Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110078 articles
Browse latest View live

KUTOKA BUNGE LA KATIBA MJINI DODOMA LEO

$
0
0
Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Iddi (Wapili kushoto) wakifurahia jambo katika mazungumzo na Spika wa Baraza la Wawakilishi, Pandu Kificho (wapili kulia) na Haidar Madeweyya .
Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba Mohamed Abood(kushoto) na Stephen Wassira wakibadlishana mawazo leo mjini Dodoma wakati wa kikao cha ishirini na mbili cha Bunge Maalum la Katiba.

Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Dodoma wakiwa Bungeni Mjini Dodoma Aprili 14, 2014 kwa ziara ya kujifunza.
Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba Sophia Simba (kushoto) na James Lembeli (katikati) na Job Ndugai (kulia) wakibadlishana mawazo leo mjini Dodoma wakati wa kikao cha ishirini na mbili cha Bunge Maalum la Katiba.
Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba Philemon Ndessamburo (kushoto) na James Mbatia (kulia) wakibadlishana mawazo leo mjini Dodoma wakati wa kikao cha ishirini na mbili cha Bunge Maalum la Katiba.
Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Samuel Sitta(wa pili kulia) akiongozana na wajumbe wengine wa Bunge hilo kuelekea katika mapumziko mafupi mara baada ya kikao kuharishwa leo mchana mjini Dodoma.
Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba James Mbatia (kushoto), Mohamed Raza( wa pili kushoto) , Profesa Ibrahim Lipumba (wa pili kulia) na Freeman Mbowe(kulia) wakibadlishana mawazo leo mjini Dodoma wakati wa kikao cha ishirini na mbili cha Bunge Maalum la Katiba. Picha na Bunge Maalum la Katiba -Dodoma.

Dk.Shein akutana na Uongozi wa Wizara ya Afya Zanzibar

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi DK.Ali Mohamed Shein (katikati) akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Afya katika utekelezaji wa mpamgo wa kazi wa miezi 9 kutoka Julai -Machi 2013/2014,katika ukumbi wa mikutano Ikulu Mjini Unguja leo.
Uongozi wa Wizara ya Afya ukiwa katika kikao cha utekelezaji wa mpamgo wa kazi wa miezi 9 kutoka Julai -Machi 2013/2014,katika ukumbi wa mikutano Ikulu Mjini Unguja leo,chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi DK.Ali Mohamed Shein (katikati).
Baadhi ya Viongozi wa Wizara ya Afya wakiwa katika kikao cha utekelezaji wa mpamgo wa kazi wa miezi 9 kutoka Julai -Machi 2013/2014,katika ukumbi wa mikutano Ikulu Mjini Unguja leo,chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi DK.Ali Mohamed Shein (katikati) [Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.].

Mhe. Kairuki asimikwa kuwa Kamanda wa UVCCM Same

$
0
0
Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana (UVCCM), Ndg. Sixtus Mapunda akimkabidhi Mhe. Angellah Kairuki (MB), Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, nyenzo za vitendea kazi za kimila wakati wa kusimikwa kuwa Kamanda wa UV CCM wa Wilaya ya Same.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana (UVCCM), Ndg. Sixtus Mapunda akimweleza majukumu ya Kamanda wa Vijana Mhe. Angellah Kairuki kabla ya kusimikwa kuwa Kamanda wa UV CCM wa Wilaya ya Same.
Mhe. Kairuki akila kiapo cha Kamanda Mpya wa UVCCM wa Wilaya ya Same wakati wa kusimikwa kwake kuwa kamanda wa umoja hu huku akisikilizwa kwa makini na viongozi wa CCM wa Mkoa wa Kilimanjanro na Wilaya ya Same waliokuwepo katika sherehe hizo.

Mh. Mkapa atembelea shule ya msingi Manyara Ranchi,Wilayani Monduli

$
0
0
Rais mstaafu wa awamu wa tatu Mh Benjamin Mkapa leo(jumatatu) amefanya ziara kumtembelea Shule ya msingi ya Manyara Ranchi inayofadhiliwa na shirika la kimataifa la uhifadhi wa wanyamapori la African wildlife foundation wilayani Monduli.

Mzee Mkapa ni Makamu mwenyekiti wa shirika hilo lenye makao yake mjini Washington Marekani.picha mbalimbali zinamuonesha waziri mkuu mstaafu na mbunge wa Monduli Mh Edward Lowassa akimuongoza Rais Mkapa kuzuru shule hiyo.
Rais mstaafu wa awamu wa tatu,Mh. Benjamin Mkapa (katikati) akimsikiliza kwa makini Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa wakati alipotembelea Shule ya msingi ya Manyara Ranchi inayofadhiliwa na Shirika la Kimataifa la Uhifadhi wa Wanyama pori la African Wildlife Foundation,wilayani Monduli.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akimueleza jambo Rais mstaafu wa awamu wa tatu,Mh. Benjamin Mkapa wakati walipokuwa kwenye moja ya madarasa ya shule hiyo.
Rais mstaafu wa awamu wa tatu,Mh. Benjamin Mkapa akiagana na Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa.

Mashindano ya Heineken foosball yaendelea jijini Dar

$
0
0
Wachezaji wa timu ya Techno wakiongozwa na kapteni wao Geoffrey Dominic (kulia) na Augustine Alex wakishangilia ushindi wao, wakiwa pia na zawadi Kutoka Heineken. Washindi hawa walishinda michuano ya foosball pale Kisuma Temeke. Washindi hao wameingia robo finali ya kuwania nafasi ya kwenda Ibiza Spain kuangalia fainali za ligi ya mabigwa ulaya UEFA champions league.
Mtanange ukiendelea.
Mwakilishi wa kampuni inayoratibu mecho wa foosball kwa naiba ya Heineken Tanzania, Jack Juma akimkabidhi kapteni wa timu Techno zawadi baada yakushinda michuano ya foosball pale Kisuma Temeke. Washindi hao pia wameingia robo finali ya kuwania nafasi ya kwenda Ibiza Spain kuangalia fainali za ligi ya mabigwa ulaya UEFA champions league.

========  ========   =========
 Entertainment fans are quickly appreciating the recently launched second edition of Heineken foosball tournament being held in various night spots in Dar es Salaam. 

 Speaking to this blog over the weekend winning players who participated in the competition whose main aim is to engage consumers to experience foosball and the UEFA champions’ league, they said that they are very happy with winning a chance to land the grand prize which is a trip to Ibiza, Spain.

 “This is the first time I have ever played such a game, at first I feared we’ll be knocked of the competition but pressed on, and now I have chance for the finals, this is very important for us, said Mr. Geoffrey Dominic who together with his partner Augustine emerged winners at Kisuma, Temeke. 

 I am very glad that we proved and showed the other teams our scoring skills. We were confident of winning, played our best and emerged winners,” said Mr. Jack Rota who is captian of team Mancity which won at Maisha club. All the winning teams gotten so far will proceed to the quarter finals to be played later this month. 

 Heineken on their part said that the 16 final teams will get a chance to battle it out for the grand prize at Club 777 in Mikocheni Dar es salaam. They also added that in addition to winners being flown to Ibiza, Spain, the owner of the Winners’ outlet will receive a whopping $10,000 worth of investment from Heineken. 

 The owner of the outlet from which the winning foosball team emerges will accompany his two customers to the ultimate Heineken® live screening of the UEFA Champions League finals on Ibiza. The semi-finals and finals will be staged at Club 777 where 16 teams will represent ‘their’ bar.

 The winners of this stage will go on to compete at the Heineken® Foosball Tournament finals which will be held on 26th Heineken® will fly the ultimate foosball champions to the legendary island of Ibiza. 

This is where they will experience the ultimate Heineken® live screening of the UEFA Champions League finals. Prize winners and VIPs from across the world will join together to celebrate a night of legendary football at this world-class Heineken® experience. of April.

KUTOKA TFF LEO

HATUTOWAVUMILIA WANAOENDEKEZA VITENDO VYA URASIMU NA UMANGIMEZA WA KUTUMIA MAKARATASI OFISINI-KINANA

$
0
0
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiwahutubia wakazi wa kijiji cha Kapalamsenga,wilayani Mpanda mkoani Katavi jioni ya leo,katika mkutano wa hadhara,Kinana alijikuta akigeuka mbogo na kuwaomba radhi wakazi wa kata ya Kirema, Ikola na Kapalamsenga,wilayani Mpanda mkoani Katavi, baada ya kubaini kuwa,kumekuwepo na kutowajibika kwa baadhi ya watendaji wa Serikali.Kinana amesema chama chake kamwe hakitowavumilia watendaji wanaoendekeza vitendo vya urasimu na umangimeza wa kutumia makaratasi ofisini badala ya kuwatumikia wananchi kwa kuwajibika ipasavyo.Kinana na Msafara wake wako mkoani Katavi kwa ziara ya siku nne ya kuimarisha uhai wa chama,kutekeleza na kuhimiza ilani ya uchaguzi ya chama hicho
 Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye akiwahutubia wakazi wa kijiji cha Kapalamsenga,wilayani Mpanda mkoani Katavi jioni ya leo.
Baadhi ya Wananchi wa kijiji cha Ikola,kilichopo pembezeni mwa Ziwa Tanganyika,Wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi,wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahaman Kinana alipozungumza nao kabla ya kukagua mradi mkubwa wa soko la Samaki (Mwalo),ambao imeelezwa kuwa utapunguza umaskini kwa kiasi kikubwa kwa baadhi ya wakazi wa eneo hilo. Hata hivyo imeelezwa kuwa mradi huo wa soko na kuhifadhia samaki umechelewa kukamilika na kupitisha miaka miwili ya zaidi ya muda ulipangwa kwenye mkataba,Kinana amewahidi Wananchi kulifuatilia tatizo hilo na kuhakikisha mradi huo unakamilika kama ilivyoahidiwa.
 Mmoja wa wakazi wa kijiji cha Ikola,kilichopo pembezeni mwa Ziwa Tanganyika,Wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi,akiuliza swali la zahanati na ,Elimu na Barabara kwa Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahaman Kinana (pichani kulia),alipozungumza nao kabla ya kukagua mradi mkubwa wa Samaki (Mwalo). 
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akishirikii ujenzi wa mradi wa soko la samaki (Mwalo),katika kijiji cha Ikola,kilichopo pembezeni mwa Ziwa Tanganyika,Wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi,
Mbunge wa Mpanda Vijijini, Moshi Kakoso, akijibu na kutoa taarifa  mbalimbali kuhusiana na jimbo lake katika suala zima la kutekeleza na kuhumiza Ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010,mbele ya wakazi wa kijiji cha Kapalamsenga,wilayani Mpanda mkoani Katavi jioni ya leo.


MAMA SALMA AZINDUA RASMI UCHUNGUZI WA SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI HUKO BAHI - MKOANI DODOMA.

$
0
0
 Rais Mama Salma Kikwete akiwahutubia mamia ya wananchi wa wilaya ya Bahi muda mfupi kabla ya kuzindua rasmi kampeni ya upimaji wa saratani ya shingo ya kizazi kwa wanawake katika wilaya ya Bahi mkoani Dodoma
 Mwenyekiti wa WAMA, Mama Salma Kikwete akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa kampeni ya kutokomeza saratani ya shingo ya kizazi kwa wanawake wa Wilaya ya Bah
 Mama Salma Kikwete akionyesha vifaa mbalimbali vinavyotumika na madaktari wakati wa kuwapima wanawake ili kufahamu kama wana maambukizi ya saratani ya shingo ya kizazi wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo wilayani Bahi 
 Mama Salma Kikwete akijumuika na wacheza ngoma na wananchi mbalimbali wa wilaya ya Bahi mara baada ya kuzindua rasmi upimaji wa saratani ya shingo ya kizazi kwa akinamama.

mabingwa wa vodacom premier league 2014 AZAM FC WAPOKELEWA KWA SHANGWE JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0


Mapokezi Azam Fc1
Basi lililowabeba wachezaji wa Azam. Baada ya kuweka rekodi mpya ya kutwaa taji la ligi ya mabingwa Tanzania bara, wanalambalamba wa Azam wametua leo katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu JK Nyerere na kulakiwa kwa shangwe na mamia ya mashabiki na wapenzi wa timu hiyo.
Azam wapokelewa uwanja wa ndege    Mapokezi Azam Fc2 Mapokezi Azam Fc

JK RAIS KIKWETE AMLILIA MAALIM GURUMO, ATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI

$
0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia salamu za rambirambi Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mheshimiwa Dkt. Fenella Mukangara kufuatia kifo cha mwanamuziki maarufu na wa siku nyingi, Muhidini Maalim Gurumo kilichotokea tarehe 14 Aprili, 2014 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) alikokuwa amelazwa kwa matibabu ya ugonjwa wa moyo uliomsumbua kwa muda mrefu.
“Nimesikitishwa na kuhuzunishwa na taarifa za kifo cha Muhidini Maalim Gurumo ambaye alikuwa mmoja wa wasanii wa muziki wa dansi nchini waliolitumikia Taifa hili kwa bidii tangu miaka ya sitini kupitia sanaa ya muziki katika bendi mbalimbali za muziki wa dansi kuanzia Bendi ya NUTA Jazz, Mlimani Park Orchestra, Orchestra Safari Sound (OSS) na Msondo Ngoma ambayo ameitumikia hadi alipostaafu mwaka 2013”, amesema Rais Kikwete katika Salamu zake.
 
Rais Kikwete amesema mchango wa Marehemu Muhidini Maalim Gurumo kwa Taifa letu ni mkubwa na wa kupigiwa mfano kupitia kipaji alichojaaliwa na Mwenyezi Mungu ambacho alikitumia kikamilifu kwa manufaa ya wananchi wa nchi yetu na Taifa kwa ujumla.

Rais Kikwete amemuomba Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kumfikishia Salamu zake za Rambirambi na pole nyingi kwa familia ya Marehemu Muhidini Maalim Gurumo kwa kumpoteza kiongozi na mhimili wa familia yao.  Amesema binafsi anaungana na familia ya marehemu kuomboleza msiba huu mkubwa kwa kutambua kuwa msiba wao ni wa wote, na anamuomba Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema aipokee na kuilaza mahala pema peponi Roho ya Marehemu, Amina.

Aidha Rais Kikwete amewaomba wanafamilia ya marehemu kuwa na moyo wa uvumilivu na subira katika kipindi hiki kigumu cha kuomboleza msiba wa mpendwa wao kwa kutambua kwamba yote ni mapenzi yake Mola.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.

14 Aprili, 2014

Usiku wa Mwambao Asilia Aprili 19

$
0
0
Na Andrew Chale
KUNDI la Dar Modern Taarab na Nadd Ikhwan (Malindi), wanatarajiwa kutoa burudani ya aina yake katika onesho maalumu la ‘Usiku wa Mwambao Asilia’, ndani ya ukumbi wa Travertine, Magomeni jijini Dar es Salaam, Aprili 19.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Mlezi wa Heshima wa kundi la Dar Modern Taarab, ambaye pia ni Mkurugenzi wa Fabak Fashions, Asia Idarous Khamsin, alisema wadau wa muziki wa taarabu watafurahia usiku huo wa Mwambao Asilia kutoka kwa wanamuziki nguli wa miondoko hiyo hapa nchini na visiwani.
“Usiku wa Mwambao Asilia, utasheheni magwiji wakongwe wa muziki wa taarabu nchini, kutoka kundi la Dar Modern Taarab na Nadd Ikhwan, ambao wataporomosha nyimbo za taarabu asili za zamani na za sasa,” alisema Asia Idarous.
Aliongeza kuwa, pia usiku huo utapambwa na ‘surprise’, ikiwemo watu mbalimbali kupita kwenye zuria jekundu ‘red carpet’ na kupiga picha za ukumbusho na mastaa watakaohudhuria usiku huo.
Alisema katika usiku huo, kiingilio kitakuwa ni sh 10,000 ambako tayari tiketi zimeshaanza kuuzwa sehemu mbalimbali.
Asia, alizitaja sehemu hizo kuwa ni pamoja na duka la Fabak Fashions, Regency Park Hotel Mikocheni na Dar Modern Taarab Hall Magomeni Ifunda. Onyesho hilo pia limedhaminiwa na Times FM, Fabak Fashions na www.nakshi255.com

ajali lugalo jijini DAr es salaam leo

$
0
0
 Ajali hii imetokea leo jirani na shule ya sekondari ya Mkongo jijini Dar es salaam

BABU NA MJUKUU WAKE WAFANIKIWA KUINGIA HATUA YA TATU KATIKA SHINDANO LA TANZANIA MOVIE TALENTS

$
0
0
Washiriki wa Shindano la Tanzania Movie Talents ambao ni babu na mjukuu wake kiuhalisia wakipongezana mara baada ya kufanikiwa kuingia hatua ya tatu ya kutafuta washiriki 15 bora na hatimaye kupatikana washindi watatu bora wa kanda ya kati ambapo kila mmoja ataondoka na kitita cha shilingi laki tano za kitanzania.
Mmoja wa washiriki wa shindano la Tanzania Movie Talents akihojiwa na Msanii Joti mara baada ya kufanikiwa kuingia hatua ya tatu hapo kesho huku mjukuu wake pia akifanikiwa kuingia hatua hiyo pia.
Washiriki wa Shindano la kusaka vipaji vya Uigizaji Tanzania lijulikanalo kama Tanzania Movie Talents wakiwa kwenye mazoezi wakati walipokabidhiwa muswada (script) kwa ajili ya kuifanyia mazoezi na kwenda kuonyesha uwezo wao kwa majaji.
Msanii wa Vichekesho Joti akihojiana na Mmoja wa washiriki wa shindano la Tanzania Movie Talents mara baada ya kutoka kwa majaji, shindano limeingia hatua ya pili leo kwa kuchagua washiriki 30 ambao watatafutwa washiriki 15 bora hapo kesho.
Mshiriki namba 00554 akihojiwa na msanii Joti mara baada ya kufanikiwa kuingia hatua ya tatu hapo kesho ambapo watapatikana washindi kumi na tano bora na hatimaye kupata washindi watatu bora wa kanda ya kati ambapo kila mmoja atajinyakulia kitita cha shilingi laki tano za kitanzania
 
Baadhi ya washiriki wa shindano la Tanzania Movie Talents wakibadilishana mawazo mara baada ya kupatikana kwa washiriki 30 ambao wataendelea na mashindano hapo kesho kwaajili ya kupata washiriki 15 bora.
 Mmoja wa washiriki wa shindano la Tanzania Movie Talents akiwa amenyongonyea mara baada ya safari yake katika mashindano kuishia leo kutokana na kukosa nafasi ya kuingia katika hatua ya tatu hapo kesho.Picha na Josephat Lukaza wa Proin Promotions - Dodoma
Na Josephat Lukaza wa Proin Promotions Limited - Dodoma
Leo Shindano la Tanzania Movie Talents limeingia ya hatua ya pili ya mchujo ambapo washiriki 30 wameweza kupatikana kwaajili ya kuendelea na shindano hilo hapo kesho ambapo washiriki 15 ndio watachukuliwa kwaajili ya kuendelea na mashindano hayo na hatimaye kupatika washindi watatu bora ambao watawakilisha kanda ya Kati na kwa kila mshindi mmoja kuibuka na kitita cha shilingi laki tano (500,000/=).
Mpaka sasa washiriki 30 wameshapatikana kwa kanda ya Kati na hatimaye kesho washindi watatu watapatikana na kuiwakilisha kanda ya Kati katika fainali kubwa itakayofanyika Mkoani Dar Es Salaam na hatimaye mshindi katika fainali hiyo kujinyakulia kitita cha Shilingi Milioni 50 za kitanzania (50,000,000/=)
Katika Washindi 30 waliopatikana leo, washiriki wawili wameweza kuonyesha vipaji vyao huku washiriki hao wakiwa ni ndugu kabisa, washiriki hao ni babu na mjukuu wake wa kike ambao wameweza kufanikiwa kuingia hatua ya tatu kesho ambapo washindi wa Kanda ya Kati watapatikana.
Shindano la Tanzania Movie Talents linatarajiwa kumalizika kesho Kanda ya Kati Mkoani Dodoma na hatimaye kuhamia Kanda ya Juu Kusini ambapo usaili utafanyika Mkoani Mbeya na usaili wa Kanda ya Juu Kusini utaanza tarehe 19 April 2014 saa 1 asubuhi na wakazi wa Kanda ya Juu Kusini wanaombwa kujitokeza kwa wingi ili kuweza kuonyesha vipaji vyao na kuweza kuitumia fursa hii, Vilevile fomu za usaili zitapatikana Siku hiyohiyo ya usaili na fomu hizo hazina gharama yoyote ile.

NI BURUDANI MWANZO MWISHO SIKUKUU YA PASAKA DAR LIVE

introducing Real Love By Daddy Face (Official Music Video)


ngoma apendazo ankal

$
0
0
EVERLYN 'CHAMPAGNE' KING anakupa "LOVE COME DOWN"

Westgate Mall attack coverage wins the New York Times a Pulitzer

$
0
0


Tyler Hicks, a New York Times staff photographer based in Nairobi, won a Pulitzer on April 14 2014 for his breaking news photos of the Westgate Mall attack by Al-Shabaab on September 21, 2013. Photo: Courtesy New York Times
Coverage by the New York Times of the September 21, 2013 Al-Shabaab attack on the upscale Westgate mall in Nairobi has won the New York Times a Pulitzer in the Breaking News Photography category. The New York Times, a prolific Pulitzer winner in written hard news, only managed wins in the photography category this year. Its other win this year was in the Feature Photography category where it took home a Pulitzer for its coverage of the Boston Marathon bombing last year. Winners were announced this morning by Columbia University which oversees the awards.

MAENDELEO YA UJENZI WA VITUO VYA UTOAJI HUDUMA KWA PAMOJA MIPAKANI (ONE STOP BORDER POSTS)

$
0
0

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini kutoka Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bi. Vedastina Justinian akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kuhusu Mradi wa Vituo vya Utoaji Huduma kwa Pamoja Mipakani (One Stop Border Posts) unaolenga kurahisisha taratibu za forodha, uhamiaji, usimamizi wa ubora wa bidhaa, ulinzi na usalama. Kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi Miundombinu ya Kiuchumi Mhandisi Abdillah Mataka na kulia ni Afisa Habari wa Idara ya Habari Maelezo Bw. Frank Mvungi.

Mradi wa Vituo Vya Utoaji Huduma Kwa Pamoja Mipakani (One Stop Border Posts – OSBP) unalenga kurahisisha taratibu za forodha, uhamiaji, usimamizi wa ubora wa bidhaa na huduma, usalama na ulinzi kwa kutoa huduma hizi upande mmoja wa mpaka kwa pamoja. Mradi umekamilika kwa baadhi ya Mipaka kama Holili, Mutukula na Sirari. Ujenzi wa Vituo vya Namanga, Horohoro na Rusumo uko katika hatua za mwisho.




Utekelezaji wa OSBPs pamoja na kuandoa utaratibu wa sasa ambapo aina zote za udhibiti zinazofanyika mpakani hufanyika mara mbili, shughuli zote za udhibiti zitaendelea kufanyika kwa ukamilifu  katika upande mmoja badala ya kulazimika kurudiwa katika upande wa pili wa mpaka kama ilivyo zoeleka.


Mradi huu unatekelezwa kwanza kwa kutunga Sheria ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ya kuanzisha Vituo Vya Utoaji Huduma Kwa Pamoja Mipakani (OSBPs)  katika Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Tayari Bunge la Afrika Mashariki lilipitisha Sheria hiyo mwezi Mei, 2013 na sasa iko katika hatua za kuidhinishwa na Wakuu wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.


Hatua ya pili ni ujenzi wa OSBPs hizo katika mipaka mbalimbali ambayo iko katika hatua  zifuatazo:


Holili/Taveta mpaka unaozitenganisha Tanzania na Kenya kwa upande wa Holili OSBP imekamilika na imekabidhiwa kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania ambao ndio waendeshaji wa OSBP zote nchini na upande wa Kenya mpaka wa  Taveta mradi huu unatarajiwa kukamilika mwezi Mei, 2014.


Katika Mipaka ya Sirari/Isebania unaozitenganisha Tanzania na Kenya kwa upande wa Mkoa wa Mara na Mpaka wa  Mutukula/Mutukula unaozitenganisha Tanzania na Uganda kwa upande wa Tanzania Vituo vimekamilika. Aidha, Ujenzi wa Kituo cha Namanga  ulioanza mwezi Desemba, 2011 kama sehemu ya Mradi wa barabara ya Arusha – Namanga – Athi River unaendelea.


Kituo cha Kabanga/Kobero kilichopo katika mpaka wa Tanzania na Burundi muda wa Mradi ni miezi 15 na ulianza mwezi Mei, 2013 na unatarajiwa kukamilika Juni, 2014, hatua ya ujenzi wake imefikia  20% hadi kufikia Februari, 2014.


Mradi wa ujenzi wa OSBP ya Rusumo mpaka uliopo kati ya Tanzania na Rwanda umefikia asilimia 69.5% upande wa Tanzania hadi kufikia mwezi Februari, 2014 na unatarajiwa kukamilika ifikapo mwezi Novemba, 2014.


Mradi huu pia unatekelezwa katika mpaka wa Horohoro/Lungalunga mpakani mwa Tanzania na Kenya kwa upande wa Mkoa wa Tanga, ambapo hadi kufikia tarehe 31 Desemba, 2013 ujenzi wa kituo hiki ulikuwa umekamilika 90% na ilitarajiwa hadi kufikia mwishoni mwa mwezi Machi, 2014 Mradi kuwa umekamilika.


Kwa upande wa Tunduma OSBP – kituo kinafadhiliwa kwa pamoja kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Trade Mark East Africa (TMEA) chini ya usimamizi wa TBA. Ujenzi bado haujaanza; TMEA wako katika mchakato wa kumpata Mkandarasi kwa ajili ya ujenzi wa jengo la OSBP.


Rasimu ya Mkataba wa Ubia (Bilaterall Agreement) ya uendeshaji wa OSBPs kati ya Tanzania na Kenya imekamilika. Taratibu za kusaini Mkataba huu zinakamilishwa ili usainiwe hivi karibuni na kuwezesha Kituo kuanza kufanya kazi.


Ujenzi wa Vituo vya Utoaji Huduma kwa Pamoja Mipakani utasaidia usafiri na usafirishaji wa haraka kwa kuondoa urasimu mipakani na hivyo kupunguza gharama za usafiri na usafirishaji kwa Wanaafrika Mashariki.



Mkurugenzi Udhibiti Ubora kutoka Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Bi. Tumaini Mtitu akiwaeleza waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam mikakati ya kudhibiti ubora wa bidhaa za ndani na zinazotoka nje ili kuepuka madhara kwa watumiaji  wa bidhaa hizo. Kushoto ni Afisa Uhusiano wa shirika hilo Bi Roida Andusamile.

Tanzania U.S. State Alumni 3rd Annual Conference

MASAA 14 YA SAFARI YA KINANA ZIWA TANGANYIKA

$
0
0
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipanda boti kutoka mkoa wa Kigoma kuelekea Karema mkoani Katavi kwa siku nne.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimia wananchi wa kijiji cha Sigunga wilayani Uvinza mkoani Kigoma alipowasili kijijini hapo kuzungumza wananchi na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi,wengine wanaonekana kwenye picha ni Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Kanali Mstaafu Issa Machibya, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Balozi Ali Abeid Karume.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana  akiondoka kijijini Sigunga baada ya  kuzungumza wananchi na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi,wengine wanaonekana kwenye picha ni Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi anayepiga kasia na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Balozi Ali Abeid Karume.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akitembea kwenye mitaa ya kijiji cha Mgombo  Kata ya Buhingu wakati aliposimama kuwasalimia wanakijiji hao,Kinana ni Katibu Mkuu wa kwanza wa CCM kufika kijiji cha Buhingu. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA
Viewing all 110078 articles
Browse latest View live




Latest Images