Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110113 articles
Browse latest View live

WAZIRI CHIKAWE AIWAKILISHA TANZANIA MKUTANO WA MAWAZIRI, NCHINI AFRIKA KUSINI

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (kushoto) akiwa na Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini (CGP), John Minja (kulia) katika Mkutano wa Mawaziri wenye dhamana na Taasisi za Urekebishaji. Mkutano huo ulioudhuriwa na mawaziri kutoka nchi mbalimbali barani Afrika unafanyika jijini Pretoria, nchini Afrika Kusini. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.


MVUA YAHARIBU SEHEMU YA BARABARA KATIKA HIFADHI YA TAIFA YA SERENGETI

$
0
0
Lori la kubeba kifusi kwa ajili ya ukarabati wa barabara iliyopo katika hifadhi ya serengeti likiwa limekwama baada ya kunasa kwenye tope na kufunga barabara kwa muda.
Magari yaliyokuwa na watalii yalilazimika kuchepuka na kuendelea na safari.
Zikafanyika jitihada za kulinasua hilo gari kutoka katika eneo hilo .
Barabara iko kwenye matengenezo.
Hatimaye gari lilifanikiwa kutoka sehemu lilipokuwa limenasa.
Safari ikaendelea kwa watumiaji wa mabasi yaendayo Musoma na Arusha.Picha na Dixon Busagaga wa globu ya jamii kanda ya kaskazini.

President Kikwete in Bilateral Talks with President of the European Commission Barroso

$
0
0
President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete meets the President of the European Commission Jose Manuel Barroso at his Office in Brussels Belgium this morning. President Kikwete was in Brussels where he attended the 4th EU Africa Summit under the theme, ”Investing in People, prosperity and peace”.(photo by Freddy Maro).

MAAFISA TUME WAFUNZWA STADI ZA UCHUNGUZI

$
0
0
Mkurugenzi wa Idara ya Haki za Binadamu, Bwana Francis Nzuki akifungua rasmi mafunzo ya stadi za uchunguzi yanayofanyika katika hoteli ya Naura Spring jijini Arusha. Mafunzo hayo ya wiki moja kuanzia Machi 31—4, 2014 yamelenga kuwaongezea maafisa wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) stadi za kiuchunguzi hasa wanapofanya uchunguzi unaohusiana na kazi za kila siku za Polisi. kushoto ni muwezeshaji kutoka Tume ya Haki za Binadamu ya Afrika Kusini Bibi. Lindiwe Khumalo na kulia ni Muwezeshaji Mkuu wa mafunzo hayo Bwana Sean Tait kutoka African Policing Civilian Oversight Forum (APCOF).Mafunzo hayo yamefadhiliwa na shirika la GIZ.
Sehemu ya washiriki wakiwa katika Mafunzo, wa kwanza kushoto ni Afisa Uchunguzi wa THBUB, Bwana Godian Binamungu na kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Msaada wa Sheria, Bwana Nabor Assey na anayeonekana kwa mbali ni Afisa Uchunguzi , Bi. Nancy Ngula.
Maafisa wa THBUB wakimsikiliza kwa makini Muwezeshaji Mkuu, Bwana Sean Tait (hayupo pichani).Kutoka kushoto ni Bibi Monica Marealle (katikati) ni Bwana Elias Sowani na (kulia) ni Bwana Pontian Kitorobombo.
Muwezeshaji Mkuu, Bwana Sean Tait akiongea na Maafisa wa THBUB wanaoshiriki mafunzo(hawapo pichani) na kuwataka kuwa wasikivu ili kwa pamoja waweze kupata faida kutokana na mafunzo hayo.Kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Haki za Binadamu, Bwana Francis Nzuki.

TFDA YATOA MATOKEO YA UKAGUZI MAALUM WA MADUKA YA BIDHAA ZA VYAKULA JIJINI DAR, YAWATAKA WANANCHI KUJENGA UTARATIBU WA KUSOMA MAELEZO YA BIDHAA KABLA YA KUNUNUA

$
0
0
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa(TFDA) Bw.Hiiti Sillo akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kuhusu ukaguzi maalum wa maduka ya kuuzia vyakula “Supermarkets” na Mini-Supermarkets katika jiji la Dar es salaam kinyume cha sheria ya Chakula , Dawa na Vipodozi sura ya 219.
Mkurugenzi wa Usalama na Chakula wa TFDA Bw. Raymond Wigenge akitoa ufafanuzi kwa waandishi kuhusu hatua zinazochukuliwa na TFDA kuhakikisha usalama wa vyakula na Dawa nchini .TFDA imekuwa ikiongeza nguvu katika kukabiliana na bidhaa zisizokidhi viwango kwa kushirikiana na mamlaka nyingine za udhibiti kwa kukagua, kukamata na kuchukua hatua za kisheria ikiwemo kuwafikisha mahakamani wanaokiuka sheria.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa(TFDA) Bw.Hiiti Sillo (kulia) akitoa ufafanuzi wa baadhi ya bidhaa zilizokamatwa katika ukaguzi maalum kwenye maduka ya kuuzia vyakula “Supermarkets” na Mini-Supermarkets katika jiji la Dar es salaam zikiuzwa kinyume cha sheria ya Chakula , Dawa na Vipodozi sura ya 219. Wengine ni Mkurugenzi wa Usalama na Chakula wa TFDA Bw. Raymond Wigenge, na Meneja wa Ukaguzi wa Chakula wa TFDA kanda ya Mashariki Bw. Emmanuel Alphonce.
Afisa Uhusiano wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) akiwaonesha waandishi wa habari baadhi ya bidhaa zilizokamatwa na mamlaka hiyo zikiwemo chumvi, vinywaji, maziwa ya watoto ambazo hazijasajiliwa na mamlaka hiyo kufuatia ukaguzi maalum uliofanyika katika jiji la Dar es salaam.
Maziwa ya watoto aina ya SMA 1,2 na 3, Promil Gold, S-26 Gold, Nursoy, Progress Gold, Cow &Gate, Isomil 2 na Infacare Soya , Nutrikids na Aptimil 1 yaliyokamatwa ambayo hayajasajiliwa na TFDA .
Vinywaji baridi ambavyo havikusajiliwa na TFDA vilivyokamatwa kufuatia ukaguzi maalum katika jiji la Dar es salaam.Picha na Aron Msigwa.

WAJUMBE WA KAMATI MBALI MBALI ZA BUNGE WAENDELEA NA VIKAO MJINI DODOMA

$
0
0
Mjumbe wa Kamati namba kumi na mbili ya Bunge Maalum la Katiba Goodluck Ole - Medeye akichangia jana mjini Dodoma wakati wa ziara ya Mwenyekiti wa Bunge hilo, Samuel Sitta alipoitembelea Kamati hiyo kujionea kazi inayoendelea ya uchambuzi wa sura ya kwanza na Sita katika Rasimu ya Katiba mpya.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati namba nne ya Bunge Maalum la Katiba, DKT Sira Ubwa Mamboya(kushoto) akifafanua jambo kwa Mwenyekiti wa Bunge hilo, Samuel Sitta(kulia) alipoitembelea Kamati hiyo jana mjini Dodoma kujionea kazi inayoendelea ya uchambuzi wa sura ya kwanza na Sita katika Rasimu ya Katiba mpya. Mwingine ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo Christopher Ole Sendeka(katikati).
Mjumbe wa Kamati namba nne ya Bunge Maalum la Katiba, Dkt. Terezya Huvisa akiuliza swali wakati Mwenyekiti wa Bunge hilo, Samuel Sitta(hayupo pichani) alipoitembelea Kamati hiyo jana mjini Dodoma kwa ajili kujionea kazi ya uchambuzi wa sura ya kwanza na Sita katika Rasimu ya Katiba mpya.
Mjumbe wa Kamati namba nne ya Bunge Maalum la Katiba, Mchungaji Christopher Mtikila akiuliza swali wakati Mwenyekiti wa Bunge hilo, Samuel Sitta(hayupo pichani) alipoitembelea Kamati hiyo jana mjini Dodoma kwa ajili kujionea kazi ya uchambuzi wa sura ya kwanza na Sita katika Rasimu ya Katiba mpya. PICHA NA KAMATI YA BUNGE MAALUM LA KATIBA(BMK)

RIDHIWANI KIKWETE AUNGURUMA KATA YA BWILINGU NDANI YA JIMBO LA CHALINZE LEO

$
0
0
 Meneja wa Kampeni wa CCM katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze,Steven Kazidi (kushoto) akiwahutubia wananchi wa Kijiji cha Mbala,Kata ya Bwilingu wakati wa kumnadi Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM kwenye Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete.
 Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM kwenye Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete akiwahutubia wananchi wa Kijiji cha Mbala,Kata ya Bwilingu wakati wa Mkutano wa Kameni za CCM.
 Diwani wa Kata ya Bwilingu,Nassar Ahmed Karama akiongea kwa kusisitiza wakati akiwasilisha taarifa ya Kata yake kwa Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM kwenye Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete ,kwenye Mkutano wa Kampeni za CCM zilizofanyika leo April 2,2014.
 Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM,Khadija Aboud akiwasalimia wakazi wa Kijiji cha Mbala,Kata ya Bwilingu wakati wa Mkutano wa Kameni na kumnadi Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM kwenye Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete.

Rais wa Zanzibar Dk Ali Shein Atembelea Mnara wa Kumbukumbu ya miaka 50 ya Mapinduzi Zanzibar Michezani na Uwanja wa mabembea wa Kariakoo Mjini Unguja

$
0
0
 Uwanja wa mabembea wa Kariakoo Mjini Unguja ukiwa katika hatua za mwisho katika matengenezo,ambapo Rais wa wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, aliahidiwa kumalizika hivi karibuni wakati alipofanya ziara leo ya kuona maendeleo ya ujenzi huo.
 
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,atembelea maendeleo ya Ujenzi wa Mnara wa Kumbukumbu ya miaka 50 ya Mapinduzi Zanzibar unaojengwa katika viwanja wa Kisonge Michenzani Mjini Unguja

TIMU YA KUSAKA VIPAJI VYA UIGIZAJI TANZANIA YAWASILI SALAMA MKOANI MWANZA, ZOEZI KUANZA JUMAMOSI

$
0
0
Mabasi yaliyokuwa yamebeba timu nzima ya Proin Promotions Limited yakiwa yamewasili Mkoani Mwanza Usiku huu.
Baadhi ya Timu ya Wafanyakazi Kutoka Kampuni ya Proin Promotions Limited ambao ndio waendeshaji na wasimamiaji wa Mashindano ya Kusaka Vipaji vya uigizaji Tanzania yajulikanayo kama Tanzania Movie Talents wakiwa wanashuka katika Moja ya Basi lililokuwa limebeba wafanyakazi na timu nzima ya Proin Promotions Limited mara baada ya kuwasili mkoani Mwanza Usiku huu.
Timu nzima ya Proin Promotions Limited imewasili salama usiku huu katika Jiji la Mwanza ikitokea Mkoani Dar Es Salaam, tayari kwa kuanza zoezi la Kusaka vipaji vya uigizaji Tanzania, Zoezi hilo limeanzia Kanda ya Ziwa katika Mkoa wa Mwanza ambapo mashindano hayo yataanza tarehe 5 aprili.
Mashindano haya yatafanyika Mkoani Mwanza kwa siku Tatu kuanzia tarehe 5 hadi 9 mshindi wa kwanza atakayepatikana atajinyakulia kitita cha Shilingi laki tano.
Tunaomba Vijana na wakazi wa Jiji la Mwanza na Vitongoji vyake waweze kujitokeza kwaajili ya kuonyesha vipaji vyao ili kuweza kuendelea ujuzi na vipaji vyao vya kuigiza Tanzania na kukuza tasnia ya filamu Nchini.

TBL YAKABIDHI KISIMA CHA MAJI ZAHANATI YA MVUTI DAR

$
0
0
 Mkuu wa Mahusiano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Bw. Stephen Kilindo (kulia) na Afisa Uhusiano wa Kampuni hiyo, Bi. Doris Malulu, wakimuongoza Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Elias Kwesi (wa pili kushoto), kwenda kuzindua rasmi mradi wa maji katika Zahanati ya Mvuti, Kata ya Msongola, Wilayani Ilala, Dar es Salaam jana, uliojengwa na TBL. (Na Mpigapicha Wetu)
 Kwesi (mwenye suti), akimshika mkono wa pongezi Afisa Uhusiano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Bi. Doris Malulu (wa pili kulia), wakati wakielekea kuzindua mradi wa maji katika zahanati ya Mvuti, iliyoko Kata ya Msongola, Manispaa ya Ilala, Dar es Salaam jana, ulichojengwa na TBL. Kulia ni Mkuu wa mahusiano na sheria wa Kampuni hiyo, Bw. Stephen Kilindo.
 Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Elias Kwesi (mwenye suti), akikata utepe kuzindua rasmi mradi wa maji katika Zahanati ya Mvuti, Kata ya Msongola, Wilayani Ilala, Dar es Salaam jana, uliojengwa na Kampuni Bia Tanzania (TBL). Wa pili kulia ni Mkuu wa mahusiano na sheria wa Kampuni hiyo, Bw. Stephen Kilindo, Diwani wa Kata hiyo, Bi. Angelina Malembeka na Ofisa Mauzo wa TBL Ilala, Bw. Godrack Kalebi. (Na Mpigapicha Wetu)

Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Elias Kwesi (mwenye suti kulia), akiondoa kitambaa kuzindua mradi wa maji katika Zahanati ya Mvuti, Kata ya Msongola, Manispaa ya Ilala, Dar es Salaam jana, uliojengwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), anayemsaidia ni Ofisa Mauzo wa TBL Ilala, Bw. Godrack Kalebi. Wanaoshudia ni Mkuu wa Mahusiano wa TBL, Bw. Stephen Kilindo na Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala,Dkt. Asenga Severin.  (Na Mpigapicha Wetu)
 Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Elias Kwesi (mwenye suti), akijaribu kufungua koki ya bomba la maji, baada ya kuzindua mradi wa maji katika Zahanati ya Mvuti, iliyoko Kata ya Msongola, Manispaa ya Ilala, Dar es Salaam jana, kilichojengwa na Kampuni Bia Tanzania (TBL). Wa pili kulia ni Mkuu wa mahusiano na sheria wa Kampuni hiyo, Bw. Stephen Kilindo, Ofisa Mauzo wa TBL,  Ilala, Bw. Godrack Kalebi na Ofisa Uhusiano wa kampuni hiyo, Bi. Doris Malulu. (Na Mpigapicha Wetu)
 Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Elias Kwesi (mwenye suti), akisaidia kumtwisha ndoo ya maji mkazi wa kijiji cha Mvuti, Bi. Aghata Senga, baada ya kuzindua mradi wa maji katika Zahanati ya Mvuti, iliyoko Kata ya Msongola, Manispaa ya Ilala, Dar es Salaam jana, uliojengwa na Kampuni Bia Tanzania (TBL). kulia ni Mkuu wa Mahusiano na sheria wa TBL, Bw. Stephen Kilindo, Ofisa Mauzo wa TBL kanda ya Ilala, Bw. Godrack Kalebi (wa pili kulia) na Diwani wa Kata hiyo, Bi. Angelina Malembeka (mwenye kilemba kushoto).

Heart warmer: The Saga of the Lost Wallet

$
0
0

I suspect it's an indication of low expectations that I was so delightfully surprised when I found a note on my door Saturday afternoon from a person who said they found my wallet a few hours earlier. Apparently, after pulling out my credit card to get gas, I put my wallet on the top of the car for a moment to answer a phone call. Obviously, I forgot and drove off.


Patrick and Catherine saw the wallet in the middle of the road a few blocks from the gas station. They stopped their car to retrieve it. It was filled with all the things one keeps in a wallet these days, including an emergency $100 bill and other cash.

There was no home phone number, but they got an address from my driver's license, and as true good Samaritans, they decided to drive to my home to return it. When I didn't answer the door, they left a note with their phone number.

When I went to get the wallet I was so relieved and grateful I intended to give them the $100 bill emergency as an expression of gratitude, but Patrick refused. He said he was just glad he could be of help.

Patrick and Catherine were instinctively honest, but they believed in the Golden Rule as well. There were business cards in the wallet with my office phone number. They could have waited until Monday to call, but they didn't. They drove over to my house because they realized the trauma the loss of a wallet and all its contents could cause.

I'm sure there are other people who would've done what they did, but not nearly enough.
Cheers!
                                                                Mdau DS 

iga ufe!

udereva uliotukuka

Article 0

Article 24


kundi la Mafikizollo kuwasili leo jijini dar

$
0
0
Kundi maarufu la muziki wa Kwaito la nchini Afrika kusini, Mafikizolo linatarajia kutua mchana huu jijini Dar es Salaam kwa ajili ya onesho moja tu linalotarajia kufanyika katika ukumbi wa Mlimani City, kesho, Jumamosi Aprili 5 mwaka huu.

Mafikizolo imekuwa na rekodi nzuri ya kushinda kwenye tuzo mbalimbali za muziki, kutokana na kupiga muziki na kucheza kwa umahiri, hasa mtindo wao maarufu wa Kwaito.

Kundi hilo linaloundwa na wasanii wawili(Nhlanhla Nciza na Tebogo Madingoane pichani juu), kwa sasa linalotamba na vibao kama "Khona" na "Happiness", watawasili nchini kesho mchana kwa ndege ya Shirika la Ndege la Afrika Kusini.

Akiongea na gazeti hili, mratibu wa onyesho hilo Vinny Magere kutoka kampuni ya Juegacassa, amesema Mafikizollo, wanatarajia kufanya onesho moja tu maalum na la kihistoria litakalodumu kwa muda wa saa nne.

Hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa kundi hili kufika nchini, tangu kuachia wimbo wao wa "Khona", wimbo ambao umesababisha kundi hilo kujizolea umaarufu mkubwa kwenye kumbi za starehe, na hata katika vituo mbali mbali vya redio.

Mafikizolo kwa sasa wanashikilia taji la kundi bora la mwaka, kwa mujibu wa tuzo za muziki za SAMA (South African Music Awards), huku wakiongozwa kwa kutajwa mara nyingi  kwenye tuzo za Ulaya kama kundi bora la muziki kutoka Afrika.

Kundi hilo maarufu kuliko yote yaliyowahi kutokea kusini mwa Afrika liliwahi kutamba pia miaka ya nyuma na nyimbo kama "Ndihamba Nawe", "Ndixolele", "Sebenza", "Ndashata" na "Ndizolila".

Onesho la hilo, linatarajiwa kuanza saa moja usiku ambapo kiingilio kitakuwa shilingi 20,000 kwa watakaolipa kabla ya onyesho, huku mlangoni watalipia shilingi 35,000 za kitanzania.

Kundi hilo mwaka huu, limeingia katika vipengele vinne kwenye kinyanga’anyiro kikubwa cha tuzo za SAMA.

Katika kinyang’anyiro hicho chenye vipengele 28, kundi hilo limepata nafasi ya kuwania vipengele vinne, ambavyo ni Kolabo Bora ya Mwaka, albam Bora ya Pop ya Mwaka, albam ya Mwaka kupitia albam ya Reunited, na kundi  bora la Mwaka.

Kwa mujibu wa tovuti ya destinyconnect, hafla ya ugawaji tuzo hizo itafanyika nchini humo Aprili 28 mwaka huu.

Kundi hili lilianza shughuli za kimuziki tangu miaka ya 1990, albamu yao ya kwanza walitoa mwaka 1996. Tangu hapo wameshatoa albamu sita, baada ya kutoa albamu yao ya tano mwaka 2003 "Kwela". 

Kundi lilianza kutetereka na baadaye mwaka 2013 waliungana tena na kutoa albamu ya sita iliyoitwa "Reunited" na kutoa singo yao ya kwanza "Khona" wimbo ambao umewatambulisha upya.

Article 22

Shule ya Motamburu Moshi yapata msaada wa vitabu toka Airtel

$
0
0
 Mkuu wa wilaya ya Rombo kulia akimkabidhi mwanafunzi Happnes John wa shule ya sekondari motamburu moja ya vitabu vya sayansi vilivyo tolewa na Airtell katika mpango wa shule yetu kwa shule ya sekondari Motamburu iliyopo Rombo mkoani Kilimanjaro.
Mkuu wa wilaya ya Rombo kulia akimkabidhi mwalimu mkuu(Abel Masuki kushoto) wa shule ya sekondari motamburu baadhi ya vitabu vya sayansi vilivyo tolewa na Airtell katika mpango wa shule yetu shuleni hapo
======  ====== =======
Shule ya Motamburu Moshi yapata msaada wa vitabu toka Airtel.

Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania kupitia Program yake ya  shule yetu  imeendelea na zoezi lake la kuinua kiwango cha ufaulu katika masomo  ya sayansi ambapo imekabidhi vitabu vya ziada na kiada katika masomo ya sayansi  kwa shule ya  sekondari ya MOTAMBURU   iliyopo  Kata ya tarakea  wilaya ya  Rombo mkoani Kilimanjaro.

Akizungumzia msaada huo  Meneja biashara wa Airtel kanda ya kaskazini Brightone Majwala   alisema" program ya shule yetu inayolenga kutoa vifaa vya kufundishia mashuleni  ikiwemo  vitabu vya kiada na ziada   kwa upande wa masomo ya sayansi  ambapo mpaka sasa wameweza kufikia shule 900 katika baadhi ya mikoa ya Tanzania bara na visiwani ".

"Tutaendelea kushirikiana na serikali chini ya wizara ya elimu katika kuhakikisha tunaboresha elimu mashuleni na kupunguza changamoto za upatikanaji wa vitabu katika shule nyingi nchini. sliongeza Majwala

Mkuu wa wilaya ya Rombo Elinasi Pallangyo  ambaye ndio  alikuwa mgeni rasmi katika hafla fupi za makabidhiano hayo ,alipokea msaada wa vitabu  na kuukabidhi  kwa uongozi wa shule baada ya kukabidhiwa na meneja biashara wa Airtel kanda ya kaskazini ambapo amewashukuru airtel kwa msaada huo ambao amesema  umekuja wakati muafaka  huku akiwakumbusha wadau wengine kuiga mfano wa Airtell Katika kuchangia maswala muhimu ndani ya sekta ya elimu hususani katika maeneo ya vijijini.

Akitoa taarifa fupi ya maendeleo ya shule kwa mkuu wa wilaya  mkuu wa shule ya  sekondari MOTAMBURU Abel Masuki  ameishukuru airtel Tanzania kwa msaada huo ambao wamesema Airtel imeonyesha kuwa mfano mkubwa kwa makampuni mengi kwa kuungana na serikali kutekeleza sera  ya  elimu ya kuwaelimisha watanzania wengi  hasa walio  maskini kuwaondolea ujinga lakini pia akatoa changamoto ya vifaa vya maabara.

MHE. LAZARO NYALANDU MGENI RASMI MIAKA 4 YA VIJIMAMBO PROMOTING TANZANIA TOURISM EXPO IN USA

$
0
0
Vijimambo kwa ushirikiano wa pamoja na Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani na Jumuiya ya Watanzania DMV wanapenda kukukaribisha kwenye sherehe ya miaka 4 ya Blog ya Vijimambo kwa kutangaza Utalii wa Tanzania nchini Marekani na kukemea ujangili wa mali asili wa nchi yetu siku ya September 13, 2014 itakayofanyika THE OXFORD EVENT CENTER 9700 Martin Luther King Jr HWY, Lanham, MD 20706. kutakua na burudani za kila aina kutoka nyumbani na hapa Marekani TEGA SIKIO MAMBO MENGI MAZURI YANAKUJA .
Mwenyekiti wa kamati ya Vijimambo Bwn. Baraka Daudi akitia saini kitabu cha wageni  Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani siku kamati ilipokutana na Ubalozi kwa kikao cha Maandalizi ya sherehe ya miaka 4 ya Vijimambo ambayo mwaka huu mbiu yake ni kutangaza Utalii na kukemea ujangili kwa nguvu zote karibu tuungane pamoja katika siku hii maalumu ili wewe, mimi pamoja na yule wakiwemo watoto wetu wajifunze mengi kuhusu Utalii wa nchi yetu ukiwemo kukemea nguvu zote swala zima la ujangili mali asili za nchi yetu.
Kaimu Katibu wa kamati ya Vijimambo Bwn Julius Katanga akitia saini kitabu cha wageni Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani siku kamati ya maandalizi ilipokutana na Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani kwa ajili ya maandalizi ya sherehe ya miaka 4 ya Vijimambo itakayofanyika September 13, 2014.
Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Liberata Mulamula akiongoza kikao siku kamati ya maandalizi ya sherehe ya miaka 4 ya Vijimambo ilipokutana na Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani kwa ajili ya maatayarisho ya mwanzo mwanzo ya sherehe hizo.
 
Afisa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani Bwn. Suleiman Saleh akifuatilia kikao.
Wanakamati ya maandalizi kutoka kushoto Julius Katanga, Mayor Mlima na Baraka Daudi wakimsikiliza Mhe. Balozi Liberata Mulamula (hayupo pichani) wakati wa kikao hicho kilichofanyika Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani

RIDHIWANI KIKWETE NA NIA YA KUWASAIDIA VIJANA WA CHALINZE

$
0
0
Mgombea Ubunge katika Uchaguzi Mdogo Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete akizungumza na Waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa mkutano wake na waandishi hao wakati akizungumzia mwenendo mzima wa Kampeni zake,leo April 4,2014,Nyumbani kwake Msoga.
Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Mgombea Ubunge katika Uchaguzi Mdogo Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete.

MGOMBEA ubunge katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze (CCM), Ridhiwani Kikwete, amesema akipata ridhaa ya wananchi, atahakikisha anajenga stendi ya mabasi na soko ili kutoa fursa kwa vijana kupata eneo la kuuzia bidhaa zao.

Ridhiwani amesema nia ni kuhakikisha vijana wanaouza bidhaa za vinywaji na zingine waweze kuwauzia abiria wa mabasi yatakayowekewa masharti ya kuingia stendi.

Akizungumza katika mkutano wake na Waandishi wa habari alipokuwa akielezea mwenendo mzima wa Kampeni zake, Ridhiwani amesema kiu yake ni kuona vijana wanapata masoko ya uhakika ya bidhaa zao.

Amesema atashirikiana na  madiwani wa halmashauri kutafuta eneo nzuri la kujenga stendi na soko hilo litasaidia kuinua jimbo la Chalinze kiuchumi.

“Nimesikia watu wanasema kuhamishwa kwa mizani ya Chalinze , vijana watakosa mahali pa kufanyia biashara zao.Kimsingi mizani si eneo la kufanyia biashara kwanza mabasi yanasimama muda mfupi lakini suluhisho ni stendi,”alisema


Alisema lengo ni kuhakikisha wanatumia fursa ya kuwa njia panda ya mikoa ya Kaskazini na Nyanda za juu Kusini na mikoa ya Kati , kuhakikisha kunakuwa na soko la uhakika.
Viewing all 110113 articles
Browse latest View live




Latest Images