Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110167 articles
Browse latest View live

NAIBU KATIBU MKUU WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI AFUNGA RASMI MAFUNZO YA JINSIA MJINI MOROGORO

$
0
0
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwamini Malemi akimsalimia Mshauri wa Masuala ya Jinsia wa Programu ya Sekta ya Sheria nchini, Wanyenda Kutta (Kulia) wakati alipokuwa anawasili katika Ukumbi wa Mikutano wa Edema mjini Morogoro kwa ajili ya kufunga rasmi mafunzo ya Jinsia kwa maafisa mbalimbali wa Jeshi la Magereza. Kushoto ni Kamishna wa Sheria na Utawala wa Jeshi la Magereza, Dk. Juma Malewa.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwamini Malemi akizungumza na maafisa mbalimbali wa Jeshi la Magereza kabla ya kufunga mafunzo ya jinsia kwa maafisa hao. Malemi licha ya kulipongeza jeshi hilo kwa hatua nzuri ya kuwateua maafisa mbalimbali wanawake, alilitaka jeshi hilo kuongeza juhudi zaidi kwa kuwapa nafasi ya uongozi wanawake ambao wana uwezo na sifa ya kuongoza.
Maafisa Magereza wakiifurahia hotuba ya mgeni rasmi, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwamini Malemi alipokuwa anatoa hotuba ya kufunga mafunzo ya jinsia yaliyokuwa yanafanyika mjini Morogoro.
Naibu Katibu Mkuu Mwamini Malemi (wa pili kutoka kulia) akimpa zawadi askari wa Jeshi la Magereza kutoka Gereza la Wilaya ya Liwale, mkoani Lindi, Beatrice Sabo kwa kuwasilisha vizuri mada ya jinsi na jinsia wakati wa mafunzo hayo. Wa kwanza kutoka kushoto ni Kamishna wa Sheria na Utawala wa Jeshi la Magereza, Dk. Juma Malewa. Anayefuata ni Mshauri wa Masuala ya Jinsia wa Programu ya Mabadiliko ya Sekta ya Sheria nchini, Bi. Wanyenda Kutta. Kulia ni Mwezeshaji wa mafunzo hayo kutoka Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, Asina Omari.
Naibu Katibu Mkuu Mwamini Malemi (Kulia), akipokea taarifa ya hali ya Utekelezaji wa Masuala ya Jinsia katika Taasisi zinazotekeleza Programu ya Maboresho ya Sekta ya Sheria kutoka kwa Mshauri wa Masuala ya Jinsia wa Programu ya Mabadiliko ya Sekta ya Sheria nchini, Bi. Wanyenda Kutta . Kushoto ni Dk Juma Malewa, Kamishna wa Sheria na Utawala wa Jeshi la Magereza.

 PICHA ZOTE NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

in loving memory

$
0
0

Memory is a way of holding onto the things you love, the things you are, the things you never want to loose. They say time is healer is it really? Or we Just burry our sorrow deeper and deeper. We wonder Death leaves a heartache no one can heal, love leaves a memory no one can steal.

Mum it is exactly One year since you went to the enternal Peace.It is not easy to keep going without Mother Love. We are trying so hard to be Strong enough to carry on as you would expect us to.
You are deeply missed by your Lovely Husband James Daudi Shikobe and childrens: Stella,Agness,Rachel,Daudi, Joseph,Peter,Abeli,Christina & Michael: 
Grand Sons & Daughters-Anderson,Tracey,James N.Mlughu,Anita,Brenda,Trisha, James David & Joshua. 
Your In Laws Bakari Nehemia Mlughu,Victor Yonah Mlay & Franco Nyang’oro. Brothers Sisters, Niece,Nephews and Friends.

2 TIMOTHEO 4:7 AMEN.
 JOHN 11:25. AMEN

Uchambuzi Wa Habari: Kwa Hili La Simu, Anne Makinda Ameonewa...!

$
0
0

Ndugu zangu,


Kwenye vyombo vya habari juma hili, moja ya habari kubwa iliyochagizwa sana ni kitendo ch viongozi wa Chadema kutoa kwa wananchi, pale viwanja vya Mwembe Yanga, namba za simu ya mkononi ya Spika Anne Makinda na Naibu wake, Job Ndugai.



Kimsingi, viongozi wa Chadema waliofanya kitendo kile walikosea. Yawezekana kabisa kuwa madai ya Chadema kuwa Spika na Naibu wake wanaisiginya demokrasia ndani ya Bunge ni madai ya msingi, lakini, namna waliyochagua ya kufikisha madai hayo kwa wananchi haikuwa sahihi.



Ni kawaida, kwa baadhi ya viongozi wawapo majukwaani kusukumwa na jazba wanapoongea, lakini, hutokea pia, kauli za viongozi hao wawapo majukwaani zinapokosa umakini, kupelekea madhara makubwa.



Katika kazi yangu ya uandishi, nimeshawahi kutofautiana na Spika Makinda, si mara moja, mara ya mwisho ni kwenye hoja yake kuwa wabunge wawapo Dodoma wana maisha magumu, hivyo, kuhalalisha ongezeko la posho zao.



Lakini bado naamini, Spika Makinda ni binadamu kama wengine. Naye ni mzazi na mwenye familia yake inayomzunguka. Kitendo cha viongozi wa Chadema kutoa hadharani namba za Spika Makinda , za simu ya mkononi, kwenye umati wa watu wenye kero mbali mbali , na unaoambiwa kuwa watumie namba hizo kumpigia na kutuma ujumbe mfupi kwa Spika Makinda, bila shaka, kwa akili ya kawaida tu, kitapelekea Spika Makinda na mwenzake Ndugai kuwa na wakati mgumu. Maana, watu wale watakuwa wamechochewa.



Ikumbukwe, kijinsia Anne Makinda anaweza kuwa mhanga zaidi wa kupigiwa na kutumiwa jumbe za simu zenye hata kumdhalilisha kijinsia. Katika dunia hii kuna baadhi ya wanaume wenye maradhi ya kisaikolojia yenye kuhusihanisha masuala ya ngono. 



Kwamba kuna wanaume ambao hutafuta namba za simu za wanawake tu. Ikifika usiku, hupiga bila kuongea, wanachosubiri ni kusikia sauti ya mwananmke ikijibu na kisha kumaliza haja zao. Hao ni wagonjwa. 



Hivyo, unapotoa hadharani namba ya simu ya mkononi ya mwanamke, basi, unaweza pia kumuingiza katika hatari ya kupokea simu za ajabu ajabu kutoka kwa baadhi ya wanaume. Wako wapi wanaharakati wa haki za kibinadamu na kijinsia wa kumtetea Anne Makinda?



Tunajifunza nini?



Viongozi wa kisiasa wawe makini wawapo majukwaani. Mambo mengine wanaweza kuyafanya na hata kuyaongea majukwaani wakidhani kuwa wameyafanya kwa dhamira njema, lakini, matokeo yake yaweza kuwa na madhara makubwa.



Ingewezekana kabisa kwa viongozi wale wa Chadema kutoa hadharani namba maalum ya simu ya mkononi, ili watu wapige na watume jumbe fupi kwenye simu hiyo. Kisha, viongozi hao wangeweza kurekodi sauti zenye maoni ya watu yasiyo na matusi wala namna yoyote ya kudhalilisha. Wangekusanya pia jumbe hizo fupi kwa kuhariri zile zenye matusi na zenye kudhalilisha. Baadae zingewakilishwa kwa Spika Makinda na Naibu wake.



Ingewezekana pia kukusanya saini kutoka kwa wananchi zenye kuonyesha kuwa wanawapinga Spika na Naibu wake, na kwamba wanawashinikiza wang'oke. Hizi zote ni njia za kistaarabu kabisa za kuwasilisha malalamiko.



Tukishindwa kuonyesha mfano sasa, wa kufuata taratibu za kistaarabu, hatari yake tunaizoesha jamii kutumia njia za ovyo na nyingine zenye maovu katika kuwasilisha malalamiko yao. Na kesho huenda Spika wa Bunge atatoka Chadema.



Itakuwaje basi, pale kesho viongozi wa CCM nao watasimama Mwembe Yanga mbele ya wananchi wenye kero zao, na kutaja namba za simu ya mkononi za Spika wa Bunge linaloongozwa na Chadema?!



Hapana, hivi tunavyoenenda sivyo inavyopaswa twende. Na hakuna aliyekamilika. Tujisahihishe.a



Maggid Mjengwa,

Rais Kikwete aongoza maelfu ya waombolezaji kumzika Askofu Dk. Thomas Laizer jijini Arusha leo

$
0
0
 Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiweka shada la maua kwenye Kaburi la aliekuwa Askofu Mkuu wa Kanisa la Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT),Dayosisi ya Kaskazini na Kati,Marehemu Askofu Dk. Thomas Laizer aliefariki Dunia Februari 7,2013 katika Hospitali ya Hospitali ya Selian,Jijini Arusha.Wakati wa Mazishi yake yaliyofanyika jioni ya leo nje ya Kanisa hilo.
Rais Mstaafu wa awamu ya pili,Alhaj Ali Hassan Mwinyi na Mkewe Mama Sitti Mwinyi wakiweka shada la maua kwenye Kaburi la aliekuwa Askofu Mkuu wa Kanisa la Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT),Dayosisi ya Kaskazini na Kati,Marehemu Askofu Dk. Thomas Laizer aliefariki Dunia Februari 7,2013 katika Hospitali ya Hospitali ya Selian,Jijini Arusha.

Rais Mstaafu wa awamu ya tatu,Mh. Benjamin Willim Mkapa na Mkewe Mama Anna Mkapa wakiweka shada la maua kwenye Kaburi la aliekuwa Askofu Mkuu wa Kanisa la Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT),Dayosisi ya Kaskazini na Kati,Marehemu Askofu Dk. Thomas Laizer aliefariki Dunia Februari 7,2013 katika Hospitali ya Hospitali ya Selian,Jijini Arusha.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa na Mkewe Mama Regina Lowassa wakiweka shada la maua kwenye Kaburi la aliekuwa Askofu Mkuu wa Kanisa la Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT),Dayosisi ya Kaskazini na Kati,Marehemu Askofu Dk. Thomas Laizer aliefariki Dunia Februari 7,2013 katika Hospitali ya Hospitali ya Selian,Jijini Arusha.
Mke wa Marehemu Askofu Dk. Thomas Laizer,Mama Maria Laizer pamoja  na familia ya Marehemu,wakiweka shada la maua kwenye Kaburi la Askofu Dk. Thomas Laizer aliefariki Dunia Februari 7,2013 katika Hospitali ya Hospitali ya Selian,Jijini Arusha.

picha zaidi zitawajia muda si mrefu.

BREAKING NYUZZZZ.....::UCHAGUZI WA TFF WAPIGWA STOP NA MAHAKAMA

$
0
0
TAARIFA YA UHAKIKA KABISA ILIYOIFIKIA GLOBU YA JAMII HIVI PUNDE,INAELEZA KUWA MAHAKAMA KUU KANDA YA MWANZA IMEUSIMAMISHA UCHAGUZI MKUU WA TFF,BAADA YA ALIEKUWA MGOMBEA WA NAFASI YA URAIS KWENYE KINYANG'ANYIRO HICHO,BW. RICHARD RUKAMBURA KUFUNGUA MASHTAKA KWENYE KESI NAMBA MOJA YA MWAKA 2013,KUPINGA KUENGULIWA KWAKE KWENYE KINYANG'ANYIRO CHA UCHAGUZI ULIOPANGWA KUFANYIKA FEBRUARI 24,MWAKA HUU.

KESI HIYO ITAANZA KUSOMWA KWA MARA YA KWANZA FEBRUARI 19.

RUKAMBURA AMBAYE ALIENGULIWA KWENYE HATUA ZA AWALI KABISA ZA MCHAKATO WA UCHAGUZI NA KAMATI YA UCHAGUZI ILIYOKUWA CHINI YA NDUGU LYATO BAADA YA KUBAINIKA KUWA AMEJAZA FOMU MBILI ZA KUWANIA UONGOZI HUKU MOJA IKIWA NI YA KUWANIA URAIS NA NYINGINE UJUMBE WA KAMATI YA UTENDAJI.

LAKINI JANA RUKAMBURA ALIFUNGUA KESI TATU DHIDI YA TFF,MOJA IKIWA NI KUTAKA MAHAKAMA IZUIE UCHAGUZI NA KUPINGA KUENGULIWA KWAKE NA KUTAKA AREJESHWE KWENYE KINYANG'ANYIRO CHA UCHAGUZI HUO.

KESI YA PILI AMBAYO BADO HAIJAPANGIWA TAREHE,ANATAKA MAHAKAMA IIZUIE TFF KUTUMIA KIGEZO CHA FIFA CHA KUWANYIMA HAKI WATU WENGINE.NA KESI YA TATU ANATAKA TFF IMLIPE FIDIA KWA SABABU IMEMDHALILISHA KWA KUMUENGUA KWA KIGEZO CHA KUJAZA FOMU MBILI WAKATI ANAEGOMBEA SHARTI AGOMBEE NAFASI MOJA.

''LAKI SABA YANGU WAMECHUKUA NA RISITI NINAZO,LAKI MBILI NILILIPA YA UJUMBE NA LAKI TANO YA URAIS,SASA KAMA SHARTI LAO NI KUGOMBEA NAFASI MOJA KWANINI WASISEME?" ALISEMA RUKAMBURA.

ALIENDELEA KUSEMA ''WAMENIDHALILISHA,MIMI NI MTU MZIMA NA NINA FAMILIA YANGU,NINA DIGRII TOKA MWAKA 2004 NA NILIGOMBEA NA TENGA MWAKA 2008 WAKANIENGUA,LAKINI SAFARI HII SIKUBALI.ALIMALIZA KUSEMA RUKAMBURA.

WALANGUZI WA NISHATI YA MAFUTA MKOANI RUKWA KUKIONA

$
0
0

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akizungumza katika kikao cha baraza la ushauri la watumiaji wa nishati na maji nchini na wadau wake walipotembelea Mkoani Rukwa kwa ajili ya shughuli mbalimbali za baraza hilo. Mkuu huyo wa Mkoa alitoa pongezi kwa kazi nzuri wanayofanya na kuahidi kuwachukulia hatua walanguzi wa nishati ya mafuta pamoja na wale wanasimamia kwa kushindwa kufanya kazi yao vizuri. Kulia ni Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Alhaj Salum Mohammed Chima.
Mwenyekiti wa baraza la ushauri watumiaji wa maji na nishati nchini Eng. Profesa Katima akizungumza katika kikao hicho ambapo alisema kazi kubwa ya baraza hilo ni kutetea na kulinda haki za watumiaji wa maji na nishati ambayo ni maji safi na maji taka, umeme, petroli na gesi asilia.
Baadhi ya wadau wa mkutano huo ambao ni vyombo vya ulinzi na usalama, Tanesco, EWURA Mkoa wa Rukwa, wawakilishi wa sheli za mafuta na shirika la Maji safi na Maji taka Mkoa wa Rukwa (SUWASA)
Wawakilishi wa baraza hilo Mkoani Rukwa
Picha ya pamoja. (Picha na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa)

HOTUBA YA NAIBU WAZIRI WA KAZI NA AJIRA WAKATI WA KUFUNGA MKUTANO WA 3 WA WADAU WA NSSF JIJINI ARUSHA

UFAFANUZI KUHUSU MADAI YA BUNGE KUTORUSHWA LIVE


PICHA ZA KADI NA VIFAA MBALIMBALI VILIVYOKUA VIKITUMIWA NA WEZI WA ATM MWANZA

$
0
0

JESHI la Polisi mkoani Mwanza kwa kusaidiana na maofisa wa Benki ya NMB imewatia mbaroni watu watatu ambao wanadaiwa kuiba kiasi cha Sh700 milioni kwa nyakati tofauti.
Akizungumza na waandishi wa habari, Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi Mwanza, Christopher Fuime alisema pia walikamata vifaa mbalimbali ambavyo walikuwa wakitumia kwa ajili ya kufanyia uhalifu huo.
Vifaa walivyokamatwa navyo
Vifaa vilivyokamatwa navyo ni kadi za bandia 194 za kuchukulia fedha katika ATM za Benki ya NMB, ambapo kati yake kadi 95 zilikuwa na namba 0225152975 zinazotumia namba ya akaunti ya 2258103695 zenye jina na picha ya mtu anayedaiwa kuwa ni mtumiaji mwenye jina la Molely L. P. Kadi nyingine 99 zilikuwa na namba 0506056317 za akaunti namba 5068000322 zikitumia jina moja la Mnuo Z. E na picha moja.
Pia walikutwa na kadi ya Benki ya Amerikani yenye namba 549012345678 zilizokuwa zikitumia jina la Richard Croswell.
Spray ya kupulizia Camera za usalama kwenye ATM
Picha na Gsengo Blog

MAZUNGUMZO NJIA SAHIHI YA KUMALIZA MIGOGORO YA KIDINI - UMOJA WA MATAIFA

$
0
0
Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Bw. Jan Eliasson 

Na Mwandishi Maalum

Wakati viongozi wakuu  mbalimbali nchini Tanzania  wakisisitiza haja na umuhimu wa viongozi wa madhebu ya dini kuwa na utaratibu wa kukutana mara kwa mara. Umoja wa Mataifa nao kwa upande wake  unaeleza kwamba ni kwa  njia ya  mazungumzo  migogoro ya dini inaweza kuepukika.

 Kauli hiyo ya Umoja wa Mataifa,  umetolewa na  Jan Eliasson,Nabu Katibu Mkuu wa  chombo hicho ya kimataifa ,  wakati wa  tukio maalum  la Muungano  kwaajili ya utamaduni wa Amani kwa njia ya  maelewano ya  madhehebu ya dini. Tukio ambalo limefanyika mwishoni mwa wiki hapa umoja wa mataifa likiwahusisha  wawakilishi kutoka  dini mbalimbali, vyama visivyo vya kiserikali na mabalozi.

“Migogoro mingi inayoendelea  hivi sasa duniani,  ni migogoro ya kidini. Mazungumzo baina ya imani mbalimbali yanaweza kusaidia kusuluhisha migogoro hii.  Tunaweza kupambana na chuki kwa njia ya mazungumzo   ili kujenga maelewano   na kujenga daraja la maisha bora kwa jamii zetu”.Akasema  Naibu Katibu Mkuu

Na kuongeza kuwa, dini zote zimekuwa  mstari wa mbele katika juhudi si tu za kuhimiza amani na upendo, bali hata katika miradi ya  kuwasaidia watu maskini kwa kutoa huduma  kama vile za afya, na kuwasaidia vijana.

 Hata hivyo akaonya kwamba, siasa kali za  kidini zimekuwa chimbuko la uharibifu wa kudumu na  mateso  katika jamii.

Na kwa sababu hiyo akasisitiza kutoachiwa kwa vikundi vya dini vyenye misimamo mikali  kuharibu na kuvuruga amani  na maendeleo na kazi nzuri inayofanywa na madhehebu ya dini .


 “Hatuwezi kuruhusu kundi dogo la watu wenye misimamo mikali  kuharibu kazi nzuri zinazofanywa na  jumuia za kidini kwa waumini wao duniani kote” akahimiza Bw. Eliasson

Akaelezea  wasi wasi wake kuhusu vijana kutumiwa  na vikundi vyenye misimamo mikali kueneza  kampeni za chuki na  vurugu kwa ahadi za kupata dhawabu au wokovu ili wao watimize malengo yao.

“Kwa kawaida  vijana wana nguvu.  Tunapashwa  kutafuta   njia nzuri na sahihi za kuwafanya wazitumie nvugu  zao kuboresha maisha yao” akasisitiza Naibu Katibu Mkuu.

Naye  Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, Bw. Vuk Jeremic kwa  upande wake alisema  Umoja wa Mataifa unaweza  kufaidika sana  kama viongozi wote wa dini watajihusisha na kufanya kazi kwa moja ili kuleta amani. Huku akiutaka  Umoja huo kuogeza kasi ya kushirikiana na madhehebu ya dini.

“ Hebu basi  na turejee na kukumbatia wito unaotolewa na imani zetu, wito wa kuwasaidia watu wengine wenye matatizo, wito wa kuheshimiana wenyewe kwa  wenyewe,ikiwa  ni pamoja na  uhuru wa kuabudu wakati wowote na mahali popote bila ya kujali tofauti zetu za imani”.

Rais huyo wa Baraza Kuu akasema kila mtu anawajibu wa kuwasiliana na mwenzake na kusahau yaliyopitia na kuonya kwamba kama vyanzo vilivyopita  vya migogoro ya kidini vitaendelea kukumbushiwa mara kwa mara, kuna hatari kubwa ya kuitumbukiza dunia katika  machafuko ya kutisha.

Mbunifu majengo maarufu, Mike Tembo achaguliwa kujenga hoteli ya nyota 7 kijijini Tanzania

$
0
0

MIke-Tembo-Wikipedia.png

Tembo Architects imetangaza kuwa kampuni hiyo imechaguliwa kusanifu jengo isiyofanana na lolote lile kaskazini mwa Tanzania. Mradi huu utamuweka katika ramani ya dunia Mike Tembo ambaye ni mbunifu anaeongoza. Mradi huu ni wa kwanza kwa Tembo kufanya kijijini, Tanzania.

Jengo hili litakalojengwa katika eneo ambalo bado halijatajwa kaskazini mwa Tanzania limefadhiliwa na tajiri mmiliki majengo toka Afrika Kusini, Nicholas Van De Kaamp. Akiwa maarufu kwa ujengaji wake wa nyumba na kuziuza kwa wananchi kwa kiasi kisichozidi 10,000 ZAR, mwanzilishi huyu inasemekana atauza nyumba vya jengo hili kwa wananchi wa kipato cha wastani.

Kwa taarifa zaidi kuhusu Tembo, Van De Kaamp na mradi huu unaokuja tembelea tovuti hii: http://bit.ly/XIZ02p

NSSF YABISHA HODI ZANZIBAR

$
0
0
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd akipeana mkono na Ofisa Uhusiano Mwandamizi wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Juma Kintu.
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd akipata maelezo kutoka kwa Ofisa Uendeshaji wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Ally Mkulembe wakati ujumbe kutoka shirika hilo ulipofika ofisini kwake kuandikisha viongozi wa Serikali katika Mpango Maalum wa Hiari wa kuchangia Mafao ya NSSF mjini Zanzibar leo.
  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd akijaza fomu ya uanachama wa Mpango Maalum wa Hiari wa kuchangia Mafao ya NSSF kwa viongozi wa Serikali mjini Zanzibar leo.
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd akifafanua jambo wakati alipokuwa akizungumza na ujumbe kutoka Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) kuhusu Mpango Maalum wa Hiari wa kuchangia Mafao ya NSSF kwa viongozi wa Serikali mjini Zanzibar leo.
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd akiweka saini ya dole gumba.
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd akiwa katika picha ya pamoja na Maofisa wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) Ofisini Kwake Vuga mjini Zanzibar baada ya kujiunga na NSSF. Kushoto ni Meneja wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Mkoa wa Dodoma, Mariam Ahmed, Ofisa Uhusiano Mwandamizi wa NSSF, Juma Kintu na Ofisa Uendeshaji NSSF, Ally Mkulemba. 
 Waziri katika Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Mohamed Aboud akimkaribisha ofisini kwake Meneja wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Mariam Ahmed alipofika kwa ajili ya Mpango Maalum wa Hiari wa kuchangia Mafao ya NSSF kwa viongozi wa Serikali mjini Zanzibar leo.
 Meneja wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Mariam Ahmed akifafanua jambo kuhusu Mpango Maalum wa Hiari wa kuchangia Mafao ya NSSF kwa viongozi wa Serikali mjini Zanzibar leo. Kulia ni Waziri katika Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Mohamed Aboud.
  Meneja wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Mariam Ahmed akimpa maelekezo ya kujaza fomu ya uanachama wa NSSF, Waziri katika Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Mohamed Aboud.
 Waziri katika Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Mohamed Aboud akiweka saini ya dole gumba.
 Meneja wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Mariam Ahmed akimpa maelekezo ya kujaza fomu ya uanachama wa NSSF, Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Said Shaaban Said.
Meneja wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Mariam Ahmed akimpa maelekezo ya kujaza fomu ya uanachama wa NSSF, Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Said Shaaban Said.

MAONYESHO YA MAVAZI YA KIMATAIFA LONDON KUHUSISHA WATANZANIA KWA MARA YA KWANZA LEO

$
0
0

Na Freddy Macha
Maonyesho maarufu ya mavazi ya kimataifa –London Fashion Week- yatamega kitengo chake cha kimataifa kusaidia kutangaza kazi za washoni wapya toka Tanzania ndani ya Ubalozi wetu leo Ijumaa mjini London.

Mada ya maonyesho haya yatakayoendelea kwa juma zima  ni “Swahili Flavour” (Ladha ya Kiswahili). Yametayarishwa kwa ushirikiano wa Ubalozi wa Tanzania London na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) kujenga vipaji na kazi za mavazi za washoni wasiofahamika duniani. 

 Kazi zitakazooyeshwa ni za washoni watatu Christine Mhando (anayetumia jina la ubunifu:  “Chichia London”),  Anna Lukindo ( “Anna Luks”) na Jacquleine Kibacha (“Heart 365”).

Mbunifu Christine Mhando
 Christine Mhando alihitimu chuo cha Usanii cha Kent mwaka 2002 na huhimiza mtindo wa Kanga na misemo na manen ya Kiswahili mathalan “Tongoza” na “Zungumza” kama wajihi wa kazi zake.  Anna Luks aliyesomea shahada yake chuo cha Middlesex, London hutumia vitambaa vya Kitanzania, kushona kwa mikono, kamba kamba, mavazi ya kike na dunia ya kisasa.  Baada ya kujiuzulu toka kazi ya kuajiriwa (kupanga sera)  Jaquileine Kibacha aliamua kufuata ndoto zake za kuwa msanii. Ubunifu wake unaochanganya desturi za kijadi na kisasa kutumia shanga shanga, manyoya ya ndege na mapambo imesanifiwa kutokana na safari aliyoifanya kuishi na Wamasai.

Kina  dada hawa  wanasisitiza kwamba  wana lengo la kukuuza sanaa na ubunifu, utamaduni wa Kitanzania, kutangaza taswira za Kiswahili na sura mbalimbali za Afrika Mashariki.

Kaimu Balozi wa Tanzania, Mheshimiwa Chabaka Kilumanga alisema kwamba maonyesho haya ya kimataifa yatakua nafasi kubwa kwa Tanzania kujenga jina  na ni sehemu mahsusi ya kujivunia utamadunina nchi  yetu.

ZIARA YA MAMA SALMA KIKWETE LINDI MJINI

$
0
0
  Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM wilaya ya Lindi mjini, Mama Salma Kikwete mkutano wa hadhara katika kijiji cha Nanyanje, wilaya ya Chikonje, wilaya ya Lindi mjini.

 Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Kata ya Chikonje, wakimsikiliza Mama Salma Kikwete alipozungumza nao katika kikao cha ndani, kwenye Ofisi ya CCM ya Kata hiyo.
 Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM wilaya ya Lindi mjini, Mke wa Rais Mama Salma Kikwete, akimsalimia mwananchi baada ya kuwasili kwenye mkutano wa hadhara aliohutubia katika kijiji cha Nanyanje, Kata ya Chikonje wilayani humo leo, akiwa katika ziara ya siku saba kukagua na kuimarisha uhai wa Chama na Utekelezaji wa ilani.


Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa CCM, Mama Salma Kikwete akipokea kadi ya CUF kutoka kwa aliyekuwa mwanachama wa chama hicho, Salma Saidi (kushoto) baada ya kutangaza kuhamia CCM katika mkutano wa hadhara uliofanyika kijiji cha Nanyanje, Kata ya Chikonje mkoani Lindi.
 Wanachama wapya wa CCM waliokabidhiwa kadi zao wakiwemo kutoka vyama vya CUF na Chadema, wakila kiapo baada ya kukabidhiwa kadi zao na Mama Salma Kikwete.

 Mama Salma Kikwete akishiriki kucheza ngoma ya zindiko ya wakazi wa Chikonje, iliyotumbuiza wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika leo.
 Wasanii wa kundi la ngoma ya zindiko ya Chikonje wakionyesha umahiri wao katika mkutano huo.
 Wananchi wakiwa kwenye mkutano huo wa kijiji cha Nanyanje kata ya Chikonje mkoani Lindi.

Wananchi wakiselebuka kwa nyimbo za CCM wakati wa mkutano huo.

Article 14


Ngoma azipendazo ankal

$
0
0
Ngoma ya 'Weekend' ya Afro 70 haitochuja kirahisi

KIGOMA ALL STARS WALIVYONOGESHA VALENTINE'S DAY VIA VIA CULTURAL CLUB ARUSHA

$
0
0

 Msanii  Ally kiba  na kundi lake wakifanya mambo katika ukumbi wa Via Via wakati wa sherehe za valentane day jijini Arusha ambapo Kigoma All Stars walitumbuiza.

WAZIRI WA HABARI,VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO ATEMBELEWA NA MKURUGENZI WA BRITISH COUNCIL OFISINI KWAKE

$
0
0
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara (Mb) akisalimiana na Mkurugenzi wa British Council nchini Sally Robinson (kulia) leo Ofisini kwa Waziri,alipokwenda kumtembelea na kufanya mazungumzo mbalimbali kuhusu tasnia ya ubunifu wa Sanaa na Utamaduni pamoja na jinsi ya kuwajengea uwezo katika fani mbalimbali za sanaa na ujasiria mali.
Waziri wa Habari ,Vijana,Utamaduni na Michezo,Dkt. Fenella Mukangara (Mb) akizungumza na Mkurugenzi wa British Council nchini (kulia) Sally Robinson leo alipomtembelea Ofisini kwake jijini Dar es Salaam na kuzungumzia masuala mbalimbali ya tasnia ya Utamaduni.
Waziri wa Habari, Vijana , Utamaduni na Michezo (kushoto) Dkt. Fenella Mukangara akiangalia kipeperushi baada ya kupokea kutoka kwa Mkurugenzi wa British Council nchini,Sally Robinson alipomtembelea leo jijini Dar es Salaam. Picha zote na Mwanakombo Jumaa-MAELEZO

Sauti za Busara 2013 at Old fort, Zanzibar

$
0
0
Owiny Sigoma Band unleashed their hypnotic afro grooves from a cross-Atlantic collaboration between the Luo of Kenya and London live at Sauti za Busara A unique blend of the sounds from London-UK and Kisumu-Kenya rented the air during Owiny sigoma's performance at Sauti za Busara's 10th edition.
From Reunion comes a voice like no other, Nathalie Natiembe who gave a sterling show at Sauti za busara yester nignt. Nathalie Natiembe with her unique voice performs to the international audience at East Africas leading festival Sauzti za Busara in Zanzibar.
Hailing from Guinea N'faly Kouyate also known as the Jimi Hendrix of the Kora enthrals festival goers at the fully packed Old fortduring Sauti za busara. The huge crowd welcomed at this years Sauti za Busara enjoyed a great performance by Guenea's N'faly Kouyate yesterday at Zanzibar's Old fort.photos By Peter Bennett.

NBC YADHAMINI HAFLA YA MFUKO WA NSSF MJINI ARUSHA

$
0
0

 Waziri wa Kazi na Ajira, Gaundencia Kabaka (kulia) akisalimiana na Kaimu Mkuu wa Idara ya Wateja Wakubwa na Uwekezaji wa Benki ya NBC, Minnie Adolf Kibuta katika hafla ya chakula cha jioni kilichoandaliwa na benki hiyo kwa washiriki wa mkutano wa tatu wa Wadau wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) kwenye ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa AICC,jijini Arusha . Katikati ni Mwenyekiti wa Bodi ya NSSF, Aboubakar Rajab.
 Waziri wa Kazi na Ajira, Gaundencia Kabaka (katikati) akizungumza katika hafla ya chakula cha jioni kilichoandaliwa na benki ya NBC kwa washiriki wa mkutano wa tatu wa Wadau wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) kwenye ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa AICC,jijini Arusha.
 Msanii wa muzii wa izazi kipya Naseeb Abdul ‘Diamond’ akikonga nyoyo za wadau wa NSSF katika mkutano huo jijini Arusha.
 Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii(NSSF), Crescentius Magori (kulia) akizungumza na  Kaimu Mkuu wa Idara ya Wateja Wakubwa na Uwekezaji wa Benki ya NBC, Minnie Adolf Kibuta katika hafla ya chakula cha jioni kilichoandaliwa na benki hiyo kwa washiriki wa mkutano wa tatu wa Wadau wa NSSF kwenye ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa AICC,jijini Arusha.
 Kaimu Mkuu wa Idara ya Wateja Wakubwa na Uwekezaji wa Benki ya NBC, Minnie Adolf Kibuta (katikati) akipozi kwa pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa NBC katika hafla hiyo jijini Arusha.
Viewing all 110167 articles
Browse latest View live




Latest Images