Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110025 articles
Browse latest View live

PANONE FC YA KILIMANJARO ILIVYOTANGAZWA BINGWA WA MKOA LIGI DARAJA LA TATU

$
0
0
Wachezaji wa timu ya Panone FC ya mkoani Kilimanjaro wakipasha misuli joto kabla ya mchezo wao wa kukamilisha ratiba dhidi ya waliokuwa mabingwa wa mkoa watetezi timu ya Machava Fc.
Wachezaji wa timu za Panone fc na Machava fc wakisalimiana kabla ya kuanza kwa mchezo wao wa kukamilisha ratiba.
Wachezaji wa Panone fc wakiomba dua kabla ya kuanza kwa mchezo.
Wachezaji wa timu ya Machava fc wakijadiliana jambo kabla ya kuanza kwa mchezo.
Waaamuzi wa mchezo huo tayari kwa kuanza pambano.
Benchi la ufundi lilikuwa Busy wakati wa mapumziko kuhakikisha vijana wanatoka na ushindi
Machava fc kwa upande wao pia waliweka mikakati ya ushindi.
Mgeni rasmi katika mpambano huo afisa michezo wa mkoa wa Kilimanjaro Anthony Ishumi akzungumza na timu zote mbili wakati wa mapumziko
Vijana wakambana kufa na kupona.
Hadi dakika 90 za mwamuzi Nathan zinamalizika ubao ulisomeka Panone fc 1 Machava fc 0.
Zikatolewa medali kwa wachezaji.
Wakatawazwa mabingwa wapya wa mkoa wa Kilimanjaro na kukabidhiwa kikombe cha Ubingwa.


Na Dixon Busagaga wa globu ya jamii kanda ya kaskazini.

RAIS SHEIN ATEBELEA MNARA WA MIAKA HAMSINI MICHENZAI PIA KIWANJA KARIAKOO UNGUJA

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,atembelea maendeleo ya Ujenzi wa Mnara wa Kumbu kumbu ya miaka 50 ya Mapinduzi Zanzibar unaojengwa katika viwanja wa Kisonge Michenzani Mjini Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(katikati) akipata maelezo kutoka kwa Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi ya Maji,Makaazi na Nishati Nd,Ali Halil Mirza,(wa pili kushoto) wakati alipotembelea maendeleo ya Ujenzi wa Mnara wa Kumbu kumbu ya miaka 50 ya Mapinduzi Zanzibar unaojengwa katika viwanja wa Kisonge Michenzani Mjini Unguja.
Uwanja wa mapembea wa Kariakoo Mjini Unguja ukiwa katika hatua za mwisho katika matengenezo,ambapo Rais wa wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, aliahidiwa kumalizika hivi karibuni wakati alipofanya ziara leo ya kuona maendeleo ya ujenzi huo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa ZSSF Abduwakil Haji Hafidh,(kushoto) wakati alipotoa maelezo ya ramani ya kiwanja cha Mapembea Kariakoo Mjini Unguja,alipofika kuangalia maendeleo ya ujenzi wa kiwanja hicho leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akiuliza jambo kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa ZSSF Abduwakil Haji Hafidh,(kushoto) kuhusu ujenzi wa kiwanja cha Mapembea Kariakoo Mjini Unguja,alipofika kuangalia maendeleo ya ujenzi wa kiwanja hicho leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akifuatana na Msaidizi Mwalimu Mkuu Taaluma Bimkubwa Ali Mohamed,wakati alipoitembelea Skuli ya Lumumba Mjini Unguja leo,baada ya kutoa agizo kuondoshwa Gereji ya magari waliovamia eneo la Skuli hiyo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akitoa maelekezo kwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali maalim Abdalla Mzee wakati alipoitembelea Skuli ya Lumumba Mjini Unguja leo,baada ya kutoa agizo kuondoshwa Gereji ya magari waliovamia eneo la Skuli hiyo,(kulia) Msaidizi Mwalimu Mkuu Taaluma Bimkubwa Ali Mohamed,na (kushoto) Katibu Mkuu Bi Mwanaidi Saleh.(Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.)

SEMINA YA UWEKEZAJI YA BENKI YA CRDB YAFANYIKA JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Naibu Waziri wa Fedha na Uchumi, Kigoma Malima akifungua semina ya uwekezaji ya Benki ya CRDB iliyofanyika jijini Dar es Salaam na kuwakutanisha wadau wawekezaji katika sekta ya fedha. 
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akizungumza wakati wa semina ya uwekezaji ya Benki ya CRDB iliyofanyika jijini Dar es Salaam na kuwakutanisha wadau wawekezaji katika sekta ya fedha.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB, Martin Mmari akizungumza wakati wa semina ya uwekezaji ya Benki ya CRDB iliyofanyika jijini Dar es Salaam, na kuwakutanisha wadau wawekezaji katika sekta ya fedha. 
 Baadhi ya washiriki wa semina hiyo.
 Washiriki na wadau wa semina hiyo.

BOFYA HAPA KWA PICHA NA HABARI KAMILI

TAZAMA KINANA NA ALI KARUME WALIVYOPOKELEWA SUMBAWANGA VIJIJINI

Navy SC, Abajalo, Mshikamano kuwakilisha Dar Ligi ya Mabingwa wa mikoa

$
0
0
CHAMA Cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA), kimetangaza timu tatu zilizofanikiwa kucheza Ligi ya Mabingwa wa Mikoa baada ya kufanya vizuri katika Ligi Daraja la Pili Mkoa wa Dar es Salaam iliyomalizika Jumapili iliyopita.

Ofisa Habari wa DRFA Mohamed Mharizo amesema timu hizo ni Navy SC ya  Temeke iliyokua vinara baada ya kujizolea pointi 34 ikifuatiwa na Abajalo ya Sinza iliyojikusanyia pointi 31 na Mshikamano ya Temeke iliyokua na pointi 30.

“Ligi yetu naweza kusema ilikua bora nay a ushindani kwa sababu tulianza raundi ya kwanza tukiwa na timu 32 na baadae zikabaki timu 16 ambazo katika hizo tatu ndio zimefanikiwa kuwakilisha mkoa wetu wa Dar es Salaam katika Ligi ya Mabingwa wa mikoa inayotarajia kuanza Aprili 20 mwaka huu.

“Kwa niaba ya uongozi wa DRFA, tunazipongeza timu hizi na tunaamini kwa dhati kabisa kuwa zitatuwakilisha vyema katika Ligi ya Mabingwa wa mikoa na hatimaye kufuzu kucheza Ligi Daraja la Kwanza,” alisema Mharizo.

HIVI NDIVYO HALI HALISI ILIVYO VIJIJI VYA MAGOWE NA MATETENI MJINI MOROGORO BAADA YA MAFURIKO MAKUBWA

$
0
0
Team nzima ya Tanzania Redcross wakiwa katika picha ya pamoja mjini Morogoro katika maeneo ya Magowe na Mateteni ambayo yaliyoathirika na mafuriko makubwa hadi leo hii watanzania zaidi ya 500 wanaishi kwenye mahema.
Kijana wa TRCS kutoka Mzizima Redcross branch ndugu Sute Samson Mtumbati akitoa elimu kwa wananchi juu ya kupambana na mazingira magumu wanayokutana nayo.
Hili ni tank la maji safi ambalo uhudumia watu zaidi ya mia tano (500) ambalo halimalizi masaa 3 yanakwisha na inasadikika kwa wiki huwa yanaletwa mara moja kutoka mjini,kwa mbali ni mahema ya wananchi walioathirika na mafuriko.
Muonekano wa makazi wa mji huko ukiwa na mahema ambayo wakazi hao wanaishi tangu hapo mafuriko yalipotokea.
Hili ni jiko la mabati ambalo wananchi wa mji huo huwa wanakaa hapo pindi mvua kubwa zikiharibu makazi yao yaani mahema.
Hili ni moja la tukio la kusikitisha lililotokea hivi karibuni kwa sababu zinazoweza kutatuliwa na serikali yaani kwa ukosefu wa hospitali katika maeneo hayo hadi wananchi hasa watoto wadogo upoteza maisha yao.

KAMPENI ZA LALA SALAMA ZA CCM JIMBO LA CHALINZE,ZAZIDI KUTIA FORA

$
0
0
Kaimu Katibu Mkuu wa CCM,Mwigulu Nchemba akimnadi Mgombea Ubunge katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze (CCM),Ridhiwani Jakaya Kikwete wakati wa Mkutano wa Kampeniza lala salama zilizofanyika leo April 4,2014,katika Uwanja wa Shule ya Msingi Pera,iliyopo kwenye Kata ya Pera,Chalinze.
Mgombea Ubunge katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze (CCM),Ridhiwani Jakaya Kikwete akiwahutubia wananchi wa Kata ya Pera,pamoja na kunadi sera zake leo April 4,2014.
Kaimu Katibu Mkuu wa CCM,Mwigulu Nchemba akitema cheche zake wakati wa Mkutano wa Kampeni za CCM kwenye Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze,leo April 4,2014.
Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi CCM,Nape Nnauye akiweka sawa taratibu za Mkutano wa Kampeni za CCM kwenye Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze,leo April 4,2014.

Mgombea Ubunge katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze (CCM),Ridhiwani Jakaya Kikwete akinadiwa kwa wananchi wa Chalinze na Mkewe,Arafa Kikwete.

taswira mbalimbali toka Bunge maalum la katiba mjini dodoma leo

$
0
0
Mwenyekiti wa kanuni za bunge maalum Mhe. Pandu Ameir kificho akiwasilisha mapendekezo ya kubadili kanuni leo asubuhi 
Makamu M/kiti Mhe.Samia Suluhu akiendesha kikao cha  bunge maalum leo baada ya siku nne za vikao vya kamati kumi na mbili zilizo undwa kufanya vikao vyao bila kumaliza kujadili kifungu cha kwanza na kifungu cha sita cha rasimu ya katiba mpya.
Bunge limeahirishwa hadi alhamishi wiki hii kutoa fursa kwa kamati kuendelea na vikao.
 Wabunge wakijadili mabadiliko ya kanuni leo baada ya siku nne za mijadala ndani ya kamati 12 za kujadili ibara ya kwanza na sita ya rasimu ya katiba
Mwenyekiti wa kamati namba sita Mhe.Steven Wassira akizungumza na waandishi wa habari leo kuhusu kinachoendelea kwenye kamati yake

Mjadala ukiendelea. Picha zote na Deusdedit Moshi wa Globu ya Jamii

VIJANA WA NYEGEZI MWANZA WAHAMASISHWA KUJITOKEZA KWA WINGI KATIKA SHINDANO LA KUSAKA VIPAJI VYA UIGIZAJI LIJULIKANALO KAMA TANZANIA MOVIE TALENTS LITAKALOFANYIKA KESHO JUMAMOSI ISAMILO LODGE KUANZIA SAA MOJA ASUBUHI

$
0
0
 Msanii wa Filamu Tanzania Elizabeth Michael (Lulu) akikumbatiana na Mmoja wa Mashabiki wa Filamu zake katika Eneo la Nyegezi Mwanza Jioni ya Leo wakati wasanii wa filamu Tanzania walipotembelea eneo hilo kwa lengo la kutambulisha Shindano la Kusaka Vipaji vya Uigizaji Tanzania lijulikanalo kama Tanzania Movie Talents litakaloanza kesho Mkoani Mwanza, Mahali ni Isamilo Lodge
Baadhi ya Wakazi wa Nyegezi Mwanza wakiwa wamekusanyika kwaajili ya kuwashuhudia wasanii wa filamu Tanzania waliofika katika Viwanja hivyo vya Stendi ya Nyegezi kwaajili ya Kutambulisha Shindano la Kusaka Vipaji vya Kuigiza Tanzania litakaloanzia Jijini Mwanza.
 Kijana Mmoja wa Kike ambaye jina lake halikuweza kupatikana haraka akionyesha jinsi ya kushtua Kijoti joti wakati wasanii wa filamu Tanzania Walipofika katika Viwanja vya Stendi ya Nyegezi jioni ya leo
 Msanii wa Vichekesho Joti akimchagua mmoja wa wakazi wa Nyegezi Mwanza kwaajili ya Kupewa zawadi kutoka kwake
 Lulu akiongea na wakazi wa Nyegezi Mwanza wakati walipotembelea Viwanja vya Stendi ya Nyegezi jioni ya Leo
 Baadhi ya wakazi wa Nyegezi wakinyoosha vidole kwaajili ya kuchaguliwa kujibu swali ambapo mshindi alijishindia Zawadi ya Kopi moja wapo ya Filamu ya Msanii Lulu
 Lulu akimkabidhi Zawadi ya Filamu yake ya Foolish Age kijana ambae alipatia kumtaja jina lake halisi wakati wasanii hao walipotembelea viwanja vya Nyegezi Mwanza 
 Picha ya Pamoja na Mshindi wa zawadi ya Filamu
 Msanii Rich Rich akiongea na wakazi wa Nyegezi Jioni ya Leo
 Msanii wa Filamu Tanzania Steve Nyerere ambe pia ni Mwenyekiti wa Bongo Movie akiongea na wakazi wa Nyegezi Jioni ya leo wakati wasanii walipotembelea viwanja vya stendi ya nyegezi kwaajili ya Kutambulisha na kuwahamasisha vijana na wazee kujitokeza kwa wingi kwaajili ya kuonyesha Vipaji vyao Vya kuigiza katika Shindano la Kuigiza lijulikanalo kama Tanzania Movie Talents ambalo linaanza rasmi Kesho jijini Mwanza mahali ni Isamilo Lodge
Wakazi wa Nyegezi Mwanza wakichungulia kwenye gari walilopanda wasanii wa kuigiza Tanzania ambao walifika katika Viwanja vya Stendi ya Nyegezi kwaajili ya kuhamasisha vijana kwa wazee kuweza kujitokeza kwa wingi Hapo Kesho katika Shindano la Kusaka Vipaji vya Kuigiza Tanzania lijulikanalo kama Tanzania Movie Talents ambalo litafanyika Isamilo Lodge kuanzia Saa Moja asubuhi na Hakuna Kiingilio.Picha na Josephat Lukaza wa Lukaza Blog

TSN BOYS KUKABILI MWANANCHI MEDIA KOMBE LA NSSF KESHO: MROKI AIAHIDI DAU NONO

$
0
0

Kikosi cha TSN Boys

TIMU ya soka ya Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) inashuka dimba la Sigara, Chang’ombe, Dar es Salaam kuikabili Mwananchi katika Kombe la NSSF kwa Vyombo vya Habari 2014.

Mechi hiyo itakayochezwa saa 2 asubuhi, itakuwa muhimu kwa timu zote mbili kwani mshindi atasonga mbele katika hatua ya robo fainali zitakazoanza Jumatatu ijayo.
TSN imetinga hatua hiyo baada ya kupewa ushindi kutokana na wapinzani wao, Mlimani Media kuwatumia wachezaji ambao hawakuwa halali. Mlimani Media ilikuwa imeshinda kwa mabao 9-0.
Mwananchi ni mechi yake ya kwanza. Mbali ya mechi hiyo, mechi nyingine kesho ni kati ya Tumaini dhidi ya Sahara Media, wakati upande wa netiboli, itakuwa ni mechi za robo fainali kati ya Business Times dhidi ya Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), wenyeji NSSF dhidi ya Tumaini Media.

TSN Boys wapo katika hamasa na ari kubwa ya mchezo huo wa kesho ambapo Meneja wa Timu hiyo, Mroki Mroki "Father Kidevu"  ameahidi kuzawadia mfungaji wa kila goli kitita cha shilingi 5,000. 


"Niliahidi katika mchezo wa awali na hata sasa bado ahadi yangu ipo pale pale kwa kila goli nitalilipia shilingi 5,000 nahiyo haina longolongo lengo ni kuhamasisha ushindi kwa timu yetu," alisema Mroki.


Aidha Mroki amesema atakuwepo uwanjani kuhakikisha ushindi unapatikana kwa vijana wa TSN Boys na kusonga mbele katika mashindano hayo. 

Katika mechi za jana, mabingwa watetezi wa soka, Jambo Leo walitolewa baada ya kufungwa mabao 2-1 na Free Media kwa mabao ya Saleh Mohammed.
Bao la Jambo Leo lilifungwa na Zahoro Mlanzi. Aidha, Changomoto ilisonga mbele baada ya kuilaza New Habari kwa penalti 7-6, baada ya sare ya bao 1-1. Free Media na New Habari zilisonga mbele kama timu bora mbili zilizoshindwa, lakini zikiwa na matokeo mazuri (best looser).

Katika netiboli, Mlimani Media ilishindwa kutamba kwa Habari Zanzibar kwa kufungwa mabao 19-15, wakati IPP iliizamisha Global Publishers kwa
mabao 27-8.

JK AOMBOLEZA KIFO CHA BABA MZAZI WA ASKOFU METHODIUS KILAINI

IBADA YA KUUOMBEA MWILI WA ASKOFU WA KANISA LA ANGLICAN DAYOYSISI YA KATI GODFREY MHOGOLO

$
0
0
 Jeneza likiwa na  mwili wa aliyekuwa Askofu wa kanisa la Anglican Dayosisi ya Dodoma Godfrey Mdimi Mhogolo aliyefariki wiki iliyopita nchini Afrika yaKusini alikopelekwa kwa matibabu likiwa ndani ya kanisa kuu la Roho Mtakatifu wakati wa ibada maarumu.
Waumini na viongozi wa kanisa la Anglican Dayosisi ya kati wakilishusha Jeneza lilibeba mwili wa aliyekuwa askofu wa kanisa hilo Godfrey Mhogolo ulipofikishwa kwa mara ya kwanza tokea alipofariki nchini Afrika ya Kusinikanisani hapo kwa ajili ya kufanyiwa ibada ya maombezi.
Wachungaji na makasisi wa Kaanisa la Anglican Dayosisi ya Kati wakiwa wamejipanga nje ya kanisa la Roho mtakatifu mjini Dodoma kwa ajili ya kuupokea mwili aliyekuwa Askofu wa kanisa hilo Godfrey Mhogolo

MHE. RAIS TEODORO NGUEMA MBASONGO AZUNGUMZA NA KAMATI YA MABALOZI WA NCHI ZA AFRIKA, KARIBIANI NA PASIFIKI (ACP)

$
0
0
 Mhe. Rais Teodoro Nguema Mbasongo (katikati)  wa Guinea ya Ikweta  akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Kamati ya Mabalozi wa ACP baada ya kuzungumza na Kamati ya Mabalozi. Mhe Rais Mbasongo amesisitiza umuhimu wa nchi za ACP kushirikiana kujenga uchumi na kufanya biashara. 
Akimkaribisha Rais huyo kuzungumza na Kamati ya Mabalozi wa ACP  Balozi wa Tanzania Ubelgiji na Mwenyekiti kamati Balozi Dr. Diodorus Kamala  (wa pili kulia) amesema nchi za ACP zinapaswa kuhakikisha  Mikataba ya Ubia wa Kibiashara (EPAs) kati ya Jumuiya ya Ulaya na ACP  inakuwa mikataba itakayosaidia  nchi za ACP kuimarisha mtangamano wa nchi za ACP, kuhahakisha mapinduzi ya viwanda yanapatikana na kuwezesha nchi za ACP zinapambana na nguvu za utandawazi.

JAJI AUGUSTINEO RAMADHANI AWATAKA WAJUMBE KUJADILI RASIMU KWA MAKINI

$
0
0
Makamu mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Mstaafu Augustino Ramadhani akiongea jijini Dar es Salaam jana Aprili 3, 2014 katika wa mjadala kuhusiana na umuhimu wa Tanzania kuwa na katiba mpya ya kipekee, Mjadala ulioandaliwa na asasi isiyo ya kiserikali ya The  Open Society Initiative  For  Eastern African Tanzania  (OSIEA). Kulia kwake ni Mwenyekiti wa Mjadala huo, Profesa Chris Maina, pamoja na Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dkt. Ayoub Rioba.
Kamishana wa zamani wa Tume ya Uchaguzi  ya Zanzibar - ZEC, Dkt. Nassor Seif Amour akitoa ufafanuzi  jijini Dar es Salaam jana Aprili 3, 2014 katika wa mjadala kuhusiana na umuhimu wa Tanzania kuwa na katiba mpya ya kipekee, Mjadala ulioandaliwa na asasi isiyo ya kiserikali ya The  Open Society Initiative  For  Eastern African Tanzania  (OSIEA).  Pembeni ni Makamu mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Mstaafu Augustino Ramadhani na Mwenyekiti wa Mjadala huo, Profesa Chris Maina.
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dkt. Ayoub Rioba akitoa maelezo jinsi vyombo vya habari vinavyoshiriki katika mchakato wa kupata katiba mpya, wakati wa mjadala kuhusiana na umuhimu wa Tanzania kuwa na katiba mpya ya kipekee, Mjadala ulioandaliwa na asasi isiyo ya kiserikali ya The  Open Society Initiative  For  Eastern African Tanzania  (OSIEA).
Washiriki walioshiriki katika mjadala kuhusiana na umuhimu wa Tanzania kuwa na katiba mpya ya kipekee, Mjadala ulioandaliwa na asasi isiyo ya kiserikali ya The  Open Society Initiative  For  Eastern African Tanzania  (OSIEA).

Washiriki walioshiriki katika mjadala kuhusiana na umuhimu wa Tanzania kuwa na katiba mpya ya kipekee, Mjadala ulioandaliwa na asasi isiyo ya kiserikali ya The  Open Society Initiative  For  Eastern African Tanzania  (OSIEA).
Washiriki katika mjadala kuhusiana na umuhimu wa Tanzania kuwa na katiba mpya ya kipekee, Mjadala ulioandaliwa na asasi isiyo ya kiserikali ya The  Open Society Initiative  For  Eastern African Tanzania  (OSIEA).
Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHWashiriki walioshiriki katika mjadala kuhusiana na umuhimu wa Tanzania kuwa na katiba mpya ya kipekee, Mjadala ulioandaliwa na asasi isiyo ya kiserikali ya The  Open Society Initiative  For  Eastern African Tanzania  (OSIEA).
Wadau wakitoa michango yao katika mjadala huo.
Wadau wakitoa michango yao katika mjadala huo. Huyu hapa ni Jiang Alipo akitoa mchango wake
Katibu Mkuu wa Chadema, Dr Wilbroad Slaa akiuliza swali mara baada ya majadiliano.
Katibu Mkuu wa Chadema, Dr Wilbroad Slaa akijadili jambo na Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Dk. Hellen Kijo-Bisimba (kushoto) na Mwenyekiti wa Mjadala huo, Profesa Chris Maina (kati). Picha zote na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog. ---
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam.
Aliyekuwa makamu mwenyekiti wa tume ya mabadiliko ya katiba Jaji Mstaafu Augustino Ramadhani amewataka wajumbe wa bunge maalumu la katiba kujadili vipengele vya rasimu hiyo kwa kuviboresha badala ya kulumbana.
Jaji Ramadhani ametoa kauli hiyo Jijini Dar es salaam wakati wa mjadala kuhusiana na umuhimu wa Tanzania kuwa na katiba mpya ya kipekee, Mjadala ulioandaliwa na asasi isiyo ya kiserikali ya OSIEA.
Amesema kuwa, tume ya mabadiliko ya katiba imefanyakazi yake ya kuwasikiliza wananchi na kuandika rasimu ambayo ipo mbele ya wajumbe hao, na hivyo kutoa wito kwao kujadili kwa makuni ili kutengeneza mustakabali mzuri wa Tanzania kwa kuzingatia hoja na kila upande wa Muungano. 
“Sisi kama tume tumefanya kwa kadiri ya uwezo wetu na tumepata rasimu ya pili, sasa ni jukumu la wajumbe wa bunge la katiba kujadili na kuboresha vipengele vilivyomo kwenye rasimu hiyo na kuachana na malumbano”. Alisema Jaji Ramadhani.
“kila mmoja akitaka kipengele chake kiwemo kwenye rasimu hiyo, ni jambo lisilowezekana, kinachotakiwa hapa ni wajumbe kujadili na kupendekeza mambo yenye maslahi kwa taifa kwa sasa na baadae”. Alisisitiza Jaji Ramadhani
Jaji Ramadhni amesema, vipengele vinavyobishaniwa vinajadilika na vinaweza kuboreshwa zaidi kwa malahi ya pande zote mbili ili kupata katiba yenye kutoa nafasi kwa kila upande wa Muungano katika kushiriki katika ujenzi wa taifa.
“Vipengele vinavyoshindaniwa vinafaamika na wajumbe wanaweza kutumia busara kuvijadili na kuvitolea maamuzi kwa manufaa ya nchi ambayo inasubiri kwa hamu Katiba Mpya” alisema Jaji Ramadhani.
Akiongelea nafasi ya vyombo vya habari kwenye mchakto huo Muhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam Dr Ayoub Rioba amesema, bado vyombo vya habari havijapewa nafasi ya kutosha kisheria kushiriki katika kuelimisha umma kuhusiana na mchakato huo.
“ Vyombo vya habari bado havijapewa nafasi yoyote kwenye mchakato huu bali vinafanya kazi kwa mazoea na pia kuna vipingamizi vingi vinawekwa kuwazuia waandishi wa habri kuandika habari za bunge la katiba” alisema Dr Rioba.
Kamishana wa zamani wa tume ya uchaguzi ya Zanzibar –ZEC, Dr Nassor Seif Amour amwataka wajumbe wa Bunge la katiba kuzingatia matakwa ya wananchi badala ya kujadili maoni yao binafsi ama matakwa ya vyama wanavyoviwakilisha.
“Sisi tunawakumbusha wajumbe wa bunge maalumu la katiba kukumbuka maoni wanayoyajidili kuwa ni ya wananchi sasa wasiweke maoni yao ama ya chama katika mchakato huu ili wasitunge rasimu mpya badala ya kuiboresha”. Alisema Dr. Nassor.
Mjadala huo umehudhuriwa na wawakilishi kutoka makundi mbalimbali ya wananchi, asasi za kiraia na wanasiasa.

JAPAN YATOA MSAADA WA MAGARI KWA JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI

$
0
0
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima (kulia) akipokea ufunguo ikiwa ishara ya kukabidhiwa magari matano kutoka kwa Balozi wa Japan nchini, Masaki Okada wakati wa tafrija fupi ya makabidhiano ya magari hayo kutoka Serikali ya Japan kwa ajili ya kusaidia Jeshi la Zimamoto na Uokoaji katika majukumu yake ya kuzima moto na uokoaji nchini. Makabidhiano hayo yalifanyika katika viwanja vya Kituo cha Zimamoto Kanda ya Ilala, jijini Dar es Salaam leo. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima (kulia) na Balozi wa Japan nchini, Masaki Okada wakikata utepe ikiwa ishara ya makabidhiano ya magari matano yaliyotolewa na Serikali ya Japan kwa ajili ya kusaidia Jeshi la Zimamoto na Uokoaji nchini. Magari hayo yamekabidhiwa katika viwanja vya Kituo cha Zimamoto Kanda ya Ilala, jijini Dar es Salaam.  Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima akiikagua  moja ya magari matano yaliyotolewa na Serikali ya Japan kwa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji. Magari hayo matano yalitolewa na Balozi wa Japan nchini, Masaki Okada wakati wa tafrija fupi ya makabidhiano ya magari hayo yaliyofanyika katika viwanja vya Kituo cha Zimamoto Kanda ya Ilala, jijini Dar es Salaam. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima akitoa hotuba fupi ya kuishukuru Serikali ya Japan kwa kuisadia wizara yake kupitia Jeshi la Zimamoto na Uokoaji magari matano kwa ajili ya kazi ya kuzima moto na uokoaji nchini. Kushoto ni Balozi wa Japan nchini, Masaki Okada ambaye alikabidhi magari hayo kwa niaba ya Serikali yake. Kulia ni Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Kamishna Jenerali Pius Makuru Nyambacha. makabidhiano ya magari hayo yaliyofanyika katika viwanja vya Kituo cha Zimamoto Kanda ya Ilala, jijini Dar es Salaam leo. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

 Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Kamishna Jenerali Pius Makuru Nyambacha akitoa hotuba fupi ya kumkaribisha mgeni rasmi ambaye ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima (katikati) ili aweze kuzungumza na baadaye kukabidhiwa magari matano ya kuzima motona uokoaji. Magari hayo yametolewa na Serikali ya Japan kupitia balozi wake nchini, Masaki Okada (kushoto) katika viwanja vya Kituo cha Zimamoto Kanda ya
 
Taswira ya magari matano yaliyokabidhiwa na Balozi wa Japan, Masaki Okada kwa niaba ya Serikali yake. Magari hayo matano yaliyotolewa kwa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji yalipokelewa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima katika viwanja vya Kituo cha Zimamoto Kanda ya Ilala, jijini Dar es Salaam. Picha zote na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. PICHA ZOTE NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI WIZARA YA MAMBO YA NDANI 

ankal uso kwa uso na wazee wa kazi jijini london leo

$
0
0
 Wazee wa kazi wa Serengeti Freight Forwarders  ya jijini London Kaka Muhsin (kushoto) na Kaka Chris  wakiwa wametulia tuli kabla ya kumpa ofa ya bonge la lunch ya usiku huu Ankal katika hoteli ya Hyatt Regency Churchill, London.
Ankal akila selfie na Wazee wa Kazi Kaka Muhsin (kushoto) na Chris ambao pia walitumia nafasi hiyo kusherehekea kuhamisha ofisi yao ya Serengeti Freight Forwarders. Wao wanakuwa wamatumbi wa kwanza kuwa na ofisi sehemu za  Tilbury Port. Soma maelezo hapo chini:

WE ARE MOVING OUR OFFICES TO TILBURY PORT, OPPOSITE BERTH 31 (BESIDE HYUNDAI)  PLEASE IF YOU HAVE ANY ITEMS AT OUR CURRENT ADDRESS COME AND COLLECT AS WE WILL NOT TAKE ANYTHING WITH US.
WE NOW SELL EMPTY CONTAINERS 40'HC £1,500 
SERENGETI FREIGHT FORWARDERS LTD
UNIT 92 THAMES INDUSTRIAL PARK, PRINCESS MARGARET ROAD,
EAST TILBURY, ESSEX, RM18 8RH
MOBILE  CHRIS(+44)07903828119  

maandalizi ya sherehe za miaka 50 ya muungano zitazofanyika Dubai april 14, 2014

$
0
0
Mhe. Omar Mjenga (shati la Mandela katikati), Balozi Mdogo wa Ubalozi Mdogo wa Tanzania uliopo Dubai, akiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa jumuiya ya watanzania waishio UAE. 
Kikao hicho kilichohudhuriwa kwa wingi na vijana wa Jumuiya kilijadili hatua za mwisho za maandalizi ya sherehe ya maadhimisho ya miaka 50 ya Muungano zitakazofanyika Le Meridien Hotel, Dubai. 
Mzee Ali Hassan Mwinyi, Rais Mstaafu na Mtukufu Ahmed Bin Saeed Al Maktoum, Rais wa Shirika la Ndege la Emirates na Mkuu wa Idara ya Anga ya Dubai, watakuwa wageni rasmi. Sherehe hizo zitafanyika tarehe Aprili 14, mwaka huu.

JK arejea nyumbani baada ya ziara ya Uingereza na Ubelgiji

$
0
0
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiongozana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Saidi Meck Sadiki baada ya kuwasili leo April 4, 2014 katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere akitokea Brussels, Ubelgiji, alikofanya ziara ya kikazi ya siku mbili na kuhudhuria mkutano wa mataifa ya Afrika na nchi za Jumuiya ya Ulaya. Kabla ya hapo Rais Kikwete alifanya zaiara ya kiserikali ya siku tatu nchini Uingereza kwa mwaliko wa Waziri Mkuu wa nchi hiyo Mhe David Camaron. PICHA NA IKULU

ngoma azipendazo ankal

$
0
0
Jipatie ngoma kibao za Mbaraka Mwinshehe Mwaruka (RIP) na Morogoro Jazz

MABONDIA ALIBABA NA ROY MBUNDA WAFANYIWA VIPIMO SASA KUPAMBANA JIONI YA LEO YMCA MOSHI

$
0
0
Bondia Roy Mbunda wa Ruvuma akifanyiwa vipimo na Dk Issa ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya pambano litakalo fanyika jioni ya leo katika ukumbi wa YMCA mjini Moshi.
Bondia Alibaba Ramadhani wa Kilimanjaro akifanyiwa vipimo na Dk Issa ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya pambano litakalo fanyika jioni ya leo katika ukumbi wa YMCA mjini Moshi.
Mwenyekiti wa chama cha ngumi mkoa wa Kilimanjaro Eliakunda Kipoko akizungumza na mabondia (hawapo pichani)mara baada ya kufanyiwa vipimo.
Bondia Alibaba Ramadhan(shoto) na Roy Mbunda(kulia)wakiwa na promota Andrew George mara baada ya kufanyiwa vipimo.
Bondia Alibaba Ramadhan(shoto) na Roy Mbunda(kulia)wakiwa na mwenyekiti wa chama cha ngumi mkoa wa Kilimanjaro (KBA)Eliakunda Kipoko(mwenye suti) pamoja na promota Andrew George mara baada ya kufanyiwa vipimo mabondia.
Mabondia wakiwa na Dokta Issa mara baada ya kumaliza kuwafanyia vipimo.
Mabondia wakiwa na viongozi wa chama cha ngumi mkoa wa Kilimanjaro (KBA) ,Eliakunda Kipoko(Mwenyekiti) na Shambe Sagafu (katibu) Picha na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii, kanda ya kaskazini,



Viewing all 110025 articles
Browse latest View live




Latest Images