Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109996 articles
Browse latest View live

Wezi waiba miundombinu ya soko la Ngiu Makete

$
0
0
Katika hali ya kushangaza na kusikitisha, wezi wasiofahamika wameiba baadhi ya miundombinu ya soko la Ngiu wilayani Makete mkoani Njombe licha ya soko hilo kuwa na mlinzi.

Mwandishi wa blog hii ambaye amefika eneo la tukio mara baada ya kupenyezewa taarifa hizi na wananchi, ameshuhudia baadhi ya miundombinu haipo ikiwemo mifuniko yote ya chuma inayofunikia masinki ya vyoo, pamoja na mabomba ya kutiririshia maji ya mvua

Taarifa kamili na picha zote za tukio hilo zitakujia baadaye kidogo.
 Muonekano wa soko la Ngiu lililopo kata ya Iwawa, Makete mjini.
 Chemba ya choo cha soko hilo ikionekana baada ya wezi kuiba mifuniko yote mitatu ya kufunikia chemba hiyo
Na Edwin Moshi wa globu ya jamii, Makete

ALL ROADS LEAD TO DALLAS CONFERENCE

MSIBA WA KADA WA CHADEMA KALOLO, VYAMA VYAWEKA UPINZANI PEMBENI NA KUFANYA MAZISHI YA KIHISTORIA

$
0
0
Diwani wa kata ya Mvinjeni Frank Nyalusi Chadema akiweka udongo
Ndugu  wakiweka mashada
Ndugu wa kalolo kutoka Kenya  akiweka shada
Kamanda wa UVCCM mkoa wa Iringa Salim Asas akiweka  shada la maua  katika kaburi la kada maarufu wa Chadema mkoa wa Iringa Gervas Kalolo  wakati wa mazishi  yaliyofanyika makaburi ya Mtwivila mjini Iringa
Mstahiki meya  Amani Mwamwindi  akiweka  shada la maua.
Kwa habari kamili na picha zaidi BOFYA HAPA

Kali TV: This week's Around Town

$
0
0
This week, Kali TV brings you highlights from the US-Africa Trade Policy Forum organized by Advancing Investment and Trade in Africa (AITA), the successful Ethiopian Community Development Council Banquet in Arlington Virginia, interview with the Sierra Leone Refugee All Stars band leader and the ongoing Diaspora World Cup soccer tournament. Enjoy!

JACQUELINE WOLPER LIKE NEVER BEFORE - The Sporah show in Dar!

Mnada mkubwa wa Isuzu Pick-Up Double Cabin na Malori kufanyika Jumamosi hii Kijitonyama, Dar es salaam

$
0
0
We shall sell 19 Isuzu PickUP Double Cabin and 9 Volvo & Leyland DAF trucks by public auction this Saturday 10th May 2014. Viewing is as from Today and Tomorrow at Mancity Car wash grounds, Kijitonyama , Mabatini road. For further info's Contact : Universal Auction Center, +255754 284926

Just in: Balozi wa Malawi nchini Tanzania Mhe. Flossy Gomile-Chidyaonga afariki dunia jijini Dar es salaam leo

$
0
0


“Ni kwa masikitiko makubwa Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa (ya Malawi) unauarifu umma kufariki dunia kwa Balozi Flossy Gomile-Chidyaonga baada ya kuugua kwa muda mfupi jijini Dar es salaam mchana huu”, imesema taarifa iliyotolewa na msemaji wa Wizara hiyo Quent Kalichero.

“Tangu mwaka 2006 Marehemu Bi Flossy Gomile-Chidyaonga alikuwa Naibu Balozi wa Malawi London kabla ya kuteuliwa kuwa Balozi wa Malawi nchini Tanzania mnamo Septemba mwaka 2011”, imesema taarifa hiyo na kuongezea kuwa taratibu za mazishi zitatangazwa baada ya taratibu kukamilika.


KINANA AWASHA MOTO IGUNGA,AWAMWAGIA SIFA LUKUKI VIONGOZI VIJANA WA WILAYA HIYO KWA UBUNIFU WA MIRADI YA VIJANA YA KUJIKWAMUA NA UMASKINI

$
0
0

Katibu MKuu wa CCM,Ndugu Kinana akikata utepe kuashiria uzinduzi wa wakala wa uuzaji wa matrekta kwa wanavikundi,yanayouzwa na Vijana SACCOS LTD,ya Igunga,inayojumuisha vikundi mbalimbali vya wilaya hiyo,wakati wa ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa na serikali pamoja na wananchi wilayani humo,Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Igunga,Mh.Elibariki Kingu.
Ndugu Kinana akiwasha moja ya trekta mara baada ya kuuzindua uwakala wa zana za kilimo wa Vijana SACCOS LTD wilayani humo.
  Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akikagua shamba la alizeti la  ekali 25 la Kikundi cha Vijana katika Kijiji cha Iborogero, wilayani Igunga, wakati wa ziara ya kuimarisha uhai wa chama , kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya CCM, kukagua maandalizi ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa na kusikiliza kero za Wananchi.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akitazama mmea wa alizeti,wakati alipokwenda kagua shamba la alizeti la  ekali 25 la Kikundi cha Vijana katika Kijiji cha Iborogero, wilayani Igunga, wakati wa ziara ya kuimarisha uhai wa chama , kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya CCM, kukagua maandalizi ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa na kusikiliza kero za Wananchi.
Sehemu ya shamba la alizeti la  ekali 25 la Kikundi cha Vijana katika Kijiji cha Iborogero, wilayani Igunga, wakati  Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana alipokagua wakati wa ziara ya kuimarisha uhai wa chama , kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya CCM, kukagua maandalizi ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa na kusikiliza kero za Wananchi.
 Katibu Mkuu wa CCM, Kinana akihututubia katika katika mkutano wa hadhara wa CCM uliofanyika katika  Uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine mjini Igunga, ambapo alisifu utenaji a Mkuu wa Wilaya ya Igunga, Elibariki Kingu na Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya hiyo pamoja na  Mkurugenzi wa halmashauri hiyo kwa uchapakazi wao. pamoja na ubunifu wa miradi mbalimbali ya kuwasaida vijana.
  Baadhi ya Wafuasi wa chama cha CCM na Wananchi mbalimbali wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye uwanja wa Sokoine mjini Igunga jioni ya leo,kwenye mkutano wa hadhara ambapo Katibu Mkutano wa CCM,Ndugu Kinana alihutubia.
 Katibu wa Itikadi n Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akihutubia katika mkutano wa hadhara wa CCM uliofanyika katika  Uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine mjini Igunga.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana (pichani shoto) akimpokea aliyekuwa Katibu wa chama cha CUF Wilaya ya Igunga, Michael Maganga (aliyenyoosha kadi yake ya CUF juu), aliyeamua kukihama chama hicho na kujiunga na CCM katika mkutano huo wa hadhara uliofanyika jioni ya leo kwenye uwanja wa Sokoine.Kinana amemaliza leo ziara yake wilayani humo kuhamia wilaya ya Nzega hapo kesho kuendelea na ziara ya siku 10 mkoani Tabora.

PICHA ZAIDI BOFYA MICHUZIJR.BLOGSPOT.COM

Article 2

Finally Kenya Gets Its Own “Diamond Platnumz”

$
0
0
It’s without a doubt that Tanzania's  Diamond Platnumz has his smooth Bongo game in the clutch. The young phenom is always being showered with praises, and admiration thanks to his soft sentimental songs.
But that is about to change because one of Kenya’s legendary producers, Tedd Josiah, has just discovered Diamond’s replacement from Kenya.

Meet Iddi Hemed. This guy is a stellar vocalist known for his smooth sounds. Whether it's a soulful story about real-life trouble or an ultra-romantic ballad, R&B's silky smooth sound is a pop music staple and Iddi is the best when it comes to getting us in touch with our emotions.

He just released his first single, “Usijali” after being signed by Tedd Josiah's Sandstone Studios.
“Usijali” is SWARNB. A new genre in the Kenyan music industry which is a fusion of a rich spicy blend of Swahili poetry fused with RnB. Iddi is currently working on his album which is set to be released later this year.
Here’s “Usijali” for your listening pleasure

RED CROSS YASAIDIA WANAFUNZI WAISHIO MAZINGIRA MAGUMU KIBAHA

$
0
0
Na John Gagarini, Kibaha 
CHAMA cha Msalaba Mwekundu mkoani Pwani kimesema kuwa kitaendela kuisaidia jamii ambayo inauhitaji pamoja na wale wanaokumbwa na majanga mbalimbali. 
Hayo yamesemwa  mjini Kibaha na katibu msaidizi wa chama hicho Felisiana Mmasi wakati wakitoa misaada ya viatu na vifaa vya shule kwa wanafunzi wa shule ya sekondari Nyumbu na vituo vya kulelea watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu vya THADEI na Buloma vilivyopo kata ya Picha ya Ndege na Mkuza wilayani Kibaha. 
Mmasi alisema kuwa lengo la chama hicho ni kuwasaidia watu wenye matatizo mbalimbali kwenye jamii ikiwa ni pamoja na kutoa msaada kwenye majanga na maafa yanoyojitokeza. 
 "Mbali ya kutoa viatu pia tumetoa madaftari na kalamu ambapo tutaendelea kusaidia wanafunzi waishio kwenye mazingira magumu kwenye mkoa mzima ambapo baadhi ya wilaya tayari zimeshapatiwa misaada hiyo," alisema Mmasi. 
Kwa upande wake mratibu wa mradi wa Life kupitia chama hicho Kibaha Mjini Agnes Lubogo alisema kuwa mbali ya kusaidia kutoa misaada mbalimbali pia wanasaidia kuwahudumia wagonjwa wa UKIMWI walio majumbani. 
Lubogo alisema kuwa wanahudumia wagonjwa ambao watoro ambao hawapati huduma mahospitalini hivyo kuwafuata huko waliko ambapo wana wahudumu wa nyumbani wapatao 73.

OFISA WA RED CROSS PWANI ISARIA TOWO AKIWAPATIA MADAFTARI
WANAFUNZI WA KITUO CHA THADEI MADAFTARI KATIKA MAADHIMISHO YA SIKU YA CHAMA HICHO YALIYOFANYIKA MJINI KIBAHA PICHA NA JOHN GAGARINI

JP AWANIA UONGOZI SIMBA

$
0
0
Bw. Alfred Martin Elia  a.k.a JP akipokea fomu ya kugombea ujumbe wa kamati ya utendaji wa Simba Sports Club toka kwa Bw. Khalid Kamuguna. Uchaguzi huo unatarajiwa kufanyika mwisho wa mwezi juni mwaka huu.

A Brief Statement On Boko Haram by The Mufti Of Saudi Arabia Shaykh Abdul-Azeez Aali Shaikh

$
0
0

Shaykh Abdul Azeez Aali Shaikh (may Allaah preserve him) said, "Boko Haraam is a misguided group and are from the Khawaarij. 

Their actions are evil and harmful for Islam and the Muslims.

Their actions are destructive.

Abducting girls is from the actions of a misguided group.

If Boko Haraam are claiming a call to jihad, then it is nothing but ignorance and enmity against Islaam and the Muslims.

Boko Haraam are not upon correctness and guidance because Islaam opposes abduction/kidnapping, unlawful killing and transgression.

Marrying off kidnapped/abducted females is haraam and it is not permissible to give them in marriage."

Kampuni ya BG Tanzania na shirika la Africare Tanzania wazindua Mradi wa Kuwawezesha Vijana Mkoani Mtwara.

$
0
0
Kampuni ya BG kwa kushirikiana na Kampuni ya Africare Tanzania wa​me​zindua Rasmi mradi wao wa kuwawezesha vijana unaoitwa "Kijana Jikwamue"Mkoani ​Mtwara​.​ 
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Kanali mstaafu Joseph Simbakalia ndiye mgeni rasmi katika uzinduzi wa mradi huo. Mradi huo una lengo la kuboresha maisha ya vijana katika Wilaya ya Mtwara kupitia mafunzo ya ujasiriamali, ushauri na stadi za maisha. 
Kampuni ya BG imedhamiria kutumia dola za Kimarekani 765,000 takribani shilingi za Tanzania, Bilioni 1.23 zitakazowekezwa kwa kipindi cha miaka mitatu, ikiendelea kujitoa kwa kujenga na kutoa fursa zitakazo wasaidia watu kuwa na uwezo kuboresha maisha yao katika ngazi ya chini mpaka ngazi ya Kitaifa. 
Akizungumza katika tukio hilo, Kanali Simbakalia alisema"Vijana ni uti wa mgongo wa Taifa na tunawashukuru Kampuni ya BG Tanzania kwa kudhamini mradi huu, Sisi kama serikali tunawahakikishia kwamba mradi huu utakuwa endelevu na utainufaisha jamii. 
Tunatoa wito kwa makampuni mengine ya gesi na mafuta kuwekeza zaidi kwenye programu za vijana hasa kwenye eneo la ujasiriamali na kuwajengea uwezo.
" Lengo la mradi huo ni kuwasaidia vijana kuwaelimisha kuhusu dhana ya ubunifu ya ujasiriamali na mipango ya kuwawezesha kuanza au kupanua biashara zao, na kujenga fursa za ajira kwa jamii zao. 
BG na Africare wameshabainisha vikundi vya ujasiriamali, mahali walipo na aina ya shughuli za kiuchumi wanazofanya katika mkoa wa huo. Mshauri wa Masuala ya Maendeleo ya Jamii na mahuisiano; Kampuni ya BG Tanzania, Bwana Emil Karuranga, amesema, " BG Tanzania inaamini kwamba ufunguo muhimu wa maendeleo ya kijamii na kiuchumi ipo katika kujengea uwezo wadau kwenye maeneo mbalimbali. Kuwekeza katika mtaji wa rasilimali watu ni njia bora ya kukuza uchumi na maendeleo ya watu kwa ujumla. 
Uwezeshaji wa vijana ni kipaumbele chetu kwa sababu wao ni tegemeo la siku za baadaye kwa nchi ya Tanzania ". Akizungumza kwa niaba ya Africare Tanzania, Naibu Mkurugenzi wa shirika hilo, Bwana Alfred Kalaghe alisema , " Africare imefurahishwa kuona BG Tanzania wametenga fedha kusaidia mradi wa vijana. 
Mradi huu utasaidia kuongeza kipato kupitia kuongezeka kwa ajira, Africare inaamini kwamba kama vijana watahimizwa kushiriki katika shughuli zitakazo boresha hali za maisha yao, basi watakuwa na uwezo wa kuchangia ukuaji wa uchumi wa Taifa na ustawi wake 
" Mradi huu ni moja kati ya jitihada za BG Tanzania katika kujenga uwezo, kama vile, ufadhiri wa mafunzo stadi wa chuo cha ufundi cha VETA katika mikoa ya Lindi na Mtwara.
Mshauri wa Masuala ya Maendeleo ya Jamii na Mahusiano; wa Kampuni ya BG Tanzania, Emil Karuranga (wa pili kushoto) na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Africare, Alfred Kalaghe (wa pili kulia) wakisaini mkataba wa makubaliano wakati wa uzinduzi wa Mradi wa mafunzo kuwawezesha vijana kiuchumi mkoani Mtwara.. 
Wanaoshuhudia (kulia) ni Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa huo, Johansen Bukwali na Meneja Mradi wa vijana, Dickson Mbita

Waziri Membe akutana na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirikas la Ndege la Uturuki

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb) wa kwanza kulia na ujumbe wake akiwa katika mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Ndege la Uturuki hayupo pichani jijini Istambul siku ya Ijumaa tarehe 09 Mei, 2014. Mhe. Membe aliliomba Shirika hilo liingie ubia na Shirika la Ndege la Tanzania. Ombi ambalo Mkurugenzi Mtendaji aliahidi kulifanyia kazi ambapo wiki ijayo atatuma timu ya wataalamu ili kuongea na timu ya wataalamu ya ATCL kutathmini namna mashiraka hayo yatakavyoweza kushirikiana.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Ndege la Uturuki wa katikati pamoja na timu yake ikimsikiliza kwa makini Waziri Membe hayupo pichani.
Ujumbe wa Tanzania na wa Shirika la Ndege la Uturuki wakiendelea na mazungumzo
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Ndege la Uturuki akifanya power point presentation kuhusu utendaji wa shirika lake na matarajio ya kibiashara katika Bara la Afrika na ulimwengu wote kwa ujumla. Alitaja Bara la Afrika kuwa ni bora zaidi kibiashara katika siku zijazo kutokana na ukuaji wa uchumi wa kasi.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa (kulia) akimkabidhi zawadi Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Ndege la Uturuki
Waziri Membe kushoto naye anapokea zawadi yake kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Ndege la Uturuki
zawadi kwa Waziri Membe.
Mkutano wa Waziri Membe na Wafanyabiashara wakubwa wa Uturuki
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (kati) akiwaeleza wafanyabiashara wakubwa wa Uturuki (baadhi yao wanaonekana katika picha ya chini) fursa lukuki za uwekezaji zinazopatikana nchini Tanzania. Aliwahamasisha waje kuwekeza Tanzania hususan, katika sekta zitakazoongeza ajira kwa wingi kama vile viwanda vya nguo na kilimo. Wafanyabiashara hao walionesha dhamira ya dhati kuja nchini kuangalia fursa walizotangaziwa.
Baadhi ya Wafanyabiashara wa Uturuki na ujumbe wa Tanzania.
Waziri Membe akibadilishana kadi za mawasiliano na Wafanyabiashara wakubwa wa Uturuki.

Kampuni ya BG Tanzania na shirika la Africare Tanzania wazindua Mradi wa Kuwawezesha Vijana Mkoani Mtwara

$
0
0
​Mshauri wa Masuala ya Maendeleo ya Jamii na Mahusiano; wa Kampuni ya BG Tanzania, Emil Karuranga (wa pili kushoto) na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa​ ​Shirika la ​Africare, Alfred Kalaghe (wa pili kulia) wakisaini mkataba wa makubaliano wakati wa uzinduzi wa Mradi wa mafunzo kuwawezesha vijana kiuchumi mkoani Mtwara juzi. ​Wanaoshuhudia (kulia) ni Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa huo, Johansen Bukwali na Meneja Mradi wa vijana, Dickson Mbita.

Kampuni ya BG kwa kushirikiana na Kampuni ya Africare Tanzania wa​me​zindua Rasmi mradi wao wa kuwawezesha vijana unaoitwa "Kijana Jikwamue"Mkoani ​Mtwara​.​ Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Kanali mstaafu Joseph Simbakalia ndiye mgeni rasmi katika uzinduzi wa mradi huo.

Mradi huo una lengo la kuboresha maisha ya vijana katika Wilaya ya Mtwara kupitia mafunzo ya ujasiriamali, ushauri na stadi za maisha.
Kampuni ya BG imedhamiria kutumia dola za Kimarekani 765,000 takribani shilingi za Tanzania, Bilioni 1.23 zitakazowekezwa kwa kipindi cha miaka mitatu, ikiendelea kujitoa kwa kujenga na kutoa fursa zitakazo wasaidia watu kuwa na uwezo kuboresha maisha yao katika ngazi ya  chini mpaka ngazi ya Kitaifa.

Akizungumza katika tukio hilo, Kanali Simbakalia alisema"Vijana ni uti wa mgongo wa Taifa na tunawashukuru Kampuni ya BG Tanzania kwa kudhamini mradi huu, Sisi kama serikali tunawahakikishia kwamba mradi huu utakuwa endelevu na utainufaisha jamii. Tunatoa wito kwa makampuni mengine ya gesi na mafuta kuwekeza zaidi kwenye programu za vijana hasa kwenye eneo la ujasiriamali na kuwajengea uwezo."

Lengo la mradi huo ni kuwasaidia vijana kuwaelimisha kuhusu dhana ya ubunifu ya ujasiriamali na mipango ya kuwawezesha kuanza au kupanua biashara zao, na kujenga fursa za ajira kwa jamii zao. BG na Africare wameshabainisha vikundi vya ujasiriamali, mahali walipo na aina ya shughuli za kiuchumi wanazofanya katika mkoa wa huo.

Mshauri wa Masuala ya Maendeleo ya Jamii na mahuisiano; Kampuni ya BG Tanzania, Bwana Emil Karuranga, amesema, " BG Tanzania inaamini kwamba ufunguo muhimu wa  maendeleo ya kijamii na kiuchumi ipo katika kujengea uwezo wadau kwenye maeneo mbalimbali. Kuwekeza katika mtaji wa rasilimali watu ni njia bora ya kukuza uchumi na maendeleo ya watu kwa ujumla. Uwezeshaji wa vijana ni kipaumbele chetu kwa sababu wao ni tegemeo la siku za baadaye kwa nchi  ya Tanzania ".

Akizungumza kwa niaba ya Africare Tanzania, Naibu Mkurugenzi wa shirika hilo, Bwana Alfred Kalaghe alisema , " Africare imefurahishwa kuona BG Tanzania wametenga fedha kusaidia mradi wa vijana. Mradi huu utasaidia kuongeza kipato kupitia kuongezeka kwa ajira, Africare inaamini kwamba kama vijana watahimizwa kushiriki katika shughuli zitakazo boresha hali za maisha yao, basi watakuwa na uwezo wa kuchangia ukuaji wa uchumi wa Taifa na ustawi wake "

Mradi huu ni moja kati ya jitihada za BG Tanzania  katika kujenga uwezo, kama vile, ufadhiri wa mafunzo stadi wa chuo cha ufundi cha VETA  katika mikoa ya Lindi na Mtwara. 

sina anuani ya facebook, iliyopo mtandaoni humo ni feki - mhe. amos gabriel makalla

serikali yafafanua juu ya mustakabali wa maafisa a wizara ya maliasili na utalii

HII NDIO FAIDA YA MICHEPUKO BARABARANI

$
0
0
 Kamera ya Globu ya Jamii,mchana hii imelinasa daladala hili linalofanya safari zake kati ya Mbagala Rangi tatu - Kawe likiwa limeingia mtararoni katika eneo la Kinondoni Moroco jijini Dar,baada ya kufanya mchepuko wakati barabara hiyo ikiwa na foleni ya Magari yaliyokuwa akisubiri ruhusa ya askari wa Usalama barabarani.Hapa ni jitihada za kulikwamua daladala zikifanyika.

JK AKUTANA NA RAIS JOSEPH KABILA LEO IKULU YA KINSHASA, AELEKEA ANGOLA

$
0
0
Rais Jakaya Kikwete  amewasili mjini Kinshasa  Jamhuri ya Watu wa Kongo (DRC) usiku wa kuamkia leo kwa ziara ya kikazi akitokea nchini Nigeria ambapo amehudhuria Mkutano wa Viongozi kuhusu Uchumi barani Afrika.
 Akiwa Kinshasa, leo tarehe 10 Mei, Rais Kikwete amefanya  mazungumzo na Rais Joseph Kabila ambapo wanatarajia kuzungumzia uhusiano baina ya nchi mbili hizi na hali ya kisiasa kwa ujumla katika ukanda wa Jumuiya ya ushirikiano wa Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC). 

 Mara baada ya Mazungumzo haya Rais Kikwete ameondoka kuelekea Luanda , Angola kwa ajili ya mazungumzo na Rais Jose Dos -Santos.

   Wakati huo huo, Rais Kikwete amemtumia salamu za rambirambi Rais Joyce Banda wa Malawi kufuatia kifo cha ghafla cha Balozi wa Malawi nchini Tanzania Flossy Gomile-Chidyaonga kilichotokea tarehe 9 Mei jijini Dar-Es-Salaam. 

 "Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za msiba wa Balozi Chidyaonga, ni huzuni kwetu sote" Rais amesema na kumuelezea Balozi Chidyaonga kuwa alikuwa mcheshi na aliyependa kushirikiana na wenzake kwa moyo mkunjufu. 

 " Ni huzuni zaidi kwetu sote kwakuwa kifo chake kimetokea ghafla mno kwa mtu tuliekua tunashirikiana naye kwa karibu katika juhudi za kukuza na kuimarisha mahusiano baina yetu" Rais amesema na kuongeza kuwa, kifo chake kimetokea wakati tunamhitaji zaidi na hivyo kusababisha pengo kubwa" 

 Rais amemuomba Rais Banda kufikisha salamu zake binafsi na za Watanzania kwa ujumla kwa familia ya marehemu, ndugu, Jamaa na Wamalawi wote kwa ujumla na kumuombea marehemu kwa mwenyezi Mungu, ampe mapumziko mema milele. 

 Imetolewa na; 
Premi Kibanga, 
Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi, 
Kinshasa-DRC 10 Mei 14
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisindikizwa na mwenyeji wake Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Demokrasia ya  Kongo ikulu ya Kinshasa leo.Rais Kikiwete alikuwa nchini DRC kwa ziara ya kikazi ya siku mbili(picha na Freddy Maro)
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiagwa na mwenyeji wake Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Demokrasia ya  Kongo ikulu ya Kinshasa leo.Rais Kikiwete alikuwa nchini DRC kwa ziara ya kikazi ya siku mbili
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na mwenyeji wake Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Demokrasia ya  Kongo ikulu ya Kinshasa walipokutana kwa mazungumzo

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete alipokuwa  katika mazungumzo na mwenyeji wake Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Demokrasia ya  Kongo ikulu ya Kinshasa leo.Rais Kikiwete alikuwa nchini DRC kwa ziara ya kikazi ya siku mbili. Picha na Freddy Maro
Viewing all 109996 articles
Browse latest View live




Latest Images