Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110175 articles
Browse latest View live

Article 11


TAARIFA KUTOKA TFF LEO Aprili 17, 2014

$
0
0
 WACHEZAJI MABORESHO STARS WATAJWA
Kocha Msaidizi wa Taifa Stars, Salum Mayanga ametangaza majina ya wachezaji 16 waliochaguliwa katika maboresho ya timu ya Taifa Taifa Stars kwenye hoteli ya Hill View jijini Mbeya.

Wachezaji hao ni kipa Benedicto Tinoko Simwanda (Temeke), mabeki wa kati; Emma Namwondo Simwanda (Temeke) na Joram Nason Mgeveje (Iringa). Walinzi wa pembeni ni Omari Ally Kindamba (Temeke), Edward Peter Mayunga (Kaskazini Pemba) na Shiraz Abdallah Sozigwa (Ilala).

Viungo ni Yusuf Suleiman Mlipili (Temeke), Said Juma Ally (Mjini Magharibi), Abubakar Ally Mohamed (Kusini Unguja), Hashim Ramadhan Magona (Shinyanga), Omari Athumani Nyenje (Mtwara) na Chunga Said Zito (Manyara).

Washambuliaji ni Mohammed Seif Saidi (Kusini Pemba), Ayoub Kasim Lipati (Ilala), Abdurahman Othman Ally (Mjini Magharibi), Paul Michael Bundara (Ilala). Wachezaji wa U 20 ni Mbwana Mshindo Musa (Tanga) na Bayaga Atanas Fabian (Mbeya).

Alisema mpango huu wa kuboresha timu ya Taifa ambayo inadhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager ni endelevu na kusisitiza kuwa hata wale 18 walioachwa watafuatiliwa na TFF na kuitwa panapokuwa na mahitaji.

“Hawa wote wapo kwenye database ya TFF na hawataachwa tu hivi hivi wapotee,” alisema kocha Mayanga.

Wachezaji ha0 waliingia kambini mjini Tukuyu, Machi 21 mwaka huu na wamefanya mazoezi kwa pamoja kwa karibu wiki nne sasa kabla ya kuchujwa.

Wachezaji 16 waliochaguliwa wanatarajiwa kuondoka Tukuyu kesho (Aprili 18 mwaka huu) na kwenda kwenye kambi ya Taifa Stars katika Hoteli ya Kunduchi ambapo wataungana na wachezaji wa Taifa Stars wa siku zote.

Baadaye watachujwa tena ili ipatikane timu moja ya Taifa iliyoboreshwa.
Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia ya Kilimanjro Premium Lager inaunga mkono utaratibu huu wa maboresho ya Taifa na imewekeza zaidi ya dola milioni 2 kwa mwaka kudhamini Taifa Stars. Huu ndio udhamini mkubwa zaidi ambao Stars imewahi kupata tangu kuanzishwa kwa TFF.

LIGI YA MABINGWA WA MIKOA KUANZA MEI 10
Michuano ya Ligi ya Mabingwa wa Mikoa (RCL) itakayochezwa kwa ligi ya mkondo mmoja katika vituo vitatu vya timu tisa kila kimoja inatarajia kuanza Mei 10 mwaka huu.

Timu ya kwanza kutoka katika kila kituo ndiyo itakayopanda daraja kucheza Ligi Daraja la Kwanza (FDL) msimu wa 2014/2015. Kwa vile ligi hii haina mdhamini, hivyo timu zitajigharamia kwa kila kitu.

Vituo vitakavyotumika kwa ajili ya RCL, kanuni pamoja na ratiba vitatangazwa kabla ya kuanza kwa ligi hiyo. Pia kituo kitakachoteuliwa kwa ajili ya ligi hiyo, timu yake haitapangwa katika kituo husika ikiwa ni moja ya njia ya kuhakikisha kanuni ya mchezo wa kiungwana (fair play) inazingatiwa.

BONIFACE WAMBURA
OFISA HABARI NA MAWASILIANO

SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

KAIMU MKURUGENZI TANESCO KIZIMBANI KWA MATUMIZI MABAYA YA OFISI

$
0
0
Na Miriam Mosses 
Aliyekuwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Robert Semtutu na wenzake wanne wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, akikabiliwa na mashitaka mawili ikiwemo kuisababishia serikali hasara ya zaidi ya Sh.milioni 200. 
 Washtakiwa wengine ni, aliyekuwa Afisa Ugavi wa Tanesco, Hanin Mahambo, Mkurugenzi wa fedha Lusekeo Kasanga,Mwanasheria Godson Ezekiel pamoja na Mkandarasi Martin Abraham. 
 Mwendesha Mashtaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Isidori Kyando alidai kuwa washtakiwa walifanya makosa hayo katika tarehe tofauti mwaka 2011. 
 Kyando alidai kuwa shitaka la kwanza ni la matumizi mabaya ya Madaraka, Desemba 2011,katika ofisi za Tanesco Ubungo, jijini Dar es Salaam washtakiwa kwa pamoja walitumia madaraka yao vibaya kwa kufanikisha malipo kwa msambazaji M/S Young Dong Electronic Co Ltd bila kuhakikisha kwamba Mkandarasi anafika katika kituo cha mwisho. Ilidaiwa kuwa washtakiwa walifanya kosa hilo kinyume na kifungu namba 35 (21) cha sheria ya manunuzi ya umma ya mwaka 2004 na kusababisha Martin Abraham kupata faida kutokana na ukandarasi huo. Katika shitaka la pili ni la kuisababishia serikali hasara linalowakabili mshtakiwa Semtutu, Mahombo,Kasanga na Ezekiel ambao wanadaiwa kwamba kati ya Januari hadi Desemba 2011 katika ofisi za Tanesco Ubungo waliisababishia serikali hasara ya Sh.275,040,000 kutokana na matumizi yao mabaya ya madaraka. 
 Washtakiwa wote walikana kutenda kosa hilo ambapo upande wa mashitaka ulidai kwamba upelelezi wa kesi hiyo umekamilika na kuomba tarehe nyingine ya kuwasomea washitakiwa hao maelezo ya awali. 
Hakimu aliwaeleza washitakiwa hao kwamba dhamana yao iko wazi ikiwa watajidhamini wenyewe kwa kuwasilisha mahakamani hapo fedha taslim Sh.milioni 27.5 au kuwasilisha hati ya mali isiyohamishika. 
Pia wawe na wadhamini wawili kila mmoja watakaoweka ahadi ya dhamana ya kiasi icho cha fedha.
Hata hivyo wadhamini hao hawakutimiza masharti na wamerudishwa rumande hadi Aprili 30, mwaka huu.

kesi ya kikatiba dhidi ya Waziri Mkuu yapigwa kalenda

$
0
0
Na Miriam Mosses 
MAHAKAMA Kuu Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam, imepiga kalenda kutoa uamuzi wa kesi ya kikatiba dhidi ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda hadi Mei 19 mwaka huu, itakapotoa uamuzi wa pingamizi la awali lililowasilishwa na upande wa Jamhuri. 
 Uamuzi huo ulipangwa kutolewa jana lakini iliahirishwa mbele ya Msajiri Benedicto Mwingwa baada ya jopo linalosikiliza kesi hiyo kuwa bado halijamaliza kuandika uamuzi huo. 
 Kesi hiyo inasikilizwa na jopo la majaji waatu likiongozwa na mwenyekiti wao Jaji Kiongozi, Fakihi Jundu. 
Kesi hiyo Namba 24 ya 2013 ilifunguliwa na Kituo Kisheria na Haki za Binadamu (LHRC) kwa kushirikiana na Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS). 
LHRC na TLS,wanadai Pinda alivunja Katiba kutokana na kauli aliyowahi kuitoa bungeni wakidai kuwa ni amri kwa vyombo vya utekelezaji wa Sheria kuwapiga wananchi, wakati wa vurugu. Hivyo wanaiomba mahakama, pamoja na mambo mengine, itamke kuwa kauli hiyo ni kinyume cha Katiba na imwamuru Pinda aifute hadharani.

taswira toka bunge maalum la katiba mjini dodoma leo

$
0
0
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu na mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, William Lukuvi akichangia Bungeni Mjini  Dodoma  leo
 Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, askofu Mkuu Mstaafu wa Kanisa la Anglican Tanzania, Donald Mtetemela akichangia Bungeni mjini Dodoma leo
  Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe Kuga Mziray akichangia Bungeni Mjini Dodoma Aprili 17, 2014.
Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Mwenyekiti wa Bunge hilo, Samueli Sitta (wapili kushoto wakizungumza na Beatrice Shellukindo (wapili kulia) na Riziki Lulida (kulia) kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma  leo Aprili 17, 2014. (Picha na Ofisi ya  Waziri Mkuu)

Umoja wa Watanzania Ethiopia wapata uongozi mpya

$
0
0
 Mhe. Naimi Aziz, Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia akiwa na viongozi wapya wa Jumuiya ya Watanzania Ethiopia (UDUGU). Wa pili kushoto ni Dr. Naftali Kilenga ambaye amechaguliwa kuwa Mwenyekiti, na wa kwanza kulia ni Dr. Florence Temu, ambaye amechaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti. Wa kwanza kushoto ni Bw. E. Lubuva ambaye amechaguliwa tena kuendelea kuwa Katibu wa UDUGU.
Mhe. Balozi Naimi Aziz akiwa na Mwenyekiti Mpya Dr. Naftali Kilenga kushoto, na kulia kwake ni Bibi Josephine Marialle Ulimwengu, ambaye alikuwa Kaimu na Makumu Mwenyekiti  katika uongozi uliopita.

KIKAO CHA 25 CHA BODI YA TAIFA YA PAROLE CHAMALIZIKA LEO JIJINI ARUSHA

$
0
0
 Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Nchini, John Casmir Minja(kulia) akichangia mjadala wakati wa kupitia mapendekezo ya Wafungwa wanaopendekezwa kuachiliwa na mpango wa Parole kabla ya kufungwa rasmi Kikao cha 25 cha Bodi hiyo leo Aprili 17, 2014 katika Ukumbi wa Hoteli ya Charity, Jijini Arusha(kushoto) ni Mwenyekiti wa Bodi hiyo Mhe. Jaji Mstaafu Eusebia Munuo akifuatilia mjadala huo.
 Wajumbe wa Bodi ya Taifa ya Parole wakipitia makabrasha yenye mapendekezo ya Wafungwa watakaoachiliwa na mpango wa Parole kabla ya kufungwa rasmi kwa Kikao hicho lei Aprili 17, 2014 katika Ukumbi wa Hoteli ya Charity, Jijini Arusha.
 Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja(kushoto) akiteta jambo na Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Parole, Mhe. Jaji Mstaafu Eusebia Munuo(katikati) mapema leo kabla ya kufungwa rasmi kwa Kikao kilichofanyika kwa siku mbili katika Ukumbi wa Hoteli ya Charity, Jijini Arusha(kulia) ni Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma Malewa.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Parole, Mhe. Jaji Mstaafu Eusebia Munuo(katikati aliyeketi) akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Bodi hiyo mara baada ya kufungwa rasmi kwa Kikao cha 25 cha Bodi hiyo kilichofanyika kwa siku mbili katika Ukumbi wa Hoteli ya Charity iliyopo Jijini Arusha(kulia aliyeketi) ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja ambaye pia ni Katibu wa Bodi ya Taifa ya Parole(kushoto aliyeketi) ni Mjumbe wa Bodi, Naibu Kamishna wa Magereza Mstaafu, John Nyoka.
Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Parole, Mhe. Jaji Mstaafu Eusebia Munuo(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Sekretarieti ya Bodi ya Taifa ya Parole(waliosimama mstari wa nyuma) mara baada ya kufungwa rasmi Kikao cha 25 cha Bodi hiyo leo Aprili 17, 2014 katika Ukumbi wa Hoteli ya Charity, Jijini Arusha(kulia aliyeketi) ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Nchini, John Casmir Minja ambaye pia ni Katibu wa Bodi ya Taifa ya Parole(kushoto aliyeketi) ni Mjumbe wa Bodi hiyo Naibu Kamishna wa Magereza Mstaafu, John Nyoka
Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza.

UZINDUZI WA GLOBAL TV ONLINE WAFUNIKA

$
0
0
Kutoka kushoto: Wasanii Dk. Cheni, Bi. Mwenda, Profesa Jay na Wema Sepetu wakishiriki kukata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa GlobaL TV Online jana.
Wema Sepetu na Profesa Jay wakifunua vitambaa wakati wa uzinduzi wa GlobaL TV Online jana katika ofisi za Global Publishers Ltd.
GlobaL TV Online baada ya kuzinduliwa rasmi.
Mkurugenzi wa Global Publishers & General Enterprises Ltd, Eric Shigongo pamoja na staa wa filamu za Kibongo, Wema Sepetu wakikata keki wakati wa uzinduzi huo. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

JK AKABIDHIWA RASMI TUZO YAKE NA WAZIRI MEMBE LEO

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akitoa maelezo mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete kabla ya kumkabidhi Tuzo ya Heshima ya Kiongozi Mwenye Mchango Mkubwa ziadi katika Maendeleo Barani Afrika kwa mwaka 2013 aliyoipokea kwa niaba ya Mhe. Rais Kikwete tarehe 9 Aprili, 2014 Jijini Washington D.C, Marekani. Heshima hiyo kwa Rais Kikwete ilitolewa na Jarida Maarufu la Kimataifa la African Leadership Magazine Group.
Mhe. Membe akimkabidhi rasmi Mhe. Rais Kikwete Tuzo yake. 
Mhe. Rais Kikwete akionesha Tuzo hiyo mara baada ya kuipokea kutoka kwa Mhe. Membe.  Picha na Reginald Phillip.

Baraza Kuu la Wafanyakazi NSSF Lakutana Dar es Salaam

$
0
0
Baadhi ya Wajumbe wa Baraza Kuu la Wafanyakazi wa NSSF wakiwa katika mapumziko mafupi kabla ya kuendelea na mkutano wao. Baadhi ya Wajumbe wa Baraza Kuu la Wafanyakazi wa NSSF wakiwa katika mapumziko mafupi kabla ya kuendelea na mkutano wao.Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Crescentius Magori (kushoto) akikaimu uenyekiti wa moja ya vikao vya Baraza Kuu la Wafanyakazi la Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii. Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Crescentius Magori (kushoto) akikaimu uenyekiti wa moja ya vikao vya Baraza Kuu la Wafanyakazi la Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii. Kulia ni Katibu wake.Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Dk. Ramadhani K. Dau (kushoto) akizungumza na mmoja wa wajumbe wa  Baraza Kuu la Wafanyakazi wa Shirika hilo katika mapumziko mafupi kabla ya kuendelea na mkutano  wao. Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Dk. Ramadhani K. Dau (kushoto) akizungumza na mmoja wa wajumbe wa Baraza Kuu la Wafanyakazi wa Shirika hilo katika mapumziko mafupi kabla ya kuendelea na mkutano.

JK AFANYA UTEUZI WA MABALOZI KUJAZA NAFASI ZILIZO WAZI

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, amefanya uteuzi wa Mabalozi ili kujaza nafasi zilizoachwa wazi na Mabalozi wastaafu kwa mujibu wa sheria.
Mabalozi wateule na aliyehamishwa kituo ni kama ifuatavyo:


1. Balozi Dora Mmari Msechu (kushioto); ameteuliwa kuwa Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Stockholm, Sweden. Hadi uteuzi huu unafanyika Balozi Dora Mmari Msechu ni Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. Anachukua nafasi ya Balozi Mohamed M .H. Mzale ambaye amestaafu.


2. Lt. Gen. Wynjones Matthew Kisamba (kulia), ameteuliwa kuwa Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Moscow, Urusi. Hadi uteuzi huu unafanyika, Lt. Gen. Wynjones Matthew Kisamba alikuwa Mkuu wa Utendaji Kivita na Mafunzo, Makao Makuu ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania. Anachukua nafasi ya Balozi Jaka Mwambi.


3. Kadhalika, Mheshimiwa Rais amemteua Ndugu Joseph Edward Sokoine  (kushoto) kuwa Balozi na Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Kabla ya uteuzi huu, Bw. Sokoine alikuwa Afisa Mambo ya Nje Mkuu na Mkuu wa Utawala katika Ubalozi wa Tanzania, Ottawa, Canada.


               Umetolewa na:
(John M. Haule)
KATIBU MKUU,
WIZARA YA MAMBO YA NJE
NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA,
DAR ES SALAAM.

jeshi la polisi latahadharisha wananchi kuwa makini wakati wa sikukuu ya pasaka

$
0
0
SSP ADVERA SENSO
Tunapoelekea kipindi hiki cha sikukuu ya Pasaka, Jeshi la Polisi nchini, linatoa tahadhari kwa wananchi kuwa makini katika suala la usalama wa maisha na mali zao. 
Uzoefu unaonyesha kwamba, katika kipindi kama hiki cha sikukuu kuna baadhi ya watu hupenda kutumia fursa hiyo kufanya vitendo vya uhalifu. Hata hivyo, Jeshi la Polisi katika mikoa yote limejipanga vizuri kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama kuhakikisha kwamba hakuna vitendo vyovyote vya uhalifu vitakavyojitokeza na endapo vitajitokeza viweze kudhibitiwa kwa haraka. 
 Aidha, ulinzi umeimarishwa kwenye maeneo yote, yakiwemo maeneo ya kuabudia, fukwe za bahari, sehemu za starehe na maeneo mengine ambayo yatakuwa na mikusanyiko mikubwa ya watu. 
 Vilevile, Jeshi la Polisi linawataka madereva na watu wote watakaokuwa wakitumia barabara, kuwa makini na kuzingatia sheria za usalama barabarani, kuepuka kwenda mwendo kasi, kujaza abiria kupita kiasi na kutumia vilevi wawapo kazini. 
Wamiliki wa kumbi za starehe wazingatie uhalali na matumizi ya kumbi zao katika uingizaji wa watu kulingana na uwezo wa kumbi hizo, badala ya kuendekeza tamaa ya fedha kwa kujaza watu kupita kiasi. 
Aidha, wazazi wawe makini na watoto wao, kutokuwaacha watembee peke yao ama kwenda disko toto bila kuwa chini ya uangalizi wa watu wazima ili kuepusha ajali na matukio mengine yanayoweza kusababisha madhara juu yao. 
 Wananchi wakumbuke kutokuacha makazi yao bila uangalizi na endapo italazimu kufanya hivyo watoe taarifa kwa majirani zao, na pale wanapowatilia mashaka watu wasiowafahamu wasikae kimya, watoe taarifa haraka kwenye vituo vya polisi vilivyo karibu yao, ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa haraka. 
 Mwisho, Jeshi la Polisi linapenda kuwashukuru wale wote ambao tayari wamefunga kamera za CCTV katika maeneo yao ya biashara hususani yale yanayokuwa na mikusanyiko mikubwa ya watu, yakiwemo maduka, mahoteli na maeneo ya benki. 
Jeshi la Polisi linaendelea kuwasisitiza ambao bado hawajaweka kamera hizo, kuweka ili ziweze kusaidia kubaini wahalifu na hata kurahisisha ukamataji wa wahalifu hao endapo uhalifu unatokea. 
 Tunawatakia Watanzania wote Pasaka njema. 

 Imetolewa na:- Advera Senso-SSP 
Msemaji wa Jeshi la Polisi.

WACHEZAJI MABORESHO STARS WATAJWA

$
0
0
Kocha Msaidizi wa Taifa Stars, Salum Mayanga ametangaza majina ya wachezaji 16 waliochaguliwa katika maboresho ya timu ya Taifa Taifa Stars kwenye hoteli ya Hill View jijini Mbeya.

Wachezaji hao ni kipa Benedicto Tinoko Simwanda (Temeke), mabeki wa kati; Emma Namwondo Simwanda (Temeke) na Joram Nason Mgeveje (Iringa). Walinzi wa pembeni ni Omari Ally Kindamba (Temeke), Edward Peter Mayunga (Kaskazini Pemba) na Shiraz Abdallah Sozigwa (Ilala).

Viungo ni Yusuf Suleiman Mlipili (Temeke), Said Juma Ally (Mjini Magharibi), Abubakar Ally Mohamed (Kusini Unguja), Hashim Ramadhan Magona (Shinyanga), Omari Athumani Nyenje (Mtwara) na Chunga Said Zito (Manyara).

Washambuliaji ni Mohammed Seif Saidi (Kusini Pemba), Ayoub Kasim Lipati (Ilala), Abdurahman Othman Ally (Mjini Magharibi), Paul Michael Bundara (Ilala). Wachezaji wa U 20 ni Mbwana Mshindo Musa (Tanga) na Bayaga Atanas Fabian (Mbeya).

Alisema mpango huu wa kuboresha timu ya Taifa ambayo inadhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager ni endelevu na kusisitiza kuwa hata wale 18 walioachwa watafuatiliwa na TFF na kuitwa panapokuwa na mahitaji.

“Hawa wote wapo kwenye database ya TFF na hawataachwa tu hivi hivi wapotee,” alisema kocha Mayanga.

Wachezaji ha0 waliingia kambini mjini Tukuyu, Machi 21 mwaka huu na wamefanya mazoezi kwa pamoja kwa karibu wiki nne sasa kabla ya kuchujwa.

Wachezaji 16 waliochaguliwa wanatarajiwa kuondoka Tukuyu kesho (Aprili 18 mwaka huu) na kwenda kwenye kambi ya Taifa Stars katika Hoteli ya Kunduchi ambapo wataungana na wachezaji wa Taifa Stars wa siku zote.

Baadaye watachujwa tena ili ipatikane timu moja ya Taifa iliyoboreshwa.
Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia ya Kilimanjro Premium Lager inaunga mkono utaratibu huu wa maboresho ya Taifa na imewekeza zaidi ya dola milioni 2 kwa mwaka kudhamini Taifa Stars. Huu ndio udhamini mkubwa zaidi ambao Stars imewahi kupata tangu kuanzishwa kwa TFF.

JUMUIYA YA MUZDALIFAT NA TAASISI YA I,H,H YA UTURUKI WATOA SADAKA KWA WATOTO MAYATIMA ZANZIBAR.

$
0
0
 Wawakilishi wa Taasisi ya I,H,H,kutoka Uturuki wakigawa sadaka ya Unga,Mchele,Mafuta ya kupikia pamoja na Nyama kwa Watoto Yatima katika maeneo mbalimbali ya Zanzibar.
 Wachinjaji mbuzi kwa ajili ya Sadaka kwa Watoto mayatima wakichinjaji mbuzi huko Kisauni nje ya Mji wa Zanzibar.
 Wawakilishi wa Taasisi ya I,H,H,kutoka Uturuki wakiendelea kugawa sadaka ya Vitu mbalimbali ikiwa pamoja na Unga wa Ngano,Mchele,Mafuta ya kupikia na Nyama kwa Watoto mayatima walio katika maeneo mbalimbali Zanzibar.
 Wawakilishi kutoka Taasisi ya I,H,H, ya Uturuki wakisalimiana na wanafunzi chekechea wa Skuli ya Muzdalifat mara baada ya kushuka kwenye gari huko Kisauni nje ya Mji wa Zanzibar.
Jumuiya ya Kiislamu ya Muzdalifat(Muzdalifat Islamic Charitable)wakishirikiana na Taasisi ya I,H,H,kutoka uturuki,wakichuna mbuzi waliokwisha kuchinjwa kwa ajili ya sadaka kwa Watoto yatima hafla iliofanyika huko Kisauni nje ya Mji wa Zanzibar. 
PICHA NA YUSSUF SIMAI - MAELEZO ZANZIBAR.

Article 22


Never pay for rabbish!! - Kansiime Anne

WAZIRI WASSIRA KATIKA MAONESHO YA MIAKA 50 YA MUUNGANO, JIJINI DAR ES SALAAM LEO

$
0
0
 Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Isaack Nantanga akimkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mahusiano na Uratibu, Steven Wassira (kushoto) katika Banda la Wizara hiyo, kupata taarifa mbalimbali za Muungano zinazotekelezwa na wizara hiyo pamoja na taasis zake. Maonesho ya siku tano ya Miaka 50 ya Muungano yanafanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam. 
 Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Hifadhi Hati wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Thomas William (kushoto) akimfafanulia Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mahusiano na Uratibu, Steven Wassira (kulia) jinsi mamlaka hiyo ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, jinsi inavyofanya kazi zake Tanzania Bara na Visiwani. Waziri Wassira alilitembelea Banda la Wizara na Taasisi zake katika Maonesho ya Miaka 50 ya Muungano yanayoendelea kufanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam. 
 Ofisa wa Jeshi la Polisi, Christina Mponji akimuonesha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mahusiano na Uratibu, Steven Wassira (wa pili kushoto) picha za Wakuu wa Jeshi la Polisi mbalimbali toka tulipopata uhuru hadi wa hivi sasa.  Waziri Wassira alilitembelea Banda la Maonesho la Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ambalo lina Taasisi tatu za Muungano ambazo ni Jeshi la Polisi, Idara ya Uhamiaji na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida). Maonesho hayo ya siku tano ya Miaka 50 ya Muungano yanafanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam. 
 Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Isaack Nantanga (kushoto) akigawa vipeperushi mbalimbali za wizara hiyo kwa wananchi waliotembelea Banda la Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi na Taasisi zake za Muungano ambazo ni Jeshi la Polisi, Idara ya Uhamiaji na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA). Maonesho ya siku tano ya Miaka 50 ya Muungano yanafanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam
 
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mahusiano na Uratibu, Steven Wassira (kushoto) akipokea vipeperushi vya Idara ya Uhamiaji alipotembelea Banda la Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi pamoja na Taasisi zake za Muungano katika  Maonesho ya siku tano ya Miaka 50 ya Muungano yanayofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam. (Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi).

TAARIFA YA HALI YA UHALIFU MKOA WA MBEYA.

$
0
0
 SACP AHMED Z. MSANGI – KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

TAARIFA KUTOKA TFF LEO Aprili 18, 2014

$
0
0
PAZIA VPL LAFUNGWA, AZAM KUKABIDHIWA KOMBE CHAMAZI
Michuano ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kuwania ubingwa wa Tanzania Bara inafikia tamati kesho (Aprili 19 mwaka huu) kwa timu zote 14 kuwa viwanjani, huku mabingwa wapya Azam wakikabidhiwa kombe lao Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam katika mechi yao dhidi ya JKT Ruvu.

Mechi zote saba zitachezwa kuanzia saa 10 kamili jioni ambapo Yanga na Simba zitakuwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kwa mechi ambayo viingilio vyake ni sh. 5,000 kwa viti vya bluu na kijani, sh. 10,000 viti vya rangi ya chungwa, sh. 20,000 kwa VIP C na B wakati VIP A itakuwa sh. 30,000.

Tayari tiketi zimeanza kuuzwa leo (Aprili 18 mwaka huu) katika vituo saba vya; Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa, Kariakoo (Kidongo Chekundu), Buguruni Shell, mgahawa wa Steers uliopo Mtaa wa Ohio na Samora, Ubungo OilCom, Dar Live Mbagala na Uwanja wa Taifa.

Mechi nyingine zitakuwa kati ya Tanzania Prisons na Ashanti United (Uwanja wa Jamhuri, Morogoro), Rhino Rangers na Ruvu Shooting (Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, Tabora), Mbeya City na Mgambo Shooting (Uwanja wa Sokoine, Mbeya), Oljoro JKT na Mtibwa Sugar (Uwanja wa Sheikh Kaluta Amri Abeid, Arusha) na Coastal Union na Kagera Sugar (Uwanja wa Mkwakwani, Tanga).

MICHUANO YA BEACH SOCCER KUANZA JUMAPILI
Michuano ya mpira wa miguu ya ufukweni (Beach Soccer) inazinduliwa rasmi keshokutwa (Aprili 20 mwaka huu) kwenye ufukwe wa Escape One uliopo Mikocheni, Dar es Salaam na kushirikisha timu 13.

Uzinduzi huo utaanza saa 5 asubuhi na mechi zitachezwa hadi saa 11 jioni. Michuano hiyo inayofanyika kwa mara ya kwanza nchini inashirikisha timu 13 kutoka vyuo mbalimbali vya jijini Dar es Salaam.

Vyuo hivyo ni Chuo Kikuu cha Ardhi (AU), Chuo Kikuu cha St. Joseph Tanzania (SJUIT), Chuo Kikuu cha Tumaini Dar es Salaam (TUDARCO), Chuo cha Ustawi wa Jamii (ISW), Chuo cha Uandishi wa Habari Dar es Salaam (DSJ) na Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere.

Vingine ni Chuo cha Utumishi wa Umma Magogoni, Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT), Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA), Chuo cha Utawala wa Kodi (ITA) na Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT).

Michuano hiyo itakuwa inachezwa Jumamosi na Jumapili kwenye fukwe za Escape One na Gorilla Beach iliyopo Kigamboni, Dar es Salaam.

WAZOEFU TAIFA STARS KUTAJWA KESHO
Wachezaji wazoefu wa Taifa Stars watakaoungana na wale 16 waliopatikana katika mpango wa maboresho wa timu hiyo watatangazwa kesho (Aprili 19 mwaka huu) saa 4 asubuhi kwenye ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).

Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager itapiga kambi kwenye hoteli ya Kunduchi Beach kujiandaa kwa mechi ya kirafiki dhidi ya Burundi itakayochezwa Aprili 26 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Wachezaji waliopatikana katika mpango wa maboresho ya Stars wanatarajiwa kuwasili leo (Aprili 18 mwaka huu), na kwenda moja kwa moja kambini kuwasubiri wenzao watakaotajwa kesho (Aprili 19 mwaka huu).

Wachezaji hao ni kipa Benedicto Tinoko Simwanda (Mara), Emma Namwondo Simwanda (Temeke), Joram Nason Mgeveje (Iringa), Omari Ally Kindamba (Temeke), Edward Peter Mayunga (Kaskazini Pemba), Shiraz Abdallah Sozigwa (Ilala), Yusuf Suleiman Mlipili (Temeke) na Said Juma Ally (Mjini Magharibi).

Wengine ni Abubakar Ally Mohamed (Kusini Unguja), Hashim Ramadhan Magona (Shinyanga), Omari Athumani Nyenje (Mtwara), Chunga Said Zito (Manyara), Mohammed Seif Saidi (Kusini Pemba),Ayoub Kasim Lipati (Ilala), Abdurahman Othman Ally (Mjini Magharibi) na Paul Michael Bundara (Ilala).

BONIFACE WAMBURA
OFISA HABARI NA MAWASILIANO
SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)


MAMA SALMA APOKEA MBIO ZA PIKIPIKI KUADHIMISHA MIAKA 50 YA MUNGANO-ATEMBELEA HOSPITALI YA MKOA WA LINDI

$
0
0
 Mjumbe wa NEC Taifa ya CCM, Mama Salma Kikwete akiwahutubia wananchi wa Kata ya Mingoyo wakati wa sherehe ya mbio za pikipiki kusherehekea miaka 50 ya Mungano zitakazofikia kilele 
  Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA), Mama Salma Kikwete akimjulia hali mtoto Seleman Salum Namputa, miezi 3, aliyelazwa katika hospitali ya Mkoa wa Lindi, Sokoine. Kulia ni Mama mzazi wa mtoto Seleman ajulikanaye kama Mariam kutoka katika kijiji cha Moka huko Lindi Vijijini. Mama Salma alitembelea hopitalini hapo tarehe
 Burudani zikiendelea
Mjumbe wa NEC wa Lindi Mjini Mama Salma Kikwete akiwasalimia wananchi wa Kijiji cha Madangwa na wageni waliohudhuria sherehe ya kupokea mbio za pikipiki kwa Mikoa ya Kanda ya Kusini inayojumuisha Ruvuma, Mtwara na Lindi katika kusherehekea miaka 50 ya Mungano. Picha na John Lukuwi. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA
Viewing all 110175 articles
Browse latest View live




Latest Images