Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 424 | 425 | (Page 426) | 427 | 428 | .... | 3278 | newer

  0 0  0 0


  0 0

  Licha ya baadhi ya wabunge wa Upinzani wa Bunge Maalum la Katiba kuamua kususia kuendelea kushiriki katika mjadala wa Rasimu ya Katiba iliyowasilishwa ndani ya Bunge hilo Kundi kubwa la Wajumbe hao waliobaki wataendelea kuchapa kazi waliyotumwa na Wananchi bila ya kujali uwamuzi uliochukuliwa na wale walioamua kutoka nje ya mjadala huo. 
  Kauli hiyo imetolewa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar ambae pia ni Mbunge wa Bunge hilo Maalum la Katiba Balozi Seif Ali Iddi mara baada ya kutembelea baadhi ya Mabanda ya Maonyesho katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Mjini Dar es salaam ikiwa ni shamra shamra za Maadhimisho ya kutimia Miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar wa Mwaka 1964. 
  Balozi Seif alisema Kundi hilo lililobakia ndani ya Bunge hilo halitatetereka kamwe na litatekeleza wajibu wake na lina uwezo kamili wa kukamilisha kazi hiyo kwa mujibu wa Sheria na Kanuni za Bunge hilo Maalum la Katiba na baadaye kuipeleka kwa Wananchi kwa ajili ya kupigiwa kura ya maoni. 
  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar ameelezea masikitiko yake na kuvunjwa moyo kutokana na kitendo hicho kilichoibuka ndani ya Bunge hilo ambacho hakionyeshi uungwana wala uvumilivu na kinaonyesha muelekeo wa kuwanyima haki ya Kidemokrasia Watanzania. 
  “ Kundi lililobakia ndani ya Bunge Maalum la Katiba ni kubwa na lina uwezo wa kutekeleza kazi hiyo muhimu katika Historia ya Tanzania kwa mujibu wa Sheria na Kanuni zetu tulizojipangia kwa pamoja sisi na wale walioamua kuukimbia mjadala huo “. Alifafanua Balozi Seif. 
  Akizungumzia suala la Muungano wa Tanzania kutimia miaka 50 tokea kuasisiwa kwake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alisema Muungano huo umeleta faida kubwa kiasi kwamba Watanzania walio wengi wamenufaika nao Kiuchumi na Ustawi wa Jamii. 
  Alisema Muungano wa Tanganyika na Zanzibar umeongeza kuleta upendo na mshikamano miongoni mwa wananchi wa pande zote mbili na kuupa fursa kubwa zaidi Zanzibar katika kupanua wigo wa Kibiashara sambamba na umiliki wa maeneo makubwa ya ardhi kwa Wazanzibari walio wengi ambao kwa muda mrefu hivi sasa wanaendelea kuishi upande wa Tanzania Bara. 
  Balozi Seif alitanabahisha kwamba kwa vile Muungano wa Wananchi wa Zanzibar na Tanzania Bara ni wa asili ni vyema kwa watu wa pande hizo mbili wakaendelea kuuenzi na kuuimarisha kwa faida ya vizazi vya sasa na vile vijavyo. 
  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi aliupongeza Uongozi ulioandaa na kusimamia Maonyeso hayo ya kutimia Miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kwa juhudi kubwa walizochukuwa na hatimae kufanikisha vizuri Maonyesho hayo. 
  Alisema Maonyesho hayo yamependeza kiasi kwamba wananchi wengi wamevutiwa nayo na kushawishika kutembelea kwa lengo la kujifunza na kuona bidhaa na harakati za kiutendaji za Taasisi na Mashirika ya Sekta za Muungano yaliyoamua kushiriki kwenye Maonyesho hayo. 
  “ Maonyesho ni mazuri na yamependeza. Ukweli nimefarajika na maandalizi ya Maonyesho hayo yenye kuonyesha maendeleo makubwa yaliyopatikana ndani ya kipindi cha miaka 50 katika Taasisi na Mashirika ya Sekta mbali mbali za Muungano zinazofanya kazi Zanzibar na Tanzania Bara“. Alifafanua Balozi Seif. Balozi Seif aliwaomba Wananchi mbali mbali Nchini kuangalia Historia ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kupitia Maonyesho hayo ili wapate fursa kamili ya kujifunza kwa undani Historia hiyo. 
  Alisema hatua hiyo muhimu itasaidia kuwapa nafasi nzuri ya kuelewa ukweli na kujiepusha na watu na makundi yenye tabia ya kuendelea kuupotosha umma juu ya historia halisi ya Muungano huo unaoendelea kuwa kielelezo kikubwa katika Nyanja za Kimataifa. 
  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akifuatana na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa { TAMISEMI } Nd. Zubeir Sarataba alipata wasaa wa kutembelea baadhi ya Mabanda yaliyoshiriki kwenye Maonyesho hayo. Miongoni mwa Mabanda hayo ni pamoja na lile la Nguvu za Atomiki,Ofisi ya Makamu wa Rais wa Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kushirikiana na Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar,Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania pamoja na Mambo ya Nje na Ushirikiano na Kimataifa. Mengine ni Banda la Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mamlaka ya Kodi ya Ongezeko la thamani { TRA } pamoja na Banda la Mahakama ya Tanzania ambapo alibahatika kujionea hatua kubwa ya maendeleo iliyofikiwa na Taasisi hizo kupitia maonyesho hayo. Jumla ya Mabanda 50 ya Mashirika na Taasisi mbali mbali za Sekta za Muungano zinazofanya kazi pande zote mbili za Muungano Bara na Zanzibar zimeshikiri kwenye Maonyesho hayo ya kutimia Miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar wa Mwaka 1964.
   Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiangalia Vibuyu na Chungu halisi vilivyotumiwa na Baba wa Taifa Marehemu Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kuchanganya Udongo kuashiria Kuunganisha Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Vitu hivyo vimewekwa katika Banda la Ofisi ya Makamu wa Rais wa Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye Maonyesho ya Kuadhimisha Miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar yanayoendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Mjini Dar es salaam.
   Balozi Seif akipezuri na kuangalia baadhi ya Machapisho yaliyoandikwa katika Gazeti Rasmi la Serikali kuhusu harakati za Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kati kati ya  miaka ya Sitini.
  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akikagua Siwa maarufu { Rungu } linalotumika katika Shughuli za Kuendesha Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania lililowekwa kwenye Banda la Maonyesho ya Miaka 50 ya Muungano wa Tanzania Mnazi Mmoja Jijini Dar es salaam.
   Ofisa wa Huduma wa Kitengo cha Kodi ya Thamani { VAT } kutoka Wizara  ya Fedha za Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ndugu Saleh Haji Pandu akimueleza Balozi Seif mfumo mzima wa Utendaji kazi wa Kitengo hicho Bara na Zanzibar kwenye Maonyesho ya Miaka 50 ya Muungano wa Tanzania. Picha na Hassan Issa wa  OMPR – ZNZ.

  0 0

   Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Mhe. Alhaj Ali Hassan Mwinyi akipokea maelezo kutoka kwa Afisa wa Bunge Bwana Patson Sobha, wakati alipowasili kwenye Banda la Bunge la maonesho ya maadhisho ya miaka 50 ya Muungano wa Tanzania yanayoendelea katika Viwanja Vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam. Maonesho hayo yatakayofikia kilele siku ya Jumamosi Aprili 19, ikiwa ni maandalizi ya siku kuu ya Muungano ambayo huherekewa Aprili 26 kila mwaka.
  Rais Mstaafu Mzee Ali Hassan Mwinyi akikabidhiwa  zawadi ya vitabu na nyaraka mbalimbali za Bunge na Bi. Devotha George alipotembelea banda la Ofisi ya Bunge kwenye Maonesho ya maadhimisho ya miaka 50 ya Muungano katika viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es Salaam.

  0 0
 • 04/18/14--05:41: Article 12


 • 0 0


  Taarifa yetu tuliyotuma hivi punde ilionesha kiingilio cha chini mechi ya Yanga na Simba ni sh. 5,000.

   Usahihi ni kuwa kiingilio hicho ni sh. 7,000 kama kinavyooneshwa kwenye tiketi.

  0 0

   Makundi mawili maarufu ya muziki wa kizazi kipya nchini TMK family na Tip Top Connections wanatarajiwa kupamba mechi za ligi kuu Vodacom ya Simba na Yanga na ile ya Azam FC dhidi ya JKT Ruvu inayochezwa kesho Jumamosi jijini dar es salaam.

  Uwepo wa burudani hizo ni sehemu ya mkakati wa mdhamini mkuu wa ligi hiyo kampuni ya huduma za mawasiliano ya simu za mkononi ya Vodacom ya kuhitimisha msimu wa ligi wa 2013/2014 kwa kishindo na burudani ya aina yake.

  Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Salum Mwalim amesema kundi la Tip Top Connections likinogeshwa na msanii mahiri Ma D litaipamba mechi ya watani wa jadi ya Simba na Yanga kwenye uwanja wa taifa huku TMK wanaume family wakiwasindikiza washabiki wa mabingwa Azam FC kwenye uwanja wa Azam Complex

   "Tumeamua kuifunga ligi yetu kwa mtindo wa aina yake kwa kutoa burudani kwa mabingwa wapya Azam FC pamoja na kuipamba mechi ya Yanga ambao walikuwa mabingwa watetezi na washindi wa pili wa msimu huu tunaoumalizia"Alisema Mwalima katika taarifa yake kwa vyombo vya habari

   Mwalim amesema mechi zote mbili zinatarajiwa kuvutia hisia za maelfu ya wapenda soka nchini kutokana na kila mechi kuwa na umuhimu wake katika historia na rekodi za soka nchini na hivyo ni wazi maelfu ya washabiki watafurika kwenye uwanja wa Taifa na Azam Complex huku wengine wakifuatilai mechi hizo kupitia matangazo ya moja kwa moja ya redio na Luninga

   "Mechi zote mbili ni muhimu sana huku Azam akitaka kuweka rekodi ya kumaliza msimu bila ya kupoteza mchezo huku timu zenye utani wa jadi za Simba na Yanga zikishuka dimbani huku kila mmoja akitaka kulinda heshima mbele ya mwezake"Aliongeza Mwalim.

   Mwalim amesema maandalizi yote kwa upande wao wameyakamilisha na kwamba kilichobakia sasa ni kwa washabiki kufika uwanjani ili kuona ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara inavyohitimishwa kwa mbwembwe za aina yake.

  Amesema katika mechi hizo, Vodacom itakabidhi kombe kwa mabingwa wapya Azam FC pamoja na medali kwa timu ya Yanga na Mbeya City zinazomaliza nafasi ya pili na ya tatu katika msimamo wa mwisho wa ligi hiyo.

   "Wakati wote tunaangalia ni vipi tunaweza kufanya mambo yatakayoinogesha ligi hii kuu ya Vodacom, na hivyo ni imani yetu kwamba makundi haya mawili ya burudani ni sahihi na yanahadhi inyoendana na ligi na michezo husika,"Aliongeza Mwalim

   Burudani katika viwanja vyote viwili inatarajiwa kuanza mapema majira ya saa saba ili kutoa nafasi nzuri kwa washabiki kupata burudani yakutosha kabla ya kuanza kwa mechi majira ya saa kumi alasiri

  0 0

  Rais mstaafu wa awamu ya pili Ali Hassani Mwinyi akimsikiliza kwa makini Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Charles Chacha wakati alipotembelea katika banda la Mamlaka hiyo katika Maadhimisho ya Miaka 50 ya Muungano yanayoendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
  Rais Msaafu wa awamu ya pili Ali Hassani Mwinyi akikabidhiwa nyaraka na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Charles Chach,zenye ujumbe wa shughuli zinazofanywa na Mamlaka hiyo wakati alipotembelea katika banda la Mamlaka hiyo kujionea shughuli zinazofanywa na Mamlaka katika Maadhimisho ya Miaka 50 ya Muungano yanayoendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.

  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali,katika kikao cha utekelezaji Mpango kazi kwa kipindi cha Julai hadi Machi 2013/2014,katika ukumbi wa mikutano Ikulu Mjini Zanzibar jana jioni.
  Baadhi ya Viongozi wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali wakiwa katika kikao cha utekelezaji wa mpamgo wa kazi kwa kipindi cha robo mwaka kutoka Julai -Machi 2013/2014,katika ukumbi wa mikutano Ikulu Mjini Zanzibar jana jioni, chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]

  0 0

  Kamanda wa Polisi mkoa waTabora Kamishna Msaidizi wa Polisi Suzan Kaganda leo tarehe 18/04/2014 amefanya Mkutano na waandishi wa habari, na kuzungumzia mambo mbalimbali hasa mafanikio yaliyopatikana katika Operesheni zinazoendelea mkoani Tabora ambapo wahalifu wa  makosa mbalimbali yamekamatwa na watuhumiwa kufikishwa mahakamani. 
   
   Maganda ya risasi ambayo yalitelekezwa yakiwa katika mfuko wa manira.

   RPC tabora akiwaonesha waandishi wa habari katika Press Conferences leo bunduki aina ya gobore ambayo alikamatwa nayo mtuhumiwa
   RPC Tabora Suzan Kaganda - ACP akiwafafanulia waandishi wa habari juu ya pikipiki zilizokamatwa na Polisi baada ya Kuporwa na wahalifu
   RPC Tabora Suzan Kaganda - ACP akiwafafanulia waandishi wa habari juu ya pikipiki zilizokamatwa na Polisi baada ya Kuporwa na wahalifu
  RPC Tabora Suzan Kaganda - ACP akiwaonesha waandishi wa habari maganda ya risasi 2256 aina ya SMG yaliyokuwa yametelekezwa na wahalifu. Picha na habari na DC Fakih Abdul
  wa ofisi ya Kamanda mkoa wa Tabora.

  0 0

  Muumini wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT),Usharika wa Azania Front, Moses Kombe, (katikati) na wenzake wakiigiza igizo la kumbukumbu ya Kuwambwa Yesu Kristo miaka 2000 iliyopita wakati wa ibada ya Ijumaa Kuu iliyofanyika katika kanisa hilo Dar es Salaam leo.
  Waziri Mkuu Mstaafu,Mh. Edward Lowasa akiwa katika ibada ya Ijumaa Kuu katika Kanisa la KKKT la Azania Front Dar es Salaam.
  Waumini wa Kanisa la Kiinjili Tanzania KKT, la Azania Front la Dar es Salaam wakiwa katika Ibada ya Ijumaa Kuu.
  Waumini wa Kanisa la Mtakatifu Joseph wakiwa kwenye ibada ya Ijumaa Kuu iliyofanyika leo kanisani hapo.
  Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Kanisa Katoriki, Mwadhama Polycap Kadinali Pengo akiubusu Msaraba wakati wa ibada ya Ijumaa Kuu iliyofanyika katika Kanisa la Mtakatifu Joseph jijini Dar es Salaam leo.
  Waumuni wa Kanisa la Mtakatif Joseph Jimbo Kuu la Dar es Salaam wakiwa wanaubusu Msaraba wakati wa ibada ya Ijumaa Kuu iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo.
  Mtoto, Vanes Mpupua akiubusu Msaraba wakati wa ibada ya Ijumaa Kuu katika Kanisa la Mtakatif Josef Dar es Salaam.
  Mmoja wa Watoto waliofika katika Kanisa la Mtakatif Josef akiubusu Msaraba wakati wa Ibada ya Ijumaa Kuu iliofanyika Dar es Salaam. PICHA ZOTE NA PHILEMON SOLOMON

  0 0

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na baadhi ya maafisa na viongozi wakati alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mjini Zanzibar leo jioni kwa ajili ya kufungua rasmi Kongamano la Muungano, linaloanza kesho katika Ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Beach Resort. Wa pili (kulia) ni mkewe Mama Zakia Bilal. Picha na OMR


  0 0

  Key: 1. RANGI YA NJANO - Njia ya Uelekeo Mmoja {One Way}.
   2. RANGI YA BLUE MPAUKO - Njia ya Mielekeo Miwili {Two Way} 
   3. RANGI YA KIJANI - Mitaa ya Kutembea kwa Miguu Magari marufuku {Walking Streets} 
   4. RANGI NYEKUNDU - Barabara za kupita Daladala
   5. RANGI YA BLUU ILIYOIVA - Barabara za DART
   6. DUARA ZA NJANO - Mzunguuko {Roundabout} 
   7. MSALABA WA KIJANI - Makutano yenye Taa za kuongozea Magari {Singnalized Intersection}

  1. Kipande cha Mtaa wa Samora kuanzia Mnara wa Askari (Askari Monument) hadi Clock Tower Magari  kutakuwa na mabadiliko ambayo magari yatakuwa yanaelekea Clock Tower badala ya Askari Monument. 

  2. Barabara ya Sokoine kuanzia Station hadi Makutano ya Mtaa wa Maktaba Posta Ya Zamani Magari yatakuwa yanaelekea Uelekeo mmoja wa Station Posta ya Zamani tofauti na ilivyo sasa Posta ya Zamani kwenda Station. 

  3. Barabara ya Kivukoni  Kuanzia Posta ya Zamani hadi Ferry itakuwa barabara ya mielekeo miwili (Two Ways).

  4. Barabara ya Samora kuanzia Mnara wa Askari hadi Ocean Road Hospitali itakuwa ni barabara ya mielekeo miwili.

  5. Daladala Zote zitakazotokea barabara za  Makataba zitakunja kulia pembeni ya Jengo la NBC na hadi Makutano ya Mkwepu na kukunja kushito kuingia Sokoine pale Posta ya Zamani na baadaye kukunja kushoto kuingia Makataba na kurudi Posta Mpya .

  Kwa Maelezo zaidi Wasiliana na Ofisi za DART
  UBUNGO PLAZA GHOROFA YA KWANZA.
  AU.
  OFISI YA MHANDISI WA MANISPAA YA ILALA
  MABALA NA SHOPRITE SUPEEMARKET JIRANK NA KAMATA

  Mtaarifu mwingine juu ya mabadiliko haya kuondoa usumbufu ifikapo siku ya Jumatatu 28/04/2014. PASAKA NJEMA

  0 0


  0 0

   Ndugu zanguni, 
   Tunapenda kuwapa habari njema watu wote kuwa kuanzia tarehe 01/05/2014 Kampuni yetu inayomilikiwa na Watanzania waishio UK, inahamishia ofisi zake ndani ya bandari kubwa kuliko zote za kusafirisha magari UK , PORT OF TILBURY. 
   Sisi tutakuwa weusi wa kwanza kabisa kupewa ofisi ndani ya hii bandari na hivyo majina yetu kuingia kwenye historia. Na serikali imetukubali baada ya kuona jinsi tulivyoweza kujibeba kutoka kwenye kiosk mpaka tulipo.
   Mkumbuke Serengeti ilianzishwa kwa mtaji wa £1,800 tu. Tumepewa mkataba wa miaka 10 na tunaweza ku-renew baada ya hapo kama bado tutakuwa tunataka kuendelea na biashara ndani ya bandari Tumechukua Yard yenye ukubwa wa ekari mbili na ofisi yenye ukubwa wa 2,500sq ft. 
   Hii itatusaidia kuboresha huduma zetu kwa sababu tuna mpango wa kukodi meli ya saizi ya kati ili magari yetu yote na makontena tuwe tunasafirisha wenyewe na pia kusafirisha magari na makontena ya makampuni mengine pia. 
   Pia usalama wa mali za wateja ni maximum kwa sababu kuna zaidi ya camera 5,000, kituo cha polisi ni hatua mia tatu tu kutoka kwetu, police patrol ni 27/7 Yard /ofisi zetu zitakuwa OPPOSITE BERTH 31, BESIDE HYUNDAI TERMINAL 
   Tukiishakamilisha mkataba wa kukodi meli tutatoa punguzo kubwa kwa usafirishaji wa magari kwa asilimia 40% ili kurahisisha watu kuweza kuagiza magari yao toka UK kwa bei nafuu. Pia tutakuwa tunatoa free storage kwa magari na free loading. 
   Kama kuna mtu ana kitu au mzigo ndani ya ofisi zetu za sasa tunaomba aje achukue sababu hatutahama na mzigo wa mtu 
   Wote mnakaribishwa. 
   CHRIS LUKOSI 
   Managing Director SERENGETI FREIGHT


  WE ARE OPEN ON SATURDAY 10:00-18:00HRS
  WE PROMISED, WE DID IT AND WE ARE MAKING IT EVEN BETTER!
  Tupigie kwa namba hizo hapo chini au  tutumie email tafadhali

  CHRIS LUKOSI +44 (0) 790 38 28 119 OR  +44 (0) 7404 27 96 33
  SIMON  LOUIS +44 (0) 79 506 89 243
  HASSAN +44 (0)7473043042RH

  0 0
 • 04/18/14--13:30: Article 1

 • 0 0
 • 04/19/14--13:30: Article 0


 • 0 0  0 0


   Viongozi wa Jumuiya ya Watanzania Columbus, Ohio wakimpokea Mhe. Balozi Liberata Mulamula (wapili toka kulia) wengine katika picha toka kushoto ni Mjumbe Eliud Mashambo, Mume wa Balozi Bwn. George Mulamula, Deo Mwalujwa, Katibu wa Jumuiya ya Watanzania Columbus, Ohio Bi. Happiness Salukele na Joe Ngwilizi ambaye ni Mjumbe.
   Mhe. Balozi Liberata Mulamula akipokea shada la maua kutoka kwa mtoto Luluwa Rashid mara tu baada ya kuwasili Hotel ya Hilton alikofikia.
   Picha ya pamoja kutoka kushoto ni mweka hazina wa Jumuiya Bi. Vera Teri, Mhe. Liberata Mulamula, Mtt. Luluwa Rashid, Mjumbe Bwn. Joe Ngwilizi na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania Columbus, Ohio Bwn. Jimmy James. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0
 • 04/18/14--20:00: ngoma azipendazo ankal
 • Solomon Mukubwa - Mfalme Wa Amani

older | 1 | .... | 424 | 425 | (Page 426) | 427 | 428 | .... | 3278 | newer