Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110186 articles
Browse latest View live

Gavana wa Mombasa County na Seneta watembelea "Live talk" ya VOA

$
0
0
Misa ya Sima na Gavana Joho in Voa 078Kutoka kushoto Seneta wa County ya Monmbasa Hassan Omar , Mtangazaji wa VOA Abdushakur Aboud , Gavana wa Mombasa County Ali Joho na waziri wa Vijana , Jinsia na Michezo wa County hiyo Hazel Koitabawalipotembelea kipindi maarufu cha "LIVE TALK " idhaa ya Kiswahili ya Sauti ya Amerika-VOA Ijumaa Aprili 18,2014.Misa ya Sima na Gavana Joho in Voa 105Kutoka kushoto Waziri wa Vijana , Jinsia na Michezo katika County ya Mombasa, Katibu wa County Hamisi Mwaguya,Barbara Aron, Chanzera, mtangazaji wa VOA Aida Issa na Tuni Mwalukumbi msimamizi mwa utawala County. Misa ya Sima na Gavana Joho in Voa 097Kutoka kushoto Abdushakur Aboud, Mkuu wa idhaa ya Kiswahili Mwamoyo Hamza , Gavana wa Mombasa Ali Joho , Sunday Shomari,Seneta wa Mombasa County Hassan Omar, waziri wa County wa Vijana , Jinsia na Michezo Hazel Koitaba na katibu wa County Hassan Mwaguya. Kusikiliza kipindi hiki fuata link hii http://www.voaswahili.com/archive/jioni/latest/2948/2948.html na kwa picha zaidi ungana na Sunday Shomari.com

MABONDIA WAPIMA UZITO KWA AJILI YA MPAMBANO WA LEO UKUMBI WA PTA SABASABA, DAR ES SALAAM

$
0
0
Bondia Sukkasem Kietyongyuth  kutoka Thailand kulia akitunishiana misuli na Fransic Miyeyusho baada ya kupima uzito leo kwa ajili ya mpambano wao wa Jumamosi ya leo April 19 katika ukumbi wa PTA Sabasaba Dar es salaam.
Bondia Sukkasem Kietyongyuth  kutoka Thailand kulia akitunishiana misuli kwa mkono na Fransic Miyeyusho baada ya kupima uzito leo kwa ajili ya mpambano wao wa Jumamosi ya leo April 19 katika ukumbi wa PTA Sabasaba Dar es salaam 
Bondia Sukkasem Kietyongyuth  kutoka Thailand kulia wakipeana salamu ya heshima na Fransic Miyeyusho baada ya kupima uzito leo kwa ajili ya mpambano wao wa Jumamosi ya leo April 19 katika ukumbi wa PTA Sabasaba Dar es salaam. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

Washiriki wa kliniki ya Airtel Rising Stars kutua Dar Jumatatu

$
0
0
 Airtel Public Relations Manager Jackson Mbando speaks to the media at a press conference to announce the forthcoming Manchester United International Soccer Clinic to be held in Dar es Salaam from 23rd-27th April under the tutelage of coaches from Manchester United Soccer Schools.  He is flanked by the Tanzania Football Federation (TFF) President Jamal Malinzi .The event was held at the Airtel Tanzania Headquarters, 18th April 2014. 
 Tanzania Football Federation (TFF) President Jamal Malinzi speaks to the media at a press conference to announce the forthcoming Manchester United International Soccer Clinic to be held in Dar es Salaam from 23rd-27th April under the tutelage of coaches from Manchester United Soccer Schools.  He is flanked by Airtel Public Relations Manager Jackson Mbando.The event was held at the Airtel Tanzania Headquarters, 18th April 2014.

========  =======  ========
Washiriki wa kliniki ya Airtel Rising Stars kutua Dar Jumatatu
·      Ni kutoka nchi 12 Afrika
·      Waziri Bernard Membe mgeni rasmi siku ya ufunguzi
·      Kliniki kuendeshwa na makocha kutoka Manchester United

Dar es Salaam, Ijumaa 18 Aprili, 2014.  Wachezaji wa soka chini ya umri wa miaka 17 kutoka nchi 12 barani Afrika wanatarajiwa kuwasili jijini Dar es Salaam Jumatatu Aprili 21 kushiriki kliniki ya soka ya kimataifa.  Hii ni mara ya pili Tanzania imepewa heshima ya kuwa mwenyeji wa kliniki ya kimataifa baada ya ile iliyofanyika kwenye uwanja wa wa kisasa wa Taifa mwaka 2011.

Kliniki ya mwaka huu itakayofanyika kwenye uwanja wa Azam, Chamazi, nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam inakutanisha wachezaji chipukizi, wasichana na wavulana, kutoka nchi za Kenya, Uganda, Malawi, Sierra Leone, Burkina Faso, Chad, Congo Brazzaville, DRC, Niger, Madagascar, Gabon, Seychelles na mwenyeji – Tanzania. Mafunzo hayo ya siku tano mfululizo chini ya makocha wazoefu kutoka klabu maarufu duniani ya Manchester United yana lengo la kuwapa vijana mbinu mbalimbali za kisoka hasa katika eneo la ushambuliaji.

Kliniki hii ya kimataifa inashirikisha vijana waliofanya vizuri mwaka jana katika mashindano ya Airtel Rising Stars kwenye nchi zao pamoja na washindi wa mashindano ya kimataifa yaliyofanyika nchini Nigeria ambapo timu ya wasichana ya Tanzania ilitwaa uchampioni wa fainali hizo hizo.

Hafla ya uzinduzi wa kliniki hiyo imepangwa kufanyika siku ya Jumatano kwenye uwanja wa Azam na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mheshimiwa Bernard Membe atakuwa mgeni rasmi.  Membe anatarajiwa kuwahamasisha vijana kujituma ili kuweza kuendeleza ipasavyo vipaji vyao vya soka.

Hafla hiyo ya uzinduzi pia inatarajiwa kuhudhuriwa na mabalozi kutoka nchi zinazoshiriki kwenye kliniki hiyo itakayojumuisha mafunzo ya uwanjani na ya darasani. Vipindi vyote hivyo vitafanyika pale pale Azam Complex.

Program ya Airtel Rising Stars ni mpango wa maendeleo ya soka kwa vijana chini ya umri wa miaka 17 barani Afrika ukidhaminiwa na kampuni ya simu za kiganjaji ya Airtel na kuungwa mkono na Manchester United. Lengo lake ni kusaidia kuibua vipaji vya soka kutoka ngazi ya chini (grassroots) hadi Taifa.

MASHINDANO YA TANZANIA MOVIE TALENTS YAANZA LEO MKOANI MBEYA

$
0
0
 Mshiriki wa Tanzania Movie Talents akihojiwa mara baada ya kumaliza usaili katika Shindano la Tanzania Movie Talents linaloendelea muda huu katika Ukumbi wa Benjamin Mkapa uliopo Soko Matola Mkoani Mbeya
 
Baadhi ya washiriki waliojitokeza kwaajili ya kuhudhuria usaili wa Shindano la Tanzania Movie Talents wakijadiliana jambo kabla ya kuanza kwa usaili.
 
 Washiriki waliojitokeza kwaajili ya kushiriki mashindano yya Tanzania Movie Talents wakijaza fomu kwaajili ya usaili wa shindano la Tanzania Movie Talents linaloendelea Mkoani Mbeya ikiwa unawakilisha Kanda ya Nyanda za Juu Kusini
 Baadhi ya washiriki kutoka Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Mkoani Mbeya wakisubiri shindano la Tanzania Movie Talents kuanza.
Kundi la Kwanza La vijana waliojitokeza kwaajili ya usaili wa Shindano la Tanzania Movie Talents linaloendelea mkoani Mbeya muda huu.Picha na Josephat Lukaza wa Proin Promotions Limited - Mbeya.

Hatimaye Shindano la Tanzania Movie Talents limeanza rasmi leo katika Kanda ya Nyanda za Juu Kusini ambapo usaili huo unafanyika Mkoani Mbeya Katika Ukumbi wa Benjamini Mkapa uliopo Soko Matola Mkoani Mbeya.

Mpaka sasa Washiriki wapatao 150 wamejitokeza kwaajili ya kushiriki shindano hili la Tanzania Movie Talents ambapo washindi watatu kutoka kanda ya Nyanda za Juu Kusini watazawadiwa kitita cha Shilingi laki tano za Kitanzania na Baadae kupewa Tiketi ya Kuelekea Mkoani Dar Es Salaam kwaajili ya kushiriki fainali itakayowakutanisha Washindi waliopatikana katika Kanda ya Ziwa, Kati na kanda zilizobakia za Pwani na Kaskazini na mshindi katika fainali hiyo atajinyakulia Kitita Cha Shilingi Milioni 50 za kitanzania pamoja na Mikataba minono kutoka Kampuni ya Proin Promotions Limited na washindi kumi katika fainali hizo watakuwa chini ya kampuni ya Proin Promotions Limited na kuweza kutengeneza filamu ya Pamoja ambapo watanufaika na Mauzo ya filamu yao.

Mashindano ya Tanzania Movie Talents yataendelea Mkoani Mbeya kwa Siku nne ambapo siku ya jumanne washindi wa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini watapatikana na kupewa Zawadi zao.

TAARIFA KUTOKA SHIRIKISHO LA SOKA SOKA NCHINI (TFF) LEO

KUELEKEA SHEREHE ZA MIAKA 50, MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUFUNGUA KONGAMANO LA MUUNGANO MJINI ZANZIBAR

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati akifungua rasmi Kongamano la Muungano katika Ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Beach Resort, mjini Zanzibar leo Aprili 19, 2014.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzanoa, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza jambo na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, (Muungano) Samia Suluhu, wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Muungano lililofanyika kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Beach Resort, mjini Zanzibar leo Aprili 19, 2014.
Viongozi waliohudhuria Kongamano hilo, wakiwa meza kuu. Wa pili (kulia) Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, (wa kwanza kushoto) Makamu wa pili wa Rais wa Zanznibar, Balozi Seif Iddi, (wa pili kushoto) ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano) na (kulia) ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa pili wa Rais, Mohamed Aboud.

VIONGOZI WA JUMUIYA COLUMBUS, OHIO WAMFANYIA DINNER BALOZI LIBERATA MULAMULA NA MUMEWE

$
0
0
 Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Liberata Mulamula akisalimiana na katibu wa Jumuiya ya Watanzania Columbus, Ohio Bi. Happiness Salukele wakiwemo wajumbe wa Jumuiya Nasra Murumah, Chiseko Hamisi na kushoto ni mweka hazina wa Jumuiya Bi. Vera Teri
 Mhe. Balozi Liberata Mulamula na Mumewe Bwn. George Mulamula wakikaribishwa kwenye mgahawa wa Mitchell's Steakhouse wa Columbus, Ohio na wajumbe wa Jumuiya wakiwemo viongozi kwenye chakula cha jioni walichomuandalia Mhe. Balozi na Mumewe. Mhe. Balozi Liberata Mulamula yupo Columbus kwa ajili ya Fundraisng ya Jumuiya ya Watanzania Columbus, Ohio itayaofanyika leo Jumamosi April 19, 2014 katika ukumbi wa Comfort Inn uliopo 1213 E. Dublin Granville Road, Columbus, Ohio na kiingilio ni $15 na muziki utaporomoshwa na Dj Luke kutoka DC.
 Wajumbe wakimpokea Mhe. Balozi Liberata Mulamula na Mumewe Bwn. George Mulamula mara tu walipowasili kwenye mgahawa wa Mitchell's Steakhouse, anayesalimia na Balozi ni mjumbe Michael Mngodo.
Kutoka kushoto ni katibu wa Jumuiya Bi. Happiness Salukele, Mume wa Balozi Bwn. George Mulamula, Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Liberata Mulamula, mweka hazina Bi. Vera Teri na mjumbe Nasra Murumah.
 Wajumbe wakiangalia menu tayari kwa kuagiza chakula cha jioni walichomuandalia Mhe. Balozi pamoja na Mumewe.
 Wajumbe wakiwemo kwenye chakula cha jioni walichomuandalia Balozi pamoja na mumewe.
 Kutoka kushoto ni Deo Mwalujuwa, mjumbe Joe Ngwilizi, mjumbe Michael Mngodo na mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania Columbus Ohio, Bwn Jimmy James.

BONANZA LA MICHEZO LA PPF LAFANA SANA

$
0
0
Mkufunzi wa mazoezi ya viungo, Taifa Liwewa (Kushoto), akiwaongoza wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, wakati wa mazoezi ya viungo, kwenye bonanza la michezo lililoandaliwa na Mfuko huo na kufanyika viwanja vya Ustawi wa Jamii, Kijitonyama jijini Dar es Salaam Jumamosi Aprili 19, 2014. Mgeni rasmi kqwenye tamasha hilo lililoshirikisha michezo mbalimbali ikiwemo, kuvuta kamba na soka, alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa PPF, William Erio.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, William Erio, akikagua timu za soka za Mfuko huo, wakati wa Bonanza hilo.
Timu ya wanawake ya kuvuta kamba ya Mfuko wa Pesnheni wa PPF, ikizidiwa nguvu na wenzao wanaume kwenye mchezo wa kuvuta kamba. Hata hivyo timu hiyo ilijitutumua kwani katika raundi ntatu, ilishinda kwa taaabu raundi moja.
Mchezaji wa soka wa timu ya PPF, kutoka idara ya Utawala, Johnson Aloyce (Kushoto), akichanja mbuga, wakati wa pambano la soka dhidi ya Idara ya kuzuia Majanga.
Meneja Uhusiano nna Masoko ya Mfuko wa Pensheni wa PPF, Lulu Mengele (Katikati), akiwa sambamba na wafganyakazi wenzake, wakati wa mazoezi ya viungo.


Mechi ya Simba na Yanga yaelimisha namna ya kupambana na Malaria

$
0
0
Kampuni ya Vodacom Tanzania kwa kushirikiana Taasisi ya Malaria No More na THT(Tanzania house of talent) leo wameitangaza rasmi nambari maalum ambayo wateja wanaotumia huduma za Vodacom wanaweza kuitumia kupata taarifa zinazohusiana na ugonjwa wa malaria.

Ili mteja kuweza kupata taarifa hizo zinazohusisha jinsi ya kujikinga, tiba na masuala mengine mbalimbali ya Malaria anachopaswa mteja kufanya ni kujiunga kwa kutuma neno "Malaria" au "Mzinduka" kwenda nambari 15760 bila malipo.

Ujio wa huduma hii ni sehemu ya kampeni kabambe ya Mzinduka inayolenga kuongeza kasi katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa malaria hapa nchini ambayo Vodacom Foundation ni mshirika wake.

Nambari hiyo imetangazwa jijini dar es salaam kwenye uwanja wa taifa muda mfupi kabla ya kuanza kwa mechi kati ya Simba na Yanga kwa lengo la kuwashirikisha washabiki wa soka nchini kuunga mkono kampeni hiyo.

WAZIRI MKUU,MH. PINDA AFUNGA MAONYESHO YA TAASISI ZA MUUNGANO

$
0
0
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akipokea zawadi ya kinyago cha umoja kutoka kwa Naibu Waziri , Ofisi ya Makau wa Rais, Umy Mwalimu baada ya kufunga monyesho ya Taasisi za Muungano kwenye viwanja vya Mnazi Moja jijini dar es salaam Aprili 19, 2014. Kulia ni Naibu Waziri wa Wizara ya Fedha, Mwiguli Nchemba na kulia kwake Ni Kati Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Florens Turuka. (Picha na Ofisi ya Wairi Mkuu)

Sijakimbia (The official Song for Dual Citizenship) #Uraiapacha by Erica Lulakwa

SIMBA NA YANGA ZATOSHANA NGUVU UWANJA WA TAIFA JIJINI DAR LEO

$
0
0
Mshambuliaji wa timu ya Yanga , Hamis Kiiza (kulia) akiwania mpira na beki wa timu ya Simba, Nassor Masoud, katika mchezo wa Ligi kuu Tanzania Bara uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam leo.hadi mwisho wa mchezo,matokeni Yanga 1-1 Simba.
Mshamuliaji wa pembeni wa timu ya Yanga,Simon Msumva (kulia) akijaribu kuwatoka mabeki wa timu ya Simba, katika mchezo wa Ligi kuu Tanzania Bara uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam leo.hadi mwisho wa mchezo,matokeni Yanga 1-1 Simba.
Mshambuliaji wa timu ya Yanga Didier Kavumbagu (katikati) akiwatoka mabeki wa timu ya Simba katika mchezo wa Ligi kuu Tanzania Bara uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam leo.hadi mwisho wa mchezo,matokeni Yanga 1-1 Simba.
Wachezaji wa timu ya Yanga,wakishangilia goli lao la kusawazisha.

MWIMBAJI WA KIMATAIFA WA NYIMBO ZA INJILI KEKE LETSO PHOOFOLO AWASILI DAR KWA AJILI YA TAMASHA LA PASAKA

$
0
0
Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha la Pasaka, Alex Msama akipeana mkono na mwimbaji wa kimataifa wa nyimbo za injili kutoka Afrika ya Kusini, Kekeletso Phoofolo mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo, kwa ajili ya tamasha la Pasaka litakaloanza kutimua vumbi kwenye Uwanja wa taifa leo. 
Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha la Pasaka, Alex Msama (kulia), akiwa na mwimbaji wa Kimataifa wa nyimbo za injili kutoka Afrika ya Kusini, Kekeletso Phoofolo mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam leo, kwa ajili ya tamasha la Pasaka litakaloanza kutimua vumbi kwenye Uwanja wa taifa Jumapili. 
Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha la Pasaka, Alex Msama akipeana mkono na mwimbaji wa kimataifa wa nyimbo za injili kutoka Afrika ya Kusini, Kekeletso Phoofolo mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimatifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya tamasha la Pasaka litakaloanza kutimua vumbi Jumapili kwenye Uwanja wa Taifa
Mwimbaji wa kimataifa wa nyimbo za injili kutoka Afrika Kusini, Kekeletso Phoofolo (kushoto), akiimba kwa hisia moja ya nyimbo zake mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya tamasha la Pasaka.

Tanzania Diaspora - The case for Dual Citizenship

MABONDIA CHEKA, MIYEYUSHO WASHINDWA KUTAMBA; KING CLASS MAWE AMSAMBARATISHA MUSTAFA DOTO

$
0
0
Bondia Francis  Cheka (kushoto) akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Gavad Zohrehvand wa Iran wakati wa mpambano wao wa kirafiki wa kimataifa uliofanyika katika ukumbi wa PTA Sabasaba Jumamosi jijini Dar es salaam. Mpambano huo uliamuliwa kwa droo ya kufungana point
Bondia Francis  Cheka kushoto akipambana na Gavad Zohrehvand wa Iran wakati wa mpambano wao wa kirafiki wa kimataifa uliofanyika katika ukumbi wa PTA Sabasaba jijini Dar es salaam mpambano huo uliamuliwa kwa droo ya kufungana point 
Bondia Francis  Cheka kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Gavad Zohrehvand wa Iran wakati wa mpambano wao wa kirafiki wa kimataifa uliofanyika katika ukumbi wa PTA Sabasaba jijini Dar es salaam mpambano huo uliamliwa kwa droo ya kufungana point 

 Bondia Sukkasem Kietyongyuth  kutoka Thailand kulia akiwa amemkalisha bondia Francis  Miyeyusho katika raundi ya kwanza ya mpambano wa raundi kumi na kushinda kwa K.O. 

CHAMA CHA MADAKTARI WANAFUNZI TANZANIA CHATOA HUDUMA ZA AFYA ZANZIBAR

$
0
0
 Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Dokta Sira Ubwa Mamboya akimkaribisha Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Iddi katika uzinduzi wa kampeni za kutoa huduma za kisukari na shinikizo la damu zitakazofanyika Mikoa yote ya Zanzibar.

 Mratibu wa mtadi wa kutoa huduma za kisukari na shinikizo la damu Mr. Siraji M. Mtulia akitoa maelezo mafupi ya mradi huo utakaoanza kutekelezwa leo na Chama cha wanafunzi Madaktari Tanzania wakishikiana na Wizara ya Afya Zanzibar.
  Mkuu wa CHUO cha (IMTU) Prof. Flora Fabian akitoa maelezo kuhusu madaktari hao walivyojipanga kufanya kazi katika Mikoa yote ya Unguja na Pemba.
 Makamu wa Pili wa Rais Balozi. Seif Ali Iddi akiwahutubia Madaktari na wananchi waliofika katika uzinduzi wa kampeni za kutoa huduma za kisukari na shindikizo la damu huko ukumbi wa Chuo Kikuu cha Taifa Suza Mjini Zanzibar.
 Balozi Seif na Naibu Waziri wa Afya Dkt. Sira wakikagua utoaji huduma mara baada ya kuzindua.
 Makamu wa Pili wa Rais Balozi. Seif Ali Iddi (wakatikati waliokaa) katika picha ya pamoja na wanafunzi madaktari kutoka vyuo mbalimbali Tanzania.
Balozi Seif akiagana na wanafunzi madaktari mara baada ya kuzindua huduma za upimaji afya katika sherehe zilizofanyika ukumbi wa Chuo Kikuu cha Taifa Suza Mjini Zanzibar.
PICHA ZOTE NA MAKAME 
MSHENGA WA MAELEZO ZANZIBAR.

mabingwa wapya wa ligi kuu ya bara Azam FC watawazwa rasmi

$
0
0
Na Sultani Kipingo
Mabingwa wapya wa Tanzania, Azam FC, wametawazwa rasmi na kukabidhiwa kombe lao na Rais wa TFF, Jamal Malinzi, katika uwanja wa Azam Complex huko Chamazi, Dar es salaam. 
Hii ni baada ya Azam FC kucheza mechi yao ya mwisho  na JKT Ruvu na kuifunga timu hiyo ya jeshi la kujenga taifa kwa mabao 1-0 
Mshambuliaji kutoka Uganda, Bryan Umonyi, ndiye alifunga bao hilo baada ya kuingia kuchukua nafasi ya Kipre Tchetche. Watu wengi sana walijazana uwanjani hapo kushuhudia  pambano hilo ambalo halikuwa na kiingilio. Vikundi mbalimbali wakiwemo Wanaume TMK walioongozwa na Mheshimiwa Temba vilitoa burudani.
 Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) akimkabidhi Kombe la ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Nahodha wa Azam FC, John Bocco jioni hii baada ya kuifunga bao 1-0 JKT Ruvu Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.

Mabingwa wakisherehekea na taji lao, sherehe za ubingwa zimeendelea Azma Complex hadi usiku wa manane. 
Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

KABLA YA KUANZA KWA MTANANGE WA WATANI WA JADI SIMBA NA YANGA-SOMO LATOLEWA KUHUSU MALARIA NO MORE

$
0
0
 Wasanii mahiri wanaounda kundi la THT wakiimba wimbo wa Malaria No More  kabla ya mechi kuanza ya watani wa jadi Simba na Yanga.Wakati Vodacom Tanzania  kushirikiana na Taasisi ya Malaria No More na THTwalipokuwa wakitangaza namba maalumu ambayo wateja wanaotumia huduma za kampuni hiyo wanaweza kuitumia kupata taarifa zinazohusiana na ugonjwa wa malaria. Ili mteja kuweza kupata taarifa hizo zinazohusisha jinsi ya kujikinga, tiba na masuala mengine mbalimbali ya Malaria anachopaswa mteja kufanya ni kujiunga kwa kutuma neno "Malaria" au "Mzinduka" kwenda nambari 15760 bila malipo.
Meneja Uhusiano wa Mambo ya nje wa Vodacom Tanzania Salum  Mwalim akitangaza namba maalumu ambayo wateja wanaotumia huduma za Vodacom wanaweza kuitumia kupata taarifa zinazohusiana na ugonjwa wa malaria. Ili mteja kuweza kupata taarifa hizo zinazohusisha jinsi ya kujikinga, tiba na masuala mengine mbalimbali ya Malaria anachopaswa mteja kufanya ni kujiunga kwa kutuma neno "Malaria" au "M zinduka" kwenda nambari 15760 bila malipo.

Mnada mkubwa wa Malori ya Mizigo aina ya Volvo na Leyland DAF

$
0
0
Jumamosi ya tarehe 26/4/2014 saa nne Asubuhi katika viwanja vya Evangelical Assemblies of God Kijitonyama kutakuwa na mnada wa hadhara wa Malori makubwa ya mizigo aina ya Volvo na Leyland Daf



ngoma azipendazo ankal

Viewing all 110186 articles
Browse latest View live




Latest Images