Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110091 articles
Browse latest View live

DK EMMANUEL NCHIMBI AZINDUA HUDUMA ZA DUTY FREE SHOPS KATIKA JESHI LA MAGEREZA. Posted: 08 Feb 2013 06:18 AM PST

$
0
0

 Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini, Kamishna Jenerali John Minja (kulia) akimkaribisha Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi (kushoto) kabla ya uzinduzi wa Supermarket ya kwanza katika Jeshi la Magereza nchini.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Supermarket ya kwanza ya Jeshi la Magereza nchini.
 Mkurugenzi wa Kampuni ya Military Shop, Afzal Meghji akimuonyesha bidhaa mbalimbali zilizopo ndani ya duka hilo, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi akizungumza na maafisa magereza (hawapo pichani) kabla ya kufungua Supermarket kubwa ya kisasa ambayo itawawezesha maafisa hao, askari na familia zao kupata huduma ya kununua bidhaa mbalimbali kwa bei nafuu. Kushoto ni Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Mbarak Abdulwakil, anayefuata ni Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini, John Minja na kulia ni Mwekezaji Mkuu wa Kampuni ya Military Shops ambaye ndiye aliyewekeza katika Supermarket hiyo, Sadrunin Virji. 
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmauel Nchimbi akipokea zawadi kutoka kwa mke wa Mwekezaji Mkuu wa Supermakert hiyo, Gulshan Virji (kulia).
 Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini, Kamishna Jenerali, John Minja akipokea zawadi kutoka kwa mke wa Mwekezaji Mkuu wa Supermakert hiyo, Gulshan Virji (kulia).
 Baadhi ya maafisa na askari Magereza wakinunua bidhaa mbalimbali katika Supermakert hiyo baada ya kuzinduliwa.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi (wa tatu kutoka kushoto waliokaa), Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Mbarak Abdulwakil (wa kwanza aliyekaa kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na maafisa mbalimbali wa magereza pamoja na wageni waalikwa.
 PICHA ZOTE NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

ngoma azipendazo ankal - enzi hizo

$
0
0

 Tancut Orchestra ya mjini Iringa enzi hizo walikuwa si mchezo. Hebu wacheki kina Abdul Salvador, John Kitime, Kasaloo Kyanga na Kyanga Songa, Kawelee Mutimana na wengineo wakikupa 'Safari sio kifo' katika mtindo wao wa Fimbo Lugoda

menyu mpya break point ya mjini

$
0
0
Hii ne menyu mpya katika kiota cha Break Point cha mjini, Dar es salaam

Taarifa za kinatharia Kupitia Vyombo vya Habari

$
0
0

Kama jibu  kwa taarifa za kupotosha za hivi karibuni kutoka kwa vyombo vya habari, Bodi ya fastjet ingependa kuchukua fursa hii kutoa ufafanuzi kuhusu taarifa zisizo za kweli na za kuchafua zilizotolewa na Don Smith wa fly540 Kenya.


Kampuni, kwa msisitizo mkubwa, inakataa madai yaliyotolewa na Don Smith kuhusu  wazo la ununuzi wa hisa ndani ya Fly540 Kenya pamoja na madai mengine mengi yaliyofanywa kupitia vyombo vya habari katika majuma ya hivi karibuni.


Akitoa kauli kuhusu madai ya hivi karibuni, mweyekiti wa fastjet David Lenigas alisema:


 “fastjet imenuia kufanya biashara zake katika hali ya uwazi, isiyofichika na ya kihalali kwa ujumla wake, kupitia itifaki zinazotakiwa. Kampuni hii haina nia ya kuendelea kukanusha madai ya uongo kupitia vyombo vya habari lakini itachukua hatua za kisheria kuhusu madai mengine zaidi kama hayo.”


“fastjet imemlipa Don Smith na wenzake zaidi ya Dola za Kimarekani milioni 6 kwa ajili ya hisa zake kwenye  Fly540 na nembo nyingine za kibiashara zinazohusiana na hiyo, na sasa kwa ari kubwa itachukua hatua kuhakikisha kuwa mikataba yake imetekelezwa.”


“Kampuni haitavumilia mikakati yoyote ya ulaghai na isiyo ya wazi. Masuala yaliyotungwa na Don Smith nchini Kenya hayatadhuru mpango wa jumla wa fastjet wa kuwa kampuni ya kwanza ya safari za ndege kwa Afrika nzima yenye gharama za chini”


 “Nafasi ya kampuni nchini Kenya, ambayo ni  sehemu ndogo tu ya upanuaji wetu, imeshawekwa salama kupitia mkataba wa makubaliano na Jetlink uliotangazwa wiki iliyopita. Tunahisi kuwa Jetlink, ambayo tayari ina ithibati ya  IOSA, ni mshirika mzuri zaidi wa fastjet ukizingatia viwango vyetu vya usalama na uaminikaji. Baada ya kufanya mapitio ya kina, tulitambua kuwa Jetlink itaweza kuipa fastjet msingi wa kudumu wa kuanzia kwa sababu ya uwezo wake mkubwa wa miundombinu na ithibati yake ya kiwango cha kutoa huduma na kusimamia ndege nyingi kubwa za kisasa”

“Afrika ina karibu asilimia 4% ya abiria wa safari za anga duniani lakini kwa bahati mbaya kwa sasa ndiyo yenye asilimia 25% ya ajali za ndege duniani. Dhima yetu ya kuleta usafiri salama kwa watu wa Afrika inahitaji viwango vya juu na uzingatiaji wa kila mara kuhakikisha kuwa haya yanatekelezwa.”


Mkurugenzi mkuu wa fastjet Ed Winter aliongeza: 
 “Pale ambapo madeni ya kihistoria yaliyoendelea kuongezwa na Don Smith na Fly540 yamekuja kuwa wazi baada ya umiliki, fastjet inafanya kazi kwa karibu na wadai wake ili kufikia muafaka unaoridhisha kwa pande zote zinazohusika. Hatukubaliani na viwango vya gharama ambavyo vimekuwa vikitamkwa katika vyombo vya habari hivi karibuni, na pale viwango vinavyodaiwa vinapotambulika, msivichukulie kwa umakini kuhusiana na biashara kwa ujumla. Masuala haya yaliyojitenga hayadhuru utendaji wa siku hadi siku wa fastjet au utendaji wowote wetu katika Angola au Ghana ambao wanasafirisha chini ya nembo nyingine ya Afrika ya Fly540”


 “fastjet itachukua hatua kurejesha madeni haya ambayo hayawekwi wazi na mengine yoyote yaliyomo chini ya waranti zilizotolewa na Don Smith na wenzake katika makubaliano yao ya kuuza hisa zao ndani ya Fly 540 Kenya na kuiuzia fastjet mwezi Juni mwaka jana”


Timu ya menejimenti ya fastjet inabaki kuwa ya wanaharakati wakubwa wa maendeleo ya kampuni, kujenga mafanikio yake Tanzania na ukuaji kuelekea kuweka demokrasia katika usafiri wa anga wa Afrika na kuwa shirika la kwanza  la usafiri wa anga barani Africa lenye gharama za chini


 “Kwa sasa, tunaendelea kufanya kazi na mamlaka zinazohusika katika mataifa mengine Afrika kupanua mtandao wa fastjet”




kuhusu utata wa Leseni ya Nembo na takwimu BOFYA HAPA


JK katika mkutano wa SADC nchini Msumbiji

$
0
0
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mwenyeji wake Rais Armando Emilio Guebuza wa Msumbiji wakiwa katika mkutano wa wakuu wa ncho za Jumuiya ya Maendeleo Kusini Mwa Afrika SADC jijini Maputo Msumbiji jana.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete, Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo(DRC) na Mwenyeji Rais Armando Guebuza wa Msumbiji wakati wa kikao cha SADC jijini Maputo jana(picha na Freddy Maro).

basata yabariki tamasha la pasaka

$
0
0

BARAZA la Sanaa la Taifa (Basata) limetoa kibali kwa ajili ya Tamasha la Pasaka linalotarajiwa kufanyika Machi 31 mwaka huu jijini Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama alisema katika taarifa yake kwa vyombo vya habari jana kuwa kutokana na kupata kibali hicho maandalizi rasmi sasa yameanza. “Nilikuwa Napata tabu hata kuanza kuhangaikia ukumbi ambao tutafanyia tamasha maana mwaka jana tulifanyia Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, sasa bado hatujaamua tutafanyia wapi kwa sababu ilikuwa hatuna kibali.

“Lakini hatua ya Basata kutupatia kibali inamaanisha tumepata baraka, hivyo tuendelee na mambo mengine ya maandalizi,” alisema Msama. Alisema wamepanga siku yenyewe ya Pasaka tamasha lifanyike Dar es Salaam na siku inayofuata bado wanaangalia wafanye wapi kwani mikoa mbalimbali imeomba ipewe uenyeji.


“Vipo vigezo tutaviangalia kwa wanaotaka tuwapelelekee, kama vitakuwa sawa basi tamasha litafanyika kwa watakaotimiza, lakini kwa sasa Jumatatu ya Pasaka bado hatujaamua wapi twende,” alisema Msama katika taarifa hiyo.


Tamasha la mwaka jana baadhi ya waimbaji mahiri waliokuwepo ni Rose Muhando, Rebecca Malope, Christina Shusho, Upendo Nkone, Upendo Kilahiro, Solomon Mukubwa, Atosha Kissava, Ephraim Sekeleti na kundi la Glorious Celebration.

Pia kwaya mahiri ya Kinondoni Revival, Mwinjilisti Faraja Ntaboba kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) zilikuwa miongoni mwa burudani zilizokuwepo siku hiyo.

harrymo body shop

$
0
0
Duka la products from US za bath n body na Victoria secret. Ni bath gel,lotion,body splash,perfume,home fragrance,hand sanitizers,miwani,accessories etc, hizi zote ni kwa wanawake na wanaume. kwa ajili ya valentine. duka liko makumbusho nyuma ya access bank. 
kwa mawasiliano Number  ni 0688704844.

MAAFISA HABARI WA SERIKALI WAMALIZA KIKAO CHAO MJINI DODOMA, WATEMBELEA BUNGE NA KUSHIRIKI ZOEZI LA UPANDAJI WA MITI CHUO KIKUU CHA DODOMA

$
0
0
Mkurugenzi msaidizi wa Idara ya Habari Bw. Raphael Hokororo akiwafundisha maafisa habari na mawasiliano wa serikali kutoka Wizara, Taasisi, wakala, mashirika ya Umma, mikoa na wilaya upigaji wa picha bora za mnato kwa matumizi ya habari wakati wa kuhitimisha kikao cha maafisa hao mjini Dodoma.
Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Bw. Clement Mshana ambaye alikua miongoni mwa waalikwa waliohudhuria kikao kazi cha maafisa habari na mawasiliano wa serikali akiongea na mafiasa hao mjini Dodoma.
Maafisa Habari na Mawasiliano wa Serikali wakiwa ndani ya Ukumbi wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mjini Dodoma kufuatia mwaliko wa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Anne Makinda na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara.
Maafisa habari na mawasiliano wa serikali wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kutoka nje ya Ukumbi wa Bunge mjini Dodoma.
Baadhi ya viongozi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Mkurugenzi wa Idara hiyo Bw. Assah Mwambene (wa nne kutoka kushoto) na Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari Usajili wa Magazeti Bw. Raphael Hokororo (wa pili kutoka kushoto) wakiwa wamesimama ndani ya ukumbi wa Bunge kuwasalimia waheshimiwa wabunge mara baada ya kuombwa na Mh. Spika wakiwaongoza maafisa habari wa serikali.
Maafisa Habari na Mawasiliano wa serikali wakiwasili Chuo Kikuu cha Dodoma kushiriki zoezi la upandaji wa miti chuoni hapo ikiwa ni sehemu ya mchango wao katika kuhifadhi mazingira ya chuo hicho.
Mhasibu mkuu msaidizi wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bw. Swalehe Chondoma akishiriki zoezi la upandaji wa miti katika kampasi ya chuo kikuu cha Dodoma.
Naibu katibu mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Sihaba Nkinga akizindua zoezi la upandaji wa miti lililowahusisha mafisa habari wa Serikali katika kampasi ya chuo kikuu Dodoma.
Maafisa habari na Mawasiliano wa Serikali wakiendelea na zoezi hilo Chuo kikuu cha Dodoma.Picha na Aron Msigwa – MAELEZO.

Taarifa kwa vyombo vya habari kutoka CCM

$
0
0
Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi itafanya Mkutano wake wa kawaida kuanzia tarehe 10 -11 /02/2013. Kikao hicho kitaongozwa na Mwenyekiti wa Taifa wa CCM, Dr. Jakaya Mrisho Kikwete.

Wajumbe wa NEC wanatarajiwa kufika Mjini Dodoma leo tarehe 9/02/2013,kwa ajili ya kikao hicho.

Pamoja na mambo mengine kikao hichi kitatanguliwa na Semina ya siku mbili kwa Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa.

Lengo la Semina hii ni kuwaongezea Wajumbe uelewa kuhusu masuala ya Chama Cha Mapinduzi na Serikali yake hasa ikizingatiwa kwamba wengi wa Wajumbe ni wapya kufuatia Uchaguzi Mkuu wa CCM wa mwaka 2012.

Mada zitakazowasilishwa kwenye Semina ni pamoja na;

1. Nafasi na Wajibu wa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa
2. Umuhimu wa Maadili kwa Viongozi na Watendaji wa Chama Cha Mapinduzi.
3. Mikakati ya kutekeleza maazimio ya Mkutano Mkuu wa Taifa wa nane wa CCM.
4. Mkakati wa kukuza ajira nchini.

Semina hii itafuatiwa na Mkutano rasmi wa Halmashauri Kuu ya Taifa ambao pamoja na mambo mengine utafanya Uchaguzi wa Wajumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi.

Imetolewa:​
Nape Moses Nnauye
KATIBU WA NEC – ITIKADI NA UENEZI
CHAMA CHA MAPINDUZI

CHAMA CHA AKIBA NA KUKOPA CHA JESHI LA MAGEREZA NCHINI (TPS-SACCOS) CHAPATA VIONGOZI WAPYA, MJINI MOROGORO

$
0
0
Kamishna wa Huduma za Urekebishaji wa Jeshi la Magereza, Dionece Chamulesile akitoa hotuba ya kuufunga Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Pili wa TPS Saccos uliofanyika mjini Morogoro.
Wajumbe wa Bodi ya TPS Saccos waliomaliza muda wao wakiondoka meza kuu na kuupisha uongozi mpya. Kulia ni aliyekuwa Mwenyekiti wa bodi hiyo, Dionece Chamulesile, wa katikati ni Dk Juma Malewa na Stanford Ntirundura waliokuwa wajumbe wa bodi hiyo.
Baadhi ya wajumbe wa mkutano huo wakifurahia kupata viongozi wapya watakaokiongoza chama hicho.
Baadhi ya viongozi wapya waliochaguliwa na wajumbe wa mkutano mkuu wa Chama cha Akiba na Kukopa cha Jeshi la Magereza (TPS Saccos) wakiwa mbele ya wajumbe hao (hawapo pichani). Kushoto ni Mwenyekiti mpya wa bodi hiyo, Joel Bukuku akizungumza na wajumbe hao. Uchaguzi huo umefanyika katika Hoteli ya Edema, mjini Morogoro.

Mdau Gustav Mwaifunga na Bi. Dorcas Dominic wameremeta leo jijini Dar

$
0
0
Mdau Gustav  Mwaifunga na Bi. Dorcas Dominic Kyoba wamemeremeta na kuwaka waka leo jijini dar es Salaam baada ya wote kwa pamoja kuamua kuamua kuachana na chama cha makapera.Mdau Gustav ni Muajiriwa wa kampuni ya MultiChoice Tanzania.
Maharushi wakiwa kwenye gari yao tayari kwa safari ya kwenda mnusoni.

Dkt Shein katika maulid Tumbatu, Jongowe

$
0
0
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein akikata utepe kufungua zawia ya Tumbatu Jongowe,alipohudhuria katika maulidi ya Mtume Muhamad (SAW)
yanayosomwa kila mwaka katika kijijini hapo
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,(kushoto)  akitia ubani kuyafungua Maulid ya Mtume Muhammad (SAW) yaliyofanyika jana  Tumbatu Jongowe,alipohudhuria akiwa mgeni rasmi,(kulia) Kadhi Mkuu Sheikh Khamis Haji
  Mwanafunzi Mhadi Haji Vuai, wa madrasa Nurmunawar ya Tumbatu Jongowe akisoma maulid ya Mtume Muhammad (SAW) mlango wa kwanza
 Wanafunzi wa madrasatul Maamur ya Tumbatu Jongowe wakisoma Qaswida wakati wa maulid ya Mtume Muhammad (SAW)
 Baadhi ya Akina Mama wa Tumbatu Jongowe na Vijiji Jirani walioalikwa katika maulidi ya Mtume Muhammad (SAW) wakiwa nje ya zawia  ya kijijini hapo palipofanyika Maulid hayo
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,(wa pili kushoto)  akitiliwa marashi wakati wa kumswalia Mtume Muhammad (SAW),yalipofanyika Maulid huko  Tumbatu
Jongowe j
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,akipokea zawadi maalum kutoka kwa mwanafunzi Mohamed Haji Mohamed,iliyotayarishwa na wazee wa Tumbatu
Jongowe wakati wa Maulid ya Mtume Muhammad (SAW),
Baadhi ya waumini wa Dini ya Kiislamu wa Tumbatu Jongowe na Vijiji Jirani walioalikwa katika maulidi ya Mtume Muhammad (SAW) wakiwa katika zawia ya  kijijini hapo palipofanyika Maulid hayo.

ngoma azipendazo ankal - enzi hizo

$
0
0

Msanii GATHO BEEVENS alipokuja na ngoma ya "Azalaki awa" alitetemesha kiasi. Sijui yuko wapi siku hizi

Orton na Zainab wameremeta

$
0
0
Mdau Orton Peterson Kiishweko akiwa kwenye pozi na mai waifu wake Zainab wakati wa mnuso wa kusherehekea kumeremeta kwao usiku huu kwenye ukumbi wa NSSF Waterfront hall jijini Dar.

Mdau Orton Peterson Kiishweko akiwa kwenye pozi na mai waifu wake Zainab wakifuria jambo usiku huu. Cheki video chini uone wana-Daily News na Habari Leo wanavyoserebuka na mwanahabari mwenzao

CHAMA CHA KUTETEA HAKI ZA WANAUME TANZANIA

$
0
0


 KATIBU WA UHAMASISHAJI WA  TANZANIA MEN'S RIGHTS ASSOCIATION (TAMRA) TAIFA BWANA HATIBU MGEJA (SHOTO) AKIWA NA MWEKA HAZINA WA TAMRA TAIFA BWANA JUMA KOMBO. KUPATA HABARI KAMIRI BOFYA HAPA

kazi na dawa

$
0
0

Picture
Spika wa Bunge, Mhe Anne Makinda akicheza muziki na Mnadhimu wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Mhe undu Lissu kwenye sherehe za kuuaga na kukaribisha mwaka mpya kwenye Viwanja vya Bunge Dodoma juzi usiku baada ya kuahirisha kikao cha Bunge.Picture
S

matokeo ya kidato cha nne bado hayajakamilika - NECTA

$
0
0

Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) limesema  matokeo ya kidato cha nne bado hayajakamilika na kuwa habari zilizozagaa wiki hii kuwa yapo tayari si za kweli.


Hata hivyo Baraza hilo limebainisha kuwa licha ya kutokamilika, matokeo hayo yanakaribia kutoka kwa mujibu wa  ratiba za baraza hilo ambapo hutakiwa kutoa matokeo hayo mwezi Februari.



 Ofisa Habari na Mawasiliano wa NECTA, John Nchimbi amesema uvumi wa kwamba matokeo hayo yako tayari ulitokana na kuzushwa kupitia mtandao wa kijamii (Facebook).



Alifafanua kwamba habari kuwa matokeo hayo yameanza kutoka kisirisiri kabla hayajatangazwa rasmi na kwamba hatua hiyo inalenga kuyachakachua, siyo taarifa sahihi.



Aliwataka wananchi kuwa makini na uvumi huo kwa vile endapo matokeo hayo yatakuwa tayari yatatangazwa na Katibu Mtendaji wa Baraza hilo na pia kuwekwa kwenye tovuti ya Baraza pamoja na wananchi kuweza kuyapata kupitia simu zao za mkononi.



ernest makulilo celebrates his son's 2nd birthday

$
0
0

Picture
Benedikt Fulbright Makulilo
WHEN LOOKING AT YOU, BENEDIKT,  HAPPY 2ND BIRTHDAY!


My dearest son, Benedikt Fulbright Makulilo,

Guess what Benedikt? It is another February 10th. On every change of calendar year, such day is very significant and special to you. It was on February 10th 2011 at 5:42pm Pacific Time when you were born. 

Today February 10th 2013 you have turned 2 years old. Celebration is not because of the change in date/number rather is the significant changes you have been through in growing as a person, how you have been influential to your mother and I as parents, spouses and persons. 

But above all, it all about you – you are such a big Blessing from God, and in every way your mother and I have to celebrate the Blessing. It is indicated in the Holy Bible, “…Children are a gift from God; they are real blessing…” (Psalm 127:3)

Kilimanjari Marathon wataja njia za mbio hizo mwaka huu

$
0
0

Picture
Waandaaji  wa mashindano ya  mbio za Kilimanjaro Marathon 2013 wametangaza kwamba mbio za mwaka huu zitafanyika katika njia zile zile zilizotumika mwaka jana. Mbio hizo limepangwa kufanyika Machi 3, mwaka huu mjini Moshi.

John Addison, Mkurugenzi Mtendaji wa Wild Frontiers, ambao ni waandaaji wa tukio hilo alisema katika taarifa jana kwamba njia zitakazotumika kwa ajili ya Kilimanjaro Marathon2013 ni kuanzia Uwanja wa chuo cha Ushirika (MUCCoBS) kuelekea katikati ya mji, na kisha kufuata barabara kuu ya kwenda Dar es Salaam kwa takriban kilomita 8 hadi 9, baadaye watageuka na kurudi Moshi mjini kupitia katikati ya mji, na badaaye watapandisha mwinuko kidogo kuelekea Mweka, “wanariadha watafurahia zaidi sehemu hii kwasababu ina mandhari ya kuvutia na kutakuwa na washangiliaji wengi  kando ya barabara”.

Addison anasema, “sehemu ya kupandisha kuelekea Mweka inahitaji kupanda kwa taratibu lakini kwa sababu Mlima Kilimanjaro ni kivutio na uwepo wa wananchi wanaoshangilia muda unaenda haraka na kuwasaidia wakimbiaji kumaliza mapema”.

Alisema kuwa kituo cha cha Mweka ambapo ndipo wanaridha waatakapogeukia ili kurudi uwanja wa Ushirika inakuwa ni takribani kilometa 32 tangu kuanza mbio ndefu ya kilomita 42. Baada ya hapo kipande kilichobaki inakuwa ni mteremko kuelekea uwanjani mwisho wa mbio na njia nzima ni mteremko tu.

Aliongeza kuwa kwa wale watakaoshiriki nusu Marathon, mbio zitaanzia uwanja wa MUCCoBS ambapo pako tambarare na baadae watapandisha kwenye mwinuko kidogo kuelekea Mweka kama ilivyo zile mbio ndefu kabla ya kurudi umbali wa takriban km 10, kuelekea tena uwanjani.

Kutakuwa na meza za maji kama ilivyo kawaida na magari maalum ya kunyunyizia maji mithili ya mvua kando ya barabara huduma ambazo zimeandaliwa maalum kuwafanya wanariadha waendelee kuwa na nguvu wakati wote wa mbio hizo.

Kuhusu burudani, Addison alisema kuwa hali ya uwanjani itakua ya kusisimua kutokana na burudani kali kutoka bendi za muziki wa nyumbani zitakazokuwepo, chakula cha kutosha, nyama choma na vinywaji na bila kusahau mbio za kujifurahisha za Vodacom 5km Fun Run ambazo pia zinatarajiwa kuleta msisimko wa aina yake.

“Ili kuhakikisha usalama wa wakimbiaji, baadhi ya barabara zitakuwa zimefungwa, asubuhi siku ya mbio, lakini kutakuwepo na njia mbadala kuzunguka mji kwa ajili ya wakazi wa Moshi. Wakazi wa Moshi ambao wanatarajia kukimbia pamoja na wakimbiaji wengine watakaofika Moshi mapema wanaweza kuanza mazoezi katika njia hizo hili kupata uzoefu wa njia na kujiandaa vizuri kwa ajili ya mbio.”

Mbio hizo zinaratibiwa na Executive Solutions na kudhaminiwa na Kilimanjaro PremiumLager, huku wadhamini wengine wa tukio hilo ni pamoja na Vodacom Tanzania (5km Fun Run), GAPCO (Nusu Marathon Walemavu), Tanga Cement, CFAO Motors, KK Security, Keys Hotel, TPC Sugar, TanzaniteOne, New Arusha Hoteli, Kilimanjaro Water, FastJet na Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu (UNFPA).

Balozi mpya wa Uingereza nchini Tanzania Dianna Melrose akaribishwa

Viewing all 110091 articles
Browse latest View live




Latest Images