Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 42 | 43 | (Page 44) | 45 | 46 | .... | 3272 | newer

  0 0


   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein,akiwa katika picha baada ya kumkabidhi kitambulisho cha Taifa, Msanii Isha Mashauzi,(msanii) akiwa miongoni mwa wananchi kutoka Tanzania Bara waliopewa vitambulisho vyao katika hafla ya utoaji wa Vitambulisho vya Taifa,kwa mara ya kwanza kwa Upande wa Zanzibar,hafla iliyofanyika katika viwanja vya Baraza la Wawakilishi Chukwani Nje ya Mji wa Zanzibar. 
  Picha na Ramadhan Othman,Ikulu, Zanzibar

  0 0

  Kundi la wake za watu walikuwa kwenye semina kuhusu namna ya kuishi kwa upendo katika ndoa. Muwezeshaji akauliza, wangapi wanawapenda waume zao? Wote wakanyoosha mikono. Akauliza tena, ‘Mara ya mwisho umemwambia mumeo nakupenda lini?. Majibu mbalimbali yalitolewa, Wengine wakisema Leo, wengine Jana, wengine hawakumbuki. Kisha akawaambia, kila mtu achukue simu yake halafu amtumie mumewe text yenye maneno. NAKUPENDA MPENZI, kisha wabadilishane simu. Wakaambiwa kila moja asome majibu kwenye simu aliyoshika, majibu yalikuwa kama ifuatavyo;

   
  Simu 1- Samahani nani mwenzangu?
   
  Simu  2- He Mama Joji unaumwa?
   
  Simu 3- Nami pia daima
   
  Simu 4- Nini tena umeshagonga gari?
   
  Simu 5- Sijakuelewa una maana gani
   
  Simu 7- Umefanya nini tena? Leo sitakusamehe
   
  Simu 8-Chukua taim yako
   
  Simu 9-?!?
   
  Simu  10- Acha kuzunguka unataka shilingi ngapi?
   
  Simu 11 – Hivi naota?
   
  Simu 12 – Kwa kweli leo usiponieleza hii mesej ulikuwa unampelekea nani atakufa mtu leo...kudadaddaddeki....
   
  Simu 13 – Nilishakwambia usirudie kunywa pombe au ntakuacha naona umechoka kuishi na mimi.
   
  Simu 14 -  Umeanza lini ?
   
  Simu  15-  Mambo ya vijana hayo !
   

  0 0

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akitia saini kitabu cha maombolezo ya Askofu Thomas Laizer wa Dayosisi ya Kaskazini Kati la Kanisa la Kiinjili cha Kilutheri Tanzania (KKKT) leo, Alhamisi, kwenye Kanisa Kuu la KKKT mjini Arusha kabla ya kutoa heshima zake za mwisho kwa mwili wa Askofu.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akitoa heshima zake za mwisho kwa mwili wa Askofu Thomas Laizer wa Dayosisi ya Kaskazini Kati la Kanisa la Kiinjili cha Kilutheri Tanzania (KKKT) leo, Alhamisi, kwenye Kanisa Kuu la KKKT mjini Arusha.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akiifariji familia ya Askofu Thomas Laizer wa Dayosisi ya Kaskazini Kati nyumbani kwa Askofu mara baada ya kuwa ametoa heshima zake za mwisho kwa mwili wa marehemu kwenye Kanisa Kuu la KKKT mjini Arusha leo, Alhamisi, Februari 14, 2013. Picha zote na Fredy Maro wa Ikulu

  0 0

  .Kamati ya uchaguzi ya Shirikisho la Vyama Vya Soka Nchini (TFF) Toka kushoto ni wakili  Karuwa, Hamidu Mbwezeleni, mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi Deo Lyato, wakili wa Jamal Malinzi  Audats Kahendaguza, Jamali Malinzi na wakili wa Agape Fue, Peter Heller, ambaye  alimkatia Jamal Malinzi rufaa kwa madai kuwa hana uzoefu wa miaka mitano na pia alipinga mabadiliko ya katiba ya TFF  hapo walikuwa wanasikiliza rufaa ya Malinzi. Kupata yaliyojiri  leo BOFYA HAPA

  0 0

   Afisa bidhaa na huduma wa Vodacom Tanzania Bw.Athanas Muhanuzi(kushoto)akimkabidhi hundi yenye thamani ya shilingi Milioni 1 Bw. Stanley Maliwa,aliejishindia katika  Promosheni ya"MAHELA"inayoendeshwa na kampuni hiyo,katikati ni Meneja Mawasiliano wa kampuni hiyo Bi.Rukia Mtingwa. Zaidi ya shilingi Milioni 400 zinaendelea kushindaniwa.
  Meneja Mawasiliano wa Vodacom Tanzania Bi.Rukia Mtingwa kushoto akimsisitiza jambo Bi.Elizabeth Kavishe(kulia)wakati wa kumkabidhi hundi yenye thamani ya shilingi Milioni 1 aliejishindia katika  Promosheni ya"MAHELA"inayoendeshwa na kampuni hiyo,katikati ni Meneja wa malipo ya baada wa kampuni hiyo Bw.Ibrahim Kiongozi. Zaidi ya shilingi Milioni 400 zinaendelea kushindaniwa.

  0 0
 • 02/14/13--19:00: ngoma azipendazo ankal
 • Pamoja ya mambo yote lakini ngoma ya 'Sea' ya Papii Kocha na baba yake Nguza Viking itaendelea kuwa juu kwa miaka kibao ijayo

  0 0

  Hatimaye basi la Timu ya Taifa, Taifa Stars lililokuwa likisubiriwa kwa hamu sasa limewasili na liko tayari kukabidhiwa na Bia ya Kilimanjaro Premium Lager kwa Shirikisho la Mpira Tanzania (TFF) ili Taifa Stars iweze kulitumia.

  Akizungumza Jijini Dar es Salaam, Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, inayodhamini Taifa Stars, George Kavishe alisema hii ni katika malengo yao ya kuinua hadhi ya timu ya Taifa ambayo kwa sasa imeonesha kiwango cha hali ya juu.

  “Wakati tukichukua udhamini wa timu ya Taifa moja ya malengo yetu ilikuwa ni kuinua hadhi ya timu hii na mojawapo ya vitu tulivyoahidi ni kuinunulia basi la hadhi,” alisema Bw Kavishe.

  Alisema basi hilo aina ya Yutong lenye thamani ya zaidi ya Shilingi milioni 200, ni kubwa na la kisasa kabisa lenye uwezo wa kubeba abiria 50 pamoja na dereva na kuwa lina nafasi kubwa kutoka kiti kimoja hadi kingine hivi kuwafanya wachezaji wakae kwa raha zaidi wanaposafiri.

  “Basi hili ni athletic coach na ni jipya kabisa, limetengenezwa mahususi kwa wanamichezo kwani lina nafasi kubwa chini ya kubeba vifaa vya michezo na mizigo mingine yeye uzito wa hadi tani tatu,” alisema Bw. Kavishe.

  Aliendelea kusema kuwa basi hilo ni imara kwani chasis yake ni 4x2, injini yake ni aina ya 300 HP Cummins, ina retarder ya umeme na breki aina ya ABS, TV mbili za kisasa, muziki wa nguvu wenye spika nane, milango na mabuti ya kisasa, friji mbili na kiyoyozi cha nguvu.

  Kwa mujibu wa Bw. Kavishe basi hili linatarajiwa kukabidhiwa kwa Taifa Stars Februari 21 katika hafla itakayofanyika katika makao makuu ya TBL Ilala Jijini Dar es Salaam na itahudhuriwa na wadau mbalimbali wa soka nchini na wageni wengine.

  Baada ya kukabidhiwa kwa Taifa Stars basi hilo linatarajiwa kuzunguka katika mitaa mbalimbali ya JIji la Dar es Salaam ili wananchi walione na wapige nalo picha za kumbukumbu.

  “Hii ni zawadi ya watanzania kwa timu ya Taifa kwani ndio wanatuwezesha kufanya mambo yote haya…kadri wanavyozidi kutuunga mkono kwa kunywa bia yetu ya Kilimanjaro Premium Lager ndivyo na sisi tunapata fedha za kuidhamini timu yetu ya Taifa,” alisema.  Bia ya Kilimanjaro Premium Lager ilianza kuidhamini Timu ya Taifa tangu mwezi Mei mwaka jana kwa kuwekeza zaidi ya bilioni mbili kwa mwaka kwenye timu hii kwa muda wa miaka mitano.

  Moja ya masuala ambayo yamo kwenye mkataba kati ya TBL na TFF ni ununuzi wa basi mpya ya Taifa Stars jambo ambalo TBL imefanikisha ndani ya mwaka mmoja wa udhamini wake.

  Mpaka sasa TFF imeonyesha kuridhishwa na udhamini mnono wa Kilimanjaro Premium Lager kwani shirikisho hilo lina uwezo wa kufanya mipango ya muda mrefu zaidi kwa uhakika.

  Udhamini wa Kilimanajro Premium Lager ndio mkubwa kabisa ambao TFF imewahi kupokea kutoka kwa kampuni au shirika lolote nchini kudhamini mpira.


  0 0

  Mkuu wa shule ya Mbeya sekondari Mwamwitu Msigwa akimshukuru Josephine Kulwa kwa msaada waliopata toka NMB

  Walimu nao wa Mbeya sekondari hawakuwa nyuma kuja kupokea msaada huo  hapa wakiangalia kompyuta hizo
  Baadhi ya watumishi wa NMB wakiwa makini kusikiliza shukrani zinazotolewa shuleni hapo
  Meneja mawasiliano wa NMB Josephine Kulwa amewataka waalimu na wanafunzi hao kutumia vifaa hivyo kwa malengo yaliokusudiwa na kuvitunza ili na wengine wapate kuvitumia.
  Mwenyekiti wa bodi ya shule ya Mbeya sekondari na pia ni mkurugenzi wa mamlaka ya maji safi na taka Mbeya  Eng. Simon Shauri akionyesha furaha yake wazi kwa wageni toka NMB kwa msaada waliotoa kwa shule yao na ameahidi kuwa kompyuta hizo zitatumika kwa malengo yaliokusudiwa 
  Mkuu wa shule ya Mbeya sekondari Mwamwitu Msigwa pia nae amewashukuru sana NMB kwa msaada waliotoa kwa shule yake
  Huu ndiyo msaada wa kompyuta na printer toka NMB

  Picha na Mbeya yetu

  0 0


  0 0

  1Mkurugenzi wa Bendi ya Kalunde Deo Mwanambilimbi akiimba huku wacheza shoo wa bendi hiyo Kushoto ni Queen Vero na kulia ni Frola Bamboocha wakati wa onesho la Valentine lililofanyika kwenye ukumbi wa Trinit Oysterbay jijini Dar es salaam usiku huu, Katika Onesho hilo pia bendi ya Kalunde imetimiza miaka 7 toka ianzishwa na kusherehekea mwaka wake wa saba wa utendaji wa kazi.
  2Mkurugenzi wa bendi ya Kalunde Deo Mwanambilimbi kushoto Debora Nyangi Meneja wa bendi hiyo pamoja na Mwapwani mwimbaji wa bendi ya Kalunde kwa pamoja wakikata keki kuashiria sherehe za kutimiza miaka saba toka bendi hiyo ianzishwe.
  3Meneja wa Bendi la Kalude Debora Nyangi akimlisha keki Mkurugenzi wa bendi hiyo Deo Mwanambilimbi katika onesho la Valentine na sherehe za utimiza miaka 7 ya kuanzishwa kwa bendi hiyo.
  4
  Mkurugenzi wa bendi hiyo Deo Mwanambilimbi akimlisha keki Meneja wa Bendi la Kalude Debora Nyangi katika onesho la Valentine na sherehe za utimiza miaka 7 ya kuanzishwa kwa bendi hiyo.
   
  5
  6Debora Nyangi akimlisha keki Shekh Mwakichui mwimbaji na mpiga kinanda wa bendi ya hiyo
  7Debora Nyangi akimlisha keki Bon Kamprobo mpiga gitaa la solo maarufu wa bendi hiyo
  8
  Debora Nyangi akimlisha keki Bob Ludala mmoja wa waimbaji maarufu na makini wa bendi ya Kalunde.
  9
  Debora Nyangi akimlisha keki Eric mmoja wa mashabiki na wadau muhimu wa bendi ya Kalunde.
  10
  Mkurugenzi wa bendi ya Kalunde Deo Mwanambilimbi akiwa  na Debora Nyangi ambaye pia ni Meneja wa bendi ya Kalunde na wote ni waanzilishi wa bendi
  11
  Mashabiki wa bendi ya Kalunde wakijimwaga stejini wakati bendi hiyo ikitumbuiza kwenye ukumbi wa Trinit Oysterbay jijini Dar es salaam usiku huu. Picha na John Bukuku


  0 0


  Ndugu Michuzi.

  Kwa niaba yangu binafsi na kanisa zima la Umoja International Outreach hapa Dallas;Ninapenda kuchukua nafasi hii kuwakaribisha wanajumuia wa jiji hili la Dallas- Texas katika sherehe ya uzinduzi wa bus la kanisa siku ya Jumapili tarehe 17/02/2013 saa kumi na mbili jioni.Shuguli ya uzinduzi wa bus hili utafanyika katika viwanja vya kanisa la Umoja  hapa Dallas na kuhudhuriwa na watu mbali mbali.Shughuli hii itafuatiwa na chakula cha jioni ambapo tutapata muda wa kubadilishana mawazo na watu mbali mbali watakao hudhuria.
   
  Anuani: 6411 Lbj Freeway Dallas Texas,75240
  Muda ni: sasa Kumi na mbili Jioni
  Simu:214 554 7381, 682 552 6402
   
  Pastor Absalom Nasuwa

  0 0
 • 02/14/13--20:45: Article 12


 • 0 0

  Na Freddy Macha 
  Maonyesho maarufu ya mavazi ya kimataifa –London Fashion Week- yatamega kitengo chake cha kimataifa kusaidia kutangaza kazi za washoni wapya toka Tanzania ndani ya Ubalozi wetu leo Ijumaa mjini London. 
  Mada ya maonyesho haya yatakayoendelea kwa juma zima ni “Swahili Flavour” (Ladha ya Kiswahili). Yategemea kutukuza kazi za Watanzania kupitia wabunifu mavazi Christine Mhando (anayetumia jina la ubunifu: “Chichia London”) na Anna Lukindo ( “Anna Luks”). 
   Christine Mhando alihitimu chuo cha Usanii cha Kent mwaka 2002 na huhimiza mtindo wa Kanga kama wajihi wa kazi zake, ilhali Anna Luks aliyemaliza chuo cha Middlesex, London hutumia fani inayosisitiza kamba kamba, mavazi ya kike kwa dunia ya kisasa. 
  Wote wanasema wana lengo la kukuuza sanaa na ubunifu, utamaduni wa Kitanzania, kutangaza taswira za Kiswahili na sura mbalimbali za Afrika Mashariki. 
  Pamoja nao wasanii hawa ni msaidizi wao–ambaye bado anasomea upambaji mavazi, Margaret Waiyego - mzawa wa Kenya. Kaimu Balozi wa Tanzania, Mheshimiwa Chabaka Kilumanga alisema jana kwamba maonyesho haya ya kimataifa yatakua nafasi kubwa kwa Tanzania kujenga jina lake na ni sehemu mahsusi ya kujivunia utamaduni wetu. 
  Shirika la maendeleo ya utamaduni na elimu British Council ndiye mgharamiaji wa shughuli hii yenye lengo la kujenga vipaji na kazi za mavazi za washoni wasiofahamika duniani. 
   Tovuti: www.freddymacha.com
   

  1.    Anna Lukindo(Anna Luks) akiwa kazini kutayarisha ufunguzi huu jana 
  1.    Mlango wa kuingilia maonyesho umeshatayarishwa          Moja ya matumizi mbalimbali ya kanga kama foronya za mito katika kochi  Msaidizi akiwa kazini kusaidia matayarisho haya


  0 0


  Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, Masheikh mbali mbali na mamia ya wananchi wa Zanzibar, akiwa katika mazishi ya Mwanazuoni na mhadhiri maalum Zanzibar na eneo la Afrika Mshariki, Sheikh Nassor Abdallah Bachu huko katika viwanja vya Mnazimmoja mjini Zanzibar jana. Alizikwa jana kijijini kwao Donge, Wilaya ya Kaskazini 'B', Mkoa wa Kaskazini Unguja.
  Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, Masheikh mbali mbali na mamia ya wananchi wa Zanzibar, akiwa katika mazishi ya Mwanazuoni na mhadhiri maalum Zanzibar na eneo la Afrika Mshariki, Sheikh Nassor Abdallah Bachu huko katika viwanja vya Mnazimmoja mjini Zanzibar jana. Alizikwa jana kijijini kwao Donge, Wilaya ya Kaskazini ‘B’, Mkoa wa Kaskazini Unguja
  Sheikh Nassor Alisaliwa katika Viwanja Vya Maisara na Kuzikwa kijijini kwao Donge
  Makamo wa kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamadi Akishuhudia Jeneza la Sheikh Nasssor Bachu
  Kutokana na watu kuwa wengi sala ya maiti ilifanywa kwenye viwanja vya Maisara na sio msikiti wa kikwajuni kama ilivyotangazwa hapo mwanzo. Mwenyezi Mungu Amuweke marehemu mahala pema peponi Ameen.

  0 0

  Goldie Harvey, one of Nigeria’s popular singers is dead. She reportedly passed on after she returned from a trip to the United States on Thursday night . A blogger who claimed she was called and informed of the incident by the singer’s best friend Denrele Edun had first broken the news. 

  The blogger also wrote that Denrele told her that Godlie who flew in from the US on Thursday died in his arms at a hospital in Victoria Island. All efforts to reach Denrele Edun on his phone proved futile. He has not also responded to questions sent to him via his tweeter handle as of the time of filing this report.

  Goldie’s Twitter handle and Facebook fan page however bear the confirmation that she has passed on as the message “It is with heavy heart that I have to inform you all that Goldie passed this night shortly after arriving Lagos from LA. May her soul rest in the eternal peace of the Lord – Admin!!” was posted around 11 pm on Thursday.

  Street Journal’s findings revealed that Goldie was brought into Reddington Hospital around 7.55 pm, dead.

  Producer, Don Jazzy also wrote on Twitter, “RIP Goldie”. In the early hours of Friday, famous actress, Stella Damasus tweeted “Rest in peace Goldie. We will miss you dearly. God grant your family the strength to bear the loss. It is well.”

  Goldie, whose real names are Susan Oluwabimpe Harvey was nicknamed “Goldie” because of her hair colour which was naturally golden. She was born in the early 1980s to an Ijebu mother and an Ikole Ekiti father. Her first single, “Komole” gave an idea of what she could do musically and since its release, Goldie never looked back. She represented Nigeria at the Big Brother Africa 7 in 2012 and was the last celebrity to exit the show, emerging as the 3rd runner up.

  SOURCE: HERE

  0 0


  0 0

   Mhe. Mwansa Kapeya, Naibu Waziri wa Habari na Utangazaji kutoka nchini Zambia (wa pili kushoto) akiwa kwenye Picha ya pamoja na Prof. Makame Mbarawa, Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia (wa tatu kushoto) nje ya jengo la Wizara hiyo. Wa pili kushoto ni Dkt. Florens Turuka, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Tanzania na Mhe. Elizabeth Phiri (wa kwanza kushoto), Naibu Balozi wa Zambia nchini Tanzania.
  Mhe. Mwansa Kapeya, Naibu Waziri wa Habari na Utangazaji nchini Zambia amefanya Ziara ya kujifunza nchini Tanzania kuhusu maandalizi na mafanikio ya kuwawezesha watanzania kuhama kutoka Teknolojia ya Utangazaji ya analojia na kutumia Teknolojia ya Utangazaji ya Dijitali. Mhe. Kapeya alifanya mazungumzo na ujumbe wake Leo ofisini kwa Mhe. Prof. Makame Mbarawa, Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia.

  Lengo la Ziara hiyo ya ujumbe huo kutoka Zambia ni kuona namna gani Tanzania ilijiandaa na kufanikisha kuzima mitambo ya analojia rasmi  nchini  tarehe 31 Desemba, 2012 kwa kuanzia na Mkoa wa Dar es Salaam ili nao waweze kujifunza na kuzima mitambo hiyo Kabla ya Desemba, 2013. Katika Ziara hiyo, Prof. Mbarawa alimueleza Mhe. Kapeya na ujumbe wake Kuwa ni vema Wizara yake iandae Mazingira mazuri ya kufanikisha uhamaji wa kutoka analojia kwenda dijitali kwa kuwashirikisha Wadau, sekta binafsi, wanasiasa, kutumia sera, Sheria na Kanuni na kuendesha Kampeni ya elimu kwa umma ili wananchi wafahamu umuhimu na manufaa ya kutumia Teknolojia ya Utangazaji ya Dijitali. Ujumbe huo kutoka Zambia utakuwa nchini Tanzania kwa Ziara hiyo ya mafunzo Hadi tarehe 15 Februari, 2013.
  Na Prisca Ulomi, Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia.

  0 0  Na Mwandishi Wetu

  Familia ya mdogo wake Hayati  Mwalimu Julius Kambarage Nyerere,  Marehemu Joseph Nyerere, imejitokeza na kusema haimtambui mtuhumiwa wa kesi ya mauaji, anayejitambulisha kwa jina la Makongoro Joseph Nyerere.

  Taarifa iliyotolewa na Nuru Nyerere-Inyangete, kwa niaba ya familia hiyo jana, ilisema hadi kifo cha baba yao, Joseph Kizurira Nyerere, mwaka 1994 haina taarifa zozote za kuwa na ndugu yao anayeitwa Makongoro Joseph Nyerere.

  “Hadi baba anafariki dunia hatukuambiwa tuna ndugu anayeitwa Makongoro Joseph Kizurira Nyerere …watoto wote wa Mzee Joseph tunafahamiana, lakini kwa huyu ndiyo kwanza tunaambiwa kuwa ni ndugu yetu. Tunauhakikishia umma kwamba hadi kifo cha baba yetu hatukuambiwa juu ya kuwapo kwa ndugu mwenye jina hilo; hii ina maana kwamba hatumtambui,” alisema Nuru.

  Naye mtoto mwingine wa Joseph, Matare, alisema, “Tangu kutangazwa kwa habari hizi tunapata simu nyingi za pole. Tunashangaa kwa sababu huyu mtu hatukuwahi kuambiwa kuwa ni ndugu yetu, na wala yeye mwenyewe hakuwahi kuja kwetu kujitambulisha kama ni mmoja wa watoto wa Mzee Joseph.”

  Matare aliongeza, “Tumesoma kwa mshituko kwenye magazeti ya Februari 14, 2013 na katika mitandao ya kijamii, kuwa kuna mtu anayejiita Makongoro Joseph Nyerere. Huyu huyu hatumtambui kwa uhusiano, taarifa wala sura. Watoto wote wa marehemu Joseph Nyerere wanafahamika, hakuna mtoto wa marehemu mwenye jina hilo.”
  Juzi, Makongoro ambaye ni mfanyabiashara, mkazi wa Dar es Salaam, alifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini humo akikabiliwa na mashitaka ya mauaji ya mfanyabiashara mwenzake, Onesphory Kitoli. Mtuhumiwa huyo anatarajiwa kuunganishwa katika kesi hiyo na mtuhumiwa mwingine mfanyabiashara maarufu, Marijani Abubakari marufu kama Papaa Msofe (50). Kesi hiyo itatajwa Februari 20, mwaka huu.

  Wakili wa Serikali, Charles Anindo, alimsomea Makongoro mashitaka mbele ya Hakimu Mkazi, Agnes Mchome, na kudai kuwa Novemba 6, 2011 huko Magomeni Mapipa, Makongoro alimuua kwa makusudi Kitoli kinyume na kifungu cha 196 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu ya mwaka 2002.

  Anindo alidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika na aliomba Mahakama iahirishe kesi hiyo hadi Februari 20, mwaka huu, ambako Makongoro ataunganishwa na Papaa Msofe kwenye mashitaka hayo.

  Mtuhumkiwa hakutakiwa kujibu chochote kwa kuwa Mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi za mauaji.

  0 0

  Naibu Waziri wa kazi na Ajira,Dkt.Makongoro Mahanga akifunga mkutano wa tatu wa Wadau wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF),uliomalizika leo,kwenye ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa AICC,jijini Arusha,ambapo kauli mbiu yake kwa mwaka huu ilihusu "Sekta ya hifadhi ya Jamii Tanzania,Njia panda-Nini kifanyike".
  wenyekiti wa bodi ya wadhamini wa NSSF,Aboubakar Rajab akizungumza machache kabla ya kufungwa kwa mkutano wa tatu wa Wadau wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) ambao kilele chake kimekoma leo,ikiwa ni siku ya tatu,kwenye ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa AICC,jijini Arusha,ambapo kauli mbiu yake kwa mwaka huu ilihusu "Sekta ya hifadhi ya Jamii Tanzania,Njia panda-Nini kifanyike".
  Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF),Dkt. Ramadhan Dau akitoa ufafanuzi wa jambo kabla ya kufungwa kwa mkutano wa tatu wa Wadau wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) ambao kilele chake kimekoma leo,ikiwa ni siku ya tatu,kwenye ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa AICC,jijini Arusha,ambapo kauli mbiu yake kwa mwaka huu ilihusu "Sekta ya hifadhi ya Jamii Tanzania,Njia panda-Nini kifanyike".
  Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Emanuel Humba(pichani shoto) akiongoza mjadala wa mambo ya Afya,kwenye mkutano wa tatu wa Wadau wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) ambao kilele chake kinakoma leo,ikiwa ni siku ya tatu,kwenye ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa AICC,jijini Arusha,ambapo kauli mbiu yake kwa mwaka huu ilihusu "Sekta ya hifadhi ya Jamii Tanzania,Njia panda-Nini kifanyike".Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF),Dkt. Ramadhan Dau.
  Mkurugenzi wa hospitali ya IMTU,ambaye pia ni mshauri wa mambo ya Afya kwa Jamii,Dkt.Ali Mzige akijibu mijadala ya maswali mbalimbali ,yaliyokuwa yakiulizwa na wadau mbalimbali kuhusiana na mada ya Afya,kwenye mkutano wa tatu wa Wadau wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) ambao kilele chake kinakoma leo,ikiwa ni siku ya tatu,kwenye ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa AICC,jijini Arusha,ambapo kauli mbiu yake kwa mwaka huu ilihusu "Sekta ya hifadhi ya Jamii Tanzania,Njia panda-Nini kifanyike".

  Mbunge wa Rombo, Mhe. Joseph Selasini (CHADEMA),akiuliza swali wakati wa mada ya Afya,kwenye mkutano wa tatu wa Wadau wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) ambao kilele chake kinakoma leo,ikiwa ni siku ya tatu,kwenye ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa AICC,jijini Arusha,ambapo kauli mbiu yake kwa mwaka huu ilihusu "Sekta ya hifadhi ya Jamii Tanzania,Njia panda-Nini kifanyike".
  Baadhi ya wadau zaidi ya 1000 waliohudhuria mkutano wa tatu wa Wadau wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) ambao kilele chake kinakoma leo,ikiwa ni siku ya tatu,kwenye ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa AICC,jijini Arusha,ambapo kauli mbiu yake kwa mwaka huu ilihusu "Sekta ya hifadhi ya Jamii Tanzania,Njia panda-Nini kifanyike".

  0 0older | 1 | .... | 42 | 43 | (Page 44) | 45 | 46 | .... | 3272 | newer