Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109591 articles
Browse latest View live

SIKU YA MKULIMA WA UFUTA BABATI YAFANA SANA

0
0
Wasanii wa Goroa Tradition Dancing group wa Kata ya Qash Wilaya ya Babati Mkoani Manyara, wakitoa burudani kwa wadau wa zao la ufuta, kwenye siku ya mkulima iliyofanyika katika kitongoji cha Maweni, Kata ya Endadosh Wilaya ya Babati Mkoani Manyara.
Afisa kilimo wa mradi wa ufuta wa shirika la Farm Africa, Tumaini Elibariki akimsikiliza Mtafiti wa Biosciences for Farming in Africa, kutoka London Uingereza, Claudia Canales kwenye siku ya mkulima iliyofanyika juzi katika kitongoji cha Maweni, Kata ya Endadosh Wilaya ya Babati Mkoani Manyara.
Mmoja kati ya wakulima wa mfano wa zao la ufuta, Edward Lemetei wa Kijiji cha Kakoi, Wilayani Babati, akipokea zawadi ya fedha kutoka kwa Afisa kilimo wa Mkoa wa Manyara, Coletha Shayo zilizotolewa na shirika la Farm Africa, katika siku ya mkulima kwenye kijiji cha Endadosh, kulia ni Afisa Mawasiliano wa Farm Africa, Goodness Mrema.
Mkulima wa zao la ufuta katika Kitongoji cha Maweni, Kijiji cha Endadosh, Kata ya Qash, Wilaya ya Babati Mkoani Manyara, John Kunda, akiwaelezea Ofisa kilimo wa huo, Coletha Shayo na Ofisa kilimo wa mradi wa ufuta wa Shirika la Farm Africa, Tumaini Elibariki namna alivyoliendeleza shamba lake la ufuta.
Afisa kilimo wa mradi wa ufuta wa shirika la Farm Africa, Tumaini Elibariki akiwa ameshikilia kifaa cha kielekrtoniki (tablet) ambacho wakulima wengi wa zao la ufuta wamekuwa wakikitumia kwa ajili ya mafunzo ya kilimo na wakulima 397 wa Wilaya ya Babati Mkoani Manyara walinufaika na kilimo kupitia mafunzo hayo.

MAMA KIKWETE AWAHIMIZA WALEZI NA WAZAZI KUWAPATIA WATOTO UJI NA UGALI WA DONA

0
0
Na Anna Nkinda – Maelezo, Lindi

Wazazi na walezi wameshauriwa kuwapa watoto uji na ugali wa unga wa dona na siyo sembe kwakuwa unga wa dona una kiini cha mahindi ambacho kinakirutubisho kinachosaidia ukuaji na uwezo wa akili ya binadamu.

Ushauri huo umetolewa jana na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi  (CCM) Taifa (NEC) wilaya ya Lindi mjini Mama Salma Kikwete wakati akiongea  kwa nyakati tofauti  na viongozi wa Halmashauri kuu ya tawi ya Chama hicho  katika matawi ya Mnazi Mmoja, Amani na  Muungano yaliyopo katika kata  ya  Mingoyo wilaya ya Lindi mjini.

Mama Kikwete ambaye pia ni Mke wa Rais Jakaya Mrisho Kikwete  alisema siku hizi watu wengi wanapenda kutumia unga wa sembe ambao hauna virutubisho vyovyote katika mwili kwani unapokoboa mahindi kiini kinabaki katika pumba ambazo wanapewa wanyama na binadamu kukosa virutubisho vya muhimu katika miili yao.

“Watoto wetu wanatakiwa kupata lishe bora ambayo itawajenga akili zao, wasiwe na mambo mengi na kufanya zaidi ya kwenda shule na kusoma . Wakiwa shuleni watahitaji kunywa uji au kula chakula cha mchana hivyo basi ni muhimu kwa walezi kuchangia  chakula cha mtoto kwakuwa mwanafunzi akishiba ataweza kusoma vizuri na kufaulu masomo yake .

MAALIM SEIF AONGOZA ZOEZI LA UPANDAJI MITI KITAIFA,MJINI UNGUJA

0
0
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akipanda mti katika uzinduzi wa zoezi la upandaji miti Kitaifa, katika eneo la barabara ya Jendele/Unguja Ukuu.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akizungumza katika uzinduzi wa zoezi la upandaji miti Kitaifa, katika eneo la barabara ya Jendele/Unguja Ukuu.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akiongozana na Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo na Maliasili, Affan Othman Maalim (kushoto) katika uzinduzi wa zoezi la upandaji miti Kitaifa, barabara ya Jendele/Unguja Ukuu.
Baadhi ya wananchi wakishuhudia uzinduzi wa zoezi la upandaji miti Kitaifa, katika eneo la barabara ya Jendele/Unguja Ukuu ambapo mgeni rasmi alikuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad. (Picha na Salmin Said, OMKR)

Familia Kitchen Party Gala ndani ya jiji la Mwanza

0
0
Wanawake wa jiji la Mwanza wamepata nafasi ya kuongea na Mama Victor,Aunt Sadaka na Getrude Mongela katika Familia Kitchen Party Gala. Shughuli imefanyika jana Jumamosi tarehe 19,katika ukumbi wa Gold Crest Hotel.

Ukiachana na maongezi kuhusu mahusiano na masuala ya kina mama,vilevile wanawake walipata nafasi ya kupata huduma na ushauri wa Uzazi wa mpango,vipimo vya saratani/kansa ya mlango wa uzazi iliyotolewa bure na Familia kupitia PSI Tanzania.
Mtaalam wa Maswala ya saikolojia,Aunt Sadaka akitoa somo kwa Wanawake wa jiji la Mwanza wakati wa hafla ya kina mama ya Familia Kitchen Party Gala.
Sehemu ya Kina mama wa Jiji la Mwanza wakifatilia mada mbali mbali zilizokuwa zikitolewa kwenye Familia Kitchen Party Gala.
Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya,Mwasiti Almas akitoa burudani kwenye hafla hiyo.

msanii wa orijino komedi mpoki aalikwa ujerumani kuhudhuria sherehe za muungano

0
0

Msanii maarufu nchini Tanzania  Kutoka kundi la Orijino Komedi al maarufu kama Mpoki a k a Muarabu wa Dubai anatarajiwa kuondoka nchini mapema mwanzo wa wiki hii kwenda nchini Ujerumani kuhudhuria  Mkutano mkuu wa Umoja wa Watanzania Ujerumani (U T U), utakaoambatana na Kongamano la kibiashara pamoja na Sherehe za Muungano wa Tanzania , zitakazoanza  siku ya ijumaa tarehe 25.04.14 na kumalizika siku ya Jumamosi Tarehe 26.04.14.

Mpoki amesema kuwa  umuhimu mkubwa wa safari yake ni  kuwakilisha wasanii wa Tanzania katika Tamasha hili kubwa  la aina yake, na  kufafanua  kuwa wakati umefika kwa wasanii wa Tanzania kushirikiana kikamilifu na Watanzania wanaoishi nje ya nchi ili kuweza kupata fursa mbali mbali  zilizopo huko. 
Amesema  amevutiwa sana na Umoja Wa Watanzania Ujerumani (U T U) kwa shughuli zake   mbali mbali ambazo umekwishazifanya nchini humo  na ameamua kutoa mchango wake wa hali na mali kuhakikisha     (U T U) inafanya vizuri zaidi  na kwamba yeye binafsi amekuwa ni mfuatiliaji wa karibu sana  wa shughuli za umoja huo.

 Mwenyekiti  wa Umoja Wa Watanzania Ujerumani Bw. Mfundo Peter Mfundo alithibitisha  safari ya msanii huyo Maarufu nchini Tanzania, na kusema U T U Ilipendelea sana wasanii zaidi kuhudhuria sherehe hizi lakini kwa bahati mbaya  haikuwezekana  kutokana na mambo yalio nje ya uwezo wao ingawa UTU  ni chombo kinachokubali sana na kuzifagilia kazi za wasanii wa Tanzania.

U T U inamtakia Bw Mpoki Safari njema.

salamu za pasaka toka globu ya jamii kwa wadau duniani kote

0
0
Uongozi wa Michuzi Media Group na watendaji wote unawatakia wadau wa Globu ya Jamii kila pembe ya dunia PASAKA njema. Furaha yenu ndio furaha yetu, na BWANA awabariki afya njema.

THE KOP IN TZ WASHEREHEKEA USHINDI WA LEO

0
0
Baadhi ya wanachama wa THE KOP IN TZ wakisherehekea ushindi dhidi ya Norwich leo. Mwenyekiti wa umoja huo, Musleh (mwenye kapelo), kwa niaba ya THE KOP wote nchini anatoa pia salamu za PASAKA na kuwatakia wanachama wote sikukuu njema ya furaha kwa zawadi hii ya YNWA.

WAUMINI WA DHEHEBU YA ORTHODOX WASHEREHEKEA SIKUKUU YA PASAKA.

0
0
Balozi wa Urusi anayefanyakazi hapa nchini  Alexander Rannikh  akiwa  na waumini wenzake wakipewa Baraka na Askofu  wa Dhehebu ya Orthodox  Askofu Dimitrios  wakati wa   Ibada ya Kusherehekea Sikukuu ya Pasaka iliyowashirikisha  Waumini mbalimbali  wakiwemo Watanzania,Wagiriki na Warusi.Ibada hiyo iliafanyika jijini Dar es Salaam.

Balozi wa Urusi anayefanyakazi hapa nchini  Alexander Rannikh akipewa Baraka na Askofu  wa Dhehebu ya Orthodox  Askofu Dimitrios  wakati wa   Ibada ya Kusherehekea Sikukuu ya Pasaka  iliyowashirikisha  Waumini mbalimbali wakiwemo Watanzania,Wagiriki na Warusi.Ibada hiyo iliafanyika jijini Dar es Salaam.
Balozi wa Urusi anayefanyakazi hapa nchini  Alexander Rannikh, akiteta jambo na Askofu Mkuu wa Dhehebu ya Orthodox  Askofu Dimitrios baada ya kumalizika kwa Ibada ya Kusherehekea Sikukuu ya Pasaka  iliyowashirikisha  Waumini mbalimbali  wakiwemo Watanzania,Wagiriki na Warusi.Ibada hiyo iliafanyika jijini Dar es Salaam
Balozi wa Urusi anayefanyakazi hapa nchini  Alexander Rannikh  akiwa  na waumini wenzake wakipewa Baraka na Askofu  wa Dhehebu ya Orthodox  Askofu Dimitrios  wakati wa   Ibada ya Kusherehekea Sikukuu ya Pasaka iliyowashirikisha  Waumini mbalimbali  wakiwemo Watanzania,Wagiriki na Warusi.Ibada hiyo iliafanyika jijini Dar es Salaam.


Baadhi ya Waumimi wa Dhehebu ya Orthodox  wakiwa katika Ibada ya kusherehekea  ufufuko wa Yesu Kristu (Pasaka) iliyofanyika katika Kanisa hilo lililpo eneo la Red Cross jijini Dar es Salaam. Picha na Albart Jackson 


UZINDUZI WA TAMASHA LA UTALII CUP MTO WA MBU MONDULI

0
0

 Mkuu wa Wilaya ya Monduli Jowika Kasunga akikagua timu ya Rift Valley B, iliyocheza na Rift Valley A na kufungwa kwa jumla ya goli 2-0
 Kikundi cha sarakasi cha mto wa mbu kikiburudisha wakati wa uzinduzi wa Tamasha la michezo la Utalii Cup  katika uwanja wa barafu katika eneo la mji mdogo wa Mto wa mbu, wilayani Monduli,Arusha.
Mkuu wa wilaya ya Monduli aliyekuwa mgeni rasmi wa uzinduzi wa tamasha la utalii CUP akipanda mti wa kumbukumbu katika shule ya sekondari ya Mto wa mbu. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

taswira za misa ya basaka kanisa katoliki jimbo la dodoma leo

0
0

 Askofu Gervas John Nyaisonga wa Kanisa Katoliki Jimbo la Dodoma akitoa Mahubiri wakati wa Misa ya Pasaka, kuadhimisha miaka zaidi ya elfu mbili tangu Ufufuko wa Yesu Kristo. Ibada hii iliyohudhuriwa na maelfu ya watu imefanyika katika Kanisa Kuu la Paulo wa Msalaba Dodoma.  
Askofu Gervas John Nyaisonga wa Jimbo katoliki la Dodoma akiwabariki waumini kwenye Misa ya Pasaka katika Kanisa Kuu la Paulo wa Msalaba Dodoma, kuadhimisha miaka Zaidi ya elfu mbili tangu Ufufuko wa Yesu Kristo kushoto kwake ni Paroko wa kanisa hilo Paroko Daudi Ngimba.

 Waumini wa kanisa katoliki Kanisa Kuu la Paulo wa Msalaba Dodoma wakifuatilia ibada ya pasaka iliyokuwa ikiongozwa na Askofu Gervas John Nyaisonga.
 Waumini wa kanisa katoliki Kanisa Kuu la Paulo wa Msalaba Dodoma wakifuatilia ibada ya pasaka iliyokuwa ikiongozwa na Askofu Gervas John Nyaisonga.
 Waumini wa kanisa katoliki Kanisa Kuu la Paulo wa Msalaba Dodoma wakifuatilia ibada ya pasaka iliyokuwa ikiongozwa na Askofu Gervas John Nyaisonga.
Waumini wa kanisa katoliki Kanisa Kuu la Paulo wa Msalaba Dodoma wakifuatilia ibada ya pasaka iliyokuwa ikiongozwa na Askofu Gervas John Nyaisonga.Na Deusdedit Moshi Mtendaji mkuu wa Photo Solutions na Mwakilishi wa Michuzi Blog Kanda ya kati.

Barua ya wazi kwa wabunge na vyama vyote vya siasa na viongozi wote na kwa umma wa Tanzania.

0
0
Na mshurukuru Mungu kwa kunipa afya na uzima mpaka leo na mpaka kufikia hapa tulipofika na kuweza kuona miaka zaidi ya hamsini ya uhuru na miaka hamsini ya Muungano  na mpaka kufikia hatuwa ya kuweza kupata katiba mpaya au mchakato wa kuandika katiba mpya,
Na wewe Bwana michuzi nashukuru kwa kazi yako unayoifanya ya kutupa matukio yanayotokea uko nyumbani kwa video na kwa picha,Mungu akurinde na akupe uzima na Afya.

Bwana michuzi wazungu wanasema  damu ni nzito kuliko maji na kubomoa ni rahishi lakini kujenga ni kazi, nayasema haya sababu Tanzania ya leo inapoelikea kuna njia ambayo ni giza na giza hilo linaweza kuleta janga ambalo lina weza umwagikaji wa damu na tukapata janga ambalo litaifanya nchi kugawanyika na  kuwa sawa sawa somalia kwa udini,ukabila,au South Sudan au nchi zingine zilozoisha pata misukosuko za west Africa liberia, Siera leon nina yasema haya kutokana na kauli zinatolewa  na baadhi ya vyama vya siasa toka vyama vya siasa vilipoanziswa,na maneno ya wabunge wa katiba.

Wa Tanzania miaka hamsini ya uhuru kuna mengi mazuri ambayo yamepatikana na mengine yalishndikana kwa sababu zetu sisi wenyewe au sera za serikari toka tulipo pata uhuru,na katika miaka hii hamsini ya muungano kuna mengi yamefanikiwa na mengine yamechukuwa muda kutatuliwa na mengine yanatakiwa kutatuliwa kwa kuangalia kule tunakotoka na kuangalia nini cha kufanya,

Dunia ya miaka ya 60 ,70,80,90,na leo kunatofauti kubwa sana kwa kifupi wakati nikiwa nasoma miaka ya 80 tulikuwa tupiga simu posta alafu posta ndio inakuunganisha na mtu wa dar au mwanza lakini leo ni sekunde, ndugu wananchi kunamambo mambo ambayo kwa ukweli lazima tuwaenzi wazee wetu hao walio tutangula Mzee Nyerere na Mzee Karume waliamua kujenga nchi mpya nchi yenye usawa nchi ambayo haina makabila nchi ambayo haina dini nchi ambayo ni ya watanzania sio wazungu wala weusi wala wahindi wala waarabu walijenga nchi ya waTanzania ambayo ina lugha moja ni kitu ambacho ni cha kujivunia nchi nying za k iAfrika zinaongea lugha za kingeni lakini Tanzania ina lugha yake ambayo siyo mkoloni.

Ndugu wananchi mimi nimeona vita ya Uganda from 83 mpaka Mzee Museveni alipochukuwa nchi 1986,vita ya Rwanda ya mwaka 1990 mpaka 1994 nimeiona na baadhi ya ndugu zangu walikufa katika hiyo vita na pia nyinyi watanzania mumeyaona na mumeyasikia ya Congo kina dada na kina mama wanavyoeteseka sana wamedakwa na kuuliwa kama wanyama sababu ya kauli za viongozi kuwa na watu wanaotaka madaraka kwa kutumia nguvu au kumwaga damu za wengine na kuwa na watu wanaojiita viongozi kumbe hawana Vision bali ni ma selfish nawaomba muwe macho na viongozi wa vyama vya siasa wawe wa CCM,CHADEMA,CUF,DP,NCCR, yule yoyote anayetumia lugha za kuleta vurugu siogopi  hapa nitasema kabisa Chadema walisema nchi haitatawalika,na juzi hapa katika bunge hili la katiba mwenyekiti wa chama cha CUF Mr lipumba aliwaita wabunge wa CCM eti ITARAHAMWE ni kitendo cha kushangaza kwa mtu aliyesoma mpaka kuwa profesa na kuamua kutumia neno kama hilo katika bunge maana yake Mr lipumba anamaanisha wana CCM wote Tanzania ni ITARAHAMWE nina omba Mr lipumba atupe jibu sababu wabunge wengi katika hilo bunge ni wana CCM

Ningependa kusema Mr Lipumba umesoma na wewe ni mwa siasa na ni kiongozi wa chama omba Radhi kwa WaTanzania kwa kutumia neno ambalo alifai katika bunge la Tanzania na kwa jamii.

Ndugu wananchi nirudi kwenye point ya katiba ni kweli tunataka katiba ya wa Tanzania na siyo ya CCM,CHADEMA,au CUF,NCCR, tunataka katiba ya Jamuhuri ya Muungano katiba yenye usawa katiba ambayo ambayo ina Raisi na makamo wake katiba ambayo ina waziri mkuu wa Tanzania bara,katiba ambayo ina waziri  waziri mkuu wa Tanzania visiwani Zanzibar katiba ambayo inaonyesha madaraka yao katiba ambayo itaongoza Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na katiba inayoonyesha ni nani amri jeshi mkuu  wa Tanzania. ndugu  maoni yangu haya ninayotowakutoka na mambo ambayo nimejifunza katika maisha au tabu namambo ambayo nimeyaona kwenye vita za wenyewe kule Uganda na kule Rwanda.
Ndugu wananchi na ndugu Wabunge, katiba si kitu kidogo na wala si kitu cha kukulupuka mumesema mengi lakini wakati umefika mumetukana lakini wakati umefika mumeitana majina lakini wakati umefika miaka ya hamsini ya uhuru imekuwa na amani na mafanikio  na miaka hamsini ya muuungano pia imekuwa na mafanikio na pia ina mengi amabayo yanatakiwa yafanyiwe marekebisho na ambayo yanatakiwa kufanywa  ninawaomba msifikiri eti kwa vile muko bungeni WaTanzania wengine hawaipendi nchi yao au watakaaa na kuendelea kusikia mambo yasiyo na maana au faida wakati nii huu mkae mutakafari kwa kirefu na muisome katiba kwa kwa kirefu kifungu kwa kifungu alafu mtuandikihe katiba ambayo italeta maendeleo kwa kizazi kinachofata,katiba ambayo ni ya wa Tanzania kama tunaenda kwenye Fedal government muundo ambao utalinda heshima ya nchi na watu wake na kuleta maendeleo.katiba ya ambayo itatujenja kiutendaji kazi katiba inayoonyesha au mwongozo wa uwajibikaji.
Cha mwisho ningependa kuwagusia Amani na maendeleo yaliyoanzishwa na Wazee wetu ndio kitu cha kujivunia kuwatukana au kuwakejeli ni kukosa adabu ni lazima kutumia majina ya kwa heshima na kuelimisha ata kama kuna makosa waliyafanya wao walikuwa ni binadamu kama wewe na mimi.
Bwana michuzi nashukuru kwa  kunipa nafasi hii tena Mungu akubariki

Mungu ibariki Tanzania na watu wake.

Mdau Yusef Israel

FUNDRAISING DINNER COLUMBUS YAFANA BALOZI LIBERATA MULAMULA ASISITIZA WATANZANIA UGHAIBUNI WAJIUNGE NA BIMA YA WESTAD

0
0

Mhe. Liberata Mulamula akipokewa na mweka hazina wa Jumuiya Bi. Vera Teri mara tu alipowasili kwenye fundraisng dinner ya Jumuiya ya Watanzania Columbus, Ohio iliyofanyika Comfort Inn siku ya Jumamosi April 19, 2014.

Mhe. Balozi Liberata Mulamula akiingia ukumbini akiwa ameongozana na mweka hazima Bi. Vera Teri. Kwa habari kamili na picha kibao
 BOFYA HAPA

Taswira za PASAKA Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara

0
0
 Wanakwaya wa Mtakatifu Cecilia wa Kanisa Katoliki Parokia ya Bikira Maria Mama wa Rozali Takatifu wa Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, wakiimba baada ya kumaliza misa ya Pasaka kanisani hapo leo asubuhi.
 Padri Modestus Makiluli, wa Kanisa Katoliki Parokia ya Bikira Maria Mama wa Rozali Takatifu wa Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara,akiendesha misa ya ubatizo na komuniyo kwenye kanisa hilo wakati wa sikukuu ya Pasaka leo


Familia ya Kalacheni, ikiwa na furaha baada ya kumaliza kusali sikukuu ya pasaka kwenye Kanisa Katoliki Parokia ya Bikira Maria Mama wa Rozali Takatifu wa Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara.
Bwana harusi Ladslaus Manyanya (kulia) na mkewe Patricia Magero, (wa pili kulia) wakiwa na wapambe wao baada ya kufunga ndoa kwenye sikukuu ya pasaka katika Kanisa Katoliki Parokia ya Bikira Maria Mama wa Rozali Takatifu wa Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara.

mpigie kura diamond ashinde TUZO ZA MTV MAMA'S

wimbo wa taifa wa bwawa la maini


ASKOFU KKKT IRINGA DKT MDEGELA ATAKA'UKAWA' WASIRUHUSIWE KUENEZA CHUKI NCHINI, AWATAKA WAREJEE BUNGENI AMA WAFUNGASHE VIRAGO WARUDI NYUMBANI ASEMA SERIKALI NI MBILI PEKEE

0
0
Askofu Mkuu wa Kanisa la Kilutheri (KKT) dayosisi ya  Iringa  Dkt. OwdenburgMdegela
Wachungaji na  msaidizi wa Askofu kulia wakifuatilia salam za  pasaka zilizokuwa  zikitolewa na askofu Dkt. Mdegela
Waumini  wa KKKT usharika wa kanisa  kuu Iringa leo.
Kwa picha zaidi BOFYA HAPA
Na  Francis Godwin, Iringa 

ASKOFU mkuu wa Kanisa la Kilutheri (KKT) dayosisi ya  Iringa  Dkt. OwdenburgMdegela ameitumia ibada  ya Jumapili ya Pasaka leo  kulaani vikali  wale wote  wanaowatukana waasisi wa Taifa  hili Sheikh Abeid Amani Karume  na Mwalimu hayati Julius Kambarage Nyerere.
Askofu Dkt  Mdegela amesema kuwa watu hao wanapaswa kuwaomba radhi  watanzania huku akisisitiza wajumbe umoja wa katiba ya wananchi (UKAWA) kurejea bungeni ama  kufungasha  virago  vyao na kurudi nyumbani kwao na sio kuzunguka kupandikiza chuki kwa wananchi.
Askofu Dr Mdegela aliyasema hayo leo  wakati akitoa  salam za pasaka kwa  waumini  wa Dayosisi hiyo kupita washarika wa  kanisa  kuu.

Dkt. Mdegela asema "Watanzania tunataka  kuikataa lulu tuliyopewa na Mungu lulu ya amani na  kuanza  kutafuta kuvuruga amani  na utulivu  wetu ambayo ni lulu ya pekee inayogombewa na nchi  nyingine na  kuwa  wanaotaka lulu  hiyo ivurugike wasivumiliwe kamwe.
"Kinachofanywa  bungeni kwa  sasa ni mzaha wa hali ya juu na  Watanzania wanapaswa  kuwachunguza vema  wawakilishi wao hao wakiwemo wabunge wa vyama  vyote na  wale wanaoeneza mbegu ya  chuki  wasichaguliwe tena...."

Asema wajumbe wa bunge la katiba  hawana  sifa ya  kutengeneza katiba kwani  wametanguliza mzaha na matusi  yasiyo na tija  na kuwa hawa  wanaokwepa  bunge na kutaka kuzunguka kwa wananchi  wanapaswa kuzuiwa kufanya  hivyo na vyombo vya usalama kwani wanataka  kuipeleka nchi pabaya.
"Kama wamekula pesa za wananchi kwa muda  wote huo kwa ajili ya kuunda katiba iweje  leo  watoke bungeni na kudai  kuja kwa wananchi mikono mitupu??" amehoji.

"Wananchi tuwakatae wajumbe  wanaotaka  kuzunguka kupandikiza  chuki kwa wananchi kwa kujiita  wao wapo kwa ajili ya katiba ya  wananchi hali  wamekimbia bunge na kutaka  kutuwakilisha nje ya  bunge 
"....tunawakataa  wao na mawazo yao na pia kama wajumbe wa bunge  hilo  wameshindwa kazi tutaikataa rasmu ya katiba ambayo italenga  kutugawa  watanzania.
"Na niweke  wazi mwenyekiti wa tume ya mabadiliko ya katiba Jaji Joseph Warioba mbali ya kazi  hiyo bado tunawajibu wa kumrekebisha pale  alipokosea kwani Wazanzibar wa Pemba wanataka serikali nne sio tatu mbona hajaeleza
" ....nasema serikali mbili ni  jibu kama haiwezekani bado tuwe na serikali moja itakayotuunganisha"
Hata  hivyo Dr Mdegela alisema  kuwa msimamo  wake na waumini  wa kanisa  hilo ni kuwa na serikali mbili na ikiwezekana  kuwa na serikali  moja  pekee na si vinginevyo na iwapo  wajumbe wa  bunge la katiba  wameshindwa kazi na kugeuza  bunge  hilo ni sehemu ya kuonyeshana ujuzi wa kutukanana ni  vema wakirudi katika mwelekeo mzuri ama kurudi majumbani kwao  ili viongozi wa dini mashekhe na maaskofu wakaifanya kazi hiyo ya kuunda katiba  bila kutukanana .

"Nimejizuia  sana kwa kipindi  hiki  cha bunge la katiba  nisiseme  chochote ila  kutokana na mambo jinsi yanavyokwenda uvumilifu  umenishinda nimelazimika  kusema na ninachosema nimekiandika ili  wale  wapotoshaji washindwe  kupotosha ninachosema....wayahudi  walikataa kuongozwa na Samweli kwa  sababu walisema  watoto wa Samweli wanatabia  mbaya ...walikataa kuongozwa na Mungu kwa madai  kuwa na  wao  wanataka mfalme wetu  uli tukienda  kupigana na watu  ili  tuwe kama mataifa  mengine  ila Mungu hakutaka wao  kuwa kama mataifa  mengine  ila  wao  wanataka  kuwa kama mataifa  mengine ....Samweli akaenda mbele ya Mungu akilia ....ila  Mungu akasema hawajakukataa wewe  wamenikataa mimi ...enyi  watanzania tukikataa lulu  tuliyopewa na Mungu ya kuwa nchi ya amani  tutakuwa hakuwakatai viongozi  wetu  tutakuwa tunamkataa Mungu"

Aliwataka  watanzania  kuyatazama mataifa  jirani kama Kenya ambao  walijipenda  wao na kushindwa  kuwapenda  majirani  sasa  Wasomari  wameingia wanawasumbua  ila tazameni pia Malawi ambao walimtaka rais  wao awe Joys Banda ila alipoingia tu Ikulu alitangaza ndoa za jinsia moja pamoja na nchi ya Kongo ambayo imesaidiwa na Tanzania kurudi katika amani ikiwemo nchi ya Burundi  ambayo Rais  wake amekuwa akishinda katika maombi kwenye kanisa lake na kuacha kuongoza nchi.

"Tunapaswa  kujiuliza amani  hii iweje  leo  ichezewe na  watu  wachache  wenye uchu wa madaraka na hata  kususa  bunge la katiba ...hatujifunzi  kutoka nchi  za majirani  zetu kama Uganda ,Rwanda kuna  vyama 10  vya upinzani na kuna  vikundi 10  vinavyotaka  kumpindua Rais huku Uganda kuna mtu anaitwa Kony yeye  siku  zote  kumshumbua Rais ....ninyi ni nani  Tanzania bara  na visiwani mkaa kwenye amani kiasi hiki na mnakataa umoja na kuanza kuwasikiliza  wanaopandikiza mbegu ya kuvuruga amani ya kutaka serikali tatu ....watanzania tunataka  kuikataa lulu tuliyopewa na Mungu lulu ya amani"

Dr Mdegela  alisema kuwa hadi  sasa mwenendo  wa  bunge la katiba unatia aibu kubwa kwa  Taifa na hata nje ya taifa   hili na kuwataka  wajumbe hao  kuwa wasikivu na kama  walisema  wanakwenda kuandaa katiba ya  wananchi iweje kabla ya  kuanza kwa  bunge  hilo walianza kwa kulilia posho kuongezwa hali  wakijua  walimu hawajalipwa malipo yao pamoja na  wafanyakazi  hawajaongezwa mishahara yao.

"Natamka  wazi  kuwa  mimi Dr Mgedela sina  imani hata  kidogo na  wajumbe wa  bunge la katiba .....kama  wanavyoonekana na  walivyo wana hadhi ya kutoridhika  watatuletea  katiba mbovu kwa  sasa na  wao  ni wabovu ..
"Natamka rasmi  kuwa  tume iliyoandaa rasmi ya katiba haukuandaa msaafu  wala Biblia  ili andaa kitu ambacho  mbacho  kinaweza  kuhojika na kukataliwa  ama kukubalika  wao  si Miungu ni  wanadamu kama  sisi madai kuwa wanavyeo vingi  serikalini hata mfagiaji anavyo ....sasa naiomba serikali hao  waliojitoa bungeni wanataka kuja kwa wananchi tunasema hatuwataki ....
"Hivi kama mtu ameshindwa  kujenga  hoja bungeni watakuja kutueleza nini nawaombeni usalama wa Taifa fanyini kazi ya kulinda amani yetu ....kama hawataki kurudi bungeni basi waende majumbani kwao"

Askofu Dr Mdegela  alisema kanuni za bunge  wametunga  wao na iweje leo  wanakimbia kanuni waliyoitunga hivyo kama  wanaona kanuni  ni mbaya  basi  watuombe Watanzania wenye akili tuwasaidie hata   yeye anaweza kwani  wajumbe hao ni walafi  wasiopenda amani ya nchi hii.

Katika  hatua  nyingine  askofu  huyo  alisema kwa  sasa  kinachoendelea na kuwa  kila kanda  itataka  serikali  yao iwapo  hoja  ya  serikali tatu  ikapitishwa.

VIDEO YA KAULI YA ASKOFU WA KKKT IRINGA DR MDEGELA KUHUSU BUNGE MAALUM LA KATIBA

Kikwete cautions EAC against rushed decisions

UJUMBE WA KICHUNGAJI WA PASAKA 2014 KWA WAAMINI NA WATU WOTE WENYE MAPENZI MEMA

BAIKOKO, FFU UGHAIBUNI NA RAS JHIKO MAN KUMWAGA LAZI UJERUMANI

0
0
Wasanii kutoka Tanzania wanatarajiwa kupamba maonesho makubwa mbalimbali nchini Ujerumani katika msimu wa joto. Waliopata nafasi hiyo ni pamoja na kikundi maarufu cha ngoma ya Baikoko kutoka mkoani Tanga (picha ya juu). 
 Wengine ni mwanamuziki nguli wa reggae, Jhikoman & Afrikabisa band kutoka Bagamoyo, Pwani (picha ya chini) ambaye amealikwa rasmi na Afrikative Organization kushiriki onyesho kubwa la International Africa Festival Tubingen 2014 yanayoanza 17 mpaka 20 julai 2014 huko Tubingen, Ujerumani. 
 Wazee wa kazi Ngoma Africa band a.k.a.  FFU Ughaibuni a.k.a. The  Anunnaki Aliens  (picha ya kati) kama kawaida yao watalishambulia jukwaa kuhakikisha washabiki wao hawapati usingizi.
Viewing all 109591 articles
Browse latest View live




Latest Images