Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live

DKT BILAL MGENI RASMI UZINDUZI WA MBIO ZA MWENGE WA UHURU

$
0
0
Na Concilia Niyibitanga MAELEZO 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Gharib Bilal, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru 2014, katika uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba, mkoani Kagera Mei tarehe 2. Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dkt. Fenella Mukangara wakati akiongea na Waandishi wa Habari Mjini Bukoba kuhusu Mbio hizo.

Mwenge huo utakaobeba ujumbe usemao “Katiba ni Sheria Kuu ya Nchi” wenye kauli mbiu “Jitokeze kupiga kura ya maoni tupate Katiba Mpya” utakimbizwa katika Halmashauri/Manispaa 165 za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kilele chake kitakuwa Mkoani Tabora tarehe14/10/2014.

Ujumbe kuhusu mabadiliko ya Katiba kwa mwaka huu, umeandaliwa mahususi kwa lengo la kuwahimiza wananchi kuendelea kushiriki kikamilifu katika mchakato wa kutengeneza Katiba Mpya unaoendelea hivi sasa ambao mwisho wake ni wananchi kupiga kura ya maoni ili tupate Katiba Mpya iliyoboreshwa kwa maendeleo ya Taifa letu. Amesema Dkt. Mukangara.

Amesema kuwa ujumbe huu utaambatana na kauli za uhamasishaji kuhusu mapambano dhidi ya UKIMWI, Malaria, Rushwa na Matumizi ya Dawa za Kulevya. Dkt. Mukangara ameeleza kuwa nchi yetu bado inakabiliwa na changamoto ya ugonjwa hatari wa UKIMWI, Malaria, matumizi ya dawa za kulevya na rushwa, hivyo mwaka huu kupitia Mbio za Mwenge wa Uhuru Serikali itaendelea kuwahimiza wananchi kupambana kwa dhati ili kumaliza changamoto hii inayoathiri maisha ya Watanzania.

“Hata hivyo, Mbio za Mwenge wa Uhuru pamoja na kuendelea kuhimiza umuhimu wa amani, umoja na mshikamano wa Kitaifa; Serikali kupitia Mbio hizi imekuwa ikiwahamasisha Wananchi, Mashirika, Taasisi na Wadau mbalimbali kuchangia kwa hali na mali kufanikisha miradi mbalimbali ya maendeleo”. Amesema Dkt. Mukangara.

Amekumbusha kuwa falsafa ya Mwenge wa Uhuru ni kumulika maovu ndani na nje ya mipaka ya nchi yetu, kuleta matumaini ambapo hakuna matumaini, upendo mahali palipo na chuki na heshima palipojaa dharau.

Aidha, Dkt. Mukangara ametoa wito wito kwa wananchi hasa kwa vijana wa Tanzania kutumia Mbio za Mwenge wa Uhuru kwa lengo la kuimarisha amani, upendo na umoja wa Kitaifa.

Pia amewataka wananchi kutumia ujumbe wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kama chachu ya kuleta mabadiliko ya kijamii hususani pale inapotolewa elimu kuhusu Mapambano dhidi ya UKIMWI, mapambano dhidi ya Rushwa na mapambano dhidi ya Dawa za Kulevya.

Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa huratibiwa kwa pamoja kati ya Wizara ya Habari Vijana, Utamaduni na Michezo (Tanzania Bara) na Wizara ya Uwezeshaji, Ustawi wa Jamii, Vijana, Wanawake na Watoto (Zanzibar).

NEWS ALERT: MTU MMOJA AJINYONGA KWA RAFIKI YAKE KWA KUTUMIA KANGA

$
0
0
Na John Gagarini, Kibaha 

 KIJANA Victor Wilfred (29) mkazi wa Keko jijini Dar es Salaam amekufa kwa kujinyonga kwa kutumia kanga aliyoifunga kwenye dirisha la chumba cha rafiki yake.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda wa Polisi mkoani Pwani Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi SACP Ulrich Matei alisema kuwa marehemu alifika kwa rafiki yake hapa Kibaha kwa lengo la kutafutiwa kazi.

Kamanda Matei amesema kuwa tukio hilo lilitokea leo Aprili 30 mwaka huu majira ya saa 5 asubuhi eneo la Maili Moja Shuleni wilayani Kibaha mkoani Pwani ambapo umati wa watu ulikuwa umejazana kushuhudia tukio hilo la kusikitisha.

Alisema kuwa tukio hilo ambalo lilitokea kwenye sebule ya chumba cha Emanuel Lawrance mkazi wa Keko Jijini Dar es Salaam ambaye amepangisha nyumba kwa Emanuel Msengi ambapo marehemu alikuwa mgeni kwenye nyumba hiyo na alifika kwa lengo la kutafuta kazi.

"Marehemu aliachwa na rafiki yake ambaye alikuwa amekwenda kazini na kwa kuwa rafiki yake alimuahidi kumtafutia kazi na aliporudi alikuta marehemu kajinyonga kwa kutumia kanga kwenye dirisha la chumba hicho," alisema Kamanda Matei.

Hata hivyo marehemu aliacha ujumbe kwenye karatasi lililokutwa pembeni ya mwili wake kuwa kutokanana na kifo chake anaomba samahani na asisumbuliwe mtu yoyote kwani kaamua kujiua yeye mwenyewe.

Matukio ya Kuaga mwili wa askari aliyeuawa na majambazi Tabora

$
0
0
Kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora ACP. Suzan Kaganda leo tarehe 30/04/2014 jioni amewaongoza waombelezaji na watendaji kutoka vyombo vya usalama, askari, taasisi za serikali na zisizo kiserikali za mkoa wa Tabora kuuaga mwili wa Askari PC JUMANNE ambaye aliyefariki baada kupigwa risasi na majambazi akiwa katika majukumu ya utendaji kazi.
Mwili wa marehemu PC JUMANNE ukishushwa 
kupelekwa ukumbini kwa ajili ya kuagwa
RPC Tabora ACP. Suzan Kaganda akiongoza 
waombelezaji kuaga mwili wa marehemu PC JUMANNE.
Waombelezaji wakiwa katika hali ya majonzi
Viongozi mbalimbali wa mkoa wa Tabora wakiwa katika hali ya huzuni.
Mchungaji wa Kanisa la Waadivensti akiongoza misa

Book with Skylink and win

MKUTANO WA MAJAJI WANAWAKE DUNIANI KUFANYIKA ARUSHA

$
0
0
Chama cha Majaji Wanawake Tanzania (TAWJA) kwa kushirikiana na Chama cha Majaji Wanawake Duniani (IAWJ) kitafanya Mkutano wake Mkuu wa 12 utakaofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa (AICC), Arusha, Tanzania. 

 Mkutano huo wa Kimataifa ambao utashirikisha jumla ya Majaji Wanawake takribani 600 kutoka nchi mbalimbali duniani wakiongozwa na Rais wao ambaye ni Mtanzania, Mhe. Eusebia Munuo, Jaji wa Rufaa (Mstaafu), utaanza rasmi mnamo tarehe 05 Mei, 2014 na utafunguliwa na Mhe. Dr. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 
 Maudhui ya Mkutano huo muhimu ni: ‘Justice for All’ ikiwa na maana ya‘Haki kwa wote’ Aidha; Mkutano huo utatoa fursa ya kupanua wigo wa mawasiliano kati ya Majaji Wanawake duniani ili kujenga mazingira mazuri ya utendaji kazi ikiwa ni pamoja na kujenga ubora na uadilifu katika utoaji haki na ukuzaji (promotion) wa Haki za Binadamu. 
 Mkutano huo ambao utadumu kwa muda wa wiki moja utafungwa rasmi na Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe Balozi Seif Alli Iddi. Wakiwa hapa nchini wajumbe wa Mkutano huo watapata fursa pia ya kufanya utalii kwa kutembelea vivutio mbalimbali vilivyopo Mkoani Arusha. Chama cha Majaji Wanawake Duniani (IAWJ) kiliundwa rasmi mwaka 1991. 
 Chama hiki kina Makao Makuu yake huko Washington DC nchini Marekani. Chama hiki kina jumla ya wanachama takribani 4,000 kutoka katika nchi zisizopungua 100 ambapo wanachama wake wanatoka katika kila ngazi ya Mahakama duniani. Chama kinafanya kazi kwa karibu na Wanachama wake kuhakikisha kuwa:- 
• Wanashirikiana na Taasisi na vyama vingine katika masuala ya upatikanaji wa haki sawa. 
• Kutoa elimu kuhusiana na masuala ya haki za binadamu na jinsi wanawake wanavyoweza kupata huduma za Mahakama n.k.
 • Kuendeleza mtandao wa Kimataifa wa Majaji Wanawake na kutengeneza fursa za kubadilishana uzoefu kuhusu utawala wa sheria kupitia mikutano ya Kimataifa, Mafunzo, vijarida n.k. 

 Imetolewa na : CHAMA CHA MAJAJI WANAWAKE TANZANIA (TAWJA).

ARTIST'S IMPRESSION OF THE PROPOSED MUHIMBILI UNIVERSITY OF HEALTH AND SCIENCES CAMPUS AT MLOGANZILA

Naibu Waziri wa Afya atembelea Makao Makuu ya NHIF

$
0
0
Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Kebwe S. Kebwe akizungumza na Menejimenti ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya alipotembelea Makao Makuu ya Mfuko huo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Balozi Ali Muchumo akitoa salaam za Bodi kwa Naibu Waziri.
Kaimu Mkurugenzi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Hamis Mdee akitoa maelezo ya awali na Taarifa ya utekelezaji ya Mfyuko.
Sehemu ya Mameneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya wakifuatilia taarifa ya utekelezaji iliyosomwa na Kaimu Mkurugenzi wa Mfuko.
 Baadhi ya Wakurugenzi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya wakisikiliza kwa makini maelekezo ya Naibu Waziri.
Mkurugenzi wa Mifumo Habari wa NHIF, Ali Othman akielezea namna Mfuko ulivyojipanga kutumia teknolojia kudhibiti udanganyifu.
Naibu Waziri akiteta jambo na Maofisa wakuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya baada ya kumaliza mazungumzo na Menejimenti.

ngoma azipendazo ankal


Taswira za Mkutano wa Viongozi Wakuu wa Jumuiya ya afrika mashariki jijini Arusha

$
0
0
 Wakuu wa Mataifa ya Jumuiya ya Afrika Mashariki wakizindua kitabu rasmi cha Muongozo wa Majaji wa Jumuiya hiyo kwenye Mkutano wa 12 wa siku moja wa Jumuiya hiyo uliofanyika ukumbi wa Kimataifa wa Arusha.  Rais Uhuru Kenyata wa Kenya ambae ndie Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni pamoja na Mwenyeji wa Mkutano huo Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Jakaya Mrisho Kikwete. Wengine ni Makamu wa kwanza wa Rais wa Burundi Bwana Bazombasa, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi aliyemuwakilisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr. Ali Mohd Sheni pamoja na Waziri Mkuu wa Rwanda Bwana Pierre Damieni Habumuryemi.
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kwa niaba yaRais wa Zanzibar Dr. Ali Mohamed Sheni akipokea kitabu wakati wa Mkutano wa Wakuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Mkoani Arusha.
 Baadhi ya Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania waliohudhuria Mkutano wa 12 wa Wakuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki huko Arusha. Wa mwanzo kutoka kushoto ni Waziri wa Ardhi wa SMZ Mh. Ramadhan Abdulla Shaaban, Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania Mh. Benard Membe na Waziri wa Afrika Mashariki Mh. Joh Samuel Sitta. 

BARAZA LA WAKALA WA USALAMA NA AFYA MAHALA PAKAZI (OSHA) LA ZINDULIWA MJINI BAGAMOYO

$
0
0
Wajumbe wa Baraza la wafanyakazi linaloshughulikia Usalama na Afya mahala pakazi (OSHA) wakiwa kwenye picha ya pamoja na Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, Dkt. Makongoro Mahanga (wa tatu kulia walioketi) mara baada ya kufunguliwa kwa Kikao cha Baraza hilo,jana kwenye Hoteli ya Millennium Mjini Bagamoyo.
Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, Dkt. Makongoro Mahanga akibadilishana mawazo na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usalama na Afya mahala pa kazi (OSHA), Dkt. Akwilina Kayumba baada ya kuzindua Baraza la wafanya kazi linaloshughulikia Usalama na Afya mahala pakazi.kulia ni Katibu wa Baraza Renalda Damas aliye chaguliwa katika kikao cha baraza kilicho fanyika katika Hoteli ya Millennium Mjini Bagamoyo.
Naibu Waziri wa Kazi na Ajira,Dkt. Makongoro Mahanga akaribishwa na Henry Mpande ambaye ni Mwenyekiti wa Hoteli ya kitalii ya Millennium iliyoko katika ufukwe wa Bahari ya Hindi mjini Bagamoyo Mkoa wa Pwani ambapo mkutano wa baraza la wakala wa usalama na afya katika mahala pakazi OSHA ulipofanyikia.Picha na Chris Mfinanga

WAKULIMA WA UFUTA WILAYANI BABATI WAPEWA MASHINE ZA KUKAMUA UFUTA

$
0
0
Ofisa Masoko wa Shirika la Farm Africa,Rahel Pazzia (kushoto) akikabidhi mashine ya kukamua ufuta kwa wana kikundi wa wakulima wa ufuta wa kikundi cha Faraja na Chemchem kwenye Kijiji cha Vilima Vitatu, Wilaya ni Babati Mkoani Manyara jana.
Wanakikundi wa Sayuni na Mti wa maziwa, ambao ni wakulima wa zao la ufuta wa Kijiji cha Ngolley Wilaya ya Babati Mkoani Manyara, wakiwa na mashine yao ya kukamua ufuta baada ya kukabidhiwa na Ofisa Masoko wa shirika la Farm Africa, Rahel Pazzia.
Wakulima wa ufuta wa vikundi vya Mkombozi na Shamabo wa Kijiji cha Shaurimoyo, Kata ya Mwada Wilaya ya Babati Mkoani Manyara, wakiwa na mashine yao ya kukamulia ufuta iliyotolewa na shirika la Farm Africa, ambapo shirika hilo liligawa mashine 10 kwa vikundi 18 vya ufuta katika Tarafa ya Mbugwe.

jarida la Wiki la Nishati na Madini

Hafla ya kumuaga Askofu wa jimbo la katoliki Dodoma,Mhashamu Baba Askofu Gervas John Nyaisonga yafana sana

$
0
0
Mamia ya wakotiliki wamejitokeza kumuaga Askofu wa jimbo la katoliki Dodoma,Mhashamu Baba Askofu Gervas John Nyaisonga ambaye anahamia Mpanda kwa ajili ya kuendelea na kazi Dini.Sherehe hiyo iliyotanguliwa na Ibada ilifanyika katika Kanisa kuu la Mtakatifu Paulo wa Msalaba mkoani Dodoma.

Mgeni rasmi katika sherehe hiyo ambayo alikuwepo Mke wa Waziri Mkuu,Mama Tunu Pina,alikuwa Kiongozi wa Kanisa Katoliki hapa nchini,Mwadhama Polcarp Kardinal Pengo. Pia sherere hiyo ilihudhuriwa na Askofu mstaafu wa jimbo la Domama Mhashamu Baba Askofu Mathias Isuja.

Katika sherehe hiyo ,Mhashamu Baba Askofu Gervas John Nyaisonga. alizawadiwa vitu mbali mbali zikiwemo fedha taslimu. Mhashamu Baba Askofu Gervas John Nyaisonga anaondoka rasmi Dodoma kuelekea Mpanda Ijumaa tarehe 2 akipitia Tabora. Amehamishiwa kwa kazi za Kichungaji Jimbo la Mpanda.

Pamoja na kuhudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mama Rehema Nchimbi,Papadri na watawa wote wa jimbo la Dodoma kulikuwepo vikundi vya kwaya kutoka makanisa mbalimbali ikiwemo kwaya ya Kanisa analosali Mhe.Waziri Mkuu Mizengo Pinda, Kwaya ya Shirikisho Hananasifu Dar es Salaam.
Kiongozi wa kanisa Katoliki hapa nchini Mwadhama Polcarp Kardinali Pengo (kulia) akipeana mkono na Askofu Gervas John Nyaisonga.
Mke wa Waziri Mkuu,Mama Tunu Pinda akibusu Pete ya Kiongozi wa kanisa Katoliki hapa nchini Mwadhama Polcarp Kardinali Pengo.
Mke wa Waziri Mkuu Mama Tunu Pinda akisalimiana na Kiongozi wa kanisa Katoliki hapa nchini Mwadhama Polcarp Kardinali Pengo.

UBALOZI WA TANZANIA KATIKA UMOJA WA FALME ZA KIARABU (UAE) WASHEREHEKEA SHEREHE ZA MIAKA 50 MUUNGANO WA TANZANIA

$
0
0
Balozi wa Tanzania katika Umoja wa Falme za Kiarabu,Mhe. Mbarouk Nassor Mbarouk (kushoto) akimpokea mgeni rasmi wa sherehe za maadhimisho ya miaka 50 ya Muungano Tanzania, Mheshimiwa Dr. Hadef Jawa’n Al Dhaheri, Waziri wa Sheria wa UAE,katika hafla iliyofanyika hivi karibuni katika Hoteli ya Intercontinental,Abu Dhabi.
Balozi Mbarouk akiwa na Chief of Protocol wa UAE Mhe. Shihab Al Faheem.
Balozi Mbarouk akimuongoza Mgeni rasmi Mhe. Dr. Hadef Jawa’n Al Dhaheri, Waziri wa Sheria wa Umoja wa Falme za Kiarabu, pamoja na Mabalozi wanao wakilisha nchi zao hapa UAE kuingia katika ukumbi wa Sherehe.

JHIKOMAN & AFRIKABISA BAND LIVE ON SAUTI ZA BUSARA 2014

$
0
0
Mwanamuziki Mkongwe wa Reggae Tanzania. Jhikoman & Afrikabisa Band Live on Sauti Za Busara Festival 2014. Huyu ni Mmoja kati ya wanamuziki wakubwa wa Muziki wa Reggae hapa nyumbani Tanzania pamoja na Afrika Mashariki. Kwa sasa Jhikoman yupo katika Ziara yake ya Ulaya kufanya Maonyesho katika Nchi za mbali mbali.

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LEO TAREHE 01.05 .2014

MRADI WA HAKUNA WASICHOWEZA WATOA ELIMU NA MISAADA YA VIFAA VYA KUJISITIRI WAKATI WA HEDHI KWA WASICHANA 6000 MKOANI MTWARA

$
0
0
Mwakilishi wa Katibu Tawala Mkoa wa Mtwara Bw. Salum Masalanga (katikati) akikabidhi msaada wa pedi kwa Mwanafunzi wa Shule ya Msingi ya Maendeleo, Neema Mohamed chini ya programu ya Hakuna Wasichoweza iliyofadhiliwa na Vodacom na T-MARC. Wakishuhudia tukio hilo, ni Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa Jamii Vodacom, Yesaya Mwakifulefule (kushoto)na Mratibu wa Mradi kutoka T-MARC Tanzania, Bi. Dorice Chalambo (kulia), mradi huo umeanza kufanya kazi mkoa wa Mtwara na Lindi na kusambaa nchi nzima.
Mwakilishi wa Katibu Tawala Mkoa wa Mtwara Bw. Salumu Masalanga (katikati) akipokea msaada wa pedi kwa niaba ya wanafunzi wa Shule ya Msingi ya Maendeleo chini ya programu ya Hakuna Wasichoweza iliyofadhiliwa na Vodacom na T-MARC. Wakishuhudia tukio hilo, ni Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa Jamii Vodacom, Yesaya Mwakifulefule (kushoto) na Mratibu wa Mradi kutoka T-MARC Tanzania, Bi. Dorice Chalambo (wa pili kulia), mradi huo umeanza kufanya kazi mkoa wa Mtwara na Lindi na kusambaa nchi nzima.
Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa Jamii Vodacom, Yesaya Mwakifulefule (kushoto) na Mratibu wa Mradi kutoka T-MARC Tanzania, Bi. Dorice Chalambo (wa pili kulia) kwa pamoja wakikabidhi msaada wa pedi kwa wanafunzi wa Shule ya Msingi ya Maendeleo chini ya programu ya Hakuna Wasichoweza iliyofadhiliwa na Vodacom na T-MARC. Akishuhudia tukio hilo (katikati) ni Mwakilishi wa Katibu Tawala Mkoa wa Mtwara Bw. Salumu Masalanga, mradi huo umeanza kufanya kazi mkoa wa Mtwara na Lindi na kusambaa nchi nzima.

Wasichana wa mkoani Mtwara wamefaidika na elimu ya afya pamoja na vifaa vitakavyowasaidia kujisitiri wakati wa hedhi. Elimu hii na msaada vimetolewa kupitia mradi wa Hakuna Wasichoweza unaotekelezwa na asasi ya T-MARC Tanzania. 

Mradi wa Hakuna Wasichoweza unaendeshwa na asasi ya T-MARC Tanzania kwa ufadhili wa watu wa Marekani kupitia Shirika la Maendeleo la Kimarekani USAID kwa ushirikiano na Vodacom Foundation.

WABUNGE WAPOKEA MAPENDEKEZO YA MFUMO WA BAJETI KWA MWAKA 2014/2015 KATIKA UKUMBI WA MWAL. NYERERE,JIJINI DAR

$
0
0
Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akitoa maneno ya utangulizi kwa Waheshimiwa Wabunge wakati wa semina ya wabunge wote kwa ajili ya uwasilishwaji wa mapendekezo ya mfumo wa bajeti ya serikali kwa mwaka 2014/2015.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Uhusiano Mhe. Steven Wazira akiwasilisha mwelekeo wa hali ya uchumi kwa mwaka 2014/2015 kwa waheshimiwa wabunge
Waziri wa Fedha Mhe. Saada Mkuya Salum akiwasilisha Mapendekezo ya Mfumo wa Mapato na Matumizi ya serikali kwa mwaka wa fedha 2014/15 kwa Waheshimiwa Wabunge.
Katibu wa Bunge Dkt. Thomas Kashilila akisikiliza kwa makini hotuna ya Waziri wa Fedha Mhe. Saada Mkuya Salum akiwasilisha Mapendekezo ya Mfumo wa Mapato na Matumizi ya serikali kwa mwaka wa fedha 2014/15 kwa Waheshimiwa Wabunge.
Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda, Waziri wa Fedha Mhe. Saada Mkuya Salum na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Uhusiano Mhe. Steven Wazira wakipitia nyaraka mbalimbali wakati Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akitoa maneno ya utangulizi kwa Waheshimiwa Wabunge wakati wa semina ya wabunge wote kwa ajili ya uwasilishwaji wa mapendekezo ya mfumo wa bajeti ya serikali kwa mwaka 2014/2015.
Wabunge wakifuatilia hotuba kwa makini.
Watendaji wa Wizara ya Fedha wakimsikiliza Waziri wa Fedha Mhe. Saada Mkuya Salum. Picha na Owen Mwandumbya

DK.MAGUFULI ALIVYOREJESHA HUDUMA ZA USAFIRI WA BARABARA ZILIZOJIFUNGA JIJINI DAR

$
0
0
Waziri wa Ujenzi Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akishirikiana na watendaji wa Wizara ya Ujenzi na TANROADS akishinda siku nzima na hata kukesha usiku mzima aliweza kushishiriki kikamilifu kama waziri mwenye dhamana kurejesha huduma za usafiri wa barabara zilizojifunga kutokana na kusombwa/kuharibiwa kwa madaraja muhimu yanayouunganisha mji wa Dar es Salaam na maeneo mengine hasa mikoa jirani. Maeneo yaliyoharibiwa ni daraja la Mpiji (Bagamoyo), Mzinga (Mbagala, Kongowe), daraja la Mto Mtokozi (barabara ya Kongowe – Mjimwema – Kigamboni) na Ruvu (Barabara ya Morogoro).

THE 17TH EDITION OF ZIFF PROMISES AN EXCITING LINEUP

Viewing all 110170 articles
Browse latest View live




Latest Images