Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110171 articles
Browse latest View live

Ankal uso kwa uso na King Maluu, apata burudani ya mdomo wa bata

$
0
0
Ankal akiwa na mpiga saxophone maarufu nchini Tanzania Akuliake Salehe a.k.a. "King Maluu"  alipogongana nae akitumbuiza kwenye hoteli ya Kunduchi Beach jijini Dar es salaam jioni ya leo akiwa na Furaha band chini ya Mohamed Amon (anaepiga gitaa). King Maluu, ambaye alitamba sana enzi za Maquis du Zaire, Orchestra Safari Sound na Wazee Sugu, hivi sasa ni lulu katika tasnia ya Bongo Flava ambapo amekuwa akiwapiga taffu vijana wa kizazi kipya na saxophone yake. Mfano ngoma ya "Number one" ya Diamond na pia ya Ommy Dimples ya "Tupogo".
Sikiliza King Maluu anavyochambua saxophone kama karanga.

DIAMOND MPAKA SASA AONGOZA KURA ZA BET KWA KUNDI LA WASANII WA AFRIKA

$
0
0
Msanii Nasibu Abdul alias 'Diamond Platnumz' kwa sasa anakimbiza katika mchakato wa upigaji kura katika Tuzo za BET 2014 ambapo mpaka saa 10:55 leo jioni alikuwa anaongoza katika kundi lake akiwa na asilimia 75.79 ya kura zote akifuatiwa na Mafikizolo wenye kura asilimia 8.34. na wengine kama jedwali linavyoonesha hapo chini. Tuzo hizo zitatolewa Juni 29 mwaka huu jijini Los Angeles, Marekani. 
Kisha telemka chini hadi utapokuta "BEST INTERNATIONAL ACT: AFRICA" bofya tundu lenye jina lake kisha bofya "VOTE"... kitu na boxi!

ngoma azipendazo ankal

KINANA AMALIZA ZIARA YAKE WILAYANI KITETO,LEO AELEKEA WILAYANI SIMANJIRO MKOANI MANYARA.

$
0
0
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akitazama sehemu maalum ya kunyweshea maji mifugo,ambayo yeye mwenyewe aliiizindua
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akimtwisha ndoo ya maji mama wa jamii ya kimasai,mara baada ya kuzindua mradi wa maji safi na salama wenye thamani ya shilingi milioni 200 na zaidi, katika kijiji cha Ilela kata ya Esekii wilayani Kiteto mkoani Manyara.

Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiwasalimia wananchi mara baada ya kupokelewa katika kijiji cha Irkiushbor,wilaya ya Kiteto mkoani Manyara.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akipata maelezo ya mradi wa maji katika  kijiji cha Ilela kata ya Esekii wilayani Kiteto mkoani Manyara,Mradi huo una thamani ya zaidi ya shilingi milioni 200 na zaidi.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiwahutubia waanchi wa kijiji cha Nalangton,Wilayani Kiteto mkoani Manyara.

Sehemu ya Umati wa wananchi wakimsikiliza katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana alipokuwa akiwahutubia kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa mpira mjini Kibaya,wilayani Kiteto mkoani Manyara
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye akiwahutubia wananchi wa kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa mpira mjini Kibaya,wilayani Kiteto mkoani Manyara
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa mpira mjini Kibaya,wilayani Kiteto mkoani Manyara.
PICHA NA MICHUZIJR-KITETO MANYARA
PICHA ZAIDI BOFYA HAPA 

MRADI WA ULINZI SHIRIKISHI WASHIKA KASI MKOANI TABORA

$
0
0
Kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora SACP Suzan Kaganda leo tarehe 01/06/2014 ametoa T-shirts mia moja kwa vikundi vya ulinzi shirikishi wilaya ya Kaliua mkoa wa Tabora.
 Baadhi ya wawakilishi wa kikundi cha ulinzi shirikishi 
wilayani  Kaliua wakionesha T-shirts walizopewa na RPC Tabora
 kamanda wa polisi mkoa wa Tabora ACP Suzan Kaganda akitoa T-shirts kwa kikundi cha ulinzi shirikishi wilayani Kaliua

Vodacom kutengeneza ajira zaidi ya 400 kupitia madukayake yaliyokwisha kufunguliwa hadi sasa

$
0
0
Kampuni ya mawasiliano nchini ya Vodacom imendelea na azma yake ya kuhakikisha inawafaidisha wateja wake kupitia huduma zake huku wakitengeneza nafasi za ajira kupitia maduka yake yanayoendelea kufunguliwa nchi nzima. 
 Hayo yameelezwa na Mkuu wa Idara ya Mauzo ya Rejareja, Upendo Richard wakati akizindua duka jipya la Vodacom maeneo ya Sinza Afrika Sana ambalo linakuwa ni la 18 kwa wilaya ya Kinondoni pekee na la 79 Tanzania nzima. 
 “Dhamira kubwa ya kusambaza maduka haya ni kusogeza na kuboresha huduma kwa wateja wetu popote walipo lakini pia tunawatengeneza watanzania nafasi za ajira. Ajira hizi kwa namna moja au nyinigine ni suluhu la upungufu wake nchini na pia hupunguza mzigo kwa serikali katika jitihada za kuhakikisha watu wanajiajiri wenyewe.” Alisema Bi. Richard 
 Ameendelea kuwa kwa kila duka la Vodacom linalofunguliwa, watu watano mpaka saba huajiri kwa nafasi kama vile za; meneja wa duka, uhasibu, wauzaji simu, watoaji ushauri kwa wateja pamoja na wakala wa M-Pesa. 
Amesema kuwa duka hili likiwa ni la 79 kufunguliwa nchi nzima, takwimu zinaonyesha kuwa kuna takribani idadi ya wafanyakazi zaidi ya 400 wanafanya kazi katika maduka yote ya Vodacom yaliyosambaa nchi nzima. 
 “Wateja wote wa Vodacom sasa wasipate tabu za kwenda maeneo ya mbali kutafuta huduma za kimawasiliano badala yake watumie duka hili lililopo hapa Sinza Afrika Sana.” Alisema Bi. Richard na kuongezea, “Huduma zinazotolewa hapa ni sawa na maduka mengine ili kuweza kutimiza haja zao na kuepukana na usumbufu wa kwenda maeneo kama Mlimani City, Quality Center. Mkifanya hivyo mtasababisha msongamano wa watu hali ambayo inapelekea na foleni ambazo zinasababisha kuchelewa kupata huduma.” 
 Nae mteja wa kwanza kutumia duka hilo mara baada ya kufunguliwa rasmi, Alfred Joseph, ambaye ni mkazi wa Sinza Afrika Sana ameishukuru Vodacom kwa jitihada zao za kusogeza huduma kwa wateja na kuwapunguzia usumbufu wa kusafiri umbali mrefu. 
 “Kabla ya kufunguliwa kwa duka hili, tulizoea kwenda Mlimani City kufuata huduma ambapo ilikua ni changamoto kubwa sana. Kwa mfano kwetu sisi wafanyakazi, muda mwingine unakuwa umetoka kazini umechoka halafu unahitaji huduma kwa uharaka lakini unashindwa kuzifikia mpaka uanze safari ya kwenda Mlimani City. Kwa kweli ulikua ni usumbufu mkubwa sana, tunashukuru kwa kuliona hilo na kulifanyia kazi na sidhani kama nitasumbuka tena kwenda huko.” Alisema mkazi huyo 
 Akitoa machache wakati wa uzinduzi Meneja wa duka hilo, Swaum Manengelo amebainisha shukrani zake za dhati kwa Vodacom kwa ushirikiano waliouonesha mpaka duka hilo linakamilika na kuanza kutoa huduma kwa wateja. 
 “Naweza kusema ndoto ya wakazi wa Sinza Afrika Sana kuwa na huduma za Vodacom karibu yao zimetimia, ufunguzi wa duka hili ni ushahidi tosha. Ningependa kuwakaribisha wateja wote wa kutoka maeneo haya na ya jirani kutembelea dukani hapa na kuhudumiwa.” Alisema Bi. Manengelo, na kumalizia, “Ningependa kuwatoa hofu wateja wetu wasihofie ubora wa huduma na bidhaa zinazopatikana hapa kwani wengi hudhani labda huduma zinazotolewa Mlimani City au Quality Centre ni bora zaidi, hilo si kweli na nathubutu waje kujaribu leo.”
 Meneja wa duka jipya la huduma kwa wateja la Vodacom lililopo Sinza Afrika Sana jijini Dar es Salaam, Swaum Manengelo akifungua mlango kuashiria ufunguzi rasmi wa duka hilo. Wakishuhudia tukio hilo ni Mkuu wa Idara ya Mauzo ya Rejareja Upendo Ricahrd (kushoto) na Meneja Uhusiano wa Nje wa kampuni hiyo Salum Mwalim (kulia).
 Mkuu wa Idara Mauzo ya rejareja wa Vodacom Tanzania, Upendo Richard  akikagua huduma na bidhaa mbali mbali ndani ya duka jipya la huduma kwa wateja lililopo Sina Afrika Sana jijini Dar es salaam muda mfupi baada ya kuzinduliwa rasmi hivi karibuni. Hilo ni duka la 18 la huduma kwa wateja Wilayani Kinondoni na la 79 nchi nzima.
Mkuu wa Idara ya Mauzo ya Rejareja wa kampuni ya Vodacom Tanzania, Upendo Richard (kushoto) akimkabidhi Meneja wa duka jipya la hudfuma kwa wateja la Vodacom Sinza Afrika Sana Swaum Manengelo funguo ya duka hilo kuashiria ufunguzi rasmi wa duka hilo kuanza kutoa huduma kwa wateja  Akishuhudia tukio hilo katikati ni Meneja Uhusiano wa Nje wa kampuni hiyo, Salum Mwalim.Uzinduzi huo umefanyika hivi karibuni jijini Dar es salaam.

mwili wa george tyson ulipowasili Dar es salaam

$
0
0
 Dada wa marehemu Tyson, Doreen akilia kwa simanzi baada ya mwili wa kaka yake kuwasili katika hospitali ya Kairuki Mikocheni jijini Dar es salaam jana jioni. 
 Jeneza lenye mwili wa George Tyson likiingizwa mochwari katika Hospitali ya Kairuki, Mikocheni jijini Dar.
Wadau wa tasnia ya filamu wakiwa na jeneza la Mwili wa Tyson ukiwa mochwari katika Hospitali ya Kairuki.
PICHA NA GPL

kongamano la kimataifa la wanasayansi lafanyika jijini Dar es Salaam

$
0
0
Wananchi wanaoishi kando ya maeneo ya ardhioevu na sehemu ambazo mito inakutana na bahari wamehimizwa kuzingatia matumizi bora ya maeneo hayo ili yasiweze kuleta madhara ya mali, uhai wao na uharibifu wa viumbe hai vilivyopo katika sehemu hizo. 
Naibu Waziri, Wizara ya Maliasili na Utalii, Bw. Mahmoud Mgimwa, alisema hayo wakati akifunga mkutano wa wanasayansi toka Afrika na nje ya bara hilo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam. Kongamano hilo lililojulikana kama Afrideltas liliangalia na kuchambua mabadiliko yanayotokea sasa katika maeneo ya ardhi oevu na makutano ya mito na bahari. 
Waziri Mgimwa alisema serikali imeyachukua mapendekezo ya wanasayansi hao kwa kuwa yanalenga kulinda maeneo hayo yaweze kutumika kwa kwa faida ya sasa na vizazi vijavyo. 
Pia alisema kuwa serikali itahakikisha sera, sheria na kanuni mbalimbali zinafuata maelekezo ya kitalaamu kama yaliyotolewa katika kongamano hilo kwa vile maeneo hayo yanafaida kubwa za kiuchumi. 
“Katika kuhakikisha jambo hili linafanikiwa, wadau wote wanatakiwa kushiriki katika kutoa elimu ya mazingira kwa wakazi wa maeneo hayo,”alisema. 
Alisema Tanzania ina changamoto ya kulinda aina mbalimbali za viumbe katika maeneo ya ardhioevu ambavyo vipo katika hatari ya kutoweka kutokana na shughuli za kibinadamu. 
Naye, mjumbe wa kamati ya maandalizi ya Kongamano hilo, Prof. Amos Majule ambaye pia ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Uthamini Raslimali (IRA) ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) alisema kongamano hilo lilikuwa na faida kubwa kwa washiriki hao wa kimataifa.
“Kila mmoja alijifunza toka kwa mwenzake na kubadilishana uzoefu na kutoa mapendekezo tuliyoona yanafaa,” alisema. 
Alisema moja ya mapendekezo hayo ni kuona elimu mbadala inatolewa zaidi kwa jamii jinsi ya kutumia na kulinda rasilimali zilizopo katika maeneo ya ardhioevu na maeneo mito inapokutana na bahari. Pia alisema watunga sera na watoa maamuzi wameshauriwa kutoa elimu zaidi kwa wananchi ili rasilimali zinazopatikana katika maeneo hayo ziweze kutumika kwa faida ya sasa na vizazi vijavyo. 
Alisema changamoto iliyojitokeza ni kwamba kuna njia zisizo endelevu za matumizi ya madawa ya mbolea katika Kilimo, ukataji misitu na ujenzi wa makazi katika maeneo hayo na kuleta athari za kimazingira. Aliongeza kusema kuwa kutokana na mabadiliko ya tabia nchi, maeneo hayo pia yanakumbwa na mafuriko na kuathiri mazao ya Kilimo, uvuvi na makazi yao jambo ambalo ni hatari kwa uhai wao. 
Naye Mradibu wa Kenya Wetlands Biodiversity, Dk. Wanja Njingi alisema kutokana na tafiti zilizowasilishwa katika mkutano huo, nchi za Africa zimefaidika na mawazo na taarifa mpya ya jinsi ya kushughulikia na kulinda maeneo ya ardhioevu.
 “Kupitia tafiti hizi sasa tunaweza kurekebisha mambo yaliyoharibika katika nchi zetu,” aliongeza kusema. 
Kongamano hilo lilijumuisha wanasayansi kutoka nchi mbalimbali zikiwemo Kenya, Afrika Kusini, Ethiopia, Sudan, Senegal, Nigeria, Uholanzi, Ufaransa, Ubelgiji na mwenyeji Tanzania. Pia wanasayansi hao walitembelea Bonde la Mto Rufiji kujionea hali ya bonde hilo na shughuli zinazoendelea.
 Naibu Waziri, Maliasili na Utalii, Bw. Mahmoud Mgimwa (katikati)akiongea wakati wa kufunga kongamano la kimataiafa la wanasayansi lililofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.  Wengine katika picha ni, Mkurugenzi wa Taasisi ya Uthamini Raslimali (IRA) ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Prof. Amos Majule (kulia) na Kaimu Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa wizara hiyo, Dkt. Iddi Mfunda.

Naibu Waziri, Maliasili na Utalii, Bw. Mahmoud Mgimwa (katikati) akifurahia jambo wakati wa kufunga kongamano la kimataifa la wanasayansi lililofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.  Wengine katika picha ni, Mkurugenzi wa Taasisi ya Uthamini Raslimali (IRA) ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Prof. Amos Majule (wa pili kulia), Kaimu Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa wizara hiyo, Dkt. Iddi Mfunda (kushoto) na Dk. Catherina Masao wa IRA (kulia) .


WAHARIRI NA WANAHABARI WATEMBELEA HIFADHI YA KISIWA CHA SAANANE JIJINI MWANZA

$
0
0
Baadhi ya Wahariri wa habari na Waandishi waandamizi toka vyombo mbalimbali vya habari wakitoka katika lango la ofisi za Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Saanane tayari kuelekea kisiwani.
Baadhi ya Wahariri wa habari na Waandishi waandamizi toka vyombo mbalimbali vya habari wakikaribishwa na Mwongoza Watalii katika Hifadhi ya Taifa ya Saanane Patricia Mtenga.
Safari ya kuelekea katika eneo la kuanzia ziara ya kitalii katika Hifadhi hiyo ikaanza.
Baadae Wahariri wa habari na Waandishi waandamizi toka vyombo mbalimbali vya habari wakapata historia ya Hifadhi hiyo kutoka kwa Muongoza Watalii Fua Hamis.
Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

TAARIFA YA KIFO/MSIBA WA BABA MZAZI WA BEATRICE SINGANO

$
0
0
MAREHEMU MAREHEMU NI MAURICE NOEL SINGANO

Bibi Maria Singano wa Sahare Tanga anasikitika kutangaza kifo cha mume wake mpendwa Lt Col (Rtd)Maurice Noel Singano kilichotokea  Chennai India tarehe 31/05/2014.
Mipango ya mazishi inafanyika nyumbani kwa mtoto wake Mikocheni B,Dar es salaam.
Kutakuwa na Misa siku ya Alhamisi kanisa la Mt. Martha Mikocheni Dar es salaam.Mazishi yanatarajiwa kufanyika siku ya Ijumaa tarehe 6/6/2014 Tanga.


BLOG HII INATOA SALAM ZA POLE KWA FAMILIA NZIMA, NDUGU, JAMAA NA MARAFIKI WOTE 

...BWANA AMETOA NA BWA BWANA AMETWA JINA LA BWANA LIBARIKIWE  

News alert: Mama Mzazi wa Mhe Zitto Kabwe Afariki dunia

$
0
0
Mbunge wa Kigoma Kaskazini Mhe Zitto Kabwe akiwa na mama yake Mama  Bi. Shida Salum, enzi za uhai wake. Mhe. Zitto kupitia mtandao wa Twitter amearifu kuwa mama amefariki dunia leo.

The 6th Welcoming Ramadhan Conference 1435H to be held on 22nd June, 2014 in Dar es salaam

$
0
0
Dear Brothers & Sisters in Islam,

Peace and Blessing of Allah be with you,
Alhamdulillah, we are set for another Ramadhan with another Welcoming Ramadhan Conference 1435H.

Tanzania Muslim Professionals Association (TAMPRO) is again 
bringing to you the 6th Welcoming Ramadhan Conferences 1435H that will be held on 22nd June, 2014 at
Julius Nyerere International Convention Centre - Shaaban Robert Street Posta/Gymkhana Area.
The Conference will bring together more than 600 Practitioners, Scholars and Experts to discuss and share their knowledge and experience on the Islamic principles, instruments and issues related to Raising Muslim Youth in today's world through the 1435H theme of “Our Youth, Our Future”.

Professor Mohamed Badamana From Nairobi University -https://profiles.uonbi.ac.ke/badamana/content/prof-badamana-mohamed, Sheikh Mussa Kundecha, Amir The Supreme Council of Islamic Organizations - Baraza Kuu,Brother Ali Masoud aka Masoud Kipanya - http://www.kipanya.de/aboutcartoonist.htm will lead the presentations to inspire the fruitful discussion on: 
1. Challenges of raising the Muslim Youth in Today's Rapid Changing world, 
2. The Qur'an, The Country Constitution and The Future of Muslim Youth 3. Muslim Youth, Media and Globalization, respectively.

The participation contribution are TZS 30,000 per person, Couple is TZS 50,000 that will cater for Food and other organization expenses.

We are also looking for the interested Brothers & Sisters who can sponsor University Students from UDSM, IFM, CBE....etc (any number) for them to be exposed in this kind of events.  Call 0715 670714 or 0789100000.

For Booking your Seat, Kindly call 0712588375 (Male) or 0686666686 (Female)
 


May Allah bless you in what you are doing in the service of Ummah-Alwaahumma Amiyn.
Wabillaah tawfiiq.

Mohamed
Do you want to make the most out of this opportunity? Then get ready and plan! Prepare your hearts for the imaan recharging journey in the month of Ramadan. Our pious predecessors used to start preparing for Ramadan days before it arrived.
Read more on Islamic Online University's blog! CLICK HERE
Do not forget to subscribe! 

TAARIFA YA MSIBA CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM

$
0
0
Familia ya Prof Cuthbert  Zebadia Kimambo wa Chuo Kikuu Dar es  Salaam inasikitika kutangaza kifo cha Mtoto wao mpendwa Samwel Cuthbert Kimambo (pichani) kilichotokea alfajiri ya leo tarehe 1 June 2014 kwa ajali ya gari. 
Habari ziwafikie wana Kimambo wote popote pale walipo, wana Tarimo wote popote pale walipo; ndugu, jamaa na marafiki pamoja na wafanyakazi wote wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.  
Mipango ya Mazishi inafanyika nyumbani kwa Baba wa Marehemu, Mtaa wa Kileleni, Nyumba namba 33, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

























CUF chafanya uchaguzi wake Wilaya ya Mjini

$
0
0
 Katibu Mkuu wa CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akisalimiana na wanachama wakati akiwasili ukumbi wa Basra Mtoni Kidatu kwa ajili ya uchaguzi wa CUF Wilaya ya Mjini
 Katibu Mkuu wa CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad,  alipowasili ukumbi wa Basra Mtoni Kidatu kwa ajili ya uchaguzi wa CUF Wilaya ya Mjini
 Naibu Katibu Mkuu wa CUF Zanzibar Hamad Massoud Hamad akizungumza wakati akifungua mkutano mkuu wa uchaguzi Wilaya ya Mjini katika ukumbi wa Basra Mtoni Kidatu.
Baadhi ya wajumbe wa Mkutano Mkuu (CUF) Wilaya ya Mjini  Unguja, wakifuatilia mkutano huo katika ukumbi wa Basra Mtoni Kidatu. (Picha na Salmin Said, OMKR)

Na Hassan Hamad, OMKR.
Chama cha Wananchi CUF leo kimeendelea na uchaguzi wake  ngazi ya Wilaya kuwachagua viongozi mbali mbali wakiwemo Makatibu wa Wilaya, Wenyeviti pamoja na wajumbe wa mkutano mkuu Taifa.

Viongozi wengine wanaochaguliwa ni wajumbe wa kamati tendaji  pamoja na wajumbe wa viti maalum ngazi ya Wilaya.
Akifungua mkutano mkuu wa uchaguzi Wilaya ya Mjini unaofanyika ukumbi wa Basra Mtoni Kidatu, Naibu Katibu Mkuu wa CUF Zanzibar Hamad Massoud Hamad, amesema viongozi wote watakaochaguliwa wana umuhimu mkubwa kwa maendeleo ya chama hicho ngazi ya Taifa.
Hivyo amewataka wajumbe wa mkutano huo kuwa makini katika uchaguzi huo, ili kuwachagua viongozi watakao kuwa tayari kukitumikia chama, na kuepuka kuwachagua viongozi kwa sababu ya kujuana.
Amesema lengo la chaguzi hizo ni kuimarisha na kujenga chama kwa kufuata misingi ya demokrasia, na kuwasisitiza wajumbe hao kutochagua viongozi wenye makundi, misimamo ndani ya chama, na badala yake wachague viongozi majasiri na walio tayari kujitolea, ili kukiwezesha chama hicho kupata ushindi katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.
Mhe. Hamad Massoud ambaye ni mwakilishi wa Jimbo la Ole (CUF), ametanabahisha kuwa iwapo wajumbe wa mkutano huo watawachagua viongozi wasio kuwa na sifa, baraza kuu la uongozi linayo mamlaka ya kutengua uamuzi huo na kuitisha chaguzi nyengine.
Katibu Mkuu wa CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, nae ameungana na wajumbe wa mkuano huo wa CUF Wilaya ya Magharibi, kuchagua viongozi wa Wilaya watakao kiongoza chama hicho kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.
Uchaguzi huo unaendelea katika Wilaya za Magharibi, Kaskazini “B”, Kati na Kusini Unguja, baada ya kukamilika kwa chaguzi hizo katika Wilaya zote nne za Pemba na mbili za Unguja, hatua ambayo inakamilisha chaguzi hizo kwa Wilaya zote za Zanzibar.
Mchakato wa uchaguzi huo utaendelea kesho kwa wajumbe wa mkutano mkuu Taifa kuchukua fomu kwa ajili ya kugombea kuchaguliwa katika baraza kuu la uongozi Taifa.

Kili music tour yavunja rekodi Mwanza

$
0
0
 Vanessa Mdee na Ommy Dimpoz wakimakinika katika show ya Kilimanjaro Music Tour iliyofanyika katika Uwanja wa Kirumba na kuwavutia maelfu ya mashabiki. Ziara hii inadhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager.
 Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Rich Mavoko akipagawisha wakazi wa Mwanza katika show ya Kilimanjaro Music Tour iliyofanyika katika Uwanja wa Kirumba na kuwavutia maelfu ya mashabiki. Ziara hii inadhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager.
 Wakazi wa Mwanza wakiwa wamefurika kwa maelfu huku wakishangilia wakati kundi la Weusi likitumbuiza  katika show ya Kilimanjaro Music Tour iliyofanyika katika Uwanja wa Kirumba na kuwavutia maelfu ya mashabiki. Ziara hii inadhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager.

NSSF YAENDESHA KAMBI ZA UPIMAJI WA AFYA BURE KANDA YA ZIWA

$
0
0

Shirika la Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), limeendesha  kambi za upimaji wa Afya Bure kwa wakazi wa Kanda ya Ziwa kwa kipindi cha mwezi mmoja.

Lengo la kambi hizi ni kuweza kutoa elimu na  kuwahamasisha wanachama wa NSSF na wananchi kwa ujumla waweze kujenga  tabia ya kupima afya zao mara kwa mara na kujiwekea mfumo bora wa maisha ili kuepukana na magonjwa sugu yasiyoambukiza.


Zoezi hili litaanzia mkoa wa Mara, Manispaa ya Musoma  kwenye Viwanja vya Shule ya Msingi Mkendo, kuanzia tarehe 28/05/2014,  kwa siku tatu mfululizo, kuanzia saa mbili asubuhi mpaka saa kumi na moja Jioni.  Baadae, Kambi hizi zitaendelea katika mikoa ya Shinyanga , Wilaya ya Kahama, Mkoa wa Geita na  Mkoa wa Kagera.


HUDUMA ZITAKAZOTOLEWA

Huduma mbalimbali zitatolewa bure kwenye kambi hizi zikiwemo;


Upimaji wa Shinikizo la damu
Upimaji wa sukari kwenye damu- Kisukari

Upimaji wa hali ya lishe (Uwiano wa Urefu kwa Unene)

Utoaji wa dawa za Minyoo Ushauri wa kitaalam kwa watakaokutwa na Matatizo Ushauri nasaha  na upimaji hiari wa VVU (UKIMWI) Kutoa vipeperushi vya Maelezo ya uboreshaji wa Afya.

Huduma  zote hizi zitatolewa na NSSF, BURE.


NSSF inaendelea kuwasii na kuwahimiza wakazi wa kanda ya ziwa kuwa waendelee kujiandikisha kwenye NSSF HIARI Scheme. NSSF HIARI Scheme ni kwa ajili ya wajasiriamali wadogo, wachimbaji wadogo, Ushirika wa Bodaboda , Ushirika wa Wakulima pamoja na wanachama wa Mifuko mingine ya hifadhi ya jamii.


Jiunge na NSSF HIARI Scheme ili uweze kujipatia mafao bora ya NSSF yakiwemo Bima ya Afya BURE kwa familia nzima (SHIB), mikopo nafuu ya SACCOS,  pamoja na Mafao bora mengineyo.


Wananchi wa kanda ya ziwa wanakumbushwa na kuhimizwa kujitokeza kwa wingi ili kupimwa na kupewa ushauri wa afya zao Bure.

NSSF INAJENGA MAISHA YAKO YA SASA NA YA BAADAE.
 Mkuu wa Wilaya ya Musoma, Jackson Msome ambaye alikuwa mgeni rasmi wakati wa ufunguzi wa Kambi ya Upimaji Afya Bure Mkoani Mara akifafanua jambo mara baada ya kutembelea banda NSSF ambapo zoezi la upimaji afya lilikuwa likiendeshwa na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF). Watu 1080 walipima maambukizi ya  virusi vya ukimwi na watu 2020 walipima magonjwa ya kawaida. Kulia ni Meneja wa Mafao ya Matibabu NSSF, Ali Mtulia.
Wakazi wa Mkoa wa Mara wakisubiri kumuona daktari kupata ushauri.
 Daktari wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Lucy Simbila (kulia), akimpima shinikizo la damu mmoja  ya  watu waliojitokeza  kupima afya mkoani Mara juzi, katika kambi ya Upimaji Afya Bure inayoendeshwa na NSSF katika mikoa ya Kanda ya Ziwa. 
 Wakazi wa Mkoa wa mara wakiwa kwenye foleni ya kuelekea kwenye vipimo wakati wa zoezi hilo.
 Baadhi ya watu waliojitokeza katika zoezi hilo wakiwa kwenye foleni kuelekea kwenye vipimo wakati wa zoezi hilo.
 Madaktari wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), wakimpa ushauri mmoja wa watu waliofika kupima afya.
Madaktari na Maofisa wa NSSF walioendesha kambi ya upimaji wa afya mkoani mara wakiwa katika picha ya pamoja.

MKUTANAO WA WADAU WA HUDUMA YA AFYA YA MSINGI (PHC) KWA JAMII MKOANI RUKWA

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya akifungua rasmi Mkutano wa wadau wa Huduma ya Afya ya Msingi (PHC - Primary Health Care) kwa Wananchi Mkoani Rukwa tarehe 30 Mei 2014 katika ukumbi wa RDC mjini Sumbawanga. Katika kikao hicho mambo mbalimbali ya msingi kuhusu afya ya jamii yalijadiliwa na kuwekewa mpango kazi wa utekelezaji katika kuimarisha afya ya jamii Mkoani Rukwa. Miongoni mwa mambo yaliyojadiliwa ni pamoja na mkakati wa kupunguza vifo vya mama wajawazito, maendeleo ya shughuli za usafi wa mazingira, utekelezaji wa shughuli za chanjo ya magonjwa mbalimbali, utaratibu wa utoaji wa PF 3, hali ya homa ya Dengu na lishe. 
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Manyanya akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano huo. Katika salam zake za ufunguzi alisisitiza juu ya usafi wa mazingira ambao ndio kinga kuu ya magonjwa mbalimbali yakiwemo ya kuambukiza kama Dengu na magonjwa ya mlipuko. Aliupongeza mpango wa Sumbawanga Nga'ara ambao kwa kiwango kikubwa umeleta mabadiliko ya usafi katika mji wa Sumbawanga tofauti na siku za nyuma. Aliipongeza pia Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga kwa hatua waliyofikia wa kuagiza magari mawili ya kubebea taka yatakasaidia katika kuimarisha mpango huo wa usafi katika Manispaa ya Sumbwanga na Mkoa wa Rukwa kwa ujumla.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Dkt. John Gurisha akiwasilisha mada ya hali ya huduma ya afya ya mama, baba na mtoto Mkoani Rukwa katika mkutano huo.
Mwanasheria Mfawaidhi wa Serikali Mkoa wa Rukwa Msomi Prosper Rwegerera akiwasilisha mada ya utaratibu wa utoaji wa PF 3 kwa mtu alijeruhiwa. Alisema PF 3 ni muhimu katika ushahidi wa kimahakama pale mtu atakapokuwa anadai haki yake mahakamani kutokana na jeraha aliliopata na pia inakuwa ni kithibitisho cha kisheria kwa kilichotokea kwa majeruhi husika. Katikati ni Afsa Afya wa Mkoa wa Rukwa Ndugu Kenedy Kyauke.
Sehemu ya wadau wa Mkutano huo wakifuatilia mada mbalimbali zilizowasilishwa kwa umahiri mkubwa. Na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa @rukwareview.blogspot.com

Castle Lager Perfect Six yanoga kuelekea fainali za Kanda

$
0
0
Timu nne za soka za kanda ya mashariki zimefanikiwa kuvuka na kutinga hatua ya ligi ndogo ya mashindano ya Castle Lager Perfect Six kwa mikoa ya Morogoro na Dodoma.

Katika michezo ya hatua ya mchujo ikirishikisha timu nane za mikoa hiyo, kwa upande wa Morogoro timu za Mzinga FC na Ndezi FC zenyewe zilikata mapema tiketi ya kucheza ligi hiyo huku kwa Dodoma ikiwa ni Schalke 04 FC pamoja na Market FC.

Schalke 04 na Market FC zilikata tiketi juzi kwa kushika nafasi ya kwanza na pili katika uwanja wa Central msikiti wa Gadaff mjini Dodoma baada ya kuvuka katika hatua ya mchujo wakati Ndezi FC na Mzinga FC zikifanya hivyo katika michezo iliyofanyika uwanja wa shule ya msingi Kiwanja cha Ndege Manispaa ya Morogoro.

Meneja wa Bia ya Castle Lager, Kabula Nshimo waandaaji wa Castle Lager Perfect Six alisema kuwa baada ya kumalizika kwa hatua ya mchujo kwa michezo iliyofanyika Morogoro na Dodoma inayounda kanda ya mashariki na kupata timu nne, timu hizo zitacheza ligi ndogo ili kupata timu moja itayowakilisha kanda ya mashariki katika mashindano hayo ya taifa jijini Dar es Salaam.

Nshimo alisema kuwa ligi ndogo itafanyika Juni 7 mwaka huu Manispaa ya Morogoro kwa kuzikutanisha washindi wa kwanza wa Dodoma ambazo ni timu za Schalke 04 na Market FC na Ndezi FC na Mzinga FC ili kucheza na kupata mshindi wa kanda ya mashariki atayewakilisha kanda hiyo kwenye mashandano hayo jijini Dar es Salaam.

Alisema shindano la Castle Perfect Six limelenga kuzungumza na wanywaji wa Castle Lager ambao wana shauku ya kucheza mpira wa miguu na kujumuika pamoja. 

Nshimo alisema kuwa mechi zilizochezwa wikendi hii zimeonyesha jinsi gani Watanzania wana mwamko na shauku kubwa ya kushiriki mashindano kutokana na watu kujitokeza kwa wingi maeneo mbalimbali ambapo yalifanyika mashindano hayo ya kwanza.

Vilevile wikendi hii yalifanyika mashindano hayo kwenye mkoa wa Dar es salaam kwenye viwanja vya Barafu Mburahati, uwanja wa Garden uliopo Kinondoni, Bulyaga Temeke katika hatua za awali za kupata wawakilishi wa Kanda hiyo watakaocheza fainali za taifa. Mashindano yanaendelea pia kwenye mikoa ya Mwanza na Musoma katika hatua ya mwanzo kupata wawakilishi wa kanda ya Ziwa.

Mechi zilizochezwa wikendi hii ilikuwa ni awamu ya kwanza ya mashindano hayo ambapo timu zitakazofuzu hatua hiyo ya mikoa zitachuana katika ngazi ya kanda na hatimaye taifa. Washindi wa fainali za taifa watajipatia fursa ya kipekee kwenda kutembelea jiji la Barcelona huko Hispania na kuiona timu ya Barcelona ikicheza na pia wataweza kujionea mambo mbalimbali ya kihistoria katika uwanja wa Camp Nou.
Mchezaji wa timu ya Matema,Hafidh Mohammed (kulia) akipiga hesabu za kumtoka mchezaji wa IP Sports Club, Hamis Daudi katika mashindano ya Castle Lager Perfect Six kwenye viwanja vya Garden Kinondoni jijini Dar es Salaam jana.Matema ilishinda 2-0.
Mchezaji wa timu ya IP Sports Club,Hassan Chidigo (kushoto) akijaribu kufunga katika gori la Matema,katika mashindano ya Perfect Six kwenye viwanja vya Garden kinondoni jijini Dar es Salaam jana.Matema ilishinda 2-0.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

kutoka maktaba: Kikosi cha pamba FC "TP LINDANDA" ya mwanza

$
0
0
Kikosi cha kazi cha Pamba FC a.k.a "TP Lindanda" ya Mwanza iliyokuwa moto wa kuotea mbali enzi zake. Mdau mwenye kukumbuka majina yao msaada tutani tafadhali. Picha kwa hisani ya Paul Rwechungura

DIAMOND AWEKA HISTORIA NEW JERSEY

$
0
0
 All Star Club Elizabeth New Jersey Diamond akikamua licha ya show kuchelewa kuanza na wapenzi wa Diamond kushikwa na jazba wakitaka aendelee lakini ikashindika kutokana na muda wa kufunga club kufika. 
 AJ nae akifanya yake baada ya kupewa nafasi ya ufunguzi katika show hiyo iliyofanyika New Jersey.
AJ Ubao na Dirty Hary wakishambulia jukwaa kwenye show ya kufubgua pazia iliyoanyika New Jersey na baadae Prezidaa wa Wasafi, Diamond Plutnumz kuwapagawisha mashabiki wake wa ukanda wa pwani ya mashariki.

Viewing all 110171 articles
Browse latest View live




Latest Images