Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 412 | 413 | (Page 414) | 415 | 416 | .... | 3348 | newer

  0 0
 • 04/07/14--01:54: BODABODA WASH.....
 • Kameraman spesheli wa Globu ya Jamii,mapema leo asubuhi alibahatika kukatiza maeneo ya Kigamboni na kukutana na taswira hii ya kituo maalum cha kuosha Pikipiki za kubeba abiria maarufu kama bodaboda.

  0 0

  Marehemu Juma Bhalo

  Mfalme wa Taarab nchini Kenya ambaye pia amejijengea jina katika nchi za Afrika Mashariki, Mohamed Khamis
  Juma Bhalo, amefariki dunia. Bhalo amefariki dunia usiku wa Jumamosi akiwa nyumbani kwake eneo la Mji wa Zamani Mombasa, baada ya kuugua kwa muda mrefu.
  Juma Bhalo  alizaliwa 1942 huko  Shela katika wilaya ya Malindi. Mwaka1954, alijiunga na shule ya msingi ya Sir Ali bin Salim , wakati huohuo familia yake ilihakikisha anahudhuria Madrassa ili kupata elimu ya dini. 
  Bhallo mwenyewe aliwahi kusema hamu yake ya kuimba ilimuanza katika wakati huu na sauti yake kuwa na mvuto kutoka kipindi hiki alipokuwa Madrassa Akiwa na miaka 9 tayari muda wake mwingi ulitumika kusikiliza santuri, na akili yake ilianza kupenda sana muziki. 
  Hakumaliza elimu ya msingi kwa kuwa wazazi wake walishindwa kulipa ada ya shule. Mwaka 1957 alihamia Mombasa na kupata kazi Forodhani, akiwa Mombasa alianza kukutana na kushirikiana na wanamuziki wa Taarab wa Mombasa. 
  Hakuipenda sana kazi ya Forodha hivyo 1959 akahamia Tanga kwa mjomba wake, na hapo akajiunga na kundi maarufu la Taarab wakati ule lililoitwa Young Noverty, hapa alipata ujuzi mkubwa wa muziki wa Taarab. 
  Alirudi kwao Malindi kwa muda mfupi na hatimae kurudi tena Tanga 1962 na kujiunga na kundi la Young Stars Taarab. 
  Mwaka 1966 alirudi Mombasa na kuanzisha kundi la Bhalo and Party, kundi ambalo amedumu nalo mpaka Mauti yake. Mwaka 2007 baada ya zaidi ya miaka 50 ya kuwemo katika muziki wa Taarab, Juma Bhalo ambaye wapenzi wake walimuita Profesa na hata Mfalme wa Taarab alitangaza kuacha kufanya maonyesho ya wazi ya Taarab, alitangaza hilo siku alipopiga katika harusi ya mwanae. 
  Alistaafu kazi hiyo kwa maneno yafuatayo  "Waswahili wasema kiwate kitu kabla hakijakuata. Kwa hivyo kama mulivyo nishuhudiya usiku huu nlivyowatumbuiza ambavyo ni kama kawaida yangu basi leo hii usiku huu kabla hawajaja watu wakasema ahhhhh Bhalo ashazeeka hawezi tena kuimba kwa hivyo najiuzulu ningali bado niko fiti. Kwa hivyo siimbi tena hadharani kikazi. Nawashkuru kwa ushabik wenu na musijali Mungu akiniwezesha Kasseti mpya ntawatoleya".
   Taarab yake iliegemea sana muziki wa Kihindi na hivyo kuwa tofauti na taarab nyingine
  MUNGU AMLAZE PEMA PROFESA 

  0 0

   Mbunge wa Jimbo la Kigamboni,Mh. Dkt. Faustine Ndugulile (mwenye fulana ya mistari mbele) akizungumza na baadhi ya kinamama wakazi wa Mji wa Kigamboni waliojitokeza kwa wingi kwenye Kituo cha Afya Kigamboni kwa ajili ya kupatiwa Huduma ya Uchunguzi na Tiba ya Kansa ya Mlango wa Kizazi kwa kina mama inayoendelea kutolewa leo kituoni hapo.
    Mbunge wa Jimbo la Kigamboni,Mh. Dkt. Faustine Ndugulile akimuuliza Muuguzi wa zamu namna zoezi hilo la Utoaji wa Huduma ya Uchunguzi na Tiba ya Kansa ya Mlango wa Kizazi inavyoendelea kwenye Kituo cha Afya Kigamboni.
   Kaimu Mganga Mkuu wa Kituo cha Afya cha Kigamboni,Dkt. Ansilla Lasway (kushoto) akimueleza Mbunge wa Jimbo la Kigamboni,Mh. Dkt. Faustine Ndugulile namna wanavyoendelea kutoa huduma za matibabu mbali mbali kwa wananchi wa Kigamboni.Mh. Ndugulile alitembelea kituo hicho leo ili kuona namna huduma zinavyotolewa kwa wagonjwa na changamoto zinazokikabili kituo hicho na kuahidi kuzifanyia kazi haraka iwezekanavyo.
   Mbunge wa Jimbo la Kigamboni,Mh. Dkt. Faustine Ndugulile akiwapongeza kinamama wa Kigamboni kwa kujitokeza kwa wingi kwenye Kituo cha Afya Kigamboni na kwa ajili ya kupatiwa Huduma ya Uchunguzi na Tiba ya Kansa ya Mlango wa Kizazi inavyoendelea kwenye kituo hicho.


  0 0

  Huku ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara ikiwa inaelekea ukingoni mdhamini Mkuu wa ligi hiyo  Vodacom Tanzania, wamesema wanavutiwa na ushindani ulipo katika mechi za sasa za ligi na mbio za ubingwa.

  Akizungumza punde baada ya kumalizika kwa mechi kati ya Yanga na JKT Ruvu iliyochezwa Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam na Yanga kuibuka na Ushindi wa Mabao 5 – 1. Meneja Uhususiano wa Nje wa Kampuni hiyo, Salum Mwalimu amesema kuwa, mafanikio waliyo yatarajia kutokana na udhamini wa ligi kuu yameanza kuonekana na kufurahia kuwa sehemu ya mapinduzi ya soka nchini.

  “Ukiangalia namna ushindani ulivyo sasa ni dhahiri kuwa ligi yetu imefikia patamu na haya ndio mafanikio tuliyokuwa tunayataka, kila timu inajitahidi kwa hali na mali kuhakikisha inashinda mechi zilizobaki ili kuchukua Ubingwa au kutoshuka daraja:, alisema Mwalim

  “Tukianza na mbio za ubingwa sasa ni wa aina ya kipekee kati ya Azam, Yanga na Mbeya City, tunashuhudia namna timu zote zinavyo hangaika kuhakikisha zinanyakua pointi zote tatu ili kujiweka mahala azuri pa kuchukua Ubingwa, tumebakiza mechi tatu lakini hadi sasa bado hatujajua bingwa ni nani, sio kama ilivyokuwa zamani,” alisema Mwalim na Kuongeza.

  “Hili ndilo tulilokuwa tunalitarajia tangu zamani, kuona timu zidi zinakuwa katika nafasi ya kuwania ubingwa na hata kutokuwa na uhakika wa kushinda katika mechi zote walizobakiwa nazo, Iwe Yanga, Azam au, Simba wote wakienda Mbeya, Kagera, Morogoro Tanga au Arusha hawana uhakika wa kutoka na ushindi ni jambo la kuvutia sana” alisema Mwalim.

  Meneja huyo alihitimisha kwa kuzitkia nafanikio timu zote za ligi kuu kuwa na mafanikio katika mechi zilizobaki huku akitanabaisha kuwa zawadi za msimu huu zitatolewa mapema na zimeboreshwa zaidi.

  0 0

  Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) kesho inatarajia kuanza kuwasajili wakazi wa Pemba baada ya kukamilisha zoezi hilo Unguja. Wananchi waombwa kujitokeza kwa wingi katika zoezi hili wakiwa na nakala za viambatisho muhimu vinavyithibitisha uraia, umri na makazi. Zoezi linahusisha ujazaji fomu na uchukuaji alama za vidole, picha na saini ya kielektroniki. Mkurugenzi wa Vitambulisho vya Taifa Ofisi ya Vuai Musa Suleima (wapili kushoto) akisisitiza jambo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari Pemba.

  0 0  Mhe. Omar Mjenga, Balozi Mdogo wa Ubalozi Mdogo wa Tanzania uliopo Dubai, akiwa katika picha na Mhe. Yousef A. Rahmani Al Mahaira, Mkurugenzi wa Wizara ya Mambo ya Nje ya UAE, Ofisi ya Dubai baada ya kikao chao leo ofisini kwa Mhe. Yousef. Kikao chao kilijadili maandalizi ya maadhimisho ya miaka 50 ya Muungano wa Tanzania. Mhe. Ali Hassan Mwinyi, Rais Mstaafu na Mtukufu Sheikh Ahmed Bin Saeed Ak Maktoum, Rais wa Idara ya Anga ya Dubai na Mwenyekiti wa Shirika la Ndege la Emirates watakuwa wageni rasmi. Sherehe hizo zitafanyika tarehe 14 Aprili katika Hotel ya Le Meridien Dubai.

  0 0

    Baadhi ya abiria kutoka sehemu mbalimbali wakipanda Ngalawa kwenye ufukwe wa ziwa Tanganyika,sehemu ijulikanayo kwa jina la Kibirizi kuelekea upande wa pili wa fukwe ya ziwa hilo pajulikanapo kwa jiina la Kagunga,ambapo abiria hulipa nauli ya shilingi Elfu tano kwa kila kichwa,na huchukua masaa mane kufika kwenye ufukwe huo,ambako ni mpakani mwa jirani na nchi ya Burundi.
  Abiria wakifunikwa turubai wasilowane na mvua,wakati ilipoanza kunyesha mjin hapa.
   Baadhi ya abiria kutoka sehemu mbalimbali wakipanda Ngalawa kwenye ufukwe wa ziwa Tanganyika,sehemu ijulikanayo kwa jina la Kibirizi kuelekea upande wa pili wa fukwe ya ziwa hilo pajulikanapo kwa jiina la Mwagongo mapema leo mchana mkoani Kigoma.
   Sehemu ya Ziwa Tanganyika kama inavyoonekana kwa mbaali mapema leo jioni mkoani Kigoma.
  PICHA NA MICHUZIJR-MICHUZI MEDIA GROUP-KIGOMA.

  0 0

  Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) kesho inatarajia kuanza kuwasajili wakazi wa Pemba baada ya kukamilisha zoezi hilo Unguja. Wananchi waombwa kujitokeza kwa wingi katika zoezi hili wakiwa na nakala za viambatisho muhimu vinavyithibitisha uraia, umri na makazi. Zoezi linahusisha ujazaji fomu na uchukuaji alama za vidole, picha na saini ya kielektroniki.
  Mkurugenzi wa Vitambulisho vya Taifa Ofisi ya Vuai Musa Suleima (wapili kushoto) akisisitiza jambo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari Pemba.

  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Viongozi alipowasili katika viwanja vya CCM Kisiwandui leo katika hitma na dua ya Rais wa kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani Karume.
  Mke wa Rais wa Kwanza wa Zanzibar Mama Fatma Karume akitia ubani wakati wa hitma ya kumuombea dua Rais wa kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani Karume,iliyosomwa leo katika ukumbi wa Ofisi ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja,wengine pia ni wake wa Viongozi.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Jakaya Mrisho Kikwete na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein wakisalimiana wajukuu wa Rais wa kwanza wa Zanzibar Mzee Abeid Amani Karume,na Viongozi wakati wa hitma na dua iliyoombwa na wananchi wa Zanzibar katika Ofisi ya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar leo mchana.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,(katikati) akiungana na Viongozi,Wananchi katika kumuombe dua kwa Kisomo cha Hitma iliyosomwa leo katika Ukumbi wa CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar,wakiwemo Rais wa Tanzania Alhaj Dk.Jakaya Mrisho Kikwete,Rais mstaafu wa Tanzania Mzee Mwinyi,Rais mstaafu wa Zanzibar Dk.Amani Abeid Karume,Makamo wa Rais wa Tanzania Dk.Bilali,Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi na Viongozi wengine (wa pili kushoto).


  0 0

   Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana, akiwa na mwenyeji wake Katibu Mkuu wa Chama Cha RPF-INKOTANYI, Francois Ngarambe baada ya kuwasili mjini Kigali, Rwanda kwenye tafrija ya viongozi wa vyama tawala barani Afrka.
  Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana, akiwa na mwenyeji wake Katibu Mkuu wa Chama Cha RPF-INKOTANYI, Francois Ngarambe baada ya kuwasili mjini Kigali, Rwanda kwenye tafrija ya viongozi wa vyama tawala barani Afrka. Kulia ni Mjumbe wa NEC, Balozi Ali Karume.
   Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, akitoa salaam za shukrani kwa niaba ya vyama Vilivyoalikwa kwa Katibu Mkuu wa RPF wakati wa hafla hiyo.
  Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana, akiagana na Rais wa Uganda Yoweri Museven baada ya maadhimisho ya kumbukumbu ya mauaji ya kimbali kwenye uwanja wa Amahoro, mjini Kigali, Rwanda.
   
  Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza, William Hague wakibadilishana mawazo kwenye Maadhimisho ya Kumbukumbu ya mauaji ya kimbari, katika Uwanja wa Amahoro leo.
  Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na Rais Mstaafu wa  Afrika Kusini Thabo Mbeki wakibadilishana mawazo kwenye Uwanja wakati wa maadhimisho hayo.
  Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahma Kinana, akiwa na Rais Mstaafu Benjamin Mkapa, Mama Anna Mkapa na Rais Mstaafu wa Botswana Sir. Ketumile Masire wakati wa maadhimisho hayo.
  Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akiwa na Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta
  Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akibadilishana mawazo na Rais wa Mstaafu wa Burundi Pierre Buyoya na mke wa Buyoya wakati wa maadhimisho hayo. Picha zote na Edward Mpogolo wa Ofisi ya Katibu Mkuu wa CCM

  0 0

  Meneja wa Hisa wa Benki ya CRDB Makao Makuu, Emanuel Ng'ui, akizungumza na wenye hisa wa CRDB Bank, katika semina ya uhamasishaji kuhusu matumizi ya Hisa.
  Mkurugenzi wa CRDB Bank, PLC, Tawi la Lumumba, John Almasy, akizungumza na Meneja wa Hisa wa Benki ya CRDB Makao Makuu, na Mkurugenzi wa CRDB, Tawi la Vijana, Pelesi Fungo, wakati wa semina hiyo.

  Umetolewa Mwito kwa Watanzania kuchangamkia fursa za uwekezaji kwa ununuzi wa hisa katika soko la hisa la Jumuiya ya Afrika linalotarajiwa kuanzishwa hivi karibuni, na ili Watanzania nao waweze kufaidika na umiliki wa hisa kupitia masoko ya hisa, mitaji na dhamana.

  Wito huo, umetolewa na Meneja wa Meneja wa Hisa wa CRDB Makao Makuu, Bw. Emanuel Ng’ui wakati wa semina ya uhamasishaji kwa wanahisa wa Benki ya CRDB, iliyofanyika leo kwenye hoteli ya Peacock.

  Bw. Ng’ui amesema, Watanzaniaq bado wana mwamko mdogo wa kiuzitumia fursa za uwekezaji kupitia masoko ya hisa mijaji na dhamana, ambapo mpaka sasa kwenye soko la hisa la Dar es Salaam, DSE, tayari tunao raia wa nchi za kigeni waliojisajili, huku Watanzania wenyewe tukiendelea kusua sua, hivyo Benki ya CRDB, imeamua kuwahamasisha wanahisa wake na wananchi kwa ujumla kuchangamkia fursa hizi.

  Mkurugenzi wa CRDB Bank, Tawi la Lumumba, Bw. John Almasy, amewahimiza Watanzania kuchangamkia fursa hizo, hivyo kuzuia Watanzania kuachwa nyuma katika utekelezaji wa Itifaki ya Soko la Pamoja la Jumuiya ya nchi za Afrika Mashariki, ambapo uanzishwaji wa soko la pamoja la hisa la Jumuiya ya Mashariki litaanzishwa.

  Mkurugenzi wa CRDB Tawi la Kijitonyama, Bw. Lucas Busigazi,  amewahimiza wanahisa wa Benki ya CRDB kuendelea kujitokeza kwa wingi katika semina hizo, ili kutimiza malengo ya Benki ya CRDB kuwa ni benki kiongozi kwa uwezeshaji Watanzania kuumiliki sio tuu uchumi wa Tanzania, bali hata uchumi wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki.

  Nae Mkurugenzi wa CRDB, Tawi la Vijana, Bw. Pelesi Fungo, amesema semina hizo ni za manufaa sana kwa wanahisa wa Benki ya CRDB na Watanzania kwa ujumla ili kuwapatia Watanzania elimu na ufahamu kuhusu uwekezaji katika hisa, hivyo kuwa ni wamiliki wa makampuni mbalimbali.

  Semina hiyo imehudhuriwa na washiriki zaidi ya 100, ambapo CRDB Bank, itaendelea kufanya semina kama hizo kwa mikoa yote Tanzania nzima.

  0 0

   Mkuu wa wilaya ya Makete mh Josephine Matiro (kulia) akizindua albamu ya video ya msanii wa nyimbo za Injili Aldo Sanga wilayani Makete, kushoto ni MC wa shughuli hiyo Bi. Happy Ngogo.Picha na Edwin Moshi, Makete.
   Mwimbaji mahiri wa nyimbo za injili Happy Kamili akitumbuisha mashabiki waliofika kwenye uzinduzi huo.


  0 0

  Kongamano la wanawake Wajasiriamali Tanzania lilofanyika katika ukumbi wa Mbezi Garden Hotel lilifana , mada mbalimbali ziliwasilishwa katika kongamano hilo liliandaliwa na Tanzania Business Entreprenuers for Women(TBEW) wakiongozwa na Haika Lawere Mkurugenzi Mtendaji wa Mbezi Garden Hotel. Kampuni na vikundi vya wajasiriamali zaidi ya 30 vilishiriki maonyesho ya bidhaa na wajasiriamali zaidi ya 100 walishiriki katika semina zilizokuwa zinafanyika sambamba na maonyesho hayo.
  Paul Mashauri wa EASB akitoa mada katika kongamano hilo.
  Ashura Katunzi Kilewela wa TBS akiongelea umuhimu wa viwango katika bidaa za kitanzania.
  Benedict Mwambela, Mkufunzi toka ILO akitoa mada.
  Washiriki wa kongamanno ambao walikuwa wakionyesha bidhaa zao.

  0 0

  Mkuu wa Idara ya Bima wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Bi. Kemibaro Omuteku (wa tatu kushoto) akiwa na baadhi ya maofisa wa benki hiyo wakionyesha vipeperushi ikiwa ni ishara ya kuzindua huduma ya Bima ya Bure ya Mkopo jijini Dar es Salaam jana. Kutoka kushoto ni; Mkuu wa Idara ya Mikopo, Andrew Lyimo, Meneja Bima ya Maisha, William Mapela na Mkuu wa Idara ya Mauzo, Mongateko Makongoro.
  Mkuu wa Idara ya Mikopo wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Andrew Lyimo, (kulia) akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa huduma ya Bima ya Bure ya Mkopo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkuu wa Idara ya Bima wa NBC, Bi. Kemibaro Omuteku.

  0 0


  Bondia Alibaba Ramadhan akiwa na mkanada wake wa Ubingwa baada ya kumtwanga Bondia Roy Mbuta kwa KO katika mchezo uliopiga jana.Pichani ni Bondia Alibaba akipata picha ya kumbukumbu na mgeni rasmi pamoja na wadhamini.
  Akapongezwa Alibaba kwa ushindi na sifa aliyoupatia mkoa wa Kilimanjaro.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akipokea msafara wa pikipiki wa vijana wa CCM (UVCCM) ambao wanaendesha mbio za Uzalendo Tanzania zikiwa na lengo la kuadhimisha Miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar jana tarehe 07-04-2014. Mbio hizo za kitaifa zinahusisha msafara wa pikipiki tano zinazoongozwa na viongozi watatu wa UVCCM ambao wanakuwa kwenye gari, aidha zinashirikisha wadau mbalimbali wa UVCCM katika kuzifanikisha. Mbio hizo  zinahimiza vijana kudumisha muungano, kuweka utaifa mbele na kutumia fursa zilizopo kwa maendeleo yao. Mbio hizo zitakuwa Mkoani Rukwa tarehe 07 na 08 April 2014 na kuelekea Mkoani Mbeya. 
  Ujumbe wa mbio hizo za Uzalendo Tanzania ambazo zinaendeshwa na UVCCM.
  Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya (kati) akiendesha duwa rasmi ya kuwaombea viongozi waasisi wa Muungano ambao wametangulia mbele za haki kama wanavyonekana kwenye picha Hayati Mwalim Julius K. Nyerere na Hayati Abeid Amani Karume muda mfupi baada ya kupokea msafara wa mbio hizi ofisini kwake jana tarehe 07-04-2014.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0
 • 04/08/14--00:49: RAIS KIKWETE APONGEZWA
 • Bw. Stanley Bergman akiteta jambo na Balozi Manongi wanaonekana pia wageni waalikwa waliojitokeza kwa wingi kwenye hafla hiyo.
  Rais na Mwanzilishi wa MCW, Bw. Eddie Bergman akielezea historia ya Taasisi hiyo ambayo aliianzisha ( 1999) akatumia fursa hiyo kutoa shukrani zake kwa wadau , wafadhili na marafiki mbalimbali ambao wameendelea kuiwezesha Taasisi hiyo na hatimaye kupitia kwayo kusaidia jamii katika maeneo mbalimbali na uwezeshaji wa vijana.
  Bw. Stanley Bergman, Mwenyekiti na CEO, Henry Schein Inc akizungumza wakati wa hafla ya miaka kumi ya uchangiaji wa Taasisi ya Miracle Corners of the World ( MCW) ambayo pia imetimiza miaka kumi na tano ya kuanzishwa kwake, katika mazungumzo yake alitoa shukrani na pongezi kwa Mhe. Rais Jakaya Kikwete kwa namna ambayo amekuwa akishirikiana na Taasisi hiyo ambayo inaendesha shughuli hususani uboreshaji na uimarishaji wa huduma ya afya ya kinywa.
  Mhe. Balozi Tuvako Manongi Muwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, akisema machache wakati wa hafla hiyo.

  0 0

  Kamanda wa Umoja wa Vijana wa CCM Mkoa wa Manyara, Christopher Ole Sendeka, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Simanjiro, akishikilia bendera ya Taifa, wakati akipokea mbio za pikipiki kwenye maadhimisho ya Karume Day yaliyofanyika jana Mji mdogo wa Mirerani.
  Kamanda wa Umoja wa Vijana wa CCM Mkoa wa Manyara, Christopher Ole Sendeka, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Simanjiro, akivishwa skafu kwenye maadhimisho ya Karume Day yaliyofanyika juzi Mji mdogo wa Mirerani.
  Kamanda wa Umoja wa Vijana wa CCM Mkoa wa Manyara, Christopher Ole Sendeka, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Simanjiro, akizungumza wakati akipokea mbio za pikipiki kwenye maadhimisho ya Karume Day yaliyofanyika jana Mji mdogo wa Mirerani.
  Baadhi ya wakazi wa Wilaya ya Simanjiro, wakimsikiliza Kamanda wa Umoja wa Vijana wa CCM Mkoa wa Manyara, Christopher Ole Sendeka, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Simanjiro, akizungumza wakati akipokea mbio za pikipiki kwenye maadhimisho ya Karume Day yaliyofanyika jana Mji mdogo wa Mirerani.
  Waendesha pikipiki wa Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro, wakishiriki mbio za pikipiki zilizoandaliwa na UVCCM Mkoani Manyara, kusherehekea maadhimisho ya Karume Day yaliyofanyika jana, ambapo mgeni rasmi alikuwa Kamanda wa UVCCM mkoani humo Christopher Ole Sendeka.

  0 0

  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) atapokea tuzo ya Africa’s Most Impactful Leader of the Year kwa niaba ya Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamahuri ya Muungano wa Tanzania mjini Washington D.C, Marekani tarehe 09 Aprili, 2014.

  Tuzo hiyo ambayo hutolewa kila mwaka na Taasisi ya Uchapishaji ya African Leadership Magazine yenye makazi yake nchini Marekani kwa viongozi wa Afrika wanaofikia vigezo vilivyowekwa na Taasisi hiyo ikiwa ni pamoja na kuzingatia utawala bora, demokrasia na kuheshimu haki za binadamu kwa Mwaka 2013 inatolewa kwa Mhe. Rais Kikwete.

  Kwa mujibu wa Taasisi ya African Leadership Magazine, Tuzo hiyo inatolewa kwa Mhe. Rais Kikwete kutokana na namna ya pekee ya uongozi wake wenye matokeo yanayopimika kiutawala bora hususan kwa mwananchi wa kawaida wa Tanzania. Aidha, uongozi wake umeiletea Tanzania heshima kubwa kimataifa na kuiweka Tanzania kama chaguo muhimu kwa wawekezaji kutokana na ukuaji uchumi na maboresho ya sera.


  Tuzo hiyo tayari imewahi kutolewa kwa Marais na Viongozi wengine mbalimbali wa Afrika wakiwemo Mhe. Ellen Johnson Sirleaf, Rais wa Liberia, Mhe. James Michel, Rais wa Shelisheli na Rais Mstaafu wa Ghana, Mhe. John Kuffor.

  Ujumbe wa Mhe. Membe utamhusisha Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Bw. Salvatory Rweyemamu, Waandishi wa Habari na Maafisa wa Serikali. Mhe. Membe atarejea nchini tarehe 11 Aprili, 2014.


  Imetolewa na: KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI, WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA, DAR ES SALAAM.

  8 APRILI, 2014

  0 0
 • 04/08/14--06:34: KIJIWE CHA UGHAIBUNI


older | 1 | .... | 412 | 413 | (Page 414) | 415 | 416 | .... | 3348 | newer