REGIONAL CHAMPIONS LEAGUE (RCL) 2014
↧
↧
MISA YA MSIBA DMV
Dada Sarah Mushi wa Ashburn, VA anapenda kuwajulisha na kuwaomba mjumuike nae katika misa ya mpendwa mama yake mzazi Mrs. Aruken Geoffrey Mushi itakayofanyika Jumamosi June 7, 2014 katika kanisa OUR SAVIOR'S WAY LUTHERAN CHURCH liliko Ashburn.
Our Savior's Way Lutheran Church,
43115 Waxpool Rd,
Ashburn,
VA 20148
Ibada itaanza saa 6:00 mchana.
Kwa taarifa zaidi unaweza kuwasiliana na
David Kisanga: 703-932-0540
Mercy Ligate: 240-461-9477.
Bwana ametoa, Bwana ametwaa na jina lake lihimidiwe - AMEN
↧
VITUO VYA MWENGE, MAKUMBUSHO KABLA NA BAADA YA MABADILIKO LEO
Mwenyekiti wa soko la Makumbusho, Bi Mary John (kulia), akiongea na Mkuu wa Usalama Barabarani Mkoa wa Kinondoni, SP Awadhi Haji (kati), na Mkuu wa Usalama Barabarani, Kituo cha Kinondoni, Solomon Mwangamilo (kushoto).
Huduma ya usafiri ikiendelea kama kawaida eneo la Makumbusho
Stendi ya Makumbusho kabla haijaanza kutumika.
Muonekano mpya wa kituo cha Mwenge baada ya kuhamishwa.Picha na GPL
↧
TANZANIA NA QATAR ZASAINI MKATABA WA USHIRIKIANO WA KAZI NA AJIRA
Mazungumzo yakiendelea. |
↧
UHURU KWA VYOMBO VYA HABARI UNA I "SHAPE" JAMII ASEMA WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII-NYARANDU
Video imepigwa na Dixon Busagaga wa
Globu ya Jamii aliyekuwa jijini Mwanza.
Globu ya Jamii aliyekuwa jijini Mwanza.
↧
↧
DKT. BILAL AZINDUA KITUO CHA TIBA, UCHUNGUZI NA MAFUNZO YA MAGONJWA YA SARATANI, MATUMBO NA INI UKANDA WA AFRIKA MASHARIKI CHAFUNGULIWA MUHIMBILI
Kituo cha uchunguzi na mafunzo ya magonjwa ya saratani, matumbo na ini Ukanda wa Afrika Mashariki kimefunguliwa rasmi mwishoni mwa juma. Sherehe hizo zilifanyika katika Hospitali ya Taifa Muhimbili mwishoni mwa juma ambapo Mgeni rasmi alikuwa Makamu wa Rais, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal. Fuatilia katika picha matukio wakati wa ufunguzi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal akipongezana na Profesa Meinrad Classen wa Chama cha Madaktari wa Matibabu ya Mfumo wa Chakula ya Ujerumani ambaye alisaidia kutafuta fedha za kujenga na kuweka vifaa tiba vya kituo hicho kutoka Kampuni ua Else Kroner Fresenius ya nchini Ujerumani baada ya kufungua rasmi kituo hicho.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal
akisaini kitabu cha wageni mara tu baada ya kufungua kituo hicho.
Dkt. John Rwegasha, Bingwa wa Magonjwa ya Matumbo na Ini akitoa ufafanuzi kwa Makamu wa Rais, Dkt. Bilal
Dkt. Edwin Masue Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Ndani akitoa maelezo kwa Dkt. Bilal kuhusu matumizi ya kifaa cha kufanyia uchunguzi.
↧
UPDATES ZA MSIBA WA GEORGE TYSON
Mwili wa Marehemu George Tyson (pichani) utapelekwa nyumbani kwa marehemu Mbezi Beach (eneo la Makonde) kesho Jumanne Juni 3 kuanzia majira ya saa kumi jioni kwa ajili ya kuaga.
Mwili utakuwepo nyumbani hapo mpaka siku ya Jumatano Juni 4,ambapo mwili utapelekwa kwenye viwanya vya Leaders Club,Kinondoni kwa ajili ya shughuli ya kuaga mwili na ibada fupi.
Baadae mwili utapelekwa kwenye Uwanja wa ndege wa Mwalimu J.K.Nyerere tayari kwa kusafirishwa kwenye jijini Nairobi nchini Kenya kwa mazishi.
Tutaendelea kuwaletea taarifa kadri zitakavyokuwa zikitufikia.
↧
introducing Mzazi Montana's 1st solo project out of Chikwaso Family
↧
Najua wajua ya Capt. Gardiner G. Habash kuanza hivi karibuni ndani ya Michuzi TV - kaa chonjo
Hiki ni kipindi kingine tena kitachokujia hivi punde kupitia MICHUZI TV, kama ulivyoambiwa hapo. Usikonde. Show hii na nyingine nyingi za kusisimua utazipata kirahisi sana kiasi utashangaa. Kaa chonjo, mboga ipo jikoni - karibu itaiva. We kaa mkao wa kula tu...
↧
↧
mama mzazi wa mwanalibeneke Kazikupenda "KK" Chale afariki dunia leo
Mdau Kazikupenda Kk Chale anasikitika kutangaza kifo cha mama yake mzazi Bi.Fides Chale (pichanii) kilichotokeo ghafla leo huko Nyumbani kwake Ubungo Msewe.
Mipango ya mazishi inaendelea nyumbani kwa mwanae, Ubungo-Msewe, Dar. Maziko yanatarajia kufanyika Dar. Taarifa zaidi zitotelewa baadae.
Bwana ametoa, Bwana ametwaa
jina la Bwana Lihimidiwe - Amen
KK anaendesha blog ya Tembea Tanzania BOFYA HAPA
jina la Bwana Lihimidiwe - Amen
KK anaendesha blog ya Tembea Tanzania BOFYA HAPA
↧
KHITMA YA MAREHEMU AMINA ZAHRA MTENGETI KUSOMWA KESHO
↧
TANZIA
MAREHEMU REDEMPTA
KATONDAABELA (MAMA RWEKAZA)
Familia ya Prosper Mutafurwa wa Mtaa wa Mwale, Tandika Maguruwe, Dar es salaam. Inasikitika kutangaza kifo cha Mke wake mpendwa Redempta KatondaAbela ai Mama Rwekaza (Pichani) kilichotokea alfajiri ya Jumapili tarehe 01/06/2014 akiwa usingizini.
Habari ziwafikie ndugu, jamaa na marafiki wote popote walipo.
Mipango ya mazishi inafanyikia Nyumbani kwa Mume wa marehemu Tandika Dar es salaam.
Mwili wa marehemu unatarajiwa kusafirishwa siku ya Jumatano tarehe 04/06/2014 kwenda Katoke, Buyango, Kiziba, Bukoba na mazishi yatafanyika Siku ya Ijumaa tarehe 06/06/2014 huko huko Katoke,Buyango, kiziba, Bukoba.
Glob ya Jamii inatoa pole kwa
familia nzima, ndugu, jamaa na marafiki wote
BWANA AMETOA NA BWANA
AMETWAAJINA LAKE NA LIHIMIDIWE
AMEN
↧
Tigo enters new partnership with DTBi and COSTECH to promote ICT and create youth employment in the country
↧
↧
DStv Rewards Customers over Tshs 26m/-
Wateja wa DStv walioshinda malipo ya mwezi ya mwaka mzima wakipongezwa na Meneja Uhusiano wa MultiChoice Tanzania, Barbara Kambogi (kulia) na Operations Manager wa kampuni hiyo Ronald Shelukindo (Kushoto). |
DStv, the leading pay television service has awarded its customers over Tshs 26,000,000 worth of subscription, in a campaign aimed at thanking and rewarding subscribers for their sustained loyalty and support. The campaign dubbed DStv Rewards has given out free annual subscriptions to customers who remained connected uninterrupted between January and March 2014.
In a brief handover ceremony held at DStv Offices Oysterbay, Public Relations Manager of MultiChoice Tanzania Barbara Kambogi said that “the DStv Rewards Campaign was open to subscribers on each of our five bouquets Premium, Compact Plus, Compact, Family and Access, all a customer had to do was to ensure they paid their subscription on time and automatically were entered into an electronic draw.
Commenting further was MultiChoice Tanzania General Manager, Peter Fauel: We are delighted to award our loyal subscribers and recognize their contribution towards our business. This is our way of thanking them. DStv has without a doubt the best programming be it in sports, movies, kids, news, lifestyle, documentary and music.
He further continued “this is an exciting period for our customers especially with the World Cup being around the corner. Our winners will be able to watch in-depth coverage of the World Cup through the dedicated SuperSport channels. We congratulate our winners and urge others who are not connected to take advantage of our hardware special offer of fully installed DStv at just Tshs 129,000.
↧
TAASISI YA FARIDA FOUNDATION KUFANYA UZINDUZI TAREHE 28/06/2014
Taasisi ya Faridas foundation inatarajia kufanya uzinduzi wake rasmi siku ya tar 28/6/2014 siku ya jumamosi katika ukumbi wa crystal hall, blue pearl hotel, ubungo plaza kuanzia saa 6 hadi 12 jioni.
Katika siku hyo taasisi itatoa misaada mbali mbali kwa walemavu ikiwemo baiskeli za walemavu, vyerehani, vifaa vya shule na vifaa vingine muhimu kwa walemavu ukiwa kama mdau au mtanzania unayeguswa na walemavu na ungependa kuhudhuria siku hyo maalumu kadi zinapatikana kwa mchango wa shilingi laki moja na kuendelea hii ikiambatana na chakula cha mchana vinywaji na burudani mbalimbali pia utakuwa umesaidia kuongeza idadi ya vifaa vitakavyotelewa kwa walemavu mbali mbali. Kutoa ni moyo sio utajiri.
Endapo una kampuni au ungependa kushiriki kama kampuni au taasisi kwa kudhamini pia nafasi bado zipo wazi wasiliana nasi kupitia +255715186262 au email faridasfoundation@gmail.com
↧
MBUNGE WA JIMBO LA SIMANJIRO,OLE SENDEKA ALIVYOUNGURUMA MERERANI
↧
Polisi Feki watiwa mbaroni mkoani Iringa
Kamanda wa polisi mkoa wa Iringa,Ramadhan Mungi akiwaonyesha maaskari feki ambao walikuwa wakifanya utapeli katika mikoa ya Iringa na Morogoro ,kulia ni Bazil Nyakunga ambae ni mwalimu akiwa na sare za polisi na katikati ni bossi wake Godlack Mbehale.
Askari polisi Mkoani Iringa (kushoto) akiwa na maaskari feki katika ofisi ya kamanda wa polisi leo |
Na Francis Godwin,Iringa
MATAPELI washindwa kubaki njia kuu sasa waanza michepuko mipya ni baada ya jeshi la polisi mkoa wa Iringa kumkamata mwalimu aliyejifanya askari akiwa na fullu kombati za jeshi la polisi na bossi wake aliyevalia kiraia ambae pia ni feki na ni mmiliki wa studio eneo la Kihesa mjini hapa.
Upo usemi usemao kuwa usiombe likukute usilo litegemea kukukuta katika maisha yako na ukipenda kudanganya uwe tayari kudanganywa ,hakuna asiyepata kusikia ama kusoma habari kuhusu utapeli unaoendelea hapa nchini kwa watu wa kada mbali mbali na mazingira yanaonyesha matapeli hawa siku zote ni watu wanaopenda wengine yawakute na sio wao na hata kupenda kudanganya na sio kudanganywa kama ambavyo mwalimu huyo Bazil Nyakunga (20) ambae anatuhumiwa kutapeli wazazi wengi Iringa na Morogoro ambao wanataka watoto wao kwenda kusomea uaskari .
Mwalimu Nyakunga akiwa na bossi wake feki Godlack Mbehale (21) walijikuta matatani kwa kukutwa na wasilotegemea kulipata baada ya jeshi la polisi kuweka mtego kufuatia wananchi wengi kufika polisi kulalamikia utapeli huo wa ajira kwa vijana wao katika jeshi la polisi.
Ramadhan Mungi ni kamanda wa polisi wa mkoa wa Iringa alilitonya gazeti hili kuwa jeshi lake lilipopata stori hiyo ya utapeli waliweka mtego eneo la Ipogolo ambapo askari huyo feki alikuwa amepiga kambi la kitapeli kwa kuwasanua mavumba wazazi wenye uchu wa watoto wao kuwa mageda (ma Askari).
Alisema kuwa vijana hao ambao mmoja Nyakunga ambae ni mkazi wa Ilula Mtua katika wilaya ya Kilolo mkoani Iringa ni kijana aliyepata kusoma kozi ya ualimu mkoani Shinyanga na kuwa ndie alikuwa akijifanya na askari polisi na muda wote alikuwa akivaa sare za jeshi hilo.
Mungi alisema kuwa kijana huyo na mwenzake wamepata kuwaliza watu wengi sana Iringa na Morogoro na kuwa mtu wa mwisho wamemliza kiasi cha Tsh 900,000 na kuwa njia wanayotumia ni Nyakunga kama askari baada ya kumpata mazazi na mtu mwinye uhitaji na ajira ya polisi amekuwa akipiga simu kwa boss wake Bw Mbehale na kuiweka simu hiyo katika mfumo wa Laudi spika ili mtu anayetapeliwa kupata kusikiliza vema mazungumzo hayo.
“ Nyakunga kama askari feki baada ya kumpata mteja wa kumtapeli amekuwa akiweka simu yake katika sauti kubwa na huyo boss wake amekuwa akisikika akipanga gharama za mtapeliwa kulipia na baada ya kutoa pesa wamekuwa wakiingia mitini kwa kumta ahadi feki….mfano anapopiga simu anajifanya samahani boss naomba maelekezo ya mwisho huyu mzazi /kijana anataka kazi anapaswa kutimiza nini kwa sasa kabla ya kuitwa katika usaili ”.
Hata hivyo kamanda Mungi alisema kuwa ni vema wananchi kuchukua tahadhari juu ya utapeli huo na kuwa kazi za polisi kwa sasa haziingizwi kwa mtindo huo na kuwa jeshi hilo lina utaratibu wake wa kuingiza vijana ikiwa ni pamoja na kuwachucha toka sekondari kwa kujaza fomo huku wale wa elimu ya juu upo utaratibu na wale wanaochukuliwa kwa utaalam wao pia wanautaratibu wao na si vinginevyo.
Alisema kuwa hakuna usaili wa askari unaofanywa mitaani ama wilayani hivyo vijana hao walikuwa wakifanya utapeli na ni vema wananchi kuchukua tahadhari kubwa .
Pia alisema jeshi lake linafanya uchunguzi ili kubaini eneo ambalo matapeli hao walipata sare hizo za jeshi la polisi na mbinu waliyotumia kuzipata sare hizo ikiwa ni pamoja na kuwafikisha mahakamani.
Hata hivyo kwa upande wao matapeli hao walidai kuwa ni kweli wanafanya kazi na ualimu na mmoja na mmiliki wa studio eneo la Kihesa mjini Iringa na kuwa sare hizo walizipata kutoka kwa rafiki yao ambae ni askari polisi aliyewatuma kuzifikisha kwa ndugu yao askari .
↧
↧
MAKAMU WA RAIS ASHIRIKI SHEREHE ZA MAKABIDHIANO YA URAIS NCHINI MALAWI
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal akimpongeza Rais mpya wa Malawi Prof. Arthur Peter Mutharika baada ya Rais huyo mpya wa Malawi kukabidhiwa madaraka jijini Brantyre kwenye hoteli Sunbird. Baada ya kukutana viongozi hao walipata fursa ya kuzungumzia masuala la kidiplomasia baina ya nchi hizi mbili na kukubaliana kuendelea kuwa na mahusiano mema kama nchi zinazoishi ndugu na jirani. Picha kwa Hisani ya Ikulu ya Malawi
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania DkT. Mohammed Gharib Bilal leo Jumatatu Juni 02, 2014 ameshiriki katika sherehe za kukabidhi madaraka kwa Rais mpya wa Malawi Profesa Arthur Peter Mutharika katika sherehe zilizofanyika kwenye uwanja wa Kamuzu Banda jijini Blantyre. Sherehe hizo pia zilihudhuriwa na Rais wa Botswana sambamba na wawakilishi wa nchi za Zimbabwe, Msumbiji, Afrika Kusini na nyinginezo.
Akihutubia baada ya kukabidhiwa sime ambayo ni ishara ya kuwa kiongozi wa watu wa Malawi, Rais Mteule Mutharika alisisitiza kuwa, katika kipindi cha utawala wake atahakikisha kuwa anaifanyia makubwa Malawi sambamba na uhakikisha kuwa anaifanya Malawi itimize majukumu yake ya kimataifa kufuatia kutambua kuwa kujitenga kunaweza kuifanya Malawi kutonufaika na fursa zilizopo duniani.
“Nchi hii ipo katika dunia na siyo rahisi tena kuwa na fikra kwamba Malawi inaweza kubaki peke yake kama kisiwa. Tunahitaji kuwa na wenzetu wa kusaidia maendeleo ya Malawi. Tunawahitaji wahisani toka Kusini ama Mashariki, tunayahitaji mataifa tajiri na mataifa yanayoendelea. Tutafanikiwa sana kama tutaendeleza urafiki kwa wote. Tufanye hivi bila kujali kuwa sisi ni taifa kwani hali ya sasa inahitaji kila mmoja wetu kushirikiana na mwenzake,” alisema.
Katika hotuba hiyo pia amesisitiza kuwa kipindi chake cha utawala atajitahidi kukabiliana na rushwa na kwamba hatakuwa na mchezo kwa wala rushwa katika kipindi akiwa madarakani. Pia alisisitiza kuhusu umuhimu wa kuiunganisha Malawi kwa miundombinu bora ili kuboresha maisha ya wananchi sambamba na kusogeza huduma za wananchi karibu.
Rais Mutharika aliapishwa juzi baada ya kuwashinda washindani wake akiwemo Rais aliyemaliza kipindi chake Joyce Banda ambaye hata hivyo hakuweza kutokea katika sherehe hizi za kukabidhi madaraka.
Akizungumzia suala la kutohudhuria kwa Rais Joyce Banda, Rais Mteule Mutharika alisema alitegemea Rais Banda kuwepo lakini hakufika na yeye anatambua kuwa wakati wa uchaguzi kulikuwa na tofauti baina yao lakini kwa sasa uchaguzi umeisha na amesahau yaliyopita ili kuanza ukurasa mpya wa kuijenga Malawi. Katika shughuli hiyo pia Rais wa zamani wa Malawi Kamuzu Banda alihudhuria.
Akizungumzia suala la kutohudhuria kwa Rais Joyce Banda, Rais Mteule Mutharika alisema alitegemea Rais Banda kuwepo lakini hakufika na yeye anatambua kuwa wakati wa uchaguzi kulikuwa na tofauti baina yao lakini kwa sasa uchaguzi umeisha na amesahau yaliyopita ili kuanza ukurasa mpya wa kuijenga Malawi. Katika shughuli hiyo pia Rais wa zamani wa Malawi Kamuzu Banda alihudhuria.
Makamu wa Rais Dkt. Bilal na msafara wake walitarajiwa kurejea nyumbani leo hii Jumatatu mara tu baada ya kukamilika kwa kazi hii ya makabidhiano.
↧
KATIBU MKUU WA CCM,AKUTANA NA MCHIMBAJI MDOGO WA MADINI,MERERANI,SUZIE DIDAS KENEDY.
↧
BALIMI EXTRA LAGER KUDHAMINI MASHINDANO YA NGOMA ZA ASILI 2014
Meneja wa Bia ya Balimi Extra Lager(kulia) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu udhamini wa mashindano ya ngoma yajulikanayo kama “Balimi Ngoma Festival 2014” TBL Dar es Salaam.Kushoto ni Meneja matukio wa Taifa TBL, George Mombeki.
Meneja matukio wa Taifa TBL, George Mombeki(kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu udhamini wa mashindano ya ngoma yajulikanayo kama “Balimi Ngoma Festival 2014” TBL Dar es Salaam.
↧
More Pages to Explore .....