Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110158 articles
Browse latest View live

MASIKINI TWIGA WETU.!

$
0
0
Pichani ni Maofisa wa TANAPA ndani ya Hifadhi ya Wanyama ya Katavi,Wakiwa wamenaswa na Camera ya Globu ya Jamii,ilipokuwa imetoka kwenye kazi maalum Wilayani Mlele mkoani humo na kukumbana na tukio hilo la Maofisa hao wakimtazama Twiga aliyegongwa na gari na kufa papo hapo,katika tukio hilo la huzuni kubwa,gari iliyohusika na ajali hiyo halikujulikana mara moja.
Maofisa wa TANAPA waliokuwa doria hifadhini,wakitafakari jambo mara baada ya kumkuta Twiga akiwa amegongwa na kufa papo hapo jioni ya leo ndani ya Hifadhi ya Wanyama Katavi.

ngoma azipendazo ankal

$
0
0
Prince Nico Mbarga anakupa "Sweet Mother"

SHUKRANI

$
0
0
Marehemu Martha Peter Lubuva
24.04.1947 – 18.01.2014

Familia ya Jaji Mstaafu Damian Z. Lubuva inapenda kutoa shukrani za dhati kwa ndugu, jamaa, marafiki na majirani wote ambao wameshirikiana na kutupa misaada ya hali na mali kipindi chote cha kuugua kwake Marehemu Martha Peter Lubuva hadi kifo chake tarehe 18 Januari, 2014 huko India.  Hii ilitupa faraja kubwa katika kipindi hicho kigumu kwa familia.

Kwa namna ya pekee, familia inatoa shukrani kwa Mheshimiwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete, kwa kutuma salaam za rambirambi na Mama Salma kufika nyumbani kutufariji, Waziri Mkuu Mizengo Pinda na Mama Tunu Pinda, kwa kufika kwao kutufariji siku ya mazishi.  Aidha, tunawashukuru Viongozi mbalimbali wa Serikali na Mashirika ya Umma wakiwemo Mh. Benjamini W. Mkapa Rais Mstaafu, Mh. Salim Hamed Salim, Mh. Joseph.S. Warioba na Edward Lowassa, Mawaziri, Mh. Fredrerick Werema, Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Majaji.

Mahsusi, Familia inawashukuru sana Baba Askofu wa Jimbo Katoliki Kondoa, Baba Askofu wa Jimbo Katoliki Dodoma na Baba Askofu wa Jimbo Katoliki Mahenge Pamoja na Paroko wa. Parokia ya Mt. Petro Oysterbay kwa kuendesha Ibada ya mazishi kanisani na makaburini.

Kwa namna ya pekee tunawashukuru Viongozi na Watumishi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Mahakama, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Kanali Kinana, Katibu Mkuu wa CCM, Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Hifadhi ya Jamii, Wizara ya Afya, Madaktari wa Muhimbili na Hospitali ya Apolo India, Ubalozi wa Tanzania India, Dr. Mvungi, Polisi, Majirani wa Mtaa wa Bongoyo Kaunda na Mazengo, Jumuiya ya Mt. Clara na Kwaya ya Mt. Petro Oysterbay.  Pia tunatoa shukrani kwa Umoja wa Wakazi wa Kondoa Dar – Es – Salaam.

Kwa vile si rahisi kuwataja wote walioshirikiana na familia katika kipindi cha msiba, kwa taarifa hii tunawaomba wote kupokea shukrani zetu za dhati kwa moyo wa upendo mkubwa mlioonyesha kwa familia ya marehemu.

MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI APUMZIKE KWA AMANI, AMINA

TANGAZO LA MSIBA MAMA BERNADA ALOYCE NJELEKELA

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Dkt. Marina Njelekela anasikitika kutengaza kifo cha mama yake mpendwa Bi. Bernada Aloyce Njelekela kilichotokea jana saa nane mchana katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Mazishi yanatarajiwa kufanyika kesho mchana Makaburi ya Agape huko Mbezi Luis.

Tumeambatanisha ratiba ya mazishi pamoja na ramani inayoonyesha ulipo msiba.


RATIBA YA MAZISHI YA MAMA BERNADA ALOYCE NJELEKELA

(26 NOV 1933 – 14 APRILI 2014)


SIKU YA JUMATANO, 16 APRILI 2014

MUDA

SHUGHULI

MHUSIKA


Saa 12.00 asubuhi

Maandalizi ya mwili


Salome Chambiri

Saa 1.00 – 8.30 asubuhi

Mwili kutoka Muhimbili Hospitali kuelekea Mbezi Luis nyumbani


John Mlay

Saa 5.30 – 7.00 mchana

Chakula

MC


Saa 7.30  - 8.00 mchana

Mwili kutokea nyumbani kuelekea Kanisani – St. Theresia wa Mtoto Yesu Mbezi Luis


Mkiti wa Jumuiya Mtakatifu Dominico- Elias Chale

Saa 8.00 – 9.00 mchana


Misa


Baba Paroko

Saa 9.00 – 9.15mchana

Shukrani za familia/Wasifu

Familia ya Njelekela


Saa 9.15- 10.15mchana

Heshima za Mwisho

MC


Saa 10.15- 10.30jioni

Kuelekea makaburini

John Mlay


Saa 10.30 – 11.30 jioni

Maziko na kuweka mashada

MC


Saa 11.30 jioni

Shukrani

Familia ya Njelekela


Saa 11.45 jioni

Mwisho wa shughuli za Mazishi

MC


TUMSIFU MARIA ENYI WANAWE


Tumsifu Maria enyi wanawe

Tumtolee salamu tumshangilie

Salaam, Salaam, salaam Maria

Salaam Salaam Salaam Maria


Katika uwingu ni mfalme mkuu

Mwondoa hatari mama wa Mungu

Salaam, Salaam, salaam Maria

Salaam Salaam Salaam Maria


Hatuna Mwombezi aombeae

Kwa Mungu mwenyezi kuliko wewe

Salaam, Salaam, salaam Maria

Salaam Salaam Salaam Maria


Nyota ya Bahari, Mlango wa Mbingu

Mwondoa hatari mama wa Mungu

Salaam, Salaam, salaam Maria


Salaam Salaam Salaam Maria

NAPE NNAUYE AMVAA TUNDULISU KUFUATIA KUMKASHIFU BABA WA TAIFA

$
0
0
Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwahutubia wakazi wa kijiji cha Maji Moto kwenye uwanja wa kijiji hicho mapema jana jioni,Wilayani Mlele mkoani Katavi.

KIJIWE CHA UGHAIBUNI

JUST IN: JK AHANI MSIBA WA MUHIDIN MAALIM GURUMO JIONI HII

$
0
0
 Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akimfariji mjane wa marehemu Muhidin Maalim Gurumo (mwenye shuka nyeupe) na wanafamilia alipokwenda kuhani msimba huo Ubungo Makuburi jioni ya leo April 15, 2014, siku ambayo marehemu alizikwa kijijini kwao Masaki, Kisarawe, Mkoa wa Pwani.
Marehemu Gurumo, aliyefariki dunia juzi katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa matatizo ya moyo, atakumbukwa kama Baba wa Muziki wa dansi nchini akianzia miaka ya 1960 na bendi mbalimbali ikiwemo NUTA Jazz na kumalizia na Msondo Ngoma kabla ya kustaafu muziki mwaka jana.
 Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete pole Bw. Abdallah Muhidin Gurumo, mtoto wa marehemu Muhidin Maalim Gurumo na wanafamilia alipokwenda kuhani msimba huo Ubungo Makuburi jioni ya leo April 15, 2014,
 Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete Bw. Omar Muhidin Maalim Gurumo na wanafamilia alipokwenda kuhani msimba huo Ubungo Makuburi jioni ya leo April 15, 2014,
 Sehemu ya waombolezaji
 Mmoja wa wana familia Bw. Salim Zagar akitoa taarifa fupi ya msiba pamoja na mazishi kwa Mhe Rais
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Muziki wa dansi Bwana Brighton akimshukuru Rais Kikwete kwa kwenda kutoa pole ya msiba huo

hati ya Makubaliano ya Muungano ilivyowasilishwa Bungeni Mjini Dodoma, "UKAWA" wasusia kikao

$
0
0
Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba,Samia Suluhu Hassan akionesha nakala ya Hati ya Makubaliano ya Muungano iliyothibitishwa Bungeni leo mjini Dodoma.
Juu na chini ni Wajumbe wa Bunge  Maalum la Katiba ambao wanaounga mkono mfumo wa  Serikali za tatu wakitoka katika Ukumbi wa Bunge leo mjini Dodoma baada ya kususia kikao.Picha na Idara ya Habari-MAELEZO

uwekaji wa saini makubaliano na Makampuni Yaliyoshinda Zabuni ya Kujenga Mtandao wa Mawasiliano.

$
0
0
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. George Yambesi (kulia) na Afisa Masoko na Mauzo TTCL Bw. Peter Ngota (kushoto) wakitia saini mkataba wa makubaliano ya kuweka mtandao mmoja wa mawasiliano Serikalini hivi karibuni jijini Dar es salaam
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. George Yambesi (kulia) akibadilishana Mkataba waliosaini  Mkurugenzi wa Kampuni ya Softnet Gilbert Herman (kushoto)  jijini Dar es salaam
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. George Yambesi akiongea na washiriki (hawapo pichani) waliohudhria hafla ya kusaini mikataba ya kuweka Mtandao wa Mawasiliano wa Serikali hivi  jijini Dar es salaam
Mtendaji Mkuu Wakala ya Serikali Mtandao Dkt. Jabiri Bakari (kushoto) akiwapongeza makampuni ya Kitanzania  ya TTCL na Sosftnet  kwa kushinda zabuni ya kujenga mtandao wa mawasiliano na kuyashinda kampuni nyingine duniani. Kulia kwake ni  Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. George Yambesi.
Baadhi ya washiriki waliohudhuria hafla ya kusaini mikataba ya kuweka Mtandao wa Mawasiliano wa Serikali kati ya hivi karibuni jijini Dar es salaam.Picha zote na Eliuteri Mangi
---
Na Eleuteri Mangi Serikali imetiliana saini makubaliano na makampuni yaliyoshinda zabuni ya kujenga mtandao wa mawasiliano. 
 Makubaliano hayo yalisainiwa  jijini Dar es salaam kati ya Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. George Yambesi kwa niaba ya Serikali na kampuni ya Softnet Teknology Ltd pamoja na Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL). 
 Katibu Mkuu Yambesi alisema kuwa mradi huo unalenga kuweka mtandao mmoja wa mawasiliano Serikalini na taasisi zake na unasimamiwa na kuratibiwa na Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma (OR-MUU). 
 “Mradi huu ni hatua muhimu ya utekelezaji wa Serikali Mtandao ukiwa na lengo la kuipatia Serikali na taasisi zake mawasiliano ya sauti, data, nyaraka na picha yenye uhakika, rahisi, salama na yanayopatikana kwa muda wote” alisema Katibu Mkuu Yambesi. 
 Akifafanua kuhusu malengo ya mradi huo Yambesi amesema yanaenda sanjari na malengo ya kujengwa kwa mkongo wa Taifa na utekelezaji wa sera ya Serikali mtandao, Sera ya TEHAMA ya mwaka 2003, programu ya mabadiliko ya utekelezaji wa kazi na utoaji wa huduma katika katika Utumishi wa Umma. 
 Malengo mengine ni Mkakati wa kukuza uchumi na kupunguza umaskini (MKUKUTA), Mpango Taifa wa Maendeleo ya miaka mitano 2012 hadi 2016 na Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025.

ALUTA KONYINYUA - Uraia Pacha na Uzalendo

$
0
0
Katika siku zilizopita suala la uraia pacha lilikuwa gumzo kwa Watanzania waishio kwenye Diaspora na wale waishio Tanzania. 
Lengo kubwa la gumzo au mjadala huu lilikuwa ni kujadili kama uraia pacha unaweza kuruhusiwa kwa raia yeyote wa Tanzania au kwa mtizamo mwingine, na lengo ni kuelimisha umma kuwa mtu yeyote aliyezaliwa Tanzania na atakayepata uraia wa pili hawezi kupoteza haki yake ya kuwa Mtanzania. 
Suala hili bado linajadiliwa na Watanzania lakini bado wapo Watanzania wanaopinga uraia pacha kwa kudai kuwa Watanzania waishio ughaibuni hawana uzalendo au “patriotism”. 
Nimeonelea ni vizuri kulijadili suala hili la uzalendo kwa vile Watanzania wengi wa ughaibuni na wale waishio Tanzania bado wanaamini kuwa si kweli kuwa Watanzania wa Ughaibuni hawana uzalendo na hapa natoa mifano iliyotolewa katika kuthibitisha ukweli huu. 
 Kwa kuanzia ingekuwa vizuri dhana ya uzalendo ieleweke vizuri. Pili, dhana ya nani ni mzalendo na nani si mzalendo itawekwa bayana na mwisho, namna ya kupima uzalendo wa Watanzania waishio Tanzania na nje ya Tanzania itaelezwa kwa kifupi. 
 Tunaanza na uzalendo na umaana wake. Uzalendo yaani “patriotism” ni hali ya kuwa mtii kwa taifa kwa maana ya kutii, kulinda na kutetea misingi iliyounda taifa. Kwa kifupi kabisa na bila kuchanganya mambo uzalendo ndio huu. 
Kwa mantiki hii, kuilinda na kuitetea misingi iliyounda taifa na hata kuhakikisha kuwa taifa halifi humfanya raia awe mzalendo. Lakini raia anaweza kuwa mzalendo kwa taifa lake na kutokuwa mzalendo kwa serikali au chama tawala. Na anapokosa uzalendo kwa serikali au chama tawala anaweza kubakia mzalendo kwa taifa lake. 
Mantiki ya kuwa na vyama vingi vya kisiasa ndio hii. Hivyo uzalendo huwa ni kwa taifa na sio kwa chama au serikali tawala. Kwa kuelezea hili, mimi mwandishi wa article hii sina chama cha siasa na naomba nisieleweke vibaya kwa chama tawala cha CCM kwa sababu natoa mifano tu ambayo inapatikana duniani kote na sina vita na CCM wala serikali yake na sina vita na chama chochote cha kisiasa. 
Natoa tu maelezo ya kiutaalamu, kwa sababu mimi ni mtaalamu wa masuala haya. Neno uzalendo yaani “patriotism” lilishika hatamu wakati wa kale ambapo nchi na serikali zililazimisha raia wafuate dini moja kwa misingi ya kujenga taifa na utaifa. 
Watawala walifikia hata kuwauwa wale waliokataa kuwa na dini ya kitaifa hasa kule Ulaya. Na mtu aliyefuata dini ya nchi ambayo kwa kawaida ilikubalika na serikali au watawala alionekana kuwa na uzalendo kwa nchi yake na yule aliyekataa kufuataa dini inayotambulika na nchi na serikali alionekana kukosa uzalendo. Baada ya usumbufu huu, baadhi ya raia wa Mataifa ya Ulaya walipinga mfumo huu na walipigania masuala ya dini na siasa yatenganishwe. 
Na kwa nchi za Ulaya ndipo ukawa mwanzo wa kutenganishwa kwa dini na siasa. Kwa lugha ya kitaalamu kwa mazingira ya Ulaya tunasema “separation of church from the state”, ili kila mtu apate uhuru wa kuabudu. Kwa nchi za Kiafrika, uzalendo uliongezeka sana wakati wa kumfukuza mkoloni kutoka kwenye ardhi ya Afrika. 
Kila Mwafrika alikuwa na lengo na dhumuni moja, kukataa kutawaliwa. Na kauli mbinu ya Waafrika ilikuwa moja na ilisikika katika kona zote za bara la Afrika kauli hiyo ilikuwa ni “Uhuru” ambayo ilisemwa katika lugha tofauti za Kiafrika. 
Kwa mfano, hata Afrika ya Kusini wakati wa “Apartheid” uzalendo uliongezeka na raia waliungana kuupinga kwa nguvu zote wakiwapinga makaburu. Kwa Tanzania, uzalendo uliongezeka wakati wa vita vya kumng’oa Nduli Iddi Amini na wakati wa nguvu kazi wakati wa vijiji vya ujamaa. Uzalendo vile vile hupotea. 
Raia anayeishi ndani au nje ya nchi anaweza kuwa au anaweza vile vile kukosa uzalendo. Mifano ni kama ifuatayo. Kama kuwa mzalendo ni kuwa mtii kwa taifa lako na kuilinda misingi ya taifa lako, pale raia au afisa wa serikali anapokuwa mbadhirifu wa mali ya umma ana uzalendo? Nadhani jibu ni la hasha au hapana. 
 Mtu huyu au afisa huyu hana uzalendo. Kumbe raia aliye “corrupted” hana uzalendo kwa taifa lake. Na raia huyu anaweza kuwa anaishi ndani au nje ya mipaka ya nchi yake lakini kwa kuwa sio mwaminifu kwa taifa lake, anakuwa si mzalendo. 
 Mfano wa pili, raia aishie ughaibuni ambaye ni mtii kwa taifa lake na hayupo “corrupted” na anayesaidia ndugu zake kwenye nchi aliyotokea kwa hali na mali, je huyu sio mzalendo? Jibu ni kuwa huyu ni mzalendo. Nadhani mifano hii ya awali inawafumbua macho kuhusiana na nani ni na nani sio mzalendo kwa taifa lake.Kwa maana hiyo, uzalendo peke yake hauwezi kuwa kigezo cha kuwanyima Watanzania uraia pacha kwa sababu hata Mtanzania aishiye Tanzania na ambaye hajawahi kutoka nje ya nchi anaweza kukosa uzalendo vile vile. 
 Mfano wa mwisho ni kuwa uzalendo vile vile unaweza kupungua au kuongezeka kufuatana na nyakati. Hivyo matukio mbalimbali ya kitaifa na kimataifa yanaweza kuua au kuhifadhi uzalendo alionao raia. 
Hivyo sio kweli kuwa uzalendo wa kila raia bila ya kujali anaishi ndani au nje ya mipaka ya nchi yake hubakia vile vile maisha yake yote mpaka mauti yamtoe duniani. 
Uzalendo huweza kupungua au kuongezeka au kupotea kabisa. Hivyo suala kumnyima Mtanzania wa ughaibuni haki yake ya kuzaliwa Tanzania na haki ya uraia pacha kikatiba kwa misingi ya uzalendo peke yake ni sababu isiyo na msingi wala umaana wowote. 
 Nadhani kwa maelezo haya dhana hii ya uzalendo inaeleweka na naamini haitatumika kama kigezo cha kimsingi nambari wani cha kuwakatalia Watanzania haki yao ya kiubinadamu ya kupata uraia pachja na haki yao ya kuzaliwa Tanzania inayowapa haki ya kuwa Watanzania kikatiba.  

Imeandaliwa na Deogratius Mhella, 
Katibu wa Vikao vya Viongozi wa Jumuiya za Watanzania na DICOTA kwa lengo la kuelimisha Watanzania kuhusu suala la uraia pacha katika jitihada za Watanzania wa Ughaibuni kuendeleza mdahalo wa Uraia pacha ili Bunge Maalumu la Katiba liweze kuingiza suala la uraia pacha kwenye katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

MBEYA ZAMU YENU SASA IMEFIKA

sherehe za muungano seattle, marekani

watu watatu mbaroni kwa kukutwa na bangi ndani ya basi la new force dodoma

$
0
0
Jeshi la Polisi Mkoani Dodoma linawashikilia watu watatu kwa kosa la Kupatikana na Bhangi kiasi cha Kilogramu 133.5 yenye thamani ya Ths. 20,025,000/= bei ya mitaani (street value). Watuhumiwa hao wamekamatwa mnamo tarehe 16/04/2014 majira ya 7:30 mchana eneo la Stend Kuu ya mabasi katika Manispaa na Mkoa wa Dodoma. 
Watuhumiwa hao walikuwa wakisafirisha Bhangi katika mabegi baada ya kupanda basi kutokea Kijiji cha MANONGA – TINDE Mkoani SHINYANGA kwenda jijini Dar es Salaam katika basi namba No. T.931 CGU mali ya kampuni ya NEW FORCE linalofanya safari zake kutokea Kahama kwenda jijini Dar es Salaam. 
Watu hao walifahamika kwa majina ya:- 
 1. CALVIN S/O PROSPER SALEKA, miaka 23, kabila Mchaga, Mwanafunzi wa chuo cha Institute of Finance Management (IFM) cha Dar es Salaam, mwaka wa pili, alikamatwa akiwa na mabegi mawili ya bhangi yenye uzito 51kgs 
 2. JOHN S/O JOSEPH, Miaka 31, kabila msukuma, mkulima na mkazi wa Kinondoni Dar es Salaam, alikamatwa akiwa na mabegi mawili ya bhangi yenye uzito wa 42.5kgs. 
 3. JOSEPH S/O CHARLES BATONI, Miaka 22, kabila msukuma, mkulima na mkazi wa Shinyanga. alikamatwa akiwa na mabegi mawili ya bhangi yenye uzito 36.5kgs 
 Watuhumiwa hao walikamatwa kufuatia taarifa za raia mwema aliyewatilia mashaka na kutoa taarifa Polisi. Mbinu waliyotumia kusafirisha ni kuhifadhi katika mabegi makubwa ya nguo na kufunga kwa mifuko ya nailoni kisha kusaga vitunguu na kuweka katika mabegi hayo pamoja na kupulizia manukato (perfume) ili kuondoa harufu wasiweze kugundulika kirahisi. 
 Tukio lingine katika kijiji cha Central Kiteto Tarafa ya Mlali Wilaya ya Kongwa zilikamatwa lita 300 za Pombe haramu ya Gongo nyumani kwa Salumu s/o Chamagulu ambaye alikimbia baada ya kuona Polisi na tunaendelea kumtafuta. 
 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi David A. Misime – SACP, anawapongeza kwa dhati raia wema wanaoshirikiana na Jeshi la Polisi kwa kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu ili kuendelea kudhibiti madawa ya kulevya na Pombe ya Moshi inayoharibu vijana wengi.
 Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma linawashikilia abiria wa tatu waliokuwa wakisafiri na Basi la New Force kutoka Kahama kuelekea Jijini Dar es Salaam.Kwa Mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma David Misime, wamekamatwa leo mchana wakiwa wanasafirisha Debe ishirini za bangi.Wanaoshikiliwa ni Kevin Prospar(aliyekaa pichani kulia),Joseph Charles (aliyekaa kulia) na John Joseph(aliye kaa katikati)
 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma David Misime kushoto akikagua bangi iliyo kamatwa.

Basi la New Force lililokamatwa likiwa limebeba abiria waliokuwa na bangi likiwalimeshililiwa kwa muda Makao ya Polisi Mkoa wa Dodoma. 
Picha na  Deusdedit Moshi wa Globu ya Jamii, Kanda yan Kati

MAMA SALMA KIKWETE AWATAKA WAKAZI WA KATA YA MSINJAHILI KUTOOGOPA KUVUTA UMEME MAJUMBANI MWAO

$
0
0
Na Anna Nkinda- Maelezo, Lindi

Wakazi wa kata ya Msinjahili wilayani Lindi wametakiwa kutoogopa kuvuta umeme majumbani mwao kwa kuhofu kuwa wakifanya hivyo wataonekana ni matajiri kwani matumizi ya umeme ni ya gharama naafuu ukilinganisha na  mafuta ya taa.

Mwito huo umetolea jana na  Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi  (CCM) Taifa (NEC) wilaya ya Lindi mjini wakati akiongea  kwa nyakati tofauti  na viongozi wa Halmashauri kuu ya tawi ya Chama hicho  katika matawi ya  Muungano, Jitegemee, Sinde na Mnali yaliyopo katika kata ya Msinjahili wilaya ya Lindi mjini.

Mama Kikwete ambaye pia ni Mke wa Rais Jakaya Mrisho Kikwete alisema ili kuboresha  maisha ya wananchi Serikali imejitahidi kupitisha  umeme wa gesi katika  vijiji vilivyopo katika kata hiyo na kupunguza gharama ya uvutaji ambazo ni nafuu  jambo la muhimu ni kwa wananchi kuutumia.

TAARIFA YA MJENGWABLOG KUTOKUWA HEWANI

$
0
0
NDUGU ZANGU,

MJENGWABLOG HAIKO HEWANI TANGU JANA SAA TATU USIKU. NI KUTOKANA NA MATATIZO YA KIUFUNDI KWENYE DATA CENTRE NCHINI MAREKANI ZINAKOHIFADHIWA.

WAHUSIKA WALIOKO KWENYE DATA CENTRE WANAFANYA KAZI KATIKA KILA DAKIKA KUHAKIKISHA HITILAFU HIYO INAREKEBISHWA HARAKA IWEZEKANAVYO.

KWA SASA UNAWEZA KUENDELEA KUTUPATA KWENYE URSTREAM KWANZAJAMII RADIO, WEBSITE KWANZAJAMII.COM, FACEBOOK: KWANZAJAMII RADIO FANS

POLENI SANA KWA USUMBUFU NA TUNAWASHUKURU KWA KUENDELEA KUTUAMINI,

MAGGID MJENGWA,
MWENYEKITI MTENDAJI
IKOLOMEDIA- MJENGWABLOG/KWANZAJAMII.

KUMBUKUMBU

$
0
0
Marehemu Anthony Simon Njeje Enzi za uhai wake 

Ni miaka Sita sasa imepita tangu ulipo enda kwenye makao ya kudumu.Hatupo nawe kimwili lakinii kiroho upo nasi daima. 

Tunakukumbuka sana Baba yetu Mpendwa. Unakumbukwa sana na Mke wako Mpendwa Mama Elizabeth Anthony Njeje, Wanao Aninziye, Luseshelo-Ernest, Fredy na Sarah. 

Wajukuu zako Anthony Jr, Shikunzi-Alvin, Amarisa na Yasinta, Pia unakumbukwa na wafanyakazi wenzako wote wa Benki, majirani zako, waumini wenzako, ndugu Jamaa na Marafiki. 

Sisi Tulikupenda sana lakinin Mungu alikupenda Zaidi. Jina la Bwana Libarikiwe.
AMEN

Mambo ya Mashindano ya Heineken foosball Wikiendi hii ya pasaka

$
0
0
Baadhi ya wadau wa mpira wa meza yani foosball unaothaminiwa na Heineken, wakicheza pale Frisha’s Arena.

Weekend hii Heineken inakuletea mchezo kabambe wa foosball karibu na pale ulipo. Kushiriki kwa michuano hii unatakiwa kufika eneo husika pata kinwaji cha Heineken, Sajili jina la timu yako na tayari utakuwa umepata nafasi yakushinda tripu kali yakwenda Ibiza Spain kushuhudia fainali za ligi ya mabigwa ulaya UEFA champions league.
MC mkali a.k.a Mr.foosball better known as Cpwaaa akihamasisha wadau kushiriki.
Washiriki wa mchezo wa foosball wakipeana mkono baada ya kujaribu bahati yao pale Frisha’s Arena.
Captain wa timu ya Champion Dean Dominic (kulia. pamoja na mwenzake Dennis Respitus wakifurahia ushindi wao pale Frisha’s Arena. Michuano ya Heineken foosball itaendelea katika sehemu mbalimbali za burudani jijini Dar.

Kwa mjibu wa Heineken Tanzania Tarehe 18 April mtanange wa Foosball utaendelea pale kisima cha burudani Brazil Tegeta. Pia Michauno ya foosball itafanyika Liquid bar and lounge kwa watu wa nguvu Chang’ombe.

Tarehe 19: Mechi zitahamia kwa wakazi wa Boko pale Hisaje bar, wadau fikeni kushuhudia mecho huu kabambe na wakipekee. Bila Kusahau bar ya kisasa Catalunya iliyopo nyuma ya hospitali roundabout ya Mlimani City. Hii siyakukosa.

KATIBU MKUU WA CCM,KINANA AHITIMISHA ZIARA YAKE YA SIKU 21 MIKOA YA RUKWA,KIGOMA NA KATAVI LEO

$
0
0
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia katika mkutano wa hadhara katika viwanja vya Kashaulili, mjini Mpanda leo, baada ya kuhitimisha ziara ya siku 21ya kikazi ya kuimarisha uhai wa chama na kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya CCM katika mikoa ya Rukwa, Kigoma na Katavi.
Baadhi ya Wanachama wa CCM na wananchi wakishangilia jambo wakati Katibu Mkuu wa CCM,Ndug Kinana alipokuwa akiwahutubia wakazi wa mji wa Mpanda jioni ya leo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa Kashaulili mjini Mpanda mkoani Katavi.
Mjumbe wa NEC Taifa,Balozi Ali Karume akiwahutubia wakazi wa Mpanda mjini mapema leo mkoani Katavi,wakati wa kufunga ziara ya Siku nne ya Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana mkoani humo.Balozi Karume aliwasisitizia wananchi hao kuwa na umoja na mshikamano katika suala zima la kuutetea Muungano,Karume akaongeza zaidi kuwa Wananchi wanahitaji Serikali mbili  na si tatu kama amabvyo wengine wamekuwa wakidai.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrhaman Kinana akipanda juu ya tanki alipokwenda kukagua mradi wa maji wa Ikolongo, eneo la Kazima, mjini Mpanda, Katavi leo.
Mjumbe wa NEC-CCM kutoka Zanzibar, Balozi Ali Abeid Karume (aliyevaa kofia) akipanda juu ya tanki kukagua mradi wa maji wa Ikolongo, mjini Mpanda leo
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrhaman Kinana akishuka juu ya tanki alipokwenda kukagua mradi wa maji wa Ikolongo, eneo la Kazima, mjini Mpanda, Katavi leo. 
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akipata maelezo mafupi kuhusiana mradi wa eneo la kuweka tanki la maji katika  eneo la Kazima, mjini Mpanda, Katavi leo.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akisaidia kutandaza mabomba katika mradi wa maji wa Ikolongo, eneo la Kazima, Kata ya Kawajense, Mpanda Mjini, wakati wa ziara ya kuimarisha uhai wa chama na kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya CCM katika Mkoa mpya wa Katavi. Kinana amehitimisha leo ziara ya kikazi ya siku 21 katika mikoa ya Rukwa, Kigoma na Katavi.

PICHA ZAIDI BOFYA MICHUZIJR.BLOGSPOT.COM

utulivu watawala bunge la katiba mjini dodoma leo - kwa mara ya kwanza toka lizinduliwe

$
0
0
 Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalumu Mhe.Samia Suluhu akiwa anafuatilia mchango wa Mhe.William Lukuvi kwa makini.
Hali ya hewa yarejea kuwa ya kawaida bunge maalum la katiba mjini Dodoma leo
  Hali ya Ukumbi Ulivyo kuwa Leo ambapo  Wabunge wakifuatilia jambo kwa makini na ustaarabu wa hali ya juu.
 Wabunge wakifuatilia jambo kwa makini.

hatimaye Mwenye simu iliyosahauliwa garini kapatikana

$
0
0
Nashukuru sana  kwa msaada wako.Wiki iliyopita niliweka tangazo langu humu nikiomba msaada wa kumpata dada aliyesahau simu yake ndani ya gari langu,wadau walitoa mawazo mbalimbali ya namna ya kumpata huyo dada.
Kuna mdau alinishauri nitoe line yake(iliyofungwa) na niweke line nyingine,nimefanya hivyo na nikampata rafiki yake akanieleza wapi mama yake anapatikana.
Bahati nzuri namfahamu mama huyo,hivyo nimeomba namba ya huyo mama kwa watu ,na nimeongea naye na wakati wowote nitaikabidhi simu hiyo kwa mama wa binti huyo.
Asanteeni sana kwa msaada wenu.
Mdau
Viewing all 110158 articles
Browse latest View live




Latest Images