Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 459 | 460 | (Page 461) | 462 | 463 | .... | 3278 | newer

  0 0

  Na Mwandishi Maalum, New York 
  Ushirikiano wa kimaendeleo baina ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mfuko wa Umoja wa Mataifa unaohudumiwa Watoto ( UNICEF) umefanikisha utekelezaji wa miradi mbalimbali inayolenga katika utoaji huduma endelevu kwa watoto . 
  Kauli hiyo imetolewa siku ya jumanne na Bibi. Anna Maembe, Katibu Mkuu, Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto , anayeiwakilisha Tanzania katika mkutano wa Mwaka wa Bodi tendaji ya UNICEF unaofanyika hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa 
   Katika siku ya kwanza ya Mkutano huu viongozi mbalimbali, akiwamo Malkia Sophia wa Uhispania, Mke wa Rais wa Bukina Faso, Bibi Chantal Compaore Mawaziri, Makatibu Wakuu na Mabalozi walipata fursa ya kuchangia mawazo kuhusu mafanikio na changamoto mbalimbali zinazomkabili mtoto na nafasi ya UNICEF. 
  Pamoja na kwamba mkutano huu wa mwaka wa UNICEF unahusu zaidi kujadili taarifa za utendaji kazi wa Mfuko mafanikio na changamoto zake. 
  Rais wa Bodi ambaye ni Mwakilishi wa Jamhuri ya Kenya katika Umoja wa Mataifa kwa kushirikiana na Secretariet yake, aliandaa mkutano maalum ambapo washiriki wakiwamo wa kutoka Umoja wa Afrika ( AU) walipata fursa ya kubadilishana mawazo na uzoefu kuhusu Maendeleo endelevu katika Afrika, mkazo ukiwa kwa mtoto. 
   Ni katika mkutano huo maalum, ambapo Katibu Mkuu Maembe alipopewa fursa ya kuzungumza kuhusu Tanzania alisema. 
   Tanzania imefanya mengi katika kumuendeleza mtoto kiafya, kielimu na utetezi wa haki zake za msingi. Hata hivyo akaeleza kwamba juhudi hizo za serikali zimekuwa zikichangiwa na UNICEF na wadau wengine wa maendeleo, huku akisisitiza kwamba serikali imekuwa na ushirikiano mzuri na mfuko huo kiasi cha kujivunia. 
   Akaitaja baadhi ya miradi ambayo Serikali inatekeleza kwa ushirikiana na UNICEF na wadau wengine kuwa ni pamoja na huduma za utoaji vyakula vyenye virutubishe ili kukabiliana na tatizo kubwa la utapia mlo, utoaji wa madini joto, vitamini, chanjo mbalimbali zikiwamo za kuzuia ugonjwa wa homa ya mapafu na kuharisha. 
  Aidha akasema misaada ya kiufudi na kifedha inayotolewa na Mfuko huo ulifanikisha kufanyika kwa utafiti kuhusu vitendo vya kikatili dhidi ya watoto. Matokeo ya utafiti huo yalionyesha kuwa kuna vitendo vingi vya kikatili wanavyofanyiwa watoto, kiasi cha serikali kufungua vituo kwaajili ya kuwahudumua watoto dhidi ya udhalilishaji na ukatili na ambavyo vimefunguliwa karibu katika wilaya zote. Katibu Mkuu akasema kuanzishwa kwa vituo hivyo kumeifanya serikali kuongeza bajeti katika eneo hilo. 
  Akaongeza kwamba serikali pia imejitahidi sana katika eneo la upunguzaji wa vifo vya watoto chini ya umri wa miaka mitano na fursa ya elimu kwa watoto wa jinsia zote. Katika eneo hilo la elimu Katibu Mkuu amesema changamoto kubwa ni mimba za utotoni na ndoa za umri mdogo, maeneno ambayo yamekuwa tatizo kubwa kwa wanafunzi wa kike na hivyo kushindwa kuendelea na masomo yao. 
  Akahitimisha kwa kuitaka UNICEF kuendelea kushirikiana na Serikali hususani katika kipindi hiki cha kumalizia utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo ya Millenia ( MDGs) na baada ya 2015 wakati ajenda mpya za Maendeleo Endelevu zitakapoanza kutekelezwa. 
  Rais wa UNICEF Balozi Kamaku, akijumuisha majadilianyo hayo ambapo baadhi ya wazungumzaji waligusia pia suala la kutekwa kwa wasichana zaidi ya 200 na kundi la Boko Haramu huko Nigeria, na kutoa wito wa kutaka waachiwe huru. alisema, malengo mapya ya maendeleo endelevu baada ya 2015 lazima yajielekeze katika kuhakikisha kwamba changamoto zinazomkabili mtoto hususani katika Afrika, kama vile magonjwa, utapia mlo, ukosefu wa chakula na mengineyo yanamalizwa na kuwa historia. 
  Akasisitiza kwamba haoni sababu ni kwa nini Afrika isiondokane na changamoto hizo na kwamba UNICEF inapashwa kuwa mstari wa mbele katika kuzipigania na kuzisemea changamoto hizo.
    Bibi Anna Maembe, Katibu Mkuu, Wizara ya  Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto akizungumza katika Mkutano Maalum   kuhusu Maendeleo Endelevu katika Afrika: Mkazo ukiwa kwa Mtoto, uliofanyika siku ya kwanza ya  Mkutano wa Mwaka  wa Mfuko wa Umoja wa Mataifa unaohudumia Watoto ( UNICEF)  Katibu Mkuu  ambaye alikuwa miongoni mwa wageni kutoka mataifa mbalimbali walioalikwa  kuhudhuria mkutano huu  akimwakilisha Mhe.  Waziri Sophia Simba Mb)  aliungana na  wageni wengine  akiwamo  Malkia Sophia wa Uhispania, Mke wa Rais wa Bukina Faso Bibi Chantal Comapore, Mawaziri  na Mabalozi kuzungumzia  mafanikio na changamoto katika utoaji wa huduma za msingi zinazomhusu mtoto. 
   Sehemu ya  wajumbe waliohudhuria mkutano maalum   Maendeleo Endelevu katika Afrika: Mkazo ukiwa kwa mtoto Mkutano huu maalum, ulitanguliwa na ule wa ufunguzi wa mkutano wa Mwaka wa UNICEF ambapo baadhi yha wazungumzaji   waligusia suala la  wasichana zaidi ya  200 waliotekwa na Kundi la Boko Haramu  nchini Nigeria wakitoa rai ya kutaka  kuachiwa  huru kwa  wasichana hao. 
  "Asante sana, nashukuru sana..  " Maneno  hayo ya kiswahili  yalizungumzwa na Bw.  Bogani C. Majora,  Msajili wa Mahakama ya  Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda ( ICTR)   aliyeshikana mkono na  Balozi Tuvako Manogi, wakati  Msajili  huyo alipofika siku ya  jumanne, katika Uwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa na kufanya mazungumzo ambapo pamoja na  mambo mengine  ameishukuru   Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuwa mwenyeji wa Mahakama hiyo ambayo  inaelekea  ukiongoni mwa utekelezaji wa majukumu yake ya msingi. Pamoja na  kwamba  ICTR inamaliza shughuli zake, Baraza Kuu la Usalama  la Umoja wa Mataifa limeipatia Tanzania  dhamana   ya ujenzi  wa kituo  kitakachosimamia    umaliziaji wa kesi za masalia pamoja na uhifadhi wa nyaraka na kumbukumbu zote muhimu za ICTR  majengo ya kituo hicho yatajendwa katika  eneo la LakiLaki  jijini Arusha  wa kwanza kushoto ni msaidizi wa Msajili na  wa   mwisho kulia ni Bi. Tully Mwaipopo Afisa wa Uwakilishi wa Kudumu

  0 0  KUNDI A
  Brazil

  Makipa: Julio Cesar (Toronto FC, Mkopo toka QPR), Jefferson (Botafogo), Victor (Atletico Mineiro).
  Mabeki: Dani Alves (Barcelona), Maicon (Roma), David Luiz (Chelsea), Thiago Silva (PSG), Dante (Bayern Munich), Marcelo (Real Madrid), Henrique (Napoli), Maxwell (PSG).
  Viungo: Oscar (Chelsea), Fernandinho (Man City), Willian (Chelsea), Paulinho (Spurs), Ramires (Chelsea), Luis Gustavo (Wolfsburg), Hernanes (Inter Milan).
  Mafowadi: Bernard (Shakhtar Donetsk), Neymar (Barcelona), Fred (Fluminense), Hulk (Zenit St Petersburg), Jo (Atletico Mineiro).  0 0

   Hatimaye Mtoto Nasra Mvungi aliyefariki Juni mosi mwaka huu kufuatia kuaishi katika matesa makubwa kutoka kwa mama yake mkubwa baada ya mama yake kufariki na kuishi katika boksi bila huduma muhimu anazostahili kupatiwa binadamu hasa mtoto mdogo mwenye umri wa mwaka mmoja amezikwa kwa heshima zote na wakazi wa Morogoro wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa huo, Joel Nkaya Bendera, Mbunge wa Morogoro mjini, Abdulaziz Abood na mfanyabiashara wa mabasi na vituo vya mafuta mkoani Morogoro Al Saed Omary. Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, ametaka vyombo vya sheria  kutoa hukumu inayowastahili waliohusika kwa mateso na kupelekea kifo cha Nasra.

   Waombolezaji wakiwa Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro, kuaga mwili wa mtoto Nasra Mvungi.
    Mbunge Abdulaziz Abood akiweka udongo katika kaburi la marehemu Nasra na kuahidi kumfanyia hitma baada ya siku 40 tangu kuzikwa kwake.
   Mfanyabiashara Al Saed Omar nae akiweka udongo katika kaburi la marehemu.

    Mazishi ya mtoto Nasra yaliendelea makaburi ya Kola mkoani Morogoro.
    Mfanyabiashara, Al Saed Omary aliyefanikisha kuleta mwili wa marehemu Nasra kutoka Dar es Salaam.


  0 0  0 0  0 0

  HYUNDAI East Africa Sales Manager, Alen Nkya (left) gestures with Vice President of Tanzania Dr. Mohammed Bilal (centre) and Minister of Works Hon. John Magufuli (right) regarding application of Construction and Mining Equipment during Contractors International Conference at Diamond Jubilee in Dar es Salaam recently.

  0 0

   Rais wa Oganaizesheni ya ngumi za kulipwa nchini T.P.B.O Yassin Abdalla 'Ostadhi' kushoto akimkabidhi leseni ya ngumi bondia Ibrahimu  'King Class Mawe' ambayo anaweza kutumia Dunia nzima kwa ajili ya kutambulika kitaifa na kimataifa ambayo inaweka rekodi mbalimbali za bondia pindi anapocheza mchezo.

  0 0

  NA RAMADHANI JUMA 
  OFISI YA MKURUGENZI-KALAMBO 
   OFISI ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Kalambo Mkoa wa Rukwa kupitia kitengo cha UKIMWI kimetumia zaidi ya shilingi milioni 8.5 kwa ajili ya kuimarisha mapambano dhidi ya ugonjwa huo katika wilaya hiyo. 
   Fedha hizo zimetumika kuwanunulia wanafunzi yatima wanaoishi katika mazingira magumu sare za shule, viatu pamoja vifaa vya kujifunzia ikiwemo madaftari na kalamu, ambapo Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Godfrey Sichona alikabidhi kwa walengwa kwa niaba ya Halmashauri. 
   Pia Halmashauri hiyo imenunua vifaa vya muziki kwa ajili ya vikundi viwili vya Sayuni kilichopo kata ya Legezamwendo na Sayuni cha Kata ya Mambwenkoswe ili vihamasishe wananchi kujikinga na ugonjwa huo. 
   Baadhi ya vifaa vya muziki vilivyotolewa na Halmashauri hiyo ya Kalambo ni gitaa tatu kila kikundi, spika, maikrofoni, genereta pamoja na vifaa vingine vya umeme. 
   Akizungumza wakati wa kukabidhi misaada hiyo, mwenyekiti huyo aliwakumbusha wakazi wa wilaya ya Kalambo na Mkoa wa Rukwa kwa ujumla kuwa, mapambano dhidi ya UKIMWI sio ya serikali pekee bali ni jukumu la kila mwanajamii zikiwezo taasisi za dini. 
   Naye mwenyekiti wa kamati ya Kudhibiti UKIMWI wilaya ya Kalambo Faustine Mwanisenga aliwataka wanavikundi waliopatiwa msaada wa vifaa vya muziki na Halmashauri hiyi kuvitunza na kuvitumia vizuri ili kufikia malengo yaliyokusudiwa.
   MWENYEKITI wa Halmashauri ya wilaya ya Kalambo Mkoa wa Rukwa Godfrey Sichona (mwenye suti) na Makamu wake Faustine Mwanisenga wakikagua gitaa wakati walipokabidhi vifaa vya muziki kwa vikundi viwili vya Kwaya katika Kata za Legezamwendo na Mambwenkoswe ili visaidie mapambano dhidi ya UKIMWI kwa njia ya nyimbo wilayani humo Kulia ni mratibu wa UKIMWI  wa wilaya hiyo Mariam Kimashi.
  MWENYEKITI wa Halmashauri ya wilaya ya Kalambo Mkoa wa Rukwa Godfrey Sichona akikabidhi sare kwa mrataibu wa Elimu wa Kata ya Legezamwendo ili zigawanywe kwa wanafunzi yatima na wanaoishi katika mazingira magumu.

  0 0

  As the inaugural CECAFA Nile Basin Cup tournament goes into the finals in Khartoum City this Wednesday afternoon, the CECAFA Secretary General Nicholas Musonye  (pictured) believes despite the numerous hurdles, the region is headed for a better destination in football development.  

  0 0

  Meneja wa Bia ya Ndovu Special Malt, Pamela Kikuli(wa pili kulia) na mpishi wa bia wa Kampuni ya Bia nchini Tanzania(TBL) Cavin Nkya(wa pili kushoto) wakiwa wameshikilia tuzo zao za ubora wa kimataifa(International Quality Trophy) za Ndovu Special malt na Safari Lager walizoshinda hivi karibuni nchini Ufaransa kutoka kwenye Taasisi ya kimataifa ya Monde Selection.
  Meneja wab Bia ya Ndovu Special Malt, Pamela Kikuli akiwa ameshikilia chupa ya bia yake iliyoshinda tuzo ya Ubora wa Kimataifa(International Quality Trophy) kutoka kwenye Taasisi ya Kimataifa ya Monde Selection.
  Meneja wab Bia ya Ndovu Special Malt, Pamela Kikuli akiwa ameshikilia tuzo ya ubora wa kimataifa(International Quality Trophy) na cheti mara baada ya kukabidhiwa na Taasisi ya Kimataifa ya Monde Selection.
  Mpishi wa bia wa Kampuni ya bia nchini Tanzania(TBL), Cavin Nkya akiwa ameshikilia chupa ya bia ya Ndovu Special Malt iliyoshinda tuzo ya Ubora wa Kimataifa(International Quality Trophy) kutoka kwenye Taasisi ya Kimataifa ya Monde Selection.
  Mpishi wa bia wa Kampuni ya bia nchini Tanzania(TBL), Cavin Nkya akiwa ameshikilia tuzo ya ubora wa kimataifa(International Quality Trophy) mara baada ya kukabidhiwa na Taasisi ya Kimataifa ya Monde Selection.
  Meneja wab Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo(kulia) na Mpishi wa bia wa Kampuni ya bia nchini Tanzania(TBL), Cavin Nkya wakiwa wameshikilia chupa za Safari Lager iliyoshinda tuzo ya Ubora wa Kimataifa(International Quality Trophy) kutoka kwenye Taasisi ya Kimataifa ya Monde Selection.

  0 0

  Waziri wa Fedha,Mh. Saada Mkuya akisoma Hotuba Bungeni,Dodoma leo.

  0 0

  DSC_0340
  Kamishina Mwandamizi wa Jeshi la Polisi nchini (SACP) Simon Sirro akizungumza kwenye ufunguzi wa mafunzo ya wiki mbili kwa makamanda wa Jeshi hilo nchini, mafunzo hayo yaliyofadhiliwa na UNDP yana lengo la kuwajengea uwezo makamanda jinsi ya kupambana na viashiria vya uvunjifu wa amani bila kuleta madhara makubwa kwa jamii. Kushoto ni Mtaalamu wa Uchaguzi kutoka UNDP, William Hogan na kulia ni wakufunzi kutoka Uingereza, Adrian Barnes (kulia) na Alan Binks (wa pili kulia).

  Na Mwandishi Wetu, Tanzania

  JESHI LA POLISI nchini limejisifu kwa kuzingatia weledi na maadili ya kazi yao kwa kuruhusu maandamano mengi kufanyika hapa nchini na ni maandamano machache tu yaliyowahi kupigwa marufuku. 

  Akizungumza na waandishi wa habari hivi karibuni jijini Dar es Salaam wakati akifungua mafunzo ya wiki mbili kwa maofisa 88 wa Jeshi la Polisi yanayofadhiliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Programu ya Maendeleo (UNDP) kupitia mradi wa Uwezeshaji Demokrasia (DEP), Kamishina Mwandamizi wa Jeshi la Polisi nchini (SACP), Simon Sirro amesema mafunzo hayo kwa makamanda ni kusaidia uelewa wao katika kupambana na maandamano au dalili za uvunjifu wa amani bila kuleta madhara makubwa kwa jamii.

  “mafunzo haya kwa makamanda wa Jeshi la Polisi nchini litasaidia kuongeza uelewa kuhusu haki za binadamu na utawala bora ili kudumisha amani na utulivu nyakati za uchaguzi,” amesema Sirro.
  DSC_0310
  Mtaalamu wa Uchaguzi kutoka UNDP, William Hogan akizungumza kwenye ufunguzi wa mafunzo hayo kwa makamanda wa Jeshi la Polisi nchini kuhusu mafunzo hayo na muhimu wake katika kudumisha amani na kusaidia uchaguzi kufanyika katika hali ya utulivu na kidemokrasia zaidi.
  Kamanda Sirro amesema kwamba mafunzo hayo yanalenga pia kusaidia uelewa makamanda jinsi ya kushughulika na wavunjifu wa amani kwa kuzingati weledi wa Jeshi la Polisi nchini.

  Amesema kuelekea katika uchaguzi mkuu mwakani 2015 mafunzo yamekuja wakati mwafaka kwa Jeshi la Polisi kupanua wigo wao katika maswala haya ya utawala bora na haki za binadamu nchini.

  “utafiti unaonyesha kwamba maandamano mengi yamewahi kuruhusiwa na Jeshi la Polisi kuzidi yale yaliyopigwa marufuku kwa hiyo yana ya kwamba jeshi linazuia haki za raia kukusanyika au kuandamana haipo isipokuwa kwa sababu za kiusalama tu,’ aliongeza Kamanda Sirro

  Kwa upande wake, Mtaalamu wa Uchaguzi, kutoka UNDP, William Hogan amesema kuwa mafunzo hayo yanahusu kumudu kuleta utulivu wa umma na yanaendeshwa katika ukumbi wa maofisa wa Polisi wa Oysterbay na ukumbi wa maofisa w Polisi Zanzibar.
  DSC_0325
  Baadhi ya Maafisa wa Kikosi cha kutuliza ghasia nchini (FFU) nchini wakifuatilia hotuba za Kamanda Sirro wakati ufunguzi wa mkutano huo jijini Dar es Salaam.

  Amesema lengo la mafunzo hayo ni kujenga uwezo wa makamanda wa polisi wa kupanga, kumudu na kuratibu kwa ufanisi hatua za kipolisi za kushughulikia matukio yanayotishia utulivu katika jamii.

  “kupitia program hii ya mfululizo wa kozi nne zitakazodumu kwa majuma mawili kila moja, maofisa 88 ngazi za kati na juu kutoka kila mkoa katika nchini watafunzwa na wakufunzi waandamizi nane kutoka katika Chuo cha Mafunzo ya Polisi cha Uingereza,” amesema Hogan
  DSC_0361
  Mgeni Rasmi Kamishina Mwandamizi wa Jeshi la Polisi nchini (SACP), Simon Sirro aliyemwakilisha Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Ernest Mangu akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mafunzo hayo.
  DSC_0355
  SACP Simon Sirro akiteta jambo na Mtaalamu wa Uchaguzi kutoka, UNDP, William Hogan baada ya picha ya pamoja.

  0 0

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mh. Dk. Eng. Binilithi Satano Mahenge wa pili (kulia), akiwa katika ziara yake ya kukagua mazingira ya Kiwanda cha bia (TBL) kilichopo kata ya Pasiasi wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza, na wa pili (kushoto) ni Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Eng. Angelina Madete,wakati maadhimisho ya siku ya Mazingira Duniani yakiendelea jijini Mwanza.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais -Mazingira, Mh. Dk. Eng. Binilithi Satano Mahenge wa tatu (kulia)akipata maelezo kutoka kwa mmoja wa wafanyakazi wa kiwanda cha bia bw. Said Lwambo wa kwanza (kushoto) juu ya jinsi mashine za Majitaka za kiwanda cha TBL kinavyofanya kazi na kulinda Mazingira.
  Mh. waziri wa Nchi Ofisi ya makamu wa Rais -Mazingira,Dk. Eng. Binilithi Satano Mahenge wa kwanza (kulia), Naibu Waziri Mh. Ummy Mwalimu wa kwanza (kushoto)na Mkuu wa Mkoa Eng. Everist Ndikilo wa pili (kulia) wakizungumza na mmiliki wa Kiwanda cha Coca Cola (Nyanza bottling) Bw. Christopher Mwita Chuma baada ya kuwasili ofisini kwake leo jijini Mwanza.
  Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Mh. Ummy Mwalimu wa kwanza (kushoto)akiwa anafanya usafi eneo la mtaa wa Pamba A jijini Mwanza stendi ya zamani.

  0 0

  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akitazama baadhi ya michoro unayotumika katika kuwafundishia wanafunzi wasiona wakati alipotombelea shule maalu ya Wasioona ya Bigiri Dodoma Juni4,2014. Kulia ni Mratibu wa Mpango wa kuifadhili shule hiyo, Bw. V. Ramadhar Reddy ambaye ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya SURA.
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akikagua majengo na vifaa vya kufundishia wakati alipotembelea Shule Maalu ya Wasioona ya Bigiri iliyopo Dodoma Juni 4, 2014 Kushoto kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr. Reheme Nchimbi Juni 4, 2014.
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na walimu, baadhi ya wanafunzi na watendaji wa wilaya ya Chamwino wakati alipotembelea shule ya wasiiona ya Bigiri Juni 4, 2014, Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dr. Rehema Nchimbi na kulia ni Mratibu wa Mpango wa kuifadhili shule hiyo, Bw. V. Ramadhar Reddy. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0

  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na makamu wa Rais Dkt.Mohamed Gharib Bilal muda mfupi baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere akitokea Toronto Canada ambapo yeye na mwenyeji wake waziri Mkuu wa Canada Stephen Harper waliongoza mkutano wa kimataifa uliohusu kuboresha afya ya wanawake na watoto na kupunguza vifo vya wanawake wanapojifungua.(picha na Freddy Maro)


  0 0

  The Minister for EAC Affairs, Hon Shem Bageine holds the Budget Speech aloft at the start of the proceedings earlier today. He is flanked by the Minister for EAC Burundi, Hon Leontine Nzeyimana, Hon Dr. Abdallah Sadala Abdallah, Deputy Minister for EAC, United Republic of Tanzania and the Counsel to the Community, Hon Wilbert Kaahwa. On extreme right is the Clerk to the Assembly, Mr. Kenneth Madete.
  the Deputy Minister for EAC, United Republic of Tanzania Dr. Abdallah Sadala Abdallah delivers the Budget Speech.

  The EAC Council of Ministers today presented Budget estimates for the Financial Year 2014/2015 totalling $124,069,695 to the East African Legislative Assembly sitting in Arusha.   Hon Dr. Abdallah Sadala Abdallah, Deputy Minister for EAC, United Republic of Tanzania, presented the Budget Speech on behalf of the Chair of the EAC Council of Ministers, Hon Phyllis J. Kandie to an attentive House. 

  The 2014/2015 Budget down from $130 Million in the previous Financial Year, prioritizes operationalisation of the single Customs Territory including the setting up of an institutional framework to manage it, the full implementation of the EAC Common Market Protocol with particular focus on free movement of goods, services, labour and capital as well as the implementation of the EAC Industrialisation policy.


  0 0

  WWF-Tanzania has donated a new boat engine YAMAHA40 HP to Selous Game Reserve and will be used at Mtemere Wildlife Camp. The ceremony took place at WWF Tanzania Country office in Dar es Salaam on Friday May 30, 2014.

  The engine, handed over by WWF Tanzania’s Conservation Manager, Mr. Gerald Kamwenda on behalf of the Country Director was received by Mr. Gregory Andrea Kalokole, Senior Game Warden from Selous Game Reserve on behalf of the Project Manager. Witnessing the event were Mr. Georgy Makumbule from WWF Tanzania and Mr. Lucas Senoya Goroi, Game Warden for Selous Game Reserve.

  “This boat engine has been purchased through WWF-Sweden funding and will go a long way in supporting law enforcement activities at Mtemere Wildlife Camp in the Selous Game Reserve”, said Mr.  Makumbule 
  On his part, Mr. Kalokole said he was very thankful to WWF for their generous support that came through Ruvuma Landscape Programme at the right time. He promised to exercise great care for the engine so that it lasts for a long time.
  WWF TZ’s Conservation Manager, Mr. Gerald Kamwenda (second left) handing-over a new boat engine YAMAHA40 HP to Mr. Gregory Andrea Kalokole, Senior Game Warden of Selous Game Reserve, witnessing are Mr. Georgy Makumbule (extreme left) from Ruvuma Landscape Programme and Mr. Lucas Senoya Goroi (extreme right), Game Warden from Selous Game Reserve.
  Posing with the new boat engine YAMAHA 40 HP are Mr. Gregory Andrea Kalokole (Right), and Mr. Lucas Senoya Goroi (Left) from the Selous Game reserve.

  0 0

  Bonanza  la waandishi wa habari na watangazaji Kanda ya Kaskazini linatarajiwa kufanyika june 28 katika viwanja vya General tyre  jijini Arusha na kushirikisha zaidi na wanahabari 150 na wadau wa habari.

  Akizungumza na waandishi wa habari jana  , Katibu wa chama cha waandishi wa habari za michezo na burudani mkoa wa Arusha,(TASWA- Arusha) Mussa Juma, alisema maandalizi muhimu ya Bonanza yameanza.

  Juma alisema bonanza hilo,ambalo huandaliwa na TASWA Arusha na kampuni ya MS UniquePromotion litatanguliwa na semina ya siku moja ya wanahabari mkoa wa Arusha,  ambayo itashirikisha baadhi ya wajumbe wa kamati ya tendaji ya TASWA Taifa.

  Hata hivyo alisema bado TASWA Arusha na kampuni ya MS Unique wanatafuta wadhamini wa bonanza hilo ambalo litakuwa ni la tisa kufanyika.

  Juma alisema hivi karibuni wadhamini wa bonanza hilo, watatangazwa sambamba na zawadi kwa washindi.

  Alisema katika tamasha hilo, wanahabari na wadau wa habari watashiriki katika michezo ya soka, kuvuta kamba, mbio za magunia,mpira wa pete, kukimbiza kuku na kucheza muziki.

  Katika tamasha la mwaka jana, hakukuwa na bingwa wa soka baada ya TASWA Dar es Salaam na timu ya chuo cha Uandishi wa habari(AJTC) kushindwa kufungana.

  Kwa upande wa mpira wa pete TASWA Dar es Salaam, alishinda, huku katika mchezo wa kukimbiza kuku TASWA Arusha ilishinda na katika kamba timu ya Sunrise ilishinda wakati timu ya radio 5 na Arusha one zilitamba katika mbio za magunia.

  Timu ya Waandishi na watangazaji toka mkoa wa Manyara ya ORS ilishinda zawadi ya timu yenye nidhamu,timu nyingine zilizoshiriki ni Wazee Klabu,Pespi,TBL na timu ya timu ya Kitambi noma.

  0 0


  0 0


  Sehemu ya Wacheza Filamu nchini waliokuwa wamebeba Jeneza lenye Mwili wa Marehemu George Otieno Okomu (George Tyson) wakijipanga tayari kwa akili ya kuongoza shughuli ya Kuga mwili iliyofanyika kwenye viwanja vya Leaders Club,Kinondoni jijini Dar es Salaam leo.Mwili huo umesafirishwa kupelekwa nchini Kenya ambako ni nyumbani kwao na Marehemu kwa ajili ya mazishi yatakayofanyika Jumamosi ijayo baada ya kukamiliza kwa mipango yote.Picha zote na Othman Michuzi.

  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Mh. Said Meck Saddick akiwaongoza waombolezaji mbali mbali kwenye shughuli ya kuaga mwili wa Marehemu George Otieno Okomu (George Tyson) waliofika kwa wingi kwenye viwanja vya Leaders Club,Kinondoni jijini Dar es Salaam leo.

  Mkurugenzi Mkuu wa Kipindi cha The Mboni Show,Mboni Massimba (kulia) akiwa ni mwenye huzuni sana kwa kuondokewa na Mwaznilishi mwenza kwa Kipindi chake hicho ambaye alifariki Dunia katika ajali ya Gari huko Mkoani Morogoro wakati wakitokea Mkoani Dodoma kukabidhi msaada wa Madawati katika moja ya shule za msingi zilizopo mkoani humo ikiwa ni maadhimisho ya Miaka miwili ya kipindi hicho.

  Aliekuwa Mke wa Marehemu George Otieno Okomu (George Tyson),Yvone Chelly (Monalisa) na Mwanae Sonia wakiwa ni mwenye Majonzi makubwa kwa kuondokewa na mpendwa wao.Kushoto ni Mama wa Monalisa,Bi. Natasha.

  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Mh. Said Meck Saddick akitoa nasaha zake wakati wa msiba huo.


older | 1 | .... | 459 | 460 | (Page 461) | 462 | 463 | .... | 3278 | newer