Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 435 | 436 | (Page 437) | 438 | 439 | .... | 3272 | newer

  0 0

   Wafanyakazi wa Shirika la Nyumba la Taifa wakipita ya mgeni wa heshima Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Eng.Evarist Welle Ndikilo wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi mkoa wa Mwanza ,matembezi hayo yalihitimishwa kwenye uwanja wa CCM Kirumba.
   Wafanyakazi wa Mkemia Mkuu wa Serikali wakiingia uwanjani CCM Kirumba Mwanza wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi mkoa wa Mwanza .
   Wafanyakazi wa Idara ya Maliasili wakiingia uwanjani CCM Kirumba katika kuhitimisha siku ya wafanyakazi..
   Mahakama ya Tanzania wakiingia uwanja wa CCM Kirumba huku wakitanguliza ujumbe mzito.
   Kibanda cha Veta kilikuwa moja ya vibanda vilivyovutia kwenye maonyesho ya Siku ya Wafanyakazi zilizofanyika kwenye Uwanja wa CCM Kirumba mkoani Mwanza.
   Wafanyakazi wa Hospitali ya Bugando wakielekea kuingia kwenye matembezi ya mshikamano katika kusheherekea siku ya Wafanyakazi kwenye Viwanja vya CCM Kirumba.
  Wafanyakazi wa Halmashauri ya Jiji Mwanza wakipita ya mgeni wa heshima Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Eng.Evarist Welle Ndikilo wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi mkoa wa Mwanza ,matembezi hayo yalihitimishwa kwenye uwanja wa CCM Kirumba.


  0 0

  Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, akimkabidhi mfano wa hundi ya shilingi milioni 5, Herman Kachima, ambaye ni Msimamizi wa huduma kwa wateja wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, wakati wa maadhimisho ya siku ya wafanyakazi Duniani kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam leo.
  Mkurugenzi wa NSSF, Dkt. Ramadhan Dau (Wapili kulia), akiteta jambo na mkurugenzi mkuu wa PPF, William Erio, na mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya udhibiti wa mifuko ya hifadhi ya jamii, (SSRA), Irene Isaka (Kushoto), na mwenyekitinwa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabida (Juu), wakati wa maadhimisho ya siku ya wafanyakazi Duniani kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam leo.
  Rais Jakaya Kikwete, akimsalimia mjumbe wa bodi ya Mfuko wa Pensheni wa PPF, Mbaraka Igangula, wakati akiwasili kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam leo.
  Wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, wakipita kwenye maandamano mbele ya mgeni rasmi, rais Jakaya Kikwete (Hayupo pichani) kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam leo.
  Mkurugenzi Mkuu wa PPF, William Erio (Kushoto), akimsikiliza kwa makini, Naibu Katibu mMkuu wa Wizara ya Habari, Vijana na Michezo, Profesa Ole Gabriel, wakati wa maadhimisho ya siku ya Wafanyakazi Duniani kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam leo.

  0 0

  Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohd Shein kushoto anaepunga mkono akiyapokea maandamano ya Wafanyakazi wa Sekta mbalimbali katika Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani (May Day) yaliofanyika Hoteli ya Bwawani Mjini Zanzibar.
  Mashirika mbalimbali yakipita mbele ya Mgeni Rasmi hayupo pichani katika Maadhimisho ya siku ya Wafanyakazi Duniani (May Day) yaliofanyika Hoteli ya Bwawani Mjini Zanzibar.
  Wafanyakazi wa Wizara ya Habari Utamaduni Utalii na Michezo wakipita mbele ya Mgeni rasmi hayupo pichani katika maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani (May Day) yaliofanyika Hoteli ya Bwawani Mjini Zanzibar.
  Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohd Shein watatu kulia akishikana mikono pamoja na Viongozi mbalimbali wakiimba wimbo wa Mshikamano kwa wafanyakazi ndani ya Ukumbi wa Salama Holl Bwawani Hotel mjini Zanzibar ikiwa ni Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani (May Day). 
  Baadhi ya Mawaziri pamoja na Wananchi waliohudhuria katika Maadhimishi ya siku ya Wafanyakazi Duniani(May Day)wakiwa ndani ya Ukumbi wa Salama Holl Hoteli ya Bwawani mjini Zanzibar.PICHA NA YUSSUF SIMAI-MAELEZO ZANZIBAR

  0 0

  Anza Siku njema na NENO la MUNGU kila siku kwa kutembelea Ibada ya Kiswahili website na Ukurasa wa Ibada ya Kiswahili kwenye Facebook.
  **   **   **            ** www.iykcolumbus.org **         **   **   **

  NENO LA LEO: Yeremia 29:11, Maana nayajua mawazo ninayowawazia ninyi, asema Bwana, ni mawazo ya amani wala si ya mabaya, kuwapa ninyi tumaini siku zenu za mwisho.
   
  TAFAKARI: Inawezekana kuna mtu aliwahi kukwambia kuwa anakuwazia mema na mwisho wa siku ukaja kugundua kuwa alikudanganya. Lakini yupo ambaye hadanganyi, wala hatakuja kufanya hivyo. Mungu hutuwazia mawazo ya amani, vyote alivyokuzuia usifanye au usipate ni kwa usalama watu sisi. Majaribu ni mafunzo ya kukabiliana na maisha ya ulimwenguni. Tuendelee kumwamini katika kiza kinene cha maisha yetu, tuwe na hakika kuwa asubuhi yetu inakuja.
   
  SALA: Baba katika Jina la Yesu. Asante kwa mema yote uliyoniandalia katika maisha yangu. Ntaendelea kukuamini siku zote nikijua kuwa hutokuja kuniacha peke yangu. Kwa Jina la Yesu, Amina. (c) IYK_NENO

  0 0

  Sehemu ya wafanyakazi wa wizara ya Uchukuzi, wakiwa wamejipanga tayari kwa ajili ya kushiriki katika maandamano ya siku ya wafanyakazi Duniani yaliyofanyika Kitaifa Jijini Dar es Salaam, katika Uwanja Wa Taifa, jijini Dar es Salaam leo Asubuhi.


  0 0

   Mkurugenzi wa NSSF, Dkt. Mohammed Dau (Wapili kulia), na mkurugenzi mkuu wa PPF, William Erio, na mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya udhibiti wa mifuko ya hifadhi ya jamii, (SSRA), Irine Isaka (Kushoto), wakifuatilia maadhimisho ya siku ya wafanyakazi Duniani kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam leo.
   Rais Jakaya Kikwete, akimkabidhi hundi ya shilingi milioni 5, mfanyakazi bora wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Herman Kachima, wakati wan kilele cha siku ya Wafanyakazi Duniani ambapo kitaifa zilifanyika kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
  Wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, wakipita kwenye maandamano mbele ya mgeni rasmi, rais Jakaya Kikwete (Hayupo pichani) kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam leo.


  0 0

  Na Nathan Mtega wa demashonews,Songea
  SERIKALI ya mkoa wa Ruvuma imeendelea kuwasihi wafanyakazi wa sekta zote nchini wasijenge zaidi utamaduni wa kudai haki bila kutimiza wajibuwao kwanza kwa sababu kauli mbiu za vyama vingi vya wqafanyakazi kikiwemo chama cha walimu nchini ambacho kauli mbiu yake  ni wajibu na haki.
   Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo,Mh. Abdula Lutavi
   -----------------
  Kauili hiyo imetolewa na mkuu wa wilaya ya Namtumbo Abdula Lutavi kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Ruvuma kwenye maadhimisho ya siku ya wafanyakazi yaliyofanyika kimkoa katika uwanja wa Maji maji mjini Songea ambapo amesema baadhi ya wafanyakazi wakiwemo walimu wamekuwa hawatimizi wajibu wao ipasavyo lakini ndiyo wanakuwa msitari wa mbele kulaumu na kudai haki pasipo kutimiza wajibu wao kwanza kwa mwajiri.
  Wanafunzi wa Chuo cha VETA Songea wakipita mbele ya jukwaa kuu huku wakionyesha mavazi wanayoshona chuoni hapo ikiwemo mavazi la maharusi na ya ulimbwende.
  -----------------------------------
  Amesema sekta ya elimu ndiyo yenye watumishi wengi ambao wapo katika kila kijiji nchini na ndiyo wataalamu wanaotumiwa na wananchi wa maeneo hayo lakini baadhi yao wamekuwa ni watoro na wazembe katika maeneo yao ya kazi na kutotimiza wajibu wao kwa makusudi na kwa visingizio mbali mbali na wakiendelea kulindwa na walimu wakuu pamoja na wakuu wa idara za kielimu hali ambayo inazidi kudumaza kiwango cha elimu mkoani Ruvuma na kuufanya mkoa kuendelea kutofanya vizuri katika sekta hiyo muhimu.

  BOFYA HAPA KWA PICHA NA HABARI KAMILI

  0 0

  Wafanyakazi wa magazeti ya serikali wa Tanzania Standard Newspapers ltd. (TSN) wachapishaji wa Daily News, Habari Leo na Sunday News wakipita kwa bashasha mbele ya mgeni rasmi karika sherehe za Mei Mosi mwaka huu katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam wakiwa na mabango na magazeti yao mkononi.
  TSN Oyeeeeeee.....
  Mzee mzima Michael Mbiro akiwa na vijana wake
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete na viongozi wengine wakiwapungia wana TSN wakati wanapita mbele yao. Rais ndiye Editor-in-Chief (Mhariri Kiongozi) wa magazeti ya serikali.
  Kwa picha zaidi BOFYA HAPA  0 0
  0 0

  Na Mwandishi Maalum 
  Tanzania imeendelea kusisitiza kwamba, nchi ambazo hazina mpango wa kuwa na silaha za nyukilia basi ziwe na haki ya kutumia nyukilia kwa matumizi salama, na pia kupewa misaada ya kiufudi na uwezeshwaji katika eneo hilo 
  Hayo yameelezwa na Naibu Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Ramadhan Mwinyi wakati alipokuwa akitoa maoni ya Tanzania katika mkutano wa Kamati ya Maandalizi kwaajili ya mkutano utakaofanyia tathmini utekelezaji wa Mkataba wa kuzuia usambazaji holela wa silaha za nyukilia ( NPT). 
   Tanzania inashiriki kikamilifu katika Mkutano huo wa maandalizi ambao ni wa wiki mbili na unafanyika Hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa. Wanaoshiriki mkutano huu ni nchi wanachama wa NPT pamoja na wawakilishi wa mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs). 
  Dhumuni la mkutano huu wa maandalizi, ni kuaanda dondoo na mapendekezo yatakayojadiliwa katika mkutano wa tathmini kuhusu NPT. Mkutano huo unatarajiwa kufanyika mwakani (2015). Akizungumza kwa niaba ya Tanzania, Naibu Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Ramadhan Mwinyi, amesema, kama Tanzania na kama ilivyo kwa mataifa mengi ingepeda kuona silaha za nyukilia zinatoweka katika uso wa dunia. 
  Lakini inaamini kwamba kila nchi Tanzania ikiwamo inayo haki ya kuwa na fursa ya kutumia nyukilia kwa masuala salama. Mwakilishi huyo wa Tanzania, amebainisha kwamba, hakuna asiyetambua madhara ya silaha za nyukilia kutokana matukioa kadhaa mbayo yametokea huko nyuma yakiwamo ya Hiroshima. 
   Akatahadharisha kwamba kuna dalili za wazi ya kujirudia kwa madhara hayo kwa kile alichosema Jumuiya ya kimataifa na hasa kwa nchi ambazo zimejilimbikizia silaha hizo hazitaki konyesha nia ya kweli ya kuachana nazo. 
  Akasema, inasikitisha kwamba yale mataifa ambayo yana malimbikizo ya silaha hizo, yameendelea kushikilia misimamo yao na hata kufikia mahali pa kutetea uhalali wa kuwa na silaha hizo. Tanzania ikaeleza kwamba, silaha za nyukilia si tisho kubwa kwa nchi za Afrika, kwani tishio kubwa na ambalo linachangia katika uvunjifu wa Amani na upotevu wa maisha ya watu ni silaha ndogo ndogo na nyepesi na siyo silaha za nyukilia. 
  Balozi Mwinyi amewahoji washiriki wa mkutano huo, kwamba ni dunia ya aina gani tunayotaka kuwarithisha watoto wetu kwa kuendelea kukumbatia silaha hizo za maangamizi. 
   Akabainisha kwamba Tanzania inaamini katika Mkataba huo wa NPT kwa kile alichosema utekelezaji wake utaifanya dunia kuwa mahali salama. Na kwamba licha ya kuridhia mkataba huo, Tanzania pia ni mwanachama wa mikataba mingine ya kikanda inayohusu uthibiti wa silaha za nyukilia.
  Mkutano wa Maandalizi  kwaajili ya  Mkutano utakaofanyika  mwakani kuhusu tathmini ya  Mkataza wa  Kuzuia Usambaaji Holela wa Silaha za Nyukilia ( NPT) unaendelea hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa,  pichani ni  Naibu Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa,  Balozi Ramadhan Mwinyi akitoa mchango wa Tanzania katika Mkutano huo wa wiki mbili. Aliyekaa  nyuma  ya Balozi Mwinyi, ni  Luteni Dkt. Edward Massala  kutoka Jeshi la Wananchi wa Tanzania ( JWTZ) ambaye ni sehemu ya ujumbe wa Tanzania katika Mkutano huu.

  0 0

   Mzee wa Kipepeo Tours akiwa vakesheni New York , hapa ni uwanja wa Barclays. Huyu ni mmoja wa wadau muhimu walioipa support Globu ya Jamii tangu inaanzishwa na hadi leo yuko nasi bega kwa bega
  Mzee wa Kipepeo na askari huko New York 

  0 0

   Baadhi ya wakulima wa vikundi vya Msange na Changamkeni wa Kijiji cha Vilima Vitatu, Kata ya Nkaiti, Tarafa ya Mbugwe, Wilaya ya Babati, Mkoani Manyara, wakijaribu mashine yao ya kukamulia ufuta baada ya kukabidhiwa jana na Ofisa Masoko wa shirika la Farm Africa, Rahel Pazzia, ambapo shirika hilo liligawa mashine 10 kwenye vikundi 18 vya wakulima wa Tarafa hiyo.
  Wakulima wa vikundi vya Mkombozi na Shamabo wa Kijiji cha Shaurimoyo, Kata ya Nkaiti Tarafa ya Mbugwe, Wilaya ya Babati, Mkoani Manyara, wakijaribu mashine yao ya kukamua ufuta baada ya kukabidhiwa  na Ofisa Masoko wa shirika la Farm Africa, Rahel Pazzia, ambapo shirika hilo liligawa mashine 10 kwenye vikundi 18 vya wakulima wa Tarafa hiyo.
   Ofisa Masoko wa shirika la Farm Africa Rahel Pazzia, kulia akiwakabidhi mashine ya kukamua ufuta wana kikundi wa wakulima wa ufuta wa kikundi cha Faraja na Chemchem kwenye Kijiji cha Vilima Vitatu, Wilaya ni Babati Mkoani Manyara
   Wakulima wa ufuta wa vikundi vya Mkombozi na Shamabo wa Kijiji cha Shaurimoyo, Kata ya Mwada Wilaya ya Babati Mkoani Manyara, wakiwa na mashine yao ya kukamulia ufuta iliyotolewa na shirika la Farm Africa, ambapo shirika hilo liligawa mashine 10 kwa vikundi 18 vya ufuta katika Tarafa ya Mbugwe.
  Wanakikundi wa Sayuni na Mti wa maziwa, wakulima wa ufuta wa Kijiji cha Ngolley Wilaya ya Babati Mkoani Manyara, wakiwa na mashine yao ya kukamua ufuta baada ya kukabidhiwa na Ofisa Masoko wa shirika la Farm Africa, Rahel Pazzia.

  0 0

  Organised jointly by the Tanzanian Training Centre for International Health, Ifakara, Tanzania, and the Swiss Tropical and Public Health Institute with the financial support of the Impact malaria, a Sanofi Access to Medicines program and the Swiss Agency for Development and Cooperation, the Malaria course is a tutorial that is aimed at strengthening competence of researchers, public health personnel and care givers to fight Malaria in Africa. Participants are taught how to conduct control programs, and learn by themselves using new communication technologies. They are involved in an active learning-teaching exercise, supported by specialized tutors. The learning process is based on self and e-learning, group discussions and extensive exchanges between the participants themselves and the experts.


  The course will take place from September 14th to October 11th2014 in Ifakara, United Republic of Tanzania, at Tanzanian Training Centre for International Health. 16 participants, mainly from East Africa, will be selected according to their profile, professional status, and letter of motivation and recommendation. The minimum requirement is a BSc or Master degree, several years of professional experience and basic computer skills (at least Word processing or equivalent).

  The tutorial lasts 4 weeks, each on focusing on one or two topics. The course will be held by experienced experts from Africa, Europe and Asia. The course is taught in English.

  Registration fee are 400 USD per participant. Course fees as well as travel, accommodation and food expenses will be taken care by the organizers health insurance are at the expense of the participants.


  Contact

  Mr.Kirungi Ruteganya


  +255782436637


  0 0

   Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Swissport Tanzania Bw Gaudence Kilasara Temu akizungumza na wanahisa wa kampuni hiyo wakati wa mkutano wao Mkuu wa Mwaka uliyofanyika jijini Dar es Salaam Jumatano jioni.
   Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa kampuni ya Swissport Tanzania Jeroen de Clercqakizungumza na wanahisa wa kampuni hiyo wakati wa mkutano wao Mkuu wa Mwaka uliyofanyika jijini Dar es Salaam Jumatano jioni. Wapili kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya hiyo Bw Gaudence Kilasara Temu akifuatiwa na mmoja wa wakurugenzi wa bodi Bw. George Fumbuka. 
   Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Swissport Tanzania Bw. Gaudence Kilasara Temu akizungumza na waandishi wa habari nje ya mkutano mkuu wa mwaka wa kampuni yake uliyofanyika Jumatano jioni jijini Dar es Salaam. 
   Afisa Fedha Mkuu wa kampuni ya Swissport Tanzania Mrisho Yassin akiwaongoza wanahisa kupitia ripoti ya mahesabu ya fedha ya mwaka 2013, wakati wa Mkutano Mkuu wa Wanahisa wa kampuni hiyo uliyofanyika jijini Dar es Salaam Jumatano jioni. Wapili kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya hiyo Bw Gaudence Kilasara Temu akifuatiwa na mmoja wa wakurugenzi wa bodi Bw. George Fumbuka na Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Bw. Jeroen de Clercq.   
  Mmoja wa wanahisa wa kampuni ya Swissport Tanzania akichangia mada wakati wa mkutano mkuu wa mwaka wa wanahisa wa kampuni hiyo uliyofanyika jijini Dar es Salaam Jumatano jioni.

  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,Dkt Rehema Nchimbi jana aliongoza mamia ya wafanyakazi wa Mkoa wake katika kusheherekea siku ya wafanyakazi Duniani inayoadhimisha kila ifikapo tarehe 1 Mei. Wafanyakazi hao kutoka Serikali kuu,Taasisi mbalimbali za Umma ,Serikali za mitaa Pamoja na sekta binafsi wamejitokeza kwa wingi na kusheherekea sikukuu ya wafanyakazi Duniani ambayo imesheherekewa kimkoa katika uwanja wa Jamhuri Mkoa wa Dodoma. Wakiongozwa na viongozi wao wa vyama vya wafanyakazi walioalanza kwa mandamano kutoka zilipo Ofisi za Bunge hadi uwanja wa Jamhuri na kupokelewa na Mgeni Rasmi ambaye alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt Rehema Nchimbi.
  Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,Dkt. Rehema Nchimbi (wa tatu kushoto) akiwaongoza wafanykazi wa Mkoa wake kuimba wimbo wa mshikamano wakiwa wameshikana mikono.Mara baada ya kupokea maandamano ya wafanyakazi wa Mkoa wake katika uwanja wa Jamhuri.
  Wafanyakazi wakishangilia maadhimisho ya siku ya wafanyakazi adauniani katika uwanja wa Jamhuri Dodoma.
  Mkuu wa mkoa wa Dodoma,Dkt. Rehema Nchimi akiwahutubia wafanyakazi wa Mkoa wake katika kilele cha maadhimisho ya siku ya wafanyakazi Duniani ambayo Kimkoa imefanyika katika Uwanja wa Jamhuri Dodoma
  Mkuu wa Mkoa Dkt Rehema Nchimbi aliyekaa akiwa katika picha ya pamoja na washindi wa jumla wa Mei Mos Kimkoa ambao ni chama cha Wafanyakazi wa serikali kuu na Afya TUGHE. Na Deusdedit Moshi Mtendaji Mkuu wa Photo Solutions wawakilishi wa Michuzi Blog Kanda ya Kati Dodoma.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0


  Kampuni ya Clouds Media International leo imetangaza kuwa imepewa leseni ya kurusha  matangazo  katika nchi za umoja wa falme za kiarabu (UAE).  Akielezea kuhusu leseni hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni  hiyo Bwana Joseph Kusaga, amesema  sasa kituo cha  Clouds TV kimataifa kitakuwa kikishuhudiwa na watu wa mataifa mbalimbali.

  Clouds TV kimataifa ni mwendelezo wa televisheni maarufu sana kwa vijana  nchini Tanzania,  hata hivyo sehemu kubwa ya maudhui yatakayokuwemo kwenye Clouds TV kimataifa itakuwa na mpangilio mpana wa vipindi kwa watazamaji vitakavyorushwa kwa  lugha za Kiingereza na Kifaransa. Akieleza zaidi Kusaga amesema "Leo ni siku ya  kihistoria na alama ya hatua moja katika mpango wetu wa kina wa kupeleka maudhui ya Clouds TV kimataifa kupitia  matangazo kwa njia ya  mitandao’’.

  Clouds TV kimataifa  haitotoa tu burudani, lakini pia itakuwa kiunganishi kwa waafrika waishio katika umoja wa nchi za falme za kiarabu pamoja na kuwapa fursa za kutangaza bidhaa zao na kuimarisha uhusiano baina yao.

  Vituo vya televisheni katika Umoja wa falme za kiarabu vipo vingi na vyenye ushindani mkubwa, lakini Clouds TV kimataifa imebahatika kupata nafasi ya kurusha matangazo yatakayowafikia walengwa katika chaneli yenye uwezo wa kuwahudumia zaidi ya watazamaji  takribani milioni 3.5 kutoka katika nchi za Afrika. Kwa sasa hakuna kituo kinachotoa huduma hii na hivyo kuwa fursa muhimu kwa watazamaji.

  Clouds TV kimataifa itarusha vipindi vya burudani, tamthilia, maigizo, ucheshi, na muziki, vyote vitakavyo kuwa vimeandaliwa kutoka nchi za mashariki, magharibi na kusini mwa bara la afrika na itapatikana kwa watazamaji walio katika Umoja wa falme za kiarabu kupitia huduma ya IPTV inayotolewa  na Etisalat na Du.

  Clouds TV kimataifa itarushwa kupitia mamlaka ya Abu Dhabi ijulikanayo kama twofour54, ikiungana na vituo kama FOX na CNN. Clouds TV kimataifa itaanza kurusha matangazo ya  majaribio katika wiki chache zijazo kabla ya tarehe 15 mwezi June mwaka huu.

  0 0  0 0

  Kiongozi wa UKAWA Freeman Mbowe, akihutubia katika mkutano wa hadhara katika viwanja vya Gombani ya Kale, Chake Chake Pemba.
  Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi James Mbatia, akihutubia katika mkutano wa hadhara katika viwanja vya Gombani ya Kale, Chake Chake Pemba.
  Mwenyekiti wa CUF Prof. Ibrahim Lipumba, akihutubia katika mkutano wa hadhara katika viwanja vya Gombani ya Kale, Chake Chake Pemba.
  Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad, akihutubia katika mkutano wa hadhara katika viwanja vya Gombani ya Kale, Chake Chake Pemba.
  Baadhi ya viongozi wa UKAWA na wananchi wakisikiliza kwa makini hotuba Maalim Seif, katika mkutano wa hadhara uliofanyika viwanja vya Gombani ya Kale, Chake Chake Pemba.
  Wafuasi na wapenzi wa vyama vya upinzani wakifuatilia mkutano wa UKAWA uliofanyika viwanja vya Gombani ya Kale, Chake Chake Pemba. (Picha na Salmin Said, OMKR).

  BOFYA HAPA KWA HABARI KAMILI

  0 0

  Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wakisheherekea Siku ya Wafanyakazi Duniani, iliyofanyika katika Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam. Mgeni rasmi kwenye maadhimisho hayo alikuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete. Kauli mbiu ya maadhimisho ya mwaka huu ni "UTAWALA BORA UTUMIKE KUTATUA KERO ZA WAFANYAKAZI"
  Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wakiwa kati maandamano
  Maandamano yakiwa yameshika kasi
  Maandamano yakiendelea
  Rais wa Jamhuri ya Muungano akiwapungia mkono Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa (hawapo pichani) walipopita kwa heshima mbele yake.
  Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wakipita mbele ya mgeni rasmi (hayupo pichani) wakiwa wamejawa na furaha na bashasha.

  Picha na Reginald Philip

  0 0

  Mkutano mkubwa wa Kimataifa wa Wafadhili { Donor Conference } kwa ajili ya kustawisha Maendeleo ya Kiuchumi na Kijamii ya Zanzibar unatarajiwa kufanyika robo mwaka ya mwisho ya mwaka huu hapa Zanzibar baada kukamilika kwa mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

  Mkutano huo utakofadhiliwa na Serikali ya Oman unatatarajiwa pia kujumuisha Wawekezaji wa sekta ya fedha na uchumi kutoka Mataifa na Taasisi tofauti Duniani . Mjumbe Maalum wa Serikali ya Oman Bwana Yahya Al – Ureim alieleza hayo wakati akizungumza na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar kuwasilisha ombi rasmi la Oman la kutaka kugharamia Mkutano huo.

  Bwana Yahya alimueleza Balozi Seif kwamba taratibu zimeanza kuchukuliwa katika kuona wafadhili pamoja na Wawekezaji wa Mataifa ya Ulaya, Carribean na Afrika wanashiriki katika Mkutano huo. “ Mambo mawili yatakayobeba Mkutano huo wa kimataifa katika kusaidia ustawi wa Uchumi wa Zanzibar yatajikita zaidi katika masuala ya ufadhili pamoja na uwekezaji “. Alifafanua Bwana Yahya.

  Mjumbe huyo Maalum wa Serikali ya Oman alifahamisha kwamba ujio wake hapa Zanzibar tayari ameshakutana kwa mazungumzo ya awali na Viongozi wa ngazi za juu wa Wizara ya Fedha Zanzibar ili kuanza maandalizi ya kuratibu sulala hilo. Akitoa shukrani zake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alielezea faraja yake kutokana na wazo hilo la Serikali ya Oman lenye kuonyesha upendo wa uhusiano wa muda mrefu uliopo kati ya pande hizo mbili.

  Balozi Seif alisema uamuzi huo wa Oman umekuja wakati muwafaka kwa vile unalenga kusaidia kustawisha Maendeleo ya Wananachi wa Zanzibar ambao wamekuwa na mafungamano makubwa na ndugu zao wa Oman. Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alimuhakikishia Mjumbe huyo Maalum wa Serikali ya Oman kwamba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itajitahidi kutoa kila msaada utakaostahiki wa ushirikiano katika kuona Mkutano huo wa Kimataifa wa Wafadhili kwa ajili ya Zanzibar unafanikiwa vyema.

  Balozi Seif ameendelea kuipongeza Serikali ya Oman kwa misaada yake mbali mbali ya Maendeleo inayotoa kwa Zanzibar ikiashiria Historia ya muda mrefu iliyopo kati ya pande hizo mbili. Alisema Zanzibar na Oman zimekuwa na Uhusiano wa miaka mingi unaotokana na maingiliano ya kidamu ya wananchi wake.
  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akisalimiana na Balozi Mdogo Mteule wa Oman aliyepo Zanzibar Bwana Ali Radhid anayetarajiwa kuanza kazi zake Zanzibar baada ya kukamilisha taratibu wa Kidiplomasia. Kati kati yao ni Mjumbe Maalum wa Serikali ya Oman Bwana Yahya Al –Ureim aliyefika Zanzibar kuwasilisha ombi la Serikali yake la kutaka kufanyika kwa Mkutano wa Kimataifa wa Wafadhi kwa ajili ya Zanzibar.
  Mjumbe Maalum wa Serikali ya Oman Bwana Yahya Al –Ureim kati kati akimtambulisha rasmi Balozi Mdogo Mteule wa Oman hapa Zanzibar Bwana Ali Rashid kwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Vuga Mjini Zanzibar.
  Mjumbe Maalum wa Serikali ya Oman Bwana Yahya Al –Ureim akiwasilisha ombi la Serikali yake la kutaka kufanyika kwa Mkutano Mkubwa wa Kimataifa wa Wafadhi kwa ajili ya Zanzibar. Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.

older | 1 | .... | 435 | 436 | (Page 437) | 438 | 439 | .... | 3272 | newer