Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109597 articles
Browse latest View live

Kali TV: This week's Around Town


President Kikwete has sent a congratulatory message to H.E. Vladimir Putin, President of the Russian Federation on the occasion of the National Day of Russia

0
0
H.E. Jakaya Mrisho Kikwete, President of the United Republic of Tanzania has sent a congratulatory message to H.E. Vladimir Putin, President of the Russian Federation on the occasion of the National Day of Russia –Victory Day, on 9th May 2014. The message reads as follows:

“H.E. Vladimir Putin, 
President of the Russian Federation,  
Moscow
RUSSIA

Your Excellency and Dear Colleague,

On the occasion of the celebration of your country’s National Day, I would like to convey to you and through you to the Government and people of Russia my most heartfelt congratulations.

Tanzania cherishes the good relations and co-operation that happily exist between our two countries. On this historic day, I take this opportunity to reaffirm my country’s commitment and desire to continue working with you and your Government in strengthening further the existing ties of friendship and co-operation for the mutual benefit of our two countries and peoples.

Please accept, Your Excellency, my best wishes for your continued good health and prosperity for the people of Russia”.

Issued by the Ministry of Foreign Affairs and International Cooperation, 
Dar es Salaam

08th May 2014

Maendeleo ya Msiba New York na Philadelphia

0
0

 
Michango kwa ajili ya kufanikisha shughuli za msiba wa Marehemu Mama Harriette Peace Kagaruki aliyefariki dunia huko Philadelphia tarehe 28 April 2014 bado inaendelea. Mpaka sasa kiasi cha dolla 8,800 zimeshapatikana. Lengo ni kuchangisha dolla 20,000 ili kufanikisha shughuli za msiba huu uliotokea tarehe 28 April 2014.
 
Tunawaomba tuzidi kuchanga ili tuweze kufikia kiasi kinachohitajika na ili tuweze kufanikisha shughuli za kuurudisha mwili wa Marehemu Tanzania. Ukipata taarifa hizi tunaomba umfahamishe mwenzako. Tafadhali, toeni michango kupitia Account Number ifuatayo:
 
Wells Fargo Bank
Routing #: 031000503
Account# 6595913119
 
Jina la mwenye akaunti ni la Mtoto wa Marehemu: Mary Kagaruki
 
Marehemu kwa sasa yuko:
Funeral Home
366 West Lancaster Avenue
Wayne PA 19087
 
Kwa taarifa zaidi za msiba huu wasiliana na:
Erick Kagaruki – 937-361-4189
Mary Kagaruki – 267-963-8190
Abbas Byabusha – 914-584-7502
Doris Rweyemamu – 646-379-9135
  
Dr. Temba  (347-489-6532) na Raphael Faida (347-869-2230) nao watakuwa wakikusanya michango kutoka kwa Wanajumuiya.
 
Tunawaomba Watanzania wote wa Marekani watusaidie kwa kutoa michango ili tufanikishe shughuli za msiba huu.
 
Kwa niaba ya Familia ya Wafiwa na Uongozi wa Jumuiya ya Watanzania,
 
Deogratius Mhella, Katibu New York Tanzanian Community.

PRESIDENT KIKWETE AT THE WORLD ECONOMIC FORUM ON AFRICA IN ABUJA

0
0
President Jakaya Mrisho Kikwete of Tanzania talks during a Leadership Council Meeting (Grow Africa Investment Forum) during the three-day World Economic Forum on Africa in Abuja, Nigeria, May 8, 2014

RATIBA YA JINSI WIZARA ZITAKAVYOWASILISHA BAJETI ZAO KWENYE MKUTANO WA KUMI NA TANO WA BUNGE UTAKAOANZA TAREHE 6 MEI, 2014 HADI 27 JUNI, 2014 KWA BAJETI YA MWAKA 2014/2015

TANZANIA YAONGOZA MJADALA WA WAZI (OPEN SESSION) WA BARAZA LA AMANI NA USALAMA LA UMOJA WA AFRIKA KUHUSU WATOTO NA VITA BARANI AFRIKA (CHILDREN AND ARMED CONFLICTS IN AFRICA) JIJINI ADDIS ABABA

0
0
 Mhe. Naimi Aziz, Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia na Mwakilishi wa kudumu  katika Umoja wa Afrika (katikati), akiongoza mjadala huo ambao ulihudhuriwa pia na Bibi. Leila Zerrougui ( wa tatu kushoto), Mwakilishi Maalamu ( Special Representative) wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya watoto na Vita, na Balozi Smail Chergui (wa nne kushoto), Kamishina wa Amani na Usalama wa Umoja wa Afrika. Aliopo nyuma ya Mhe. Balozi Naimi Aziz, ni Bi. Suma Mwakyusa, Afisa Ubalozi Mwandamizi.
 Bw. Samwel Shelukindo, Afisa Ubalozi Mkuu, akitoa mchango wa Tanzania katika mjadala huo, ambao pamoja na mambo mengine, Tanzania ilisisitiza umuhimu wa kuingozea nguvu (mandate) mahakama ya Afrika inayoshughulia masuala ya haki za binadamu ( African Court on Justice and Human Rights) ili iweze kuwashughulikia watu wanaotenda uhalifu dhidi ubinadamu katika vita ikiwemo kuwatumua watoto vitani. Aliopo nyuma ya Bw. Shelukindo ni Bw. Nsavike Ndatta, Afisa Ubalozi Mkuu akifuatilia mjadala huo.
Baadhi ya washiriki wakifuatilia kwa makini mjadala huo.

KATIBU MKUU WA CCM,NDUGU KINANA AWASILI WILAYANI IGUNGA MKOANI TABORA JIONI LEO,KUANZA ZIARA YA SIKU 10 MKOANI HUMO.

0
0
 Pichani Kulia ni  Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Tabora,Ndugu Hassani Wakasubi akimpokea mgeni wake,Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana na Ujumbe wake alipowasili jioni ya leo katika kijiji cha Makomelo wilayani Igunga mkoani Tabora kwa ziara ya siku 10,ya Kuimarisha uhai wa chama,kukagua miradi  ya Maendeleo inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya CCM,Kukagua maandalizi ya uchaguzi za serikali za mitaa pamoja na kusikiliza kero za Wananchi. 
 Mkuu wa Mkoa wa Tabora,Mh.Fatma Mwasa akisalimiana na Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana mara baada ya kuwasili kijiji cha Makomelo Wilayani Igunga mkoani humo tayari kwa kuanza ziara ya siku 10 ya Kuimarisha uhai wa chama,kukagua miradi  ya Maendeleo inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya CCM,Kukagua maandalizi ya uchaguzi za serikali za mitaa pamoja na kusikiliza kero za Wananchi.


 Ndugu Kinana akisalimiana na Wananchi mbalimbali waliofika kumpokea mara baada ya kuwasili katika kijiji cha Makomelo mapema leo jioni.

 Ndugu Kinana akisalimiana na Viongozi wa chama serikali pamoja na Wananchi mbalimbali waliofika kumpokea mara baada ya kuwasili katika kijiji cha Makomelo mapema leo jioni,Wilayani Igunga mkoani Tabora,kulia ni Katibu wa NEC-Itikadi na Uenezi CCM Taifa,Nape Nnauye
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akitazama ngoma ya kiasili iliondaliwa wilayani Igunga wakati wa mapokezi ya Ndugu Kinana, ambaye ameambatana na Katibu wa NEC-Itikadi na Uenezi CCM Taifa,Nape Nnauye na viongozi mbalimbali wa chama hicho,mara baada ku kuwasili kijiji cha Makomelo Wilayani hummo jioni ya leo.
 Ndugu Kinana akipokelewa na vijana wa Green Gard tayari kwa kuvalishwa skafu na kukaribishwa wilayani humo.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora,Mh.Fatma Mwasa akiwa sambamba na viongozi mbalimbali wa CCM Wilaya na Mkoa wakisubiri kumpokea Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana katika kijiji cha Makomelo Wilayani Igunga mkoani humo tayari kwa kuanza ziara ya siku 10 ya Kuimarisha uhai wa chama,kukagua miradi  ya Maendeleo inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya CCM,Kukagua maandalizi ya uchaguzi za serikali za mitaa pamoja na kusikiliza kero za Wananchi.
  Baadhi ya wananchi mbalimbali waliojitokeza kumpokea Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana na Ujumbe wake alipowasili jioni ya leo Wilayani Igunga mkoani Tabora.

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LEO “PRESS RELEASE”TAREHE 09.05.2014.


THE MBONI SHOW SASA KUANZA KUONEKANA KWENYE DSTV

SHINDANO LA TANZANIA MOVIE TALENTS LAKONGA NYOYO ZA WAKAZI WA KANDA YA KUSINI, MAMIA WAJITOKEZA KUSHIRIKI

0
0
Kundi la Kwanza la Washiriki wa Kanda ya Kusini wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kupewa semina elekezi juu ya maswala mbalimbali kuhusiana na filamu na maisha kwa ujumla wakati walipofika katika ukumbi wa safari lounge kwaajili ya kushiriki kwenye shindano la Tanzania Movie Talents linaloendelea kufanyika Mjini Mtwara leo.
Baadhi ya washiriki kutoka Kanda ya Kusini wakiwa wamejitokeza katika usaili wa Kushiriki shindano la Tanzania Movie Talent katika Ukumbi wa Safari lounge uliopo Eneo la Maduka Makubwa, Mtwara Mjini wakiwa kwenye foleni tayari kwa shindano kuanza.
Baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya Proin Promotions wakiwabandika washiriki namba za ushiriki katika Shindano la Tanzania Movie Talents linaloendelea kufanyika katika Kanda ya Kusini, Mkoani Mtwara leo.
Washiriki wa shindano la Tanzania Movie Talents wakisubiri kuingia kwa majaji kwaajili ya kuanza kuonyesha Vipaji vyao vya kuigiza katika shindano la Kusaka Vipaji vya Kuigiza la Tanzania Movie Talents linaloendelea kufanyika Kanda ya Kusini Mkoani Mtwara.

TAARIFA KUTOKA SHIRIKISHO LA SOKA NCHINI (TFF) LEO

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUNGUA KONGAMANO LA SIKU MBILI LA KUDHIBITI UJANGILI NA KUTOKOMEZA MAUAJI DHIDI YA TEMBO

0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, asalimiana na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri, Job Ndugai, wakati alipowasili kwenye viwanja vya Hoteli ya Hyat Kilimanjaro, jijini Dar es Salaam leo Mei 9, 2014 kwa ajili ya kufungua Kongamano la siku mbili la Kampeni ya kudhibiti Ujangili na kukomesha mauaji dhidi ya Tembo. Kongamano hilo linatarajia kumalizika kesho.

Makamu Wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati akifungua rasmi Kongamano la siku mbili la Kampeni ya kudhibiti Ujangili na kukomesha mauaji dhidi ya Tembo. Kongamano hilo lililofunguliwa leo Mei 9, 2014, linatarajia kumalizika kesho kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Hyat Kilimanjaro, jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, akizungumza wakati wa Kongamano hilo.

Baadhi ya washiriki wa Kongamano hilo, wakimsikiliza Makamu wa Rais Dkt. Bilal, wakati akihutubia kufungua rasmi Kongamano hilo, leo kwenye Hoteli ya Hyat Kilimanjaro jijini Dar es Salaam.

KUTOKA BUNGENI MJINI DODOMA LEO

0
0
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akijibu maswali ya wabunge wakati alipohitimisha hoja ya Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu, bungeni mjini Dodoma Mei 9, 2014.
Spika wa Bunge Mhe.Anna Makinda akiwa anaendesha kikao cha Bunge leo wakati wa majadiliano ya mapato na matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu na TAMISEMI.
Wabunge wakifuatilia mjadala ndani ya Bunge.
Spika wa zamani ambaye pia ni Waziri wa Ushirikiano wa Africa Mashariki Mhe.Samweli Sitta kushoto akijadiliana jambo na Spika wa Bunge Mhe.Anna Makinda Mara baada ya Bunge kuahirishwa hadi jioni leo. 
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akipongezwa na Mkewe Tunu baada ya Bunge kupitisha bajeti ya Ofisi yake mjini Dodoma Mei 9, 2014. Kushoto ni Mbunge wa Viti Maalum, Pudenciana Kikwembe na watatu kushoto ni mbunge wa Temeke, Abas Mtemvu.
Waziri Mkluu, Mizengo Pinda akipongezwa na katibu Mkuu katika Ofisi ya Waziri Mkuu, Florens Turuka baada ya bunge kupitisha bajeti ya Ofisi yake mjini Dodoma Mei 9,2014. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI YATARAJIA KUTUMIA SHILINGI BILIONI 955.934 KATIKA MWAKA WA FEDHA 2014/2015

0
0
Waziri wa Mambo ya Ndani yaNchi, Mathias Chikawe akizungumza na wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa wizara hiyo katika Kikao cha Pili cha Baraza hilo kilichofanyika Giraffe Hotel jijini Dar es Salaam leo. Katika kikao hicho, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi imependekeza kutumia Shilingi Bilioni 955.934 katika Mwaka wa Fedha 2014/2015. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Sehemu ya wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi wakimsikiliza kwa makini mgeni rasmi, Waziri wa wizara hiyo, Mathias Chikawe (hayupo pichani) wakati alipokuwa anatoa hotuba ya kufungua mkutano wa wafanyakazi wa siku moja unaofanyika katika Hoteli ya Giraffe jijini Dar es Salaam. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (wapili kulia), Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Mbarak Abdulwakil (wapili kushoto), Naibu Katibu Mkuu, Mwamini Malemi (kulia) na Katibu Msaidizi wa Baraza la Wafanyakazi wa wizara hiyo, JenithaNdone wakiimba nyimbo ya mshikamo daima katika Kikao cha Baraza la Wfanyakazi wa wizara hiyo kilichofanyika katika Hoteli ya Giraffe jijini Dar es Salaam leo. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe akimkabidhi Staford Busumbiro (kushoto) Shiingi milioni Mbili kwa niaba ya Haidhuru Kita kwa kuchaguliwa kuwa mfanyakazi bora wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi katika mwaka 2014. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Mwamini Malemi na Kulia kwa Waziri ni Katibu Mkuu, Mbarak Abdulwakil na Jenitha Ndone, Katibu Msaidizi wa Baraza la Wafanyakazi Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Mkurugenzi wa Sera na Mipango, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Haji Janabi akiwasilisha makadirio ya bajeti ya Wizara hiyo kwa mwaka 2014/15 kwa Wajumbe wa wizara hiyo katika Kikao cha Baraza la Wafanyakazi kilichofanyika katika Hoteli ya Giraffe, jijini Dar es Salaam. Katika Mwaka wa Fedha wa 2014/2015 wizara hiyo inatarajia kutumia Shilingi Bilioni 955.934. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (watatu kulia-waliokaa). Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil (wapili kushoto waliokaa), Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Mwamini Malemi (wapili kulia waliokaa) wakiwa katika picha ya pamoja na wakuu wa idara wa wizara hiyo na wajumbe wa Baraza la wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi baada ya kufunguliwa Kikao cha siku moja cha Baraza hilo kilichofanyika katika Hoteli ya Giraffe, jijini Dar es Salaam leo. Picha zote na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

MAADHIMISHO YA SIKU YA NDEGE WAHAMAO DUNIANI KUFANYIKA TAREHE 10 – 11 MEI 2014


Documentary: Persians of Zanzibar

IGP AFUNGUA MAFUNZO YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA

0
0
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Ernest Mangu akiongozana na Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Nchini DCI Issaya Mngulu wakati alipokuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa Mafunzo ya Haki za binadamu na Utawala bora yaliyokuwa yakiwashirikisha Wakuu wa Upelelezi wa Mikoa, Wilaya na Waendesha Mashtaka wa Sertikali, Mjini Dodoma jana
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Ernest Mangu akizungumza na Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Nchini DCI Issaya Mngulu kabla ya kufungua Mafunzo ya Haki za binadamu na Utawala bora yaliyokuwa yakiwashirikisha Wakuu wa Upelelezi wa Mikoa, Wilaya na Waendesha Mashtaka wa Serikali, Mjini Dodoma jana.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Ernest Mangu akizungumza na Mratibu wa Maboresho ya Jeshi la Polisi Lucas Kusima, kabla ya kufungua Mafunzo ya Haki za binadamu na Utawala bora yaliyokuwa yakiwashirikisha Wakuu wa Upelelezi wa Mikoa, Wilaya na Waendesha Mashtaka wa Serikali, Mjini Dodoma jana. kushoton ni Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Nchini DCI Issaya Mngulu.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Ernest Mangu pamoja Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Nchini DCI Issaya Mngulu na Mkurugenzi Msaidizi kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini (DPP) Bi. Neema Ringo, wakiimba wimbo wa Maadili wa Jeshi la Polisi wakati wa ufunguzi wa Mafunzo ya Haki za binadamu na Utawala bora yaliyokuwa yakiwashirikisha Wakuu wa Upelelezi wa Mikoa, Wilaya na Waendesha Mashtaka wa Serikali, Mjini Dodoma jana.(Picha na Frank Geofray wa Jeshi la Polisi)

BENKI YA CRDB KUUZA HISA ZAKE KATIKA SOKO LA HISA LA NAIROBI

0
0
Benki ya CRDB inatarajia kuuza Hisa zake katika Soko la Hisa la Nairobi, fursa ambayo itatoa wigo mpana zaidi wa biashara ya hisa za Benki hiyo katika soko la Afrika Mashariki.

Hayo yalisemwa leo na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Dk. Charles Kimei wakati wa siku ya kwanza ya mkutano mkuu wa wanachama wote unaofanyika hapa jijini Arusha.

Kimei alisema uuzaji wa hisa katika Soko la Hisa la Nairobi utafanya bei ya hisa za benki ya CRDB kupanda kutokana na ukweli kwamba katika soko la Dar es Salaam bei ya hisa zote ipo chini sana.

Mfano kama ingeweza kufanyika mahesabu ya kitaalam, bei halisi ya hisa ya CRDB  ingetakiwa iwe zaidi ya shilingi 500 badala ya 310 ya sasa. Na kitendo cha kuuza hisa kwenye soko la Nairobi ina maana wafanyabiashara wengi watavutiwa na wataweza kununua na kuuza hisa hizo.

Pia ikizingatiwa ukweli kuwa sehemu kubwa ya wanahisa wa Benki ya CRDB ni wanahisa mmoja mmoja ambao huuza na kununua hisa zao kutokana na hali ya maisha inayowakabili kwa wakati Fulani.
 Kumbe kwa kuingia kwenye Soko la Nairobi ina maana kutakuwa na mchanganyiko na wafanyabiashara wakubwa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akifungua semina ya Wanahisa wa Benki ya CRDB iliyofanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa AICC jijini Arusha jana. Kulia ni Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, anayeshughulika na Uendeshaji na Huduma kwa Wateja, Saugata Bandyadhiyay na Naibu Mkurugenzi Mtendaji Huduma Shirikishi wa Benki ya CRDB, Esther Kitoka. (Na Mpiga Picha Wetu)
 Washiriki wa semina ya Wanahisa wa Benki ya CRDB wakiwa katika Semina hiyo.
 Washiriki wa semina ya Wanahisa wa Benki ya CRDB wakiwa katika Semina hiyo.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

News Alert:WANAFUNZI 212 WA UASKARI CHUO CHA TAALUMA YA POLISI MOSHI WAFUKUZWA BAADA YA KUBAINIKA KUTUMIA VYETI FEKI

0
0
Na Dixon Busagaga wa globu ya jamii kanda ya kaskazini.


CHUO cha mafunzo ya taaluma ya Jeshi la polisi Moshi (MPA), kimewafukuzisha mafunzo jumla ya wanafunzi wa uaskari 212, kutokana na sababu za kughushi vyeti vya elimu ya sekondari..

Hayo yamesemwa leo na Mkuu wa Taaluma na Utumishi wa jeshi la Polisi, Kamishna wa Polisi Thobias Andengenye katika kikao na waandishi wa habari kilichofanyika kwenye ukumbi wa chuo cha mafunzo ya taluma ya Polisi mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro.

Kamishna Andengenye alisema Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA), lilifanya uhakiki wa Vyeti vya wanafunzi wote 3,415 waliojiunga na mafunzo hayo Desemba mwaka jana ambapo waligundua kuwa wanafunzi 212 kati yao hawakuwa na sifa kutokana na
sababu za kughushi vyeti.

"Katika kuhakikisha kwamba tunaendelea kuwa na askari wenye ueledi na uaminifu kwa raia na taifa kwa ujumla, tuliendelea na zoezi la kuhakiki vyeti kwa kushirikiana na baraza la mitihani la taifa, ambapo
vyeti vya wanafunzi wa uaskari 212 kati ya walioripoti vimeonekana kuwa ni vya kughushi," alisema Andengenye.

Alisema kufuatia hali hiyo pamoja na kuwaachisha mafunzo wanafunzi hao 212, Jeshi la Polisi nchini kwa kushirikiana na taasisi nyingine linaendelea kufanya upelelezi ili kuhakikisha kuwa hatua za kisheria



zinachukuliwa dhidi ya wanafunzi hao na maaskari wote watakaobanika kughushi vyeti.

BASI LA DAR EXPRESS LAPATA AJALI ENEO LA WAMI

0
0

Bari mali ya kampuni ya Dar Express iliyokua ikitokea jijini Dar na kuelekea Jijini Nairobi,Nchini Kenya limepata ajali mapema leo asubuhi katika eneo la kijiji cha jirani na Mto Wami.Chanzo cha ajali hiyo hakijajulikana. Abiria wengi wamenusurika na kufanikiwa kutoka,japo kuna wachache ambao wamejeruhiwa.

Viewing all 109597 articles
Browse latest View live




Latest Images