Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110173 articles
Browse latest View live

michango ya waheshimiwa zakhia meghji na Frederick Migala wavutia wengi bungeni dodoma

$
0
0
 Mheshimiwa Zakia Hamdani Meghji ambaye uchangiaji wake uliwavutia wengi baada ya kuweka wazi kuwa anaunga mkono Serikali mbili na kuwa hayuko tayari kuona muungano unakufa wakati akichangia kifungu namba moja na  namba sita.Kulia kwake ni Mhe.Hilda Ngoye.Wote wawili wamewahi kuwa wakuu wa Mkoa wa Kilimanjaro kwa Nyakati tofauti
 Mhe.Frederick Migala kutoka kundi la walemavu akichangia.
Mhe.Kingunge Ngombale Mwiruakimpongeza Mhe.Frederick Migala kutoka kundi la walemavu akichangia baada ya kuvutiwa na hoja za mchango wake kifungu namba moja na nambasita cha katibampya. Picha na Deusdedit Moshi wa Globu ya Jamii, Dodoma.

NEWS ALERT: Balozi Sefue aonesha Hati ya Muungano

$
0
0
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akiowaonesha waandishi wa habari hati halisi ya Muungano ikulu jijini Dar es Salaam leo jioni(picha na Freddy Maro)

WANANCHI KUNUNUA MAFUTA YA GARI KUPITIA M PESA

$
0
0
Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Tanzania Salum Mwalim akiongea na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa huduma ya kulipia mafuta kwa Mpesa kwenye vituo vya mafuta vya Total nchini. Kulia ni Mkurugenzi wa Biashara wa Total Romee de Villeneuve. Uzinduzi huo umefanyika leo jijini Dra es salaam.  
Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Tanzania,Salum Mwalim akiwaonesha waandishi wa habari (hawapo pichani) jinsi ya kulipia mafuta kwa Mpesa kwenye vituo vya mafuta vya Total muda mfupi baada ya kuzinduliwa rasmi kwa huduma hiyo kwenye kituo cha Total cha Morocco jijini Dra es salaam. Kulia ni Mkurugenzi wa Biashara wa Total Romee de Villeneuve. Huduma hiyo itakuwa ikipatikana kwenye vituo vyote vya Total hapa nchini.
Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Tanzania Salum Mwalim (wa pili kushoto) akimsadia dereva Taxi Said Juma kulipia mafuta kwa njia ya M-pesa katika kituo cha Mafuta cha Totola Morocco jijini Dar es salaam akiwa ndie mteja wa kwanza kutumia huduma hiyo muda mfupi baada ya kuzinduliwa kituoni hapo. Kushoto ni Mkurugenzi wa Biashara wa Total Romee de Villeneuve na kulia ni mhudumu wa kituo hicho Malaki Peter. Huduma hiyo itakuwa ikipatikana kwenye vituo vyote vya Total nchini.
Wafanyakazi wa Vodacom wa idara ya mauzo wakibandika stika kwenye kituo cha mafuta cha Total Morocco jijini Dar es salaam zinazoonesha nambari ya biashara ya kulipia huduma ya mafuta kwa njia ya Mpesa kituoni hapo. Huduma hiyo imezinduliwa kituoni hapo na kwamba itapatikana kwenye vituo vyote vya Total nchi nzima ikiwa ni mwendelezo wa Vodacom kuwawezesaha watanzania kupata huduma kwa urahisi, uhakika na usalama kupitia huduma ya M-pesa.
Mfanyakazi wa kituo cha mafuta cha Total Morocco jijini Dar es salaam akitoa huduma ya mafuta kwa wateja. Total na Vodacom imezindua ubia wa kibiashara unaowawezesha wateja kulipia huduma ya mafuta kwa M-pesa kwenye vituo vyote vya Total nchi nzima. Huduma hiyo inalenga kutoa unafuu na urahisi wa malipo kwa wateja.

KATIBU MKUU WIZARA YA MAJI AJIONEA UHARIBIFU MKUBWA WA MABOMBA JANGWANI

$
0
0
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Inj. Bashir Mrindoko leo ametembelea eneo la Jangwani, Darajani, barabara ya Morogoro kujionea uharibifu mkubwa wa mabomba ya maji.

Mabomba hayo ya inchi 16 yenye urefu wa mita 12 yamezolewa na maji kutokana na athari iliyoletwa na mvua kubwa ya mwishoni mwa wiki inayoendelea jijini Dar es Salaam.

“Ni athari kubwa ambayo imesababishwa na mvua hii na mpaka kukata mabomba ya maji, ni muda mrefu tangu mvua ya aina huu kutokea Dar es Salaam”, alisema Inj. Mrindoko.

“Nimekuja kuangalia hali halisi na kuona namna gani tutafanya kufanya ukarabati wa mabomba haya, ili kurudisha huduma ya maji kwa maeneo yaliyoathirika baada ya tukio hili. Tumefanya tathmini na kuona nini cha kufanya na utekelezaji utaanza mara moja”, aliongeza Inj. Mrindoko.

Uharibifu huu umeleta athari kwa maeneo ya Muhimbili, TBL, Mchikichini, Upanga na Kariakoo na katikati ya Jiji kukosa maji.

Maeneo mengine yaliyoathirika ni Mtoni kwenye mtambo wa maji, ambapo pampu za kusukuma maji kwenye chanzo cha maji zimefunikwa na maji.

Pia, Mtambo wa Ruvu Juu, Mlandizi kipande cha bomba la inchi 4 la kupoza pampu za maji ghafi cha urefu wa mita 18 kimekatika.

Hii imesababisha maeneo ya Temeke, Tandika, Mtoni, Kurasini, Wailes na Mbagala wanaohudumiwa na mtambo huo kukosa huduma, kutokana na uzalishaji kusimama.

Vile vile, mfumo wa kupooza pampu za kusukuma maji ghafi kuathirika hivyo kukosekana kwa uzalishaji tangu jana saa 11.30 jioni.

Katika ziara hiyo Katibu Mkuu aliongozana na Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASCO, Jackson Midala, Inj. Pascal Hamuli wa Wizara ya Maji na wataalamu wengine kutoka DAWASA na kampuni za Uhandisi.
Mabomba yaliathirika baada ya mvua kubwa iliyonyesha mwishoni mwa wiki eneo la Jangwani.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Inj. Bashir Mrindoko (wa pili kulia) akiwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASCO, Jackson Midala (wa kwanza kushoto) walipotembelea eneo la Jangwani kkuangaliaa mabomba yalioathirika na mvua.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Inj. Bashir Mrindoko akipata maelekezo kutoka kwa Mhandisi ya namna ya kukarabati mabomba yaliyokatika eneo la Jangwani.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Inj. Bashir Mrindoko akiwa katika masikitiko makubwa mara baada ya kujionea athari kubwa ya kukatika kwa mabomba iliyotokea Jangwani baada ya mvua kubwa zinazonyesha jijini Dar es Salaam.

KUTOKA BUNGENI MJINI DODOMA LEO

$
0
0
Waziri Mkuu,Mizengo Pinda akizungumza na Waziri wa Nchi Katika Idara ya Nishati na Mabadiliko ya Tabia Nchi wa Uingereza, Mhe. Gregory Baker (Minister of State at the Department of Energy and Climate Change), Ofisini kwake, Bungeni Mjini Dodoma Aprili 14, 2014.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka katika kikao cha Bunge Maalum la Katiba Mjini Dodoma,Aprili 15, 2014.
Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt, Seif Rashid (kushoto) na Mwanasheria Mkuu wa Serikali wa Zamani, Andrew Chenge (katikati) wakiteta kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma Aprili 15, 2014.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na watoto wa Waziri Mkuu wa Zamani, Hayati Rashidi Mfaume Kawawa, Vita (katikati) na Zamaradi (kulia) kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma Aprili 15, 2014. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Wajumbe wa Bunge la Katiba wakiwa wamehamishia mjadala nje wakati Bunge maalum likiendelea ndani.kutoka kulia ni Mhe.Haji K.Kai,Haroub Shamis,Khatibu S.HAJI,S.Khamis Faki na Abdallah J.Hassan. 
Wajumbe wa Bunge la Katiba Mhe. Ester Bulaya kushoto akijadiliana jambo na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe. Anna Makinda.
Wajumbe wa Bunge la Katiba,Waziri wa Mambo ya Ndani, Mhe.Mathias Chikawe akibadilishana mawazo na Naibu Waziri wa Sheria na Katiba,Mhe. Mhe Angellah Kairuki.
Naibu Katibu wa Bunge Maalium la Katiba,Dkt. Thomas Kashilila kushoto akijadiliana jambo na Mbunge wa Mpanda Mjini ambaye pia ni Mbunge wa Bunge Maalum la Katiba,Mhe. Said Arfi.
Mhe.Stephen Wasira kulia ambaye alikuwa Mwenyekiti wa Kamati namba sita akiwa na msemaji wa walio wachache katika kamati yake Mhe Ismail Jussa (wapili kulia) wakijadiliana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,Mhe. Bernard Membe na Naibu Waziri wa Mawasiliano,Sayansi na Teknolojia Mhe. January Makamba.Picha na Deusdedit Moshi,Globu ya Jamii.

FAMILIA KITCHEN PART GALA 2014 ILIVYOFANA MJINI DODOMA

$
0
0
Mwanamuziki maarufu hapa nchini Shilole akitumbuiza wanawake katika onesho maalum alilo lifanya katika FAMILIA KITCHEN PART GALA 2014 ambapo zaidi ya wanawake 300 walijumuika katika jukwaa na kuhamasika kushiriki katika zoezi la upimaji afya zao ikiwemo ukimwi na saratani ya shingo ya kizazi.
Mwanamuziki maarufu hapa nchini Shilole akitumbuiza wanawake katika onesho maalum alilo lifanya katika FAMILIA KITCHEN PART GALA 2014 ambapo zaidi ya wanawake 300 walijumuika katika jukwaa na kuhamasika kushiriki katika zoezi la upimaji afya zao ikiwemo ukimwi na saratani ya shingo ya kizazi.
Mwazirishi wa jukwaa la FAMILIA KITCHEN PARTY GALA 2014 bi Vida Mndolwa (katikati) akizungumza jambo na wanawake waliohudhulia jukwaa hilo hawapo pichani (kushoto) ni meneja wa uzazi wa mpango shirika la PSI Tanzania bi Catherine Paul (kulia) aliye kuwa mshehereshaji katika jukwaa hilo.
Baadhi ya wanawake waliojitokeza kwa wingi katika jukwaa la FAMILIA KITCHEN PARTY ambalo limefanyika mjini Dodama katika ukumbi wa kilimani, wanawake zaidi ya 300 walijumuika katika jukwaa na kuhamasika kushiriki katika zoezi la upimaji afya zao ikiwemo ukimwi na saratani ya shingo ya kizazi.
Meneja wa uzazi wa mpango shirika linalojighulisha na masuala ya afya Catherine Mndolwa akihojiwa na waandishi wa habari katika jukwaa la FAMILIA KITCHEN PARTY GALA 2014 lililo fanyika katika ukumbi wa Kilimani mjini Dodoma wanawake zaidi ya 300 walijumuika katika jukwaa na kuhamasika kushiriki katika zoezi la upimaji afya zao ikiwemo ukimwi na saratani ya shingo ya kizazi. PICHA NA IPSHA MEADIA.

SERENA HOTEL YAKABIDHI MSAADA WA VYANDARUA NA MAJI KWA JWTZ KWAAJILI YA WAATHIRIKA WA VITA DARFUR

$
0
0
Mkurugenzi wa masoko wa Hoteli ya Dar es Salaam Serena,Bw. Seraphin Lusala akimkabidhi vyandarua kwa Mkuu wa Tiba wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ),Meja Jenerali AS Mwabulanga wakati wa hafla fupi ya kukabidhi misaada ya vyandarua na maji,vitakavyokabidhiwa kwa waathirika wa vita huko Darfur ambapo misaada hiyo itatolewa na Jeshi letu la kulinda amani huko Darfur,ikiwa ni katika kusherehekea sikukuu ya Muungano wa Tanzania.Kushoto anayeshuhudia ni Mkurugenzi wa Operesheni za Ulinzi wa Amani, Brigedia Jenerali, HS Kamunde.
Mkurugenzi wa masoko wa Hoteli ya Dar es Salaam Serena,Bw. Seraphin Lusala akimkabidhi katoni za maji Mkuu wa Tiba wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ),Meja Jenerali AS Mwabulanga.
Picha ya pamoja baada ya hafla hiyo,mstari wa mbele kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Operesheni za Ulinzi wa Amani, Brigedia Jenerali, HS Kamunde,Meneja wa masoko kutoka Hoteli ya Dar es Salaam Serena, Bi Jackie Namatovu, Mkuu wa Tiba wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ),Meja Jenerali AS Mwabulanga, Mkurugenzi wa masoko wa Hoteli ya Dar es Salaam Serena,Bw. Seraphin Lusala, Afisa Mnadhimu wa Logistiki za Ulinzi wa Amani,Lt. Kanali DC Kakoko na wa mwisho ni Shaban Kaluse Meneja masoko wa Hoteli ya Dar es Salaam Serena.

NMB YATOA MADAWATI MJINI ZANZIBAR

$
0
0
Bw. Jaha Khamis Saidi, Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Kitope akimshukuru Kaimu Meneja wa tawi la NMB Zanzibar, Bakar Mohamed baada ya kupokea madawati kutoka benki ya NMB. Msaada huo wa madawati ulikabidhiwa kutoka NMB kwa shule ya msingi Kitope ili kupunguza uhaba wa madawati unaoikumba shule hiyo.
Wanafunzi wa shule ya msingi Kitope mjini Zanzibar wakiwa wamekaa kwenye madawati yaliyotolewa na Benki ya NMB kwa ajili ya kupunguza uhaba wa madawati unaoikabili shule ya msingi Kitope . Jumla ya madawati (50) hamsini yamekabidhiwa hivi karibuni katika shule hiyo.

Tume ya Haki za Binadamu na Utwala Bora yazindua taarifa ya ukaguzi wa vyombo vya dola dhidi ya watoto

$
0
0
Mgeni rasmi, Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali George Masaju akitoa hotuba ya uzinduzi wa taarifa ya ukaguzi wa Magereza na sehemu walimozuiliwa watoto pamija na nyezo za ufuatiliaji wa hali na haki za watoto hao, hafla hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Ofisi za Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora zilizo mtaa wa Luthuli leo jijini Dar es salaam.
Mgeni rasmi, Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali George Masaju (wa pili kushoto) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa taarifa ya ukaguzi wa Magereza na sehemu walimozuiliwa watoto pamoja na nyezo za ufuatiliaji wa hali na haki za watoto hao leo jijini Dar es salaam, hafla hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Ofisi za Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora. Wa kwanza kushoto ni Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Katibu Mtendaji wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (wa kwanza kulia) na wa pili kulia ni mwakilishi wa UNICEF nchini na Mkuu wa Idara ya kutetea Haki za Watoto Birgithe Lund-Henriksen.
Pix No.03. Mgeni rasmi, Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali George Masaju (katikati) akionesha taarifa ya ukaguzi wa Magereza na sehemu walimozuiliwa watoto pamoja na nyezo za ufuatiliaji wa hali na haki za watoto mara baada ya uzinduzi huo leo jijini Dar es salaam, hafla hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Ofisi za Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora. Wa kwanza kushoto ni Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Amiri Manento na wa pili kulia ni mwakilishi wa UNICEF nchini na Mkuu wa Idara ya kutetea Haki za Watoto Birgithe Lund-Henriksen.
Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Amiri Manento (kushoto) akitoa neno kabla ya kumkaribisha Mgeni rasmi, Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali George Masaju (kulia) juu ya taarifa ya ukaguzi wa magereza, vituo vya polisi, mahabusi za watoto na shule ya maadilisho.
Kamishna Msaidizi wa Magereza makao makuu (ACP) George Mwambashi akitoa ufafanuzi juu ya namna magereza zilivyotenganisha selo za watoto na za watu wazima nchini.
Picha ya pamoja ya wajumbe waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa taarifa ya ukaguzi wa Magereza na sehemu walimozuiliwa watoto pamoja na nyezo za ufuatiliaji wa hali na haki za watoto hao katika ukumbi wa Ofisi za Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora zilizo mtaa wa Luthuli leo jijini Dar (Picha zote na Eleuteri Mangi- Maelezo)

RAIS KIKWETE AFUNGUA MKUTANO WA WADAU WA UKANDA WA KATI JIJINI DAR LEO

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete, akifurahia jambo wakati akitoa hotuba yake katika mkutano wa Wadau wa Ukanda wa kati(alignment meeting on central corridor), alioufungua leo mchana katika ukumbi wa Mwl. Julius Nyerere. Mkutano huo wa wadau ni sehemu ya utekelezaji wa maamuzi ya Mkutano wa Jukwaa la Kiuchumi Duniani (World Economic Forum) iliofanyika Davos Uswiss Mwezi Januari 2014.
Waziri wa Uchukuzi, Dkt. Harrison Mwakyembe, akitoa hotuba kabla ya kumkaribisha kufungua mkutano wadau wa Ukanda wa kati (alignment meeting on central corridor), uliofanyika leo mchana katika ukumbi wa Mwl. Julius Nyerere. Kulia kwa Waziri Mwakyembe ni Mkurugenzi wa Jukwa la Kiuchumi Duniani kwa upande wa Afrika, Bi. Elsie Kanza.
Sehemu ya washiriki wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dkt. Shaaban Mwinjaka wakati akiwasilisha mada katika mkutano wa wadau wa Ukanda wa kati (alignment meeting on central corridor), uliofanyika leo mchana katika ukumbi wa Mwl. Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete, akimwambia jambo Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Bw. Richard Sezibera, wakati wa mkutano wa Wadau wa Ukanda wa kati (ALIGNMENT MEETING ON CENTRAL CORRIDOR), uliofanyika leo mchana katika ukumbi wa Mwl. Julius Nyerere. Mkutano huo wa wadau ni sehemu ya utekelezaji wa maamuzi ya Mkutano wa Jukwaa la Kiuchumi Duniani(World Economic Forum) iliofanyika Davos Uswis Mwezi Januari 2014.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dkt. Shaaban Mwinjaka akiwasilisha mada ya fursa ya uwekezaji katika Ukanda wa kati, katika mkutano uliowakutanisha Wadau wa Ukanda wa kati(alignment meeting on central corridor), uliofanyika leo mchana katika ukumbi wa Mwl. Julius Nyerere,jijini Dar es Salaam. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete (wa sita kutoka kulia), akiwa katika picha ya pamoja na Wahisani wa maendeleo, na waadau wa mkutano wa Wadau wa Ukanda wa kati wa(alignment meeting on central corridor), uliofanyika leo mchana katika ukumbi wa Mwl. Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. Mkutano huo wa wadau ni sehemu ya utekelezaji wa maamuzi ya Mkutano wa Jukwaa la Kiuchumi Duniani (World Economic Forum) iliofanyika Davos Uswiss Mwezi Januari 2014, ambao ulichagua Ukanda wa kati kuwa mradi wa majaribio ya kuwezesha uwekezaji kwa njia ya ubia(PPP).(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Uchukuzi)

DK. MAGUFULI ASIMAMIA URUDISHWAJI HUDUMA DARAJ LA MTO MZINGA, KONGOWE

$
0
0
Maelfu ya abiria waliotarajia kusafiri kwenda mikoa ya Kusini (Lindi na Mtwara walishindwa kufanya hivyo baada ya daraja la Mto Mzinga lililopo eneo la Kongowe, jijini Dar es Salaam, kubomoka na kusombwa na mafuriko kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha jijini Dar es Salaam na mikoa ya jirani.

Daraja hilo lilibomoka tarehe 13 Aprili, 2014 majira ya saa 12:00 asubuhi baada ya mabasi matatu kuvuka.

Daraja lilibomoka majira ya saa 12:00 na kufanya msururu wa mabasi yaendayo mikoa ya Kusini kushindwa kufanya safari zake na hata watembea kwa miguu hawakuweza kupita.

Kutokana na daraja hilo kubomoka, watu walioko upande wa Kongowe na Mbagala hawakuweza kuvuka kutoka upande mmoja kwenda mwingine.

Msururu wa mabasi ya abiria yanayofanya safari zake kwenda mikoa mikoa ya Lindi na Mtwara ulikuwa mkubwa , mabasi hayo yakiwa na abiria.

Tarehe 14.04.2014 saa nne na nusu usiku Dk.Magufuli alisimamia urudishwaji wa huduma hizo na watembea kwa miguu walianza kupita na kisha magari makubwa yalifuatia.

Michauno ya Heineken foosball yazidi kufana jijini Dar

$
0
0
Wachezaji wanaochuana katoka Michuano ya Heineken foosball inayoendelea katika sehemu mbalimbali za burudani jijini Dar,wakishindana katika moja ya michezo yao iliyofanyika jana katika kiota cha Maisha Club.Zidi kutembelea blog ilikupata taarifa zaidi.
Mwakilishi wa kampuni ya Heineken Tanzania, Muhana Kibuta akimkabidhi kapteni wa timu Mancity zawadi baada yakushinda michuano ya foosball pale Maisha Club. Washindi hao pia wameingia robo finali ya kuwania nafasi ya kwenda Ibiza Spain kuangalia fainali za ligi ya mabigwa ulaya UEFA champions league.

Article 14

Tanzania tops Africa with first declaration of Seven Natural Wonders

$
0
0
The Seven Natural Wonders of Africa were declared in February 2013 and now the Seven Natural Wonders of Tanzania join the official list of wonders from around the world.

Tanzania, with Mount Kilimanjaro, Ngorongoro Crater, and the Serengeti Migration, is home to three of Africa’s seven wonders. Tanzania Tourist Board shared, “We are excited that three of Africa’s natural wonders are in Tanzania. The entire country is honored to be Home to these icons.”
Tanzania now has the distinction and honor to be the first African country to declare the winners for the country’s Seven Natural Wonders. As would be expected, the big three from Africa’s list top the winners. Ms. Devota Mdachi, Director of Marketing, Tanzania Tourist Board stated, “To have three of Africa’s seven and to now be the first African country to declare its seven natural wonders, will definitely place Tanzania on the World Tourist Map.”
Reaching the final four was a close race between several wonder candidates from throughout Tanzania. Tanzania is a beautiful country from border to border with an array of encounters with nature that would make any country envious. Ms. Mdachi added, “It was a thrill to watch the various Tanzanian wonders compete for the distinction of being one of the seven. The world will now get a taste of Tanzania’s natural splendor.”
The initial wonders were vetted and voted on by the Declaration Committee and the voting body of conservation experts for Seven Natural Wonders. A campaign, which started in 2008, was enhanced with collaboration from the Tanzania Tourism Board, Tanzania National Parks and Ngorongoro Conservation Area Authority, who together championed voting throughout Tanzania and by leveraging the international voice through visitors to the various national parks and Ngorongoro Crater.

KAPOTIVE STAR SINGERS-BUKOBA KUFANYA TAMASHA LA PASAKA LINA'S CLUB, PASAKA PILI NI KATIKA MJI WA BIHARAMULO

$
0
0
Kikundi mahiri cha KAPOTIVE Star Singers- Bukoba,Wanayo furaha kuwatangazia kuwa kwa mapenzi ya Mungu, Tar. 20/04/2014 sikukuu ya Pasaka watakuwa na tamasha la Pasaka LINA’S CLUB -Bukoba, kuanzia saa 9 mchana hadi 2 usiku na kesho yake tar. 21/04/2014 Watakuwa katika mji wa Biharamulo. 

 Mratibu wa Tamasha hilo Bw. Andrew Kagya amesema kuwa Mwimbaji mgeni (Guest singer) atakuwa Flora Mbasha na kundi lake zima kutoka jijini Dar es Salaam na pia Kutakuwepo kwaya mbalimbali za RC, KKKT na SDA za hapa Bukoba.Kiingilio kitakuwa kama ifuatavyo:Mtu mmoja 10,000/-
Watu watatu  25,000/-,  Watoto 5,000/-
Kutokana na udhamini wa kinywaji maridadi cha Climax Non-Alcoholic Herbal drink, kila atakayenunua ticket ya 10,000, atapewa kinywaji kimoja cha Climax mlangoni, na atakayenunua ticket ya 25,000 atapewa CD moja mpya ya KAPOTIVE Star Singers (Zawadi ya Pasaka) na vinywaji vitatu vya Climax bure. Karibuni tusherekee ufufuko wa Bwana wetu Yesu Kristu kwa nyimbo na shangwe.Baadhi ya waimbaji wa Kapotive Star wakiimba kwenye matamasha yao yaliyopitaKazaliwa!! Njoo mumuone!!

Mhe. Asha Bakari Makame kwa umahiri wake wa kupinga udhalilishaji wa kijinsia katika bunge la katiba

$
0
0
 Keki Maalum  ambayo imeandaliwa na baadhi ya Wajumbe Wanawake wa Bunge Maalum la Katiba kumpongeza Mjumbe wa Bunge hilo Mh. Asha Bakari Makame kwa umahiri wake wa kupinga udhalilishaji wa kijinsia ndani ya Bunge hilo.
 Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Mh. Asha Bakari Makame akitoa shukrani zake kwenye hafla fupi ya Kupongezwa kutokana na kutetea jinsia ya Wanawake ndani ya Bunge la Katiba.
  Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Mh. Asha Bakari Makame akikata Keki Maalum kuashiria uzinduzi wa hafla fupi ya kupongezwa kwake kutokana na msimamo wake ndani ya Bunge Maalum la Katiba linaloendelea Mjini Dodoma.Kushoto yake ni Waziri wa Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, Maendeleo ya Vijana wanawake na Watoto Mh. Zainab Omar Mohammed.
 Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Mh. Asha Bakari akimlisha Keki Mjumbe mwenzake wa Bunge hilo Mh. Zainab Omar Mohammed kwenye hafla fupi ya kupongezwa kwake.
Mbunge wa Bunge Maalum la Katiba Mh. Waride Bakari Jabu akitoa neno la shukrani kwenye hafla fupi ya Kupongezwa Mjumbe mwenzake Mh. Asha Bakari Makame kwa  msimamo wake ndani ya Bunge hilo.

introducing Natty E Ft Zedy Song HAinaga Noma

KATIBU MKUU WA CCM,KINANA ATEMBELEA MIRADI MBALIMBALI WILAYA MPYA YA MLELE MKOANI KATAVI LEO

$
0
0

Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelezo mafupi kutoka kwa Afisa Zana za Kilimo wa Wilaya ya Mlele,Lawlence Elias kuhusiana na Mradi wa Mashine ya Kusindika Mpunga mapema leo jioni,katika kijiji cha Mwampuli,Wilaya mpya ya Mlele mkoani Katavi,Mashine hiyo ina uwezo wa kusindika mpunga tani 30 kwa siku.Kushoto ni Mjumbe wa NEC Taifa,Balozi Ali Karume nae akisikiliza kwa makini.Kinana yupo Mkoani Katavi kwa ziara ya siku nne ya kuimarisha uhai wa chama,kukagua na kuhimiza ilani ya Uchaguzi ya 2010.
Mradi wa Mashine ya Kusindika Mpunga kama uonekavyo pichani uliopo katika kijiji cha Mwampuli,Wilaya mpya ya Mlele mkoani Katavi,Mashine hiyo ina uwezo wa kusindika mpunga tani 30 kwa siku.
Katibu Mkuu wa CCM,akikagua Ujenzi wa Mradi wa Maji safi,katika kijiji cha Kibaoni,Wilaya ya Mlele,mkoani Katavi.Tanki hilo la maji safi linatarajia kuhudumia wakazi wa kijiji cha Kibaoni na vijiji vingine tisa.

Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana wa tatu kulia akishiriki kukusanya mawe pamoja na viongozi mbalimbali wa Taifa,Mkoa na Wilaya (CCM),kukusanya mawe kwa ajili ya mradi wa ujenzi wa shule ya msingi Maji Moto iliyopo katika kijiji cha Maji Moto,Wilaya mpya ya Mlele mkoani Katavi
Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye akiwahutubia wakazi wa kijiji cha Maji Moto jioni ya leo kwenye mkutano wa hadhara,Nape amewataka wana CCM na wananchi kwa ujumla kuishi kwa amani na upendo katika suala zima la kudumisha amani tulionayo na kuwapuuza wanaotaka kuleta mgawanyiko katika nchi yetu kwa namna moja ama nyingine.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiwahutubia wakazi wa kijiji cha Maji Moto jioni ya leo kwenye mkutano wa hadhara,Kinana ameeleza kuwa kumekuwepo tatizo kubwa kila mahali aendapo kufanya ziara kuhusiana na migogoro ya ardhi kati ya Wakulima na Wafugaji,Wafugaji na Hifadhi ,jambo ambalo linapaswa kufanyiwa kazi kwa umakini mkubwa ,aliongeza kuwa migogoro hiyo imekuwa janga la Taifa,kutokana na idadi ya watu kuongezeka katika maeneo mengi,huku mipaka yake kubaki kama ilivyo kwa muda mrefu.
Kinana akijaribu kuelewesha jambo katika shamba la Ufugaji nyuki la Waziri Mkuu Pinda,katika kijiji cha Kibaoni Wilaya ya Mlele mkoani Katavi mapema leo mchana
Kinana akikatiza kwenye Shamba la Ufuta na Nyuki mara baada ya kujionea ufugaji wa nyuki unavyofanyika.

Twanga Pepeta kupamba utambulisho Miss Tabata SIKU YA Pasaka

$
0
0
 Bendi ya African Stars “Twanga Pepeta” itasindikiza uzinduzi wa Redds Miss Tabata itakayofanyika Jumapili ya Pasaka katika ukumbi wa Da’ West Park, Tabata.
Mratibu wa shindano hilo Joseph Kapinga amesema bendi hiyo itatambulisha nyimbo zao mpya kama zawadi yao ya Pasaka kwa wapenzi wao.
Pia bendi hiyo ijulikanayo kama Wakali wa Kisigino pia watapiga nyimbo zao zote kali hadi majogoo.
Mratibu huyo wa Bob Entertainment na Keen Arts alisema kuwa wapenzi wa urembo watapata fursa ya kuwaona warembo hao siku hiyo kabla hawajashiriki kwenye shindano la Miss Tabata ambalo limepangwa kufanyika mwishoni mwa mwezi ujao.
Katika uzinduzi huo warembo wa Tabata watasindikizwa na washiriki wenzao wa Miss Mzizima na Miss Ukonga.
Pia watakuwepo viongozi waandamizi kutoka kamati ya Miss Tanzania ikiongozwa na Hashim Lundenga na Redds Miss Tanzania Happiness Watimanywa.
Warembo 21 wanaendelea na mazoezi ya Miss Tabata katika ukumbi wa Da West Park chini ya wakufunzi wawili -  Neema Chaki na Pasilida Bandari.
Warembo hao ni Esther Frank Kiwambo (20), Jemima Huruma Mawole (22), Badra S. Karuta (20), Mercy Mathias Kazula (19), Lydia Charles (22), Agnes Tarimo (18), Agnes Alex (20), Catrina Lawrence Idfonsi (20), Nuru Omary Athumani (19) na Happyclarrice Wilson Mbahi (19).
Wenine ni Annatolia Raphael (21), Mary Henry (21),  Evodia Peter (22), Fatma Hussein Ismail (20),  Ester Wilson Mbayi (20), Ambasia Lucy Mally (22), Faudhia Hamisi (21), Najma Charles Mareges (19), Lightnes Olomi (18), Husna Ibrahim (19) na Ramta Mkadara (20).
Warembo watano kutoka Tabata watashiriki kwenye shindano la kanda ya Ilala, Miss Ilala baadaye mwaka huu.
Mrembo anayeshikilia taji la Miss Tabata ni  Dorice Mollel ambaye pia ni Redds Miss Ilala.

Homa ya kidinga popo yasambaa Tanzania, mmoja athibitika kufariki

$
0
0
Mbu anayeambukiza kidinga popo

Nchini Tanzania watu 147 wamethibitika kuwambukizwa ugonjwa wa homa ya kidinga popo yaani homa ya dengu huku mtu mmoja akiripotiwa kufariki dunia kwa ugonjwa huo.
Kasi ya ugonjwa huo ambao ikiwa hautadhibitiwa unaweza kuleta madhara dalili zake zinashabihiana na zile za malaria kwani unaambukizwa kwa kupitia mbu na unadaiwa kusambaa katika maeneo mengine nchini Tanzania ingawa kwa sasa uko zaidi mjini Dare salaam.
Taarifa zinasema kuwa kuna visa vya wagonjwa nchi jirani ya Msumbiji taifa linalopakana na mkoa wa Mtwara jambo linalozua wasiwasi wa kuwa na visa vingine mkoani humo. Kutaka kufahamu hatua zinazochukuliwa na serikali ya Tanzania Joseph Msami amezungumza na Dk Janet Mgamba ni kaimu mkurugenzi msaidizi wa udhibiti na ufuatailiaji wa magonjwa ya milipuko ambaye anaanza kwa kueleza hali ya kidinga popo ilivyo.

(SAUTI MAHOJIANO)
KUSIKILIZA BONYEZA HAPA
Viewing all 110173 articles
Browse latest View live




Latest Images