Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110173 articles
Browse latest View live

KAMPUNI YA PUMA ENERGY TANZANIA YAZINDUA VILAINISHI VYA CASTROL NA KITUO CHA MAFUTA CHA OYSTERBAY, DAR

$
0
0
Meneja wa Usalama wakati wa Kazi wa Kampuni ya PUMA Energy Tanzania, Jonathan Mmari akizungumza machache.
Walioko mbele kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya kampuni ya PUMA Energy Tanzania, Dkt. Ben Moshi na  Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya PUMA Energy Tanzania, Bw. Phillipe Corsaletti wakiwa na wageni waalikwa wakati wa uzinduzi wa Vilainishi vya Castrol vilivyoendana na uzinduzi wa kituo kipya cha Mafuta kilichopo Oysterbay jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya PUMA Energy Tanzania, Bw. Phillipe Corsaletti akionyesha picha ya sanamu itakayotumika kutambulisha vilainishi vya Castrol wakati wa uzinduzi wa Vilainishi vya Castrol vilivyoendana na uzinduzi wa kituo kipya cha Mafuta kilichopo Oysterbay jijini Dar es Salaam. Pembeni yake ni Mshereheshaji Shebe Machumani.
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya PUMA Energy Tanzania, Bw. Phillipe Corsaletti na Mshereheshaji Shebe Machumani wakionyesha vilainishi vya Castrol. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

TAMASHA LA ZIFF June 14 to June 22, 2014

$
0
0
Festival Program 2014

Festival Program 2014

TIMES and VENUES for SCREENINGS    
BONGO MOVIES SELECTION

BONGO MOVIES SELECTION

  Mimi na Mungu wangu: Dir. Iddy Bigilwa Fan's Death: Dir.Vincent Kigosi Hard Price: Dir.Vincent Kigosi Twisted: Dir.Vincent Kigosi Foolish Age: Dir. Chiddy Classic Dala dala: Dir.Suleiman Barafu Money Talk: Dir. Haji Adam Witch Doctor: Dir. Leah R. Mwendamseke Bad Luck: Dir.Adam Kuambiana Vanessa in Dilemma: Dir.Saguda George Kitendawili: Dir. Single Mtambalike Zero (Short Film) Dir. Adam Juma Lost Souls: …
Storytelling Workshops at ZIFF 2014

Storytelling Workshops at ZIFF 2014

Storytelling is a very creative endeavour. From childhood we find fun in playing and in that way develop ways in telling stories. As we grow we learn even to tell lies and those are also stories we learn to develop. When we tell stories in film we however have a different focus- we focus on the audience, the timespan …

BALOZI MTEULE WA TANZANIA NCHINI SWEDEN DORAH MSECHU AMUAGA WAZIRI MKUU

$
0
0
 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na Balozi  Mteule wa Tanzania nchini Sweden, Dora Msechu kabla ya mazungumzo yao,ofisini kiwa Waziri Mkuu  mjini Dodoma,  May 16, 2014. Balozi huyo mteule alikwenda kuaga. 
Waziri Mkuu Mkizengo Pinda  akizungumza na Balozi Mteule wa Tanzania nchini Sweden, Dora Msechu, ofisini kwake mjini Dodoma May 16, 2014. Balozi huyo Mteule alikwenda kuaga.

PLEASE HELP ME

$
0
0
With salams and jambo from IZAAS

My name is Rosi. I am 13 years old. When i was only 4 years old, something started growing on my left shoulder blade. I could not go to school as it was getting heaver. Please see my photos below.
Prepared by Mubaarak Abdullah.

Send off ya Safia Jumanne Mkakile

KATIBU MKUU WA CCM,NDUGU KINANA AWASILI WILAYA YA KALIUA,AKAGUA MIRADI YA MAENDELEO

$
0
0
 Katibu MKuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM,Wilaya ya Kaliua,katika ukumbi wa Millenium mkoani Tabora mara baada ya kupokea taarifa mbalimbali za maendeleo ya miradi na hali ya kisiasa wilayani Kaliua. Kinana yupo mkoani Tabora kwa ziara ya kuimarisha uhai wa chama, kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya CCM, kukagua maandalizi ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.
 Baadhi ya Wananchi wa kijiji cha Usindi  wakishuhudia Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akikagua mradi wa ujenzi wa jengo la Zahanati ambayo tayari imwekwisha kamilika,isipokuwa inasubiri kibali kutoka Wizara ya Afya na kukamilika nyumba ya mganga.Kinana ameambatana na Katibu wa NEC Itikadi,Siasa na Uenenezi Nape Nnauye,ambapo walipokelewa na Mbunge wa jimbo la Urambo Magharibi,Mh.Prof Juma Kapuya 
Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akipata taarifa fupi juu ya mradi wa ujenzi wa jengo la nyumba ya Mganga wilayani Kaliua katika kijiji cha Usindi,Kata ya Ushokora,Katika ziara hiyo ya siku 11,Kinana ameambatana na Katibu wa NEC Itikadi,Siasa na Uenenezi Nape Nnauye,ambapo walipokelewa na Mbunge wa jimbo la Urambo Magharibi,Mh.Prof Juma Kapuya .
  Katibu Mkuu wa CCM,dugu Kinana  akilakiwa na Mbunge wa jimbo la Urambo Magharibi,Mh.Prof Juma Kapuya,mara baada ya kuwasili wilayani Kaliua,katika kijiji cha Usindi kata ya Ushokora akiwa ameambatana na  Katibu wa NEC Itikadi,Siasa na Uenenezi Nape Nnauye (hayupo pichani). mkoani Tabora.
Mbunge jimbo la Urambo Mashariki,Mh.Samwel Sitta akisalimiana na Mbunge wa jimbo la Urambo Magharibi Prof.Juma Kapuya mapema leo kwenye wilaya ya Kaliua,mara baada uusindikiza msafara wa Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana aliyekuwa Wilayani Urambo Mashariki kwa ziara ya siku 11 ndani ya mkoa wa Tabora.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akipokelewa katika kijiji cha Usindi,Kata ya Ushokora wilayani Kaliua mkoani Tabora mapema leo asubuhi,akiwa ameambatana na Katibu wa NEC Itikadi,Siasa na Uenenezi Nape Nnauye na kupokelewa na Mbunge wa jimbo la Urambo Magharibi,Mh.Prof Juma Kapuya.

PICHA NI MICHUZIJR-KALIUA TABORA
PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

Diamond atamba kutwaa tuzo MTV

$
0
0
 Msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini Naseeb Abdul ‘Diamond’akiongea na waandishi wa habari kabla ya kuanza show hiyo,(kushoto), ni wasanii wa kundi la Sauti Sol.
 Picha ya pamoja.
 Watangazaji wa MTV Base Vanessa Mdee (kushoto),  na Nomuzi Mabe (kulia), wakiwaelezea mashabiki wa muziki kuhusina na show  hizo.
 Kundi la Mi Casa likitoa burudani.
 Diamond akitoa burudani.
  Mashabiki mbalimbali waliofurika katika ukumbi huo wakifuatilia show.
Mashabiki mbalimbali waliofurika katika ukumbi huo wakifuatilia show.

=======  =====  ======
MSANII nyota wa muziki wa kizai kipya nchini Naseeb Abdul ‘Diamond’ ametamba kufanya vizuri katika tuzo za MTV Africa ‘Mama’ zinazotarajiwa kufanyika Juni 7 mwaka huu nchini Afrika Kusini.

Diamond ameingia katika tuzo hizo kwenye vipengele viwili ambavyo ni msanii bora wa Afrika pamoja na msanii mwenye nyimbo bora ya kushirikisha.

Wimbo ambao umembeba kwa kiasi kikubwa msanii huyo ni wa Number One aliomshirikisha Davido wa Nigeria ambapo amewaomba mashabiki wake kumpigia kura kwa wingi.

Akizungumza katika hafla ilioandaliwa na kituo cha runinga cha MTV Base kama sehemu ya kusherekea tuzo za MTV Africa mwaka huu iliyofanyika Mei 16,2014  kwenye Ukumbi wa Billcanas,jijini Dar es Salaam  Diamond alisema kuwa anafanya muziki wa Afrika na ndio maana amepata mafanikio makubwa. wasanii waliotumbuiza ni pamoja na Sauti Solo,Mi Casa Msic

Alisema kuwa wasanii wanatakiwa kujituma zaidi ili kuhakikisaha wanafikia malengo zaidi.

“Ninafanya muziki wenye ladha ya Afrika na hivyo ninatarajia kufanya vizuri zaidi katika tuzo za MTV nawaomba Watanzania wazidi kunipigia kura ili niweze kuibuka kinara, wasanii wanatakiwa kufanya juhudi za ziada kwa kutoa kazi nzuri ili kuhakikisha wanafikia malengo,” alisema

NAFASI ZA KAZI YA UALIMU BAGAMOYO

$
0
0


Shule ya sekondari ya wasichana ya Premier iliyoko Kiromo Bagamoyo inapenda kuwatangazia nafasi za kazi ya ualimu kwa masomo yafuatayo

ENGLISH
SWAHILI
BOOKKEEPING
COMMERCE

Fika shuleni Kiromo kwa kuleta maombi yako siku ya mahojiano ni tarehe 22 na 23 May 2014 au kwa maelezo zaidi piga simu namba 0715836237

CHUO KIKUU CHA IRINGA WAZINDUA TAWI LA WANAFUNZI WANAOSOMA KISWAHILI AFRIKA MASHARIKI, WATAKA KATIBA MPYA KISWAHILI KIPEWE NAFASI

$
0
0
Mlezi wa chama  cha Chawakama na mwalimu wa kiswahili chuo kikuu cha Iringa Tulla Tweve  akitambulisha  wageni
Mmoja kati ya  viongozi akieleza malengo ya Chawakama
Mwalimu Chalamila akieleza  maana ya lugha ya kiswahili
Mwalimu wa kiswahili  chuo cha Iringa ambae ni msanii wa wimbo wa Mufindi yetu  akiburudisha
Wanachama  wakicheza  na msanii  huyo.
Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

MTU MMOJA ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA DODOMA KWA KUSABABISHA AJALI NA KIFO

$
0
0
Na Sylvester Onesmo 
wa Jeshi la Polisi Dodoma. 
 Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Jackson s/o Venance, umri miaka 33, kabila Mhaya, mfanyakazi wa NSSF Bukoba aliyekuwa akitembea kwa miguu pembeni mwa barabara ya Nyerere maeneo ya TRA Dodoma katika Manispaa na Mkoa wa Dodoma amefariki dunia alipokuwa akitibiwa katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma baada ya kugongwa na gari lenye namba za usajili T.399 CWG aina ya NISSAN iliyokuwa ikiendeshwa na Dotto d/o Onesmo, umri miaka 25, kabila msukuma, mwanafunzi wa Chuo cha Mipango Dodoma. 
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi David Misime – SACP amesema kabla ya kifo chake, Marehemu alifika Dodoma kwa ajijli ya kuchukua cheti chake katika Chuo cha Biashara Dodoma (CBE). 
 Kamanda Misime amesema uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa chanzo cha ajiali hiyo ni uzembe wa dereva wa gari kutokuwa mwangalifu. 
Uchunguzi zaidi wa ajali hiyo unaendelea na dereva atafikishwa mahakamani muda wowote kuanzia jumatatu mara baada ya taratibu kukamilika. 
 Aidha Kamanda Misime ametoa wito kwa madereva wa Magari na Pikipiki (Bodaboda) kuwa wawe na udereva wenye tahadhari ambao utaweza kupunguza ajali zisizo za lazima. 
Pia amewataka madereva hao wakumbuke kuwa wanapoendesha maeneo ya makazi na mikusanyiko ya watu wazingatie mwendo wao usizidi na uwe chini ya speed 50 zilizotamkwa kisheria. 
 Alisisitiza kuwa atakaye kiuka maelekezo hayo ya kisheria atachukuliwa hatua kali za kisheria.

ULIMWENGU, SAMATA WAJIUNGA STARS

$
0
0

Wachezaji Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu wametua Dar es Salaam leo (Mei 17 mwaka huu) mchana, na kujiunga moja kwa moja kwenye kambi ya Taifa Stars kwa ajili ya michuano ya Afrika dhidi ya Zimbabwe (Mighty Warriors).

Mechi hiyo ya kwanza ya raundi ya kwanza ya michuano hiyo itafanyika kesho (Mei 18 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Washambuliaji hao wa Taifa Stars wamewasili saa 7.25 mchana kwa ndege ya Ethiopian Airlines wakitokea Khartoum, Sudan ambapo jana (Mei 16 mwaka huu) timu yao ya TP Mazembe ilicheza mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Hilal ya huko.

Kocha wa Taifa Stars, Mart Nooij amesema kikosi chake kipo tayari kwa ajili ya mechi hiyo, kwani kimepata mechi za kirafiki na mazoezi ya kutosha kwenye kambi iliyoanzia Tukuyu mkoani Mbeya ambapo kulikuwa na utulivu mkubwa.

Naye Kocha Msaidizi wa Zimbabwe, Kalisto Pasuwa amesema hawaifahamu vizuri Taifa Stars lakini wamekuja kwenye mechi hiyo itakayoanza saa 10 jioni kwa ajili ya kushinda, na kuwataka washabiki wajitokeze kwa wingi kuona kiwango cha timu yake.

Milango kwa ajili ya mechi hiyo itakayochezeshwa na waamuzi kutoka Ghana wakiongozwa na Joseph Odartei Lamptey itakuwa wazi kuanzia saa 6 kamili mchana, na tiketi zitapatikana katika magari maalumu uwanjani hapo.

Viingilio katika mechi hiyo ni sh. 5,000 kwa viti vya rangi ya chungwa, kijani na bluu, sh. 10,000 kwa VIP C na B, na sh. 20,000 kwa VIP A.

BONIFACE WAMBURA
OFISA HABARI NA MAWASILIANO

SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

JK AMFARIJI JAJI WARIOBA KWA KUFIWA NA MKWEWE

RAIS KIKWETE AMFARIJI JAJI WARIOBA KWA KUFIWA NA MKWE WAKE

$
0
0
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka saini katika kitabu cha kumbukumbu alipokwenda kuhani msiba wa mama mkwe  wa Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba (aliyesimama pembeni) ,Marehemu Hedwig Laurent Ojjik,    Oysterbay jijini Dar es salaam leo Mei 17, 2014.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa mama mkwe  wa Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba,Marehemu Hedwig Laurent Ojjik, Oysterbay jijini Dar es salaam leo Mei 17, 2014
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifariji wanafamilia baada ya kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa mama mkwe  wa Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba, Marehemu Hedwig Laurent Ojjik, Oysterbay jijini Dar es salaam leo Mei 17, 2014
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakiwa na Jaji Joseph Warioba na mkewe Mama Evelyne Warioba walipokwenda kuhani na kutoa heshima za mwisho katika msiba wa mama mkwe  wa Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba, Marehemu Hedwig Laurent Ojjik,   Oysterbay jijini Dar es salaam leo Mei 17, 2014
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakimfariji Mama Evelyne Warioba  alipokwenda hunai msiba wa mama yake mzazi 
Marehemu Hedwig Laurent Ojjik  Oysterbay jijini Dar es salaam leo Mei 17, 2014

MAZISHI YA PRIVATE BRIAN SALVA RWEYEMAMU

$
0
0
Mkurugenzi wa Mawasiliano Ofisi ya Rais Ikulu Bw. Salva Rweyemamu na mkewe Mama Isabella Salva Rweyemamu wakijiandaa kuweka shada la maua wakati wa mazishi ya mtoto wao Private Brian Salva Rweyemamu yaliyofanyika jioni ya leo kwenye makaburi ya Kinondoni jijini Dar es salaam.
Wazazi wakiweka shada lao la maua
Majonzi makubwa
Dada wa marehemu na shada lao maalumu kwa kaka yao
Dada wakiweka shada lao
Rais Kikwete na Mama Salma Kikwete wakiweka mashada yao
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe Bernard Membe akiweka shada
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akiweka shada.

BURIANI ADAM KUAMBIANA

$
0
0
Marehemu Adam Kuambiana enzi za uhai wake.


MWIGIZAJI na Muongozaji filamu maarufu Bongo, Adam Kuambiana amefariki dunia wakati akipelekwa hospitali ya Mama Ngoma iliyopo Mwenge jijini Dar es Salaam kwa matibabu alfajiri ya leo. 

Habari zinasema Marehemu alianguka chooni akiwa location katika hoteli ya Silver Rado iliyopo Sinza kwa Remmy, Dar es salaam. 

Kabla ya mauti kumfika, Adam alikuwa akilalamika kuwa anasumbuliwa na tumbo.

Globu ya Jamii inaungana na familia ya marehemu, ndugu, jamaa, marafiki na wadau wote wa Bongo Movie katika kuomboleza kifo cha nyota huyu wa filamu.

Mola aiweke roho ya marehemu

mahala pema Peponi

AMINA

ARSENALI MABINGWA WA FA

$
0
0
 Kocha wa Arsenali Arsene Wenger akimbusu mchezaji wake baada ya kuulopu kwa kuwashinda Hull City bao 3-2 kwa shida na kunyakua kombe la Meeee oh.... samahani.... kombe la FA baada ya miaka kenda.
Kocha Wenger akifurahia kombe la Meeeeeee....leo

introducing Ommy Dimpoz's "Ndagushima" Official Video

HOTUBA YA WAZIRI WA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA NA WATOTO MHESHIMIWA SOPHIA M. SIMBA (MB.), AKIWASILISHA BUNGENI MAKADIRIO YA MATUMIZI YA FEDHA KWA MWAKA 2014/15

$
0
0
WAZIRI  WA  MAENDELEO  YA
JAMII, JINSIA NA WATOTO MHESHIMIWA SOPHIA M. SIMBA (MB.)

MAADHIMISHO YA SIKU YA MAKUMBUSHO DUNIANI YAENDELEA KUFANA KATIKA MAKUMBUSHO NA NYUMBA YA UDAMADUNI JIJINI DAR

$
0
0
Kundi kubwa la wanafunzi kutoka shule mbali mbali wakisherekea Maadhimisho ya Siku ya Makumbusho Duniani yanayo adhimishwa Kitaifa katika Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dar es Salaam.
Kundi kubwa la Wanafunzi walio udhuria maadhimisho yaSiku ya Makumbusho Duniani katika Viwanja vya Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dar es Salaama wakimsikiliza Mwendesha kipindi cha watoto, Bw Chance Ezekiel (Uncle Bilinge) hayupo Pichani.
Pichani ni Chance Ezekiel (Uncle Bilinge) na safu nzima ya uongozaji wageni wakiwa wanawanafunzi wa shule mbali mbali (hawapo pichani) katika kipindi cha Chemsha bongo na Burudani ambayo ni sehemu ya Maadhimisho ya Siku ya Makumbusho Duniani.

MKUU WA MKOA WA RUKWA AKAGUA UJENZI WA MIRADI YA MAJI KATIKA MANISPAA YA SUMBAWANGA, APIGA MARUFUKU UHARIBIFU WA VYANZO VYA MAJI

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya (Mb) katikati akitoa maelekezo kwa watendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga na Mkandarasi anaejenga mradi wa maji wa kijiji cha Malonje ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa ahadi za Serikali za kufikisha huduma muhimu kwa wananchi. Mradi huo wa maji ambao unaelekea kukamilika umefadhiliwa na benki ya dunia kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania kwa gharama ya Tsh. Milioni 279. Katika maagizo aliyoyatoa ni pamoja na kupiga marufuku shughuli zote za kilimo na ufugaji karibu na vyanzo vya maji kulinda vyanzo hivyo.
Sehemu ya banio la kukingia maji kwenye chanzo cha maji (chemchem) katika kijiji cha Malonje ambalo ni sehemu ya mradi huo, baadhi ya wananchi wameonekana kuendesha shughuli zao za kilimo na ufugaji karibu na chanzo hicho ambapo wamepigwa marufuku kuendeleza shughuli hizo za uharibifu wa chanzo hicho cha maji. 
Bwana Danford Anania Kaimu Injinia wa Maji Manispaa ya Sumbawanga wa pili kulia akitoa maelezo ya tenki la maji lenye ujazo wa lita 45, 000 kwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya. Tenki hilo limejengewa pampu itakayotumia nguvu ya nishati ya jua kusukuma maji katika vijiji vya jirani vya Malonje ikiwa ni sehemu ya mradi wa maji wa Kijiji cha Malonje katika Manispaa ya Sumbawanga.
Banio la kukinga maji kwenye chanzo (chemchem) ikiwa ni sehemu ya ujenzi wa mradi wa Maji katika kijiji cha Mlanda Manispaa ya Sumbawanga ambapo mradi huu utakaotumia zaidi ya Tsh. Milioni 394 unajengwa na mkandarasi Safari General Traders na unategemewa kuhudumia wanachi wa kijiji cha Mlanda. Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya alitembelea jumla ya miradi mitano ya Maji katika Manispaa ya Sumbawanga ambayo ni Malonje, Mlanda, Pito, Chilenganya na Kanondo. Aliwataka wakandarasi waharakishe kumaliza kazi walizobakisha ili wanancni waweze kupata huduma hiyo muhimu ya maji. Aidha alikataa kukagua moja ya mradi kwa vile mkandarasi husika amekua akitoa visingizio mbalimbali vya kutokumaliza kazi. 
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya akizungumza na wananchi wa kijiji cha Malonje muda mfupi baada ya kukagua mradi wa maji na Zahanati katika kijiji hicho, aliwataka wananchi hao kuwaendeleza watoto wao kielimu na kushirikiana na uongozi wa kijiji katika kuhifadhi mazingira na kulinda vyanzo vya maji. Kulia ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Sumbawannga Ndugu William Shimwela.(Na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa @rukwareview.blogspot.com)
Viewing all 110173 articles
Browse latest View live




Latest Images