Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109996 articles
Browse latest View live

WAZIRI WA NISHATI NA MADINI PROFESA SOSPETER MUHONGO APOKEA NISHANI YA HESHIMA NCHINI NIGERIA

$
0
0
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo mapema Machi mwaka huu alikabidhiwa nishani ya kumbukumbu ya Profesa M.O. Oyawoye aliyewahi kuwa Profesa wa kwanza duniani kutoka Bara la Afrika katika masuala ya jiolojia huko nchini Nigeria. Profesa Muhongo alikabidhiwa nishani hiyo na timu ya wanajiolojia kwa kutambua mchango wake mkubwa barani Afrika na duniani kwa ujumla. Nishani hiyo alikabidhiwa balozi wa Tanzania nchini Nigeria Mhe. Daniel Ole Njoolay kwa niaba yake.
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo akiwa ofisini kwake huku akiwa amevaa nishani hiyo

Mdau Alfred Martin Elia achukua fomu ya kugombea ujumbe wa kamati ya utendaji wa Simba Sports Club

$
0
0
Mdau Alfred Martin Elia akipokea fomu ya kugombea ujumbe wa kamati ya utendaji wa Simba Sports Club toka kwa Bw. Khalid Kamuguna. Uchaguzi huo unatarajiwa kufanyika mwisho wa mwezi juni mwaka huu"

DISCUSSION ON EU-TANZANIA TRANSFER AGREEMENT WHICH ALLOWS TO TRIAL PIRATES CAPTURED BY EUROPEAN NAVAL FORCES IN TANZANIA COURTS

$
0
0
1
From left is Political Officer Delegation of the European Union Tom Vens, Rear Admiral Commander Task Force 465 Jürgen zur Mühlen , and the Chargé d´Affaires a.i. Hans Koeppel of the German Embassy in press conference for the role of EUNAVFOR, its cooperation with Tanzania and the recently signed European Union-Tanzania Transfer Agreement which allows to trial pirates, who are captured by European naval forces, in Tanzanians courts.
2
The Chargé d´Affaires a.i. Hans Koeppel from Embassy of Federal Republic of Germany welcomed the visit of the flagship as “an important sign of the common fight against piracy along the coast of the Indian Ocean”. He also talk about the aim of Task Force to fight against pirates with the countries bordering the coast of Indian Ocean including Tanzania.
3
Political Officer Delegation of European Union Tom Vens discuss about Europe day and Europe day , He also talk about the European Task Force that help security situation in the Earth lastly he discuss about good relationship between European Union and East African Community and Good Political relationship Between European Union and Tanzania.
4
Commander Force Force 465 Rear Admiral Jürgen zur Mühlen emphasized that the threat of piracy continues to exist. 10 days ago, the crew of Brandenburg boarded an Indian dhow which was formerly held hostage by pirates. The pirates fled from the captured dhow as EU naval forces intervened from the air and sea. “This event confirms that the piracy threat is still very real in the Indian Ocean. The deterrence and swift action by EU Naval Force once again denied the freedom of action to pirates”,
IMG_0221
Public Relation Officer of European Union Dormann addressing some issues during Press Conference.
8
9
Different media During the Press Conference at Umoja House today.
To Listen Click the Link down

STEVE NYERERE ATEULIWA KUONGOZA KIKOSI CHA WASANII KUTANGAZA AMANI NCHI NZIMA

$
0
0
 Mwigizaji na Mchekeshaji ambaye ni Mwenyekiti wa Kundi la Bongo Movie Unity, Steven Mengere a.k.a 'Steve Nyerere' (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) jijini Dar es Salaam juzi baada ya kuteuliwa kuwa msimamizi mkuu wa Wasanii wa nje ya Bunge Maalum. kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Tanzania Kwanza nje ya bunge, Renatus Muadhi, na katikati ni Mwenyekiti wa Taasisis hiyo, Agustino Matefu.
 Mwigizaji na Mchekeshaji ambaye ni Mwenyekiti wa Kundi la Bongo Movie Unity, Steven Mengere 'Steve Nyerere' (kushoto) akikabidhiwa mkataba wa kuwa msimamizi wa mkuu wa wasanii wa nje ya Bunge Maalum na Mwenyekiti wa Taasisi ya Tanzania Kwanza nje ya bunge, Agustino Matefu. Makabidhiano hayo yalifanyika juzi jijini Dar es Salaam.
---
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam.
WASANII wa Bongo Movie, muziki wa dansi, taarab, maigizo na tamthilia wametangaza kuzunguka nchi nzima wakiwa na kamati ya Tanzania Kwanza Nje ya Bunge Maalum la Katiba kwa lengo la kutangaza amani kwa vijana wa rika lote bara na visiwani.
Baadhi ya wasanaii hao ni pamoja na Steven Mengele ‘Steve Nyerere’ ambaye ameteuliwa kuwa msimamizi mkuu wa uwakilishi kwa upande wa wasanii katika Tanzania kwanza nje ya Bunge maalum, Muungano huo uko chini ya Mwenyekiti Augustino Matefu.
Akizungumza juzi na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Steve amesema kwamba ataungana na wasanii ambao wako katika vyama mbalimbali kama vile Chama Cha Demokrasia na Maendeleo, NCCR, Mageuzi , Cuf na vyama vingine huku wote wakiwa na lengo moja tu la kuhimiza mchakato wa katiba uendelee huku wanasiasa wakizingatia kudumisha amnai na umoja wa Watanzania.
Nyerere aliongeza kwa kusema kuwa yeye hakuwa na kipingamizi pindi alipoambiwa amechaguliwa kuwa miongoni mwa wasimamizi wa mpango huo ambao umewakutanisha vijana kutoka katika itikadi mbalimbali za vyama vya siasa.
“Nilipoambiwa hili jambo niliweka itikadi zangu za chama pembeni na kuuvaa Utanzania kwanza ili kuunganisha fani zetu wote kwa pamoja na kuweza kuwahimiza wananchi wadumishe amani tuliyokuwa nayo nchini” alisema Nyerere.
Aliongeza pia kwa kuwaomba viongozi wa dini masheikh na maaskofu wakiwemo mapadri wote kuungana nao wasanii hao katika kuhimizaani ya amani ya nchi.
“Sisi wasanii tunapata riziki zetu kutokana na amani na utulivu uliopo nchini mwetu hivyo kila msanii na Mmtanzania aone ni jambo la fedheha kuiichezea amani ambapo siku ikipitea tutakwenda kuomba hifadhi katika nchi za jirani zilizopata uhuru na kufuata ushauri kutoka kwetu”.,
Aliongeza kwa kusema kwamba ana imani kubwa watanzania watawaelewa pindi watakapokuwa katika ziara hiyo kuzunguka nchi nzima huku wakiwa na mabalozi watano kutoka kila nyanja ya sanaa ambazo ni muziki wa taarab, Hip Hop, Sanaa za maigizo, Michezo na tamthilia. Mkutano mkubwa unatarajiwa kufanyika Kibanda Maiti Zanzibar.

TEAM TANZANIA KATIKA MATEMBEZI YA SUSAN G. KOMEN WASHINGTON, DC

$
0
0

 Mmoja ya waandaaji wa matembezi ya Susan G. Komen ya saratani ya matiti akielezea jambo kabla ya kuanza kwa mbio kwa ajili ya mapambano ya Saratani hiyo hatari kwa akina mama ambayo Team Tanzania imeshiriki kwa mwaka watatu mfululizo.
 wanandugu wa Susan G. Komen wakiadhimisha siku ya dada yao kwenye maadhimisho ya mbio za saratani ya matiti zilizofanyika leo Jumamosi May 10, 2014 Washington, DC na mbio zilikuwa za maili 5.
Watanzania wa DC walioshiriki mbio hizo.
 Team Tanzania katika picha ya pamoja baada ya kumaliza mbio za maili tano.
Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

MAELEZO YA MHESHIMIWA MIZENGO P. PINDA (MB), WAZIRI MKUU, WAKATI AKIJIBU HOJA ZA WABUNGE KUHUSU HOTUBA YA BAJETI YA OFISI YA WAZIRI MKUU NA TAASISI ZAKE KWA MWAKA WA FEDHA 2014/2015

balozi seif aagiza usimamizi wa makubaliano kati ya mwekezaji wa hoteli ya sea cliff na wanakijiji

$
0
0
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ameuagiza Uongozi wa Serikali ya Mkoa wa Kaskazini Unguja pamoja na Wilaya ya Kaskazini “B” kusimamia ipasavyo makubaliano yaliyofikiwa kati ya Muwekezaji wa Hoteli ya Kimataifa ya Sea Cliff iliyopo katika Kijiji cha Kama na Wananchi wa Vijiji vinavyoizunguuka Hoteli hiyo. 
Amesema makubaliano hayo yalifikiwa na pande hizo mbili kufutia Vikao mbali mbali vilivyokuwa vikiendelea vya kutafuta maridhiano ambapo yeye binafsi alikuwa shahidi wa vikao hivyo. Balozi Seif alitoa agizo hilo hapo katika Ukumbi wa Hoteli ya Sea cliff wakati wa kikao maalum kilichotayarishwa kwa ajili ya utiaji saini wa makubaliano ya pande hizo mbili lakini chakusikitisha wale wawakilishi wa kamati husika na makubaliano hayo hawakuhudhuria licha ya kupata taarifa kamili ya kikao hicho. 
Alisema makubaliano ya pande hizo mbili bado yataendelea kuwa halali kwa vile vikao vyake vilishirikisha wajumbe na Viongozi wa pande zote zinazohusika ukiwemo uongozi wa Serikali wa Mkoa wa Kaskazini Unguja pamoja na ule wa Wilaya ya Kaskazini “ B”. 
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alielezea kusikitishwa kwake na uamuzi wa Wajumbe wa upande wa Kamati za Uvuvi, Mikoko, Mazingira na Diko za Vijiji vinavyoizunguuka Hoteli hiyo wa kususia kikao hicho bila ya sababu zisizoeleweka. 
Alifahamisha kwamba hali ya mgogoro wa Kiomba mvua ulifikia hatua ya makubaliano mazuri lakini kinachoonekana hivi sasa baadhi ya watu kuanza kuhusisha makubaliano hayo na masuala ya Kisiasa. “ Mimi nimekuja hapa kama Kiongozi wa Serikali ili kuona namna gani hatma ya pande hizi mbili inafikia pahali pazuri. Kinachoonekana kwa sasa hivi ni baadhi ya watu kujaribu kujitafutia umaarufu kwa mgongo wa Kisiasa “. Alisema Balozi Seif. 
“ Wenzetu tuliokuwa nao katika vikao karibu vitatu hii hatua ya mwisho kabisa hawakuja bila ya sababu. Lakini Vikao vya kujadili makubaliano ya muongozo uliotolewa na Kamati ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar nao pia walishirikishwa kikamilifu “. Alisisitiza Balozi Seif. 
Mapema Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Mh. Pembe Juma Khamis alisema Serikali ya Mkoa huo haiwezi kustahamili uchochezi unaoonekana kuanza kupaliliwa na baadhi ya wana siasa kwa kujaribu kuwapotosha Wananchi. 
Mh. Pembe alisema juhudi kubwa zimechukuliwa katika kuona kwamba pande hizo mbili zilizokuwa zikizozana inafikia pahali pazuri lakini kinachojitokeza hivi sasa ni kwa baadhi ya wana siasa kuanza tabia ya kushawishi wananchi hao kuyakataa yale makubaliano ambayo tayari wameshayapitia na kuyaridhia. 
“ Sisi kama viongozi wa Mkoa na Wilaya tumefikia mwisho wetu kufuatia hatma ya tatizo hilo liloashiria kutaka kuvunjika kwa amani. Kilichobakia hivi sasa ni utekelezaji wa mapendekezo yote yaliyokubaliwa kati ya muwekezaji huyo na Wananchi hao “. Alifafanua Mh. Pembe. 
Akitoa ufafanuzi Mkurugenzi wa Ardhi Nd. January Fusi alisema kwamba ni jukumu la Serikali Kuu wakati wote kulinda mali za Wananchi sambamba na zile za Wawekezaji walioamua kuwekeza Vitega Uchumi vyao Nchini. Nd. Fusi alieleza kwamba Ardhi hivi sasa inaeleweka kuwa ni moja ya cyanzo vikuu vya uchumi wa nchi ambayo hutumiwa katika uwekezaji vitega uchumi mbali mbali ikiwemo sekta ya Utalii inayoonekana kuchukuwa nafasi ya juu katika uchumi wa Dunia. 
Naye  Muwakilishi wa Muwekezaji wa Hoteli ya Kimataifa ya Sea Cliff Bwana Yassir De Costa alisema muwekezaji wa mradi huo bado ana nia safi ya kutaka kusaidia maendeleo ya Wananchi kupitia mradi huo wa Utalii. 
Bwana De Costa alisema mradi wa Hoteli ya Sea Cliff ambao unalenga kujenga uwanja wa Mchezo wa Golf unatarajiwa kutoa fursa kubwa za ajira na kusisitiza kwamba kipaumbele kitawekwa kwa wananchi walio jirani na mradi huo. 
Mwakilishi huyo wa mradi wa Sea Cliff aliiomba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuhakikisha kwamba mradi huo unaohusisha watalii wa daraja la juu Duniani kwa nia ya kusaidia kuongeza mapato ya Nchi na wananchi wake unafanikiwa kwa maslahi ya muwekezaji, Serikali pamoja na Wananchi wa Vijiji jirani. 
Vikao vya pamoja kati ya Uongozi wa Hoteli ya Sea Cliff na Viongozi wa Kamati Nne za Vijiji vya Kiomba Mvua vilikuwa vikifanyika kwa pamoja kupitia muongozo uliotolewa na Kamati ya Baraza la Wawakilishi kuhusu maridhiano ya pande hizo mbili. 
Hivi karibuni Wajumbe wa Kamati hizo Nne walikuwa wakisisitiza ulazima wa kuwepo kwa vikao vya pamoja na muwekezaji huyo ili kujadili mzozo wa ardhi ambayo inatarajiwa kutumika kwa mchezo wa Golf suala ambalo liliridhiwa na muwekezaji huyo na hatimae kufikia makubaliano hayo ambayo wanakamati hao walishindwa kuhitimisha.
 Mzozo kati ya Hoteli ya Sea Cliff na Wananchi wa Kiomba Mvua ulikuwa unahusu matumizi ya bandari, eneo la kuanikia madagaa pamoja na Bara bara masuala ambayo yote yamekubaliwa na muwekezaji huyo. 
Katika muelekeo wa kusaidia maendeleo ya wananchi wa Kiomba Mvua na Maeneo jirani Mradi wa Hoteli ya Sea Cliff umekubali kuwanunulia mashine ya kuanikia dagaa, kusaidia utunzaji wa mazingira ya Mikoko, Gari ya usafiri, Mabanda ya Wavuvi, na vyoo vyake pamoja na ujenzi wa bara bara. 
 Hata hivyo Wananchi hao walipendekeza gharama za ununuzi wa mashine hiyo ielekezwe katika kuwaanzishia miradi mipya itakayowasaidi kuongeza kipato chao na kupunguza ukali wa maisha omabi ambalo limeridhiwa na muwekezaji huyo. Othman Khamis Ame Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif  Ali Iddi akizungumza kwenye Kikao cha Utiaji saini makubaliano maalum kati ya Mradi wa Hoteli ya Sea Cliff na Uongozi wa Kamati Nne za Vijiji vya Kiomba Mvua, Zanzibar.
Hata hivyo Viongozi wa Kamati za Wana Vijiji hao hawakufika kwenye kikao hicho licha ya kushiriki hadi hatua ya mwisho na kuridhia kwa pamoja makubaliano yaliyofikia hatua ya kutiwa saini hiyo.
Kulia ya Balozi Seif ni Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Mh. Pembe Juma Khamis na kushoto yake ni Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini : B” Nd. Khamis Jabir.
 Baadhi ya watendaji wa Taasisi mbali mbali za Serikali walioshiriki vikao vya usuluhishi wa mzozo wa ardhi kati ya Mradi wa SEA Cliff na Wananchi wanaouzunguuka mradi huo.
 Baadhi ya Viongozi wa Mradi wa Hoteli ya Kimataifa walioshiriki vikao vyote vya kutafuta suluhu ya matumizi ya ardhi kati yao na Wananchi wa jirani na Mradi huo. Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.

Maendeleo ya Msiba wa Mama Kagaruki na Safari ya Marehemu Mama Harriette Peace Kagaruki kuelekea Tanzania

$
0
0
 Michango kwa ajili ya kufanikisha shughuli za msiba wa Marehemu Mama Harriette Peace Kagaruki aliyefariki dunia huko Philadelphia tarehe 28 April 2014 imekamilika. Mpaka sasa kiasi cha dolla 20,000 kimepatikana kama ifuatavyo:

·      Watanzania Marekani wametoa dolla 5,300
·      Familia, ndugu na Jamaa wa Tanzania wametoa dolla 11,000
·      Watoto wa Marehemu Erick na Mary Kagaruki wametoa kiasi kilichobakia cha dolla 3,700.
 
Watoto wa Marehemu Erick Kagaruki na Mary Kagaruki na familia nzima ya Marehemu mama Harriette Peace Kagaruki wanapenda kuwashukuru wote mliotoa michango, rambirambi na mliofanikisha kwa namna moja au nyingine shughuli hizi za msiba ziweze kufanikiwa.
 
Shukrani nyingine ziende kwa Watanzania wote na rafiki wa Watanzania waliochangia shughuli za msiba huu hapa Marekani na Tanzania.
 
Mwili wa Marehemu umeshaletwa New Jersey kutoka Philadelphia tayari kupelekwa Tanzania siku ya Jumanne usiku saa tatu kupitia airport ya Newark na British Airways via Entebbe.
 
Mwili utawasili Entebbe Jumatano kabla ya safari ya kuelekea Bukoba kuanza kwa ajili ya shughuli mazishi kuanza.
 
Familia inapenda tena kuwashukuru wote kwa kufanikisha michango na shughuli za sasa za msiba huu. Tunawaomba Watanzania wote tuendelee kushirikiana katika nyakati za shida na raha kama tulivyoshirikiana wakati huu wa msiba.
 
Kwa taarifa zaidi wasiliana na:
Erick Kagaruki – 937-361-4189
Mary Kagaruki – 267-963-8190
Abbas Byabusha – 914-584-7502
   
Kwa niaba ya Familia ya Wafiwa na 
Uongozi wa Jumuiya ya Watanzania,
 
Deogratius Mhella, 
Katibu New York Tanzanian Community.

WAZIRI NYALANDU AKABIDHIWA MAGARI YA KUSAIDIA KAMPENI YA KUTOKOMEZA MAJANGILI WA MAUAJI YA TEMBO

$
0
0
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nayalandu, akisainiana mkataba wa makabidhiano wa magari matatu aina ya Land Cruiser, yenye thamani ya Sh. milioni 350, na Mwenyekiti wa Taasisi ya Uhifadhi Wanyamapori Tanzania, Eric Pasanisi (wa pili kushoto) wakati wa hafla ya makabidhiano hayo iliyofanyika leo kwenye Hoteli ya Hyatt Kilimanjaro wakati wa Kongamano la Kampeni ya kudhibiti Ujangili na kukomesha mauaji dhidi ya Tembo. Kongamano hilo lililofunguliwa na Makamu wa Rais Dkt Bilal, jana limemalizika leo Mei 10, 2014. Kushoto ni Naibu Spika wa Bunge la Jamhri, Job Ndugai (kulia) ni Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mahmoud Mgimwa
 Wakibadilishana nyaraka za mkataba huo baada ya kutiliana saini. Kushoto ni Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri, Job Ndugai
 Baadhi ya washiriki wa Kongamano la Kampeni ya kudhibiti Ujangili na kukomesha mauaji dhidi ya Tembo, wakiwa katika Kongamano hilo, lililomalizika leo kwenye Hoteli ya Hyatt Kilimanjaro, jijini Dar Es salaam.

JK akutana na Rais Jose Eduardo Dos Santos wa Angola jijini Luanda leo

$
0
0
 Rais wa Angola Mhe. Jose Eduardo Dos Santo akimkaribisha Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete katika ikulu ya nchi hiyo jijini Luanda na kufanya naye mazungumzo leo. Rais Kikwete alikuwa nchini Angola kwa ziara ya kikazi ya siku moja
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete  akiwa na mazungumzo na Rais wa Angola Mhe. Jose Eduardo Dos Santo  katika ikulu ya nchi hiyo jijini Luanda leo. .Rais Kikwete alikuwa nchini Angola kwa ziara ya kikazi ya siku moja
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete  akibadilishana mawazo  na Rais wa Angola  Mhe. Jose Eduardo Dos Santo  katika ikulu ya nchi hiyo jijini Luanda wakati akihitimisha  ziara ya kikazi ya siku moja nchini humo.
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete  akiagana na Rais wa Angola  Mhe. Jose Eduardo Dos Santo  katika ikulu ya nchi hiyo jijini Luanda wakati akihitimisha  ziara ya kikazi ya siku moja nchini humo.Picha na Freddy Maro

MAADHIMISHO YA WIKI YA ELIMU MKOANI DODOMA YAFANA SANA LEO

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikabizi kikombe na cheti Naibu Waziri wa Habari Mhe. Juma Nkamiya kutokana na Wizara yake kuweza kufanya vizuri katika kutoa mchango wa kufanikisha maadhimisho ya siku ya Wiki ya Elimu Kitaifa yaliyoadhimishwa leo Mei 10-2014 Mkoani Dodoma.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikabizi zawadi kwa wanafunzi Abi Sambuche wa Shule za Sekondari Lusinde zilizofanya vyema katika mitihani ya mwaka 2013, kwenye maadhimisho ya siku ya Wiki ya Elimu Kitaifa yaliyoadhimishwa leo Mei 10-2014 Mkoani Dodoma.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizindua mpango wa kuboresha Elimu na mpango wa kuwezesha kusoma, kuandika na kuhesabu, kwenye maadhimisho ya siku ya wiki ya Elimu kitaifa mwaka 2013, yaliyoadhimishwa leo Mei 10-2014 Mkoani Dodoma.

JK ATETA NA AKINA SAMATTA NA ULIMWENGU KINSHASA

$
0
0
Rais Kikwete akiwa na Mbwana Samatta kulia na Thoams  Ulimwengu kushoto mjini Kinshasa leo

RAIS wa Jamhuri ya Muungano Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete leo amewatembelea washambuliaji wawili Watanzania wanaocheza TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Mbwana Ally Samatta na Thomas Emannuel Ulimwengu.
Tovuti ya TPM imeandika kwamba Rais Kikwete aliwatembelea wachezaji hao leo mjini Kinshasa ambako wapo na timu yao kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu ya DRC dhidi ya mahasimu wao katika mbio za ubingwa AS Vita.
Rais Kikwete aliye ziarani DRC, alikuwa ameambatana na maofisa wawili wa Ubalozi wa Tanzania majira ya Saa 6:15 mchana alipokutana na wachezaji hao pamoja na Mwenyekiti wa klabu yao, Moses Katumbi.
Rais Kikwete alikuwa  Kinshasa  kwa ziara maalum ya Siku mbili  juu ya ushirikiano wa DRC na Tanzania, ambako alikutana na Rais  Joseph Kabila.
Kikwete alitumia robo saa kuzungumza na akina Samatta katika hoteli ya Congo River, ambako wameweka kambi kwa ajili ya mechi ya kukata na shoka kesho.
Rais Kikwete aliwakumbusha Samatta na Ulimwengu kwamba, Watanzania wanajivunia kuwaona wakiwa na jezi za TPM na kwamba wao ni tegemeo la timu ya taifa, Taifa Stars kwa sasa.
CREDIT:BIN ZUBEIRY

KITUO CHA DALADALA SINZA MAKABURINI

$
0
0
Hini ni moja ya kibanda kati ya vibanda vingi vinavyotumika kupimzikia abiria wa usafiri wa daladala pindi wasubiriapo usafiri huo kwenye maeneo mbali mbali ya vituo vya daladala hapa jijini Dar.lakini tofauti na maeneo mengine,kituo hiki ambacho kipo pale Sinza Makaburi,kimeondolea sehemu husika na kuwekwa juu ya mtaro wa maji katika eneo hilo kama Kamera ya Globu ya Jamii ilivyoweza kukinasa.

KATIBU MKUU WA CCM,NDUGU KINANA AKAGUA MIRADI MBALIMBALI YA MAENDELEO NA KUFANYA MKUTANO MKUBWA WA HADHARA WILAYANI NZEGA LEO

$
0
0
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akimpongeza Mjumbe wa Mkutano mkuu wa CCM,Taifa,Ndugu Hussein Bashe mara baada ya kukabidhi piki piki kwa viongozi wa kata na UWT wilaya
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akimpongeza Mbunge wa Nzega,Mh.Hamisi Kingwangalla mara baada ya kukabidhi mashine ya kutotolea vifaranga kwa kikundi cha vijana.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiwahubia baadhi ya Wananchana na wafuasi wa chama cha CCM,katika mkutano wa hadhara wa chama hicho uliofanyika Nzega mjini mapema leo.
Sehemu ya Wananchama na wafuasi wa chama cha CCM,wakimsikiliza Katibu MKuu wa CCM,Ndugu Kinana (hayupo pichani) akizungumza kwenye mkutano wa hadhara wa chama hicho uliofanyika Nzega mjini mapema leo.
Nape Nnauye akiwahubia Sehemu ya Wananchana na wafuasi wa chama cha CCM,katika mkutano wa hadhara wa chama hicho uliofanyika Nzega mjini mapema leo.
Baadhi ya Baiskeli zilizotolewa na Mjumbe wa Mkutano Halmashauri kuu CCM Taifa,Ndugu Hussein Bashe kwa ajili ya kuwakabidhi viongozi wa mbalimbali wa chama hicho katika suala zima la kurahisha utendaji wao wa kazi.   

OFISI YA TAIFA YA TAKWIMU YAENDELEA NA UANDISHI WA RIPOTI ZA KINA ZINAZOTOKANA NA SENSA YA WATU NA MAKAZI YA MWAKA 2012

$
0
0
Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa akifungua kikao cha kupitia taarifa ya Uandishi wa Ripoti za Kina (Thematic reports) zinazotokana na Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012 kutoka kwa watalaam mbalimbali wa Wizara, Idara na Taasisi za Serikali kilichofanyika leo katika Hotel ya Peacock Jijini Dar es Salaam.
Mshauri mtaalam wa Sensa ya Watu na Makazi Bw. Collins Opiyo kutoka Shirika la Kimataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu Duniani akitoa ushauri wakati wa kikao cha kupitia taarifa ya ripoti hizo kilichofanyika leo katika hoteli ya Peacock jijini Dar es Salaam.
Wataalam wanaoandika Ripoti za Kina (Thematic reports) kutoka Wizara, Idara na Taasisi mbalimbali za Serikali wakimsikiliza kwa makini Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa (hayupo pichani) wakati wa kikao cha kupitia taarifa ya ripoti hizo kilichofanyika leo katika hoteli ya Peacock jijini Dar es Salaam. (PICHA ZOTE NA VERONICA KAZIMOTO)

Rais Kikwete atembelea kiwanda cha saruji kikubwa zaidi duniani

$
0
0
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na mfanyabiashara na mwekezaji maarufu wa Nigeria Alhaj Aliko Dangote katika uwanja wa ndege wa kiwanda chake cha saruji cha Dangote Cement Obajan Plant kilichoko kilomita 400 Kaskazini Mashariki mwa Lagos alipotembela May 9, 2014. Kushoto ni Balozi wa Nigeria nchini Tanzania Mhe. Dkt. Ishaya Samaila Majanbu
Rais Dkt Jakaya Mrisho kikwete akipata maelezo toka kwa mfanyabiashara na mwekezaji maarufu wa Nigeria Alhaj Aliko Dangote wakati akizungushwa kuangalia kiwanda cha saruji cha Dangote Cement Obajan Plant kilichoko kilomita 400 Kaskazini Mashariki mwa Lagos alipotembela May 9, 2014.
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akitembezwa kwenye machimbo ya kiwanda cha saruji cha Dangote Cement Obajan Plant kilichoko kilomita 400 Kaskazini Mashariki mwa Lagos alipotembela May 9, 2014.

KINANA AWAKUTANISHA WATANI WA JADI HAMIS KIGWANGALAH NA HUSSEIN BASHE WILAYANI NZEGA

$
0
0
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (kulia) akisalimiana na wananchi wa katika mkutano wa hadhara wa CCM katika Kata ya Ndala, wilayani Nzega, Tabora leo, wakati wa ziara ya kuimarisha uhai wa chama, kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya CCM na kukagua maandalizi ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa pamoja na kusikiliza kero za Wananchi.


Mbunge wa Jimbo la Nzega Hamis Kigwangalah (kushoto), akimpongeza Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa, Hussein Bashe aliyetoa mchango wa sh. 50,000 za kusaidia ujenzi wa jengo la CCM tawi la Puge, wilayani Nzega leo.


Wakazi wa Kata ya Ndala, wilayani Nzega. wakishangilia kwa kuonesha ishara ya CCM wakati wa mkutano wa hadhara katika kata hiyo, uliohutubiwa na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana leo.




Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye (kushoto) akijadiliana jambo na Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa, Hussein Bashe  walipokutana wakati wa ziara ya Katibu Mkuu wa CCM wilayani Nzega.


Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana 9kulia) akisaidiwa na Mbunge wa Jimbo la Nzega, Hamis Kigwangalah kujenga jengo la Hospitali ya Wilaya ya Nzega.





Kinana akisalimiana na wasanii wa ngoma ya asili  waliotumbuiza wakati wa ujenzi wa jengo la ofisi ya CCM Kata ya Nkiniziwa


Kinana akizungumza baada ya kukagua maabara  katika Shule ya Sekondari ya Kampala, katika Kata ya Ndala, wilayani Nzega, Tabora. Kutoka kushoto ni Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa, Hussein Bashe na Mbunge wa Jimbo la Nzega.

KHAKI FOUNDATION WITH LAURIAN THE BIG PILLOW

$
0
0
With salams and jambo from IZAAS,
  To watch part one of this program open the attachment and click the link East African Countries will watch live the part 2 of this program at Chanel 10 today Sunday 11/5/2014 at 6:30pm God Bless IZAAS, and all the sponsors. 
 Mubaarak Abdullah

JWTZ lashiriki Mkutano wa Baraza la Michezo la Kimataifa (General Assembly and Congress of the International Military Sports Council - CISM)

$
0
0
Na Luteni Kanali Juma Sipe 
(PA, Marekani). 
 Jeshi la Wananchi (JWTZ) limeshiriki Mkutano wa Baraza la Michezo la Kimataifa (General Assembly and Congress of the International Military Sports Council -CISM) uliofanyika Mjini Quito, Equado America ya Kusini kuanzia tarehe 05-09 Mei, 2014.
 Mkutano huo ulijadili na kuendelea kusikilizana ushiriki wa majeshi katika Michezo ya Kimataifa chini ya Kaulimbiu ya Baraza hilo isemayo Urafiki kupitia Michezo (Friendship through sports), msisitizo ukiwa katika kutumia michezo kama chombo cha kueneza amani na utulivu kati ya mataifa duniani. 
Badala ya kukutana na kushirikiana katika maeneo ya vita na migogoro, majeshi yakutane katika michezo na kujenga uelewano na mashirikiano yatakayopunguza uwezekano wa kuingia katika vita kama njia ya kutatua migogoro. 
 Moja ya mambo yaliyojitokeza katika mkutano huo ni pamoja na ushiriki mdogo wa nchi za Afrika ikilinganishwa na mabara mengine, uliodaiwa kutokana na kukosekana fedha, mwamko mdogo wa viongozi wa majeshi ya nchi husika na kutoona umuhimu wa kujenga mahusiano kupitia michezo. Aidha, Mkutano ulimchagua pia Rais mpya wa Baraza hilo, Kanali Abdul Hakeem kutoka Bahrain na Kanali Dorah Mumby (Guinea) kuwa Katibu Mkuu wa kwanza kutoka Afrika. 
 Ushiriki wa Tanzania na utekelezaji wa maazimio ya CISM umekuwa wa mfano kwa miaka kadha sasa. Kwa mfano, katika mkutano wake wa mwaka 2008 uliofanyika Paramaribo, Suriname, Meja Joseph Bakari (sasa Luteni Kanali) alitunukiwa na Bodi ya Wakurugenzi ya Baraza hilo Nishani iitwayo ‘Order of Grand Knight’ kwa mchango wake uliopelekea kuanzishwa kwa “Twalipo Youth Sports Foundation” (twalipo soccera cademy.blogspot. com) nchini Tanzania. 
 Katika mkutano huo jumla ya wanachama 76 walihudhuria kati ya wanachama 104 wa Baraza hilo. Tanzania iliwakilishwa na Kanali Martin Busungu, Mkurugenzi wa Utimamu wa Mwili, Michezo na Utamaduni kutoka Makao Makuu ya Jeshi na Luteni Kanali Joseph Bakari, Afisa mnadhimu kutoka Kurugenzi hiyo.
 Mkutano huo wa mwaka hutanguliwa na mikutano ya kimabara (Afrika, Ulaya, Asia na Amerika) ambako masuala ya michezo ya Majeshi yanayogusa mabara husika hujadiliwa. 
 Kutoka ukanda wa Afrika Mashariki na Jumuiya ya Maendeleo  Kusini mwa Afrika  nchi zilizoshiriki ni pamoja na Kenya, Uganda na Zambia. 
 Kwa uelewa zaidi tafadhali tembelea wavuti www.cismmilsport.org











 Ujumbe wa Tanzania Kanali Martin Busungu (kushoto) na  Luteni Kanali Joseph Bakari wakati wa mkutano.
 Kanali Busungu akipiga kura wakati wa uchaguzi wa viongozi wapya ya Baraza.

 Luteni Kanali Bakari akichangia mada wakati wa Mkutano.
 Kanali Busungu akiteta jambo na Mkuu wa Ujumbe wa Kenya, Brigedia Jenerali Lipakio wakati wa mapumziko.
  Meja Bakari (sasa Luteni Kanali) wakati akitunukiwa nishani mwaka 2008.
Ujumbe wa Tanzania ukiinua bendera juu kuashiria uwepo wao mkutanoni.

ngoma azipendazo ankal

$
0
0
Sipho Hotstix Mabuse  anaimba "Zanzibar"
Viewing all 109996 articles
Browse latest View live




Latest Images