Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 41 | 42 | (Page 43) | 44 | 45 | .... | 3270 | newer

  0 0

  With the dust from the 2013 Africa Cup of Nations still settling, football is about to kick up another storm in the form of the knockout stages of the Champions and Europa League, the home straight of domestic cup competitions and the title run-ins of major European and African leagues.

  Over the next three months, SuperSport will broadcast live over 500 matches which will culminate in the crowning of the Champions League, Europa Cup, Copa del Rey, FA Cup, Nedbank Cup, League Cup, Spanish La Liga, English Premier League, South African Premier Soccer League, German Bundesliga and Italian Serie A champions.

  Add to that the start of a new search for the next Kenya Premier League, Zambia Super League, Zimbabwe Premier Soccer League and Nigerian Premier League champions.

  The greatest football show on earth, the Champions League, gets proceedings underway on SuperSport’s three-month football marathon with the collision of giants: Real Madrid against Manchester United and Barcelona against AC Milan, teams who between them share 23 European Cup titles. The last time Madrid and United met in the Champions League, in 2003, Ronaldo was at the peak of his powers and proved the difference, scoring a hat-trick as Madrid advanced to the semi-finals at the expense of United. This time round, another Ronaldo (Cristiano) is at the peak of his powers. Will he be the difference?

  After dramatically surrendering their league titles to arch-nemesis, Madrid and Manchester City, Barcelona and United look to already have one hand on the La Liga and EPL trophy as they both enjoy healthy 12-point leads.

  Participation in the domestic cups, the Copa del Rey and the FA Cup, means that both teams are very much on for the historic treble of the Champions League, domestic league and cup.

  In the last 15 years, only three teams have been able to achieve the treble, two of them being United and Barcelona in 1999 and 2009 respectively.

  In Naples, Diego Maradona enjoys demi-god status after he single-handedly turned Napoli into an Italian championship-winning team. This was back in the 1980s and since then, the Partenopei’s have never quiet managed to get their hands on the Scudetto again.

  Edinson Cavani, like Maradona a South America native, is looking to follow in the great man’s footsteps by single-handedly dragging Napoli to the title. Cavani’s deadly exploits in front of goal have Napoli seriously challenging for the Serie A title after a long time and the Uruguayan’s goals will be crucial in the next three months as Napoli look to re-live the Maradona days.

  UPCOMING FOOTBALL DERBIES

  EPL

  - 03 March – Tottenham Hotspurs vs. Arsenal (London derby)
  - 06 April – Manchester United vs. Manchester City
  - 04 May – Liverpool vs. Everton (Liverpool derby)

  Italian Serie A

  - 24 Feb – Inter Milan vs. AC Milan
  La Liga

  - 27 Feb – Barcelona vs. Real Madrid
  - 03 March – Real Madrid vs. Barcelona

  Bundesliga

  - 09 March – Schalke 04 vs. Borussia Dortmund (Revier derby)

  UEFA Champs League

  - 13 Feb – Real Madrid vs. Manchester United
  - 20 Feb – AC Milan vs. Barcelona

  0 0


  0 0

  Serikali inapenda kuufahamisha umma wa Watanzania kuwa hivi karibuni kumezuka kundi la Watu wadanganyifu ambao wamekuwa wakitumia majina ya viongozi waandamizi wa serikali na Taasisi nyeti ikiwemo Usalama wa Taifa kujipatia fedha kwa madai ya kutumwa na viongozi hao.

  Watu hao wamekuwa wakituma ujumbe mfupi wa simu (SMS) kwa maofisa mbalimbali wa wizara, mashirika ya umma na Idara za Serikali zinazojitegemea kuomba pesa ili wawafanye mipango ya kupandishwa vyeo.

  Utapeli huo umekuwepo nchini kwa kipindi kirefu sasa , ambapo watu huwapigia simu viongozi wa Taasisi za fedha , Mifuko ya Taasisi za Jamii na watu binafisi wakiomba fedha kwa madai ya kutumwa na viongozi waandamizi Serikalini wakati si kweli.

  Watu hao wamekuwa wakiwatapeli maofisa mbalimbali kuwa wanaweza kuwafanyia mipango ya kupandishwa vyeo endapo watawapatia kiasi cha fedha jambo ambalo halipo katika taratibu za utumishi wa umma.

  Utumishi wa umma unazo taratibu zake za kuwapandisha vyeo watumishi wake kulingana na sifa za kada zao na wala haiwezekani kwa viongozi waandamizi kuwachangisha fedha kwa ajili ya kuwapandisha vyeo.

  Serikali inawataka wananchi kuwapuuza matapeli hao na watoe taarifa katika vyombo vya dola na usalama mara wapatapo ujumbe wa aina hiyo ili hatua zichukuliwe dhidi yao.

  IMETOLEWA NA:
  IDARA YA HABARI (MAELEZO) DAR ES SALAAM.

  0 0
 • 02/12/13--03:51: Article 15

 • 0 0

  UONGOZI WA HOTELI YA JB BELMONT YA JIJINI DAR ES SALAAM ,UNASIKITIKA KUTANGAZA KIFO CHA MKURUGENZI MKUU WA HOTELI HIYO,NDG. JUSTICE BAGUMA (PICHANI) ALIEFARIKI ASUBUHI YA LEO WAKATI AKIWAHISHWA HOSPITALI KWA MATIBABU YA UGONJWA WA SHAMBULIO LA MOYO ULIOKUWA UKIMSUMBUA.

  GLOBU YA JAMII IMEPOKEA KWA MASIKITIKO MAKUBWA TAARIFA HIYO,NA INAUNGANA NA WAOMBOLEZAJI WENGINE KWENYE MSIBA HUO MKUBWA.

  TAARIFA KAMILI ITAFUATA BAADAE JUU YA TARATIBU YA MSIBA HUO.

  0 0

  Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia wanachama wa CCM wakati wa hafla ya kuwatambulisha wajumbe wapya wa Kamati kuu ya CCM ilkiyofanyika katika viwanja vya Makao makuu ya CCM mjini Dodoma leo.
  Mwenyekiti wa CCm Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM nje ya ukumbi wa White House,Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma leo.
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa pamoja na waliokuwa viongozi waandamizi wa CHADEMA.Kushoto anayevaa kofia ya CCM ni aliyekuwa mgombea Ubunge jimbo la Mbozi Magharibi kwa tiketi ya CHADEMA Bwana Mtela Mwampamba na kulia ni Aliyekuwa Makamu Mwenyekiti Baraza la Vijana CHADEMA Bi Juliana Shonza.Weninge katika picha ni Katibu mkuu wa CCMNdugu Abdulrahman Kinana(kulia) na kushoto ni Makamu Mweyekiti wa CCM Bara Ndugu Philip Mangula.(picha na Freddy Maro).

  0 0

  Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima akimsalimia Mwezeshaji wa Mafunzo ya Jinsia kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Asina Omari (kulia) kabla ya kufungua mafunzo ya Jinsia awamu ya pili mjini Morogoro leo. Kushoto ni Kamishna wa Sheria na Utawala wa Jeshi la Magereza, Dk. Juma Malewa. Pereira aliwataka maafisa wa jeshi hilo wahakikishe msongamano ndani ya magereza nchini unapungua.
  Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini, Kamishna Jenerali John Minja akitoa hotuba fupi ya kumkaribisha mgeni rasmi Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima ili afungue mafunzo ya jinsia kwa maafisa hao.

  Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima akizungumza na maafisa mbalimbali wa jeshi la magereza kabla ya kufungua mafunzo ya jinsia kwa maafisa hao.
  Maafisa Magereza wakimsikiliza kwa makini Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Pereira Ame Silima (hayupo pichani) wakati alipokuwa anatoa hotuba ya ufunguzi wa mafunzo ya jinsia mjini Morogoro.
  Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima (wa katikati waliokaa) akiwa na Viongozi watendaji, maafisa wa Jeshi la Magereza, wawezeshaji wa mafunzo ya Jinsia, na watumishi raia wa jeshi hilo katika picha ya pamoja baada ya ufunguzi mafunzo hayo. 

   PICHA ZOTE NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

  0 0

  Mkurugenzi wa Bendi ya Extra Bongo,Ally Chocky akiimba wakati wa Bonanza la kila jumapili Garden Breeze Magomeni jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

  Wacheza shoo wa Bendi ya Extra Bongo wakicheza wakati wa onyesho la Bendi hiyo katika Bonanza la kila jumapili Magomeni Garden Breeze jijini Dar es Salaam
  Mkurugenzi wa Bendi ya Extra Bongo,Ally Chocky,akicheza sambamba na wacheza shoo wake katika Bonanza la kila jumapili Garden Breeze Magomeni jijini Dar es Salaam.
  Mpiga Dramu wa Bendi ya Extra Bongo,Martine Kibosho akiwajibika wakati wa onyesho la Bendi hiyo katika Bonanza la kila jumapili Magomeni Garden Breeze jijini Dar es Salaam

  0 0


  Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuhukumu kifungo cha miaka tatu jela mtu aliyedaiwa kumuibia Sh milioni 37 Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Alhaj Ally Hassan Mwinyi.

  Mshitakiwa huyo ni Abdallah Mzombe ambaye amehukumiwa baada ya kumkuta  na hatia. Mbali ya adhabu hiyo, Mahakama imeamuru mshitakiwa kulipa fedha hizo wakati akitumikia kifungo hicho.

  Hakimu Genvitus Dudu alitoa adhabu hiyo baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa na upande wa mashitaka ambao ulikuwa na mashahidi saba.

  Mshitakiwa huyo alikuwa anadaiwa kuiba fedha hizo baada ya kuaminiwa na Mwinyi kusimamia na kukusanya kodi ya nyumba zake mbili zilizopo Mikocheni B na Msasani jijini Dar es Salaam.

  Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Dudu alisema, mshitakiwa amepatika na hatia ya makosa mawili ya wizi wa kuaminiwa,na anahukumiwa kifungo cha miaka mitatu jela kwa kila kosa lakini atatumikia vifungo hivyo kwa wakati mmoja ambapo ni sawa na miaka mitatu.

  kwa mujibu wa ushahidi mshitakiwa haibishaniwi alikuwa wakala wa kukusanya kodi katika nyumba za Mwinyi na alipokea fedha za kodi kutoka kwa wapangaji.


  Katika makubaliano yao Mwinyi alimwambia Mzombe akipokea kodi, fedha nyingine afanye ukarabati wa nyumba hizo na nyingine fedha zinazobaki ampelekee lakini mshitakiwa hakufanya hivyo badala yake alizitumia kwa matumizi yake binafsi.

  0 0


  This week, Kali TV covers Mali Benefit concert organized by Malian artists and Embassy of Mali in Washington DC. Also Kali TV was part of the St.Croix US Virgin Island reggae band Midnite Unites States tour in Washington DC

  0 0

  Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na
  Teknolojia Mhe. Januari Makamba 

  Na Mwandishi Wetu, Dodoma
  Serikali imeanza mchakato wa kumiliki Kampuni ya Mawasiliano Tanzania (TTCL) kwa asilimia 100  ikiwa ni njia mojawapo ya kufanya mageuzi ya kibiashara na kuliendesha shirika hilo kisayansi zaidi ya ilivyo sasa.
  Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Mh. Januari Makamba aliyasema hayo mkoani Dodoma mwanzoni mwa wiki hii wakati akielezea mikakati mbalimbali inayotaka kuchukuliwa na serikali ili kuweza kulimiliki shirika hilo kwa asilimia 100 badala ya 65 za sasa.
  Kwa sasa TTCL inamilikiwa kwa ubia, serikali ikiwa na asilimia 65 wakati 35 zinamilikiwa na kampuni ya simu za mikononi ya Airtel.
  “Mazungumzo tayari yameshaanza na dhamira yetu ni kununua aslimia 35 ya hisa zinazomilikiwa na wenzetu ili serikali iweze kumiliki asilimia 100,” alisema Mh. Makamba.
  Alisema katika kufanya mipango ya kwenda mbele kimaendeleo kupitia shirika hili ni lazima kufanya mchakato wa kulimiliki kwa asilimia 100 ili serikali iweze kufanya mageuzi kwa utashi wake kadiri inavyofaa.
  Alifafanua kwamba hatua hii ni Kutokana na changamoto zilizopo za kimuundo, kiungozi na ndio maana serikali imechukua hatua za kinidhamu miongoni mwa baadhi ya watendaji waliobainika kutumia madaraka yao vibaya ikiwa ni pamoja na kufanya ubadhirifu na hivyo kulisababishia shirika hasara.
  “Hii ni moja ya hatua muhimu katika kuelekea kufanya mageuzi katika shirika hili kongwe hapa nchini,” alisema.
  Alizitaja changamoto nyingine kuwa ni matatizo ya mtaji, na kusema kuwa ni lazima yashughulikiwe ikiwa ni pamoja na kwenda na teknolojia mpya na kulifanya shirika lijiwekeze kibiashara zaidi ya ilivyo sasa.
  “Naamini katika kufanya mageuzi makubwa bodi itachukua nafasi yake kwa maana ya uongozi wa shirika katika kurekebisha mambo na mapungufu yaliyopo, kwa maana ya kuweka uongozi mpya utakaoleta mabadiliko ili kulibadilisha liwe shirika kubwa la kisasa linalotengeneza faida,” alisisitiza.
  Alisema kutokana na historia yake huko nyuma kampuni hii ilipaswa kuwa ndio kampuni inayoongoza kimapato na pia kwa kutoa huduma nchi nzima kutokana na kuwa ipo kila wilaya katika nchi, lakini kutokana na changamoto mbalimbali imekuwa ni tofauti na matarajio yaliyowekwa wakati huo.
  Alisisitiza kuwa wakati sasa umefika kwa shirika kuwa katika mtazamo wa kuwekeza kibiashara zaidi na ushindani.
  “Shirika hili kongwe limeendelea kubaki kama lilivyo na serikali imeliona hilo, kinachohitajika ni kuwekeza katika rasilimali fedha na watu ili kukabiliana na ushindani wa kibiashara uliopo sasa,” aliongeza.
  Alisema mbali na changamoto zote hizo lakini TTCL imefanikiwa kuunganisha Ofisi za Serikali, mashirika mbalimbali, Taasisi za kifedha, utangazaji na Taasisi za elimu na hivyo kuboresha matumizi ya huduma za mtandao wa mawasiliano kupitia Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano katika utoaji wa huduma mbalimbali kwa wananchi.

  “Kwa mfano huduma za video conferencing zinawezesha kuendesha mafunzo au mikutano kwa wahusika na hivyo kuongeza ushiriki, na kupunguza gharama,” alisema.

   Akisikiliza kero za wafanyakazi wa kampuni hiyo hivi karibuni, waziri Makamba aliiagiza bodi ya Wakurugenzi ya TTCL kumtumia Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG) kufanya ukaguzi wa mahesabu ili kuthibitisha tuhuma za ubadhirifu wa fedha za kampuni hiyo ili hatua za kisheria wakibainika.
  Baadhi ya malalamiko yaliyotolewa na wafanyakazi hao ni pamoja na uongozi na bodi dhaifu katika ufuatiliaji mambo, ubadhirifu wa fedha za kampuni pamoja na uhamisho wa wafanyakazi usofuata taratibu.

  0 0

  Timu ya Highway ya Madaba mjini imechezea kichapo cha Mabao 3-0 kutoka kwa mabingwa wa kombe la Muungano Mufindi timu ya Holy Family ya Bombambili Songea Mjini. Hapa mshambuliaji hatari wa Highway akiwatoka mabeki wa Holy Family lakini waaaaapi!!!!! 
  Picha na mdau Gerson Msigwa

  0 0


   Mgeni Rasmi katika hafla ya Ufunguzi wa Mkutano wa tatu wa Wadau wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF),Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,Balozi Seif Ali Idd (wa tatu kulia)  na Mkewe,Mama Asha Seif Idd (wa pili kushoto) wakiwasili kwenye hoteli ya Mount Meru,Jijini Arusha usiku huu tayari kwa ufunguzi wa Mkutano huo utakaoanza kufanyika kuanzia Februari 13,kwenye ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa AICC,jijini Arusha.Wengine pichani ni Waziri wa Kazi na Ajira,Mh. Gaudencia Kabaka (katikati),Naibu Waziri wa Kazi na Ajira,Mh. Dkt. Makongoro Mahanga (wa pili kulia),Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa NSSF,Ndg. Aboubakar Rajab (nyuma ya Waziri Kabaka) pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF),Dkt. Ramadhan Dau (kulia).
  Mgeni Rasmi katika hafla ya Ufunguzi wa Mkutano wa tatu wa Wadau wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF),Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,Balozi Seif Ali Idd akisoma hotuba yake wakati wa hafla ya Uzinduzi wa Mkutano wa tatu wa Wadau wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) utakaoanza kufanyika kuanzia Februari 13,kwenye ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa AICC,jijini Arusha.
  Waziri wa Kazi na Ajira,Mh. Gaudencia Kabaka akisoma hotuba yake usiku huu wakati wa hafla ya Ufunguzi wa Mkutano wa tatu wa Wadau wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) utakaoanza kufanyika kuanzia Februari 13,kwenye ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa AICC,jijini Arusha.
  Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF),Dkt. Ramadhan Dau akizungumza machache usiku huu wakati wa hafla ya Ufunguzi wa Mkutano wa tatu wa Wadau wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) utakaoanza kufanyika kuanzia Februari 13,kwenye ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa AICC,jijini Arusha.
  Mgeni Rasmi katika hafla ya Uzinduzi wa Mkutano wa tatu wa Wadau wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF),Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,Balozi Seif Ali Idd akipongezwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa NSSF,Ndg. Aboubakar Rajab mara baada ya kutoa hotuba yake ya ufunguzi wa Mkutano wa tatu wa Wadau wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) utakaoanza kufanyika kuanzia Februari 13,kwenye ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa AICC,jijini Arusha.
  Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Crenscentius Magori akitangaza majina ya washindi wa tuzo mbali mbali za NSSF kutoka mashirika,makampuni pamoja na watu binafsi.

  0 0
 • 02/12/13--19:00: ngoma azipendazo ankal
 • Céline Dion na ngoma yake ya 'The Power of Love' kwa msimu huu ni pahala pake...

  0 0

   Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akifungua Mkutano Mkuu wa Mwaka wa maofisa waandamizi wa Jeshi  la Polisi ulifanyika katika ukumbi wa Pius Msekwa mjini Dodoma jana.
   Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Maofisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi muda mfupi baada ya kufungua mkutano wao wa Mwaka uliofanyika katika ukumbi wa Pius Msekwa Mjini Dodoma jana Jioni,Kauli Mbiu ya mkutano Huo ni” Tujenge Uwezo wa Jamii na Polisi kukabiliana na Vurugu kwa Kuimarisha Utii wa Sheria Bila Shuruti,”.Walioketi Mbele ni.Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dkt.Emmanuel Nchimbi,Inspekta Jenerali wa Jeshi la Polisi Saidi Mwema,Spika wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Anna Makinda na Naibu Spika Johna Ndugai.
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akijadiliana jambo na Waziri wa Mambo ya Ndani Dkt.Emmanuel Nchimbi pamoja na Inspekta Jenerali wa Jeshi la Polisi Saidi Mwema muda mfupi baada ya kufungua Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Maofisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi Mjini Dodoma jana. Picha na Freddy Maro wa Ikulu

  0 0

  Na Profesa J. Mbele

  Kuanzia tarehe 3 hadi 28 Januari, nilikuwa Tanzania na wanafunzi 29 wa Chuo cha St. Olaf, kwenye kozi juu ya mwandishi maarufu Ernest Hemingway.

  Niliitunga kozi hii kwa makusudi, ili kuwapa wanafunzi fursa ya kuyaelewa mambo ya mwandishi huyu ambayo hayajulikani sana au hayajulikani vizuri, hata miongoni mwa wasomi.

  Tulisafiri katika maeneo kadhaa nchini Tanzania, ambamo Hemingway alipita mwaka 1933-34, tukiwa tunasoma maandishi yake kuhusu sehemu hizo. Wanafunzi walipata fursa tele ya kukutana na wa-Tanzania, kuanzia watoto wadogo hadi wazee.

  Walipata fursa ya kukutana na wa-Tanzania wa dini mbali mbali. Walipata fursa ya kuona maisha ya mijini na vijiji. Walipata ufahamu mpana na wa kina kuhusu maandishi na falsafa ya Hemingway.

  Kitu kimoja muhimu ni jinsi wanafunzi wote walivyopendezwa na hali waliyoiona Tanzania, hali ya ukarimu mkubwa kila walipopita. Walishangaa kuona kuwa wa-Tanzania wanajisikia raha kabisa kuwakaribisha wageni. Wamefurahi sana kupata fursa ya kuifahamu Tanzania. Wanaipenda kiasi kwamba walisononeka siku walipoondoka kurejea Marekani.

  Katika picha ya juu, anaonekana mwanafunzi mmojawapo akiwa ameshika kitabu cha Africans and Americans: Embracing Cultural Cultural Differences, ambacho wanafunzi walikitumia katika maandalizi ya safari yao. Katika picha ya chini tunaonekana mjini Karatu, tukiwa na mwanasheria Alex Shilla, ambaye ameshika kitabu hicho hicho, na amekuwa mdau na mpiga debe wake. Wanaonekana pia akina mama wawili ambao ni mahakimu mjini Karatu.

  0 0


  Sauti za Busara works to increase local attendance in next week’s festival. Busara managing director, Rebecca Corey says that the percentage of Zanzibari and Tanzanian citizens has gone down since the beginning of the festival, but explains that it is due to more international visitors, not less local attendance.  Corey worries that this gives the mistaken impression that Busara is for foreigners. 

  “Sauti za Busara is not just an event for tourists. Yes, the festival is meant to give local Zanzibari and East African artists a platform to share their music with the world and get some much-deserved international attention. The foreign visitors who come to the festival buy CDs of local musicians and take back to their home countries lots of enthusiasm and excitement about the acts they have seen. But the festival is also about bringing top live African acts to the stage for local people to enjoy. This year, we include lots of local favorites such as This year, we include lots of local favorites such as DDC Mlimani Park Orchestra aka Sikinde, Super Maya Baikoko, Culture Music Club, Lumumba Theatre, Msafiri Zawose, Peter Msechu and Safi Theatre Group, as well as international superstars of African music that many Tanzanians may never have heard of, like Cheikh Lo from Senegal and Khaira Arby from Mali,&rd quo; said Corey.

  Msafiri Zawose is the son of musical legend Hukwe Zawose and his music carries on the cultural traditions of his father and Gogo music.  Culture Musical Club is Zanzibar’s most successful taarab orchestra, touring Zanzibar and Europe since they were founded in 1958.  Safi Theatre Group from Dar es Salaam uses acrobatics to spice up dancing and traditional music. Festival Director Yusuf Mahmoud believes that Sauti za Busara is an opportunity for artists and young people. “Sauti za Busara invigorate s young people’s interest in local culture, gives opportunities for artists and music professionals to meet and learn from each other, keeps local traditions alive and creates employment for local people. The festival provides a catalyst for taking local music in new directions, as regional artists are exposed to and inspired by sounds from other parts of the continent,” said Mahmoud.

  Busara works to attract local attendance by keeping ticket prices low for Tanzanian citizens, 3000 TSH per day.  Busara also gives away free tickets to listeners through local radio shows and through their ‘gari bomba’ road show that travels around Zanzibar on Valentine’s Day this year, 14 February 2013.  Nearly half of the performers are from Tanzania and Zanzibar. “The festival organizers love to see lots of Zanzibaris and Tanzanians at the festival, dancing side by side with visitors from the rest of East Africa, Europe, and America. This year we have even gotten messages on our Facebook from fans coming all the way from Australia just to enjoy the festival! We try to keep ticket prices affordable for locals—only 3,000 TSH—to make sure we have a very diverse crowd. I think it’s fair to say that Sauti za Busara truly brings people from all walks of life together,” said Corey.

  To see a full list of performers and find out more about Sauti za Busara, visit www.busaramusic.org.  
  Tickets can be purchased starting on 13/02/2013 at 10:00 am at the Old Fort in Stone Town. 


  0 0

  Join us on Saturday 2nd March 2013 at FACE CLUB READING the Biggest & Baddest Saturday night in town as we present the all-exclusive "AFRO-BEATS & BASHMENT" Hosted by BongoDeejays Bringing you the freshest sounds this is gonna be another unmissable URBAN EVENTS PARTY!!!

  0 0

  Ankal,
  Kama nilivyokuambia mchana nimemfuatilia yule mtu aliyepiga simu chuo kusema ana vitu vyangu. Nimekuta ni kijana aliyemaliza form four anafanya kibarua Tanesco akingoja matokeo. Amaniomba msamaha sana kwa usumbufu nioupata kwani angetakiwa anitafute na kunirudishia mapema. 

  Kanirudishia wallet yangu na kila kitu isipokua fedha ambazo anasema wenzake walizigombania mara tu walipoiokota pale petrol station. Pia anasema alichelewa kunitafuta kwa sababu wenzake walimshawishi kuwa anaweza kujiingiza kwenye matatizo ya kudaiwa fedha nyingi iwapo angejitokeza na kusema kuwa ni yeye kaikota.

   Kwa mara nyingine nikushukuru sana wewe na wengine wote walionisaidia kutangaza na kufuatilia upatikanaji wake. Mungu awabariki sana.


  Mdau M. Mndeme

  0 0older | 1 | .... | 41 | 42 | (Page 43) | 44 | 45 | .... | 3270 | newer