Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 40 | 41 | (Page 42) | 43 | 44 | .... | 3278 | newer

  0 0


   Mtoa huduma wa kampuni ya mawasiliano ya Vodacom  akimwelekeza jambo  mteja eneo la Buguruni Sokoni jijini Dar es Salaam jana wakati Vodacom Tanzania walipokuwa wakifanya promosheni ya kuwajuza wananchi pamoja na wateja wake kuwa imeboresha mtandao kwa ajili ya kuwafikia wananchi mahali popote Tanzania.

   
  Mtoa huduma wa kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Najma Rashid akiwahudumia wateja eneo la Buguruni Sokoni jijini Dar es Salaam jana wakati Vodacom Tanzania walipokuwa wakifanya promosheni ya kuwajuza wananchi pamoja na wateja wake kuwa imeboresha mtandao kwa ajili ya kuwafikia wananchi mahali popote Tanzania.

   Watoa huduma wa kampuni ya mawasiliano ya Vodacom  wakiwahudumia wateja eneo la Buguruni Sokoni jijini Dar es Salaam jana wakati Vodacom Tanzania walipokuwa wakifanya promosheni ya kuwajuza wananchi pamoja na wateja wake kuwa imeboresha mtandao kwa ajili ya kuwafikia wananchi mahali popote Tanzania.
  Sehemu ya wananchi walijitokeza karibu na gari la matangazo la kampuni ya mawasiliano ya Vodacom   eneo la Buguruni Sokoni jijini Dar es Salaam jana wakati wa zoezi la kugawa laini na kuwasajili wateja papo hapo pia kuwawezesha kutumi huduma ya M-PESA

  0 0

  ARISE BEAUTY SUPPLY- WAUZAJI WA BIDHAA ORIGINAL WANA SALE (25 -70% OFF) YA BAADHI TU YA BIDHAA, HIZO KWENYE PICHA, ZIKIISHA NA SALE INAISHA, NI CHACHE TU. WAHI. WAPO MIKOCHENI KWA MWALIMU NA SINZA MAPAMBANO JIJINI DAR ES SALAAM. WASILIANA NASI KWA NAMBA  0714311283, 0784456046, 0784521171

  0 0

  Mawaziri wakuu wastaafu,Mh. Edward Lowassa (wa tatu kushoto) na Mh. Fredrick Sumaye (wa nne kulia) wakiwa wamejumuika na waombolezaji wengine katika msiba wa mama yake na Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa CRDB Bank,Dkt. Charles Kimei mwishoni mwa wiki huko Komakundi, Marangu,  Mkoani Kilimanjaro.
  Waziri Mkuu Mstaafu,Mh. Edward Lowassa akitia saini kitabu cha maombolezo ya kifo cha bibi Eliangi Chopasia, ambaye ni mama yake na Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB Bank,Dkt. Charles Kimei, aliefariki akiwa na umri wa miaka 97.
  Waziri Mkuu Mstaafu wa awamu ya tatu,Mh. Fredrick Sumaye akitoa salamu za rambimbai kwa niaba ya viongozi wengine wa kiserikali waliohudhulia kwenye msiba huo,akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Mh. Leonidas Gama.
  Mawaziri wakuu wastaafu,Mh. Edward Lowassa (wa pili kushoto) na Mh. Fredrick Sumaye (wa nne kulia) pamoja na waombolezaji wegine wakiwa wamesimama wakati mwili wa marehemu ulipokuwa ukiwasili nyumbani kwao kijiji cha Komakundi Marangu Moshi mwishoni mwa wiki.
  Waziri Mkuu Mstaafu,Mh. Edward Lowassa akiwapa pole Dr Kimei (katikati) na dada yake.

  0 0


  0 0

  Msanii nyota wa muziki wa hip hop hapa nchini ajulikanae kwa jina la Kisanii ROMA,akitumbuiza jukwaani,mbele ya umati wa watu mapema jioni ya leo ambapo kampuni ya simu za mikononi ya Tigo imezindua kauli mbiu yake mpya iitwayo "Tabasamu,upo na Tigo na kuchana na ile ya zamani iliyokuwa ikiitwa 'Jielezee mwenyewe',tamasha hilo ambalo limefana kwa kiasi kikubwa limefanyika kwenye fukwe za Coco Beach,jijini Dar na kuhudhuriwa na maelfu ya watu.Tamasha hilo limeratibiwa na kampuni bingwa ya burudani hapa nchini ya Prime Time Promotions Ltd.
  Msanii nyota wa muziki wa Bongofleva kutoka kundi la TMK Wanaume Halisi Sir Juma Nature sambamba na wasanii wenzake wakizikonga nyoyo za mashabiki na wapenzi wa muziki huo waliofika kwenye fukwe za Coco beach,ambapo kampuni ya simu za mikononi ya Tigo imezindua kauli mbiu yake mpya iitwayo "Tabasamu,upo na Tigo na kuchana na ile ya zamani iliyokuwa ikiitwa 'Jielezee mwenyewe',tamasha hilo ambalo lilifana kwa kiasi kikubwa,lilifanyika jana kwenye fukwe za Coco Beach,jijini Dar na kuhudhuriwa na maelfu ya watu.Tamasha hilo limeratibiwa na kampuni bingwa ya burudani hapa nchini ya Prime Time Promotions Ltd.
  Msanii wa kizazi kipya kutoka THT,ajulikanae kwa jina la Rachael akitumbuiza mbele ya maelfu ya watu waliofika kushuhudia uzinduzi wa kauli mpya ya kampuni ya Tigo kwa wateja wake.
  Naitwa Mr Blue kijana machachari sana awapo jukwaani,pichani akiwarusha wakazi wa jiji la Dar na viotongoji vyake waliofika kulishuhudia tamasha hilo likirindima kwenye fukwe za Coco beach.

  Pichani juu ni kikundi cha wasanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka TMK Orijino likiongozwa na Mh Themba sambamba na Chege wakilishambulia jukwaa namna ya kipekee kabisa.

  0 0

  The University of Dar es Salaam (UDSM), Center for Virtual Learning(CVL) is organizing a 5 days training to equip participants with the skills, knowledge and techniques for designing and developing good websites without even being experts by using Open Source Content Management System (CMS) called Joomla! CMS 2.5.8

  Joomla is an award-winning CMS, which enables people to build Websites, as well as Web based applications. A summary of course outline can be found from the College website: www.coict.udsm.ac.tz


  Target Audience

  • Individuals who would like to have their very own website.

  • Owner of an existing Joomla website built by another 3rd party.

  • SMEs and small businesses who wish to cut down the costs of web development projects and manage their own websites.

  • Individuals who wish to be self-employed in Website development


  • Web masters, website administrator, computer systems analysts, public relationship officers, communication officers and entrepreneurs.


  Training fee:  Tsh. 500,000/= (excluding breakfast and lunch)

  Venue:  UDSM Kijitonyama Campus (Former TTCL Staff College), Dar Es Salaam

  Registration:Please register NOW through the College website: www.coict.udsm.ac.tz

  Certificate of attendance:  will be provided upon completion of the course.

  For more information contact us at saganda@udsm.ac.tz; Telephone: +255715471705


  0 0


   The Azania Bank Director in the Managing Director's office (Treasury Management and Business Development) Godwin Seiya (left) hands over a 5m/- dummy cheque to the Aga Khan Hospital Medical Director Dr. Jaffer Dharsee (right) being support for the 2013 Breast Cancer Awareness Campaign organized by the hospital. 
   The Azania Bank Director in the Managing Director's office (Treasury Management and Business Development) Godwin Seiya (left) hands over a 5m/- cheque to the Aga Khan Hospital Medical Director Dr. Jaffer Dharsee (right) being support for the 2013 Breast Cancer Awareness Campaign organized by the hospital.
   The Azania Bank Director in the Managing Director's office (Treasury Management and Business Development) Godwin Seiya briefs reporters at the weekend on the bank’s donation to the 2013 Breast Cancer Awareness campaign by Aga Khan Health Service. Centre is the Aga Khan Hospital Medical Director Dr. Jaffer Dharsee and the Azania Bank Principal Business Development Officer Othman Jibrea (left).
  ======  ====== ======
  Azania Bank donates 5m/- to support 2013 Breast Cancer Campaign

  By Staff Reporter.
                                                                                        
  AZANIA Bank Limited has donated 5 million shillings to Agha Khan Health Services that will help boost this year’s breast cancer awareness drive in a bid to create public awareness on the fatal disease.

  Speaking during a handover ceremony at the bank's headquarters in Dar es Salaam, Azania Bank Director in the Managing Director's office (Treasury Management and Business Development) Godwin Seiya, said the bank is committed to support various social programs as part of its Corporate Social Responsibility (CSR) and in the course of giving back a certain percentage of the Bank earnings to the society they work with.

  Mr. Seiya noted that his bank has decided to support the campaign to sensitize women and the public in general to make routine tests at least once a year, with the view of minimizing risks for many women who are potential future victims.  "Records indicate that up to 1.5 million women have breast cancer problems. Tanzania accounts for 1,307 of the breast cancer victims. We at Azania Bank believe that the only way to minimize the risk is through public sensitization.

  "We believe with proper information dissemination, victims of breast cancer   can seek early medication thus increasing their chances of living. We are today donating five million shillings to support this year’s Breast Cancer awareness campaign," he said. The Aghakhan Hospital Medical Director Dr. Jaffer Dharsee during the event said the campaign targets to screen up to 5000 women throughout the country this year.

  He said last year’s campaign that was held in Dar es Salaam, Mtwara, Dodoma and Lindi cost upto $ 100,000 (Tsh 160m) and reached 3000 women in the four regions. “We will continue with the campaign this year and our target is screening 5000 women across the country this year. We will also bring on board cervical cancer screening this year. We call upon various corporate companies to render support to the campaign,” he said.

  0 0

  Kwa zaidi ya wiki tatu zilizopita, kuanzia tarehe 19 Januari 2013 mpaka 10 Februari 2013 mashabiki wa soka barani Afrika na duniani kote walikuwa hawabanduki katika viti vyao au sofa kwa ajili ya kutizama mashindano makubwa kabisa ya soka barani Afrika ya kuwania Kombe la Mataifa Ya Afrika mashindano ambayo kwa kizungu yanajulikana kama Orange Africa Cup Of Nations. Wenyeji wa mashindano ya mwaka huu walikuwa Afrika Kusini. Jumla ya mechi 32 zilichezwa na zote zilionyeshwa Live bila chenga kupitia channels za SuperSport zinazopatikana kupitia DStv, wakongwe wa digitali. Wakati wa fainali, DStv kupitia kampuni mama ya MultiChoice Tanzania walijumuika na mashabiki wa soka na wadau mbalimbali visiwani Zanzibar katika viota vya Gymkhana Club na Mtoni Marine. Huko palikuwa na special screening ya mchezo huo wa fainali ambapo Nigeria waliibuka mabingwa (kwa mara ya tatu sasa) baada ya kuwalaza Burkina Faso kwa goli 1-0. Kwa mapana na marefu umekuwa msimu wa kufurahi na marafiki na pia kutizama jinsi ambavyo kabumbu linazidi kutamba kama mchezo unaopendwa zaidi sio tu Afrika bali duniani kote.
  Picha moja ni sawa na maneno elfu moja. Sehemu ya umati wa mashabiki wa soka Zanzibar wakifuatilia kwa makini mchezo wa fainali kati ya Nigeria na Burkina Faso wakati wa special screening ya fainali hiyo iliyowezeshwa na DStv ndani ya Gymkhana Club.
  Experience The Spirit Of Africa- wadau wa soka ndani ya kiota cha Mtoni Marine wakiwa wenye tabasamu wakati wa fainali ya AFCON 2013.
  Mashabiki wa soka wakifuatilia kwa makini mtanange wa fainali ndani ya Mtoni Marine.Uwapo Zanzibar na unataka kuangalia michezo kama huu wa fainali ya AFCON 2013, Mtoni Marine ni sehemu inayohusika. Kila kona pametapakaa TV Screen ambazo zote, Live bila chenga hurusha matukio ya michezo kupitia DStv, wakongwe wa digitali.
  Meneja Masoko wa MultiChoice Tanzania, Furaha Samalu(kushoto) akiwa na wakurugenzi wa Island Promotions, Adelina Ngalo(katikati) na Ameir Kombo.
  Macho yote katika screen. Mchezo wa fainali unaendelea-Gymkana Club.
  Mkurugenzi wa Island Promotions,Ameir Kombo, akisaidia zoezi la maswali na majibu kuhusiana na michuano ya mwaka huu ya Kombe la Mataifa Afrika-AFCON 2013. Kushoto kwake ni Mohamed kutoka IBS-, mahali ambapo unaweza kupata huduma za aina zote zinazohusiana na DStv.
  Mbali na kufurahia Soka, mashabiki mbalimbali walijishindia zawadi mbalimbali kutoka DStv.
  Ni SuperSport, Ni Zanzibar, Ni DStv.
  Sehemu ya umati wa mashabiki wa soka waliofurika kushuhudia Live mchezo wa fainali ya AFCON 2013.
  Baadhi ya washindi wa zawadi mbalimbali zilizokuwa zikitolewa na DStv wakati wa special screening ya fainali ya Africa Cup Of Nations wakiwa katika picha ya pamoja na wawakilishi wa DStv akiwemo Meneja Masoko wa MultiChoice,Furaha Samalu.

  0 0
 • 02/10/13--22:53: Kumbukumbu
 • Gadi Stephano Nkalang’ango
  (11 July 1941-10 February 1980)  Miaka 33 imepita tangu alipotutoka baba Yetu mpendwa Gadi. Alipata ajali akiwa njiani kutoka Morogoro kwenda Dar-es-salaam. Alikuwa amemaliza kazi zake za ukaguzi wa mahesabu katika Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Elimu ( Zilizopo Morogoro). Ndipo alipopata ajali sehemu ya mlandizi tarehe 08 Februari na kufariki siku mbili baadaye. Kwa kweli pengo lake halilizibiki.  Lakini Mungu ni Mwema ambaye amekuwa akitufariji na kututia nguvu siku hadi siku na sasa tu watu wazima.

  Anakumbukwa na Mke wake mpenzi Hellena, Dada yake Magdalena (Mwalimu Kitururu) na wadogo zake Abasi, Naisai, Nambuyu, Nambua, Mwanahawa, Suni, Keto Bakari, Nkalang’ango, Sembua, Kosoni na Mtango.

  Pia anakumbukwa sana na Wanawe Wapendwa sana Mramba (Baba Wawili), Neema (Mama Nyamaka), Ididi, Kighenda, Mshighwa (Emmanuel/Baba Alice), Nshighia (Tula/Mama Frida), Martha na Gadi Junior (Samweli) ambaye alizaliwa siku 9 baadaye baada ya baba Kufariki.  Na pia wakwe zake Wapendwa pia wanamkumbuka; Wanoga (Mama Wawili), Kosmas (Baba Nyamaka), Ansila (Mama Gadi) na Abraham (Baba Frida) na Alvin.

  Wajukuu wamekuwa wakimtazama tu kwenye picha na kuangalia kaburi la Babu yao mpendwa. Wangependa leo hii wanataniana naye, wanacheza naye na kupewa hadithi za zamani lakini haikuwa mapenzi ya Mungu. Wajukuu hawa wataendelea kumi-miss kampani yake, Praise-God (PG), Praise-Jesus (PJ), Nyamaka, Gisela, Alice, Moses, Gadi, Msogoleka, Frida na Richard (Gadi).

  Bwana ametoa na Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe [Ayub. 1:21]

  0 0


   Kaimu Mkurugenzi wa Biashara, Bi. Mwanamvua Ngocho, akizungumuza na wageni waalikwa, abiria waliosafiri na ndege la shirika hilo, pamoja na maofisa wa uwanja wa ndege la Mtwara (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa safari za ndege za Shirila la Ndege la Tanzania (ATCL) mkoani Mtwara , mara tu baada ya kutua ndege hiyo uwanjani hapo mwishoni mwa wiki.
   Meya wa Mtwara Mikindani, Selemani Mtalika Shilingi ambaye alikuwa mgeni rasmi wakati wa uzinduzi wa safari za ndege za Shirila la Ndege la Tanzania (ATCL) mkoani Mtwara, akizungumuza na wageni waalikwa, abiria waliosafiri na ndege la shirika hilo, pamoja na maofisa wa uwanja wa ndege la Mtwara (hawapo pichani) mara tu baada ya kutua ndege hiyo uwanjani hapo mwishoni mwa wiki. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Biashara, Bi. Mwanamvua Ngocho na kulia ni Meneja Rasilimali watu na Utawala, Bi. Halima Nabalang’anya.  
  Baadhi ya abiria waliopanda dege ya Shirika la ndege la Tanzania (ATCL), wakitembea kuelekea katika chumba cha kupumzikia abirai, wakati wa uzinduzi wa safari za ndege za shirila hilo mkoani Mtwara iliyofanyika mwishoni mwa wiki.

  0 0

  Mabondia Fransic Miyeyusho kushoto akitunishina msuri na Sadiki Momba wakati wa utambulisho wa mpambano wao utakaofanyika siku ya sikukuu ya Pasaka.


  Mabondia Fransic Miyeyusho kushoto akitunishina msuri na Sadiki Momba wakati wa utambulisho wa mpambano wao utakaofanyika siku ya sikukuu ya Pasaka, wanashudia katikati ni Promota wa mpambano huo, Kaike Silaju na Makamu wa Rais wa PST, Aga Peter .
  Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

  0 0  Onyesho kubwa la mavazi Afrika Mashariki na kati la Swahili Fashion Week, limepanga kufanya onyesho kubwa visiwani Zanzibar katika Hoteli ya Mbweni Ruins siku ya Ijumaa ya tarehe 15/02/2013 ambapo wabunifu nguli kutoka Tanzania bara na Visiwani wamethibitisha kwa shauku na hamu kubwa ya kuacha kumbukumbu  nzuri ndani ya usiku huo wa onyesho la mitindo katika visiwa hivyo vya marashi ya karafuu.

  Tukio hili la Swahili Fashion Week Zanzibar litawaleta kwa pamoja zaidi ya wabunifu kumi kutoka ndani ya nchi kuonyesha ubunifu na umahiri wao katika tasnia ya sanaa ya ubunifu na kuongeza kasi ya maendeleo ya tasnia ya mitindo nchini Tanzania huku ikitangaza dhana nzima ya kujali vitu vinavyotengenezwa Afrika (Promote Made in Africa Concept)

  “Maandalizi yameshika kasi, tuko tayari kupeleka ladha ya Swahili Fashion Week katika visiwa vya Zanzibar, Kama inavyofahamika kwamba watu wengi watakuwa visiwani humo kufuatilia Sauti za Busara, huu ni mwezi wa burudani na vitu vizuri kwa watu wote Zanzibar, timu ya Swahili Fashion Week inafanya kazi usiku na mchana kuhakikisha kwamba inatibu kiu ya wapenzi wote wa Swahili Fashion Week na wadau wa maswala ya Ubunifu na Mitindo Zanzibar” Alisema Mustafa Hassanali muanzilishi na muandaaji wa Swahili Fashion Week.

  “Kupeleka Swahili Fashion Week kwa mashabiki waliopo visiwani Zanzibar, ni kuendeleza utamaduni wetu wa kuwa tukio bora la burudani na biashara katika tasnia ya mitindo, tukio hili la Zanzibar litawashirikisha wabunifu nguli toka bara na visiwani kuonyesha ubunifu na ladha tofauti za kiutamaduni, na wapenzi wa ubunifu na mitindo kupata ladha kutoka kwa wabunifu wa ndani ikiwa ni kama sehemu ya kuongeza familia yetu ya mitindo na ushirikiano baina ya wabunifu wa bara na visiwani” Aliongezea Hassanali

  Baadhi ya wabunifu watakaoshiriki ni Asia Idarous (Mshindi wa tuzo ya Humanitarian katika tuzo za SFW 2012), Dominick Godfrey, Subira Wahure, Ailinda Sawe, (Mshindi wa tuzo ya Origin Africa, SFW 2012), Martin Kadinda (Mbunifu Bora wa Nguo za Kiume, SFW 2012), Sarah Masenga (Mbunifu Bora Chipukizi, SFW 2011), Gabriel Mollel (Mbunifu Bora wa Mwaka na Mbunifu Mvumbuzi wa mwaka, SFW 2012), Subira Wahure, Jamila Vera Swai, Salim Ali, Ahmed Abdul pamoja na mshindi wa tuzo ya Mbunifu Anaechipukia wa SFW 2012, Lucky Creation.   

  “Swahili Fashion Week Zanzibar ni onyesho rasmi na la kwanza kufanyika visiwani humo, Swahili Fashion Week ilishafanya onyesho la mitindo mkoani Arusha mwaka 2011 na mipango ni kufanya maonyesho mbalimbali katika miji mikubwa hapa Tanzania” Alimalizia Meneja Uhusiano wa Swahili Fashion Week, Hassan Mrope.

  Onyesho limepangwa kuanza mapema ambapo kuanzia saa moja usiku milango itakuwa wazi. Tiketi za onyesho hili zinapatikana katika Hoteli ya Mbweni Ruins na Hotspot Bistro.

  Onyesho hili la Swahili Fashion Week Visiwani Zanzibar limedhaminiwa na Mbweni Ruins, ZG Tours, Daja Salon & Spa, Vayle Springs Clouds TV, Coconut Fm na 361 Degrees.

  Swahili Fashion Week mpaka sasa ndio ni tukio kubwa la mitindo Afrika ya Mashariki na Kati. Ni mwaka wa sita sasa, Swahili Fashion Week ni jukwaa la wabunifu wa mitindo na vito vya urembo kutoka nchini zinazoongea Kiswahili na Bara la Afrika kwa ujumla kuonyesha vipaji vyao, kutangaza ubunifu wao na kutengeneza mtandao na wadau duniani. Dhamira kubwa ni kuweka mkazo katika ukanda huu kwamba ubunifu ni tasnia inayotengeza vyanzo vya mapato huku ikitangaza bidhaa zinazotengenezwa Afrika “Promoting Made in Africa concept”.

  KWA MAELEZO ZAIDI:

  Hassan Mrope
  Meneja Uhusiano
  Swahili Fashion Week  
  Simu: +255 713 441892

  0 0


  LINDI CEMENT (3).JPG
  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Membe (wa pili shoto) akiwa na viongozi wa mkoa wa Lindi na wa kampuni ya Dangote inayojenga bonge la kiwanda cha Saruji pamoja na wakandarasi, akikagua maendeleo ya ujenzi wa kiwanda hicho ambacho kitapokamilika kitakuwa na uwezo wa kuajiri wananchi zaidi ya 7,0000

  LINDI CEMENT (5).JPG
  LINDI CEMENT (6).JPG
  LINDI CEMENT (7).JPG
  LINDI CEMENT (11).JPG
  LINDI CEMENT (12).JPG
  LINDI CEMENT (9).JPG
  Click here to Reply or Forward

  0 0

  Picha na Habari na Dotto Mwaibale 
   RAIS Jakaya Kikwete ameiagiza Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii na Jeshi la Polisi nchini kufanya msako na kuwafichua watu wote watakaopatikana na dawa za Serikali katika maduka binafsi. Maagizo hayo ylitolewa na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii kwa niaba ya Rais Kikwete ambaye angekuwa mgeni rasmi kwenye sherehe za ufunguzi wa ghala la kisasa la kuhifadhia dawa katika Makao Makuu ya Bohari ya Dawa jijini Dar es Salaam leo. 
   "Natambua kuwa lipo tatizo la dawa na vifaa tiba vya serikali kupatikana katika maduka ya dawa ya watu binafsi jambo ambalo linanikera sana nawaagizeni wachukukieni hatua za kisheria wale wote watakao patikana na dawa hizo" alisema Rais Kikwete. 
   Alisema Serikali haiwezi kuendelea kununua dawa kwa dharama kubwa na zikaishia katika mifuko ya watu wachache badala ya wananchi walio wengi hususani wa vijijini. Alisema Bohari ya dawa iliundwa mwaka 1994, ikiwa na dira ya kufikisha dawa na vifaa tiba karibu na wananchi ambapo tumeambiwa kuwa shughuli za MSD zimepanuka sana hususani uwezo wa maghala umefikia mita za mraba 51,800 na nusu ya hizo ni za kukodisha kwa watu binafsi. 
   "Natambua kuwa gharama za ukodishaji wa magahala ni kubwa sana na ni vema MSD ikawa na maeneo yake yenyewe bila kutegemea maghala binafsi" alisema Rais Kikwete. Rais Kikwete alizielekeza Halmashauri husika katika kanda za MSD kuisaidia Bohari ya dawa kupata maeneo mkakati ya uhifadhi wa dawa na maeneo waliyonayo tayari yaweze kupewa haki miliki. Alisema chanjo ni hatua muhimu kwa ajili ya ya afya za mama na mtoto ambapo mpango wa taifa wa chanjo ulianza mwaka 1975 ukiwa unatoa chanjo dhidi ya magonjwa kama KifuaKikuu, Polia, Surua, Dondakoo, kifaduro na Pepo Punda. 

   Alisema magonjwa mengine yaliyongezeka ni kinga dhidi ya Homa ya Ini, Homa ua Uti wa mgongo, nimonia na kinga dhidi ya magonjwa ya kuhara. Rais Kikwete aliongeza kuwa kinga ni haki ya kila mtoto hivyo mahitaji ya chanajo yamekuwa yanaongezeka kwaka hadi mwaka kutokana na ongezeko la idadi ya watu. "Ongezeko la idadi ya chanjo pamoja na ongezeko la aina za chanjo imesababisha kuwa na hitaji kubwa la maeneo ya kuhifadhi chanjo na kuzisambaza" alisema Kikwete. 

   Alisema Utunzaji wa chanjo unahitaji mfumo wa mnyororo baridi hivyo kuhitaji vyumba maalumu vyenye ubaridi, pamoja na gari lenye vifaa vya kutunza ubaridi huo ili kuhakikisha mnyororo baridi. Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk. Hussein Mwinyi alisema ufunguzi wa gahala hilo ni sehemu ya kutekeleza mpango mkakati wa MSD wa kuhakikisha upatikanaji wa dawa na vifaa tiba vyenye ubora unaokubalika na kwa bei nafuu.
   "Mpango huu umeandaliwa kwa kuzingatia Sera ya Afya ya kufikisha huduma bora za afya kwa kila Mtanzania" alisema Mwinyi. Alisema vyumba vya kuhifadhia chanjo na magari maalumu ya kusafirishia chanjo uliozinduliwa vitasaidia katika kutunza na kusafirisha chanjo katika hali ya ubaridi kwa mujibu wa miongozo ya Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) ambayo Tanzania inatekeleza. 
   Alisema ghala hilo linauwezo wa kuhifadhi dawa na vifaa tiba lina mita za mraba 4,280 na kuwa limejengwa kwa msaada wa Serikali ya Marekani na Mfuko wa Dunia wa Kupambana na Ukimwi, Kifua Kikuu, Malaria na limegharimu jumla ya Dola za Marekani milioni 4 sawa na takribani sh.bilioni 6.4 za Kitanzania. Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Cosmas Mwaifwani alisema ujenzi wa ghala hilo ni matunda yaliyotokana na safari za Rais Kikwete nje ya nchi hususan Marekani ambapo mei 2 mwaka 2009 akiwa katika ziara nchini Marekani Rais wa nchi hiyo Barack Obama aliahidi kuendelea kutoa misaada katika maeneo mbalimbali likiwemo la kuboresha huduma za kupambana na maradhi ya Ukimwi kupitia shirika la PEPFAR. 
   Alisema moja ya miradi inayoratibiwa na PEPFAR ni ujenzi wa maghala makubwa katika kanda za Dar es Salaam, Dodoma, Mbeya, Tanga na Tabora. Mwaifwani alitumia fursa hiyo kumpongeza Rais Kikwete kwani matokeo ya juhudi zake zimeleta matunda ambayo yanaonekana kwa Taifa. 
   Alisema ukamilishwaji wa miradi hiyo utaisaidia Bohari ya Dawa kukomboa jumla ya shilingi za Tanzania bilioni 1 katika mwaka ujao wa fedha ambazo wamekuwa wakilipa kwa ajili ya kukodi maghala ya watu binafsi kwa ajili ya kuhifadhi dawa, vifaa tiba na vitendanishi kabla ya kusambazwa kwa walengwa. 
  Alisema Bohari ya Dawa imeendelea kutekeleza jukumu lake la msingi la kusambaza dawa na vifaa tiba katika vituo vya afya hapa nchini kwa niaba ya Serikali. Aliongeza kuwa katika kutekeleza majukumu hayo Bohari ya Dawa imefanikiwa kufanikisha upatikanaji wa dawa ambapo imefikia kati ya asilimia 70 hadi 75 ya mahitaji dhidi ya asilimia 44 wakati Taasisi hiyo ilipo anzishwa mwaka 1994. 
   Alisema mikoa 10 imeingizwa katika mfumo wa kufikisha dawa moja kwa moja hadi vituo vya afya na mikakati imewekwa ya kuingiza mikoa yote ya Tanzania katika mfumo huo kuanzia julai 2013 na kuwa mkakati huu unazihusu pia hospitali za Wilaya, Mikoa na Hospitali za Rufaa. Mwaifwani alisema MSD imefungua mfumo mpya wa kisasa wa TEHAMA (EPICOR) ili kurahisisha shughuli za usambaji ambao pia umefadhiliwa na USAID.

   Wafanyakazi wa Bohari ya Madawa (MSD), wakiwa kwenye hafla hiyo
   Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk.Hussein Mwinyi (wa pili kushoto), akikata utepe kuashiria upokeaji wa  magari  maalumu ya kusafirishia chanjo kwa kuzingatia mnyororo badiri. Kushoto ni Mwakilishi Mkazi wa Shirika la kuhudumia watoto duniani (UNICEF), DK. Jama Gulaid, Balozi wa Marekani nchini Alfonso Lenhardt na Mbunge wa Temeke Abbas Mtemvu. Mbali na kupokea magari hayo kwa niaba ya Rais Jakaya Kikwete, Dk. Mwinyi 
  alifungua Jengo la Kisasa la ghala la kuhifadhi dawa katika Makao Makuu ya Bohari ya dawa Dar es Salaam leo
   Kaimu Mganga Mkuu wa Serikali Dk.Donan Mmbando akihutubia kwenye sherehe hiyo.
   Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk.Hussein Mwinyi, akikata utepe kuashiria kupokea madawa na vifaa tiba vilivyotolewa na Madaktari wa Afrika kwa Serikali. Kutoka kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Cosmas Mwaifwani, Mkurugenzi wa Tiba wa Madaktari Afrika, Dk.Dilan Ellegale na Balozi wa Marekani nchini Alfonso Lenhardt.
   Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Cosmas Mwaifwani (kulia),akimuelekeza jambo Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk.Hussein 
  Mwinyi (kushoto), juu ya ubora wa ghala  jipya la kisasa la kuhifadhia dawa, baada ya kulizindua katika Makao Makuu ya Bohari ya Dawa (MSD), Dar es Salaam. Wa pili kushoto ni Mbunge Viti maalum Martha Mlata na Balozi wa Marekani nchini  Alfonso Lenhardt. 
   Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk. Hussein Mwinyi  (wa tatu kushoto waliokaa), akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Bohari ya madawa  (waliosimama nyuma). Kutoka kushoto ni Kaimu Mganga Mkuu wa Serikali Donan Mmbando, Balozi wa Marekani nchini Alfonso Lenhardt, Kaimu Mkurugenzi  Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Cosmas Mwaifwani, Mbunge wa Kigamboni Dk. Faustine Ndungululile, Mwakilishi Mkazi 
  wa Shirika la kuhudumia watoto duniani (UNICEF), DK. Jama Gulaid na Mbunge wa Temeke, Abbas Mtemvu.


  0 0
 • 02/12/13--02:17: taarifa ya msiba

 • Marehemu Mzee Wilfred Mahendeka Mtaki

  Ndugu Sospeter E Mtaki wa Kimara King’ong’o jijini Dar es Salaam, anasikitika kuwatangazia kifo cha baba yake Mzazi, Mzee Wilfred Mahendeka Mtaki kilichotokea Jumatatu, Februari 11, 2013 jijini Dar es Salaam.

  Mipango ya Mazishi inafanyika Nyumbani kwa mtoto wa Marehemu Kimara King’ong’o. Misa ya kumwombea Marehemu itafanyika Alhamisi Februari 14 kuanzia saa 5 asubuhi Katika Kanisa la Mt. Marie Clare Michungwani.

  Heshima za mwisho zitaanza saa 7 mchana na baade safari ya kuelekea kijijini kwake Kisorya-wilayani Bunda itaanza.

  Bwana Alioa na Bwana ametwaa- Jina lake Lihimidiwe.

  0 0

  Barabara ya Morogoro -Iringa imekuwa tegemezi kwa wasafirishaji hasa wanaosafirisha mizigo kwa kutumia magari makubwa kwenda nchi za jirani za Zambia na Malawi ikitokea Bandari ya Dar es Salaam.Kwa sasa ni kiunganishi kikubwa cha nchi hizo. Picha na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii.

  0 0

  CHAMA cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) kimefuta wazo la kuendesha mdahalo kwa wagombea wa nafasi za juu za uongozi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).

  Mdahalo huo ulikuwa ufanyike Februari 15, 2013 na tayari chama kilikuwa katika hatua nzuri ya mazungumzo na wadhamini pamoja na kituo kimoja cha televisheni kwa ajili ya kurusha 'live' tukio hilo, ambapo kesho ilikuwa tutangaze utaratibu mzima wa mdahalo huo.

  Katika mazungumzo ya leo na uongozi wa kituo hicho ambao hautaki tukitangaze, tumekubaliana kufuta wazo la mdahalo kwa sababu nafasi ya urais amebaki mgombea mmoja, hivyo mdahalo hautakuwa na tija.

  Dhamira ya awali ya kufanya mdahalo ilikuwa kuwapa fursa wapiga kura wasikie vyema sera za wagombea urais na Makamu wa Rais, ili wananchi wawasikilize wagombea hao na pia wapiga kura wawatambue vizuri.

  Hata hivyo TASWA itatafuta utaratibu mwingine mzuri ambao utawezesha wagombea kuzungumza na waandishi wa habari na kuulizwa maswali mbalimbali ambayo tunaamini kwa kiasi fulani yatasaidia wapiga kura katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Februari 24 mwaka huu. TASWA inawatakia kila la kheri wagombea wote wa TFF waliobakia.

  TASWA imekuwa ikifanya mdahalo kwa wagombea wa nafasi za juu kwenye uchaguzi wa TFF, ilifanya hivyo mwaka 2001 na mwaka 2004 ingawa haukuwa wa live, ikafanya wa live mwaka 2008, ambapo yote ilikuwa ya mafanikio makubwa.

  Nawasilisha.
  Amir Mhando
  Katibu Mkuu TASWA

  0 0

  Birthday boy Allan Rwechungura (kulia) akionyesha ishara ya peace akiwa na marafiki zake waliohudhulia hafla ya siku yake ya kuzaliwa iliyofanyika hivi karibuni kwenye kiota cha maraha cha Mel Moz,Mikocheni jijini Dar.
  Mdau Terence (kulia) akiwa na marafiki zake  Philly na Ombeni wakati wa hafla fupi ya kusherehekea kuzaliwa kwa rafiki yao Allan Rwechungura (hayupo pichani).
  Birthday Boy,Allan Rwechungura (kati) akiwa na warembo waliohudhulia kwenye hafla yake hiyo.

  0 0
 • 02/12/13--02:57: MSAADA TUTANI
 • WATANZANIA WENZANGU MIMI NI MDAU NINAYEISHI SWEDEN YA KUSINI. NINATAKA KUANZISHA KAMPUNI YA KUUZA MAGARI/ SPEA PARTS SWEDEN- TANZANIA. ILA KUNA CHALLANGES NDOGONDOGO NAPATA. KAMA YUPO MTU MWENYE AIDIAZ NA HILI, MWENYE KUTOA USHAURI AU ANAYEPENDA KUFANYA BIASHARA HII NA ANAISHI HAPA, NAOMBA TUWASILIANE KWA EMAIL:florence.mndeme@yahoo.com 

   ASANTE SANA

  0 0


older | 1 | .... | 40 | 41 | (Page 42) | 43 | 44 | .... | 3278 | newer