Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109593 articles
Browse latest View live

bwawa la maini oye!


heshima za mwisho kwa marehemu Meja Jenerali Kelvin Gabriel Msemwa

0
0
Hafla ya kuaga mwili wa aliyekuwa Kamishna wa Jeshi wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Marehemu Meja Jenerali Kelvin Msemwa iliyofanyika uwanja wa makao makuu ya Jeshi, Upanga, Dar es salaam, April 6, 2014. Marehemu alifariki dunia April 3, 2014 katika hospitali ya Jeshi ya Lugalo. Mwili wake unasafirishwa kuelekea Songea kwa mazishi Jumatatu April 7, 2014
 Amiri Jeshi Mkuu Rais Kikwete na Mama Salma Kikwete wakitoa heshima zao za mwisho
 Wakitoa pole kwa wafiwa
 Mkuu wa Majeshi Jenerali Davies Mwamunyange akielekea kutoa heshima zake za mwisho
 Mkuu wa Majeshi Jenerali Davies Mwamunyange akitoa heshima zake za mwisho
 Mkuu wa Majeshi Jenerali Davies Mwamunyange akimfariji mjane wa marehemu. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

RISALA YA WATANZANIA WAISHIO UINGEREZA KWA MHESHIMIWA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO TANZANIA

0
0
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea risala toka kwa Katibu wa Jumuiya ya Watanzania waishio Uingereza Bi Mariam Mungula alipokuwa London kwa ziara ya kiserikali kwa mwaliko wa Waziri Mkuu wa uingereza Mhe David Cameron. Risala hiyo inasomeka hapa chini...

SOMO LA BURE LA LEO: KUWA MAKINI KATIKA KUTOA TAARIFA BINAFSI MITANDAONI

0
0
Na ticha Yusuph Kileo.
Katika Muendelezo wa Kuelimisha Jamii jinsi ya kubaki salama mitandaoni, leo najikita katika maswala ya USIRI  (PRIVACY)  ambapo taarifa nyingi za mtu binafsi si vyema kuwekwa mitandaoni na pia maelezo mafupi ya namna wahalifu mtandao wanatumia taarifa hizo za siri mitandaoni kuleta madhara. 
Njia za awali ambazo wahalifu mtandao wanatumia kabla ya kusababisha madhara ni kukusanya taarifa za mhusika ambaye wanategemea kumdhuru kwa njia inayojulikana kitaalam kama “RECONNAISSANCE” ambapo mara nyingi taarifa za awali zinapatikana kwenye mitandao ya kijamii kwani inaaminika wengi hawana umakini katika kutoa taarifa zao kupitia mitandao ya kijamii.
Jamii inashauriwa kujenga umakini wa taarifa binafsi wanazo ziweka mitandaoni ili kuweza kubaki salama. “Takwimu inaonyesha asilimia kubwa ya watumiaji wamekuwa wakiweka taarifa ambazo zinaweza kutoa urahisi wakugundua mambo mengi kutoka kwa muhusika” – Yusuph Kileo.


Mfano, Kuna wale ambao hadi leo wanatumia maneno ya siri “PASSWORDS” kwa kutumia mwaka wao wa kuzaliwwa wakati kuo huo mwaka huo wa kuzaliwa umewekwa kwenye mitandao ya kijamii hapo inaonyesha ni jinsi gani muhusika huyu anatengeneza urahisi kwa mhalifu kuweza kumuingilia kumdhuru.

Aidha, Umuhimu mkubwa unahitajika katika utoaji wa siri za mtu binafsi kwani panapokua na ugumu katika kukusanya taarifa za awali za mtu binafsi kunajengeka ugumu wa ukusanyaji wa taarifa za muhusika ambapo kunapelekea ugumu kwa mhalifu kuleta madhara kirahisi kwa mhusika.

Pia Kumekua na wimbi la wahalifu wanao omba moja kwa moja kupitia baruapepe au mitandao ya kijamii taarifa za watu na takwimu zinaonyesha kuna wale ambao bado wanatoa taarifa hizo bila kujua athari zake.


“Nashauri Unapo pokea jumbe inayo kuhitaji utoe taarifa zako binafsi aidha kwa maelezo kuwa kuna matengenezo katika akaunti yako au kukuwezesha kifedha na kuanzisha uhusiano kuwa makini kwani ni moja ya hatua za ukusanyaji wa taarifa za mtu ili kujenga njia ya kuanzisha madhara” 

Picha: inaonyesha mambo ya msingi kuzingatia utumiapo mitandao ya kijamii ili kuweza kujenga ugumu kwa wahalifu mtandao kuleta madhara.

watanzania wanne wakamatwa na polisi huko macau, china, wakijihusisha na biashara ya ngono

VISIT this year's Wedding Fair: 11&12 April

0
0
The complete list of all Participants for this year wedding fair will be available on 8 April 2014.
HARUSI TRADE FAIR MAGAZINE
The Fourth annual publication will be Available during the wedding Fair. All grooms & brides for 2014 make sure you get your hardcopy at the Fair for FREE

Copyright © 2014 Harusi Trade Fair, All rights reserved.
Our mailing address is:
Harusi Trade Fair
48B, Drive In, Namanga
P.O. Box 10684
Dar Es Salaam
Tanzania


WIZARA YA FEDHA YAWEKA WAZI JINSI ITAKAVYOTEKELEZA MATOKEO MAKUBWA SASA 'BRN'

0
0
Msemaji Mkuu wa Wizara ya Fedha, Ingiahedi Mduma, akizungumza wakati wa Semina maalum kwa 'Mablogger', iliyofanyika katika Hoteli ya Kilimanjaro Park, Misugusugu Kibaha, hivi karibuni. Semina hiyo imeandaliwa na Wizara ya Fedha kwa lengo la utaratibu wa kutimiza utekelezaji wa Matokeo Makubwa Sasa (Big Results Now).
*************************************************
Na Sufianimafoto Reporter
wizara ya fedha imeeleza wazi kuhusu mipango yake ya kutekeleza matokeo makubwa sasa(BRN) ikiwa ni utraatibu unaotumiwa na Serikali katika kusimamia na kufuatilia utekelezaji wa baadhi ya majukumu yake kwa lengo la kupata matokeo makubwa kwa muda mfupi

Akieleza malengo hayo hayo msemaji mkuu wa wizara ya fedha, INGIAHEDI MDUMA amesema wizara ya fedha imejipanga Kutafuta mapato ya ziada kiasi cha shilingi trilioni 3.8 hadi kufikia mwaka 2015/16

Pamoja na hayo Mduma amesema pia wamedhamiria kupunguza nakisi katika bajeti ya Serikali kwa shilingi trilioni 4 kufikia mwaka 2015/16 na Kutekeleza miradi ya PPP yenye thamani ya shilingi trilioni 6 kufikia mwaka 2015/16

Malengo mengine ni kuhakikisha kwamba shughuli za BRN zinapatiwa fedha za kutekeleza miradi iliyopangwa ili kuweza kusimamia malengo yaliyokusudiwa 
Aidha amesema viashiria vya utafutaji wa mapato vinavyotekelezwa na Wizara ya Fedha vimegawanyika katika sehemu kuu nne ikiwemo ya mapato ya kodi, mapato yasiyo ya kodi, ubia katika sekta ya umma na sekta binafsi na kudhibiti matumizi ya serikali.

katika kuelezea malengo hayo amesema Katika kipindi cha Julai – Disemba, 2013 jumla ya shilingi bilioni 215.0 zimekusanywa kutokana na hatua mpya za kodi zilizoibuliwa kwenye maabara za BRN.

Nchimbi mgeni rasmi Tamasha la Pasaka Songea.

0
0
 
ALIYEKUWA Waziri wa Mambo ya Ndani, Emmanuel Nchimbi anatarajia kuwa mgeni rasmi katika Tamasha la Pasaka linalotarajia kufanyika Aprili 26 Wilayani Songea mkoani Ruvuma.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama wakazi wa mkoa huo na maeneo ya jirani wajitokeze kwa wingi  kufanikisha sherehe ya kufufuka kwa mwokozi Wetu Yesu Kristo.
 Msama alisema mbali ya Nchimbi kuwa mgeni rasmi Songea, jijini Mbeya mgeni rasmi atakuwa ni Mbunge wa viti maalum, Mary Mwanjelwa  wakati mkoani Dodoma mgeni rasmi atakuwa mbunge wa Tarime, Nyambari Nyangwine. Aidha Msama alitoa fursa kwa wakazi wa mikoa litakapofanyika Tamasha la Pasaka kujitokeza kwa wingi ili kufanikisha ufanikishaji wa ujenzi wa Kituo cha Kimataifa cha wenye uhitaji Maalum cha Jakaya Mrisho Kikwete rafiki wa Wasiojiweza.

AFISA MAHUSIANO WA TANZANIA MOVIE TALENTS AKIONGELEA KUHUSU MASHINDANO YA KUSAKA VIPAJI VYA UIGIZAJI TANZANIA

Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Manyara, SACP Deusdedit Nsimeki afanya ukaguzi wilayani simanjiro

0
0
 Askari wa kituo cha polisi Mirerani Wilayani Simanjiro wakifanya mazoezi mbele ya Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Manyara, SACP Deusdedit Nsimeki, alipofanya ziara ya ukaguzi wilayani humo mwishoni mwa juma.
 Askari wa kituo cha polisi Mirerani Wilayani Simanjiro wakifanya mazoezi mbele ya Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Manyara, SACP Deusdedit Nsimeki, 
 Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Manyara, SACP Deusdedit Nsimeki, akikaribishwa kukagua  askari polisi jamii wa Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara juzi, alipotembelea wilaya hiyo.
 Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Manyara, SACP Deusdedit Nsimeki, akiwakagua askari polisi jamii wa Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyarai, alipotembelea wilaya hiyo.
Askari wa kituo cha Polisi Mirerani Wilayani Simanjiro wakijiandaa kukaguliwa na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Manyara, SACP Deusdedit Nsimeki alipotembelea wilaya hiyo kufanya ukaguzi
 Mkuu wa kituo cha Polisi Mirerani Wilayani Simanjiro, SP Ally Mohamed Mkalipa (kushoto) akimwelezea Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Manyara, (SACP) Deusdedit Nsimeki, kuhusiana na maendeleo ya polisi jamii, kwenye mji mdogo wa Mirerani  alipokuwa akiwakagua mwishoni mwa juma.
Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Manyara, (SACP) Deusdedit Nsimeki (kushoto) akizungumza na askari polisi wa kituo cha Mirerani Wilayani Simanjiro wakati alipokuwa akiwakagua mwishoni mwa juma.

SIKILIZA KWANZAJAMII RADION LIVE KUTOKA SOKO LA HABARI KARIAKOO...!

0
0
Leo Jumatatu, Aprili 7, Redio yako ya Kijamii ya KwanzaJamii imeandika historia kwa kuwa redio ya kwanza hapa nchini kuwaletea wasikilizaji dondoo za habari za magazetini kutokea kwenye soko lenyewe la habari, ni  pale kona ya Uhuru na Msimbazi, Kariakoo.
Ni kipindi cha kila siku kuanzia saa kumi na moja na nusu alfajiri. Mwandishi/ Mtangazaji wa KwanzaJamii atakuwa sokoni hapo na kuungana moja kwa moja na studio za Kwanzajamii radio Iringa.
Sambamba na redio, habari hizo na picha za magazeti yenyewe zitarushwa pia kwenye Mjengwablog.com. Ikumbukwe, Mjengwablog ilikuwa ni blogu ya kwanza hapa nchini kuanza kurusha kwenye blogu dondoo za magazetini.
Usikose kufuatilia na kuzipata habari zikiwa motomoto kutoka Soko la habari Kariakoo...http://www.mjengwablog.com/habari-za-kijamii/item/10489-kutoka-soko-la-habari-kariakoo.html#.U0JH6ldQ7U4

RIDHIWANI KIKWETE ASHINDA KWA KISHINDO UBUNGE WA JIMBO LA CHALINZE

0
0
Ridhiwani Kikwete akizungumza na waandishi wa habari baada ya kupiga kura mjini Chalinze jana.

Na John Bukuku  
Ridhiwani Kikwete aliyekuwa mgombea ubunge uchaguzi mdogo jimbo la Chalinze wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani kupitia CCM ameibuka kidedea kwa asilimia 86.61 katika uchaguzi huo kwa kuwamwaga wagombea wengine kutoka vyama vinne vya upinzani.

Matokeo hayo rasmi yametangazwa usiku wa kuamkia leo April 7, 2014 majira ya saa nane usiku katika shule ya sekondari Chalinze na  Msimamizi wa uchaguzi huo  Bw.Samwel Salianga.

Msimamizi huyo wa uchaguzi  amesema Ridhiwani Kikwete (CCM) amepata kura  20,828 sawa na  86.61%, Mathayo Torongei  (CHADEMA) amepata kura 2,544 sawa na asilimia 10.58, Fabian Skauki  (CUF) 476 sawa na asilimia 1.98, Hussein Ramadhani (NRA) kura 60 asilimia 0.25 na  Ramadhani Mgaya (AFP) amepata kura 186 sawa na asilimia 0.59.
 Bw. Salianga amesema kati ya watu waliojiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura ni watu elfu 92, na waliojitokeza katika zoezi hilo ni watu 24,422 ambapo kura halali zilikuwa 24,047 na  kura 375 zikiharibika.
Wagombea waliokuwepo wakati wa kutangaza  matokeo katika uchaguzi huo na kusaini fomu ya kukubaliana na matokea ni wagombea wa NRA na CCM pekee. 

Aidha Wakizungumza baada ya kupokea matokeo hayo aliyekuwa mgombea wa chama cha NRA pamoja na Ridhiwani Kikwete kupitia CCM, kila Mmoja ameshukuru wananchi na kuahidi kushirikina na wana Chalinze kuleta maendeleo.

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LEO TAREHE 07.04.2014.

0
0
MWANAFUNZI WA SHULE YA SEKONDARI NANDANGA KIDATO CHA KWANZA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA LUKAS MSUKWA (16) ALIFARIKI DUNIA BAADA YA KUTUMBUKIA KATIKA SHIMO LA MAJI LILILOCHIMBWA NA WATENGENEZA BARABARA YA MPEMBA HADI WILAYANI ILEJE.

TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 05.04.2014 MAJIRA YA SAA 13:00 MCHANA HUKO KATIKA KIJIJI CHA NANDANGA, WILAYA YA MOMBA. INADAIWA KUWA CHANZO CHA TUKIO HILO NI BAADA YA MAREHEMU KUTELEZA NA KUTUMBUKIA KATIKA SHIMO HILO LENYE UREFU WA KINA KATI YA FUTI 20 NA ZAIDI AMBALO LILIKUWA NA MAJI.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUFUKIA MASHIMO YALIYO WAZI BAADA YA KUTUMIKA KWANI NI HATARI KWA WATOTO NA HATA WATU WAZIMU. AIDHA ANATOA WITO KWA WAZAZI/WALEZI KUWA MAKINI NA WATOTO WAO HASA WALE WANAOISHI JIRANI NA MITO/MABWAWA KUTOWARUHUSU KUSOGELEA MAENEO YENYE MAJI KWANI NI HATARI KWA MAISHA YAO.

TAARIFA YA MSAKO: 
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA FESTO SALILE (39) MKAZI WA MBUGANI AKIWA NA BHANGI KETE 10 SAWA NA UZITO WA GRAMU 50.

MTUHUMIWA ALIKAMATWA KATIKA MSAKO ULIOFANYIKA MNAMO TAREHE 05.04.2014 MAJIRA YA SAA 15:30 ALASIRI HUKO KATIKA KIJIJI NA KATA YA MALEZA, TARAFA YA KWIMBA, WILAYA YA CHUNYA. MTUHUMIWA NI MUUZAJI NA MTUMIAJI WA BHANGI HIYO, TARATIBU ZA KUMFIKISHA MAHAKAMAI ZINAENDELEA.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.

Signed by:

[AHMED Z. MSANGI – SACP]


KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

DAKIKA 90 ZA DUNIA. Mauaji kwenye kambi ya jeshi Fort Hood MAREKANI

0
0
Jenerali Mark Milley, Kamanda wa Fort Hood akizungumza na waandishi wa habari
Wiki iliyopita, nchi ya Marekani ilikumbwa na mauaji mengine yaliyotokea kwenye kambi ya jeshi huko Fort Hood, Texas.
Jumatano Aprili 2, askari mmoja wa Jeshi la nchi hiyo, Ivan Lopez ambaye inasemekana alikuwa na matatizo ya msongo wa mawazo, aliwafyatulia risasi na kuwaua wanajeshi wenzake 3, kujeruhi 16 kabla hajajigeuzia bastola na kujiua
Mauaji haya, yanarejesha kumbukumbu ya mauaji makubwa kabisa kutokea kwenye kambi za jeshi nchini humo, yaliyotokea kwenye kambi hiyohiyo takriban miaka 5 iliyopita.

TIMU YA WATOTO WA MITAANI YATWAA UBINGWA WA DUNIA

0
0
Timu ya Taifa ya Watoto wa Mitaani ya Tanzania imetwaa ubingwa wa Dunia wa Watoto wa Mitaani baada ya jana (Aprili 6 mwaka huu) kuilaza Burundi mabao 3-1 katika mchezo wa fainali uliochezwa jijini Rio de Janeiro, Brazil.

Mshambuliaji Frank William alifunga mabao matatu katika mechi hiyo iliyochezwa uwanja mkongwe na maarufu wa klabu ya Fluminense huku mgeni rasmi akiwa Waziri wa Fedha wa Uingereza, George Osborne.

Tanzania ilipata tiketi ya kucheza fainali baada ya kuitandika Marekani mabao 6-1 ambapo hadi mapumziko ilikuwa mbele kwa mabao 4-0.

Burundi ilipata tiketi ya kucheza fainali baada ya kuifunga Pakistan mabao 4-3 katika mechi ya nusu fainali ya pili.

Timu ya Tanzania inarejea nchini Alhamisi (Aprili 10 mwaka huu) ambapo itatua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) saa 10 jioni kwa ndege ya Emirates.

BONIFACE WAMBURA
OFISA HABARI NA MAWASILIANO
SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

WATANZANIA WASOMAO BEIJING CHINA WACHAGUANA, WAWEKA MIKAKATI YA KUDUMISHA MUUNGANO

0
0

 Mwenyekiti mpya Suleiman Serera akishikana mkono na Mwenyekiti aliyemaliza muda wake Bw. Daninga Philip. Wengine katika picha ni uongozi mzima wa Watanzania wasomao Beijing.
  Mwenyekiti aliyemaliza muda wake wa Umoja wa wanafunzi wanaosoma Beijing, China (TzBeijing ) Bw.Philip Daninga akiongea na wanachama wa umoja huo muda mfupi kabla ya zoezi la kupiga kura lililofanyika mwishoni mwa wiki hii kwenye Ukumbi wa Ubalozi wa Tanzania, China. Wengine katika picha kutoka kushoto ni Bw. Eusebia John (Makamu Mwenyekiti) na Suleiman Serera (Kaimu Mhasibu). Kwa habari kamili na picha zaidi BOFYA HAPA.

UNHCR WAKABIDHI GARI MPYA KWA AJILI YA IDARA YA WAKIMBIZI NCHINI.

0
0
 Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe. Mathias Chikawe (kushoto) akipokea ufungua wa gari kutoka kwa Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi Duniani (UNHCR), Bi. Joyce Mends-Cole. Gari hiyo ambayo ni mpya aina ya Toyota Land Cruiser imetolewa na Shirika hilo kwa ajili ya kusaidia shughuli mbalimbali za kiutendaji zifanywazo na Idara ya Wakimbizi nchini iliyopo ndani ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. Tukio la makabidhiano hayo lilifanyika katika ofisi za wizara hiyo, jijini Dar es Salaam leo

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (kulia) akiifurahia gari mpya aina ya Toyota Land Cruiser baada ya kukabidhiwa na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi Duniani (UNHCR), Joyce Mends-Cole (kushoto). 
Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani.

TAARIFA MUHIMU KWA WANAHABARI WA MKOA WA MBEYA

0
0
Tarehe 3/5/2014 ni siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani, hivyo kila sehemu huadhimisha siku hiyo kulingana na mipango yao.

Kwa Mkoa wa Mbeya siku hiyo itaadhimishwa kwa kufanya bonanza kubwa litakalowashirikisha waandishi wa habari pamoja na wadau na baadaye kuwa na tafrija fupi ukumbini majira ya jioni. Kwa mantiki hiyo basi kwa mwandishi wa habari Mkoa wa Mbeya bila kujali ni mwanachama wa Mbeya Press ama la unaarifiwa kuanza mazoezi kwa ajili ya kushiriki bonanza hilo litakaloanza majira ya saa mbili asubuhi eneo mtaambiwa. 
 Aidha kuhusu sherehe ya jioni kwa asiye mwanachama wa Mbeya press Club utapaswa kuchangia gharama za ukumbi lengo likiwa ni kufanikisha sherehe hiyo na kuonesha uhai wetu sisi waandishi wa habari Mkoa wa Mbeya kwa wadau wetu ambao tutakuwa nao uwanjani. 

 Mchango kwa Mwandishi asiye Mwanachama wa Mbeya Press Club ni Shilingi Elfu Ishirini tu(20,000/=) kwa kila mtu na mwisho wa kuchangia ni tarehe 30/4/2014 lengo ni kuiwezesha kamati ya maandalizi kuandaa shughuli iliyoenda shule. 
 Ukiwa na mchango tafadhali wasilisha kwa Joachim Nyambo 0756409597, Emmanuel Madafa 0712199378 au Venance Matinya 0755063513. 
Tunategemea ushirikiano wenu katika kufanikisha sherehe za uhuru wa vyombo vya habari duniani May 3, kila mwaka.

IMETOLEWA NA KAMATI YA MAANDALIZI

introducing new song by Cjamoker

mhe kipozi ala pozi na wanahabari waliokuwa wakiripoti kampeni za ubunge jimbo la chalinze

0
0
Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Mhe. Ahmed Kipozi (wa nane, waliosimama) akiwa na kundi la wanahabari kutoka vyombo mbalimbali waliokuwa wakiripoti taarifa za uchaguzi mdogo wa jimbo la Chalinze uliomalizika mwishoni mwa juma na mgombea wa CCM Ridhiwani Kikwete kuibuka mshindi. Mhe. Kipozi, ambaye yeye mwenyewe ni mwanahabari mkongwe,  amewashukuru sana wanahabari hao pamoja na vyombo vyote kwa uahirikiano waliotoa pamoja na kazi iliyojaa weledi katika kipindi chote cha kampeni
Viewing all 109593 articles
Browse latest View live


Latest Images