

  WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amesema Tanzania ni miongoni mwa nchi za kwanza katika Jumuiya ya Afrika Mashariki kuingia kwenye ubia na sekta binafsi katika mradi mkubwa wa usafirishaji abiria. Ametoa kauli hiyo leo mchana wakati akifungua Mkutano wa Majadiliano yenye lengo la kuutangaza mradi wa mabasi yaendayo kasi kwenye ukumbi wa Mlimani City. Mkutano huo wa siku mbili, utamalizika kesho.
  Waziri Mkuu amesema kutèkelezwa kwa mradi huo kutatoa fursa za ubunifu utakaowezesha kupatikana kwa suluhisho la usafiri mijini na hasa kwenye miji ambayo inakua kwa kasi barani Afrika. 
   "Mbali ya kutoa huduma za hali ya juu, za haraka na ambazo siyo ghali kwa wakazi wa Jiji la Dar es Salaam, nia ya Serikali ni kuona mfumo mpya wa matumizi ya kadi kwenye mpango huu wa usafiri unatumika ipasavyo," alisema. 
   Alisema ni matumaini ya Serikali kwamba wadau kutoka sekta binafsi ambao ni wazawa na wa kutoka nje ya nchi watashiriki kwenye mradi huu ili uweze kuboresha matumizi ya kadi ambayo mtu hatatakiwa kulipia fedha taslimu akiwa ndani ya basi bali kutumia kadi anayoilipia kabla ya kuingia ndani ya basi husika. 
   Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kufungua mkutano huo, Waziri Mkuu alisema Serikali iliamua kuanzisha mradi huo ili kupunguza msongamano wa magari kwenye barabara za Jiji la Dar es Salaam. 
   "Hii ni awamu ya kwanza ambayo inakaribia kukamilika na inaanzia Kimara hadi Kivukoni na itakuwa na matawi mawili ya Morocco na Karikoo. Mradi wote una awamu sita za ujenzi kuelekea maeneo tofauti ya Jiji," alisema. 
   Mbali na mradi huo wa mabasi yaendayo kasi, Serikali inaangalia uwezekano wa kutumia usafiri wa majini kwa kutumia boti kati ya Dar es Salaam na Bagamoyo kama njia mojawapo ya kupunguza msongamano wa magari jijini Dar es Salaam. 
   “Vilevile tutaimarisha usafiri wa reli kama njia nyingie ya kupunguza tatizo hili. Dk. Mwakyembe (Waziri wa Uchukuzi) ameanza na sote tumeona ni jambo linalowezekana. Cha msingi ni kuimarisha tu usafiri huu,” aliongeza Waziri Mkuu. 
   Mapema, akiwakaribisha wajumbe wa mkutano huo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI), Bibi Hawa Ghasia alisema Serikali imedhamiria kuhakikisha kuwa mradi huo unafanikiwa. Pia alitumia fursa hiyo kuishukuru Benki ya Dunia ambayo alisema imetoa kiasi cha dola za Marekani milioni 200 kwa ajili ya kufadhili mradi huo. 
   Mkutano huo unawashirikisha wadau mbalimbali wakiwemo wa ndani na wa nje wanaotarajiwa kutoa huduma za mabasi makubwa na madogo, utoaji tiketi, ulinzi, usafi na huduma za maduka.
    Waziri Mkuu, izengo Pinda  akifungua Mkurano wa Majadiliano wa Kutangaza Mradi wa Mabasi yaendayo haraka (Dar Rapid Transit) kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam,  leo Juni 3, 2014.
   Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na baadhi ya washiriki wa Mkutano wa Majadiliano wa Kutangaza Mradi wa Mabasi yaendayo haraka kwenye ukumbi wa Mlimani City jijiniDar es salaam Juni 3, 2014. Kulia kwake ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe Hawa Ghasia
  Waziri Mkuu,, Mizengo Pinda akizungumza na   Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia nchini, Bw. Philippe Dongier baada ya kufungua  Mkutano waMajadiliano wa kutangaza Mradi wa Mabasi yaendayo  haraka kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam  leo Juni 3, 3014. 
  Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

  0 0
 • 06/03/14--10:27: APPRECIATION


 • 0 0
 • 06/03/14--10:41: Article 3


 • 0 0


  CNN's African Voices highlights Africa's most engaging personalities. Recently, African Voices met Patrick Ngowi who founded his own solar power company in Tanzania at just 22 years.


  Showtimes were: (all times GMT
  Friday: 0730 
  Saturday: 1430 
  Sunday: 0230, 0800, 1730 
  Monday: 0930, 1430 
  Tuesday: 0430


  0 0

  Watuhumiwa wa  wizi wa mali  zilizokuwa  zikisafirishwa na lori la kampuni ya Dandu 
  Hili ndilo lori  lililokuwa na mali  hizo  chini kukiwa na ubichi wa mafuta  ya taa yaliyomwagwa ili  kulilipua lori hilo bila mafanikio 
  Mwonekano wa lori hilo kwa ndani baada ya mali zote  kuhamishwa 
  Kamanda wa polisi mkoa wa Iringa Afande Ramadhan Mungi akionesha  lori hilo mali ya kampuni ya Dandu ambalo limechomwa moto na dereva na utingo wake baada ya  kufaulisha mali zote kwa lengo la kuiba 
  JESHI la  polisi  mkoa  wa Iringa kupitia dhana ya polisi  jamii na ulinzi shirikishi  limefanikiwa  kukamata  mali za wizi zilizokuwa  zikisafirishwa kwenda nchi ya DRC Kongo zikiwa na thamani ya  Tsh milioni 100 pamoja na lori  lenye thamani  ya Tsh milioni 100 ambalo liliteketezwa kwa  moto kabla ya dereva na utingo wa  lori hilo  kulichoma moto kama njia ya kupoteza ushahidi. 
  Imedaiwa  kuwa  watu  zaidi ya sita   wanashikiliwa na  jeshi  hilo la polisi akiwemo  dereva  na utingo  wake ambao wanadaiwa  kuhusika na tukio  la wizi  huo.
  Kamanda  wa  polisi mkoa  wa  Iringa Ramadhan Mungi  alisema  kuwa  tukio hilo  lilitokea juzi May 31 ambapo  askari  wa  doria  wilaya ya Mufindi  wakiwa katika shughuli   hiyo ya doria  walifanikiwa  kuliona  lori hilo  likiwa  limeegeshwa kando ya  barabara ya Iringa –Mbeya  eneo la Kinegembasi wilaya ya Mufindi  huku likiwa  limeteketea kwa moto katika kibini yake.
  Alisema kuwa  watu hao waliteketeza lori lenye namba za usajili  T527 DPQ likiwa na tela lenye namba  T 974  EFE  aina ya  scania mali ya kampuni ya Dandu ambalo  walilikuta  likiungua   huku silizi  zake zikiwa  zimefunguliwa na  baada  ya uchungu wa awali  walibaini  kuwa lori hilo  lilikuwa limebeba mitumba na viatu  na baada ya msako  ndipo  walipofanikiwa  kukuta mitumba  hiyo  ikiwa imefichwa katika  nyumba moja kuukuu mali ya mama  Gray Mpinga  mwenyeji wa Maguhani Mufindi.
  Alisema  kuwa mali  hizo ambazo ni mabelo ya mitumba na viatu  yalitoka Bandarini kwenda DRC  chini ya  dereva wa  lori hilo ni Enedia Christian (26) mkazi wa Mbeya  na utingo wake  Deus  Gendo (20) mkazi wa Mbeya .
  Kamanda  Mungi  alisema kuwa utingo na dereva wa  lori hilo baada ya kufika kijiji  hicho cha Maguhani  walivunja kontena na  kushusha mali zote na kuzihifadhi katika  nyumba   hiyo kabla ya  kutafuta mteja na kisha  lori  kulichoma moto.
  Alisema kuwa  baada ya  kufanya  wizi huo  walitoweka na simu zao kuzimwa na kutokana na jitihada za  jeshi la  polisi  kupitia mtandao wa kimawasiliano wa kuthibiti na wizi  wa mitandaoni  walifanikiwa  kuwanasa  watuhumiwa hao wakiwa kijiji cha Nyololo.
  Mbali ya kuwakamata  dereva na  tingo  pia  polisi  wamekamata  watu  mbali mbali  wahusika  wa mtandao huo na kuendelea  kumsaka Masko Buhewa mkazi wa Nyololo kwa  kuhusika na umilikiwa wa mtandao huo.

  0 0

  Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki leo wameendelea na mchakato wao wa  kumuondoa spika  Mhe. Dkt. Margaret Nantongo Zziwa,  baada mahakama ya Afrika ya Mashariki ( East Africa court of Justice) jijini Arusha kukataa kuzuia zoezi la kumuondosha katika kiti hicho.
  Ripota wetu anataarifu kutoka huko kuwa bunge liliahirishwa kukutana tena leo asubuhi baada ya suluhu kukosekana. "Hili linazuia mchakato mzima wa bajeti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kusomwa", Mbunge mmoja alisikika kusema. 
  Habari kutoka ndani ya Bunge hilo zinasema baadhi ya Wabunge wa Tanzania katika bunge hilo wameondoa saini zao na kusema kuwa wao hawaungi mkono  kumuondoa Spika huyo madarakani, jambo ambalo limeleta zongo zaidi bungeni leo.
  Wabunge walioondoa saini ni Mh Maryam Ussi Yahya, Mh Adam Kimbisa na Mh Shyrose Bhanji. Wabunge kutoka Tanzania -  Mh Abdullah Mwinyi na Mh Nderakindo Kessy, inasemekana hawakutana kuondoa saini zao.
  Tayari barua ya kuomba saini za Wabunge wa Tanzania ziondolewe katika orodha za wanaopinga imeshaandaliwa na kupelekwa kunakohusika.
  Bunge hilo lililoanza Mkutano wake wa Tano mwezi Machi 26, mwaka huu, kwa ufunguzi uliofanywa na Mwenyekiti wa EAC ambaye pia ni Rais wa Kenya, Mhe. Uhuru Kenyatta, lilipangwa kumaliza shughuli zake Aprili 4.
   Lakini haikuwa hivyo. Kiti cha Spika kiliwaka moto na mwishowe alikipooza kiti kwa kuahirisha Bunge kwa muda usiojulikana. Spika alitumia kifungu cha kanuni ya 82(2) ya kanuni za mwenendo wa Bunge hilo kufafanua kanuni.

  Inasemekana kwamba Wabunge 36 kati ya 44 hawamtaki. wakimtupia shutuma za  kuwagawa wabunge na kupoteza imani kwao.Wanamtuhumu kwa kuliongoza bunge hilo bila kuwa na viwango na ujuzi mdogo wa uongozi, matumizi mabovu ya ofisi, dharau kwa wabunge wenzake inayoambatana na matumizi ya lugha chafu na ubabe kwenye vyombo vya habari dhidi ya wabunge na hivyo kuvunja heshima ya wabunge hao mbele ya jamii. 
  Mazingira ya kuwaka moto kiti yalijitokeza Aprili Mosi mwaka huu, majira ya saa 10 jioni baada ya hoja ya kumuondoa kwenye kiti kuwasilishwa bungeni na Mbunge wa Kenya, Peter Mathuki.

   Dk Zziwa anasema tuhuma dhidi yake zinatokana na yeye kugoma kupandisha mishahara yao, na kwamba  baadhi ya wabunge walikuwa wakidai nyongeza ya asilimia 100 ambayo ingeongeza maradufu mishahara yao hadi kufikia dola za Marekani 10,000 (Sh 16.25 milioni.

  Alisema ameshindwa kukubaliana nao ndiyo maana sasa wamemtafuta mbunge mwingine ambaye ameahidi kuwatekelezea nyongeza hiyo hadi asilimia 200 kama watamchagua kuwa Spika.

  Kuhusu suala la uwezo wake kiutendaji na madai ya kufanya kazi kwa kiburi, alisema inatokana na hatua yake ya kulivalia njuga suala la wabunge kupokea posho na baadaye kutohudhuria vikao.

  wabunge wa EALA walimchagua Dk Zziwa kuwa Spika wao kwa kipindi cha miaka mitano, Katika ukumbi wa bunge wa jengo la Mikutano la Kimataifa la Arusha (AICC), Juni 5, mwaka juzi katika Uchaguzi uliojaa ushindani mkubwa kati yake na mpinzani wake, Dora Byamukama.

  Wagombea wote hao ni wanasheria wakitokea Uganda kwa kuwa awamu hii ni zamu ya nchi hiyo kutoa Spika baada ya Tanzania na Kenya kumaliza zamu zao. Iwapo wabunge watafanikiwa kumng’oa Dk Zziwa nafasi hiyo itaendelea kubakia Uganda.

  Inasemekana uchaguzi huo ulizua  makundi ya kampeni na wapambe wao. Matokeo ya uchaguzi yalipotangazwa, mpinzani wake alikataa kumpa mkono wa kumpongeza, hawakuweza kukumbatiana kama ishara ya kukubali kushindwa na kushinda na kuahidi kufanya kazi kwa pamoja. Aliendelea kununa na inawezakana mpaka sasa bado amenuna wakiwamo wapambe wake.

  0 0

  Waziri wa Uchukuzi, Dr. Harrison Mwakyembe akiongea wakati wa kuwakaribisha ujumbe wa maafisa wa serikali kutoka jimbo la Katanga nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Jumatatu usiku katika uwanja wa kimataifa wa Julius Nyerere.  Wengine ni Naibu Gavana wa Jimbo hilo, Bw. Yav Guilbert (kushoto) na Waziri wa Uchukuzi wa Jimbo hilo, Bw. Kahozi Sumba (kulia). Ujumbe huo upo nchini kuimarisha mahusiano kati ya nchi hizo.


  0 0


  Kikosi cha timu ya soka ya Panone fc ya Mkoani Kilimanjaro.
  Wachezaji wa timu ya Panone fc ya mkoani Kilimanjaro wakishangilia baada ya kuifunga tmu ya Town Small Boys na kufanikiwa kutinga ligi daraja la kwanza. Picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0
 • 06/03/14--20:00: ngoma azipendazo ankal

 • Jagwa Music @ Roskilde Festival 2011

  0 0

  Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa (katikati)akikabidhiwa vifaa vya usafi vyenye thamani ya sh.mil. 15 na Ofisa Uhusiano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Dorris Malulu katika 
  hafla iliyofanyika, Ilala, Dar es Salaam, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani. Wafanyakazi wa TBL walishiriki kufanya usafi eneo la Karume, Ilala. Kushoto ni Meneja  
  Uhusiano wa TBL, Emma Oriyo.
   Meneja wa Uhusiano Mambo ya Nje wa Kampuni ya Bia Tanzania  (TBL), Emma Oriyo (kushoto) akishiriki na viongozi mbalimbali kufanya usafi, Ilala, Dar es Salaam juzi, katika  maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani Dar es Salaa
   Meneja wa Uhusiano Mambo ya Nje wa Kampuni ya Bia Tanzania  (TBL), Emma Oriyo (kushoto) akishiriki na viongozi mbalimbali kufanya usafi, Ilala, Dar es Salaam juzi, katika  maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani Dar es Salaam.
   Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa,(wa pili kulia) akishiriki na viongozi mbalimbali  na wafanyakazi wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), kufanya usafi Ilala, Dar es Salaam, 
  katika  maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani.
   Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa (katikati) akikabidhiwa vifaa vya usafi vyenye thamani ya sh.mil. 15 na Ofisa Uhusiano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Dorris Malulu katika 
  hafla iliyofanyika, Ilala, Dar es Salaam, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani. Wafanyakazi wa TBL walishiriki kufanya usafi eneo la Karume, Ilala. Kushoto ni Meneja  
  Uhusiano wa TBL, Emma Oriyo.

older | 1 | .... | 458 | 459 | (Page 460) | 461 | 462 | .... | 3278 | newer