Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110144 articles
Browse latest View live

ASASI TANO ZINAZOPATA RUZUKU TOKA MFUKO WA MSAADA WA KISHERIA (LSF) KWA MIKOA YA KANDA YA ZIWA ZAMALIZA ZIARA YA SIKU 3 SHIRIKA LA KIVULINI

$
0
0
Mkurugenzi wa Shirika la KIVULINI Bw Ramadhan Masele akifunga ziara ya kimafunzo ya siku tatu kwa mbele ya washiriki wa ziara hiyo (hawapo pichani), Bw Masele alitoa shukrani kwa maafisa toka mashirika matano ya mikoa ya kanda ya ziwa pamoja na maafisa toka Mfuko wa Msaada wa kisheria (LSF) na Foundation for Civil Society kwa ziara hiyo ya mafunzo.
Mwanakijiji wa kata ya Mwamala Wilaya ya Kwimba Bi. Grace Masanja akieleza msaada wanaopata juu ya elimu na ushauri wa kisheria toka kwa msaidizi wa kisheria katika kata yao, Bi. Grace alitanaibisha kwamba bado kuna tatizo kubwa la unyanyasaji wa kijansia unaofanywa na wanaume dhidi ya wanawake licha ya elimu ya haki za kila jinsi zinatolewa kila siku na kuwaomba wadau wa sheria kuzidisha nguvu kuweza kukomesha tabia za wanaume kupiga wanawake.
Mwanakijiji wa kata ya Mwamala Bw. James Ngosha akiwashukuru wageni toka KIVULINI pamoja na washirika wengine kwa msaada wa kuwapatia muelimishaji wa haki na sheria katika kata yao kwani amekuwa akiwasaidia sana katika kutatua migogoro ya ardhi kijijini kwao.
Maafisa toka Asasi tano za kanda ya ziwa pomoja na wawezeshaji wa KIVULINI, LSF na Foundation for Civil Society wakifanya tathmini ya ziara yao nzima ya siku tatu katika kijiji cha Mwamal baada ya kumaliza ziara ya kutembelea kata za Ngudu, Mwamala na Hungumalwa katika wilaya ya Kwimba.


Maafisa Miradi pamoja na Maafisa Wakaguzi na Tathmini Miradi toka mashirika matano ya Kiraia yanayopata ruzuku kutoka Mfuko wa Msaada wa Kisheria (LSF) Tanzania, yamemaliza ziara ya kimafunzo ya siku tatu katika Shirika la Kutetea Haki za Wanawake na wasichana Tanzania, KIVULINI la jijini Mwanza, ziara iliyolenga kujifunza na kuboresha ufanyaji kazi wa mashirika hayo kupitia Miradi mbalimbali inayoendeshwa na KIVULINI.


Mashirika hayo matano toka mikoa ya Kagera, Shinyanga, Mara, na Tabora yalianza mafunzo hayo Jumatatu ya tarehe 28 Aprili, 2014 na kumaliza mafunzo hayo tarehe 30 Aprili, 2014 kwa kutembelea Wasaidizi wa Kisheria wanaofanya kazi ya kutoa elimu na ushauri wa kisheria katika vijiji mbalimbali vya Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba chini ya shirika la KIVULINI kupitia mradi wa Msaada wa Kisheria unaofadhiliwa na LSF.


Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa Ziara hiyo Mkurugenzi wa Shirika la KIVULINI Bw. Ramadhan Masele aliwashukuru maafisa wote toka mikoa hiyo mitano ya kanda ya ziwa kwa kuhudhuria mafunzo hayo lakini pia aliwashukuru Mfuko wa Msaada wa Kisheria kwa heshima waliyowapa KIVULINI kuwa kituo cha mafunzo kwa asasi nyengine.


“Ziara hii imetoa hamasa nzuri hasa kwa upande wa kimahusiano baina ya Asasi zinazotekeleza mradi wa msaada wa kisheria kwa kanda ya ziwa, pia uzoefu tuliobadilishana kwa siku zote tatu za mafunzo naamini utaenda kuimarisha utendaji kazi wa asasi zetu na kuinua hali ya maisha ya Watanzania kupitia sisi” alisema Mkurugenzi wa KIVULINI Bw Ramadhan Masele.


“Lakini pia tuwashukuru wadau wetu wakubwa katika mradii huu wa msaada wa kisheria, LSF, kwa ubunifu waliouleta wa kutuwezesha kukutana pamoja na kubadilishana uzoefu katika utendaji kazi, na hivyo hivyo shukrani zetu ziende kwa Foundation for Civil Society kwa kushirkiana na SLF kuwa pamoja nasi, tunaomba huu uwe ni mwanzo tu na usiwe mwisho” alimalizia Bw Masele


Ziara hiyo imeratibiwa na LSF kwa kushirikiana na Foundation For Civil Society kutoa hamasa na kuinua utendaji kazi wa Asasi za Kiraia nchini katika kuhakikisha asasi hizo zinatoa matokeo bora katika mradi wa Msaada wa kisheria.



Mashirika yaliyohudhuria ziara hiyo ya Kimafunzo ni Jamii Salama Development Volunteers (JSDV) toka Tabora, Centre for Widows and Children Assistance (CWCA) la mkoani Mara, Mama’s Hope Organization for Legal Aid (MHOLA), Paralegal Aid Centre Shinyanga (PACESHI), Sheria na Haki za Binadamu (SHEHABITA) la mkoani Mara.


Maandamano katika sherehe za mei mosi uwanja wa uhuru jijini dar es salaam

$
0
0
 Wakala wa Ndege za Serikali wakiwa katika maandamano hayo yaliyofana sana
 Wizara ya Mambo ya Ndani nao ndani
 Benki Kuu
 Wakala wa Ndege za Serikali
Ofisi ya Waziri Mkuu.

Bayport Yazindua Bima Ya Elimu

$
0
0
Bayport yazindua Bima Ya Elimu,Kwenye hafla ndogo kwenye ofisi ya Wizara ya   Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto. Kuanzia mkono wa kushoto katika picha ni Mhe. Sophia Simba (Waziri) akifutiwa na wawakilishi wa Bayport Financial    Services Maneja Masoko Ngula Cheyo na Matthew Mbaga, Meneja wa Bima.
======  ======  =======

Bayport Financial Services, ambayo ni moja kati ya wakopeshaji akubwa kwa ajili ya wafanyakazi imezindua mpango wa bima kwa ajili ya elimu. 
Mfumo huo wa bima ni kwa ajili ya kuendeleza elimu kwa watoto pale ambapo wazazi wao wanafariki. Kwa kiwango cha chini cha TZS 2,500 kwa mwezi, bima hii ni nafuu kwa wafanyakazi wenye kipato cha chini na inamhakikishia mwanafunzi kupata mahitaji yake ya msingi katika elimu.

Akiongea katika ufunguzi wa huduma hii mpya jana, Meneja Masoko wa Bayport Financial Services, Ngula Cheyo aliwaeleza waandishi wa habari kwamba lengo la kubuni huduma hii ni kutokana na kuwepo kwa pengo kwenye soko la huduma ambayo inakidhi watu wenye kipato kidogo. ‘Kuwepo kwetu hapa Tanzania kwa muda mrefu kumetupa fursa ya kutambua kuwa huduma ya bima haiwafikii watu wengi na huduma hii ingewanufaisha watanzania wengi ambao wanajali watoto wao’, alisema Ngula.

Katika uzinduzi huo uliofanyika ofisini kwake, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, jinsia na Watoto, Meshimiwa Sophia Simba, aliisifu kampuni ya Bayport Financial Services kwa kuzindua huduma hii ambayo itasaidia kupunguza mzigo kwa ndugu wa mfiwa na kuhakikisha motto anaendelea na elimu yake. ‘Elimu ni haki ya kila mtoto na huduma hii itapunguza wanafunzi ambao wanaacha shule kwa sababu ya kushindwa kulipa ada pindi wazazi au walezi wao kufariki. Elimu inasaidia watanzania wengi kujikomoa na umasikini na kusiwe na pingamizi yoyote kwa mtoto kutoipata,’ alisema Mheshimiwa Simba.

 Wazazi na walezi wanauwezo wakuchagua jinsi ya kulipa na idadi ya wanafunzi wanaotaka kuwalipia bima hii. Bima hii inapatikana katika matawi yote ya Bayport ambayo yamesambaa katika mikoa yote hapa nchini. Matthew Mbaga ambaye ni Meneja wa Bima pia alieleza waandishi pia umuhimu na manufaa ya bima hii katika uzinduzi huo.

HOTUBA YA RAIS KIKWETE KWENYE KILELE CHA SIKUKUU YA WAFANYAKAZI DUNIANI, MEI MOSI 2014, DAR

$
0
0
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia katika kilele cha Siku ya Wafanyakazi Duniani (MEI MOSI)  Mei 1, 2014 katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

King Majuto atoa msaada wa Steps Solar kwa kituo cha Polisi Mjimwema

$
0
0
Mwigizaji mkongwe katika tasnia ya filamu nchini,Amri Athuman ‘King Majuto’ wiki iliyopita akiwa kama Balozi wa Steps Solar alitoa msaada wa kukifungukia Solar kituo cha Polisi cha Mjimwema, ikiwa ni katika kampeni za kuhakikisha kila mtanzania anafaidika na matumizi ya nishati ya umeme Nuru.

Akiongea na Waandishi wa habari katika hafla iliyoandaliwa na kampuni ya Steps Entertainment ambao ndio wafadhali wa msanii huyo, alisema kuwa kampuni hiyo imekuwa ikisambaza filamu zake lakini kuna utaratibu wa kutoa misaada kwa jamii, kwake yeye ameona tatizo linalowakabili watu wengi nje ya miji ni umeme.

“Nimeanza kampeni kama Balozi wa Steps Solar kuwasaidia wapenzi wa kazi zangu, ambazo ninaamini bila wao siwezi kabisa kuwa King, kama vile mnavyopenda kuniita, nimeanza katika kituo cha Polisi cha Mjimwema lakini nikiwa na wenzangu tutafika sehemu nyingi zaidi,”alisema King Majuto.

Afisa mahusiano wa kampuni hiyo Moses Mwanyilu amesema kuwa mradi huo ni endelevu ambapo wanatarajia kufunga Steps Solar katika Kituo cha Yatima Tuangoma, Mjimwema, vituo vya Polisi ni Mjimwema na Ferry, vituo vya afya ni Mjimwema, Ungindoni, Homboza Chanika na Tuangoma.

Msanii huyo aliambatana na wasanii wengine ambao pia ni mabalozi wa Steps Solar, ambao ni Jacob Stephen ‘JB’ na Salma Jabu ‘Nisha’ mgeni wa heshima katika hafla hizo alikuwa Mh. Dr. Faustine Ndugulile mbunge wa Kigamboni.
Mbunge wa Jimbo la Kigamboni,Dkt. Faustine Ndugulile (kushoto) akizungumza jambo wakati wa hafla ya kupokea Vifaa vya Solar kutoka kampuni ya Steps Solar kwa ajili ya Kituo cha Polisi cha Polisi cha Mjimwema,Kulia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Steps Solar,Dilesh Solank. 
Mmoja wa Mabalozi wa Steps Solar,Jacob Stephen akiongea na wananchi wa Mjimwema.
Mabalozi wa Steps Solar Jacob Stephen (JB) na Amri Athuman (King Majuto) wakiwa kwenye hafla hiyo.

Wafanyabiashara DRC wahamasishwa kutumia ofisi mpya za TPA Lubumbashi

$
0
0
Na Mwandishi wetu, Lubumbashi

Serikali ya Tanzania imesema imedhamiria kuhakikisha wafanyabiashara toka Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo wanaotumia bandari ya Dar es Salaam wanapata huduma nzuri kwa faida ya nchi zote mbili.

Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe amesema wakati wa uzinduzi wa ofisi ya mawasiliano ya Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) mjini Lubumbashi, DRC kuwa wizara yake na bandari ya Dar es Salaam watahakikisha kuwa huduma za bandari zinasogezwa karibu na DRC.

“Nawahimiza wafanyabiashara wa DRC kutumia kwa ufanisi ofisi hii kwa faida ya jamii nzima ya nchi yao,” alisema.Waziri alisema kuwa ofisi hizo mpya zitasaidia wafanyabiashara wa DRC kumaliza matatizo yao Lubumbashi badala ya kusafiri hadi Dar es Salaam.

“Wataweza kufanya malipo ya bandari wakiwa Lubumbashi na kuepuka hatari ya kusafiri na kiwango kikubwa cha pesa na kuibiwa,” alisema Waziri Mwakyembe.Alisema tatizo lililokuwa linawakabili wafanyabiashara hao la kukabiliana na wakala wa kupakia na kupakua mizigo wasio waaminifu, sasa litakuwa historia kwa kuwa ofisi ya Lubumbashi itakuwa na orodha ya wakala wanaokubalika na waaminifu.

Pia mienendo ya taarifa za mizigo itafanyika mjini humo na hivyo kuharakisha taratibu za mizigo bandarini hapo.Waziri Mwakyembe alisafiri kwa barabara tokea Dar es Salaam hadi Lubumbashi kupitia Zambia kwa barabara zaidi ya kilometa 2000 kuangalia na kupata taarifa za changamoto wanazokumbana nazo wafanyabiashara wa DRC bandarini Dar es Salaam njiani wanaposafiri.

Ofisi ya Lubumbashi inalenga kuondokana na changamoto mbalimbali zinazowakumba wafanyabishara hao zikiwemo ucheleweshaji, wizi, vikwazo visivyohusiana na kodi na wakala wa kupakia na kupakua mizigo wasio waaminifu.

“Juhudi zinaendelea kuhakikisha kuwa vikwazo na urasimu wote unaowakabili wafanyabiashara wa Congo unakwisha,” alifafanua Waziri.Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Bw. Peter Serukamba ambaye ni mmoja wa ujumbe wa Tanzania aliyesafiri na Waziri alisema hatua hiyo ni muhimu kwa maendeleo ya nchi zote mbili.

Aliishauri TPA kuhakikisha inaweka wafanyakazi wenye moyo na uadilifu katika ofisi hiyo mpya.
“Naishauri mamlaka hii iweke wafanyakazi wenye moyo na kazi, waadilifu na wazalendo kwa heshima ya nchi yetu,” alisema.

Makamu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA), Bw. Saidi Sauko amesifu hatua hiyo akisema kuwa itasaidia shirika lao kuongeza ufanisi wa kazi zao.Shirika hilo linahusika sana katika kusafirisha mizigo ya DRC kupitia reli ya TAZARA.

Mizigo ya DRC imekuwa ikiongezeka kwa asilimia takribani 24 kwa mwaka tangu mwaka 2004 ikiongezeka toka tani 155,611 hadi tani 1,117,249 mwaka 2013.Nchi ya DRC ni ya pili kwa kupitisha mizigo mingi katika bandari ya Dar es Salaam.  kwa mujibu wa takwimu zilizopo, mizigo ya DRC inachukua asilimia 25 ya mizigo yote ya nchi jirani inayopita katika bandari hiyo.

Pamoja na maafisa wengine, ujumbe huo ulijumuisha pia maafisa waandamizi toka TPA, Mamlaka ya Usafiri wa nchi kavu na Majini (SUMATRA), Tanzania Railways Limited (TRL), TAZARA na wengine.

DKT. SHEIN AZUNGUMZAA UONGOZI WA OFISI YA RAIS,KAZI NA UTUMISHI WA UMMA

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akizungumza na Uongozi wa Ofisi ya Rais,Kazi na Utumishi wa Umma katika mkutano wa utekelezaji mpango kazi wa robo tatu ya mwaka Julai-Machi 2013/2014,katika ukumbi wa mikutano Ikulu Mjini Unguja.Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.

WANARIADHA WA MBIO NDEFU WAWASILI ADDIS ABABA KWA AJILI YA MAZOEZI YA KUJIAANDAA NA MASHINDANO YA JUMUIYA YA MADOLA

$
0
0
Mhe. Naimi Aziz, Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia ( wa nne kutoka kulia) akiwa na baadhi ya wanariadha wa Mbio ndefu kutoka Tanzania waliowasili jijini Addis Ababa siku ya Alhamisi tarehe 1/5/2014, kwa ajili ya kufanya mazoezi ya nguvu ya kujiandaa na Mashindano ya Jumuiya ya Madola yatakayofanyika nchini Scotland mwezi wa Saba mwaka huu. Wizara ya Michezo ya Ethiopia imeamua kutoa makocha watatu ambao watasaidiana na kocha Shabaan Bayu katika kukinoa kikosi hicho. Aidha, mwanariadha mashuhuri wa Ethiopia Haile-mariam Gabresilas na ye amepangiwa kukutana na kikosi hicho.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AZINDUA RASMI SHEREHE ZA MBIO ZA MWENGE WA UHURU MKOANI KAGERA

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwasha Mwenge wa Uhuru wakati wa Sherehe za uzinduzi wa mbio za Mwenge huo zilizofanyika kwenye Uwanja wa Kaitaba, mjini Bukoba Mkoa wa Kagera leo Mei 2, 2014. Mwenge huo unatarajia kuitimisha mbio zake Oktoba 14 mkoani Tabora, ambapo zinatarajia kufungwa na mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Mwenge wa Uhuru, Kiongozi wa mbio za Mwenge Taifa, Rachel Kasanda, baada ya kuuwasha rasmi wakati wa Sherehe za uzinduzi wa mbio za Mwenge huo zilizofanyika kwenye Uwanja wa Kaitaba, mjini Bukoba Mkoa wa Kagera leo Mei 2, 2014. Mwenge huo unatarajia kuitimisha mbio zake Oktoba 14 mkoani Tabora, ambapo zinatarajia kufungwa na mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Kanali Mstaafu, Fabian Masawe, akipokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Kiongozi wa mbio za Mwenge Taifa, Rachel Kasanda, baada ya kukabidhiwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakati wa Sherehe za uzinduzi wa mbio za Mwenge huo zilizofanyika kwenye Uwanja wa Kaitaba, mjini Bukoba Mkoa wa Kagera leo Mei 2, 2014. Mwenge huo unatarajia kuitimisha mbio zake Oktoba 14 mkoani Tabora, ambapo zinatarajia kufungwa na mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete.
Vijana wenye dhamana ya kukimbiza mwenge wa Uhuru 2014, wakianza rasmi mbio hizo baada ya kuwashwa na kukabidhiwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakati wa Sherehe za uzinduzi wa mbio za Mwenge huo zilizofanyika kwenye Uwanja wa Kaitaba, mjini Bukoba Mkoa wa Kagera leo Mei 2, 2014. Mwenge huo unatarajia kuitimisha mbio zake Oktoba 14 mkoani Tabora, ambapo zinatarajia kufungwa na mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete.

NSSF YATOA WITO KWA WANACHAMA WA HIARI KUJIUNGA NA UANACHAMA

$
0
0
Na Francis Dande

SHIRIKA la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), limewataka wafanyakazi wasio katika sekta isiyo rasmi kujiunga na NSSF ili kuboresha maisha yao ya sasa na baadae.

Akizungumza wakati wa Bonanza la Michezo kwa Makampuni, ambapo NSSF ilikuwa ni miongoni mwa wadhamini Ofisa Uhusiano Mwandamizi wa NSSF, Said Malawi alisema kuwa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), imekuwa ikitoa elimu kwa wanachama wa kupitia huduma ya NSSF Mobile kwenye M-PESA.

Kwa kuwajali wanachama wake NSSF imekuwa ikiwafuata wanachama walio katika sekta isiyo rasmi, mwanachama anaweza kuangalia salio kupitia simu ya mkononi kwa kuandika neno Sajili ikifuatiwa na namba za NSSF zenye tarakimu nane kwenda namba 15747 kisha kuandika neno Salio kwenda namba 15747 na anaweza kupata taarifa za michango aliyotoa. ambapo mwanachama anaweza kuanza kuchangia kuanzia shilingi 20,000 na kuendelea.

NSSF ndio Shirika pekee la Mfuko wa Hifadhi ya Jamii linalokopesha wanachama wake kupitia Saccos zilizosajiliwa kisheria. Aidha mwanachama anaweza kunafaika na huduma za matibabu ya bure yanatolewa kwa mwanachama pamoja na familia yake wakiwemo watoto wane.

“NSSF inatoa mikopo kupitia Saccos iliyosajiriwa kisheria, iwe inakaguliwa mahesabu yake kupitia Mkaguzi Mkuu wa Mahesabu aliyehidhinishwa na Serikali”

NSSF pia inauza viwanja vilivyopo katika eneo la Kilunvya vyenye hati miliki ya kudumu, umeme, maji na barabara za kudumu , pia NSSF inauza nyumba zake zilizopo Mtoni Kijichi kuanzia shilingi milioni 64 bila ya VAT.

kulimelililodhaminiwa na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), na kufanyika katika viwanja vya Leaders Club jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kusherehekea Siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi).

Katika mchezo uliozikutanisha timu za NSSF na Fastjet timu ya timu ya Fastjet iliichapa bila huruma timu ya NSSF kwa idadi ya magori 5-1.
Mshambuliaji wa timu ya NSSF, Mahadhi Mahmoud (katikati) akiwatoka wachezaji wa timu ya Fastjet, Boniface Mwaikelela (kushoto) na Charles Fidelix wakati wa Bonanza la Makampuni la Sports Extra Day ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Sikukuu ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi), lililofanyika kwenye viwanja vya Leaders Club jijini Dar es Salaam jana. Fastjet ilishinda 5-1. NSSF ilikuwa ni miongoni mwa wadhamini wa Bonanza hilo. (Picha na Francis Dande)
 Mwanachama mpya wa NSSF akipigwa picha wakati wa zoezi la kuandikisha wanachama wapya lililofanyika katika viwanja vya Leaders Club jijini Dar es Salaam.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

THE KILIMANJARO CHALLENGE AGAINST HIV and AIDS 2014

$
0
0
Dr. Fatma Mrisho, Executive Director for Tanzania Commissions for AIDS (TACAIDS), joined by AngloGold Ashanti Sustainability Vice President Mr. Simon Shayo and their colleagues during the launch of Kilimanjaro Challenge campaign in Dar es Salaam.

Sherehe za mei mosi uwanja wa uhuru jijini Dar es salaam

A brand new video by Azma-"Kuwa na azma"

SABA KIZIMBANI KWA WIZI KATIKA BENKI YA BARCLAYS

$
0
0
WATU saba wakiwemo wafanyakazi wawili wanawake wa benki ya  Barclays wamepandishwa  katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa kosa la kula njama na unyang'anyi wa kutumia silaha pamoja na wiza wa sh milioni 390.2 , dola za kimarekani 55,000 na Euro 2150.

Washtakiwa hao ni Alune Kasililika (38), Neema Batchu (26) wafanyakazi wa benk hiyo, Kakame Julius (38), Iddy Khamis (32), Sezary Msolopa (31), Boniphace Muumba (29) na Ruth Macha (30) wafanyabiashara.

Wakisomewa mashitaka yao mbele ya  hakimu Mkazi, Nyigulila Mwaseba ambapo Wakili wa Serikali Tumaini kweka akisaidiana Mwanaamina  Kombakono  walidai kuwa wastuhumiwa hao wanakabiliwa na mashtaka mawili.

Aliieleza mahakama kuwa katika tarehe  tofauti zisizo fahamika washtakiwa  wakiwa ndani ya jiji la Dar es Salaam walikula njama  kwa nia ya kutenda kosa la wizi.

Katika shtaka la pili washtakiwa wanadaiwa kuwa Aprili 15 mwaka huu, wakiwa katika benki hiyo tawi la Kinondoni, Dar es Salaam waliiba fedha tasilimu sh.
milioni 390.2, Dola za Marekani 55, 000 na Euro 2150 mali ya Barclays.

Hata hivyo, ilidaiwa kuwa kabla ya kufanya wizi huo walimtishia kwa silaha Anifah Ahmad na Anna Tegete ambao ni wafanyakazi wa benki hiyo ili kuweza
kujipatia na kumiliki fedha hizo.

Baada ya washtakiwa hao kusomewa mashtaka hayo walikana kuhiska na tukio hilo, ambapo wakili Kweka alidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika
wanaomba tarehe nyingine ya kutajwa.

Hakimu Mwaseba alisema kwa mujibu wa sheria shtaka la pili halina dhamana, kwa hiyo washtakiwa watakuwa chini ya ulinzi na kupelekwa gerezani hadi Mei 15 kesi hiyo itakapotajwa.
mwaka huu.

Katika tukio hilo ilielezwa kuwa majambazi hao walifika katika benki hiyo Aprili 15, mwaka huu, saa 9:00 mchana wakiwa na magari mawili na bunduki aina ya SMG pamoja na bastola, kisha waliingia ndani ya benki hiyo na kupora fedha walizotoka nazo kwenye mfuko na kukimbia nazo kwa kutumia pikipiki.

Hivi karibuni Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Sulemain Kova akizungumza tukio hilo alisema kuwa wamegundua baadhi ya matukio ya wizi wa fedha unafanywa na wafanyakazi wa benki.


Alisema katika wizi huo, robo tatu ya fedha zote zilizoibwa zilichukuliwa siku moja kabla ya tukio linalodaiwa kutengenezwa la wizi, kwa lengo la kuficha wizi huo na kwamba kulikuwa na vikao mbalimbali vya maandalizi ya kufanikisha tukio hilo.

Alisema Aprili 15, mwaka huu siku ambayo wizi huo unatajwa kufanyika, kilichotokea ni tukio la kukamilisha njama hizo.

“Tukio hili lilileta utata tangu mwanzo tulipokwenda kukagua eneo la tukio, kwani siku moja kabla, yaani Aprili 14, gari la kubebea fedha kupeleka Benki Kuu lilifika katika tawi hilo kama ilivyo kawaida lakini fedha hazikutolewa kumbe ilikuwa ni mkakati uliowekwa kufanikisha wizi huo.”

MALAWI YAWASILI NCHINI TAYARI KWA MTANANGE DHIDI YA STARS, KIINGILIO NI BUKU 5 TU !

$
0
0
Timu ya Taifa ya Malawi (Flames) imewasili jijini Mbeya tayari kwa mechi ya kirafiki dhidi ya Taifa Stars itakayochezwa Jumapili (Mei 4 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine.

Flames ikiwa na msafara wa watu 31 imewasili jana (Mei 1 mwaka huu) saa 1 jioni kwa njia ya barabara, na imefikia hoteli ya Manyanya. Nayo Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager ipo jijini Mbeya tangu Aprili 27 mwaka huu kujiandaa kwa mechi hiyo.

Kiingilio katika mechi hiyo kitakuwa sh. 5,000 wakati tiketi zitauzwa siku ya mchezo kuanzia saa 2 asubuhi katika vituo vya Uyole, Mwanjelwa,, Mbalizi, Stendi Kuu, Holiday Inn na Uwanja wa Sokoine.

Magari yatakayoruhusiwa kuingia uwanjani ni ya wachezaji, gari la wagonjwa, gari la zimamoto na gari la waamuzi pekee.

BONIFACE WAMBURA
OFISA HABARI NA MAWASILIANO

SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

Vodacom yachangia mbio za mwenge wa uhuru

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Kanali Mstaafu Fabian Massawe akiongea ofisini kwake mjini Bukoba wakati wa hafla fupi ya kupokea mchango wa Sh. 10 Milioni kutoka kampuni ya Vodacom kwa ajili ya kuchangia sherehe ya uwashaji mwenge wa Uhuru kitaifa iliyofanyika Mkoani humo. Kutoka kushoto Ni Mkuu wa Vodacom Kanda ya Ziwa Domician Mkama, Mkuu wa Vodacom Foundation Yessaya Mwakifulefule na Meneja Uhusiano wa Nje wa Kampuni hioyo Salum Mwalim.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Kanali Mstaafu Fabian Massawe akihakiki thamani ya hundi ya mfano iliyotolewa na Kampuni ya Vodacom kuchangia sherehe ya uwashaji mwenge wa Uhuru kitaifa iliyofanyika Mkoani humo.Wanaofurahia kitendo hicho kutoka kushoto ni Mkuu wa Vodacom Kanda ya Ziwa Domician Makama, Meneja wa Uhusiano wa Nje wa Vodacom Salum Mwalim, Mkuu wa Vodacom Foundation Yessaya Mwakifulefule na Katibu Tawala wa Mkoa Nassor Mnambila (wa kwanza kulia). Makabidhiano hayo yalifanyika mjini Bukoba.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Kanali Mstaafu Fabian Massawe akimshukuru Mkuu wa Kampuni ya Vodacom Kanda ya Ziwa kwa mchango wa Sh 10 Milioni kampuni hiyo illiyoutoa kusaidia sherehe ya uwashaji mwenge wa uhuru zilizofanyika kitaifa mkoani kwake. Katikati ni Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Salum Mwalim na Mkuu wa Vodacom Foundation Yessaya Mwakifulefule (kulia).
Meneja wa Uhusiano wa Nje wa Kampuni ya Vodacom Salum Mwalim (kushoto) akifafanua jambo kwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera Kanali Mstaafu Fabian Massawe nje ya ofisi yake mjini Bukoba muda mfupi baada ya kumkabidhi Mkuu huyo wa Mkoa mchango wa Vodacom wa Sh.10 Milioni kusaidia shughuli ya uwashaji mwenge wa Uhuru ambayo kitaifa imefanyika Kagera. Kushoto ni Mkuu wa Vodacom Kanda ya Ziwa Domician Mkama.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Kanali Mstaafu Fabian Massawe( mwenye suti) na Mkuu wa Vodacom Foundation Yessaya Mwakifulefule wakikumbushana enzi za Shule ya Sekondari ya Jitegemee ya jijini Dar es salaam ambayo Kanali Massawe alikuwa Mkuu wake wa Shule na Mwakifulefule akiwa ni mwanafunzi. Wawili hao walikutana wakati Vodacom ilipofika ofisni kwa Mkuu huyo wa mkoa kukabidhi mchango wa Sh 10 Milioni kusaidia sherehe za uwashaji mwenge wa Uhuru ambazo kitaifa zimefanyika Mkoani Kagera.

WAANDISHI WA HABARI MSIKUBALI KUTUMIWA, UNGANENI

$
0
0
Na Waandishi Wetu, Arusha
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri (TEF), Absalom Kibanda ametoa wito kwa waandishi wa habari nchini kuyapa uzito matukio yanayowatokea waandishi wa habari na kuyapigia kelele kwa nguvu zote ili kuyakomesha.

Kibanda aliyasema hayo jana mjini Arusha katika kongamano lililoandaliwa kama sehemu ya maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani na kuongeza kwamba wakati umefika kwa waandishi wa habari kuondoa tofauti zao na kuungana pamoja kuongeza nguvu waliyonayo kukabiliana na ukatili unaoendelea dhidi ya waandishi wa habari katika miaka ya hivi karibuni.

“Baadhi ya wahariri huwa hawayaandiki madhila yanayowasibu waandishi wa habari na kuyapa uzito unaostahili aidha kwa huyapuuzia au kudharau kwa kuwa hayawahusu moja kwa moja,” alisema Kibanda.

Aliongeza kwa kusema kuwa vyombo vya habari mara nyingi vimekuwa vikinyooshewa vidole na kulaumiwa kwa kutokufanya kazi kwa uadilifu jambo ambalo linatafsiriwa kuwa ni la uonevu, vinatumiwa vibaya na hakuna anayesimama kuvitetea kutokana na mchango wake mkubwa katika jamii.
DSC_0053
Afisa Mipango Kitengo cha Mawasiliano, Habari na Tehama UNESCO, Bw. Al Amin Yusuph, akiwasilisha mada kuhusu mchango wa uhuru wa vyombo vya habari katika utawala bora, kukuza uwezo na kupunguza umaskini kongamano la waandishi wa habari lilioandaliwa kama sehemu ya maadhimisho ya siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani yanayofanyika jijini Arusha.

“Kwa sasa tasnia hii iko kwenye wakati mgumu sana kwani hata marais wa nchi mbalimbali mfano Uganda, Kenya hata Marekani wanakinzana na vyombo vya habari kwa madai kuwa kauli zao zinapotoshwa, laikini ukweli ni kwamba ni vyema kauli hizo za viongozi zikachunguzwa kwa undani zaidi ili kuelewa iwapo zina uwajibikaji ndani yake,” alisema Kibanda.

Kibanda aliongeza kuwa wakati umefika sasa kwa waandishi kutambua kuwa kuna ajenda za siri zilizojificha dhidi ya uteswaji wa waandhishi wa habari hivyo yasidharauliwe, yafanyiwe kazi kwa kina ili kuelewa kiini cha tatizo kwa kupata ufumbuzi.

Kwa upande wake mwandishi mkongwe na aliyetunukiwa tuzo ya maisha mwaka 2012 na Baraza la Habari Hamza Kasongo alisema vyombo vya habari vina nguvu kubwa katika kushawishi hivyo vitumie nguvu hiyo kama muhimili wa nne wa nchi katika kuzikabili changamoto zilizopo.

“Kuwe na mtandao unaoeleweka wa mawasaliano kati ya waandishi wa habari nchini ili kuhakikisha kuwa matatizo yaliyopo yanatatuliwa bila woga na kwa ujasiri kwa lengo la kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa,” alisema Kasongo.
DSC_0060
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Kitivo cha Sheria , Bw. James Jesse, akitoa mada kuhusu umuhimu wa sheria katika kulinda haki ya uhuru wa kujieleza kwa kila mtu wakati wa kongamano la waandishi wa habari lilioandaliwa kama sehemu ya maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani yanayofikia kilele leo jijini Arusha.

KATIBU MKUU WA CCM AWASILI KISIWANI PEMBA MCHANA HUU,KUFANYA MKUTANO WA HADHARA GOMBANI YA KALE JIONI YA LEO

$
0
0
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndg. Abdulrahman Kinana (kushoto) akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Zanzibar,Ndg. Vuai Ali Vuai wakati alipowasili kwenye uwanja wa Ndege wa Pemba,Mchana wa leo tayari kwa Mkutano wa Hadhara wa CCM kwa Mikoa ya Miwili ya Pemba.wengine pichani ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kaskazini Pemba, Ndg. Mzee Mbelwa (kulia) akifatiwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kusini Pemba,Abdallah Mshindo.Katibu Mkuu atahutubia mkutano wa hadhara katika eneo la Gombani ya Kale.
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM - Zanzibar,Ndg. Vuai Ali Vuai (katikati) akifurahia jambo na Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye wakati akimkaribisha Kisiwani Pemba leo.
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndg. Abdulrahman Kinana (kushoto) akizungumza jambo na Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Zanzibar,Ndg. Vuai Ali Vuai mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Pemba,mchana huu.
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndg. Abdulrahman Kinana (kushoto) na Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye wakisalimiana na baadhi ya wanaCCM wa Kisiwani Pemba waliofika uwanjani hapo kuwapokea.
 Msafara wa Katibu Mkuu wa CCM,Ndg. Abdulrahman Kinana ukitokea kwenye Uwanja wa Ndege wa Pemba kuelekea Ofisi Kuu ya CCM Pemba. 

AUDIO YA MAHIJIANO NA PROFESA BOAS KUHUSU MUUNGANO

$
0
0
Profesa Boas akiwa na Cheif wa swahilivilla Abou Shatry baada ya Mahojiano siku ya Ijumaa Mei 2, 2014 Maryland Nchini Marekani.   Sikiliza Audio ya Mahojiano kuhusu Muungano na Profesa Boas ambaye ni Mwalimu wa Mawasiliano na Sera (Communication and Public Policy) University of Maryland University College Washington DC

WASICHANA 30 JIJINI MWANZA WAPATIWA MAFUNZO YA SIKU TANO KUHUSU ELIMU YA UKATILI WA KIJINSIA MAJUMBANI

$
0
0
Mkurugenzi wa Shiriki la KIVULINI Bw Ramadhan Masele akisisitiza jambo wakati akifunga mafunzo maalum kwa wasichana 30 walio na umri kati ya miaka 18 mpaka 25 kutoka wilaya ya Ilemela na Nyamagana za jijini Mwanza hapo jana. Wasichana hao wamepewa mafunzo kuhusu ukatili wa kijinsia majumbani pamoja na Kingono lengo likiwa ni kuzalisha waelimisha rika wengi zaidi mitaani na kutengeneza jamii isiyokuwa na ukatili wa kijinsia na kingono kwa kwa watoto wa kike.
Mkufunzi wa Masuala ya Kijinsia Bi. Tumaini Kyola akitoa mafunzo kwa kundi la Wasichana 30 ambao hawako mashuleni juu ya mbinu mbalimbali za kuelemisha jamii kuhusu masuala Ukatili wa Majumbani na wa kingono pia. Wasichana hawa wanategemewa kwenda kuwafundisha wasichana wenzao wa mitaani, kila mmoja amepewa lengo la kufikia wasichana 50. 
Baadhi ya wasichana 30 wakiwa makini kufuatilia mafunzo waliokuwa wakipatiwa na mkufunzi wao (hayupo pichani), hili ni kundi la kwanza kwa wasichana waliokuwa nje ya shule ambapo mafunzo ya kundi la pili kwa wasichana waliopo mashuleni yanatarajiwa kuanza mwezi wa sita kwa kushirikisha shule zipatazo 40 toka wilaya za jiji la Mwanza.

Wasichana thelathini pamoja na Mkufunzi wao na baadhi ya maafisa wa Kivulini wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumaliza mafunzo hayo ya siku tano hapo jana katika ukumbi wa VETA jijini Mwanza.
Mkurugenzi wa shirika la kutetea Haki za Wanawake na Wasichana KIVULINI lenye makao yake makuu jijini Mwanza Bw. Ramadhan Masele amefunga rasmi mafunzo ya siku tano yanayolenga  kuwajengea wasichana uwezo wa kutoa elimu juu ya masuala ya ukatili na unyanyasaji wa kijinsia chini ya mradi wa kuwashirikisha vijana kuzui Ukatili wa majumbani ikiwa ni pamoja na ukatili wa  kingono kwa watoto wa kike na wasichana.  

Akizungumza na washiriki wa mafunzo hayo Bw. Masele aliwataka washiriki wote kutumia elimu hiyo muhimu waliyoipata kutoa elimu na kuongeza uwelewa zaidi kwa jamii yao kuanzia ngazi ya familia, marafiki na vikundi mbalimbali na kuwa chachu ya mabadiliko  juu ya kupigania haki za wanawake na wasichana wanaonyanyaswa kijinsia katika jamii zao.


“Imani yangu ni kuwa semina hii itakuwa ni kiwanda kizuri cha kuwatengeneza nyinyi wote kuwa mabalozi wazuri katika jamii, baada ya mafunzo haya tunaamini kuwa mtakuwa chachu ya mabadiliko katika kutetea na kulinda haki za wanawake na wasichana kwa kukemea, Kupinga, kuripoti na kuzuia aina zote za ukatili wa majumbani na kingono kwa wasichana na wanawake na kutoa taarifa pindi vitendo hivi vinapotokea” alisema Bw. Masele


“Kila mmoja aliyehudhuria mafunzo haya  kwa nafasi aliyonayo tunaamini anaweza kuwa chachu ya mabadiliko endapo atatimiza wajibu wake kwenye eneo analoishi. Hili suala la ukatili wa kijinsia si suala geni nchini hasa eneo hili la kanda ya ziwa hivyo kuna kila sababu ya kuzidisha mapambano dhidi yake, cha muhimu ni kuzingatia mafunzo mliyopewa na muwezeshaji wenu” aliongeza Bw. Masele.


Mafunzo hayo yamefanyika kwa muda wa siku 5 kwa vijana 30 wa kike wenye umri kati ya miaka 18-24 kutoka wilaya mbili za Nyamagana na Ilemela jijini Mwanza. Lengo la Mafunzo ni kuwajengea vijana uwezo wao binafsi na uwezo wa kuelimisha jamii hasa Vijana wenzao  kupambana na kupinga Ukatili dhidi ya wanawake na wasichana katika maeneo wanayoishi.


Mafunzo yalianza Jumatatu tarehe 28 Aprili, 2014 mpaka tarehe 2 Aprili, 2014 katika Ukumbi wa Chuo cha Ufundi Stadi, VETA kilichopo Nyakato nje kidogo ya jiji la Mwanza.


Takwimu zinaonyesha bado jamii inakabiliwa na ukatili mkubwa wa kijinsia ambapo ubeberu wa wanaume pamoja na mila na desturi potofu zimeonekana kukandamiza jinsi ya kike zaidi kuliko jinsi ya kiume, ukatili huo ni wa kijamii, kiuchumi pamoja na kisaikolojia hivyo kunaitajika juhudi za dhati na makusudi kuweza kukabiliana na tatizo lilopo kwa jamii.


Akimalizia mawaidha yake kwa washiriki Bw. Masele alisema lengo la mafunzo hayo ni kuona mabadiliko katika mfumo juu ya kujali na kuheshimu haki za mwanamke na wasichana, kwani jamii nyingi zinapambana na mifumo miwili mikubwa, ambayo ni mfumo dume ambao umekuwa ukiwakandamiza wanawake katika jamii na mfumo wa kitabaka unaoongeza nafasi kati ya matajiri na masikini.


Shirika la KIVULINI kwa kushirikiana na Asasi ya Vijana  inayojulikana kama Wadada Centre for Solution Focus Approach ndio waandaji wa mafunzo hayo kupitia mradi wa kuwashirikisha vijana kuzui Ukatili majumbani na Ukatili wa Kingono chini ya ufadhili wa Shirika la terre des hommes ch (tdhschweiz) - Fursa kwa Vijana  la nchini Switzerland


Kivulini ni shirika lisilo la kiserikali linalojishughulisha na kutetea pamoja na kulinda Haki za Wanawake na Wasichana. Shiriki la Kivulini linahamasisha jamii (Wanawake, Wanaume na Vijana ) kulinda, kutetea Haki za Wanawake na Wasichana kwa kupinga vitendo vyote vya ukatili wa kijinsia. Makao makuu ya shirika yapo jijini Mwanza, Wilaya ya Ilemela, Tanzania.

Viewing all 110144 articles
Browse latest View live




Latest Images