Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110171 articles
Browse latest View live

Timu ya Jamhiri ilivyoigaragaza timu ya Polisi Zanzibar kwa bao 1-0

$
0
0
Mshambuliaji wa timu ya Jamhuri Samir Said (kushoto) akiwania mpira wa juu na mchezaji wa timu ya Polisi Abdalla Mwalim katika mchezop wa Ligi kuu ya Grand Malta Zanzibar uliochezwa juzi kwenye Uwanja wa Aman, Zanzibar.Jamhuri ilishinda 1-0.
Winga wa timu ya Polisi Mohamed Mohamed (kushoto) akiwania mpira na beki wa timu ya Jamhuri Mohid Said katika mchezo wa Ligi Kuu ya Grand Malta Zanzibar uliochezwa kwenye Uwanja wa Aman juzi. Jamhuri ilishinda 1-0.
Mshambuliaji wa timu ya Polisi Abdalla Ali (katikati) akiwatoka mabeki wa timu ya Jamhuri katika mchezo wa Ligi Kuu ya Zanzibar Grand Malt, uliochezwa kwenye Uwanja wa Aman juzi. Jamhuri ilishinda 1-0.
Winga wa timu ya Jamhuri Hussein Said (kushoto) akiwania mpira na beki wa timu ya Polisi Mohamed Vual katika mchezo wa Ligi Kuu ya Zanzibar Grand Malt uliochezwa kwenye Uwanja wa Amaani juzi. Jamhuri ilishinda bao 1-0.


Maangalizi ya afya Washington DMV...bure

$
0
0
Wataalam wa afya DMV (HCP Metro DC) wanatuleta huduma ya afya kwa walewasiokuwa na bima ya afya. Huduma hii itatolewa kwa usawa bila kujali dini,rangi,umri,uraia au uchumi.

Kama una rafiki, ndugu au  mzazi asiyekuwa na bima ya afya tunaomba mshiriki ili tuwe na jamii inayoshamiri na yenye afya njema. Zoezi hili litachukuwa hatua ya kuwaona wale watakaokuwa na hali pungufu ya afya njema mara moja kwa mwezi.


Tarehe: 04/12/2014   (Jumamosi)
Saa 3:00 asubuhi hadi mchana 7:00 (waweza kuja hata kwa saa moja)  
MAHALA
3621 Campus Drive, 
College Park, MD 20740

Leo hii wadau wetu tunaomba tujitolee kufanikisha huduma hii ya maangalizi ya afya ya bure kwa wadau wa DMV. 
Unaweza kujitolea kwa namna mbalimbali
  • Iwe ni kumsadia mtu usafiri,
  • kuandikisha majina ya wanaokuja
  • kubeba na kupanga meza kabla na baada ya maangalizi
  • au kushiriki katika timu ya kitaalam
Tafadhali wasiliana nasi kupitia barua pepe nesiwangublog@gmail.com ili tuweze kupata idadi na uhakika wa msaada wako.

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LEO TAREHE 08. 04.2014

MTN Group and Bharti Airtel partner to launch international money transfer

$
0
0
MTN Group and Bharti Airtel today announced a cross-border remittance partnership that seeks to remove the hassles of transferring money between Ivory Coast and Burkina Faso for the operators’ Mobile Money customers on either side of the border.

The landmark partnership will enable Mobile Money customers of MTN Ivory Coast and Airtel in Burkina Faso to easily transfer money between the neighbouring countries. Until now, moving money between the two countries was mired by high fees, high usage of informal channels and a lack of proximity to withdraw money.

MTN and Airtel already enjoy great adoption of Mobile Money services in their respective footprints, and connecting their operations through remittance services appears a logical next step.

“MTN has reached a great level of adoption of Mobile Money in Ivory Coast, and Airtel has done the same in Burkina Faso. With a sizeable community of Burkinabe working in Ivory Coast and sending money back to their home country, the partnership will greatly enhance the Mobile Money service for customers in both countries. MTN brings the same added value to international transfers that we offer in local transfers; reliable, instant, affordable and proximity with customer through our distribution network,” says Pieter Verkade, MTN Group Chief Commercial Officer.

“This partnership between Airtel and MTN is quite symbolic; it is the first time that two leading providers of mobile money services are cooperating to offer a service. Secondly, this is the first cross border mobile to mobile remittance service in West Africa and it has been designed to eliminate current pains associated with remitting funds between both countries whilst offering best in class security that protects the “sweat” of hard working Burkinabes that want to remit funds back home to their loved ones” says Chidi Okpala, Airtel Africa Group Director for Airtel Money.

MTN Mobile Money enables users to perform local and international money transfers, make utility and other service payments, purchase airtime and access range of mobile financial products. As of 31 December 2013, MTN Mobile Money had 14,8 million registered users, and was available in 14 countries. MTN continues to pursue opportunities to develop unique offerings to add to its growing financial services portfolio.

Verkade paid tribute to the Central Bank of West African States (BCEAO) for their support in enabling this service to the customers.

WAZIRI MKUU KUWA MGENI RASMI, HAFLA YA KUKABIDHI HUNDI ZA RUZUKU KWA WACHIMBAJI WADOGO

$
0
0
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mizengo Pinda atakuwa mgeni rasmi katika hafla iliyoandaliwa na Wizara ya Nishati na Madini ya kukabidhi hundi za ruzuku ya Dola za Marekani 500,000 kwa wachimbaji wadogo 11 waliokidhi vigezo.

 Hafla ya Utoaji wa hundi hizo kwa wachimbaji wadogo itafanyika mjini Dodoma tarehe 9/4/2014 katika Chuo cha Madini ambapo Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo akiambatana na Naibu Waziri anayeshughulikia Madini, Stephen Masele pamoja na watendaji kutoka Benki ya Rasilimali Tanzania (TIB), Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) pamoja na Shirikisho la Wachimbaji Wadogo Tanzania (FEMATA) watashuhudia utoaji wa hundi hizo. 

 Ruzuku hiyo ya Dola za Marekani 500,000 imetolewa na Benki ya Dunia kupitia Mradi wa Usimamizi Endelevu wa Rasilimali Madini (SMMRP) ulio chini ya Wizara ya Nishati na Madini. 

 Kutolewa kwa hundi hizo ni matokeo ya mkataba ambao Wizara ya Nishati na Madini iliingia na Benki ya Rasilimali Tanzania (TIB) ili Benki hiyo iwe Wakala wa kutoa mikopo na ruzuku kwa wachimbaji wadogo kwa niaba ya serikali. 

 Mkataba wa uendelezaji wachimbaji wadogo ulioingiwa kati ya TIB na Serikali unasisitiza ruzuku kutolewa kwa wachimbaji wadogo wenye sifa ili kuwawezesha kufanya shughuli zao za uzalishaji mali, wakiwepo wanawake wanaojishughulisha na utoaji huduma katika maeneo ya uchimbaji mdogo.

 Wachimbaji wadogo 11 watakabidhiwa hundi hizo za ruzuku baada ya kukidhi vigezo vya kuwa na uzoefu wa uchimbaji mdogo usiupungua miaka Tano, kuwa na leseni hai ya uchimbaji, uchenjuaji na biashara ya madini pamoja na kuwa na ushahidi wa upatikanaji wa mashapo au mali ghafi inayohitajika kwa ajili ya mradi unaoombewa ruzuku.

 Imetolewa na; 
 BADRA MASOUD 
 MSEMAJI WA WIZARA

BTS reception for president Kikwete in London

Wadau wa filamu nchini waaswa kuendelea kupeperusha bendera ya Tanzania Kimataifa

$
0
0
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Sihaba Nkinga akitoa hotuba ya ufunguzi wa kikao cha wadau wa filamu kuhusu mstakabali wa soko la filamu nchini leo jijini Dar es salaam.
Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu nchini Bi Joyce Fisoo akieleza lengo la kikao cha wadau wa filamu ni pamoja na kujadili masuala ya maendeleo ya tasnia ya filamu nchini na mapendekezo ya wadau kuhusu bodi ya filamu kuitisha mjadala wa wazi wa wadau wa filamu hususani wasambazaji, waandishi wa miswada na watayarishaji ili kujadili masuala mbalimbali yanayohusu tasnia hiyo leo jijini Dar es salaam.
Baadhi ya wadau wa filamu walioshiriki kikao cha kujadili masuala mbalimbali ya husuyo tasnia hiyo leo jijini Dar es salaam. Pichani ni wasanii wa “Bongo Movie” (wa kwanza kushoto ni Steven Mengele “Manyerere”, Emmanuel Muyamba (katikati) na Jacobo Steven “JB”(wa kwanza kulia).
Picha ya pamoja ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Sihaba Nkinga (wa sita kutoka kushoto mstari wa mbele) baada ya ufunguzi wa kikao cha wadau wa filamu kuhusu mstakabali wa soko la filamu nchini leo jijini Dar es salaam. (Picha zote na Eleuteri Mangi-MAELEZO)

BURUDANI ZATAWALA KANUMBA DAY DAR LIVE


OFISI YA TAIFA YA TAKWIMU YAFUNGUA RASMI MAFUNZO YA NAMNA YA UANDISHI BORA WA TAARIFA ZA KINA (THEMATIC REPORTS), ZINAZOTOKANA NA SENSA YA WATU NA MAKAZI YA MWAKA 2012

$
0
0
Mgeni Rasmi Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha Bi. Evelne Itanisa (katikati) akimsikiliza kwa makini mwakilishi wa Wadau wa Maendeleo (hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya Namna ya Uandishi Bora wa Taarifa za Kina (Thematic Reports) zinazotokana na Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2012 yaliyonguliwa jana mkoani Arusha. Kulia kwake ni Mkurugeni wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa na kushoto kwake ni Kamishna wa Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2012 Hajjat Amina Mrisho Said.
Mgeni Rasmi Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha Bi. Evelne Itanisa (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu na Ofisi ya Mtakwimu Mkuu, Zanzibar pamoja na baadhi ya washiriki wa mafunzo ya Namna ya Uandishi Bora wa Taarifa za Kina (Thematic Reports) zinazotokana na Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2012 yaliyoandaliwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu, mafunzo hayo yamefunguliwa jana mkoani Arusha.
Kamishna wa Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2012 Hajjat Amina Mrisho Said akiwa katika mahojiano maalumu na waandishi wa habari mara baada ya kufungua mafunzo ya Namna ya Uandishi Bora wa Taarifa za Kina (Thematic Reports) zinazotokana na Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2012 yaliyoandaliwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu, mafunzo hayo yamefunguliwa jana mkoani Arusha. (PICHA ZOTE NA VERONICA KAZIMOTO).

TANGAZO LA KUCHIMBA DAWA

MAHAKAMA KUU KANDA YA MOSHI YAWAACHIA HURU WASHTAKIWA 9 NA KUWATIA HATIANI 3 KATIKA KESI YA MAUAJI YA NMB MWANGA

$
0
0
Mshtakiwa namba 3, Kalisti Joseph Kanje ( aliyebeba mafaili),  Mshtakiwa namba moja, Samwel Gitau Saitoti (alifunika uso) na mwenzake  Mshtakiwa namba 2, Michael Kimani wakitoka nje ya mahakama kuu baada  ya mahakama hiyo kuwatia hatiani kwa kosa la kuua Askari polisi katika  tukio la uporaji wa benki ya NMB Mwanga
Washtakiwa namba 4 hadi 12, wakisaidiwa kupanda kwenye gari la Polisi baada ya mahakama kuu  kanda ya Moshi, mkoani Kilimanjaro, kuwaachia huru leo mchana katika kesi ya mauaji ya askari polisi yaliyotokea Julai 11 mwaka 2007.

BOFYA HAPA KWA HABARI KAMILI

Ankal atua Washington, D.C

$
0
0
Ankal akiwa na Afisa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani,Bw Suleiman Saleh wakati akimpokea katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dulles,Washington DC leo.

KATIBU MKUU WA CCM,KINANA AWASILI MKOANI KIGOMA JIONI YA LEO KWA ZIARA YA SIKU TANO

$
0
0
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kigoma Dk. Walid Kaborou akimkaribisha Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana kwenye Uwanja wa Ndege wa Kigoma pamoja na (pichan nyuma) Mjumbe wa NEC,Balozi Ali Karume walipowasili jioni ya leo kwa ziara ya siku tano mkoani Kigoma.

 Viongozi mbalimbali wa ngazi za juu za chama cha CCM Taifa na Mkoa wakiwa uwanja wa ndege mapema leo jioni ,mjini Kigoma wakimsubiri kumpokea Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akisindikizwa na Mwenyekiti wa CCM wa mkoa Dk. Kaborou wakati akipita katika paredi la UVCCM alipopokelewa Uwanja wa Ndege wa Kigoma jioni ya leo.


Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akisalimiana na Katibu wa NEC Siasa,Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye,Mkuu wa mkoa wa Kigoma,Kanali Mstaafu Issa Machibya na Kamanda wa Vijana na Mchumi wa CCM mkoa wa Kigoma,Ndugu AbdulKadir Mushi mara alipowasili jioni ya leo kwenye uwanja wa ndege wa Kigoma.

Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akisalimiana na Mkuu wa mkoa wa Kigoma,Kanali Mstaafu Issa Machibya jioni ya leo mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Kigoma.


Sehemi ya Waendesha boda boda wakiupokea msafara wa Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana mapema leo jioni,mara baada ya kuwasili mjini Kigoma.
PICHA NA MICHUZIJR-MICHUZI MEDIA GROUP-KIGOMA

UFUNGUZI WA WARSHA YA KUJENGA UELEWA WA WADAU KUHUSU MPANGO WA KUNUSURU KAYA MASKINI – TASAF AWAMU YA TATU MKOANI KATAVI

$
0
0
 Meneja Uratibu kutoka TASAF Makao Makuu Tunu Munthali (aliyesimama) akiwasilisha kwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dkt. Rajab Rutengwe (wa kwanza kulia) salaam za Mkurugenzi mtendaji wa TASAF Bw. Ladislaus Mwamanga. 

Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Dkt. Rajabu Rutengwe akihutubia washiriki wa Warsha ya kujenga uelewa wa wadau kuhusu mpango wa kunusuru Kaya maskini – TASAF awamu ya tatu Mkoani Katavi .
Hawa nao ni sehemu ya washiriki wa warsha hiyo inayoshirikisha watendaji mbalimbali wa ngazi ya Mkoa, Wilaya, Tarafa na Kata wakifuatilia kwa makini maelezo ya ufunguzi toka kwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dkt. Rajab Rutengwe (hayupo pichani)
Baadhi ya washiriki wa Warsha hiyo wakimsikiliza hotuba ya ufunguzi ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dkt. Rajab Rutengwe  (hayupo pichani)
 Picha hii na zingine zilizopo chini yake ni za picha ya pamoja ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dkt. Rajab Rutengwe (wa tatu kwa waliokaa) na makundi mbalimbali ya washiriki wa warsha  ya kujenga uelewa wa wadau kuhusu mpango wa kunusuru Kaya maskini – TASAF awamu ya tatu Mkoani Katavi, wengine waliokaa kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Mpanda Bw. Seleman Lukanga, Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Bw. Paza Mwamlima na Meneja uratibu TASAF Tunu Alice Munthali. Wengine ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mpanda Enock Gwambasa na Makamu M/Kiti Yusuf Msengi Ngassa

TBL YAFANIKISHA UPANDANJI MITI 1250 CHUO KIKUU CHA MOUNT MERU ARUSHA

$
0
0

 Mkuu wa Chuo Kikuu cha Maunt Meru, mkoani Arusha Mchungaji Profesa Harrison Olang' (kulia), akishikana mikono na Meneja Mauzo na Usambazaji wa Kampuni ya Bia Tanzania TBL), Bw. Devis Deogratius, baada ya kampuni hiyo kutoa miti 1300 kwa ajili ya mkoa wa Arusha, ambapo miti 1250 ilipandwa Chuoni hapo na miti 50 ilipandwa kwenye kiwanda cha TBL.

 Meneja Mauzo na Usambazaji wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), mkoani Arusha Bw. Devis Deogratius (aliyepiga magoti), akishiriki kupanda moja ya miti 1250 iliyotolewa na kampuni hiyo kwa ajili ya mkoa wa Arusha, baada ya kampuni hiyo kutoa miti 1300 kwa Manispaa ya Arusha, ambapo miti 1250 ilipandwa Chuoni hapo na miti 50 ilipabswa kwenye kiwanda cha TBL Arusha.
 Mkuu wa Chuo Kikuu cha Maunt Meru, mkoani Arusha Mchungaji Profesa Harrison Olang' (aliyepiga magoti kushoto), akishiki kupanda miti 1250 chuoni hapo, iliyotolewa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), kwa ajili ya Manispaa ya Arusha. Wanaoshuhudia katika picha ni baadhi ya wafakazi wa TBL na wafanyakazi wa Chuo hicho.
 Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Bi. Stella Kaaya akishiriki kupanda moja ya miti 1300 iliyopandwa katika Chuo Kikuu cha Maunt Meru, mkoani Arusha, iliyotolewa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL). 
Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Bi. Stella Kaaya (kulia) akimsikiliza kwa makini Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Maunt Meru mkoani Arusha Mchungaji Profesa Harrison Olang' (kushoto), baada ya kushiriki zoezi la kupanda miti 1300 kwenye eneo la Chuo hicho, iliyotolewa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL).

mama salma kikwete azindua chama cha umoja wa wanawake wa mbagala

$
0
0
   Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akikata utepe ikiwa ni ishara ya uzinduzi rasmi Umoja wa vikundi vya Wanawake Mbagala (UWAMBA) katika sherehe iliyofanyika kwenye ukumbi wa Dar Live
   Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akizindua nembo wakati wa  uzinduzi rasmi Umoja wa vikundi vya Wanawake Mbagala (UWAMBA) katika sherehe iliyofanyika kwenye ukumbi wa Dar Live
 Mke wa Rais na Mwenyekiti wa WAMA, Mama Salma Kikwete akimkabidhi komputa Mwenyekiti wa UWAMBA, Zenna Hanga kwa ajili ya matumizi ya ofisi ya UWAMBA mara tu baada ya kuzindua rasmi Umoja huo huko Mbagala
Mwenyekiti wa WAMA na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akisaidiana na Mama Tabu Likoko kutoka WAMA, wakimkabidhi Mwenyekiti wa UWAMBA, Mama Zenna Hanga moja ya charahani walizozitoa kwa umoja huo wakati wa sherehe za uzinduzi huko Mbagala. Picha na John Lukuwi

mkuu wa mkoa wa kagera Kanali Massawe aishukuru Vodacom kuikomboa Goziba

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Kanali Mstaafu Fabian Massawe, amezungumzia jinsi ambavyo uboreshawaji wa huduma za mawasiliano zinavyochochea kubadili maisha ya watu kupitia kuboreka kwa shughuli za kiuchumi na kijamii huku akipongeza maamuzi ya kampuni ya Vodacom ya kupelekea mawasiliano kwenye kisiwa cha Goziba kilichopo Ziwa Viktoria eneo la mkoa wa Kagera. 
Kanali Masawe, ameyasema hayo wakati alipotembelea Makao Makuu ya Kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom jijini Dar es salaam na kukutana na Ofisa Mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano wake Georgia Mutagahywa ikiwa ni sehemu ya kutoa Shukurani kwa kufanikisha kuweka mnara wa simu katika kisiwa cha Goziba pamoja na kusaidia ujenzi wa kituo cha afya kisiwani humo kupitia Vodacom Foundation. 
Amesema tangu Goziba ilipounganishwa kwenye mtandao wa simu za mkononi kumekuwepo na mabadiliko makubwa katika maisha ya wakazi wa kisiwa hicho huku ikisaidiwa kwa kiwango kikubwa suala la ulinzi na usalama na kuifungua Goziba. 
“Tunawashukuru sana Vodacom, mmekuwa wa kwanza kufikisha huduma za mawasiliano ya simu kisiwani Goziba na hivyo kuwafanya wakazi wake kuendelea kuwakumbuka kwa namna mlivyowakomboa. “Alisema Massawe. 
“Hali ya ulinzi na usalama kwenye kisiwa cha Goziba haikuwa nzuri hata kidogo, kisiwa kilikuwa kikibaliwa na wimbi kubwa la uvamizi wa majambazi waliokuwa wakiwavamia wavuvi na kuwapora fedha na mali zao ikiwemo nyavu na mashine za boti huku wakikosa msaaada wowote kwani kisiwa hakina kituo cha Polisi na hawkauwa na namna ya kuomba msaada kutoka Bukoba kutokana na kukosa huduma za mawasiliano.” 
Pamoja na kuipongeza kampuni hiyo, Kanali Masawe amesema kuwa, huduma hizo za Mawasiliano pia zimefungua fursa za kiuchumi kwa wakazi wa kisiwa hicho ambacho sasa wanawasiliana moja kwa moja na watu walioko katika maeneo mengine ya nchi na hata nje ya Nchi hususa Nchi jirani ya Kongo ambayo wanafanya nayo biashara ya kuuza dagaa. 
 Mkuu wa Mkoa wa Kagera Fabian Massawe akihojiwa na Mhina Shemweta wa kampuni ya Gin Din inayotoa huduma za ushauri wa masuala ya Mawasiliano kwa kampuni ya Vodacom Tanzania. Katikati ni Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Salum Mwalim. Kanali Massawe alifika Makao Makuu ya Vodacom jijini Dar es salaam kwa shughuli za kikazi
 Mkuu wa Mkoa wa Kagera Fabian Massawe akifurahia jambo na Mfanyakazi wa Vodacom Shomary Shomary mara baada ya kukumbushana enzi za Kanali Massawe alipokuwa Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Jitegemee wakati huo Shomary nae akiwa ni mwanafunzi shuleni hapo. Wawili hao walikutana wakati Mkuu huyo wa Mkoa alipofika Makao Makuu ya Vodacom kwa shughuli za Kikazi.Kanali Massawe ni mmoja
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Fabian Massawe (wa tatu kushoto) na Mkuu wa Wilaya ya Muleba Lembris Kipuyo (wa pili kushoto) wakiwa pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom ambao baadhi yao walifundishwa na Kanali Massawe wakati alipokuwa Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Jitegemee jijini Dar es salaam.Kanali Massawe alifika Makao Makuu ya Vodacom kwa shughuli za kikazi ambapo alivuta hisia za wafanyakazi waliowahi na hata ambao hawakuwahi kupitia mikononi mwake enzi za ualimu na hivyo kuleta hali ya furaha ikitawaliwa na utani na ukumbusho wa matuko ya Shule.

Twanga pepeta yaingia makubaliano na Proin Promotions kupambana na wezi wa kazi zao

$
0
0
BENDI ya muziki wa dansi nchini ya African Stars 'Twanga Pepeta', wameingia mkataba maalumu na kampuni ya Proin Promotions Limited kwa ajili ya utengenezaji wa kazi zao. 
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Twanga Pepeta, Asha Baraka, alisema mkataba huo una manufaa kwa bendi hiyo kutokana na kutaka kuwanufaisha wanamuziki na wasanii wa nchini kwa ujumla. 
Baraka alisema kampuni hiyo ambayo awali ilikuwa ikijishughulisha na usambazaji wa kazi za filamu, imeamua kuingia mkataba na bendi yake kutokana na ubora wao. 
Alisema wasanii nchini wanatakiwa kunufaika na kazi wanayoifanya, na Prain wameihakikishia Twanga kuwa kazi zao sasa zimetengenezwa kwa ubora wa hali ya juu kiasi cha kumshinda mtu yeyote kuirudufu. 
"Tunataka maendeleo ya wasanii, tumekuwa tukiwakumbatia zaidi wasanii wa nje, lakini muunganiko wetu sasa utasaidia kuinua hali ya kipato sahihi kwa wanamuziki tulionao," alisema Baraka. 
Kwa upande wake, Ofisa Masoko wa Prain Promotions, Evance Steven, alisema kampuni yao imeamua kuingia kwenye muziki na kuichagua Twanga Pepeta kuwa bendi ya kwanza kutokana na kazi yao wanayofanya katika burudani. 
Steven alisema kazi kubwa waliyoanza nayo katika albamu ya Twanga Pepeta ya Dunia Daraja ni kuhakikisha kuwa haiwezi kunakiliwa (kurudufiwa) upya na maharamia wa kazi za kisanii nchini kama ilivyozoeleka. 
"Tumewahakikishia wenzetu wa Twanga Pepeta kuwa kazi zao sasa ziko salama kuuzwa kihalali kutokana na kuziwekea programu maalumu ya kushindwa kunakilika, hivyo kila mtu atanunua kihalali kazi za bendi hii za Dunia Daraja," alisema ofisa huyo. 
Twanga itaanza kuuza kazi hizo katika kila maonesho yao huku zikionekana kufungwa katika ubora wa hali ya juu alipokuwa akiwaonesha waandishi wa habari utofauti mkubwa uliofanywa na Proin, ambapo pia zina stika maalumu za TRA (Mamlaka ya Mapato Tanzania).
Mkurugenzi wa ASET, Asha Baraka akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuingia makubaliano na kampuni ya Proin Promotions Ltd ya kutengeneza kazi zao kwa ubora zaidi. Kampuni hiyo tayari imetengeneza DVD ambazo huwezi kunakili kwa lengo la kupambana na wezi wa kazi za wasanii. kulia ni Meneja Masoko wa kampuni hiyo, Evans Steven na Afisa Mauzo, Kaisi Masoud.

introducing new Track : Skylighy Band ~ Kariakoo

KINANA AUNGURUMA KASULU, AKAGUA MRADI WA MAJI

$
0
0
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia maelfu ya wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika leo, Aprili 9, 2014, kwenye Kijiji cha Kurugongo, Kata ya Kurugongo, wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma. Kinana yupo katika ziara ya mkoa huo kukagua utekelezaji wa ilani ya Chama, kusikiliza kero za wananchi na kujadiliana nao njia ya kuzitatua.(Picha na Bashir Nkoromo)
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasabahi wananchi wa kijiji cha Nyumbigwa ambapo alikagua mradi wa maji.
Mbunge wa Viti Maalum Josephine Gezabuke akizungumza na wananchi  wakati waziara ya Katibu Mkuu Ndugu Abdulrahman Kinana kukagua mradi wa maji wa kijiji cha Nyumbigwa .
 Diwani wa Kata ya Nyumbigwa Benjamini Chalukula akiwa amebebwa juu na wananchi wa kata yake ikiwa ishara ya kuwatumikia vizuri wakati Katibu Mkuu wa CCM alipofanya ziara kwenye kata hiyo iliyopo wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma.
Tanki la maji la kijiji cha Nyambigwa lina uwezo wa kubeba lita 290,975 na kuwahudumia zaidi ya watu elfu 11
Viewing all 110171 articles
Browse latest View live




Latest Images