Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110078 articles
Browse latest View live

BALOZI LIBERATA MULAMULA AMKARIBISHA RAIS MSTAAFU BENJAMIN MKAPA NA MKEWE CHAKULA CHA JIONI NYUMBANI KWAKE

$
0
0
 Picha ya pamoja ya Balozi Liberata Mulamula na Mhe. Benjamin Mkapa na mkewe Mama Anna Mkapa wakiwa pamoja na marafiki zao wa siku nyingi Bi.Toyin Rose(kushoto) na mumewe. 
 Picha ya pamoja Mhe. Benjamin Mkapa na mkewe Mama Anna Mkapa pamoja na mwenyeji wao Mhe. Libarata Mulamula.
Picha ya pamoja na Maafisa Ubalozi


BRN yapongezwa kwa kuwasaidia wakulima wadogo

$
0
0
Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN) umepongezwa kwa kuweka katika moja ya sekta zake za kipaumbele, miradi ya kilimo inayolenga kuwasaidia wakulima wadogo nchini.

Kauli hiyo imetolewa Dar es Salaam jana na Mwakilishi wa Rais wa Mpango wa UN wa Kusaidia Uwekezaji katika Kilimo (IFAD), Yaya Olanirani, wakati ujumbe wa taasisi hiyo ulipokutana na watendaji mbalimbali wa Serikali. IFAD ni asasi ya Umoja wa Mataifa inayosaidia uwekezaji katika kilimo.

"Tumefurahishwa na miradi ya BRN inayolenga katika kuwasaidia wakulima wadogo si tu katika jitihada za kuwaondolea umaskini bali pia kujiongezea kipato na kuwawezesha kupata utajiri.

"IFAD iko katika kufanya tathmini ya maeneo gani zaidi ya kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika siku zijazo lakini kwa sasa tutaendelea kusaidia juhudi za uwekezaji katika miundombinu ya kilimo na hasa eneo la kuwainua wakulima wadogo," alisema.

Kwa upande wake, Mtendaji Mkuu wa Ofisi ya Rais-Usimamizi wa Utekelezaji wa Miradi (PDB) inayoratibu Mpango wa BRN hapa nchini, Bw. Omari Issa aliueleza ujumbe huo kuwa kupitia BRN Serikali ya Tanzania imedhamiria chini ya mfumo maalum wa usimamizi kuondoa changamoto za wakulima wadogo.

Akiwasilisha mada katika kikao hicho Mkurugenzi wa Sekta za Kilimo katika PDB, Bw. Henry Kinyuah alisema katika moja ya miradi ya mfano inayosimamiwa chini ya BRN ni shamba jipya la miwa lililopo Bagamoyo.

"Mradi wa uzalishaji wa miwa Bagamoyo peke yake utazalisha tani 150,000 za sukari kwa mwaka, makapi yatatumika kuzalisha mafuta, utazalisha umeme megawati 32, utazalisha ajira za moja kwa moja 2,300 na pia utawawezesha wazalishaji wadogo wadogo kuzalisha kati ya tani 300-400 za sukari," alisema.

Jeshi la Polisi Mkoani Lindi lamsaka askari Mwenye tuhuma za kujihusisha na biashara haramu ya Meno ya Tembo

$
0
0
Jeshi la polisi mkoani Lindi linamtafuta askari wake mmoja mwenye namba F6508 Detective Constable JOSEPH YONA MASANJA mwenye Umri wa miaka 34 mzaliwa wa Wilaya ya ILEMELA Mkoani MWANZA Abae alikuwa akifanya kazi kituo cha polisi KILWA kwa tuhuma za kuhusika na wizi wa vipande 62 vya meno ya tembo vyenye uzito wa kilo 568 yaliyokuwepo kituoni hapo kama Vielelezo.

Hayo yamebainishwa na Kamanda wa polisi mkoa wa Lindi,Kamishna Msaidizi Renatha Mzinga alipokuwa Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari kufuatia jitihada mbalimbali za kumtafuta kutoleta Mafanikio.

 Mtuhumiwa Huyo ambae alikuwa mtunza Vielelezo katika kituo cha polisi Wilayani Kilwa toka mwaka 2004 ambaye kwa sasa amefukuzwa kazi kutokana na utoro kazini ,kabla ya kugundulika kwa wizi huo baada ya kuomba ruhusa ya kwenda kusoma Chuo Kikuu cha DSM ambako baada ya uchunguzi alibainika kuwa alibadili chuo na kwenda chuo kikuu cha SAUT -Mwanza ambako hata hivyo amebainika ametoweka.

Kufuatia kutoweka kwake Jeshi la polisi mkoani LINDI limewaomba wananchi kutoa taarifa za mtuhumiwa huyo popote watakapomuona kwani ametumia nafasi yake vibaya na kuhujumu rasilimali za taifa kwa manufaa yake binafsi.

'ndg zangu wanahabari naomba mtusaidie maana Huyu jamaa Mara ya mwisho alikuwa Chuo cha SAUT cha Mwanza tulipomfuatialia akawa ametoweka ghafla na suala tulilibaini baada ya vielelezo hivyo kukataliwa mahakamani na maafisa wanyamapori kuwa si vyenyewe na vina upungufu mkubwa ikiwemo kupunguzwa ukubwa wake.

Katika tukio lingine Kamanda Mzinga alieleza kuwa polisi wamemkamata SAID ALLY MASOUD katika kisiwa cha POMBWE wilaya ya KILWA akiwa amejeruhiwa vibaya na bomu alipokuwa akivua samaki kinyume cha sheria kwa kutumia baruti.

Mtuhumiwa huyo amelazwa katika hospitali ya KILWA ya KINYONGA na hali yake imeelezwa kuwa ni mabaya kiasi cha kushindwa kujieleza baada ya baruti kumfyatukia yeye badala ya samaki.

Waendesha Pikipiki Wilayani Temeke wakutana

$
0
0
Umoja wa Waendesha Pikipiki wilayani Temeke ( UWAPITE) umekutana na kufanya mkutano wao mkuu leo katika ukumbi wa CCM kata 14 Temeke. Mgeni rasmi alikuwa ni Mjumbe wa NEC Ndg. Phares Magesa, ambaye aliwataka wanaboda boda hao kutii sheria na taratibu zote kama walivyotakiwa na Mamlaka husika, pia Ndg. Magesa aliwaasa wanabodaboda hao kuimarisha Umoja wao ili waweze kufanikiwa kufikia malengo yao. Ndg. Magesa aliahidi kufikisha katika Mamlaka husika mambo mbalimbali ambayo wanabodaboda hao waliomba ikiwa ni pamoja na suala la utaratibu wa kuingia mjini na aliwaomba wawe na subira wakati mambo hayo yanashugulikiwa. Mkutano huo pia ulihutubiwa na viongozi wengine toka taasisi mbalimbali akiwemo Afisa Usafirishaji wa Mkoa, Kamanda wa Polisi, Sumatra, Bima (NIC) na wawekezaji toka kampuni ya Yamaha ambao wanatoa mikopo nafuu kwa wanachama wa Chama hicho.
Wanachama wa Chama Cha Waendesha Pikipiki Temeke wakisiliza hutuba mbalimbali zilizotolewa.
Mgeni rasmi Ndg.Phares Magesa akitoa nasaha.

TUTAAINISHA FURSA ZA KUIVUSHA TANZANIA KIMATAIFA

$
0
0
Na Saidi Mkabakuli

Serikali imeweka wazi mkakati wa kuainisha fursa za kipaumbele zitakazoiwezesha kuivusha nchi kikanda na kimataifa kwa kusimamia na kufuatilia utekelezaji wa miradi ya maendeleo kama inavyobainishwa na Mpango wa Kwanza wa Maendeleo wa Miaka Miaka Mitano (FYDP I) unaosimamiwa na  Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango.

Mkakati huo umewekwa wazi na Naibu Katibu Mtendaji mpya wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, anayeshughulikia Biashara za Kimataifa na Mahusianao ya Kiuchumi Bw. Paul Sangawe mara baada ya kula kiapo cha kuitumika nafasi hiyo. 

Bw. Sangawe amesema kuwa lengo la Serikali ni kuhakikisha kuongeza mauzo ya bidhaa na huduma pamoja na kufaidika na misaada kutoka nchi marafiki na mashirika ya kimataifa.

“Kwa mujibu wa Mpango Wa Maendeleo Wa Taifa  Mwaka 2012/13 thamani ya mauzo ya bidhaa na huduma nje ilikuwa dola za Kimarekani 6,796.3 milioni mwaka 2011, ikilinganishwa na dola 5,805.0 milioni mwaka 2010 sawa na ongezeko la asilimia 17.1. hivyo mkakati wetu ni kuongeza hali hii,” alisema Bw. Sangawe.

Kwa mujibu wa Mpango huo thamani ya bidhaa za kukuza mitaji zilizoagizwa toka nje iliongezeka hadi dola za Kimarekani 3,560.5 milioni kutoka dola 2,715.2 milioni mwaka 2010, sawa na ongezeko la asilimia 31.1. Ongezeko hili lilichangiwa zaidi na kuongezeka kwa uagizaji wa mitambo hasa ile ya viwandani. 

Aidha, thamani ya uagizaji wa bidhaa za kati iliongezeka hadi dola za Kimarekani 4,139.0 milioni mwaka 2011, kutoka dola 2,741.2 milioni mwaka 2010, sawa na ongezeko la asilimia 51.0. Uagizaji wa mafuta kwa wingi ulitokana na matatizo yaliyojitokeza ya kutozalishwa kwa kiasi kinachohitajika cha umeme unaotokana na maji, hivyo kupelekea mitambo mingi ya mashine kuendeshwa kwa kutumia umeme unaozalishwa na mafuta. 

Vilevile, thamani ya mafuta yaliyoagizwa katika mwaka 2011 ilikuwa dola milioni 3,228.7 ikilinganishwa na dola milioni 2,024.2 mwaka 2010. Uagizaji wa bidhaa za matumizi ya kawaida uliongezeka hadi dola 2,128.0 milioni kutoka dola 1,709.2 milioni mwaka 2010, sawa na ongezeko la asilimia 24.5.

Bw. Sangawe ameongeza kuwa Serikali inajikita katika kutambua masoko kwa bidhaa za Tanzania na vyanzo vipya vya uwekezaji katika uchumi wa Dunia na Kikanda ili kuwezesha sekta binafsi kuchangia kufanikisha utekelezaji wa miradi hiyo ya maendeleo ili kuwezesha nchi kuchanmkia fursa za masoko ya kimataifa ikiwemo AGOA na nchi za jumuiya za Ulaya. 

“Kipaumbele itakuwa ni kutumia rasilimali chache kuchochea uwekezaji wa sekta binafsi pamoja na kuendelea kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji ili kuvutia uwekezaji katika maeneo ya kipaumbele na ya matokeo makubwa,” aliongeza Bw. Sangawe.

Serikali imeaandaa Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano ukiwa na lengo la kuwa na mfumo madhubuti wa kutekeleza Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025. Lengo la Dira ni  kuibadili Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa kati ifikapo 2025.
Naibu Katibu Mtendaji (Biashara za Kimataifa na Mahusianao ya Kiuchumi) mpya wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bw. Paul Sangawe (Kulia) akila kiapo cha utii na utumishi mbele ya Rais Dkt. Jakaya Kikwete (Kushoto).

Vodacom kukabidhi zawadi kwa Bingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara Mei 27

$
0
0
Meneja uhusiano wa Nje wa Vodacom Tanzania, Salum Mwalim, akizungumza na waandishi wa habari (Hawapo pichani) wakati wa kutangaza siku ya kukabidhi zawadi za washindi wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Pamoja nae katika picha, wa kwanza kutoka kushoto ni Ofisa Matukio na Udhamini wa Vodacom Tanzania, Ibrahim Kaude, Ofisa Habari wa TFF, Boniface Wambura.

Bingwa wa Ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara 2013/2014 timu ya Azam FC itakabidhiwa kitita chake cha zawadi Sh 75 Milioni Mei 27 mwaka huu kutoka kwa mdhamini wa ligi hiyo kampuni ya huduma za mawasiliano ya simu za mkononi nchini ya Vodacom.

Aidha, pamoja na Azam fc, Vodacom itakabidhi pia zawadi za fedha kwa Yanga, Mbeya City na Simba waliomaliza msimu katika nafasi ya pili hadi ya nne.

Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Salum Mwalim amesema tayari maandalizi ya tukio hilo litakalohusisha chakula cha jioni yameshakamilisha kwa kiasi kikubwa na kinachoendela sasa ni maandalizi ya mwisho ikiwemo kusambaza mialiko.

Mwalim amesema tukio hilo hilo litafanyika kwenye ukumbi wa JB Belmonte uliopo kwenye jengo la Golden Jubilee jijini Dar es salaam na kuwataka washabiki wa soka nchini kuaka mkao w akuhushudia tukio kubwa na la aina yake.

DKT. SHEIN AKUTANA NA BW.RAYMOND KATIBU MKUU WA KIMAIFA WA USAFIRI WA ANGA

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein akisalimiana na Katibu Mkuu Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga Bw.Raymond Banjamin,(kulia) alipofika Ikulu Mjini Unguja leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein (kulia) akizungumza na Katibu Mkuu Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga Bw.Raymond Banjamin,alipofika Ikulu Mjini Unguja leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein (kulia) akifuatana na Katibu Mkuu Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga Bw.Raymond Banjamin,baada ya mazungumzo yao alipofika Ikulu Mjini Unguja leo.Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA VIETNAM ZIARANI NCHINI

$
0
0
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Dkt. Mahadhi Juma Maalim (Mb.) akizungumza na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Vietnam, Mhe. Nguyen Phuong Nga mara baada ya kumpokea katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere. Mhe. Nguyen yupo nchini kwa ziara ya kikazi ya siku tano.
Mhe. Dkt. Maalim na Mhe. Nguyen wakizungumza huku Balozi wa Vietnam nchini, Mhe. Vo Thanh Nam (kushoto), Bw. Nathaniel Kaaya (kulia), Mkurugenzi Msaidizi katika Idara ya Asia na Australasia na Bw.Emmanuel Ruangisa, Afisa Mambo ya Nje  wakifuatilia mazungumzo hayo.

Mhe. Nguyen akimkabidhi zawadi Dkt. Maalim mara baada ya mazungumzo yao.

Rais Kikwete akutana na wajumbe wa IFAD

$
0
0
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na wajumbe wa Bodi ya utendasji ya mfuko wa Kimataifa wa maendeleo ya kilimo(IFAD) wakati walipomtembelea ikulu jijini Dar es Salaam leo.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Bodi ya Utendaji(Executive Board) ya mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo(IFAD) ikulu jijini Dar es Salaam leo.(picha na Freddy Maro).

Mem Bulletin 16th Edition

dhifa maalum iliyoandaliwa kwa ajili ya Ujumbe wa Bodi ya Utendaji ya IFAD ZANZIBAR

$
0
0
Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo { IFAD }umeombwa kuendelea kuunga mkono Sekta ya Kilimo Zanzibar katika njia ya kuwajengea uwezo wazalishaji wa Sekta hiyo mama ya uchumi kupitia mfumo wa Teknolojia ya kisasa. 
Ombi hilo limetolewa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi hapo Serena Hoteli Shangani Mjini Zanzibar wakati wa dhifa maalum iliyoandaliwa kwa ajili ya Ujumbe wa Bodi ya Utendaji ya Mfuko huo uliofanya ziara maalum kukagua miradi mbali mbali inayofadhiliwa na Taasisi hiyo ya Kimataifa. 
Balozi Seif alisema Sekta ya Kilimo Zanzibar bado inaendelea kukabiliwa na changa moto kadhaa ambazo zinaweza kupunguwa iwapo msukumo wa Mfuko wa IFADI utaongeza kasi ya kitaalamu katika kusaidia sekta ya Kilimo Nchini. 
Alielezea matumaini yake kwamba juhudi zinazochukuliwa na Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo zinaweza kusaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza umaskini, njaa na kuongeza mara dufu uzalishaji wa chakula. Balozi Seif alifahamisha kwamba Serikali kwa kushirikiana na Taasisi tofauti za ndani na nje ya Nchi imekusudia kuimarisha uzalishaji wa mazao ya chakula na matunda ili kuwapunguzia mzigo wananchi hasa wanaoishi sehemu za Vijiji. 
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amewapongeza wajumbe wa Bodi hiyo Tendaji ya Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo kwa uamuzi wao wa kutembelea miradi inayoifadhili hapa Tanzania kitendo ambacho kitaongeza upeo wa ushirikiano kati ya Uongozi huo na Serikali zote mbili. Mapema Mkuu wa Bodi hiyo yenye Makao Makuu yake Nchini Italy Dr.Yaya Olaniran alisema ujumbe huo ulipata fursa ya kuona hali halisi ya miradi mbali mbali inayofadhiliwa na mfuko huo pamoja na kukutana na wakulima ambao ndio wahusika wakuu wa miradi ya Mfuko huo. 
Dr. Yaya alisema Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo { IFAD } utaendelea kuunga mkono Serikali zote mbili Nchini Tanzania katika sekta ya Kilimo ikijikita zaidi katika kuwajengea uwezo wakulima pamoja na jumuiya za Kilimo ili zifikie hatua ya kujitegemea kiuzalishaji badala ya kusibiri misaada. 
“ Ushirikiano wetu uliopo kati ya IFAD pamoja na SMT NA SMZ ndio sababu ya msingi iliyochangia Mfuko huo kuchangia harakati za maendeleo ya wakulima katika maeneo mbali mbali Nchini Tanzania “. Alisema Dr. Yaya Olaniran. 
Naye Mkurugenzi wa Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo { IFAD } Kanda ya Mashariki na Kusini mwa Bara la Afrika Bwana Perin Saint Ange akitoa shukrani kwa niaba ya Ujumbe huo alisema Visiwa vya Zanzibar vina rasilmali nyingi ambazo iwapo zitajengewa miundo mbinu imara zinaweza kunyanyua maisha ya Wananchi pamoja na kuongeza pato la Taifa. 
Bwana Perin alizitolea mfano rasilmali zilizomo ndani ya Bahari ya Tanzania kwamba zinafursa ya kukomboa maisha ya wavuvi wengi waliomo pembezini mwa bahari hiyo ambapo wengi kati yao hujishughulisha na kazi hiyo wakitumia vifaa duni visivyohimili masafa ya bahari kuu. 
Dhifa hiyo fupi kwa Wajumbe wa Bodi Tendaji ya Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo { IFAD } ilijumuisha pia baadhi ya Maafisa na watendaji wa Wizara ya Kilimo na Mali Asili Zanzibar. Othman Khamis Ame Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar 16/5/2014.
 Katibu  Mkuu wa Mfuko wa Kimataifa  wa Maendeleo ya Kilimo { IFAD } Bwana Rasit Pertev akijipatia mlo kwenye dhifa Maalum walioandaliwa wajume wa Bondi ya Mfuko huo hapo Serna Hoteli Shangani.
 Mkuu  wa Programu ya Mfuko wa IFAD Tanzania Dr. Mwatima Abdulla Juma ,Mkurugenzi wa Mfuko huo Kanda ya Mashariki na Kusini mwa Afrika Bwana Perin Saint Ange, pamoja na wajumbe wengine wa bodi ya mfuko huo wakijipatia mlo kwenye dhifa hiyo.
  Mkuu wa Bodi Tendaji ya Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo { IFAD } yenye Makao Makuu yake Nchini Italy Dr.Yaya Olaniran akifafanua malengo ya mfuko mara baada ya dhifa maalum ya chakula cha usiku waliyoandaliwa kwenye Hoteli ya Serena Inn Shangani Mjini Zanzibar.Kulia ya Dr. Yaya ni  Mkurugenzi wa Mfuko huo Kanda ya Mashariki na Kusini mwa Afrika Bwana Perin Saint Ange na kushoto yake ni Katibu  Mkuu wa Mfuko huo wa            { IFAD } Bwana Rasit Pertev.
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na Ujumbe wa Bodi Tendaji ya Mfuko wa Kimataifa wa Kilimo { IFAD }  mara baada ya dhifa maalum waliyoandaliwa wageni hao hapo Serena Hoteli Shangani.
 Mkurugenzi wa Mfuko wa IFAD Kanda ya Mashariki na Kusini mwa Afrika Bwana Perin Saint Angeakitoa shukrani mara baada ya kumalizika kwa dhifa maalum iliyoandaliwa kwa ajili ya Ujumbe wake.
 Balozi Seif akiagana na baadhi ya wajumbe wa Bodi Tendaji ya Mfuko wa IFAD baada ya kukmilika kwa dhifa maalum hapo Hoteli Serena Inn Shangani Mjini Zanzibar. Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ

RATIBA YA MAZISHI YA PRIVATE BRIAN SALVA RWEYEMAMU, NA WASIFU WAKE

$
0
0
MAZISHI KESHO JUMAMOSI TAREHE 17.05.2014 

SHUGHULI ZOTE ZITAFANYIKA NYUMBANI KWA BW. SALVA RWEYEMAMU KINONDONI, MKABALA NA VIJANA HOSTEL NA MANGO GARDEN, JIJINI DAR ES SALAAM

SAA      1.00:  ASUBUHI KIFUNGUA KINYWA - NYUMBANI


SAA 4.00-5.00:  CHAKULA CHA MCHANA - NYUMBANI


SAA 5.00-6.00: KUAGA MWILI - NYUMBANI


SAA 6.00-7.00: MISA KATIKA KANISA KATOLIKI MWANANYAMALA


SAA  8.00 Mchana: SHUGHULI ZA MAZISHI MAKABURI YA KINONDONI
---------------------------------------------------------------
WASIFU WA PRIVATE  BRIAN SALVA RWEYEMAMU


Rwechungura Brian Salvatory Rweyemamu, aliyefariki dunia alfajiri ya juzi, Alhamisi, Mei 15, 2014 ni mtoto wa kwanza wa Salva Rweyemamu na Isabella Kafumba Rweyemamu. Alizaliwa Desemba 27, mwaka 1987, katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dar Es Salaam.

Alipata elimu ya awali katika Shule ya Awali ya Mama wa Kiganda, Kinondoni na Kwa Mama Kate eneo la Chang’ombe, Dar es Salaam kabla ya kuhamia Kenya ambako alianza darasa la kwanza katika Shule ya Msingi ya Top Hill na Lukenya. Hatimaye alihamia kwenye mji Mkuu wa Ubelgiji wa Brussels ambako aliendelea na elimu ya msingi mwaka 1996.



Brian alijiunga na shule ya Bweni ya Trinity Exeter nchini Uingereza ambako aliendelea na kumalizia elimu ya msingi. Ili kumrudisha katika mazingira ya Kitanzania, Bwana Brian alirudia tena darasa la saba katika Shule ya Msingi ya Julius Nyerere iliyoko Mbezi Beach, Kinondoni, Dar Es Salaam, mwaka 1998.



Alijiunga na Shule ya Sekondari ya St. Albans ya mjini Pretoria, Afrika Kusini, mwaka 1999, ambako alikaa miaka minne kabla ya kujiunga na Shule ya Sekondari ya Kaboja nje kidogo ya mji mkuu wa Uganda wa Kampala ambako alimaliza kidato cha sita mwaka 2005.



Alijiunga na Chuo Kikuu nchini Malaysia ambako alichukua masomo ya International Trade, masomo ambayo yalikuwa bado yanamdai credits za semester ya mwisho kabla ya kuaga dunia.



Alijiunga na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Kambi ya Mlale, Songea, 2010 na kumaliza kumaliza mafunzo yake mwaka 2011 na hatimaye alijiunga na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (TPDF) ambako alifanya na kumaliza mafunzo katika Kambi ya Mafinga mjini Iringa mwaka 06/12/2013 kabla ya kuajiriwa na JWTZ mwishoni mwa mwaka jana.



Aliomba na kupewa likizo yake ya kwanza ndani ya JWTZ wiki mbili zilizopita ambako alikaa nyumbani kwa siku chache kabla ya kushambuliwa na malaria kali wiki iliyopita. Alilazwa Jumamosi iliyopita tarehe 10/05/14 katika Hospitali Kuu ya Jeshi ya Lugalo akiwa na malaria na kupoteza fahamu.
Alianza kupata fahamu kwa mbali siku ya Jumanne usiku na kujaribu kuongea siku ya Jumatano. 

JK aongoza waombolezaji kumfariji Salva Rweyemamu na familia yake kwa msiba wa Private Brian

$
0
0
Waziri Mkuu Mstaafu Dkt Salim Ahmed Salim akisaini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Ofisi ya Rais Ikulu Bwana Salva Rweyemamu Kinondoni jijini Dar es Salaam kufuatia kifo cha mwanaye Private Brian Salva Rweyemamu kilichotokea jana katika hospitali ya jeshi Lugalo jijini baada ya kuugua kwa muda mfupi. 
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisaini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Ofisi ya Rais Ikulu Bwana Salva Rweyemamu Kinondoni jijini Dar es Salaam kufuatia kifo cha mwanaye Private Brian Salva Rweyemamu kilichotokea jana katika hospitali ya jeshi Lugalo jijini baada ya kuugua kwa muda mfupi. Marehemu Private Brian anatarajiwa kuzikwa kesho mchana(Jumamosi) katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akipa pole Bibi Isabela Salva Rweyemamu ambaye ni mama wa Marehemu Private Brian Salva Rweyemamu wakati alipokwenda kutoa pole nyumbani kwa marehemu Kinondoni jijini Dar es Salaam leo.
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho kikwete akiwafariji Mkurugenzi wa Mawasiliano Ofisi ya Rais Ikulu Bwana Salva Rweyemamu na Mkewe Isabela Salva Rweyemamu ambao ni wazazi wa Marehemu Private Brian Salva Rweyemamu nyumbani kwao Kinondoni jijini Dar es Salaam leo.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na kuifariji familia ya Marehemu Private Brian Salva Rweyemamu nyumbani kwao Kinondoni jijini Dar es Salaam leo Picha na Freddy Maro.
Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

JK aongoza Harambee ujenzi wa Kanisa la KKKT Bumbuli

$
0
0
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiteta jambo na Naibu waziri Mawasiliano Sayansi na Technolojia na mbunge wa Bumbuli January Makamba wakati wa harambee ya kuchangia ujenzi wa kanisa la Bumbuli Shughuli hiyo imefanyika katika Hotel ya Golden Tulip
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akifurahia wimbo wa wanabumbuli mara baada ya kuwasili katika ukumbi wa Hotel ya Golden Tulip kwa ajili ya harambee ya kuchangia ujenzi wa kanisa la Kilutheri la Bumbuli, Kushoto ni askofu mkuu wa KKKT DKt.Gerhas  Malasusa, Watatu Kulia ni Dkt.Steven Munga wa Lushoto na kulia ni mbunge wa Bumbuli ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na teknolojia Mh.January Makamba Katika harambee hiyo jZaidi ya Shilingi milioni mia tatu zilipatikana
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na watu walioshiriki katika harambee ya kuchangia ujenzi wa kanisa la KKKT Bumbuli jana iliyofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Golden Tulip jijini Dar es Salaam jana jioni.Walioketi mbele Wapili kushoto ni Mkuu wa Kanisa la KKKT Tanzania Askofu Dkt. Gerhaz Malasusa,Askofu wa Lushoto Steven Munga(Wanne kushoto) na Watano kushoto ni Mbunge wa Bumbuli ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Mh.January Makamba.Zaidi ya Shilingi milioni mia tatu zilikusanywa katika harambee hiyo ikiwa ni ahadi,vifaa vya ujenzi na fedha taslimu Picha na Freddy Maro

ngoma azipendazo ankal

$
0
0
The Temptations wanakupa "Papa Was A Rolling Stone"

KUMBUKUMBU

$
0
0
MAREHEMU AYOUB FELIX MLAY 

Ni mwaka mmoja umepita tangu uhai wako ulipotolewa bila sababu na bila kutuaga na kutangulia kwenye pumziko la milele mbinguni. Unakumbukwa na Wazazi wako Felix na Amina Mlay wa Kiboriloni Moshi,watoto wako Erick,Dereck na Michelle,pamoja na Mama zao,Jane na Vicky. 

Bila kuwasahau wadogo zako Adam,Gabriel,Charles,John,Richard na Dada zako wapendwa Sarah,Eunice,Neema,Diana,Ludie na Marafiki zako wote wa Moshi,Arusha na Dar es Salaam wakiwakilishwa na Ndugu Theoflo na Muheshimiwa Rita Mlaki na Wanachama wote wa RG Sports Club (Rose Garden Club) ya Dar es Salaam. Upole na ucheshi wako utakumbukwa daima na tunaanini siku moja tutakutana mbinguni. Upumzike kwa Amani.

KINANA AWAHUTUBIA WANANCHI WA URAMBO,ASIMIKWA UCHIFU WA KABILA LA WANYAMWEZI.

$
0
0
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu  Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi wa jimbo la Urambo,katika Mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Mwananchi Skwea mjini Urambo,mkoani Tabora.

Ndugu Kinana akiwa ameambatana na Katibu wa NEC Itikadi,Siasa na Uenezi,Nape Nnaye yuko katika ziara ya mikoa mitatu ya Tabora,Singida na Manyara,ya kuimarisha uhai wa chama,kukagua miradi mbalimbali ya maenedeleo inayotekelezwa na kusimamiwa na Serikali ya CCM,na pia kusikiliza matatizo ya wananchi na kuyapatia ufumbuzi.

Katika mkutano huo wa hadhara uliowakutanisha Wana Urambo kwa wingi,Kinana pia alisimikwa Uchifu wa kabila la Wanyamwezi.Kubwa zaidi Kinana pia alikabidhi piki piki 16 na baiskeli 95 kwa ajili ya watendaji wa chama cha CCM katika kata na matawi,zilizotolewa na Wabunge Mh,Samwel Sitta wa jimbo la Urambo Mashariki na Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Tabora,Mh.Magreth Sitta.
 Baadhi ya Wananchi wa Mji wa Urambo wakiwa wamefurika kwenye uwanja wa Mwananchi Skwea,wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana kwenye mkutano wa hadhara,uliofanyika Wilayani Urambo,Kinana akiwa ameambatana na Katibu wa NEC Itikadi,Siasa na Uenezi,Nape Nnaye yuko mkoani Tabora kwa ziara ya siku 11,za kuimarisha uhai wa chama,kuhimiza utekelezaji wa Ilani ya CCM,na kusikiliza matatizo mbalimbali ya wananchi.
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akikabidhi moja ya piki piki 16 kwa mmoja wa makatibu wa Kata,Bwa.Baraka ambazo zilizotolewa na Wabunge Mh,Samwel Sitta wa jimbo la Urambo Mashariki na Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Tabora,Mh.Magreth Sitta.
  Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akikabidhi baiskeli kwa mmoja wa viongozi wa chama hicho,Bi Fatma Ulaya mjini Urambo katika mkutano wa hadhara.
 Katibu wa NEC Itikadi,Siasa na Uenezi,Nape Nnaye akiwahutubia Wananchi wa Mji wa Urambo kwenye uwanja wa Mwananchi Skwea 
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiwa ameketishwa kwenye Kigoda akifanyiwa tambiko mara baada ya kusimikwa Uchifu wa kabila la Wanyamwezi.
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu  Abdulrahman akikabidhiwa silaha ya jadi Mkuki,na mmoja wa wazee wa Kinyamwezi mara baada ya kusimikwa Uchifu wa kabila hilo mbele ya umati mkubwa wa wakazi wa mji wa Urambo.PICHA NA MICHUZIJR-URAMBO TABORA.

Udanganyifu kwenye biashara ya gesi ya kupikia (LPG)

$
0
0
Mfano wa mitungi midogo ambayo haikutimia uzito unaotakiwa.
 Salaam Ankal Michuzi.
Tafadhali wahadharishe wadau kuhusu udanganyifu mkubwa unaofanyika hivi sasa kwenye mitungi ya gesi ya kupikia.
Wajanja hao hupunguza gesi kutoka kwenye ile mitungi mikubwa na kupata mitungi midogo ambayo haijatimia uzito unaotakiwa.
Jinsi ya kukwepa udanganyifu huu mkubwa ni  kuwa,  kila unaponunua gesi ya kupikia, kuhakikisha mtungi huo una "seal" kwenye sehemu ya kutolea gesi.
Pili, usinunue mtungi wa gesi bila kuhakikisha kuwa umeupima kwenye mizani iliyopo kwa muuzaji wa gesi. 
Ni matakwa ya sheria kwamba, kila muuzaji wa gesi ya kupikia, anakuwa na mizani dukani kwake ili mteja aweze kuhakiki uzito wa mtungi anaponunua.

Tafadhali mweleze rafiki,  ndugu, jamaa, jirani na hata wenzako kazini au kwenye sehemu ya biashara, ili wasikumbwe na wizi huo wa mchana.
Tafadhali Ankal wajuze wadau wako wajihadhari, kwani taasisi husika (Wakala wa Vipimo) hata wakiwa wengi kiasi gani hawawezi kufika kila kona ya nchi hii ili wafanye kaguzi za kuwabaini Wajanja kama hao.
Ni mimi, Mdau  wa Gesi.


Jinsi gesi inavyopunguzwa toka kwenye mitungi mikubwa.

OFISI ndogo ya Bunge la Jamhuri la Muungano wa Tanzania leo imetialiana saini na Chama cha kupunguza Matumizi ya Silaha na Maridhiano cha Jamhuri ya Watu wa China (Chinese Peoples’ Association for Peace and Disarmament) wenye thamani ya dola laki moja za kimarekani.

$
0
0
  Katibu wa Bunge la Jamhuri la Muungano wa Tanzania Bw. Thomas Kashililah (kulia) akiwakabidhi zawadi baadhi ya wajumbe aliokuja nao mgeni wake.
  Katibu wa Bunge la Jamhuri la Muungano wa Tanzania Bw. Thomas Kashililah (kulia) akimkabidhi zawadi mgeni wake Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha kupunguza Matumizi ya Silaha na Maridhiano cha Jamhuri ya Watu wa China (Chinese Peoples’ Association for Peace and Disarmament) Bi. Chen Huaifan (kushoto) mara baada ya kutia saini mkataba wa makubaliano wenye thamani za fedha za kimarekani dola laki moja leo ofisi ndogo za Bunge zilizopo jijini Dar es Salaam.
 Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha kupunguza Matumizi ya Silaha na Maridhiano cha Jamhuri ya Watu wa China (Chinese Peoples’ Association for Peace and Disarmament) Bi. Chen Huaifan (kushoto) akimkabidhi zawadi Katibu wa Bunge la Jamhuri la Muungano wa Tanzania Bw. Thomas Kashililah (kulia) mara baada ya utiaji saini mkataba wa makubaliano wenye thamani za fedha za kimarekani dola laki moja leo ofisi ndogo za Bunge zilizopo jijini Dar es Salaam.
 Katibu wa Bunge la Jamhuri la Muungano wa Tanzania Bw. Thomas Kashililah (kulia) pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha kupunguza Matumizi ya Silaha na Maridhiano cha Jamhuri ya Watu wa China (Chinese Peoples’ Association for Peace and Disarmament) Bi. Chen Huaifan wakitia saini mkataba huo wa thamani za fedha za kimarekani dola laki moja leo ofisi ndogo za Bunge zilizopo jijini Dar es Salaam.
  Katibu wa Bunge la Jamhuri la Muungano wa Tanzania Bw. Thomas Kashililah akitoa maelezo juu ya kazi mbalimbali zifanywazo na Bunge la Jamhuri la Muungano wa Tanzania leo wakati wa sherehe fupi ya utiaji saini mkataba wathamani ya dola laki moja za kimarekani kati ya Chama cha Kupunguza matumizi ya silaha na Maridhiano cha China na Ofisi za Bunge la Jamhuri la Muungano wa Tanzania.
 
 Baadhi ya viongozi toka pande zote mbili wakiwa katika sherehe ya utiaji saini mkataba wa thamani ya dola laki moja za kimarekani kwaajili ya ununuzi wa vifaa vya ofisi za Bunge la Jamhuri la Muungano wa Tanzania uliofanyika leo ofisi ndogo za Bunge zilizopo jijini Dar es Salaam.
Katibu wa Bunge la Jamhuri la Muungano wa Tanzania Bw. Thomas Kashililah (aliyekaa kulia mstari wa mbele) akiwa katika picha ya pamoja na mgeni wake Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha kupunguza Matumizi ya Silaha na Maridhiano cha Jamhuri ya Watu wa China (Chinese Peoples’ Association for Peace and Disarmament) Bi. Chen Huaifan (aliyekaa mstari wa mbele kushoto) mara baada ya utiaji saini mkataba wa makubaliano wenye thamani za fedha za kimarekani dola laki moja leo ofisi ndogo za Bunge zilizopo jijini Dar es Salaam.
--- 
Na. Benedict Liwenga-MAELEZO.
OFISI ndogo ya Bunge la Jamhuri la Muungano wa Tanzania leo imetialiana saini na Chama cha kupunguza Matumizi ya Silaha na Maridhiano cha Jamhuri ya Watu wa China (Chinese Peoples’ Association for Peace and Disarmament) wenye thamani ya dola laki moja za kimarekani.

Utaiji saini huo umefanyika leo katika Ofisi ndogo za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ukihusisha viongozi wa pande zote mbili akiwemo Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Bw. Thomas Kashililah pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha kupunguza Matumizi ya Silaha na Maridhiano cha Jamhuri ya Watu wa China (Chinese Peoples’ Association for Peace and Disarmament) Bi. Chen Huaifan.

Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Bw. Thomas Kashililah amesema kuwa mkataba huo wenye thamani ya dola laki moja za kimarekani utasaidia ofisi ya Bunge kuweza kupata vifaa mbalimbali vya ofisi vikiwemo kompyuta, mashine ya kudurufu, vipaza sauti, kamera pamoja na vifaa vya kurekodia.

“Ndugu zetu kutoka China pamoja na hiki Chama chao wamesaini pamoja nasi mkataba wenye thamani ya dola laki moja za kimarekani ambao wametutaka sisi tuamue wenyewe ni vifaa gani tunahitaji kwaajili ya ofisi yetu ya Bunge mjini Dodoma ili wao waweze kutununulia na kutukabidhi”. Alisema Kashililah.

China na Tanzania zimekuwa zikitiliana saini mikataba mbalimbali ya maendeleo ambayo kwa namna moja mikataba hiyo imekuwa ikizinufaisha pande zote mbili kiuchumi na mpaka hivi sasa uhusiano huu umedumu kwa muda miaka hamsini.

MAKALLA ATAKA TATHMINI MPYA BWAWA LA MWANJORO MEATU

$
0
0
Na Athumani Shariff
Naibu Waziri wa Maji, Mh. Amos Makalla amewaagiza wataalamu wa maji kutoka Wizara ya Maji na Sekretarieti ya Mkoa wa Simiyu kufanya tathmini mpya ya bwawa la Mwanjoro lililopo katika kijiji cha Jinamo umbali wa kilometa 35 kutoka makao makuu ya Wilaya ya Meatu Mkoani Simiyu. Makalla alilazimika kutembelea bwawa hilo baada ya kupokea maombi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu Rosemary Kiring’ini kuja kujionea hali halisi ya bwawa la Mwanjoro.
Kiring’ini alisema taarifa zinazotolewa na kupelekwa Wizarani kuwa, bwawa hilo limekamilika kwa asilimia 80 si za kweli kwani Mkandarasi ametelekeza mradi na amekimbia, ilihali wananchi wanaendelea kupata tabu ya kero ya maji. 
“Mh. Naibu Waziri hata hiyo asilimia 80 wanayosema imekamilika si kweli, tutakapokwenda utajionea mwenyewe hatua ya bwawa hilo ilipofika” alieleza DC. Kiring’ini. 
Baada ya kufika katika bwawa la Mwanjoro na kujionea hali halisi, Makalla hakuridhishwa na hatua iliyofikia bwawa hilo na kushangazwa kwa kiasi cha pesa ambazo tayari mkandarasi ameshalipwa. 
 “Siridhiki na hatua ya mradi ulipofikia na siamini kama kazi iliyofanywa inafikia thamani ya shilingi milioni 800 ambazo mkandarasi ameshalipwa” alisema Makalla. 
Kutokana na hali hiyo na baada ya kujionea hali ilivyo katika mradi huo mkubwa wa bwawa, Mh. Makalla aliwaagiza wataalamu wa maji kutoka Wizara ya Maji kufanya tathmini upya ya kazi iliyofanywa, kazi iliyobaki, gharama za kazi hiyo, pamoja na muda utakaotumika katika kulikamilisha bwawa hilo. 
“Nawaagiza mufanye tathmin upya ya gharama za kukamilisha kazi hiyo, kasoro zilizopo, mapendekezo, gharama za kukamilisha na muda wa utekelezaji wa shughuli hiyo na taarifa hiyo niipate wiki ijayo”. Aliagiza Makalla. 
Akihutubia wananchi wa kijiji cha Jinamo Naibu Waziri Makalla aliwaahidi wanchi hao kuwa serikali itakamilisha mradi huo katika mwaka wa fedha wa 2014/2015 endapo bajeti ya Wizara ya Maji itapita. Katika hatua nyingine Makalla hakufurahishwa na Mkandarasi wa bwawa hilo Nyakirang’ani Construction Limited kwa kulitelekeza bwawa hili huku akiwa ameshachukua zaidi ya shilingi milioni 800 na kuahidi kuwa atahakikisha hatopata kazi katika Wizara ya Maji nchi nzima. 
Bwawa la Mwanjoro lilianza kujengwa mwaka 2009 kwa gharama ya shilingi bilioni moja na milioni mia moja na hamsini chini ya Mkandarasi Nyakirang’ani Construction Limited nakwa usimamizi wa Mtaalamu mshauri Netwas Tanzania Limited.
 Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla akikagua bwawa la Mwanjoro huku akipokea taarifa za bwawa hilo.
 Bwawa la Mwanjoro kama linavyoonekana, lilianza kujengwa tangu mwaka 2009 kwa gharama ya shilingi bilioni 1.15.

 Mtaalamu wa mabwawa kutoka Wizara ya Maji Inj. Ayub Shaban akimfafanulia Naibu Waziri wa Maji namana bwawa hilo linavyotakiwa kujengwa.

Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla akiwasimamisha wataalamu wa Wizara ya Maji nakuwapa maelekezo mbele ya wanakijiji cha Jinambo mahali ambapo bwawa la Mwanjoro lilipojengwa wakati alipokuwa anahutubia.

Viewing all 110078 articles
Browse latest View live




Latest Images