Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 454 | 455 | (Page 456) | 457 | 458 | .... | 3270 | newer

  0 0

  Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Mhe. Sophia M. Simba (Mb.) na Mhe. Amina Makilagi (Mb) Katibu Mkuu wa UWT, Mhe. Dk. Pindi H. Chana (Mb) Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto na Anna T. Maembe Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto wakipongezana baada ya kupitishwa kwa Bajeti ya Wizara hiyo jumamosi iliyopita Bungeni Dodoma.
  Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Mhe. Sophia M. Simba (Mb.), Mhe. Dk. Pindi H. Chana (Mb) Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto na Anna T. Maembe Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto wakipongezana baada ya kupitishwa kwa Bajeti ya Wizara hiyo jumamosi iliyopita Bungeni Dodoma.

  0 0

  Timu ya JKT Ruvu leo itaanza mchakato wa kutafuta wachezaji wapya kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara kwenye uwanja wa JKT Mlalakuwa jijini.

  Zoezi la kusaka wachezaji hao ni la wazi na meneja wa timu hiyo, Joel Frank amewataka wachezaji wote wenye nia ya kucheza ligi kuu msimu ujao kufika kwa wingi katika uwanja huo kuanzia saa 1.30 asubuhi.

  Frank alisema kuwa wameamua kutafuta wachezaji kwa mtindo huo kwa lengo la kuona uwezo wao halisi na wala si kwa kukisia kama ilivyokuwa kwa timu nyingine.

  Alisema kuwa zoezi hilo litasimamiwa na kocha wao mkuu, Fred Felix Minziro kwa kushirikiana na wasaidizi wake, Azishi Kondo na Greyson Haule.

  “Hatusajili kwa kufuata majina, sisi ni tofauti na timu nyingine, tumeamua kubadili mfumo wa kusajili kwa mazoea na sasa tunasajili kwa kuona uwezo wa mchezaji mwenyewe uwanjani si kwa kusikia,” alisema Frank.

  Alisema kuwa zoezi hilo litaendeshwa kwa wiki moja na pia linahusisha wachezaji wanaotaka kucheza timu yao ya chini ya miaka 20 (U 20).

  “Hii ni fursa kwa wachezaji wenye uwezo na tunahitaji wachezaji 10 kwa ajili ya msimu ujao. Kamwe hatutasajili kwa kufuata wachezaji katika timu nyingine, sis tunasajili uwanjani na tunawaomba wajitokeze kwa wingi,” alisema.

  Aliongeza kuwa lengo la kufanya hivyo ni kuepuka matatizo waliyokumbana nayo katika msimu uliopita na pia kutwaa ubingwa wa ligi kuu ya Tanzania Bara kwa mara ya kwanza.

  “Tumechoka kushiriki, tunataka kutwaa ubingwa msimu ujao, msimu uliopita tulianza vizuri, tukapatwa na matatizo na kupoteza nafasi, tumeweka mikakati mipya na kwa sasa tumeanza kuifanyia kazi, tunauhakika itafanikiwa,” alisema.

  0 0

  Mkurugenzi wa Rangers Bureau De Change na Rangers Tours and Travel Agent, Daudi Madega (kushoto) akikabidhi jezi kwa mwenyekiti wa Taswa FC, Majuto Omary katika hafla fupi iliyofanyika makao makuu ya kampuni hiyo, Magomeni.
  Nahodha wa timu ya soka ya wandishi wa habari za michezo nchini, Mbozi Katala akizungumza mara baada ya makabidhiano hayo.

  Duka la kubadilishia fedha za kigeni la Rangers Bureau De Change lililopo Magomeni Mapipa, limetoa msaada wa jezi kwa timu ya soka ya Waandishi wa Habari za Michezo nchini (Taswa FC)  kwa ajili ya kuzitumia katika mechi zake mbali mbali za kirafiki na mashindano.

  Mkurugenzi Mkuu wa Rangers Bureau De Change na Rangers Tours and Travel Agent, Daudi Madega alikabidhi jezi hizo kwa mwenyekiti wa Taswa FC,  Majuto Omary katika hafla fupi iliyofanyika makao makuu ya kampuni hiyo, Magomeni.

  Madega alisema kuwa wametoa msaada huo kama mchango wao kwa timu hiyo ambayo inaonyesha mfano kwa kujishughulisha na michezo mbali ya kuandika.

  Alisema kuwa Taswa FC imedumu kwa muda mrefu na wao kama wadau wakuu wa michezo nchini, wameamua kuanza na timu hiyo na baadaye kuipa vifaa vya michezo timu yao ya netiboli (Taswa Queens) ambayo ipo katika kiwango cha juu.

  “Rangers Bureau De Change na Tours and Travel Agent ni wadau wakuu wa michezo hapa nchini, hii inatokana na mmiliki wake kuwa na timu ya soka (Baker Ranger) ambayo ina historia kubwa katika soka la Tanzania, hivyo msaada huu si wa kubahatisha, tunaahidi kufanya makubwa na timu ikiwa kuwapa mabasi yetu mbali mbali mbali katika safari za timu,” alisema Madega.

  Mwenyekiti wa Taswa FC, Majuto Omary aliishukuru kampuni hiyo kwa msaada huo na kuahidi kuutumia kwa mafanikio ya timu na wala si vinginevyo.

  0 0

   Mjomba wake na Ankal wa Libeneke la Globu ya Jamii, Bi. Shahada Ibrahim (wa tatu kulia) akiwa na Wahitimu wenzake wa Ualimu kwa ngazi ya Cheti wakirusha kwa pamoja kofia zao juu mara baada ya kula Nondozz zao katika Chuo ya Ualimu cha Mtakatifu Rock kilichopo Wilayani Korogwe,Mkoani Tanga,ikiwa ni mahafali ya Nane ya chuo hicho ambayo yalifanyika jana Mei 17,2014 Chuoni hapo.
  Ankal Shahada Ibrahim akipozi na Wahitimu wenzake.
   Shahada Ibrahimu akiwa ni mwenye furaha tele baada ya kulamba Nondozz yake hiyo aliyoisotea kwa miaka mibeee...
   Shahada akiongezwa na mjomba wake mkubwa Ismail.
   Mama Mzazi wa Shahada, ambaye ni dada wa Ankal, akimpongeza mwanae huku wote wakiwa na furaha tele.


  0 0

  Waziri Mkuu mstaafu na mbunge wa Monduli,Mh. Edward Lowassa akimjulia hali Mwenyekiti mstaafu wa CCM mkoa wa Arusha,Mzee Jackson Kaaya nyumbani kwake Poli Meru wakati alipofika kumuona na kumsabahi.Pembeni ni mkewe Bibi Jacobert Kaaya.Mzee Kaaya mwenye umri wa miaka 94 alikuwa Mwenyekiti wa kwanza wa TANU Mkoa wa Arusha hadi alipostaafu mwaka 1984.

  Mh. Lowassa alikuwa Katibu wa Chama wa mkoa enzi za uenyekiti wa Mzee Kaaya na ndiye aliyemfudisha uongozi wa kisiasa.Katika maongezi yao Mzee Kaaya amesema anasikitishwa na viongozi wa kizazi hiki kwa kuongoza kwa kulalamika badala ya kuchapa kazi.

  0 0

  baadhi ya walimu wakuu wa shule za sekondari Tanzania kanda ya mashariki kupitia umoja wao TAHOSSA wakimsikiliza ofisa elimu mkoa wa pwani hayupo alipofungua mkutano wao mjini Kibaha.
  Picha ya pamoja na baadhi ya walimu wakuu wanaounda umoja wao wa TAHOSSA Kanda ya mashariki.

  Na John Gagarini, Kibaha

  OFISA Elimu Mkoa wa Pwani Yusufu Kipengele amewataka walimu mkoani humo kuachana na tabia ya kutumia vilevi waingiapo madarasani kufundisha kwani hali hiyo inachangia kushuka kwa kiwango cha elimu.
  Imebainika kuwa baadhi ya walimuwa wamkuwa wakitumia vilevi aina ya viroba kabla ya kuingia madarasani kufundisha hali ambayo ni moja ya sababu ya kiwango cha elimu kushuka ambapo mwalimu husika kufundisha chini ya kiwango.

  Aliyasema hayo juzi mjini Kibaha wakati akifungua kikao cha umoja wa walimu wakuu wa shule za sekondari Tanzania (TAHOSSA) kanda ya Mashariki na kusema kuwa tabia kama hiyo haipaswi kufumbiwa macho na viongozi wa idara ya elimu ili kurekebisha mwenendo wa walimu.

  “Baadhi ya walimu wamekuwa wakitumia pombe aina ya viroba jambo ambalo limekuwa lickichangia maadili kuvunjika kwa walimu na wanafunzi wanaowafundisha,” alisema Kipengele.
  Alisema kuwa baadhi ya walimu wamekuwa wakitumia vilevi hivyo pamoja na wanafunzi hivyo kufanya taaluma kushuka kwani walimu hao uwezo wao unashuka na kushindwa kuwapatia kile wanachotakiwa kuwafundisha wanafunzi.

  Akijibu baadhi ya hoja ikiwemo ya kukosa fedha kwa ajili ya wasimamizi wa mitihani ya vitendo aliwataka kuhakikisha wanapeleka suala hilo kwenye uongozi wa bodi ili waridhie ili wazazi wachangie sehemu ya gharama hizo ambapo kwa upande wa serikali nayo itachangia kwa kiasi.

  Awali akimkraibisha mgeni rasmi ambaye ni ofisa elimu wa mkoa mwenyekiti wa TAHOSSA Omary Msami alisema kuwa wanakabiliwa na changamoto kubw aikiwa ni pamoja na mitihani ya vitendo kutokuwa na fedha toka wizarani.

  “Tunaomba tupatiwe mafunzo kazini kwani walimu hawapatiwi jambo ambalo linasababisha walimu kushindwa kwenda na wakati kwani baadhi ya mambo ya ufundishaji yamekuwa yakibadilika,” alisema Msami.

  Aidha aliomba ukaguzi mashuleni ufanywe kila mwaka ama baada ya miaka miwili ili kurekebisha kasoro zinazojitokeza na kuwalipia wakaguzi hao ili kuzipunguzia mizigo shule.
  Umoja huo unaundwa na mikoa ya Pwani na Morogoro ambapo kuna jumla ya shule 384 na walimu wakuu 131.

  0 0


  0 0

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongozana na Balozi wa Tanzania, nchini Japan, Salome Sijaona, mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Haneda, Tokyo, nchini Japan kwa ajili ya kuanza ziara ya siku sita. Kulia ni mke wa makamu, Mama Asha Bilal.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwasili kwenye Uwanja wa ndege wa Haneda, Tokyo, kwa ajili ya kuanza ziara ya siku sita. Kushoto kwake ni aliyekuwa Balozi wa Japan nchini Tanzania, Masaki Okada, (nyuma yao) ni Mke wa Makamu, Mama Asha Bilal na Balozi wa Tanzania nchini Japan, Salome Sijaona. Picha na OMR

  0 0

   Baadhi ya wafanyakazi wenzake wakitoa heshima za mwisho na kuuaga mwili wa aliyekuwa mwanasheria wa Wizara ya Maliasili na Utalii marehemu Luke Seyayi iliyofanyika katika kanisa la AIC Magomeni jijini Dar es salaam.
   Wanasheria wenzake wakiwa wameubeba mwili wa Marehemu Luke Seyayi tayari kwa mazishi katika makaburi ya Kinondoni.
  Wanasheria wenzake wakiwa wameubeba mwili wa Marehemu Luke Seyayi tayari kwa mazishi katika makaburi ya Kinondoni. 
   Familia ya Seyayi Mama mzazi (watatu toka kushoto) wakiwa na  nyuso za uzuni.
  Kaka zake Marehemu wakiweka shada la maua.   

  0 0

  BONDIA Cosmas Cheka anatarajia kupanda ulingoni Juni 1, 2014 kwa ajili ya kutetea taji lake la ubingwa wa TPBO anaoshikilia kwa kupambana na Suma Ninja katika ukumbi wa vijana socil hall wa Morogoro.
  Cheka amesema amejiandaa kupigana kawa raundi kumi hivyo mashabiki waje kuona kazi anayoifanya akiwa ulingoni bondia huoyo ambaye anatamba sambamba na kaka yake Francis Cheka ambaye alikuwa bingwa wa WBF ambao alivuliwa kizembe. Amesema yeye anataka afike mbali zaidi ya kaka yake huyo.
  Mpambano huo utakaosimamiwa na TPBO utasindikizwa na mapambano ya utangulizi kati ya Kudura Tamimu atakaevaana na Sadiki Yusufu wakati Mohamed Matimbwa ataoneshana umwamba na Twaha Kassimu.
  Siku hiyo kutakuwa pia na huzwaji wa DVD kali za ngumi wakiwemo mabondia wakali wanaotamba Duniani na hapa nchini kama Mohamed Matumla vs Fransic Miyeyusho, Japhet Kaseba Vs Thomas Mashali, Floyd Mayweathar na Manny Paquaio, Saul 'canelo' Alverez, Mike Tyson, Mohamed Ali, Felix Trinidad, Miguel Cotto na wengine wengi.
   DVD hizo za ngumi kali zitakuwa zikiuzwa na kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' Pamoja na kutambua sheria na taratibu za mchezo huo siku hiyo pia kuta kuwa na vifaa vya mchezo huo wa masumbwi vitakavyotolewa zawadi kwa mabondia na Kocha Super D ambaye ameahaidi kutoa, Gum sheets, Clip Bandeji, DVD za Mafunzo kwa mabondia, Bukta,Protector na vifaa mbalimbali kwa mabondia watakao onesha uwezo wa hali ya juu wa kutupiana masumbwi
  Cosmas Cheka (kushoto) baada ya kutangaza mpambano wake na Suma Ninja katika ukumbi wa vijana socil hall  wa Morogoro

  0 0

  Mshambuliaji wa Taifa Stars , Mbwana Samatta (juu) akikwepa kwanja wakati akijaribu kumtoka beki wa timu ya Taifa ya Zimbabwe, katika mchezo wa kwanza wa mchujo kuwania kupangwa kwenye makundi ya kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Mataifa ya Afrika 2015 zinazotarajia kufanyika nchini Morocco, wakati wa mtanange huo uliopigwa kwenye uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam. Katika mchezo huo Taifa Stars, ilishinda bao 1-0.
   ***********************************************
   Na Sufianimafoto, Reporter-Dar
  TIMU ya soka ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars leo imeiichapa timu ya Taifa ya Zimbabwe bao 1-0, katika mchezo wa kwanza wa mchujo kuwania kupangwa kwenye makundi ya kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Mataifa ya Afrika 2015 zinazotarajia kufanyika nchini Morocco, wakati wa mtanange huo uliopigwa kwenye uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.

  Katika mchezo huo uliochezeshwa na mwamuzi, Joseph Odartei Lamptey aliyesaidiwa na Malid Alidu Salifu na David Laryea wote wa Ghana, hadi mapumziko Taifa Stars walikuwa mbele kwa bao hilo 1-0, lilofungwa na John Boko katika dakika ya 13 na kudumu hadi mwisho wa mchezo huo.

  John Bocco ‘Adebayor’ alifunga bao hilo akiunganisha kwa guu la kushoto krosi maridadi ya mshambuliaji wa TP Mazembe ya DRC, Thomas Ulimwwengu.

  Kocha wa Tanzania, Mholanzi Mart Nooij alisema baada ya mchezo huo kwamba vijana wake wamecheza vizuri, lakini wangeweza kupata mabao zaidi kama wangetumia vizuri nafasi walizotengeneza.

  Kwa upande wake, kocha mzalendo wa Zimbabwe, Ian Gorowa alisema vijana wake walicheza vizuri, lakini walikosa bahati ya kupata mabao licha ya kutengeneza nafasi zaidi ya tatu nzuri.   Kikosi cha Tanzania kilikuwa; Deo Munishi ‘Dida’, Shomary Kapombe, Oscar Joshua, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kevin Yondan, Frank Domayo/Amri Kiemba dk71, Mrisho Ngassa/Haroun Chanongo dk77, Mwinyi Kazimoto, John Bocco/Khamis Mcha ‘Vialli’ dk85, Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu. 

  Zimbabwe; George Chigova, Partson Jaure, Danny Phiri, Hardlife Zvirekwi, Stephen Alimenda, Rendai Ndoro, Milton Ncube, Kudakwashe Mahachi, Cuthbert Malajila, Peter Moyo na Eric Chipeta.
  Mechi za marudiano zinatarajiwa kuchezwa  mwisho wa wiki ya mwezi Mei 30 na washindi wataingia kwenye hatua ya mwisho ya mchujo ili kuwania kupangwa kwenye makundi tayari kwa mbio rasmi za Morocco 2015.

  0 0

  BRAND NEW HITS FROM AJ & DIRTY HERRY ON THE STAGE WITH WCB 
  #WE SUPPORT OUR TALENTS#ENT WILL BE TELEVISED ON THE RED CARPET#
  GET YOUR TICKETS NOW WWW.DIAMONDUSATOUR.COM

  0 0

   Basi likiwa na wachezaji wa Arsenal likipita mitaa ya London kulikofurika mashabiki kila kona kushangilia ushindi wao wa ubingwa wa FA walioupata baada ya miaka 9
  Mzee mzima Asene Wenger bado haamini kuwa kalinyakua....

  0 0

   Pamoja na kupigwa marufuku mara kadhaa wachimabji hawa bado wameendelea kuchimba mchanga katika Mto Mbezi huku wakijaza magari makubwa yasiyo na idadi na tena wakifanya kazi hii mchana kweupeeee pyeeee  bila hata kuwa na woga. 
  Wachimbaji hawa wamekuwa wakifanya hivi kila inaponyesha mvua kubwa inayokusanya mchanga mwingi kutoka eneo jingine kusogeza eneo hili, na wao wamekuwa wakiuhamisha mchanga huo kwa kuuchimba na kuupakia katika magari na kisha kwenda kuuza. Zoezi hili linachangia mmomonyoko mkubwa wa kingo za mto huo ambako nyumba kibao zipo.
   Wachimbaji wakiendelea na kazi...


  0 0

  Mabigwa wa Sports Xtra Day 2014 mkoa wa Mwanza wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya mchezo wa fainali dhidi ya NMB Mwanza, ambapo SAUT walitawazwa kuwa mabingwa mara baada ya kushinda kwa mikwaju ya penati 5 - 4.
  BOFYA PLAY KUSIKILIZA TAARIFA.
  Washindi nafasi ya pili NMB Mwanza katika picha ya pamoja kabla ya kuvaana na SAUT.
  Kandanda safi la kuvutia limeonekana katika mchezo wa fainali kila timu ikicheza kwa umakini mkubwa kuepuka makosa kiasi kilichosababisha mchezo huo kuamriwa kwa mikwaju ya penati ambapo SAUT walitawazwa kuwa mabingwa mara baada ya kushinda kwa mikwaju 5 - 4 dhidi ya NMB Mwanza.
  Patashika langoni mwa NMB Mwanza.
  Kasi, ufundi, umakini vimevuta hisia za mashabiki viwanja vya Raila Odinga Chuo cha SAUT Mwanza katika michuano ya Bonanza la Sports Xtra kwa mkoa wa Mwanza. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0

  Shebo ni msanii mpya wa RnB ambaye amekuwa akifanya poa katika mikoa ya kanda ya ziwa hasa Mwanza ambako ndiyo kwao. Amekuja na style ya pekee sana katika RnB ya Tanzania. Ni tishio kubwa kwa wasanii wakongwe kama Benpol na Steve RnB.

  0 0

  Umoja wa Watanzania Ujerumani (U T U) Umezindua Mtandao wake leo hii Tarehe 19.05.2011, mjini Aschaffenburg ujerumani. Mtandao huo ambao umeaza kutumika kwa lugha ya Taifa ya Ujerumani (kijerumani) upo mbioni pia kutandaza habari kwa lunga za kimataifa ikiwemo kiswahili. Akiongea na vyanzo vyetu vya habari mwenyekiti wa umoja huo mheshimiwa Mfundo Peter Mfundo amewataka wanachama wa U T U  na Watanzania wote kwa Ujumla kuwa na subira kidogo kwani mtandao huo utaanza kupatikana kwa lugha ya kiswahili kwa ajili ya kuwapasha kila taarifa na kinachoendelea kutoka kwenye umoja wenu. 
  Mtandao huo  unapatikana katika www.ututz.com 
  au http//www.ututz.com 
  kwa mawasiliano zaidi  wasiliana na kamati.utu@googlemail.com  
  kamati ya UTU inawatakia kila la heri katika kurambaza kwenye mtandao wetu.

  0 0

   Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia katika mkutano wa hadhara katika Uwanja wa Stendi Kuu ya Zamani mjini Tabora, baada ya kumaliza ziara yake ya siku 11 katika mkoa huo, ya kuimarisha uhai wa chama, kukagua, kuhimiza na kusukuma miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa kufuata  Ilani ya CCM, kukagua maandalizi ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa pamoja na kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi
  Wakazi wa Mji wa Tabora Mjini  wakiwa wamejitokeza kwa wingi kwenye mkutano wa hadhara uliondaliwa na CCM leo jioni,ambapo Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana amehitimisha siku za ziara yake ya siku 11 mkoani humo,ya  ya kuimarisha uhai wa chama, kukagua, kuhimiza na kusukuma miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa kufuata  Ilani ya CCM, kukagua maandalizi ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa pamoja na kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.Kinana na msafara wake kwesho wataelekea mkoani Singida kwa ziara siku kadhaaa tena.
   Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akihutubia katika mkutano wa hadhara wa CCM, Mjini Tabora leo, ambapo aliwafananisha Wapinzani na Boko Haramu wa waasi wa Nigeria kwa kuwachonganisha wananchi kwa maneno,hali ambayo imeeleza kuwa kinaweza kusababisha vurugu nchini.
   Kinana akihudumiwa na Mama Lishe alipokwenda kula yeye na msafara wake kwa akina mama lishe eneo la Stendi Mpya Tabora mjini. Kushoto ni Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Tabora, Munde Tambwe,kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Tabora, Aden Rage ukiungana na Kinana kula msosi kwa mamaLishe mjini Tabora leo.
    Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye na Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Fatma Mwassa wakipata mlo kwa Mama Lishe mjini Tabora leo.
  Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiapata mlo wa mchana kwa Mama ntilie katika stendi mpya ya mabasi mjini Tabora,Kushoto ni Mbunge wa jimbo la Tabora Mjini ,Mh Aden Rage,katikati ni  Mbunge wa viti maalum CCM mkoani Tabora,Mh.Munde Tambwe wakishiriki pamoja na naye katika mlo huo sambamba na vijana wa mjini Tabora.
   Baadhi ya Wabunge mbalimbali walioshiriki kwenye mkutano huo wa Hadhara uliofanyika mjini Tabora,ikiwa ni siku ya mwisho ya kuhitimisha ziara ya siku 11 ya katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana mkoani humo. 

  0 0

  Wakazi wa eneo la Makunguru jijini Mbeya wakiwa wamesimama nje nyumba iliopo kwenye eneo hilo ambayo imepatwa na dhahma ya kuungua moto na kuteketea kwa mali zote zilizokuwemo ndani ya nyumba hiyo, kutokana na kinachosadikiwa kuwa ni hitilafu ya umeme. Bado haijadhibitika mpaka sasa kama kuna mtu yeyote aliedhurika kwenye tukio hilo lililotokea mchana wa leo jijini humo.
  Sehemu ya mali zilizokuwemo kwenye nyumba hiyo zikiwa zimeteketea zote kwa moto huo.
  Majirani wakichungulia  kupitia dirishani kuona namna moto ulivyoteketeza mali zilizomo kwenye nyumba hiyo.
  Wengine walikuwa wakihadhithiana  tukio hilo.


  0 0
 • 05/18/14--14:24: Ankal akiwa out na familia
 • "...Upatapo nafasi, japo mara moja kwa mwezi,  usikose kuitoa familia out", anasema Ankal akiwa na familia ufukweni Kunduchi.

older | 1 | .... | 454 | 455 | (Page 456) | 457 | 458 | .... | 3270 | newer