Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 456 | 457 | (Page 458) | 459 | 460 | .... | 3348 | newer

  0 0


  Kunradhi kwa picha ya kusumbua hisia

  Mtu mmoja ambaye hakufahamika jina lake mara moja ameuawa kwa kupigwa risasi na majambazi eneo na Clock Tower jijini Arusha. 

  Inasemekana majambazi hayo yalikuwa yakipora kwenye Bureau Change iitwayo Nothern ambapo marehemu alikuwa akipita jirani na eneo hilo na alipowaona alipiga kelele ndipo akafyatuliwa risasi kadhaa na kupoteza maisha.  0 0

  Na Paul Mallimbo, Kampala, Uganda
  Rais Yoweri Museveni, amesema kiongozi bora ni yule anayefuata maagizo ya Mungu na kuwatumikia binadamu wote kwa usawa na haki. Rais Museveni aliyasema hayo (Juni mosi) wakati ibada ya kuombea mchakato wa kumfanya Marehemu Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere kuwa mwenyeheri na hatimaye kutangazwa mtakatifu. 
  Alisema hata kwenye maandiko matakatifu ya Biblia kuna mistari inayomtaka binadamu ampende binadamu mwenzake kama anavyojipenda yeye;“Kwenye biblia kuna sehemu inauliza kuwa utampendaje Mungu ambaye hujawahi kumuona, na ushindwe kumpenda binadamu mwenzako,” Alisema kwa sababu aliwahi kufanya kazi na mwalimu, anaweza kutoa ushahidi kwamba mwalimu alifanya yote mawili, kumtii Mungu na kuwatumikia binadamu. 
  Alisema mojawapo ya sababu iliyomfanya Marehemu Papa Paulo II kutangazwa mtakatifu kuisaidia Ulaya Mashariki, ambayo wananchi wake walikuwa hawamwamini Mungu. “Marehemu Papa Paulo II alisaidia kuikomboa Ulaya Mashariki kutoka kwenye ukomunisti, wananchi walikuwa hawaamini kuna mungu, lakini kwa juhudi zake aliwafanya wamwamini na kumpenda Mungu,”alisema. 
  Rais Museveni alisema anatarajia kupeleka ushahidi kwa Papa Benedict kwamba Mwalimu anasifa za kutangazwa kuwa mtakatifu kwa sababu alimtii Mungu na kuwatumikia binadamu. “Mimi nitapeleka ushahidi kwa Papa, kwamba mbali na mwalimu kumtii Mungu na kuwpenda binadamu wote, pia aliwakomboa Waafrika kutoka Ruvuma mpaka Capetown, huu ni ukweli siyo hadithi,alisisitiza Rais Museveni. 
  Kufuatia hatua hiyo ya kwenda Roma kutoa ushahidi, Rais Museveni amesema katika maadhimisho ya kuombea mchakato wa Mwalimu kuwa Mtakatifu yatakayofanyika mwakani, ameahidi kuwaita maraisi wote waliowahi kufanya kazi na Mwalimu Nyerere ili kuuthibitishia ulimwengu kuwa Marehemu Baba wa Taifa ameweza kuwaunganisha Waafrika. 
  Alifafanua kuwa Mwalimu ametoa mchango mkubwa wa ukombozi kwa nchi za Msumbiji, Zambia, Zimbabwe, Namibia, Angola, Afrika Kusini, Uganda na Tanzania yenyewe. Hivyo kuja kwa viongozi hao kushiriki ibada hii itakuwa Baraka kubwa. 
   Rais Museveni ambaye alitumia muda mwingi wa hotuba yake kuzungumza Kiswahili, alisema baada ya jitihada za mwalimu kuikomboa Uganda, ndipo na wao walipoweza kuzisaidia nchi za Rwanda, Sudan Kusini na Congo kujikomboa na kuongeza kuwa kama si juhudi za mwalimu wasingekuwa na uwezo wa kuwasaidia wengine. 
  Aidha Rais huyo wa Uganda ambaye amekuwa madarakani tangu mwaka 1986, alisema kuwa, kwa upande wa viongozi weusi, hakuna kiongozi ambaye ametoa mchango mkubwa kama Marehemu Mwalimu Nyerere. 
  “Hapa Duniani sidhani kama kuna mtu mweusi mwingine ambaye ametoa mchango kama mwalimu, na hili nimelishudia mwenyewe sikuambiwa na mtu, aliongeza kuwa, hata mzee wetu Nelson Mandela alifanya kazi kubwa Afrika ya Kusini lakini Mwalimu alifanya kazi kubwa zaidi ya ukombozi wa Afrika, Alisema. 
  Alisema Mwalimu aliikomboa Tanzania na kuwafundisha dini ya Kristu, kwa vitendo siyo kwa maneno. Aliongeza kuwa nchi nyingine za Afrika zimepatwa na machafuko ya ukabila na dini kutokana na msingi mbaya wa viongozi waliotangulia. 
  “Tanzania ni nchi ya Wakristo, Waislamu na wale wengine wanaoamini dini za kienyeji lakini mwalimu aliwafundisha Watanzania fikra za kizalendo za umoja,alisema . 
  Alisema Uganda haikupata elimu nzuri juu ya jambo hilo, viongozi wa kwanza wa taifa hilo waliwapandikiza wananchi chuki, kwamba dini ni kumchukia mwenzako, waumini wa dini moja kuwachukkia waumini ya dini dini nyingine na matokeo yake ni umwagaji wa damu.
   “Biblia inasema kile unachopanda ndicho unachovuna, kwa hiyo sisi hapa tulipanda mbegu mbaya na tukavuna umwagaji wa damu,” alisema na kuongeza kuwa Tanzania haijawahi kuona umwagaji mkubwa wa damu zaidi ya ajali za magari na ile ya kipindi kile wakati askari wa Tanzania walipokwenda Uganda kupigana na Idd Amin.
  Nadhani hii ndiyo damu pekee mmeona,” alisema. 
   Alisema baadhi ya waasisi wa Uganda waliwafundisha kuwa wakristu kuwachukia Waislamu, matokeo yake nchi imekuwa katika umwagaji wa damu tangu ilipopata uhuru. Aliongeza kuwa mpaka 1986 wakati anaingia madarakani raia 800,000 wa Uganda walikuwa wamekufa kutokana na chuki za udini na ukabila. 
  “Uganda imeshuhudia umwagaji mkubwa sana wa damu, Congo wameona damu, Sudan, Somalia, Kenya, Rwanda na Burundi ni Tanzania pekee ambayo imekuwa kama kisiwa cha amani, hii yote ni kutokana na mchango wa mwalimu Nyerere ambaye alidumisha amani, umoja na maendeleo kwa watu wake.
   Alisisitiza kuwa, kwa sababu mojawapo ya sababu ya kumfanya mtu awe mtakatifu ni watu kutoa ushahidi wa matukio mbali mbali yaliyofanywa na mtu huyo wakati wa uhai wake, aliahidi kwenda Roma kutoa ushahidi kuhusu matendo ya Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere. 
  “Nikienda kwa Baba Mtakatifu, Papa Benedict nitatoa ushahidi mzuri juu ya marehemu Mwalimu Nyerere tena nitatoa kwa maandishi siyo kwa maneno pekee yake”alisisitiza. 
  Ibada ya kumuombea Baba wa Taifa ilifanyika katika Kanisa la Mashahidi wa Uganda, Namugongo, ambapo ibada hiyo iliendeshwa na Askofu Mkuu wa Jimbo la Kampala, Dk. Cyprian Kizito Lwanga, ambaye aliiomba serikali kusaidia kuboresha eneo la kanisa hilo ili liwe na miundombinu ya kisasa zaidi. 
  Hii ni mara ya nane ibada ya kuombea mchakato wa kumfanya baba wa Taifa kuwa Mwenyeheri na hatimye mtakatifu unafanyika katika kanisa hilo nchini Uganda. Mchakato huo ulianza mwaka 2006. 
   Katika ibada hiyo ambayo imehudhuria na maelfu ya Watanzania, pamoja na mataifa mbali mbali duniani, pia ilihudhuriwa na familia ya Marehemu Baba wa Taifa, Waziri Mkuu wa Uganda Amama Mbabazi mawaziri na wabunge kutoka Uganda, ambapo Tanzania iliwakilishwa na Balozi wa Tanzania nchini Uganda.
  Flashback: Hayati Baba wa Taifa enzi za uhai wake akiingia katika kanisa la Mtakatifu Peter la Oysterbay jijini Dar es salaam. Alifanya hivyo kila siku asubuhi

   Baadhi ya Watanzania wakati Rais wa Uganda, Mhe Yoweri Kaguta Museveni akiwatubia mamia ya wananchi waliohudhuria misa ya kuombea mchakato wa kumfanya Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere kutangazwa Mwenyeheri na hatimaye mtakatifu
   Rais wa Uganda, Mhe. Yoweri Kaguta Museveni akiwatubia mamia ya wananchi waliohudhuria misa ya kuombea mchakato wa kumfanya Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere kutangazwa Mwenyeheri na hatimaye mtakatifu
   Baadhi ya watu waliohudhuria walikwenda kumpa mkono Mama Maria Nyerere
  Flashback: January 21, 2006 - Bodi ya Dayosisi ya iliyoundwa kuanza mchakato wa mwalimu Nyerere kutangazwa Mwenyeheri na hatimaye mtakatifu


  0 0

  Kwa wasanii wao kila usemi ni sehemu ya maisha yao! Juzi baadhi ya wasanii huko Ughaibuni wameibuka kwa kuyabandika majina mazoezi ya kukata uzito au unene wa mwili " Zoezi hili sasa lipewa jina la "UZEE MWISHO CHALINZE" usemi ambao umebuniwa na msanii Joti wa Ze Komedi. Zoezi hilo maalumu la kupiga vita unene au minyama ya uzembe limeshaanza kufanyiwa kazi kisawa sawa na wasanii,mmojawapo ni mwanamuziki Jhikoman ambae kwa sasa ana ziara ndefu huko Ulaya
  Mwanamuziki Jhikoman akijifua kupiga vita unene huko ughaibuni
  Hii ndio maana mwanamuziki Jhikoman huwa hachoki awapo jukwaani


  0 0

  Mbunge wa Kigoma Kaskazini Mhe Zitto Kabwe akiwa na Mwenyekiti wa CUF Profesa  Ibrahimu Lipumba wakati wa kuuaga Mwili wa mama yake kipenzi Bi Shida Salumu aliyefariki leo kabla ya kusafirishwa kwenda Kigoma kwa mazishi
  Ndege Ikiandaliwa Ili kuweza Kuingiza Mwili wa Marehemu Mama yake Zitto Kabwe
  Waheshimiwa Wabunge na Baadhi ya Viongozi wakibeba Jeneza lililobeba Mwili wa Marehemu Mama Yake Zitto Kabwe Bi Shida Salum  kuingiza kwenye ndege Tayari kwa safari ya kwenda Kigoma Kwenye mazishi
  Prof Ibrahimu Lipumba akijadili jambo na Mwenzie baada ya kupakia mwili wa marehemu kwenye ndege kuelekea kigoma Kwenye maziko
  Rais wa TASWA Juma Pinto akiwa VIP ya Terminal 1 JKN Airport alipokutana na Cardinal Pengo wakati wa kuaga mwili wa Mama yake Zitto Kabwe

  0 0

   Makamu wa Rais Dkt. Mohamed Ghalib Bilali, Rais Mstaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi na viongozi wengine na waombolezaji wakiwa katika mazishi ya marehemu Amina-Zahara Shabani Mtengeti katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es salaam jioni hii. Marehemu, ambaye ni mdogo wa Hajat Mwantumu Malale, Dkt. Asha-Rose Migiro, Balozi Radhia Msuya, alifariki jana
   Shughuli za mazishi zikiendelea
   Makamu wa Rais Dkt. Mohamed Ghalib Bilali akiweka udongo kaburini
   Rais Mstaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi akiweka udongo kaburini
   Waziri Mkuu Mstaafu Dkt Salim Ahmed Salim akiweka udongo kaburini.

  0 0

  Mtoto Nasrah Rashid, aliyekuwa akitibiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili baada ya kuugua na kupata ulemavu kwa kufungiwa kwenye boksi miaka minne amefariki dunia leo na kuacha huzuni kubwa miongoni mwa wananchi wakiosikia mkasa wake wa kusikitisha. 
   Nasra alifichwa kwenye boksi na mama yake mkubwa aitwaye Mariamu Said mkazi wa Kiwanja cha Ndege Manispaa ya Morogoro tangu akiwa na miezi tisa baada ya mama yake mzazi kufariki dunia.
  Bw. Rashid Mvungi akimuangalia mtoto wake Nasrah Rashid (4) ambaye ni mlemavu wa viungo aliyefungiwa chumbani na kufichwa kwenye boksi bila ya kufanyiwa usafi tangu akiwa na umri wa miezi tisa.  0 0

  Ankal akiwa na mchambuzi maarufu nchini wa mambo ya soka Dr Liky Abdallah wakati wakiandaa kipindi maalumu ya Kombe la Dunia 2014 ambacho kitarushwa Michuzi TV hivi karibuni. Hivyo mdau kaa chonjo usikilize uchambuzi wa uhakika toka kwa mtaalamu huyu.

  0 0

  Waziri Mkuu Mizengo Pinda anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika mkutano wa mashauriano ya  uwekezaji wa awamu ya kwanza ya Mradi wa Mabasi yaendayo Haraka (DART) unaoanza leo.

  Mkutano huo wa siku mbili unawakutanisha wawekezaji mbalimbali wa ndani na nje kwenye kituo cha mikutano Mlimani City, jijini Dar es Salaam.

  Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mabasi yaendayo haraka Dar es salaam (DART), Bi. Asteria Mlambo, amewaambia waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam kuwa mkutano huo wa mashaurino utatoa nafasi kwa wawekezaji kuzijua fursa mbalimbali za uwekezaji zitakazopatikana kwenye mradi huo unaojengwa kwa mabilioni ya pesa.

  “Washiriki wote kwenye mkutano wa majadiliano watapata fursa ya kutembelea eneo la mradi na watapata nafasi ya kuuliza maswali na kupata ufafanuzi wake kuhusu mradi,” Bi. Mlambo alisema na kuongeza kuwa mkutano huo ni muhimu sana.

  Akifafanua zaidi, Mtendaji huyo Mkuu alisema   mabenki  na taasisi mbalimbali za kifedha, makampuni ya kutengeneza mabasi, makampuni ya mawasiliano, mifuko ya kijamii na mengineyo mengi yamealikwa kwenye mkutano huo.

  “Mada mbalimbali kuhusu mradi zitatolewa ambapo Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu ,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Bw.Jumanne Sagini atawasilisha mada kuhusu mradi wa DART,” alisisitiza.

  Hivi karibuni, Wakala huo uliandaa mkutano ambao uliwakutanisha wamiliki wote wa daladala jijini Dar es Salaam pamoja na Kampuni ya Usafirishaji Dar es Salaam (UDA) na wadau wengine ili kuwafahamisha na kushaurina ni jinsi gani wataweza kunufaika na mfumo mpya wa usafiri jijini Dar es Salaam.

  Katika mkutano huo, wadau hao walielezwa faida na fursa zitakazopatikana kwenye mfumo mpya wa usafirishaji jijini na jinsi wao watakavyoweza kuwa sehemu ya mradi.

  Mwezi April mwaka huu, wakala wa DART ulikamilisha zoezi la kusajili mabasi ya daladala yanayopita katika barabara ya Morogoro au kukatiza katika njia hiyo.
   
  Hatua hiyo ya kuandikisha mabasi hayo ilikuwa moja ya matayarisho ya kupisha mradi huo wa mabasi yaendayo haraka.
   
  Kwa sasa wakala huo uko kwenye mchakato wa kuwezesha upatikanaji wa watoa huduma kwenye mfumo mpya wa mabasi yaendayo haraka awamu ya kwanza ambayo inajumuisha barabara ya Morogoro, Kawawa na mtaa wa Msimbazi kwa njia kuu na nyingine za kiungo. 

  Kulingana na mpango wa uendeshaji wa mfumo wa DART, barabara zinazohusika zitapaswa kutumiwa na mabasi ya mfumo huo pekee.

  Jumla ya njia 64 jijini Dar es Salaam zitakoma kutumika kutokana na kuanza kwa mradi huo.

  0 0

  Katika kuendelea kusherehekea Muungano wetu na pia kujiunga na wenzetu wa nchi ya Zambia ambao nao mwaka huu wanasherehekea miaka 50 tangu wapate Uhuru (25 Oktoba), Ubalozi wa Tanzania nchini Zambia unapenda kuwajulisha kuwa umeandaa maonesho ya bidhaa zinazozalishwa nchini Tanzania.

  Ubalozi wa Tanzania nchini Zambia unachukua nafasi hii kuwakaribisha rasmi Watanzania kuja kushiriki katika maonesho haya. Tuna amini ni nafasi nzuri ya kujitanganza na kuonana uso kwa uso na wadau mbalimbali ili kupanua wigo wa biashara.
  Maonesho haya ambayo yamebeba jina la "TANZANIA WEEK" yatafanyika katika viwanja vya Ofisi ya Ubalozi Lusaka, Zambia, kuanzia tarehe 25 hadi 31 Julai 2014.

  Kwa maelezo zaidi na mawasiliano tumia njia zifuatazo:

       Nukushi ya Ubalozi: tanzanhighcom@zambia.co.zm
       Namba ya Simu: +260211253323/4 
       
  Maafisa wa Ubalozi;
        
  i)Bibi Justa M. Nyange - simu ya kiganjani +260-979-401-433 
        Nukushi : kitutuj@yahoo.com

      ii)Bw. Richard M. Lupembe  - simu ya kiganjani +260-965-031-754
            Nukushi : rlupembe@yahoo.com.

      iii)Bw. Mogosi S. Munatta - simu ya kiganjani +260-979-411-011
            Nukushi : munatta@yahoo.co.in.
        
     iv)  Bw. Huddy A. Kiangi …….simu ya kiganjani +260-977-934-240
           Nukushi : hkiangi@yahoo.com.


  KARIBU SANA LUSAKA, ZAMBIA

  0 0

  Mkuu wa Wilaya ya Tarime, John Henjewele (kushoto) akitembelea banda la Shirika la Heifer International Tanzania katika maonyesho ya maadhimisho ya wiki ya maziwa mjini Musoma Mkoani Mara hivi karibuni.
  Mfugaji wa Shrika la Heifer, Emannual Mgesi (aliyevaa Kaunda suti nyekunde) akimweleza Mkuu wa Wilaya ya Tarime, Joh Henjewe pamoja na wakazi wengine wa Musoma kuhusu ufugaji bora wa ng’ombe wakati wa maadhimisho ya wiki ya maziwa mjini Musoma Mkoani Mara hivi karibuni.
  Meneja wa Shirika la Heifer nchini, Dk.Henry Nyakoi (katikati) akimweleza Mkuu wa wa Wilaya ya Butiama, Angelina Mabula (kulia) kuhusu kazi mbalimbali za shirika hilo wakati wa maadhimisho ya wiki ya maziwa mjini Musoma hivi karibuni. Kauli mbiu ya mwaka huu ni ‘Fuga ng’ombe wa maziwa uboreshe kipato na lishe.

  0 0

  Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Ndg. Fanuel Mbonde akifungua mafunzo kuhusu uzingatiwaji na uelewa wa masuala ya jinsia kwa watumishi wa Wizara hiyo jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
  Mkufunzi wa Masuala ya Jinsia na Rais wa Chama cha Majaji Wanawake Duniani (TAWJA) Jaji Mstaafu Eusebia Munuo akiongea wakati wa mafunzo kuhusu uzingatiwaji na uelewa wa masuala ya jinsia kwa watumishi wa Wizara ya Katiba na Sheria jijini Dar es Salaam mwishoni mwaka wiki.
  Mkufunzi wa Masuala ya Jinsia na Mwenyekiti wa Chama cha Majaji Wanawake Nchini (TAWJA) Jaji Engera Mmari Kileo akiongea wakati wa mafunzo kuhusu uzingatiwaji na uelewa wa masuala ya jinsia kwa watumishi wa Wizara ya Katiba na Sheria jijini Dar es Salaam mwishoni mwaka wiki. (Picha na Wizara ya Katiba na Sheria).

  Na Mwandishi Wetu

  Watumishi wa Wizara ya Katiba na Sheria na watumishi wa umma kwa ujumla wametakiwa kuwa chachu ya mabadiliko yatakayoondoa vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia katika maeneo mbalimbali ya kazi.

  Akiongea na watumishi hao mwishoni mwa wiki, Mwenyekiti wa Chama cha Majaji Wanawake Tanzania (TAWJA), Jaji Engera Mmari Kileo alikumbusha kuwa vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia bado vipo katika maeneo mengi ya kazi na kuwa wakati umefika kwa watumishi wa umma kushiriki kikamilifu katika kuvikomesha.

  “Vitendo vya matumizi mabaya ya madaraka yanayoambatana na rushwa ya ngono (sextortion) vipo Tanzania na duniani kote, ndiyo maana chama chetu kimeamua kuvisema, kuvikemea na kuvimaliza kabisa,” alisema wakati akiendesha mafunzo kuhusu uzingatiwaji wa masuala ya jinsia yaliyoendeshwa kwa ushirikiano kati ya Jaji Kileo na Rais wa Chama cha Majaji Wanawake Duniani (IAWJ), Jaji Mstaafu Eusebia Munuo.

  Kwa mujibu wa Jaji Kileo, pamoja na kufanyika katika maeneo ya kazi, vitendo hivyo pia hufanywa maeneo ya vijijini ambapo watu wenye madaraka huyatumia vibaya kwa kushinikiza rushwa ya ngono.

  “Wanawake na wanaume huathirika na ‘sextortion’, ingawa kwa kiasi kikubwa waathirika wakubwa ni wanawake,” alisema Jaji Kileo katika mafunzo hayo yaliyohudhuriwa na watumishi wote wa Wizara ya Katiba na Sheria na kufanyika katika ofizi hizo jijini Dar es Salaam.

  Akiongea katika mafunzo hayo, Jaji Munuo alisema Tanzania imeridhia mikataba mbalimbali ya kimataifa na kikanda kuhusu uzingatiwaji wa haki za binadamu na kijinsia ambayo inalenga kuhakikisha kuwa vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia vinamalizwa.

  “Tunapaswa sasa kuona utekelezaji katika maeneo yetu ya kazi, la sivyo haya mambo mazuri yatabaki katika makaratasi tu,” alisema Jaji Munuo ambaye amestaafu hivi karibuni akiwa Jaji wa Mahakama ya Rufani.

  Akisisitiza kuhusu umuhimu wa kukomesha vitendo vya unyanyasaji, Jaji Munuo alisema vitendo hivyo vikiachwa viendelee, kuna uwezekano wanawake wakaacha kuzaa kwa sababu ya kuhofia kutopata muda wa kutosha kuwahudumia watoto mara wanapojifungua.

  “Katika baadhi ya nchi za ulaya, wanawake wasomi wamekataa kuzaa na sasa mamlaka zinawaomba wazae na kupewa likizo ya miaka miwili na hata matunzo ili kujenga nguvu kazi,” alikumbusha Jaji Munuo.

  Akiongea wakati wa kufungua mafunzo hayo, Katibu Mkuu wa Wizara Ndg. Fanuel Mbonde alisema mafunzo hayo ni sehemu ya mkakati wa Wizara yake wa kutekeleza maagizo ya Serikali kuhusu uzingatiwaji wa masuala ya jinsia katika mipango ya Serikali.

  “Serikali imeagiza taasisi zake kuzingatia masuala ya jinsia katika kila jambo linalotekelezwa, kwa hiyo mafunzo haya ni muhimu ili kuongeza uelewa wa watumishi,” alisema Ndg. Mbonde.

  0 0

  Zenith Media Yatwaa Kombe la Sports Extra Day Bonanza kwa Jiji la Arusha.
  Timu ya Banana investiments ikisali kabla ya kuanza kwa mchezo.
  Huyu nae alikuwa aki #BRAZUCA katika mchezo wa Sports Xtra Day Jijini Arusha.
  Mbwiga wa Mbwiguke the Captain wa Sports Xtra akiwapanga vijana wake.

  0 0
 • 06/02/14--04:11: MAGESE ALILIA MTOTO


 • 0 0

  SACO AHMED Z. MSANGI – KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA

  0 0

   Both AFC Leopards and Academie Tchite players pose for a joint group photo with H.E Arown Suge the Kenyan Ambassador to Khartoum before kick off of their game. Ambassador Suge has been a blessing in all AFC matches.
  AFC Vs Academie Group stage match

  Today [Semis]:

  AFC Leopards [Kenya] Vs Academie Tchite [Burundi], 5:30pm

  Victoria University [Uganda] Vs Ahly Shandi [Sudan], 8:30pm


  The inaugural CECAFA Nile Basin Cup tournament goes into the semifinals this Monday evening here in Khartoum City, Sudan with both games causing a lot of tension.


  AFC Leopards Vs Academie Tchite

  Both clubs were part of the Group ‘B’ composition and AFC Leopards struggled to edge their opponents 1-0 in their last group stage match. Their late goal [83’] came through Benard Mangoli.

  But both teams qualified for the quarters with Leopards leading the group on maximum points and Academie finishing 3rd with only 3 points. Academie however later registered the biggest shock of the tournament when they dumped the hosts and tourney favourites Al-Merreik 3-2 on spot kicks after a 1-1 draw in the normal time of the second quarter finals last Friday.


  Victoria University Vs Ahly Shandy

  The two clubs have never played each other and Ahly Shandy coach Elnnagar Al-Ftih confesses knowing nothing much about their opponents. Victoria’s Muzamir Mutyaba is expected back in action after serving his one match suspension.


  Ahly Shandy is however an attack minded club with almost all departments functioning to perfection.  The Ugandan defence commanded by Captain Martin Mpuga will have a busy evening to contain the speeding strikers of Saaed Mustafa, Bashir Mohamoud, Awad Mohamoud and Addis Hintsa 


  Extra time granted

  In case no winner is decided in the 90 minutes of the normal time, the matches will go into a 30-minute extra time and if the same result doesn’t change after the added time, it will be penalties. Tuesday will be a resting day before the finals on Wednesday.


  ROGERS MULINDWA

  CECAFA MEDIA MANAGER

  +249-927-320-683  0 0

  The World Bank’s Board of Executive Directors has approved a US$50 million credit from the International Development Association (IDA) to provide continuing support to Tanzania’s efforts to improve the quality of life for urban residents through improved fiscal management and improved infrastructure. The project will benefit some 1.4 million Tanzanians, of which nearly half are women.

  The Tanzania Strategic Cities Project (TSCP) focuses on eight urban centers: Mwanza, Arusha, Mbeya, Mtwara, Kigoma, Tanga, Dodoma and Ilemela. The Danish foreign aid agency, DANIDA, will provide an additional US$6 million to support critical complementary activities.

  “The project supports the establishment of well-functioning and productive urban centers in Tanzania, which are essential for accelerating job creation and catalyzing the transformation of the Tanzanian economy and reducing poverty throughout the country,” says Philippe Dongier, World Bank Country Director for Tanzania.

  Launched in 2010, the original TSCP project notched significant gains including better fiscal management at local government levels, improved urban governance and planning, construction of first-ever sanitary landfills as well as storm drains, bus terminals and street lights. The project includes support for a new urban management tool (the Local Government Revenue Collection Information System, ‘LGRCIS’) that uses a GIS platform and will support local governments tax reporting, revenue collection, operations and maintenance, urban planning, permitting and land management systems. The modernized system allows online payments including via mobile phones. This system will improve how local governments collect taxes, with significant gains in transparency, accountability, and customer-focused timely responses.

  “Tanzanian cities are the locus of formal and informal activity and account for over 50 percent of the country’s economic growth said Onur Ozlu and Andre Bald, World Bank Co-Task Team Project Leaders. “Yet, institutional capacity and access to basic infrastructure has lagged significantly. This project will support the Government of Tanzania’s efforts to create dynamic urban areas that are conducive to inclusive growth and job creation.”

  0 0

  Serikali imeshauriwa kuweka mgawanyo sawa ya utekelezaji katika miraji ya Maji nchini ili kuondoa tatizo sugu la Maji kwa maeneo yenye ukame na upungufu mkubwa wa Maji.

  Akichangia wakati  wa bajeti ya Wizara ya Maji, mbunge wa Singida Mashariki Mh Tundu Lissu alisema imefika wakati serikali lazima iweke uwiano sawa wa mgawanyo wa fedha za miradi ya maji kwenye mikoa na sehemu zenye upungufu mkubwa wa Maji hapa nchini.

  Akitolea mfano jimboni kwake alisema bajeti ya mwaka huu kwa jimbo lake la Singida Mashariki jumla ya Milioni 839 zimetengwa kwa ajili ya jimbo lake. Alipongeza serikali kwa miradi miwili ya Maji iliyoanza kutekelezwa jimboni kwake katika wilaya ya Ikungi na Mungwaa na kwamba ukarabati wa visima vilivyojengwa na taasisi ya Catholic Service Relief (CSR) ukiendelea.

  Aliongeza kuwa kwa mikoa yenye vyanzo vya Maji kama vile Mito na Maziwa ni muhimu fedha kidogo zikatumika na nguvu nyingi ikaelekezwa kwenye maeneo yenye ukame mkubwa wa Maji kama vile Singida, Dodoma, Shinyanga na Simiyu.
  Mbunge wa Singida Mashariki, Mh Tundu Lissu akichangia hoja ya wizara ya Maji wakati wa Bajeti ya Makadirio na Matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka 2014/2015.

  0 0

  Kamishna Jenerali wa Magereza John Minja (kushoto) akisaini kitabu cha wageni mara alipowasilishwa katika ofisi ya Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT) Prof. Tolly Mbwete (kulia).
  Kamishna Jenerali wa Magereza John Minja (wa pili kulia) na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT) Prof. Tolly Mbwete (wa tatu) wakisani hati za makubariano ya ushirikiano kati ya Taasisi hizo mbili. Wakwanza kulia ni Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza nchini Dkt Juma Malewa na wa nne kulia ni Naibu wa Tatu wa Makamu Mkuu wa Chuo Prof. Modest Valisango anayeshughulikia Teknolojia na Huduma za Kujifunzia Chuoni hapo.
  Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza nchini Dkt Juma Malewa(wa kwanza kulia) na Prof. Modest Valisango (wa kwanza kushoto) wakisaini hati za makubaliano ya ushirikiano kati ya Jeshi la Magereza na Chuo Kikuu Huria cha Tanzania.
  Kamishna Jenerali wa Magereza John Minja ( kulia) na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT) Prof. Tolly Mbwete ( kushoto)wakibadilishana nyaraka muhimu za makubaliano ya ushirikiano mara baada ya kutiwa sahini.
  Kamishna Jenerali wa Magereza John Minja (wa pili kulia) akitoa maelezo kwa waandishi wa habari juu ya undani wa ushirikiano kati ya Jeshi la Magereza na Chuo Kikuu Huria.Wa kwanza kulia ni Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza nchini Dkt. Juma Malewa, wa nne kulia ni Naibu wa Tatu wa Makamu Mkuu wa Chuo Prof. Modest Valisango aliyepia Mkuu wa Teknolojia na Huduma za Mafunzo chuoni hapo.
  Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria (wa tatu kulia) akitoa maelezo kwa waandishi wa habari juu ya undani wa ushirikiano kati ya Jeshi la Magereza na Chuo Kikuu Huria.Wa kwanza kulia ni Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza nchini Dkt. Juma Malewa, wa nne kulia ni Naibu wa Tatu wa Makamu Mkuu wa Chuo Prof. Modest Valisango aliyepia Mkuu wa Teknolojia na Huduma za Mafunzo chuoni hapo. 

  Aliyewahi kuwa mfungwa kwa takribani mika 20 gerezani Ukonga Ng. Haruna Pembe (mwenye suti) akitoa ushuhuda wa jinsi alivyoweza kusoma na kumaliza shahada yake ya sharia akiwa gerezani.Picha zote na Insp Deodatus Kazinja, PHQ

  0 0  0 0


   MWANAMITINDO wa kimataifa wa hapa nchini na Miss Tanzania 2001 anaefanya kazi yake hiyo nchini Marekani Millen Magese ameiomba serikali kumpatia eneo ambalo atalitumia kujenga hospitali maalum ya kushugulikia afya ya wanawake.

  Millen alitoa ombi hilo jana wakati akizungumza na watu mbalimbali waliohudhuria semina ya bure kuhusiana na hali ya Endometriosis inayowakabili wanawake wengi hapa nchini na Afrika kwa ujumla. Millen anakabiliwa na tatizo hilo la Endometriosis ambalo ni hali ya mwanamke kushindwa kupata siku zake za mwezi katika hali ya kawaida na yenye kuleta madhara kwa afya yake hususan kwenye uzazi.

  Millen alisema kuwa akiwa kama mwanamke maarufu na mwenye ushawishi katika jamii yake ameamua kutoa elimu ya tatizo hilo ili kusaidia kuongeza uwelewa wa suala hilo ili kuwasaidia wanawake wengine. 

  Alisema kuwa kwa kuwa suala hilo linahusiana na afya hivyo linahitaji msaada wa ukaribu zaidi kutoka kwa wataalamu wa afya kwa ajili ya kusaidia wasichana na wanawake wenye matatizo mengine ya kiafya pia. Alisema kuwa mwanamke anaekabiliwa na tatizo kama hilo anafikia wakati anakuwa akitakiwa kufanyiwa upasuaji na lakini kutokana na ugeni wa tatizo husika kwa hapa nchini hakuna vifaa vya kutambua na kufanyia upasuaji huo. Ambapo mpaka sasa ni KCMC pekee ndio wana kifaa cha kuweza kutambua tatizo hilo.

  Alisema kuwa ameshaanza kupata misaada kutoka kwa watu mbalimbali wa Marekani kama vile taasisi ya Swan Development LLC, Texas ambao wameahidi kumpatia mashine za za kutambua tatizo na upasuaji pamoja na dawa, ambapo angependa ziwekwe hospital ya Dar es salaam kulingana na mapendekezo ya wadau ingawa lengo lake la muda mrefu ni kufungua hospital itakayojihusisha na magonjwa ya wanawake na ndio maana anaomba msaada wa serikali na wananchi kwa ujumla ili kufanikisha lengo hilo.

  "Ningependa kama kufungua hiyo hospitali basi iwe ni Dodoma au Bagamoyo kwa kuwa ni rahisi zaidi kwa Dodoma watu mbalimbali kufika na kwa Bagamoyo inakuwa ni rahisi pia kuzifikisha mashine kutoka Bandarini"alisema Millen. Aliongeza kuwa kwa kuwa tatizo hilo linakuja kutokana na kushindwa kulishughulikia mapema hasa wakati msichana anapokuwa amevunja ungo na kuanza siku zake za hezi akiwa na maumivu makali.

  Aliwataka watoto kuwaambia wazazi pindi wanapokuwa wakipatwa na maumivu makali yaliyopitiliza wakati wakiwa kwenye siku zao za hezi na pia wazazi kujadiliana na watoto wao punde hali hiyo inapotokea na kuwawahisha hospital ili wapatiwe huduma sahihi.

  Katika tukio hilo la jana Millen aliambatana na madaktari bingwa wa wanawake wawili ambao ni daktari Fadhlun M. Alwy na daktari Belinda Ballandya wote kutoka chuo kikuu cha Afya Muhimbili ambao walitoa elimu ihusianayo na tatizo hilo na Endometriosis.

  Watu wengi walijitokeza kupata somo hilo na kuzungumzia suala hilo wakiwemo, wanawake, wananume na watoto.

older | 1 | .... | 456 | 457 | (Page 458) | 459 | 460 | .... | 3348 | newer